Inspecta Moto
akatoka pale mahakamani kwa haraka akimfuatilia yule nesi, ....alimuona akiwa
kasimama ....akionyesha kuwa na wasiwasi, akionyesha kuwa kuna kitu
kinamsumbua, ....akajiuliza ni kwanini kaamua kufika hapo mahakamani, wakati
alipoongea naye alisema hatafika, anataka kupumzika kwa ajili ya kazi, kwa hali
kuna kitu kimemleta, je ni huo mziko aliogizwa akauchukue kwa fundi.
‘Inawezekana, atakuwa na, inawezekana, kaja nao kwa
nia ya kumpa huyo mtu wake...’akasema
Inspecta.
Wakati anawaza hayo, akawa anatafuta mwanya wa kutoka,lakini
haikuwa kazi rahisi kuwapita watu waliopata nafasi ya kupenya na kusimama eneo
la mahakamani, kwa muda huo watu wengi walikuwa wamejazana mlangoni, ilionekana
kama vile polisi waliamua kuwaachia watu waliokuwa wamendelea kubakia waingie
tu, maana wengine walishaamua kuondoka,.…
Hata Inspecta alipotoka eneo hilo,alikuwa bado hajamuona
nesi alipokuwepo, akageuka huku na kule kumtafuta na baadaye akamuona akiwa kwenye eneo la barabara kuu, kunaposimama
bajaji, alikuwa kasimama karibu na bajaji, kuashiria kuwa anataka kuondoka, na pembeni yake alikuwa kasimama jamaa mmoja wakiongea naye, jamaa
huyo alikuwa kavalia vyema kabisa, suti, na mawani meusi machoni, alionekana kama
hawo jamaa wanaojiita ‘misheni town’.
Inspecta akawa anajaribu kumpungia nesi mkono, ili
amone, lakini nesii hakuwa akiangalia muelekeo wake, alikuwa akiendelea kuongea
na huyo jamaa huku bajaji tayari imeshawashwa,..Inspecta akawa anajitahidi
kwenda pale waliposimama, ili amuwahi kabla hajaingia kwenye hiyo bajaji ...
Ilionena kuna kitu walikuwa wanakabidhiana, maana nesi alitoa bahasha kwenye mkoba wake
akampa yule jamaa, na yule jamaa akawa anatoa bahasha nyeupe anamkabidhi nesi,
lakini nesi hakuiweka ile bahasha moja kwa moja kwenye mkoba wake, ...aliifungua,
akatoa karatasi, ni kama barua, ni
karatasi yenye maandiko, na nesi akawa anayasoma.
Nesi akawa akawa akatoa peni kwenye mkoba wake, akawa
anaandika kitu, zilionekana ni nakala mbili, moja akamrudishia yule mtu na
nyingine akabakiwa nayo huyo nesi, nesi akawa kama karizika, bila kurudishia
ile barua kwenye bahasha, akaingia kwenye bajaji akiwa kshikilia ila karatasi mkononi, na yule
jamaa akawa kashikilia ya kwake, akaikunja na kuweka kwenye koti lake pamoja na
ile bahasha ya mwanzo, wakashikana mkono wa kukubalina.
Inspecta Moto kwa wakati huo alikuwa anawakaribia,
tatizo kubwa lilikuwa ni watu, jinsi ya kupata njia ya haraka ya kuwafikia,
lakini matendo yote hayo yalionekana wazi. Inspecta akawa anatembea kwa haraka akisukumana na
watu, akijaribu kupunga mkono na hata kuita, lakini ukelele wa magari
yaliyokuwa yakipita na mngurumo wa ile bajaji ambayo ilikuwa ipo tayari
kuondoka, iliwafanya nesi na mwenzake wasimsikia Inspecta akiita.
Na Inspecta akawa karibu yao, lakini kabla hajawafikia , nesi akawa
ameshaingia kwenye bajaji na kuanza
kuondoka;
‘Nesi subiri....’Inspecta Moto akasema kwa sauti, lakini
alikuwa keshachelewa, bajaji ikawa imeshaondoka kwa mwendo wa kasi, na yule
jamaa aliyekuwa na huyo nesi akawa anatembea muelekeo wa kwenda mahakamani.
Inspecta Moto akamfuata yule mtu aliyepewa ile bahasha
na karatasi,, akamuonyesha kitambulisho na kuamwambia
‘Mimi ni askari-usalama, nimekuona ukikabidhiwa bahasha
na yule nesi, nataka kujua ni kitu gani kipo ndani ya hiyo bahasha...’akasema Inspecta
na kumfanya yule jamaa kwanza aonyeshe kushangaa, halafu akatoa maneno kama ya
ukali;
‘Mimi sijui ni kitu gani, kazi yangu ni kumpelekea
muhusika,....’akasema huyo mtu akionyesha kukasirika.
‘Nataka kumjua huyo muhusika unayetaka kumpelekea huo
mzigo ni nanii...hicho kitu kimeibiwa ni mali ya mahakama, ni ushahidi,
tumekuwa tukiutafuta toka asubuhi, kwahiyo unakamatwa kwa kuhusika katika
upotevu wa ushahidi wa kimahakama...’akasema Moto akiwa hana uhakika kama ndio
chenyewe au la, alifanya hivyo kama kubahatisha tu.
‘Wewe mwenyewe umeona nikikabidhiwa na huyo mdada,....siumesema
hap umeona nikibabidhiwa na huy o mdada, sasa iweje unishuku kwa kuchukua, au
kuiba ushahidi wa mahakama, ....mimi sijui lolote, mimi ni wakala tu, wala
sijui ni kitu gani. unachozungumzia..’akasema
‘Nimekuuliza unatakiwa kumpelekea nani, usipoteze muda,
maana nasubiriwa mahakamani?’ akaulizwa huyo mtu, na alipoona huyo mtu wa
usalama hatanii, akasema;
‘Nimeambiwa nimkabidhi askari mmoja aliyewaleta hao
washitakiwa, ambaye ataufikisha huo mzigo kwa mlengwa, sijui mlengwa ni nani...’akasema
‘Twende ndani ya mhakama, unahitajika ukakabidhi hicho
kitu mbele ya hakimu, na uelezee ulivyokipata , na tunatakakumfahamu huyo
askari ambaye unahitajika kumkabidhi,...’akaambiwa,
‘Mimi huyo
anayetakiwa kukabidhiwa simfahamu....na mimi siwezi kufanya kazi hiyo...unaniingiza
kwenye matatizo nisiyyafahamu.....’akalalamika
‘Hapo huna jinsi, ni lazima ukabaliane na hayo
niliyokuambia, up chini ya ulinzi....’akasema Moto.
‘Sikiliza afande, kwanza ujue mimi ni wakala , ukitaka
nifanye hivyo, unataka kazi yangu iharibike, nitaonekana sio mwaminifu kwa
wateja wangu,..tafadhali, elewa umuhimu wa kazi yangu, kama ningelijua ni kitu
cha kimahakama nisingelikubali kukipokea....’akasema huyo mtu akionekana sasa
kuwa na wasiwasi.
‘Nimeshakuambia huna jinsi yoyote, kwa usalama wako ni
muhimu twende ndani ya mahakama, nitakuonyesha
mtu ganii sahihi wa kumkabidhi hicho kitu, na wewe utakuwa salama kuwa
umewakilisha nyaraka za kimahakama kwa muhusika, vinginevyo utakamatwa, na hata
hiyo kazi yako hutaweza kuifanya tena...unanisikia haya twende ndani
usinipotezee muda...’akaambiwa na yule
mtu akawa hana la kufanya wakaongozana na
Inspecta Moto hadi ndani ya mahakama,
na wakati wanaingia ndio pale muendesha mashitaka alikuwa akiulizwa kwa mara ya
mwisho kuwa anahitaji muda gani, masaa au siku, ili kuwakilisha ushaidi wake
...
********
‘Muendesha mashitaka, umesema unahitaji muda, ili uweze
kuwakilisha ushahidi wako, na maelezo sahihi dhidi ya huyu mtuhumiwa, je unahitaji muda gani…?’ akaulizwa muendesha
mashitaka na kabla hajajibu akamuona Inspecta Moto akiingia na huyo mtu, na
muendesha mashitaka akasema
‘Muheshimiwa hakimu, kabla sijajibu hilo swali naomba
niongee na mwenzangu, ....’akasema na akamsogelea Inspecta Moto akisema;
‘Ushahidi upo wapi, nashindwa hata kuelezea, maana jamaa
katushinda ujanja,…niambie umeleta nini?’ kauliza
Inspecta Moto akasema kumuambia yule mtu;
‘Mkabidhi huo ushahidi muendesha mashitaka na mwambie
ilitokeaje kwa haraka na kwa kifupi, ....’akasema Moto na yule jamaa akasema
kama alivyomwambia Inspecta Moto, na muendesha mashitaka, akasita kuipokea ile
bahasha kwanza, akasema;
‘Kuna nini ndani?’ akauliza
‘Mimi sijui kuna nini, kazi yangu ilikuwa kumpa mzigo
niliopewa dada huyo nay eye kunikabidhi huu mzigo ambao natakiwa kuufikisha kwa
askari, hayo mengine hayanihusu, sasa
ukiniuliza kuna nini, mimi hiyo sio kazi yangu kutegemeana na makubaliano yetu
, lakini kwa kusika mkononi, inaonekena kuwa na kitu kigumu kama simu…’akasema
huyu jamaa
‘Hebu kitoe hicho kitu kwa haraka, tunataka kuhakiki
kama kama ndio chenyewe…’akasema muendesha mashitaka na yule mtu jamaa akaifungua
ile bahasha, na kutoa kitu kilichokuwemo ndani, na Inspecta Moto akasema;
‘Ndio chenyewe…..’na muendesha mashitaka akapumua kama
mtu aliyekuwa akishusha mzigo mnzito , na kwa haraka, akageuka kumuangalia
hakimu akasema;
‘Ndugu muheshimiwa hakimu naomba samahani kwa
kuchelewesha taratibu za mahakama yako tukufu, lakini tumefanya hivi ili
kuhakikisha kuwa haki inatendeja, ndugu muheshimiwa hakimu, ushahidi tuliokuwa tukuitafuta ambao uliibiwa
tumefanikiwa kuupata, na tunaomba tuuwakilishe mbele yako, ...’akasema muendesha mashitaka, na mshitakiwa akasema;
‘Ushahidi gani huo, na huo ushahidi kwa kesi ya nani…..?’
akauliza mshitakiwa mkuu kwa kujiamini.
‘Kwa kesi yako wewe, wewe ndiye mshitakiwa ...’akasema
muendesha mashitaka
‘Mimi kama nani, maana mliyemshitakia, kutokana na jina,
mtu mwenyewe, kiukweli hayupo hapa, je mimi ndiye huyo mkuu wenu? Jibu ni
hapana, sasa je mimi nashitakiwa kama nani na kama mnanishitakia mimi kama
mhalifu, basi mfuate taratibu za kisheria, na hiyo itakuwa kesi nyingine sio
hii hapa....’akasema kwa kujiamini, na akaendelea kuongea kwa mbwembwe
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, tuwaulize hawa wanaoshitakii
watu bila utatibu, je ushahidi huo walioleta unanihusu mimi au huyo mshitakiwa
waliyemtaja, au huyo mliyemtaja hapo kama mshitakiwa ni mimi, maana uthibitishe
wa kitaalamu unaojulikana kimataifa umethibitisha kuwa sio mimi, kuna mtu
anapinga DNA test?’ akauliza mshitakiwa akionyesha kujiamini...
Wakati anaongea hivyo , alikuwa hajamuona yule mtu
aliyeingia na Inspecta Moto, lakini sasa akamuona, na sauti ile ya kujiamini
ikafikia, akasema;
‘Niambieni mimi ndiye huyo mhalifu mliyemtaja hapo, au
mnamshitaki nani, akawa sasa anamuangalia yule mtu aliyekuwa karibu na Inspecta
Moto kwa macho ya chuki.
‘Tunakushitakia wewe kama muhalifu, uliyehusika na
matendo maovu ikiwemo ya kuongoza kundi haramu, mauaji, na
udanganyifu...’akasema Inspecta Moto akisogea pale aliposimama muendesha
mashitaka. Na muendesha mashitaka akadakia, na kusema;
‘Umeshitakiwa wewe , kwa vile wewe ni mhalifu kutokana
na makosa hayo yaliyoainishwa, kutofautiana kwa jina sio sababu, tunachoangalia
kwa sasa ni muhusika mwenyewe, ambaye kapatikana na ushaidi utathibitisha hilo,
na mhalifu mwenyewe ni wewe uneyeongea?’ akasema muendesha mashitaka
‘Na wewe unaongea hapa kama nani?’ akauliza mshitakiwa
akimuangalia Inspecta Moto
‘Kama msaidizi wa muendesha mashitaka...’akasema
Inspecta Moto, na hakimu akaona aingilie kati kwa kusema;
‘Hebu tuwekane sawa hapo, muendesha mashitaka na
msaidizi wako mnasema mumeleta ushahidi wa kesi dhidi ya mshitakiwa, lakini
mshitakiwa mliyemtaja kwenye hii kesi, ameshakana kuwa sio yeye, mumeshika yeye kimakosa, na ameweza
kuthibitisha hilo kuwa yeye sio huyo
mliyemshitakia, kwa uthibitisho wa
kipimo kinachitambulikana cha DNA,...sasa huo ushahidi mliouleta ni wa nani, na
kwa kesi ipi?’ akauliza hakimu.
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, kundi hili limeundwa na watu wajanja
sana, watu ambao wanatumia sheria, akili za watu, na ujanja ujanja kuhakikisha
mambo yao yanakamilika. Ushahidi huu utaonyesha mbinu zilizotumiwa na hawa watu
, huyu mshitakiwa akiwa kama kongozi, yeye ndiye mshitakiwa mkuu,
tutalithibitisha hili kwenye huu ushahidi, kwa jinsi gani anahusika....’akasema
Moto.
‘Lakini huyo
mliyemshitakia kwa ,maandishi, sio huyu kweli si kweli, …?’ akauliza hakimu.
‘Muheshimiwa hakimu ndiye huyu huyu, ….tutaona kwenye
huo ushahidi, huyu mtu katumia ujanja tu, nahapa anataka kuruka ili asionekane
ndio yeye, ukimuachilia leo akitoka hapa hatutampata tena ushahidi huo
utaonyesha kila kitu….’akasema Moto, na mshitakiwa akataka kupinga lakini hakimu
akasema;
‘Kwa vile muda umekwisha, na sioni sababu ya malumbano
zaidi, kama mna uhakika na huo ushaidi wenu, uonyesheni, lakini nawaonya kama
hautakuwa na hayo yanayohitajika, na kuwa na uthibitisho kuwa muhusika huyu
ndiye anayehusika, basi sheria itawaandama nyie..i,kwa huvi sasa nabidi kukiuka
baadhi ya vipengele ili kuokoa muda....’akasema hakimu.
‘Sawa muheshimiwa hakimu, tupo tayari kwa hilo, tunaomba
mtaalamu wa mitandao aje hapa atuwekee chombo kitakachowezesha sote kuona kila
kitu kwa uwazi zaidi….’akasema na mshitakiwa akawa kashika mdomo, huku akitoa kauli za kulalamika kuwa sheria
haifuatwi, lakini hakimu hakumsikiliza
na mara ushahidi ukatolewa kwenye bahasha
Mshitakiwa akaonekana akishika mdomo kwa mshangao,
hakuamini, na hapo akaanza kusema sema ovyo kwa sauti
‘Haiwezekani, kwanini umewapa hao watu, uliambiwa nini
uwape hao watu hicho kitu,….kwanini , haiwezekani…nitakuonyesha kazi yangu wewe
mtu, nikitoka hapa ujue wewe umekwisha.....’akawa anapiga kelele,, na kutaka
kutoka ile sehemu aliyokuwepo ya mshitakiwa, lakini askari wakamdhibiti……
Na ikafika muda wa kuangalia kile kilichokuwepo kwenye
huo ushahidi, watu hawakuamini, ...ukweli wote ukabainika, na ndoto za bwana
Diamu, zikafikia ukingoni , na hapo hapo mtu huyu akadondoka na kupoteza
fahamu.
Mwisho wa 'dunia yangu' ukafika......
NB: Kisa hapa ni kama kimekwisha, lakini hatuwezi kuachia hapa maana Maswali hapo ni mengi, tutakuwana sehemu mbili zitakazofuata ambazo ni hitimisho la hiki kisa likifafanua
kilichoonekana kwenye huo ushahidi wa kifaa cha komputa, kwa ufafanuzi
uliotolewa na Inspecta Moto mbele ya waandishi wa habari baadaye.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment