‘Ndio,.... ndivyo ilivyofanyika, ngozi ya uso wa
mkuu wangu ikahamishwa kwenda kwa bwana Diamu na ya bwana Diamu kwenda kwa mkuu
huyo…..Diamu akawa mkuu na mkuu akawa Diamu…..!’
‘Lakini
mungu kaumba vitu vyake na tabia zake, hulka nk…ujue hiki kimefanyika bila
hiari ya mkuu , mkuu aliitwa, akijua anakwenda kwenye kikao, kafika kaleweshwa,
na akiwa hajitambui hayo yakafanyika, anazindukana, anajikuta yupo katika hali
nyingine.
Je
baada ya upasuaji huu na Mkuu kujikuta yupo katik ahali nyingine, itauwaje,
maana kwa Mkuu mpya hakuna tatizo, yeye alipenda hiyo hali, lakini tatizo ni kwa huyu Diamu mpya,....je Diamu mpya atakubaliana na hiyo hali,..
Tuendelee na kisa chetu…..
****************
Diamu mpya akazindukana, na akawa anahisi mabadiliko,mwili wa binadamu, huhisi …wao kwa hatua za awali, walichojitahidi kwanza ni kuhakikisha haoni sura yake,…akawa anauliza kuna
nini kimetokea, kinachoendelea, akawa hapaji jibu lenye kurizisha....
'Wewe unaumwa, shinikizo lilikupata ukapoteza fahamu, ndio maana upo hivyo, tumekutibia docta huyo hapo....'akaambiwa siku ya kwanza, ya pili....lakini mbona sijielewi...akawa najiuliza.
Na kama unavyojua hapo alipokuwepo ni ofisi, na watu wakimuona wanafahamu huyo Diamu..huwa anatoka kutembea humo ndani, anakutana na wafanyakazi, wengine hawajui kinachoendelea,wanamuuliza mambo ya kikazi...anashindwa kuajibu, anajiuliza kwanini wanamuuliza mambo kam hayo...
Siku moja akawa kwenye chumba chake, akasikia chumba cha pili kikifunguliwa, akaona atoke, akafungua mlango ka siri, akamuona mtu,...
'Oh, mbona yule mu anafanana na mimi, akashikwa na mshangao mkubwa maana yule mtu sura ni kama yeye…akashituka, …haikutakiwa kabisa aje kumuona huyo mtu mapema hivyo, alitakiwa kujengwa taratibu halafu watafute njia za kumweka sawa,lakini hali hiyo ikaja kugundulikana mapema.
Jamaa akahisi kuna tatizo, kwanza kuona jinsi gani anavyochungwa haruhusiwi
kutoka akiulizwa anaambiwa alizidiwa na akawa kama kachanganyikiwa ndio maana
wanahakikisha kuwa hali yake ipo salama kwanza, kabla hawajamruhusu kutoka hapo, na docta yupo kwa kwa jili hiyo.
‘Kama ni hivyo kwanini sijapelekwa hospitalini?’
akauliza
‘Hili sio tatizo la hospitalini kwa hivi sasa, na docta yupo hapa, anakuangalia usiwe na wasiwasi,…wewe tulia utapona
tu….’akaambiwa.
Sasa siku hiyo akamuona mtu anayefanana naye, sura kama yake...kila mtu anajifahamu sura yake au sio.....akamuona mtu akiingia kwenye chumba cha jirani yake, sura kama yake,..akasubiri, akitaka kuhakikisha, na mara mtu huyo akatoka akiwa kavalia sare zake za kikazi, sare ambazo huzivaa kwa siku maalumu, akienda kukutana na wakubwa zake wa kazi.
'Haiwezekani....'akasema na hapo, akili ikamjia,
akajua kuna kitu kachezewa, akimbilia kutafuta kiyoo, hadi akakipata
kujiangalia…loooh, mshituka alioupata hakutegemea.
Ukumbuke huyu mtu alishaanza kuwa na tatizo la shinikio
la damu, kwahiyo mshituko huo ukazidi kumauthiri, akapoteza fahamu, na Bahati
nzuri, walikuwa wakimchunga kwa kumuangalia kwenye video , kwenye mtandao,
docta alipoona hivyo akafika,a kamfanyia huduma ya kwanza.
‘Nataka kuonana na huyu mshenzi…’akasema
‘Mshenzi gani?’ akauliza docta
‘Huyu aliyenifanyia hivi…’akasema
‘Hapo sasa ikaanza kujengwa hoja kuwa jamaa kachanganyikiwa, anadai mambo ambayo hayapo,
mara yeye ni mkuu, mara kabadilishwa sura, …ikaenea kuwa Diamu kachanganyikiwa…
Ukumbuke maumbile ya hawa watu yanafanana sana, kwahiyo
hakuna mtu angaliweza kutilia mashaka, na ukumbuke watu hawa walikuwa marafiki
wakubwa, kwahiyo Diamu alishamsoma rafiki yake, tabia zake, na kama ulivyoona mara
kwa mara alikuwa kimtembelea rafiki yake huyo ofisini kwake, na huko ofisini
kwake aliweka mitego yake ambayo aliweza kuona kila kitu mwenzake
anachokifanya.
Bwana Diamu, ni mtaalmu, anajua kuigiza, anajua
kujibadili akafanya mambo kutegemeana na nyakati, kwahiyo kwa rafiki yake huyo
haikuwa kazi ngumu kumuigiza na kuwa kama yeye, na kila kilichowahi kufanyika
hapo ofisi alikuwa anakifahamu, ….Japokuwa sio yote aliyawezea, hasa yale ya
kitaalamu zaidi , lakini kwa kiasi kikubwa alishajivika tabia ya mkuu huyo
kabla tendo halijafanyika.
‘Na upasuaji ulifanyika vyema kabisa, Diamu akawa ndiye mkuu, na mkuu akawa ndiye
Diamu, hata hivyo siku zilivyozidi kwenda ikaonekana ni hatari , mkuu huyo
ambaye sasa ni Diamu, akawa analeta fujo, ….akawa kila mara anapigwa msindano
ya kumtuliza,
‘Sasa huyu mtu ni hatari, akitoka hapa anaweza kuharibu
kila kitu, hatujui jinsi gani anaweza kulithibitisha hilo, kwani watu
wameshajua kuwa amechanganyikiwa…..’wahusika wakaongea.
‘Huyu dawa yake ni moja tu….’akasema mama
‘Tumfanyeje?’ akauliza mtoto mtu
‘Si kachanganyikiwa huyu, kwa mtu kama huyu anaweza
kufanya lolote,..doct aongeze madawa ya kuchanganyikiwa,….na ni lazima
atajimaliz amwenyewe..’akasema mama.
Madawa ya namna hiyo yakuharibu akili yalikuwepo. Docta bingwa mwingine mtalamu wa madawa akaagizwa dawa za namna hiyo, na huyo docta alikuwa hajui
kinachoendelea, ya akaitikia wito na kuwakabidhi hizo dawa.
Jamaa, yaani mkuu, ambaye sasa ni bwana Diamu, akapigwa sindani ya hizo dawa,ambazo lengo lake ni kumuharibu akili, sasa akawa kachanganyikIwa, akawa anajipiga piga ovyo, na siku hiyo
mlango ukaachwa makusdi jamaa akatoka akiwa kachanganyikiwa kabisa….
Ungelimuona muda hu ungelimuonea huruma, kwani alikuwa akijikwangua, anajipiga piga
kichwani, kuashiria kuna kitu kinamkera kichwani, maumivu au hayo madawa
yanaleta shida kichwani, akakimbilia baharini, kwani hayo yote yalikuwa
yakifanyika kule eneo la makaburini kwenye ofisi ya chini ya ardhi..
Taarifa ikatolewa kuwa Diamu kachanganikiwa kapotea,
hata taarifa ikafika polisi, watu wakaanza kumtafuta, na mara ikaja taarifa
kuwa maiti yake imeonekana ufukweni mwa bahari, na taarifa akafikishwa kwa
familia, na familia ambayo ni mama , sasa mama ni wa kufikia, mama akafika
kukagua maiti akakubali kuwa ni mwanae,...!
Msiba ukatangazwa japokuwa hakutanganzwa sana, ilikuwa kimiya kimiya....
Mazishi yakafanyika kisiri...na watu wa kijijini wa
kimila wakaitwa, na wao walijua kuwa kweli wamemzika mrithi wa kiti maalumu cha
kimila..japokuwa kuna wazee walihisi kuna jambo, lakini wakanyamazishwa kwa
vitisho na pesa, na ukumbuke kuwa mama huy alikuwa akiogopewa, kwa imani za
kishirikina.
Mama, akaonekana akiombeleza kifo cha mwanae, japokuwa
ni kwa geresha, ..lakni akilini mwenyewe
anafahamu ni kitu gani kilichofanyika. Kosa walilolifanya ni kuweka kumbukumbu
hizi zote kwenye chombo hicho, ….chombo
hicho kilicholetwa mahakamani kama ushahidi, ndicho kilichowezesha hayo
kufahamika,…na mama ndiye aliyekuwa mlinzi wa hiki chombo..mama huyu alitaka
iwe hivyo, alisema anahitaji kumbukumbu za kila kitu za kumuhusu mwanae, maana
hajui huko mbeleni itakuwaje.
Sasa mkuu mpya kaingia kazini, baada ya kutoka mapumziko
ya muda kiutaratibu wa kiofisi, ndivyo
ilivyojulikana hivyo kazini kwake, na kazi zake zikawa zinafanywa na msaidizi
wake, utakumbuka kuwa msaidizi wake alikuwa akifanya karibu kila kazi baadaye,..kitu
ambacho hakikuwepo kabla, enzi za mkuu mwenyewe alikuwa mchapakazi sana, lakini
alipokuja huyu mkuu wa bandia, kazi nyingi zikawa zinafanywa na huyu msaidizi, hata
watu walikuja kujiuliza inakuwaje, mkuu hafanyi kazi kama ilivyokuwa kabla,
lakini baadaye walikuja kumzoea, wakijua ni kwa vile alishaanza kuumwa umwa.
Mkuu huyu mpya ni mjanja, ana akaili ya ziada, akili ya
kuweza kumsoma mtu na kufanya kama alivyokuwa huyo mkuu wa awali, lakini ujue
yeye aliingia hapo kwa lengo gani, kwahiyo chini kwa chini akawa anajenga
himaya yake ndani ya kitengo hicho, hadi akawa kakidhibiti, , lakini kuna kazi za kiutendaji zenye utaalamu wa
hali ya juu, hizi asingeliweza kuzifanya bila msaidizi wake. Akamjenga msaidizi
wake kiujanja, akamuwezesha, na msaidizi huyo akawa sasa kama bendera kufuata
upepo.
Kuna watu wengine ambao aliamua kuwaingiza moja kwa moja
kama akina Maneno, na watendaji wengine, kuna wengine wakawa wanatumiwa kama
chambo, kama Mrembo Jembe, ambaye alikujaiwa na akatumika kama chambo,
akitokea nyumba ya mama urembo,....
Baadaye siri hii ikaonekana inaweza kuvuja, ikaanza
kutafutwa njia ya kuhakikisha kuwa wale wote wanaofahamu wanazibwa mdomo, ndio
ikaonekana watu kupotea, kuonekana wamekufa au kujiua. Wakawa sasa wamebakia
wale wataalamu wa kazi mbalimbali, kama Docta, mtaalamu wa mitandao, mama
Urembo, na wengineo....hawa nao walitakuwa kuondolewa mmoja mmoja, kutegemeana
na unyeti wa kazi yenyewe.
‘Docta wa upasuaji, alikuwa anafahamu siri kubwa sana,
huyo alionekana kama ataendelea kuwepo ipo siku atavujisha siri, ukumbuke docta
huyo sio docta Chize,docta Chize alikuwa na utaalamu wake mwingine wa madawa na
upasuaji wa mambo mengine tofauti na docta huyu, hata docta Chize hakujua
kilichofanyika siku hiyo ya kubadilisha sura, yeye aliombwa madawa ya namna
fulani na fulani, lakini hakujua kabisa dawa hizo zilikuja kufanya nini.
Baadaye huyu docta wa ngozi akauliwa , na ndio siku ile
kesho yake yakatokea mabomu, nia ya yale mabomu ni kuharibu kumbukumbu zote za
nyuma....kwani eneo hilo chini ya ardhi ndipo kulikuwa na mitambo na mambo
mengi yaliyokuwa yakifanyika humo, na mambo hayo yakatakiwa kuharibiwa kinamna,
kwani kuna habari kuwa siri za hapo zimeshavuja.
Ikapangwa pamoja na kuharibu mitambo hiyo na eneo hilo,
pia waharibu, na kuwamaliza kabisa wataalamu wote, na hapo ndipo mtu huyu
atajiona yupo huru kufanya mambo yake. Lakini ya mungu mengi, hayo
hayakufanikiwa,kwani wataalamu hao walikuja kuokolewa kimiujiza.
‘Je waliokolewaje kimiujiza akauliza mmoja wa waandishi
wa habari
**********
Aliyekuja kuwaokoa ni kiongozi wa usalama mstaafu , baba
mkwe wangu, ambaye alishalichunguza kwa undani kundi hilo kwa siri, baada ya
binti yake kufariki, na alihisi kufa kwake kuna sababu, katika kuitafuta hiyo
sababu ndio akaligundua hilo kundi.
Tunamshukuru sana mzee wetu huyu, hii
inaonyesha kuwa wazee wetu hao ni hazina kubwa, ambayo tunahitajika kuitumia
vyema, na cha kuwalipa hawa watu ni kuwaenzi kwa kuwatunza, tuwape matunzo
mema.
Siku ile ya tukio mzee huyo kwa kutumia uzoefu wake,
alifika huko, alishafahamu kitakachotokea, hakushirikiana na mtu, maana hali
ilivyokuwa usiingeliweza kumuamini yoyote, ...wataalamu hao walipoingia, wakiwa
wanasubiri kwenye chumba maalumu cha kikao, wakajikuta wanapambana na gesi,
gesi maalumu ya kupoteza fahamu, na wote wakazimia,...alifanya hivyo Diamu,
akijua watakuja kufa na bomu na itakuwa mwisho wao.
Mzee wetu huyu akawa ameshafika eneo hilo, alichofanya
ni kuwatoa hao wahusika kutoka mle ndani, uzuri kulikuwa na kigari cha kukokota
kwa mkono ndicho kilichomsaidia kuwahamisha hao watu peke yake. Na mle ndani
kulikuwa na maiti za watu wengine waliokwisha uliwa na hilo kundi, ambao walisubiria
kuja kutupwa, waonekane wamejiua, lakini kwa pale ilitakiwa wote waonekane
wamefia humo kwenye huo mlipuko.
Muda huo, Diamu au mkuu wa kituo alikuwa anawajibika
kama kiongozi, na alisubiria muda muafaka, ambao sisi tutaingia, kwani
alishatoa amri hiyo kuwa kikosi chetu kingie na kukagua humo ndani kuona kama
kuna watu au vifaa vyovyote.
‘Yeye alikuwa na mipango yake, kuhakikisha kuwa kweli
hicho kifaa hakipo, ndicho kilichofanya aingie tena humo ndani,...
‘Huyu kiongozi mstaafu akafanya kazi ya ziada, hakutaka
hali hiyo igundulikane mapema, kwani ingeliharibu kila kitu, alichofanya ni
kuwavalisha wale marehemu nguo za hao
watu waliotakiwa kuuwawa, akina Chize, mama urembo, mtaalamu wa mitandao na
wataalamu wengine, alifanya kazi hiyo kwa haraka sana, akawatoa hao watu ambao
walishaleweshwa na madawa, akawaficha nyumba ya jirani. Nikitendo cha ujasiri,
na aliweza kufanikiwa.
Alipokuja Diamu, ambaye ndiye mkuu wa kituo mpya, akajua
ni wale watu wake, waliotakiwa kuuwawa, wakati huo akili yake ilikuwa
kukitafuta hicho kifaa, akawa anahangaika huku na kule, kwahiyo hakupata muda
wa kuchunguza tena hilo bomu, alipoona nachelewa akaona atoke,..
Wakati huo sisi na kikosi changu tulishaingia ndani,…ukumbuke
kiongozi huyu mstaafu alikuwa ni mtaalamu wa mabomu pia, yeye alishaliona hilo
bomu likiwa limetegeshwa, alichokifanya ni kuligeuza muelekeo kitaalmu…lilipuke kuelekea muelekeo
wa baharini
‘Na pia hilo bomu, aliyelitengeneza, hakuliweka kama
ilivyotakiwa alitengeneza kivingine kinyume na maagizo ya bosi wake, kwani hata
yeye hakutaka mauaji zaidi yaendelee, na alijua akifanya kama alivyotaka huyo
bwana mkubwa, watu wengi wangaliweza kufa siku hiyo, na wakati alipoambiwa
alitengeneze hakujua kuwa na na yeye ni mmoja wa watu waliotakiwa kufa na hilo
bomu.
‘Yeye akili ikamtuma kulitengeneza kwa namna itakayopunguza uharibufu na mauaji
zaidi, ni kama umeme, unaweza kuunganisha waya , na umeme ukawa ni wa kurusha,
au wa kunasa,..sasa bomu hilo akalitengeneza likawa kama umeme wa kurusha,akalitengeneza
anavyojua yeye, kwahiyo lile bomu likawa halina nguvu, likawa kama upepo wenye
nguvu, ndio maana kile kilichotakiwa kufanyika kikawa kinyume chake,
lililipuka,lakini halikuweza kuleta hayo madhara.
Kipindi bomu linalipuka kuna muda bwana Diamu alifika hapo kama
mvuvi...anapofika eneo hilo hujabadilisha akavaa kama mvuvi, akitoka hapo
hupitia mlango mwingine akaingia nyumba ya jirani ambapo alikuwa na chumba,
hubadilisha nguo akawa mtu mwingine tofauti, kavalia kofia pana na koti la kawaida, hutoka hapo akaingia hoteli za karibu akavalia vizuri, ....kikazi au mfanyabiashara...
Kilichomfanya kuingia mle siku ile, aligundua kuwa mama
yake kumbe alificha hicho kifaa cha komputa chenye kumbukumbu humo ndani, ndio
maana akaingia humo ndani kukitafuta,
lakini hakujua kuwa muda wa kulipuka hilo bomu ulipunguzwa, akajikuta ananaswa mwenyewe
humo ndani, na lilipolipuka akawa humo ndani, lakini akawahi kuruka dirishani....
Wakati anaruka dirishani mimi nikamuona, sikujua kuwa ni yeye, lakini nilijua ni mmoja
wa hao watu wa hilo kundi, na haraka nikaitumia silaha yangu, nikiwa hewani,
maana tulisharushwa na bomu, ….kama askari
unakuwa mwepesi, nikafyatua
risasi iliyomjeruhi huyo mtu…eneo la begani.
Lengo langu halikuwa kumuua, kumbe hiyo risasi ilimuathiri
sana, na sehemu yake ya matibabu ni hospitali ya bwana Chize, na docta huyo ni
mmoja wa watu aliotaka wafe , na alijua kwa muda huo ameshakufa na hilo bomu,
hata hivyo, kulikuwa na docta mwingine, huyo alijua jinsi gani ya kumuweka sawa.
Kwahiyo alipofika hapo hospitalini, akaagiza docta huy afike, na akamuarifu
amfanyie matibabu ya haraka.
Docta huyu ni mtaalmu wa upasuaji, ni docta bingwa pia,
japokuw akiwango chake sio sawa na cha docta Chize, kwahiyo huyu docta ndiye
aliyeweza huyu mtu maana kwa muda huo alikuwa katika hli mbaya, kuungua na moto
wa lile bomu, na risasi iliyomjeruhi na damu ningi ilishapotea.
Kiongozi huyu alipotoka hapo akiwa kajeruhiwa, akakutana
na watu wake wa karibu, akawapa mikakati, kuwa inahitajika ajali ya haraka
maana hataki kujulikana kuwa kaumia kwenye mapambano…yeye aliwaambia kaumia
kwenye mapambano ya kupambana na kundi haramu, watu wake wana akili za haraka,
wakajua nini bosi wao anataka, ....
‘Ajali ikatengenezwa kuwa yeye wakati anakuja
kushirikiana na wenzake kwenye hayo mapambano na kundi haramu, kwenye eneo hilo
lilipotokea mabomu, ndipo akakutana na hiyo ajali, kwa haraka gari lake likapelekwa mahali likatengenezewa ajali, na
mkuu huyo, ikaonekana alikuwepo, na akachukuliwa hadi kwenye hiyo hospitali na
zoezi hilo likafanikiwa, mkuu akawa anatibiwa kimiya kimiya ikijulikana kuwa
kaumia kwenye ajali, na risasi ikatolewa kwa siri na docta msaidizi.
Wakati anafanyiwa upasuaji, ikabidi docta aulize, ili
ajue nini cha kuandika kwenye taarifa yake, akauliza swali ilikuwaje, ulipigwa
wapi hiyo risasi.Aliyeuliza swali hilo alikuwa docta msaidizi wa docta Chize,
swali hilo hakulipenda huyu mtu, lakini alitaka kutumia busara, ili mambo
yasije kuharibika.
Ujue docta Msaidizi hakuwa miongoni mwa kundi, ni wale
wanachama wanaotumiwa tu bila kujijua ila wanafaidika kinamna, kwa kupewa mishahara
mikubwa, kuwezeshwa, na hali zao za kiuchumi ziliboreshwa, kwahiyo hawana
shida,wanachoambiwa na wakubwa zao wanafuata tu....Yeye aliambiwa na huyo
mgonjwa kuwa;
‘Ajali hii imetokana na maadui zangu, wakati naendesha
gari walitaka kuniua, kuna mtu nilimuona akitaka kunipiga risasi, nikakwepesha
gari, lakini alishafyatua hiyo risasii ndio risasi hii ikanilenga hapa begani,
lakini, sitaki hili lijulikane, ikijuliakana nitawapa nafasi maadui zangu
kujigamba, kwahiyo nataka iwe siri…unasikia…’akasema mkuu huyo.
Alifanya hivyo, kwa vile hakutaka watu kama akina Moto
kuja kumgundua,alijua mtu, hasa Inspecta Moto, angeliweza kuunganisha mambo na
kuja kumgundua kuwa ndio yeye aliyekuwepo siku ile, kutokana na hilo jeraha la
risasi. Kwahiyo swala la kujeruhiwa na risasi haikujulikana kabisa. Ikawa ni
siri kati ya mkuu huyu na huyo docta.
Baada ya tukio hilo, mkuu akawa anaombea apone haraka,
akajua akipona, mambo sasa ni huru, hakuna atakayemfahamu kabisa….lakini
wasiwasi wake ilikuwa hicho chombo chenye hizo kumbukumbu zake, hakuwa na
uhakika kama kweli kilikuwepo kwenye lile jengo, na je kama kilikuwepo kitakuwa
kimeharibiwa na huo mlipuko wa bomu, lakini kwa kumbukumbu zake, chombo hicho
ni imara sana ..hakiungui au kuharibika kirahisi….hilo likawa linampa shida,
ndio maana akawa anataka kutoka mara kwa mara kuchunguza akimtumia nesi,
aliyemrubuni.
Siku kabla ya huo
mlipuko, wakati mama yake akiwa hai, bwana Diamu, aliwahi kumuuliza mama huyo
kuhusu hicho kifaa cha kumbukumbu kipo
wapi, mbona hakionekani sehemu yake,
lakini alipomuuliza mama yake, kiajabu kabisa mama yake akasema hajui kilipo,…
Mtoto akajua kuwa mama yake kumbukumbu zake zimeshaanza
kuleta shida, na kweli kipindi hicho mama huyu alikuwa ameshaanza kujiwa na
hali kama ya kuchangabyikiwa akawa anaanza kuropoka ovyo, kuna muda anamkana
mtoto wake huyo akija kumsalimia, anamwambia yeye sio mtoto wake, mtoto wake hana sura kama hiyo….
‘Wewe sio mtoto wangu, mtoto wangu ni huyu hapa, wewe sio mtoto wangu, ondoka hapa, sikutaki, namtaka mtoto wangu mwenye sura hii hapa….’anamwambia
akimuonyesha picha yake ambayo alikuwa akilala nayo…hadi mtoto huyo akaja
kuichkua na kuiharibu.
‘Kwa hali ile ikaonekana kuwa mama huyu anaweza kufichua
siri, lakini huyu ni mama yake bila yeye hayo yote aliyo nayo asingeliyapata…ikawa
nayo inampa shida, ikabidi mama huyo awe na ulinzi wa ziada, hakuna kutokatoka
nje kuonana na watu....
NB: Haya naona sehemu ya pili ya hitimisho inazidi kuwa
kubwa, ngoja tuishie hapa , tutakuka kumalizia kwenye sehemu ya tatu, Je chombo
hiki aligundua kipo wapi, na alifanya nini…na ni yeye aliyemuua mama yake.
WAZO
LA LEO:
Malezi ya watoto huanzia kwa wazazi,hiyo ni shule ya kwanza ya binadamu, shule
ya sili aliyoiridhia mungu. Mtoto hapa humfahamu mama yake kwa vile muda wote
yupo naye na akisikia njaa, anajua wapi pa kushika na kupata nyonyo yake. Lakini
kutokana na nakama za kimaisha, wazazi huwaachia watoto wadogo, wafanyakazi wa
ndani.
Tatizo linalojitokeza hapa ni uwezo na tabia ya hawa
wafanyakazi wa ndani. Kwani tunahitaji kubana matumizi , tunahitaji wale ambao
hawajajua gharama , tuwalipe mshahara kidogo. Wafanyakazi hawa wengine
walishindikana na wazazi wao, wengine kutokana na malezi, hawajui nini maana ya
upendo, hawajui jinsi gani ya ulezi, na
huduma kwa watoto.
Ni kweli inabidi wazazi tuhangaike, lakini tukumbuke kosa
dogo kwa hawa watoto wetu linaweza kumharibu huyu mtoto, achilia mbali afya yake, lakini kuna swala la tabia…mtoto huyu kwa vile aanshinda na
mfanyakazi wa ndani, basi ujue hata tabia atakayoifahamu kwa haraka ni ile ya
mlezi wake huyo.Tuweni makini kwa hili.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment