‘Huyu mtu hafanani kuwa mvuvi….kwa jinsi anavyoonekana japokuwa kavalia hayo mavazi, lakini wavuvi tunawafahamu hali zao bwana,..huyu bwana hata, hafanani hivyo….labda ndio hao wavuvi matajiri,...
'Hata jana tu, nilimuona akiwa katika hiyo hali, kavalia koti,akionekana na wasiwasi, akaingia humo ndani na sijamuona akitoka, kama kawaida yake, unamuona akiingia lakini akitoka humuoni,…’akasema huyo mtu
Inspecta aliposikia hivyo, akawa na hamasa ya kuonana na huyo mtu, hata hivyo, hali ya hiyo nyumba ilionekana kuwa hatarini, kulikuwa na kila dalili kuwa kuna moto ndani ya hiy nyumba na usipodhibitiwa unaweza kuwa mkubwa ukanguza hiyo nyumba na nyumba za jirani...
Amri ikatolewa...,
'Tuvunje tuingie....'
Moto akiwa na kikosi chake wao walibaki nyuma, wakawaachia wahusika wa moto na milipuko kama mabomu watangulie mbele, mlango mkubwa wa kwanza ukavunjwa, na watu wakaingia ndani.
Mwanzoni watu walihisi labda ni lile bomu la makaburini ndilo limeleta athari hadi hapo, labda kuna kipande cha mabaki ya bomu kilidondokea humo ndani na kuleta moshi, na ukumbuke watu wengi walikuwa wamelikimbia hilo eneo, na wachache sasa ndio walikuwa wakirudi rudi, kuona kama kuna amani.
Wakaingia kikosi cha Zima moto na askari wa mabomu, na Inspecta Moto akawafuatia kwa nyuma....
Mlango ulipovunjwa, tu, watu wakakaribishwa na harufu mbaya, ilikuwa ni harufu ya gesi, na haikupita muda ghafla mlipuko mkubwa ukasikika…….
Tuendelee na kisa chetu
**********
Tulia
utazidi kujiumiza….’
Inspecta
Moto alifungua macho huku akihema kama
mtu aliyekuwa akikimbizwa, na alipofungua macho alionyesha kuwa mwingi wa
wasiwasi, akainua mkono, akitaka kushika
kichwa lakini hakuweza ,mkono ulikuwa mnzito kuinuka, akakunja sura kuashiria
maumivu, halafu akainua mkono mwingine,
huo mkono ukawezekana kuinuka,na ndipo akaweza kushika kichwa , lakini badala
ya kugusa kichwa akaguswa kitu kingine, mmh, kichwa changu kina nini,mbona
kimefungwa...
Akafunua
macho na kuangaza huku na kule hakujua yupo wapi, akawa anahangaika, akahisi
kuna kitu kinamkandamiza miguuni, akakumbuka
ile ndoto, ndani ya ndoto hiyo alikuwa yeye na wakewe, alikuwa kaumia mguu,
mkono, na kichwa, majeraha hayo aliyapata kutoka kwa jitu moja la kutisha, linalomomonyoka
uso na kuwa na sura mbaya, …
Alipofika
kwa mke wake hakawa hajiwezi, mkewew akawa anamtibia hayo majereha na alikuwa
akitumia maji ya moto, yaliyokuwa yakiunguza sana, lakini kwa ajilii ya mumivu,
akawa anakataa kukandwa, akijua yatamzidishia...
Na
wakati mkewe akiwa anaendelea na hayo matibabu, kwa kupitia dirishani akaliona
hilo jitu, jitu lile sasa limezidi kuwa kubwa, linatoa cheche mdomoni, uso umekuwa mpana, na sura ya kutisha, sasa linataka kumuumiza hata mke wake, na kwa vile mkewe alikuwa kalipa
mgongo hilo jitu, alikuwa hajui ni nini kinachoendelea.
Inspecta Moto akawa anajaribu
kumuonyesha mke wake kwa ishara lakini mkewe
akawa haelewi, yeye akawa anaendelea kumkanda na maji ya moto, na katika
purukushani za kukataa kuendelea kuumizwa na maji ya moto, na kutaka kumuokoa
mkewe ndipo hapo akazindukana na kujiona yupo eneo ambalo hakujua yupo wapi..
Akawa
anahema kwa wasiwasi, na sasa akawa anajitutumua kuinuka, na mara sauti ikasema
‘Tulia,
utazidi kujiumuza.....?’ ilikuwa sauti ya kike ooh ni sauti ya mke wake, kumbe
ni kweli,sio ndoto , kumbe ni kweli ni mke
wake anamkanda, akajaribu kuinua kichwa
ili kumuangalia vyema, ...mmmh, kumbe sio ndoto, kumbe ni kweli, mke wangu yupo
name, akili ikawa inamuambia hivyo,
akatabasamu,....lakini macho mbona kazidi kuwa msichana, akawa anajiuliza, …akatabasamu
tena
Muda
ukawa unapita na macho yakaanza kuzoea,na ule ukungu wa giza, na uzito wa kukumbuka ukaanza
kuondoka, macho yakaanza kuona vyema, na akili ikaanza kujua kinachoendelea mbele
yake, akagundua kuwa sura iliyopo mbele yake sio ile ya mke wake...
‘Oh,
kumbe ni wewe tena, ..nilijua wewe ni mke wangu’akajikuta akisema
‘Mhh,
mke wako, jamanii `but’nakumbuka
uliwahi kunambia kuwa mke wako auwawa jamani,kwani mimi nafanana na mke wako....?’
huyo binti akauliza
‘Huafanani
na yeye moja kwa moja, lakini kisifa mnafanana sana....unanikumbusha enzi
nilipokutana na mke wangu kwa mara ya kwanza, alikuwa kama wewe,binti mdogo
mdogo mrembo, .....’akasema na Yule binti akatabasamu na kusema;
‘Mhh,
natamani ningelimuona huyo mke wako,..ana bahati sana,..’akasema
‘Kwanini?’
akauliza
‘Kumpata
mume kama wewe, ila mimi sipenzi kuolewa na askari...’akasema kwa haraka na
kuonyesha aibu, kama alilotamka halikufaa kutamkwa.
‘Kwanini?’
Moto akamuuliza kwa sauti kama ya ukali vile.
‘Nitaishi
maisha ya mashaka mashaka, angalia hali yenyewe ndio kama hii, kila mara upo
taabani,na kwa mfano ukichelewa kurudi kazini, unafikiri nitakuwa na amani
moyoni, nitakuwa naishi maisha ya mashaka mashaka, ...’akasema
‘Basi
ukiolewa na askari ndio maisha yako yatakuwa salama, maana mume wako anajua
jinsi ya gani ya kujilinda na kukulinda,
na kulinda taifa lako, na raia wake wema
unaona eeh, huyo ndiye mume anayekufaa unaonaje hilo...’akasema kama anauliza
na mara akahisi kichwa kama kinaanza kuuma tena, lakini akajikausha
‘Pole
sana, unajisikiaje, nakuona kama unakunja uso, kichwa inazidi kuuma?’ Yule binti
akamuuliza
‘Hata
sijui, kichwa kilikuwa kinauma sana, lakini cha ajabu nilipoanza kuongea na
wewe maumivu yamepotea, ni kama vile umenipa dawa, na ghafla tena kuna amumivi
kwa mbali...’akasema
‘Mhh,
jamani mbona sijakupa dawa….ngoja nikupe dawa, nimesahau kabia, kuna dawa niliambiwa
nikupe ukizindukana.’akasema.
‘Hapana
, usinipe dawa yoyote, hakuna maumivu tena….alisema hivyo akiwa anaogopa dawa,
kwani hakuamini dawa, alihisi zisije
zikawa zimetoka kwa hao jamaa .
Akili
ya Inspecta Moto ikawa anafunguka na kumbukumbu zikawa zinaanza kumrejea
vyema, akasema;
‘Najiuliza
nimekuwaje..nimefikaje hapa, hapa ni hospitali, nimefikaje hapa.., kwanini
mmmh, hata sikumbukia, ilikuwaje…kichwa sasa kinaanza kuleta matatizo, je watu
wote waliokolewa, na wale waliokuwa humo ndani....?’akajiuliza huku akijaribu
kutuliza akili, na mara kumbukumbu ndio zikaanzaa kujirudi kichwani kwake na
kuanza kukumbuka yaliyotokea,
************
Ilikuwa
wakati wamevunja mlango kuingia, na mlango ulipofunguka, kwanza waliweza
kuingia wataalamu wa moto na na silaha
zao tayari, Inspecta Moto, akawa nyuma yao akijua hilo sio jukumu lake kwa muda
huo,akawa anawaangalia wale watalaamu
wakitoa ishara kwa mikono, wakionyesheana ishara kuwa moto huo upo kwenye chumba cha pembeni kinachoangaliana na
ukuta unaozunguka eneo la makaburini ndipo moshi ulikuwa ukitokea na ufukutoa
ulikuwa mkali, na kila mmoja akageuka kuelekea huko
‘Lakini
nahisi kuna harufu ni ya gesi tusifungue huo mlango kwanza, hakikisheni kila mmoja kavaa kinga, vaeni
vifaaa vya kinga hiyo ya gesi, hiyo ni harufu ya gesi, rudini nyuma..’akawa anaonya kiongozi wao,
na mmojawapo aliyekuwa mbele alikuwa tayari keshaukaribia mlango, akawa
ameugusa mlango kwa silaha yake, kabla onyo hilo halijatoka, kumbe ule mlango
ulishaathirikia kutokana na moto uliokuwa ukitokea ndani, kwahiyo alipougusa
tu, ukamong’onyoka na hapo hapo ndio kukatoka hicho kizaa zaa.....
Loooh…..,
Iilikuwa kama upepo mkali wa kupuliza, hewa kali upepo mkali uliwazoa zoa watu
wote waliokwemo humo ndani na kutupiwa nje, na hiyo ndio ilikuwa salama yao,
kwani kama wangedondokea humo ndani, wote wangelikuwa ni maiti
Inspecta
Moto yeye wakati wataalamu hao wanakagua sehemu hizo, wakivaa vifaa vya kinga,
yeye, alikuwa nyuma yao, akiwaachia wafanye kazi yao. Yeye akawa anakagua
upande wa pili, kwani ule mlango ukifunguka unajikuta kati kati ya njia panda, kuna sehemu mbili mbele, moja ya kuelekea huko
moto unapotokea na sehemu ya pili, ni kwa upande ambapo hakukuwa na moto, na
huko ndipo harufu ya gesi ilikuwa inatokea sana
Ule
upande wa pili, akaona kama kuna mtu kwa kupitia kwenye upenyo wa mlango, na
wakati huo alishahisi hiyo harufu, akakumbuka taarifa ya kundi hilo kuwa kuna wataalamu
wa kila aina ambao wanaweza kutengeneza
silaha za ina mbalimbali, ikiwemo wa mabomu ya hewa, ...akajua hiyo inaweza
ikawa ni hewa ya bomu, sio hewa ile ya gesi inayjulikana, ni gesi maalumu
ambayo ikigusana na hewa hugeuka kuwa bomu, akashika pua kujihami, lakini kule
kwenye chumba cha pili alijua kabisa kuna mtu,...
Akakisogelea
kile chumba na hayo yalifanyika kwa haraka sana,, aliona kabisa kuna kitu kikitembea, akakisogelea kile chumba cha pili, akashika kiuononi, kuhakikisha
kama silaha yake ipo tayari, mkono
mwingine umeshikilia puani, akasogea hatua mbili za haraka, hadi pale kwenye
chumba akanyonga mlango, ..
Alimuona
jamaa akiwa kavalia vifaa mdomoni vifaa vya
kujizuia asizurike na alikuwa kasimama akiwa kampa mgongo mkononi alikuwa na
silaha, ya aina yake, hajawahi kuiona,
huyo mtu alionekana kama anataka kuruka kwa kupitia dirishani na kwa
chini pembeni yake kulikuwa na miili ya watu imelala sakafuni..
Inspecta Mot akajua asipomuwahi huyo mtu
atakimbia, haraka akatoa bastola, lakini ndio muda huo mlipuko ulipotokea, hata
hivyo aliweza kufyatua risasi, ambayo alikuwa na uhakika ilimjeruhi huyo jamaa
sehemu ya mkononi, na muda huo huo ndio nay eye akajikuta akirushwa hewani, na
kutupwa nje
Na
kipindi anarushwa hewani, ndio hapo akamuona jamaa akiruka kwa kupitia
dirishani kati kati ya moto, na usoni akaonekana akiwa kama anaungua ngozi ya
usoni, na huyo jamaa akaibandua hiyo
ngozi, lakini hakuweza kumuona vyema usoni , jamaa akatupa kitu kwenye moto na
kuanza kukimbia, na Inspecta Moto aligonga kichwa, pale alipodondokea, na
kuhisi moto ukimpamab mwilini.
‘Wamwagieni
maji, sogea…..waondoeni hapo haraka moto unazidi…..’ni sauti za mwisho
kuzisikia kabla hajazama kwenye giza nene, maana, hewa ilikuwa nzito, na hata
alipojaribu kusimama hakuweza, akapoteza
fahamu......
********
Inspecta alipokumbuka hivyo, akajitutumua
kuinuka, na akitaka kuondoka,akijua kuwa kuna kazi nzito anahitajika kwenda kukabiliana
nayo, na inatakiwa kufanyika kwa haraka, je yule mtu ni nani, na je wale watu
waliokuwepo mle ndani waliweza kuokolewa, au ndio waliteketea na huo moto, ndio
maana akauliza hilo swali, na yule binti akasema;
‘Nasikia
watu wengi wamejeruhiwa sana, ila cha ajabu wanasema kuna upepo mkali ulitupoa
watu nje, kila mtu alijua hakuna aliyepona...mimi huko sikufika, nimeambiwa tu,
nikuulize, hivi kwanini hao watu wanafanya hivyo, kuna nini wanataka,?’
akauliza huyo binti
‘Na
hilo jengo limekuwaje, na je watu waliokuwepo ndani walitolewa?’ akauliza tena
hilo swali
‘Mimi
sijui,...sijasikia kama kulikuwa na watu ndani ya hilo jengo....’akasema huyo
binti
‘Simu
yangu ipo wapi?’ akauliza
‘Lakini
nimeambiwa ukizindukana unywe dawa, na usifanye kitu chochote….’akasema huyo
binti.
‘ni
muhimu sana nijue kinachoendelea la sivyo, itabidi nitoke humu niende huko
nithibitishe mwenyewe…’akasema na Yule binti alipoona hivyo akasogea pembeni
ambapo kulikuwa na nguo za huyo askari, akapekua na kuona simu.
‘Ndio
hii?’ akauliza
‘Yah,
nipe….’akasema , na alipoishika mkononi, akaanza kutafuta namba anayoihitajia
na kuanza kupiga kuwasiliana na watu wake, lakini kila aliyempigia simu
hakuweza kumpata, akajikuta akiguna.
‘Mhhh...’
‘Mhh,
vipi tena hawapatikani?’ akauliza
‘Hawapatikani,
au kuna baya limewakumba….mmh, sijui nimpigie nani, ngoja nimpigie mkuu….’akasema
na kuanza kuitafuta namba ya mkuu wake wa kazi….
************
WAZO LA LEO: Je hawa watu
wanaoua wenzao kwa madhumuni ya kupata utajiri, hawana utu wa kibinadamu..?’ ni
swali kutoka kwa mtoto mdogo tu, na sijui wewe utalijibuje.
Vyovyote
iwavyo, watu kama hao,utu, ubinadamu umeshawavuka,na watu kama hao wapo wa aina
nyingi, wapo wanaotumia silaha, lakini wapo wengine, hawatumii silaha za moto,
lakini ni wauwaji, watu wanaodhulumu haki za wenzao, wakijua haki hiyo ni
rasilimali ya wanyonge, rasilimali ambayo ingelinunulia hata dawa kuokoa maisha
ya watu, wagonjwa…kusomesha watoto ili waje kuwa madakitari, walimu, nk na
kufanya mambo mengi kwa masilahi ya
wengi, na kuokoa maisha ya wenza wao, wao wanaifisidi, na watu wanateseka,
wanaumia, na wanakufa hawa ni wauwaji wabaya sana, sawa na hao wanaotumia
silaha za moto kupata utajiri,….
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment