‘Kuna
maombi kuwa kesi iahirishwe kwa vile mashahidi wote hawajulikani wapi walipo,
lakini pia wengi wa watu wetu ukiwemo wewe ni majerehi, je wewe unasemaje?’
akaulizwa Inspecta Moto na msaidizi wa mkuu wake, walipokutana ofisini kwa
kikao maalumu.
‘Mkitaka
ushauri wangu,na ndivyo nionanvyo mimi, kesi iendelee kama kawaida, mashahidi
wapo na watapatikana zaidi, kwa hivi sasa siwezi kuwataja wengine, ila ni
muhimu mashahidi wetu wa awali wapatikane, hilo nalifanyia kazi siku ya leo
nina uhakika watapatikana tu, ilimradi wapo hai....’akasema Moto.
‘Mkuu
mwenyewe katoa hiyo taarifa kuwa kwa vile anaumwa ni vyema kesi hii
iahisrishwe, hataki kuwaingiza watu kwenye hatari zaidi, anahisi tunajionyesha
zaidi kwa maadui badala ya kufanya kazi kama askari kanzu, ...’akasema msaidizi
wake.
‘Kesi
hii ina mitihani mingi, tukiamua kuiahirisha kama watakavyo wapinzani wetu, tutakuwa
tumefanya kosa kubwa, na mimi sitakubaliana na hilo,…hawa wenzetu kila mwanya
kwako ni hazina, na kwa jinsi walivyojipanga
nia yao hii kesi hii ichukue muda mrefu, ili wahusika halisi wapotee, na jinsi
tunavyocehelewa kundi hili haramu linakuwa kubwa na baya zaidi, kwa uoni wangu,
mimi nataka kesi kesi hii iendelee, na ni vyema kila hatua ijulikane kisheria,
mahakamani...’akasema Moto
‘Hii
kesi ipo mikononi mwako, ulishapewa wewe jukumu la kuisimamia na ukahidi mbele
ya mkuu kuwa utaimaliza kwa haki na kwa sheria, na kwa hiyo ujue kama itakwenda kombo utawajibika
wewe...’akasema msaididzi wa mkuu
‘Kama
ipo mikononi mwangu , basi mimi nasema hivi kesi iendelee kama kawaida, mimi
nitaongoea na muendesha mshitaka, msiwe na wasiwasi na kuwajibika kwangu, nina
imani hii ndio njia muafaka ya kuwashinda hawa watu, vita iwe mahakamani, mbele
ya sheria....’akasema Moto.
Kikao
hicho kikaisha, na Inspecta Moto akandoka kuonana na muendesha mashitaka, na
wakati anaondoka, simu yake ikaingia ujumbe; akaona ujumbe huo hauna namba, na
maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa yakasomeka;
‘UNAKUMBUKA
UCHAFU WAKO....? huu hapa...’ kulikuwa na kibahasha cha kuashiria kuna picha au
video fupi...
Inspecta
hakuifungua ile bahasha, akaufuta ule ujumbe, mara ujumbe mwingine ukaingia
ukisema;
‘
KAMA UTAENDELEA NA HII KESI, TUTAKUCHAFUA, UTAADHIRIKA KUTOKANA NA UCHAFU WAKO,
SASA HIVI TUTAANZA KUTUMA KWA WATU WAKO
MUHIMU, FUNGUA HAPA UONE BAADHI YA UCHAFU WAKO..’kukawa na kialama
cha kifurushi, kuonyesha kuna video ya kucheza
Inspecta
hakutaka kuendelea kuusoma huo ujumbe
akaufuta, na kutoka kuendelea na shughuli zake, na ujumbe mwingine ukaingia,
ukisema;
‘Hata
kama hutaucheza huo ujumbe na kuona klichopo kesho angalia gazeti la udaku
utaona uchafu wako,kama onyo, na mengine mabaya yatafuata, tutahakikisha maisha
yako yanakuwa hayana amani...’hakujali, akatoka hadi kwa muendesha mashitaka,
Alipofika
alimkuta muheshimiwa huyo akiongea na simu, na alisubiri mpaka akamaliza, ndipo
akaingia na kukaa kwenye sofa, hakukaa kwenye meza ya mongezi, na muheshimiwa
huyo akaonyesha uso wa mshangao, na bila kusema jingine, akauliza;
‘Unasema
kesho tuendelee na kesi yatu kama kawaida, hao mashahidi wapo wapi?’ akauliza
muheshimiwa huyo
‘Nina
shahidi mmoja ambaye nahisi tukimsimamisha, yeye atakuwa kawakilisha mashahidi
wote....’akasema
‘Ni
nani,.... docta Cheza....?’akauliza muendesha mashitaka
‘Kwani
huyo docta yupo?’ akauliza Moto akifunua macho ya mshangao.
‘Kamtibia
mkuu wako wa kazi , nimepewa taarifa na watu wangu, nikaona ajabu, ina maana
watu wako wanafanya kazi gani,?’ akauliza muendesha mashitaka kwa sauti ya
ukali kidogo.
‘Hilo
hata mimi nimelisikia hapa karibuni, hii ni kuonyesha kuwa kumbe hao watu wapo,
na wamefichwa mahali...inanipa shida sana kuliweka hilo akilini, kwani
nakumbuka kwa macho yangu mwenyewe aniliona watu wamelala hawajitambui pale
kwenye lile jengo kabla ya mlipuko na nilijua ndio wao...’akasema Moto.
‘Uliwaona
sura zao...?’ akaulizwa
‘Hapana,
ila mavazi yao, ...’akasema
‘Kwa
vipi, mavazi yao yanawezaje kukutambulisha hao watu?’ akaulizwa
‘Siku
ile ya tukio, nilifika maeneo ya makaburini, na niliwaona hao watu wakifika na
magari yao, na mavazi yao, ambayo ndiyo yaliyonitambulisha kuwa wale waliokuwa
wamelala pale sakafuni walikuwa ndio hao mashahidi....’akasema
‘Kwahiyo
kuna mchez ulichezwa hapo, viini macho....’akasema muendesha mashikata
‘Naona..na
karibu wanipate, ...nilishaamini kuwa hao watu wamekufa kwenye hilo jengo, na
nia yao ni kutaka nitambue hivyo...’akasema Moto, na muendesha mashitaka akatoa
simu yake na kupiga namba
‘Ngoja
niongee na mtu kwenye hospitalia anapotibiwa mkuu wako, nihakikishe
kitu....’akasema
Muendesha
mashitaka akapiga simu kwenye huko hospitali
, na kuuliza maendeleao ya mkuu wa Inspecta Moto, akaambiwa hajambo kiasi, akauliza ni nani
aliyemshughulikia akaambiwa ni Docta wa hiyo hospitali.
‘Docta
gani, hana jina?’ akauliza na simu ikakatika.
Muendesha
mashitaka akamgeukia Inspecta Moto na kusema;
‘Kwanini
huyu mtu kakata simu, ..?’ akauliza
‘Anataka
kuuliza ajue ni kitu gani cha kusema, na ukimpigia tena atakuja na jibu
jingine,....muhimu kuwatafuta hawa watu, kuna sehemu wamefichwa....’akasema
Moto
‘Ina
maana hawa watu wapo wanatuchezea akili yetu...?’ akauliza muendesha mashitaka
kwa hasira
‘Ndio
maaana nataka kesi hiyo iendelee ili hakimu ajue kuwa hao watu wapo, ila kwa
mbinu mbali mbali wamefichwa kinamna, mwanzoni tuliambiwa wametekwa nyara,sasa
watasema nini..amri itolewe wakatafutwe wakamatwe....’akasema Moto
‘Sioni
haja ya kusubiri amri ya mahakama, hili lifanyike haraka
iwezekanavyo...’akasema muendesha mashitaka kwa hasira.
***********
Muendesha
mashitaka akapiga simu polisi, na kutoa amri kuwa mashahdii wote watafutwe,
kwani wapo na wakamatwe haraka iwezekanavyo, na haikupita ,muda, simu kutoka
kwa mkuu ikapigwa kwa muendesha
mashitaka, ikisema, kuwa kesi iahirishwe.
‘Kwanini
mkuu,...kutokana na mtu wenu anayesimamia uchunguzi anasema kila kitu kipo
tayari, sasa kwanini tuendelee kusubiri....?’ akauliza muendesha mashitaka.
‘Lakini
hajanifahamisha hivyo,...mimi nijuavyo, nikuwa mashahidi wote wanaohusika,
hawapo, wamepotea, sasa iweje tena, kesi iendelee kuna mashahidi wengine?’
akauliza
‘Hao
hao watapatikana, ..na hata wasipopatikana wao, bado ana mashahidi wengine
wanaoweza kuendeleza kesi kuliko kuahirisha...’akasema muendesha mashitaka
‘Nimesikia
pia kuna amri ya kukamata watu, hilo agizo limetoka kwa nani?’ akauliza mkuu
huyo
‘Limetoka
mahakamani...’akasema muendesha mashitaka
‘Hakimu
gani aliyetoa agizo hilo, bila ya mimi kuhusushwa.....?’ akauliza
‘Hakimu
anayeendesha hii kesi mkuu, na hata hivyo, tuliona tusikusumbue kutokana na
hali yako ilivyo, mkuu...’akasema muendesha mashitaka.
‘Ni
kweli, hali yangu ilikuwa mbaya, na hata sijaamini kuwa nipo hai, lakini bado
wangeliweza kuja kuniambia muendelezo huo wa kesi, mimi sioni haja ya kukamata
watu, na je mna uhakika kuwa hao watu wapo,..msiwasumbue familia zao, maana
hizo familia hazina makosa...’akasema
‘Ina
bidi tufanye hivyo, kwani familia hizo
zinaweza kufahamu wapi walipo hao ndugu zao, au hao watu kama wamejificha
wakisikia familia zao zimeshikiliwa watajitokeza...’akasema muendesha
mashitaka.
‘Hizo
ni mbinu za kitoto...hilo mimi siliafiki, na huyu Inspecta Moto yupo wapi,
nampigia simu hapokei?’ akauliza
‘Anashughulikia
msako wa hao mashahidi mkuu...’akasema
‘Ok,
nitawasiliana naye, ila agizo la kukamata familia za wahusika, lisitishwe,
hatuwezi kutumia nguvu kwa kitu kama hicho, kuna mbinu nyingine za kuwapata hao
watu bila kuisumbua jamiii, na kwaa jili hiyo tarehe ya kesi hiyo ibadilishe
hadi hapo tutakapokamilisha ushahidi na mashahidi, sitaki kazi za aibu....’akasema
na kukaat simu.
Muendesha
mashitaka, akatulia kidogo, akataka kumpigia Inspecta Moto simu, na kabla
hajafanya hivyo, simu yake ikaanza kuita, na aliyekuwa akipigia alikuwa
Inspecta Moto,
‘Wakuu
wako wanakutafuta...’akaanza kusema
‘Nitakwenda
kuonana nao, nimeshapata huo ujumbe,...ila napenda kukufahamisha kuwa
tumewakamata baadhi ya mshahidi wetu...’akasema
‘Mumewakamatia
wapi wapo salama.... ?’ akauliza muendesha mashitaka kwa hamasa.
‘Hutaamini
wapo hapa kwa docta Chize kama wagonjwa waliolazwa....’akasema Moto
‘Wagonjwa
na docta Chize mwenyewe?’ akauliza
‘Docta
Chize hayupo, ....na tunahisi anataka kukimbilia nchi za nje, lakini tuna watu
wetu waaminifu uwanja wa ndege hawezi kupita, ......’akasema
‘Kazi
nzuri, nina imani sasa kesi inaweza kuendelea......,’ akauliza
‘Ila
kwa hali waliyo nayo, siwezi hata kuongea nao, ni kama mateja, wamepigwa
masindan ya usingizi, nimewaamrisha madakitari wa hapo wahakikishe, hali hiyo
inaondoka, la sivyo, hospitali hiyp inafungwa, na sasa hivi hospitali hiyo
isimamishwe, lakini....wanaonekana kutokujali, sijui wana kiburi gani hawa
watu....’akasema Moto.
‘Mkuu
wako umemuona?’ akauliza
‘Bado
yupo chumba cha wagonjwa wasiotakiwa kusumbuliwa, nahisi hao watu wanajiamini kwa vile mkuu wangu anatibiwa
hapo, lakini hilo sio tatizo sana , sheria ni sheria.....’akasema
‘Ngoja
hilo nilifanyie kazi, nahisi kuna tatizo, kuna jambo limejificha hapo, natumai
hata wewe ueliona, lakini kwanini tuandikie mate wakati wino upo,…..ngoja
niongee na mkuu wako moja kwa moja, nisikie atasemaje’akasema
‘Mimi
naona sio muda wa kuongea na mkuu wangu wa kazi, kwa vile anaumwa, watu wapo wa
kufanya kazi yake, isitoshe, walishanikabidhi mimi hii kazi…’akasema Moto
‘Kwahiyo…..?’
akauliza Muendesha mashitaka, akitaka kuongea zaidi, lakini moto akamkatisha
kwa kusema
‘Kwanza
ni muhimu sana, hawa watu kuwaondoa kwenye hii hospitali, na tuwapeleke kwenye
hospitali nyingine, tukiifungulishia
mashitaka hii hospitali, kwa kosa hili…..’akasema
‘Kwa
kosa gani?’ akauliza muendesha mashitaka
‘Waliwapokeaje
hawa watu, najua watasema hao watu wameletwa kwao,. Kwa matibabu, na nani,
nimejaribu kumuuliza msaidizi wa hii hospitali, yeye kasema hakuwepo, na mkuu
wake wa kazi hayupo, hajui ni nini kilitokea..kuna kutupiana mpira, kwahiyo
tukuchukue sheria, hospitali ishaitakiwe, na wawekezaji wake….’akasema Moto.
‘Hapo
uwe makini..ngoja tuone tutawachukulia hatua gani, lakini kwanza tushughulikie
hili la kesi yetu, tusichanganye mambo…’akasema muendesha mashitaka.
‘Hawa
watu ni mashahidi muhimu wanahitajika kuwa tayari kuongea, kwa hivi sasa
hawajiwezi, ni muhimu wachunguzwe vyema, tuone kama hawajapigwa madawa ya
kulevya, kama imefanyika hivyo, tutazidi kuwa na ushahidi wa kuweza kuifunga kabisa hii hospitali...’akasema Moto
‘Ok,
hilo ni sawa, na…naona hapa kwenye makabrasha, hiyo hospitali inamilikiwa na
Chize kwa hisa kubwa, lakini ina wawekezaji wengine, ...mmojawapo ni huyu eeh, ina maaana
hata huyu marehemu kawekeza hapa, huyu aliyekuwa mumiliki mkuu wa hoteli ya
Paradise...mmh, naanza kuitamani hii kesi, nahisi kuna madudu humu
ndani...’akasema muendesha mashitaka.
‘Unaonaeeeh,...kumbe
ulikuwa hujapitia taarifa yangu yote, kuna mambo mengi sana yamejificha nyuma
ya pazia, utakuja kuyaona mwenyewe kwenye hii kesi, na utakuja kugundua kuwa
kuna waheshimiwa wengi wamewekeza kila kwenye hayo makampuni ya hawa watu
tuliowashika,ndio maana hao watendaji wanajiamini, wanajua wana godfather juu...’akasema Moto.
‘Unajua
nilichukulia hii kesi juu juu, nikijua ni zile kesi zenu za hapa na pale,
lakini sasa naanza kuiona jinsi gani kesi hii ilivyo, ni kesi ngumu,na itazidi
kuwa ngumu kama kuna waheshimiwa ndani yake….sijui lakini nahisi siasa zitatusumbua
sana kwenye hii kesi..ila nikuambie kitu, hapa hapendwi mtu, sheri ndio itaongea
tu, mimi nipo pamoja na wewe, ...sasa kwanza nataka nimjue vyema huyu marehemu...asili
yake, katokea wapi huyu mtu...’akatulia
‘Kwenye
ripoti niliyokupa utamuona vyema, japokuwa hutaamini hakuna picha yake….kitu
cha ajabu kabisa….’akasema Moto.
‘Na
huyu mama yake, inaonekana alikuwa na nguvu fulani za utajiri, utawala eeh,..unajua
bado najiuliza, kwanini huyu mama, masikini sasa na yeye ni marehemu, kwanini alidai kuwa, mtoto wake yupo
hai,...nahisi kuna jambo ndani yake,.....nataka kila kitu kuhusu huyu mama, na
je mtoto huyu alikuwa vipi na wazazi wake, hasa baba yake, nahisi kuna kitu
kurithi hapa, huenda chimbuko zima la hii familia likatupa jibu , ....’akatulia
halafu akasema
‘Pia
nataka taarifa za hawa wawekezaji wote wa hiyo hoteli, na miradi yote ambayo,
marehemu alikuwa na hisa nazao, pia nataka taarifa zote za hawa mashahidi
nataka kujua hisa zao , makampuni yao....na..na...kila kitu chao, unaweza
kunipatia hiyo taarifa, kabla ya kesi yenyewe.....?’ akauliza
‘Yote
hayo utayapata.....’akasema Moto akionyesha hamasa
‘Utayapata
kabla ya hiyo kesi..usijali muheshimiwa…’akamalizia kuongea maneno hayo wakati
alishakata simu.
NB:
Sasa naona tuingie kwenye hitimisho ndani ya mahakama, sijui wenzangu mnasemaje
WAZO LA LEO: Asili ya mtu, tabia ya mtu, inaweza ikawa sababu ya uadilifu au ufisadi wa huyo mtu katika utendaji wake
wa kazi, hasa akiwa madarakani na hili tuliangalie pale tunapochagua viongozi
wetu, kiongozi ni lazima achunguzi , alipotokea, utoto wake, maendeleo yake
shuleni, na maisha yake na wenzake shuleni, au katika jamii, hadi hapo
anapokuja kwako kukuomba kura, Manen0 mazuri sio tija ...tija ni ukweli wa hayo
maneno yanayotoka mdomoni mwa huyo mtu
No comments :
Post a Comment