‘Sawa
muheshimiwa hakimu, tupo tayari kwa hilo, tunaomba mtaalamu wa mitandao aje
hapa atuwekee chombo kitakachowezesha sote kuona kila kitu kwa uwazi
zaidi….’akasema na mshitakiwa akawa kashika mdomo, huku akitoa kauli za kulalamika kuwa sheria
haifuatwi, lakini hakimu hakumsikiliza
na mara ushahidi ukatolewa kwenye bahasha
...ukweli
wote ukabainika, na ndoto za bwana Diamu, zikafikia ukingoni , na hapo hapo mtu
huyu akadondoka na kupoteza fahamu.
Je
kwenye huo ushahidi kulikuwa na nini, tuhitimishe kisa chetu kwa kumsikilza
Inspecta Moto akitoa maelezo kwa waandishi wa habari….
**********
Inspecta
Moto, akiwa ameongozana na muendesha mashitaka, walipotoka nje ya mahakama na
hapo hapo wakajikuta wakikabiliwa na waandishi wa habari, waandishi wakitaka
kujua kilichotokea ndani ya mahakamani, na muendesha mashitaka akamwambia
Inspecta Moto awaelezee, kwani yeye kwa muda huo alikuwa na haraka ya kurudi
kukutana na hakimu ili kumalizia hiyo kesi na taratibu nyingine za kisheria.
Baadaye gari
la waginjwa lilifika na mtu aliyebebwa kwenye chombo cha wagonjwa akatolewa,
akiwa katika uangalizi wa madakitari na walinzi….hapo kila mtu akawa
anasogelea, waandishi wakjitahidi kupata picha …ikawa ni heka heka, hadi gari
la wagonjwa lilipoondoka.
Baadaye Inspecta
Moto, akakaa na waandishi wa habari, ili
wajue kilichotokea na kupata ufafanuzi, kwa hicho kichotokea huko mahakamani na
ukweli wenyewe kwani yeye ndiye anayefahamu ukweli wote tokea mwanzo, akaanza
kwa kusema;
‘Tumeona ni
vyema tuwaambia ukweli, ili kusije kupotoswa…tunawafahamu waandishi mlivyo, na
kitakachoongewa hapa ndio ukweli ulivyo, mkiandikka kinyume chake, mjue
mnakosea, na mtahitajika kutoa ushahidi wa hicho mtakachokiandika, mjue mpaka
sasa hukumu bado….’akaanza kusema.
‘Tunakuelewa
mkuu, …..tunachohitaji ni ukweli tu…’wakasema
‘Nisingeliependelea
maswali mengi,..mimi nitaelezea kwa ufasaha…nay ale nitakayoacha mjue ni mambo
ya kisheria zaidi…’akasema
‘Muhimu ni
kuhusu kilichoonekana kwenye huo ushahidi ulitolewa mahakamani….umekubalika, na
yote yaliyoonekana ni kweli tupu…’akasema.
‘Kiukweli hata
wakati chombo hicho cha komputa kinatolewa kama ushahidi, bado nilikuwa na mashaka,
bado nilikuwa na wasiwasi kuwa huenda kile nilichokuwa nimekiwazai inawezekana
isiwe hivyo,lakini mimi na wenzangu tulishaweka imani kuwa huo utakuwa ndio
mwisho wa yote, mjue kundi hili ni wajanja sana, lakini mungu akasaidia, ikawa
ni kweli na yote yakabainika.….’akatulia.
‘Kila kitu
kiliwekwa wazi, chombo kilitusaidia sana kuweka mambo yote bayana, yakiwemo
mikakati ya kundi hilo, na watu walioshirikishwa, na jinsi gani wahusika walivyojengwa,...wengine
kwa kulazimishwa kwa `skendo’ na
wengine kwa tamaa zao tu za kupata utajiri wa haraka…’akatulia
‘Humo
walonekana wakubwa, matajiri, waheshimiwa ambao mkiwaona majukwaani mnajua hawa
ndio watu, lakini moyoni mwao ni wachafu wananuka, wanayoyafanya, ni aibu, ni
ulafi, ni tamaa, ufisadi uliokithiri ...lakini siwezi kuwataja hapa…hayo ni
mambo ya kimahakama…..’akasema.
‘Tupe angalau
sifa zo ni akina nani hao kwanini usiwataje…?’waandishi wakawa wanataka
kuwajua, lakini Inspecta Moto akawaambia kisheria haruhusiwi kuwataja kwani watu
hao wana kesi yao itakayofuata kwa kushirikiana na huyu muhusika mkuu..
‘Pia kati yao
kuna waliokaidi, hawakupenda kabisa kuwa ndani ya kundi hilo hasa pale
walipofahamu mikakati na mbinu za hilo kundi….’akasema
‘Lakini kwa
vile walishaingia, na wameshakujua siri ya kundi, sio rahisi tena kukubaliwa
kutoka…ndio maana kukawa na uzalilishaji, uteswaji, wengine hadi kuuwawa....kama
mnamkumbuka muheshimiwa yule, aliyefariki, huyo ni mmojawapo wa watu wa
mwanzoni waliuwawa na kundi hili, lakini ilionekana ni shinikizo la damu…’akasema
Moto.
‘Ndani ya
hili kundi, kuna wataalamu wa dawa, madawa yalitumika kufanya maasi, sumu za ina yake zimetengenzwa, na mtu anapewa
hiyo sumu anakufa inaokena ni kifo cha kawaida tu, kuna wengine walifikia hatua
ya kujiua wenyewe, kutokana na matezo kutokana…, na majuto ya hayo
waliyoyafanya, dhambi ainawasuta, kama mke wangu, mke wangu aliaamua kujiua,
alishindwa kuvumilia....’akasema Inspecta kwa uchungu.
Hayo yapo
kwenye hicho chombo, na kila kitu kitu kilihifadhiwa, ….mtaalamu wa mitandao,
aliweza kuweka kitu ambacho kiliweza kunasa mengi, …japokuwa mengona hakuweka yeye, lakini ule
utaalamu wa kuwezesha kumbukumbu kuhifadhiwa sehemu moja…na walipokuja kugudnua
kuwa kuna kitu kama hicho, ndio wakakitoa hicho chombo, na aliyekaa nacho ni
mama…..hata hivyo mama alitaka kumbukumbu …..kwahiyo kikawa kwenye mamlaka
yake.
Sasa kwenye
hicho chombo, kuna sehemu nyeti ambazo hata mtaalamu wa mitandao, hakuwa
kuziona…ni mama mtoto wake na watu wachache walioaminiwa, na wote sasa hivi ni
marahemu kuacha huyu muhusika mkuu.
‘Sehemu
muhimu ni ile sehemu iliyobainisha
ukweli kuhusu huyu mtu anayeitwa Diamu.
Diamu kwa tafsiri zao ni damu, au mtoto wa shetani, huyu ndiye chanzo cha hili kundi, huyu ndiye
aliyeingiwa na ndoto ya kuunda kundi, ambalo yeye aliona kaunda ‘dunia yake’.
Huyu mtu ni hatari na mtu wa ajabu sana, sehemu hiyo ilionyesha yeye na
mahusiano yake na mkuu wa kituo, ambaye ni mkuu wangu wa kazi.
‘Kikweli,
hakuna aliyeamini hayo yaliyokuwepo, …tungeliongea kabla ya huo ushahidi
tusingeliaminika,…lakini ukweli ndivyo ulivyokuwa, na ukabainika hadharani,
iliyobakia ni mahakama kuamua, na kutoa hukumu...’akasema Moto na waandishi
wakaona kama kamaliza na wakaanza kuuliza maswali kwa fujo ili kujua zaidi.
‘Kwani Dia-mu
si alikuwa amekufa mapema tu, na mkuu wako ndio akawa mrithi wake?’ akauliza
mwandishi wa habari aliyekuwa karibu na Iinspecta Moto
‘Ndio..Diamu-alikufa
maema tu,…na aliyekuwa akiongoza hilo kundi ni mkuu wangu…..’akasema Moto.
‘Kiukweli, kwenu
nyie ilitakiwa ionekane hivyo…’akatulia na waandishi wakaguna.
‘Unajua
dunia hii inaongozwa na prpoganda, na
ndivyo matukio mengi yanavyofichwa na nyie waandishi wa habari mkatumika kama
vyombo vya propaganda,…kalamu yenu hiyo itakuja kuwapeleka motoni,….’akatulia
‘Ndivyo
ilivyotakiwa iwe hivyo….Diamu alikufa mapema, na akazikwa…. lakini je ndivyo ilivyotokea,….kwenye hicho chombo
ukweli ulikuja kubainika kwani, kila kitu kilikuja kubainika kama
nitakavyoelezea, naomba mvute subira kwani mengine ni mpaka nipate kibali cha
mahakama...’akasema Moto.
‘Tunahitajia
ukweli…kwasababu kila kitu kipo wazi iliyobakia ni hukumu, na maelezo yako
hayawezi kubadilisha kitu….’akasema mwandishi mmoja, na wakati huo Moto alikuwa
akiwasiliana na muendesha mashitaka wake, na badaye akasema;
‘Kundi hili lilipoundwa, na kukamilika, muhusika
mkuu, yaani Diamu, akaona anahitajia kuwa mtu mkubwa…alitaka awe sehemu, awe ….yaani,
zaidi ya raisi…ndoto za huyu mwendawazimu zilikuwa hivyo, lakini akaona aanzie
sehmu nyei, ili kuhakikisha ndoo za dunia yake zinakamilika…..’akatulia kidogo.
‘Lakini
angeliwezaje hayo,…mtu kma yeye kwenda kushikilia wadhifa mkubwa, au sehemu
nyeti, sehemu, ambazo anaweza kufanya mambo yake bila kipangamizi,…na mwisho wa
siku yeye awe kiongozi wa kweli, ashike nyadhifa mojawapo serikalini , awe hata
zaidi ya raisi..ni ndoto za ajabu za huyu mtu…’akatulia
‘Sio rahisi
kihivyo,…. lakini kwa ujanja wake
alifanikiwa kupenya na kuingia sehemu nyeti, ni hatari kubwa sana ..ujue huyu
mtu kasoma, lakini hakusomea nafasi aliyoitaka yeye…ana akaili za ziada, lakini
zilitumikaje..ni tatizo…..akaanza kuwekeza kwenye ndoto yake.
‘Yeye kwa
mawazo yake aliona ni muhimu awe kwenye kitengo nyeti, nafasi nyeti ambayo kiongozi wake hachaguliwi ovyo…lakini
akataka aipate hiyo sehemu, kwani akiwepo hapa, utawala, usalama utakuwa
mikononi mwake….hebu fikiri mtu wa namna hii, mtu hatari kama huyu, ….lakini
alichokifanya hutaamini…...
Diamu na mkuu
wa kituo cha kati wakati huo, walikuwa marafiki sana, na urafiki wao ni kutoka utotoni, kwani walikulia sehemu moja. Kwahiyo Diamu,
anamfahamu huyu mtu na wamezoeana sana, na hata mwenzake alipojiunga na jeshi,
yeye alishauriwa naye afanye hivyo, ila yeye alikataa….muda huo alikuwa na ndoto
zak zingine tofauti na hizi za sasa.
Mkuu huyu
yeye akasomea mambo hayo, na ukuu wake aliupata kwa juhudi kubwa za utendaji
, hakuupata hivii hivi, unajua tena
maswala ya jeshi. Mkuu huyu kwa uadilifu wake akaingizwa kwenye kitengo nyeti,
mnakifahamu sina haja ya kukitaja….’akatulia.
Diamu,
alipojiwa na ndoto zake,…baada ya kuupata utajiri kutoka kwa baba yake, akawa anataka kumtumia mkuu huyu ili kupata
yale anayoyahitajia, si rafiki yake bwana, wamekua pamoja, kwahiyo akazidisha
urafiki huo zaidi, na kwa vile alikuwa
tajiri, haikuwa vigumu, kufanya mambo fulani fulani kwa mgongo wa huyu mkuu,
ambaye alijitahidi kumlinda, japokuwa hakupenda. Diamu,akawa anaweza hata
kufika kazini kwa rafiki huyo na kukaa wakaongea, na hapo akawa keshamjulia
rafiki yake huyu nje ndani, mitaani na kazini.
‘Rafiki yake
alipopandishwa cheo na kuwa mkuu wa kitengo hicho maalumu, ambacho ni nyeti
ambacho ndio alichokuwa akikitafuta bwana Diamu, baada ya kuingiwa a ndoto yake
hiyo ya ajabu. Bwana huyu akajiwa na husuda, tamaa, … akawa kaingiwa na ile hamasa
yake ya kufika kule anapotaka, kuwa sehemu hiyo aliyoishikilia rafiki yake
alitakiwa aipate yeye. Hebu fikiria mtu hajaisomea hiyo kazi, na sio fani yake,
lakini kwa tamaa tu, anahitajia awe hapo.
‘Kwanza
mawazo yake ya awali ilikuwa amtumie huyo rafiki yake na kumshirikisha huyo
rafiki yake ili afanikiwe kupata kila anachokihitajia, lakini akaona bado inakuwa
ni vigumu , maana mwenzake keshajengwa, yupo ndani ya sheria, maadili ya kazi
yanamsuta….ikawa ni vigumu…ikawa hapati kila anachokitaka, na hata wakati
mwingine anaogopa kumwambia huyo rafiki yake,...akaona aendelee na mpango
mwingine…’plan B’, mpango wake wa
siri, na mpango wake huo aliyekuwa akiufahamu ni mama yake tu…..
Mama yake
alikuwa msiri wake mkuu, na mama yake ndiye aliyemfikisha hapo alipo, mama yake
ndiye aliyemjenga huyo mtoto kuwa shetani….. bila mama yake huenda hata huo
utajiri aliokuwa nao huyu mtu asingeupata, utajiri huo umepatikana kwa kumwaga
damu, ukifuatilia historia yake ya nyuma utayagundua hayo yote. Historia ya
maisha yake ya nyuma ni ndefu na siwezi kuwatajia leo hii, ni ya kutisha ….’akasema
Moto
‘Yeye na
mama yake wakapanga mpango huo wakiwa na uhakika kuwa inawezekana, kwani mipango mingine ilishafanikiwa pesa nyingi
ilishatumika kufanikisha mambo mengine , kama kuwajenga wataalamu, ambao ndio waliounda
dunia yangu, kutokana na utaalamu wa mikono na akili zao….
‘Mtu huyu alishawekeza
pesa nyingi sana kuwatengeneza watalaamu hao, kuwasomesha na huko
walipopelekewa walisoma zaidi ya utaalamu waliotakiwa kuusomea, nia ni
kufanikisha ndoto za huyu jamaa, na mmoja wa wataalmu hao alikuwepo dakitari mtaalamu wa ngozi, ….huyu ni docta bingwa
kweli,…hakujulikana sana kama Chize, lakini alikuwa docta bingwa kiukweli. Yeye
alikubaliana na bwana huyo moja kwa moja toka awali.
‘Huyu
alihitajika kwa maswala ambayo hayakuwekwa wazi mapema.
Mkuu wa
kituo akawa anaingizwa kwenye kundi kidogo kidogo,kinamna…skondo zake zikawa
zinahifadhiwa,..mwenyewe siku moja alipoonyeshwa, karibu afe kwa mshituko wa
moyo, lakini akapozwa na rafiki yake huyo…akajengwa sasa kiushawishi….lakini
sio kwa nia mbaya, akaambiwa ni kwa nia ya uwekezaji, japokuwa kwa wadhifa
wake, hakutakiwa kushiriki sana kwenye mambo hayo, lakini rafiki yake akamtoa
hofu kuwa atamsimamia kwa hali na mali.
Mkuu huyu
kama binadamu wengine, naye alihitajia maisha mazuri….akafikia mahali akaona
hakuna tatizo, kama wengine wanafanya, wanaishi vyema, kwanini yeye…, akawa
anashirikiana na mtu huyu, akawa anajiunga kwenye vikao vya uwekezaji, mkuu huyu
akanogewa, ni nani asiyependa utajiri, mali na maisha bora, na ukionja asali
utaweza kuonja mara kweli…..’akatulia Moto
‘Mkuu akaonogewa, na akawa anashiriki sasa kwenye baadhi ya mipango,akawa miongoni mwa
wanachama wa siri, yeye akijua ni yupo
na rafiki yake mwenzake, hata kama itatokea bahati mbaya akatimuliwa lakini
sasa ana vitega uchumu, hana shida..ogopa uongozi wa serikali ukachanganya na
uwekezaji binafsi, biashara na tamaa za utajiri mkuubwa….utashindwa kuwajibika,
hapa kuna hekima sana, lakini hilo kwa sasa watu wanalidharau….’akasema Moto.
‘Siku moja
mkuu huyu, akaitwa kuwa kuna kikao maalumu,…kipindi hiki mkuu huyu alianza
kuumwa, umwa…ule mshituko alioupata wakati anaonyeshwa `skendo ‘ zake
ulimuathiri sana kiafya, akaanza kuingiliwa na tatizo la shinikizo la damu,…unajua
tena, ukichangana haya mambo, kazi za watu na huku una mambo yako ya siri, dhuluma
inakuandama, moyo hautulii, …akawa kiafya sio mnzuri sana.
‘Mkuu kuna
mpango maalumu, nataka tujadili mimi na wewe maana wewe ndiye msaidizi wangu,
kama sipo duniani wewe ndiye utashiilia huu usukani…’akaambiwa na rafiki yake, na
yeye kwa muda huo alikuwa likizo ya
kiafya, mapumziko mafupi….yeye akasema hakuna shida maana yupo lizoo fupi….yeye
akijua ni moja ya mikutano yao ya siri, akaenda, kumbe wenzake walikuwa na
ajenda nyingine ya siri.
Mkuu huyu
alipofika, wakaanza kula a kunywa, wakiongea hili na lile , mikakai mingi ya
uwezekaji…kumbe kule kunywa na kula kuna mambo yamewekwa kwenye vinywaji,
akapoteza fahamu….alipozindukana akwa sio yeye tena…..’akatulia
*******
Walichofanya
ni kwanza ni kumpoteza fahamu mkuu huyo, wakati hana fahamu, aliitwa yule docta
bingwa wa maswala ya ngozi ambaye alikuwa keshaambiwa nini cha kufanya, akafika
na kilichofanyika, ni kuchunwa kwa ngozi ya sura ya mkuu huyo ya usoni
ikahamishwa…’hapo akatulia maana watu walikuwa wakishangaa kwa mshangao mkubwa.
‘Ndio, ndivyo
ilivyofanyika, ngozi ya uso wa mkuu
ikahamishwa kwenda kwa bwana Diamu na ya bwana Diamu kwenda kwa mkuu huyo…..’akatulia
na waandishi wakahema, kila mmoja akitaka hiyo hoja imuingie kwa makini, ili
aweze kupamba kwenye vyombo vyao vya
habari…
Tukio hilo,
jinsi livyofanyika tumeliona wazi wazi, sio kitu cha kutunga, na sio mchezo wa
kuigiza…tukio zima lilionyeshwa wazi wazi kwenye kile chombo, jinsi dakitari
huyo alivyofanya kuanzia mwanzo hadi mwisho, na akaonekana mkuu mpya, yaani
Diamu, akiwa hana tofauti na mkuu yule
wa zamani, na Diamu mpya akiwa hana tofauti na yule wa zamani.
Lakini mungu
kaumba vitu vyake na tabia zake, hulka nk…ujue hiki kimefanyika bila hiari ya
mkuu , kashikwa kaleweshwa, na upasuaji umefanyika,tatizo ni huyu Diamu mpya,....je atakubaliana na hiyo
hali,..alipozindukana ilikuwaje,….’akasema
Moto, na waandishi wa habari kila mmoja akiw ana shauku, akisubiri kusikia
zaidi…
NB: Hata
mimi nina shauku kusikia,lakini kidole kinauma kwa kuchapa, tuonane kwenye
sehemu ya pili ya hitimisho la kisa hiki
WAZO LA LEO: Uongozi wa hekima, uongozi wenye kujali na kujua kuwa
cheo ni dhamana, ni ule unaoweka msilahi ya watu mbele.
Kiongozi huyu hafikirii kwanza tumbo lake, akijua kuwa kile atakachokila
na kushiba yeye, ni jasho la anaowangoza, kwahiyo atajitaidi kwanza kuona kuwa
katimiza wajibu wake, watu wake wameshakula, wamepata haki zao, na hapo ndipo atakunja
magoti na kuanza kula. Kiongozi huyu ndiye kiongozi wa watu, na huyu ndiye
tunatakiwa tumtafute. Uchaguzi unakaribia tuweni makini kwa hilo.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment