‘Yah, nipe….’akasema
, na alipoishika simu yake mkononi, akaanza kutafuta namba anayoihitajia na
kuanza kupiga kuwasiliana na watu wake, lakini kila aliyempigia simu hakuweza
kumpata, akajikuta akiguna.
‘Mhhh..hapa sasa
kuna tatizo.’ Akasema akiendelea kumpigia mwingine na mwingine maka akawamaliza
watu wake muhimu.
‘Mhh, vipi tena
hawapatikani?’ akauliza Yule binti, mdada
Tuendelee
na kisa chetu….
*************
‘Hawa
watu hawapatikani kabisa, au kuna baya limewakumba….mmh, sijui nimpigie nani
kwasasa, wengi wa hawa watu wetu siwaamini sana, ok, …., ngoja nimpigie mkuu
wangu wakazi, sijui kama karudi kutoka mapumziko ya muda….’akasema na kuanza
kuitafuta namba yake….
Alipoipata
akapiga, simu kwanza iliita, lakini ikakatwa….., akajaribu tena, ikawa sasa
haipatikani, akajaribu tena na tena lakini haikupatikana kabisa, akatulia
kuwaza, akataka kusimama,lakini akasita, akasema;
‘Ni
nani alinileta hapa hospitalini?’ akauliza.
‘Mimi
sijui, mimi nimekuja, niliposikia umelazwa hapa, sikuuliza hilo swali, muhimu
ni kukuona wewe…’akasema
‘Ni
nani alikuambia kuwa nimelazwa hapa?’ akauliza.
‘Ni
baba alikuja kunitembelea kuona maendeleo yangu ndio akakutana na taarifa hizo
za mabomu, kuna siku alikuja kwako akakukosa, akapanga aje jana, ni jana
vile...ndio akapata taarifa kuwa yamekukuta hayo….akanipa taarifa na mimi
nikamwambia ni lazima nije nikuone….’akasema.
‘Oh,
nashukuruni sana kwa moyo wenu huo wa upendo, sasa huyu docta yupo wapi?’
akauliza.
‘Alitoka
muda ule ule kabla hujazindukana, na alisema kama kuna dharura nimpigie simu, au
nimuite…’akasema.
‘Basi
tafadhali naomba ukaniitie….’akasema na Yule binti akasimama na kuondoka,
Inspecta hakuchukua muda, alismama na kuanza kuvaa nguo zake, alipohakikisha
kuwa kila kitu kipo sawa, akasogea dirishani, madirisha ya hapo kwenye hiyo
hospitali ni ya viyooo, unaweza kulifungua lote, akafungua na kuangalia nje,
akaona hakuna mtu, akarukia nje.
*********
Inspecta
Moto, alitembea kwa haraka hadi sehemu wanaposimamisha mabajaji, akaingiza
mkono mfukoni, akaona pesa zake bado zipo, akamuambia mwenye bajaji...
‘Unaweza
kunipeleka Msasani, makabaurini, ….’akasema.
‘Msasani
makaburini, mhh, ni makaburi ya eneo gani, mmh….ni yale ya karibu na baharini?’
akauliza akionyesha wasiwasi.
‘Yah, huko
huko…’akasema Moto.
‘Mhh, kule
tunaogopa hata kwenda, maana siku za karibuni kumebadilika kweli, kumekuwa ni uwanja
wa mabomu, lakini twende tu, nitakuacha sehemu karibu na eneo hilo mimi sitafika
huko ndani maana hakuruhusiwi watu kufika kwa hivi sasa….’akasema.
‘Hamna shida
, wewe twende utaniacha sehemu unayooona wewe ni salama kwako…’akasema na
wakaondoka, huku dereva akiuliza maswali ambayo Moto hakutaka kuyajibu, alikuwa
na mambo mengi kichwani;
‘Kwanini
wewe unakwenda huko, wakati kuna tishio, mbona umefungwa mkononi, ulipata ajali
nini, naona kama uliungua, unakuwa kama hao waliookolewa kwenye huo moto, nasikia
waliungu sana, nasikia mpaka sasa wengine hawajiweza hata kuongea….’akawa
anauliza na kuongea, lakini Inspecta alikuwa kimiya, akilini akawa anajiuliza
imekuwaje taarifa kama hizo zizagae haraka mitaani.
Walipofika
karibu na bara bara inayoingia kuelekea makaburini,yule dereva akasimamisha gari,
na kusema;.
‘Mimi
nitaishia hapa bosi wangu, huko ndani sifiki,… unaona kule, wapo wenyewe,
wanacheza na vitu vya moto, wameshazungushia uzio wa hatari, kwahiyo safari
yetu imeishia hapa…’akasema.
Inspecta akamlipa
huyo jamaa pesa yake, na Yule jama bado akawa anamchunguza sana Inspecta kwa
makini, lakini Inspecta hakumjali, yeye akaanza kutembea kulekea huko ndani. Na
akachukua simu yake akapiga namba.
Inspecta
hakugeuka nyuma, alitembea kuelekea eneo
la makaburini hadi kwenye ule uzio wa hatari,…akageuka kuangalia wapi walipo
askari, bila kujali akauruka ule uzio , na alipofanya hatua chache mbele
akatokea askari akiwa na silaha yake mkononi na vifaa vyote vya kinga mwilini,
ni mmoja wa maaskari wanaolinda hapo, Inspecta Moto akamuonyesha kitambulisho,
na mara akatokea askari mwingine akiwa kavalia kiraia tu, akasema;
‘Mkuu vipi
unaendeelaje, maana mimi nilikuwa mapumziko, nilipofika nikakutana na hili
jukumu, nasikia ulikuwa katika hali mbaya sana, mbona umerudi huku tena mkuu,
wewe kapumzike tu mkuu, sisi tutahakikisha mamb hapa yapo shwari…’akasema
askari mmoja anayemfahamu.
‘Hebu
niambia mumegundua nini hadi muda huu?’ akauliza.
‘Hakuna
zaidi mpaka sasa, jengo kama unavyoliona hapo, limeungua lote, hakuna
kilichoweza kuokolewa, wasiwasi wetu ni kuwa huenda bado kuna mabaki ya mabomu
chini ya ardhi, ndio maana tunaendelea kulinda hapa…’akasema.
‘Kuna watu
nawatafuta,…..’akatulia, halafu akawataja majina.
‘Mhh, mkuu
hao jamaa hali zao ni mbaya, walikuwa kama wewe, nashangaa wewe umeweza kuja
hapa, kwa taarifa nilizo nazo, wengine bado hawajazindukana, nasikia mabomu
hayo yana sumu, au madawa ya kulevya,ni mabomu ya aina yake ambayo
hayajajulikana yametengenezewa wpi, au yametengenezwa na mchanganyiko gani…..’akasema.
‘Ok, kwahiyo
kwa jinsi unavyojua wewe,…mmh’ akatulia kwanza akiangalia kwa mbele, kuna watu
walikuwa wakipite eneo la baharini karibu na lile boti, ambalo bado lilikuwa
hapo;
‘Kwani
wakati tukio hili linatokea wewe ulikuwepo?’ akaulizwa.
‘Hapana mimi
nilikuwa mapumziko, nimekuja baadaye wakati kumeshaanza kutulia, kwahiyo jinsi
ilivyotokea mimi sikuona…na hakuna cha zaidi tulichoambiwa zaidi ya kuendeleza na
ulinzi hapa….’akasema.
‘Yah, naona
hutaweza kunisaidia kitu, maana kulikuwa na watu ndani ya hili jengo, nilitaka
kujua kuwa waliweza kuokolewa au ndio wameteketea humo ndani wote, na kule
karibu na bot kuna nani wapo huko….?’ Akauliza.
‘Nijuavyo
mimi, jengo hili ni kama halishi watu, yupo jamaa mmoja anafika mara chache na
kuondoka, wanahisi huenda ndiye mumiliki, lakini tukio likitokea hakuwepo, na
uanuliza kule kwenye boti, wapo watu wa usalama, hakuna shida mkuu…’akasema.
‘Wewe umepata
wapi hizo taarifa na ulikuwa mapumzikoni?’ akauliza.
‘Mkuu,
ukikabidhiwa lindo ni lazima upate taarifa zote, vipi mkuu, naona ajali
imekupoteza kumbukumbu nini..pole sana mkuu…ila….’akatulia kidogo.
‘Nilipofika
ili kutimiza wajibu wangu, nikajaribu kupiga ndogo ndogo, huwezi jua, nikawa
nawahiji baadhi ya majirani, watu wanaoishi eneo hili, nimejaribu kuwahoji
baadhi tu, wakasema hivyo, kuwa ni kama jengo lililohamwa,…’akatulia.
‘Wanasema
kuna jamaa mmoja anaonekanaonekana, huyo
jamaa wanasema huenda hata yeye sio mwenye jengo, ili kaamua kuishi hapo kwa
kubahatisha, ili awe anawahi kwenye shughuli zake, na hata wakati moto
unatokea, sizani kama alikuwemo humo ndani, kama unavyoona jengo halijulikani
tena, kama kulikuwa na nyumba…’akasema.
‘Kwahiyo
ulipowahoji hao watu walisema hata hiyo jana, hakukuwepo na watu waliingia humo
kabla ya tukio?’ akauliza.
‘Yah,
wamesema hapakuwepo na watu humo ndani,…wanasema kwa vile ni sehemu haishi mtu,
hakuna aliyekuwa na shauku ya kuangalia, na bomu la kaburini lilipotokea, watu
wakakimbia, kwahiyo hakuna anayejua kilichotokea, kama kulikuwa na watu au la…’akasema.
‘Ahh, ok…’akasema
Inspecta alipoona anapoteza muda, lakini huyo askari kanzu akaendelea kusema;
‘Nimesikia
kuwa nyie wakati mnaingia mlitupiwa nje na upepo,…inanishangaza ni upepo gani
huo mkuu, …?’ akauliza.
‘Nani
kakuambia ni upepo…hata mimi sijui,ndio tunachunguza hivyo…’akasema Inspecta
‘Kwa ujumla
mimi nilichopata kwa watu ndio hivyo, hakuna maelezo kuwa kulikuwa na watu humo
ndani, na hata wachunguzi wetu, walijaribu kuchunguza, kwa taarifa nilizopewa,
hawakuona dalili za maiti, au mabaki ya watu kuwemo humo ndani mkuu…’akasema
‘Ok, basi
ngoja nipitie mara moja nione kama kuna dalili yoyote ya kitu ninachokihitajia,
maana hizi taarifa kwasasa zinaanza kuchakachukuliwa, tutaona mwisho wake
itakuwaje, ….’akasema huku akitembea kuelekea sehemu ya gofu la jengo,…
‘Mkuu hakuna
kitu kabisa, nimepita kila sehemu , sijaona kitu cha kusaidia, ila wewe nenda
kaangalie, na kama unahitajia msaada nije tusaidiene huenda tukapata chochote,
ila sizani….’akasema na Moto hakumjibu akaelekea eneo hilo, na Yule askari
mwenzake simu yake ikapigwa, akawa anasikiliza na kumuacha Inspecta Moto
akielekea kwenye tukio akiwa peke yake.
Alijaribu
kuangalia upande ule ambao anafahamu kulikuwa na chumba cha pili, lakini
hakuona dalili na kitu kama miili, kulikuwa na mabaki mabaki ya takataka,
lakini hakuna mlunduikano wa kuashiria mwili wa mtu au kitu kama hicho, au
mabaki ya mifupa…akajaribu kuchunguza zaidi, hakuna kitu.
‘Ina maana
hao watu walitoka,..haiwezekani,..niliwaona kwa macho yangu, watu wakiwa wamelala sakafuni, sizani kama walikuwa
na uwezo wa kutoka kwa haraka vile bila kuonekana…’akasema akizidi kuchunguza
zaidi.
Na wakati
anaendeela kuchunguza huku na kule, akaona sehemu yenye matofali yaliyojipanga kinamna,
na kutengeeza kama boksi, akavutiwa na sehemu hiyo, akaisogelea, akainua yale
matofali, na kwa chini ya hayo matofali, akaona kitu…simu….
Akainama
kuikota, kwa uangalifu, akasita, akachukua leso yake, akainama kuchunguza
vyema, akaigeuza akihakikisha haigusi kwa mkono wake bila kinga, ilikuwa sio
simu ni ‘flash’ za kuwekea kumbukumbu za komputa, ni zile flash kubwa kama simu…
Akawa na
uhakika kuwa sio kitu cha hatari, akiwa na leso yake vyema mkononi akaikota ile
`flash’ na akasimama na kugeuka huku na
kule akaona mfuko mdogo mweusi wa plastiki, akaiweka ile flash ndani ya huo
mfuko, na kuiweka ndani ya mfuko wake wa suruwali…
‘Ni ajabu
kabisa, haikuguswa kabisa na moto, inaonekana ilidondoka baadaye, au kuna mtu
alikuwa nayo mfukoni ikadondoka, na ilikuwa sehemu ambayo haikuweza kuguswa na
moto.
Akakagua
kila mahali na aliporizika, akaanza kuondoka, na wakati anatoka eneo hilo, Yule
asksri mwenzake akaja kwa haraka na kumuuliza;
‘Kuna kitu
chochote umekiona…?’ akauliza
‘Kama kitu
gani?’ aakuliza Moto
‘Chochote
cha kuweza kusaidia,…maana macho ya wawili sio sawa nay a mmoja…’akasema
‘Sijaona
kitu ….’akasema Moto
‘Ok, hata
mimi sijaona chochote, wanasema tujaribu kuangalia kila kona, kama kuna kitu
chochote kinachoweza kusaidia, iwe simu, au chombo chochote cha komputa, hawa
watu ni wataalamu sana….’akasema
‘Nani kakupa
maagizo hayo?’ akauliza
‘Msaidizi wa
Mkuu…..’akasema
‘Ok, hamna
shida, ndio kazi yetu kufanya hivyo, …’akasema na mara simu ya Inspecta Moto
ikawa inaita, akaipokea bila kuangalia mpigaji , akasema kwa haraka..
‘Nani
mwenzangu…?’ akauliza
‘Ina maana
huna namba yangu..?’ sauti ya msaidizi wa mkuu wake ikasika hewani
‘Hii namba
ni ngeni,… mkuu, sikuwa nimeihifadhi kwenye simu yangu…’akasema
‘Ni hivi,
mkuu hali yake ni mbaya, wakati wanakuja kutoka nyumbani, kama unavyojua kuwa alikuwa mapumziko mafupi
ya kumuuguza mzazi wake..sasa wakati anarudi kuwahi kuja kuwa ansi kwenye
uwanja wa mapambano, wakiwa njiani akapatwa na ajali, na hali yake ni mbaya
yupo chumba maalumu cha wagonjwa mahututi, ….’akasema.
‘Oh, hiyo
ajali imetokea lini..ina maana ni siku hiyo ya tukio?’ akauliza.
‘Ni jambo la
ajabu sana, ndio, ni siku hiyo hiyo yalipokuwa yakitokea mabomu, ni kama hawa
watu walijiandaa kuhakikisha wanavunja nguvu zote….inavyoonekana hata hiyo
ajali imepangwa, japokuwa hatujathibitisha, mpaka mkuu atakapoweza kuongea,
sasa hivi hajiwezi kwahiyo hatuwezi kujua lolote …..’akasema.
‘Kupangwa
kwa vipi?’ akauliza Moto.
‘Wewe huoni
hilo, hayo mabomu yalipangwaje, yalipangwa kinamna, mnataka kukimbili ahuku,
huku linalipuka , mnakuwa mumechanganyikiwa, hamjui muende wapi,…hata hiyo
ajali ilitokea muda huo huo, huoni kuwa
kulikuwa na njama za kumuua,..’akatulia kidogo na Inspecta Moto akwa kimiya,
‘Anyway, uchunguzi unaendelea, cha muhimu
ni nyie mpone haraka muingie kazini, maana hawa watu wanajiona wameshinda,
hawajashinda bado, ni lazima tuhakikishe wote wamepatikana vipi wewe mbona
nasikia umetoroka hospitalini…?’akauliza.
‘Umesema
mkuu wetu kalazwa wapi?’ akauliza swali kabla ya kujibu swali la mkuu wake.
‘Hospitali
ya Docta Chize, mara nyingi huwa anatibiwa huko..’akaambiwa.
‘Docta
Chize, kwani huyu docta yupo?’ akauliza.
‘Yah, ..yupo
kwani alienda wapi?’ akaambiwa, na
kuulizwa, na simu ya Inspecta moto ikakata mawasiliano, akaangalia, akaona ni
mtandao umekata.
‘Hii ni
ajabu kabisa, simu yangu haina tatizo la mtandao, ni kitu gani hiki,
…..’akasema na kuzima simu yake halafu akaiwasha tena..na alipoiwasha akaona
ujumbe unaingia kwenye simu yake, akausoma, ulikuwa na maneno machache tu
‘BADO
WEWE….’
WAZO LA LEO: Utawala bora ni pamoja na kuwa
karibu na wale unaowatawala, ukahisi uwepo wao, na shida zao. Hutaweza kuwajua
na kujua shida zao, kama utakuwa mbali na watu wako, ukajiwekea mazingiza ya
juu kuliko ya wale unawatala, huo utakuwa ni ubinafsi. Ni sawa huenda ni lazima
mtawala awe na hali tofauti na watawaliwa, lakini utajuaje shida zao, kama
hujapatwa na hiyo shida, je mwenye shibe kweli anaweza kumtambua mwenye
njaa..najiuliza tu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment