Msaidizi
wa mkuu, akiwa ndiye kiongozi wa kikao kingine maalumu kilichoitishwa kwa haraka, alionekana kuchoka, na kuwa na wasiwasi, ndani ya kikao hicho alikuwepo muendesha mashitaka, Moto na msaidizi mwingine, ...na mwanzoni ilijulikana kuwa ni kikao cha kupeana majukumu kuhusu kesi iliyopo mbele yao, lakini ikaja hoja nyingine kinyume na matarajio.
'Nimetumwa tena na mkuu, kuwa kesi iahirishwe kwanza, kwani mkuu anaona maandilizi ya kesi hii ambayo ni kubwa sana, haijakamilika ‘itakiwavyo’,
na pia yeye mkuu ana mambo mengi ambayo keshayagundua kuwa yanahitajika
kufuatiliwa kwanza...
‘Kesi
iendelee, ..nyie mliniteua mimi kama msimamizi wa hiyo kesi, ...kama hamtaki
basi mniondoe mumuweke mtu mwingine, mimi nina uhakika na kazi niliyoifanya, na
kila kitu nimeshakiweka wazi kwa muendesha mashitaka, sasa kwanini tuahirishe
hii kesi....’akasema Moto
‘Mkuu
ana maana yake kuwa, kesi hii inaingilia
mambo mengi, na inawagusa watu mashuhuri
na wawekezaji muhimu, huoni kwa namna moja tunaweza kuleta sintofahamu
katika nchi, kisiasa na kiuchumi na hata tunaweza kukosa misaada kama wenye
nchi wanapotoka hao wawekezaji watapelekewa taarifa mbaya dhidi yetu...’akasema
msaidizi.
‘Kila
nchi ina sheria zake, na sheria hizo zinatambulikana kimataifa, hatuwezi
kuwapendelea wawekezaji hata kama wamekiuka sheria, walipokuja kuomba
uwekezaji, waliambiwa wafuate sheria, sasa iweje wazivunje, cha muhimu ni
sheria ifuatwe, na mahakama ndiyo yenye
nafasi nzuri ya kuamua hilo...’akasema Moto.
‘Hujanielewa,
hilo linaeleweka vyema, lakini tunatakiwa tuwe na tahadhari, na tahadhari hiyo
ndio anayotaka kuichukua mkuu, kuongea na wakubwa kwanza, ili tuone jinsi gani
ya kufanya, ili kukwepa lawama baadaye, hata kama ...itabidi tunaweza kutumia njia
nyingine,kesi hii isiwepo kabisa, wahusika wakarudishwa kwao...’akasema
msaidizi
‘Mimi
sioni kama kuna tatizo hapo, mahakama ndicho chombo kizuri cha kuliangalia
hilo, kama ni muwekezaji, kama ni mtu mashuhuri mhakama italiangalia hilo na
haki itatendeka....’akasema muendesha mashitaka
‘Mkuu
kasema hataidhinisha hiyo taarifa ya kuwa kesi iendelee, kwahiyo tusubiri
kibali chake , na mimi kama msaidizi wake, siwezi kukiuka amri yake, siwezi
kuidhinisha hili kuwa kesi ifanyike...’akasema msaidizi.
‘Kwa
hatua iliyofikia, hatuna haja ya kusubiria kibali chako mkuu,….tumeshafanikisha
kila kitu, kwa vile kuna kibali tayari cha kunipa mimi mamlaka ya kusimamia hii
kesi, mimi sioni kama kuna haja ya nyie kusaini chochote, sisi tunakwenda
mahakamani....’akasema Moto na kumuangalia muendesha mashitaka
‘Ni
kweli hilo halihitaji kibali chenu tena, maana mlishaidhinisha mapema kuwa Moto
aendelee na kesi hiyo ipo mikononi mwake, na kibali hicho ninacho, kesho
tunaanza kesi....’akasema muendesha mashitaka
‘Kwahiyo
kesi hiyo mumejiamulia wenyewe,haihitaji baraza za sisi wakubwa zenu ...’akasema
msaidizi
‘Mlishanipa
Baraka hizo mapema, unakumbuka siku ile, tena kimaandishi, mkuu, kwani kuna nini cha kutilia mshaka hapo,
msiwe na wasiwasi kila kitu kitakwenda vyema mkuu, ...kama kuna tatizo jingine
tuambieni...’akasema na kumuangalia muendesha mashitaka
‘Tatizo
jingine ni kwa hao mashahidi je wataweza kutoa ushahidi wao kwa hiyo hali
waliyo nayo?’ akauliza huyo msaidizi
‘Tutapata
taarifa kutoka kwa muuguzi, sizani kama watashindwa kutoa ushahidi ..hali zao sio mbaya kihivyo….’akasema
Moto
‘Una
uhakika na hilo,...?’ akauliza mkuu huyo
‘Kwanini
unatia uwalakini, wapo hospitali, kama ingelikuwa haiwezekani tungelishapata
taarifa, tukitoka hapa tutapitia na muendesha mashitaka, kukamlisha baadhi ya
taratibu...’akasema Moto
‘Bora
upige simu huko hospitali, uthibitishe hilo, ni moja ya vitu alivyokuwa
akiniuliza mkuu, hasa kuhusu mashahidi, ….mambo ya kisiasa, uchumi,….mambo
mengi tu, ana wasiwasi kuwa hao mashahidi wataitwa mahakamani washindwe
kujielekeza na hapo itakuwa aibu kwetu...’akasema
‘Mkuu
anaumwa, hawezi kujua afya za hao watu, hil ni jukumu letu, na wewe ndiye
mwenye mamlaka kwa sasa, je wewe unahisi halitawezekana hili, wakati sisi
watendaji wako tumeshakuthibitishia....’akasema Moto
‘Piga
simu huko hospitalini, uhakikishe, ni muhimu sana, kama wapo tayari nitamuondoa
wasi asi mkuu, ....’akasema na moto akapiga simu hospitalini
‘Je
wale wagonjwa, tuliowaleta hapo wanaendeleaje?’ akauliza na kusikiliza kwa muda,
halafu akasema
‘Mbona
hamkuniambia mumekaa kimia na mnajua hao ni watu muhimu mahakamani
kesho..’akasema moto na kusikiliza kwa makini, baadaye akasema kwa mshangao
‘Ina
maana, Msaidizi wa mkuu anajua, mlishamuambia, haiwezekani kwanini...’akasema
na kumgeukia msaidizi wa mkuu, halafu akakata simu
‘Mkuu
kumbe uliambiwa kuhusu hali ya hao watu kuwa bado hawajagundua tatizo ni nini,
na bado wana hali mbaya, lakini hukunipa hiyo taarifa..’akalalamika
‘Ndio
maana nikataka uthibitishe wewe mwenyewe,…, hii ilikuwa ni kazi yako
kuhakikisha hayo, unaona jinsi gani unavyopeleka mambo yako,…. Na ndio maana
nilipoongea na mkuu wetu, akasema kwa hali hiyo inaidi tuahirishe
kesi....’akasema
‘Kesi
haitaahirishwa mkuu, kwasababu ya watu hao,...kuna mashahidi wengine watasimama
kabla yao na wao ni muhimu vile vile...’akasema Moto
‘Akina
nani hao wengine, wakati mahakama inawasubiria mshahidi hawa ambao tulishaona
ni muhimu kwenye hi kesi...?’ akauliza huyo mkuu na kumuangalia moto inspecta
Moto akachukua simu yake na kupiga namba, akasikiliza kwa makini halafu
akauliza
‘Kila
kitu kipo sahihi, umehakikisha,..sawa, tutakutana mahakamani kesho...’akasema
na kugeuka kumuangalia muendesha mashitaka, halafu akageuka kumuangalia mkuu.
‘Tuna
mashahidi watatu wengine muhimu, mmojawapo ndio huyo niliyekuwa nikiongea naye
yupo tayari, na wawili wengine, tukitoka hapa tutawapitia na muendesha
mashitaka, ila ,..kuna mambo nayafuatilia kwanza, nahitajia kupata kibali kwa
mshahidi wengine maana ni watu wakubwa...’akasema
‘Kibali
kutoka kwa nani, na ni watu gani hao wakubwa..?’ akauliza
‘Tutakutana
jioni,...ngoja nifuatilie hicho kibali,...’akasema Moto, na kutoka akiwaacha
msaidizi wa mkuu na muendesha mashitaka
‘Unamuelewa
huyu mtu kibali anatakiwa akipate kutoka kwangu, ananikiuka mimi , kama mkuu
wake wa kazi anakwenda kutafuta kibali wapi, huyu mtu hatufai, anakiuka sheria
za kijeshi...’akasema na kusimama kwa hasira
Muendesha
mashitaka akawa kautulia kimiya, halafu akasema;
‘Vita
imeanza mkuu, na ukiona kiongozi wa vita anarudi nyuma,b asi huyo hafai kuwa
kiongozi, na hatuwezi kusimamisha vita wakati tumeshafika uwanja wa mapambano,
ina maana tumeshindwa, ...’akasema muendesha mashitaka
‘Vita
haiwezi kuendeshwa, kiholela, kuna wakuu wa vita , na wakuu ndio sisi, kama
tumeona muda wa vita bado ni lazima mtuskilize,mimi kama mkuu wenu, ni lazima
mtii amri yangu kwahiyo kesi hiyo
haitafanyika kesho, mimi mwenyewe nitaongea na hakimu aiahirishe....’akasema
muendesha mashitaka
‘Haiwezekani
mkuu,maana kila kitu tumeshakiwakilisha kwa hakimu na tumemthibitishia kuwa kesi ipo, na kibali cha
kuiendesha, mlichomkabidhi moto kipo,kimeshawakilishwa kwa hakimu, sioni kwanini tumsumbue hakimu kwa swala hilo
tena, wakati keshawasiliana na sisi na keshawaeka ratiba ya hiyo kesi kesho na
imeshatanganzwa, mimi nakushauri, acha kesi iendelee kama kuna wasiwasi
mwingine, niambieni, mimi nitajua jinsi ya kuusawazisha kinamna ndani ya
mahakama, maana hiyo ndio kazi yangu...’akasema
‘Mkuu
kasema nisije kufanya makosa kuipeleka hii kesi mahamani, kwani kuna mambo
mengi yanahitajika kufuatiliwa kwa
undani,, unafikiri mimi nitakwenda kumuambia nini, sikiliza fanya
ufanyalo hii kesi isifanyike kesho, ...’akaambiwa
‘Haiwezekani
mkuu, nashangaa hata jana nimepokea ujumbe wa vitisho, sijui ni wahuni gani,
hata hivyo hawanibabaishi..!’ akauliza muendesha mashitaka
‘Ujumbe
gani huo…hata mkuu katumiwa ujumbe kama huo, wa vitisho, ndio maana anasema
kuna mambo ya kuangalia kwa makini…hivi kwanini mnataka kukimbilia mahakamani wakti mnaona kuna mambo muhimu
hatujakamlisha?’ akauliza
‘Mhh,tutaonana
mahakamani, mimi sibabaishwi na vitu kama hivyo...kesi ipo pale pale, na kibali
kikipatikana, tutaweza kuwasimaisha mashahidi wengine wakubwa.....’akasema
‘Kwani
kibali kitolewe juu , kwanini manakiuka sheria za utendaji, hata wewe mtu
unayejua sheria unalikubali hili, huyu Moto, inabidi awajibike kijesh na hili
nitahakikisha linafanyika....’akasema mkuu huyu akismama kwa hasira.
‘Wakati
mwingine inabidi ifanyike hivyo, …tutaonana
mahakamani….’akasema muendesha mashitaka akiweka makabrasha yake kwenye
mkobwa wake.
*************
Siku
hiyo usiku kukawa na heka heaka za hapa na pale, mashahidi wapya waliotafutwa
wakawa wanahojiwa na muendesha mashitaka ili kuona utaratibu mzima unakamilika,
akawa sasa anahojiwa mtu ambaye anaishi karibu na eneo la makaburini, ambapo
kunahisiwa kuwa huenda ilikuwa ni makao maalumu ya magaidi
‘Wewe umeishi maeneo hayo kwa muda gani…?’ wakaulizwa
‘Zaidi
ya miaka kumu, nipo hapo, nilikuwa na kibanda changu hapo, badaye nikapauza,
lakini bado nikawa naendelea kuishi hapo nikiwa na biashara yangu ya genge…’akasema
‘Kwahiyo
nyumba iliyolipuliwa unaifahamu sana, na mwenye nyumba hiyo?’ akauliza
‘Nawafahamu
sana, mwenye nyumba hiyo ni mume wa marehemu, huyu mama anayeitwa Kikagula,
hapo ndipo walipoanzia maisha yao awali kabla hajawahamia huko mjini….’akasema
‘Kwahiyo
hii nyumba ni ya muwekezaji wa hoteli ya
Paradise?’ akaulizwa
‘Nasikia
alipofariki mjengaji wa hiyo nyumba,…yaani mume wa Kigagula, waliamua kupauza,..na
mnunuzi aliyekuja kupanunua, akapotea
kiajabu, ikaja kanunuliwa na mtu mwingine ikawa hali hiyo hiyo , kukaanza
tetesii kuwa nyumba hiyo ina majini…’akasema
‘Kwanini?’
akaulizwa
‘Kwanza
kila anayenunua eneo hilo hufa , au hupotea kimiujiza, na waliowahi kupanga
humo wanasema kuna vitu vinatembea usiku, kuna kama karakana, watu wanagonga
gonga vyuma, kama wanajenga, sauti hiyo inasikika hewani, au ..chini
hakueleweki na watu wanaongea, na kuna muda watu wanapiga ukelele kama
wanateswa….lakini kukipambazuka, kunakuwa kimiya…’akasema
‘Kwahiyo
unahisi kulikuwa na nyumba ya chini kwa chini?’ akaulizwa
‘Hapana,..wengi
wanadai sio chini, ni kwenye paa la nyumba, …sizani kama kulikuwa na kitu kama
hicho, eti kuna nyumba ardhini, hapana..tungelijua, sisi tulioishi hapo miaka
mingi, nyumba hiyo naifahamu sana….’akasema
‘Lakini
bomu lilitokea ardhini, …’akasema na shahidi akawa hana zaidi hata alipohojiwa
kuhusu mabomu na akaitwa shahidi mwingine.
Mwingine
nay eye alikuwa jirani na yeye maelezo yake
yalikuw a hayo hayo…ila huyu alipoulizwa mtu ambaye anaonekana kuishi hapa
anamfahamu akasema;
‘Huyu
mtu ni mvuvi, ambaye aliamua kuishi hapa tu kwa vila anajiamini, nahisi hata
yeye ni mchawi, kwahiyo akikutana na wachawi wenzake kunakuwa hakuna tatizo…’akasema
‘Kwanini
unasema ni mchawi?’ akaulizwa
‘Hajulikani,
haongei na watu,..jirani gani huyo, na kuonekana kwake ni mara chache sana,
akija anaingia ndani , lakini humuoni muda wa kutoka..na mara nyingi hapendi
kuonekana usoni, huwa kavalia mawani, au kavaa sweta lenye kofia, ya kuficha
sehemu kubwa ya kichwa..ni mtu wa ajabu sana….’akasema
‘Je
wakati mabomu yanalipuka huko makaburini mlikuwepo maeneo hayo, ...?’
wakaulizwa
‘Mimi
nilikuwa ndio nimerudi kutoka sokoni, nilikwenda kuchukua bidhaa zangu
Buguruni, nikawa nimerudi na gunia la viazi, wakati naweka hilo gunia la viazi
chini , ili nianze kuvichambua viazi, kitu kikalia, tuuuh….ooh, ardhi yote
ikatetemeka, mimi haraka nikalala chini, niliposimama, sikuangalia kushoto au
kulia, nikalala mbele..sijui kilichotokea huku nyuma…’akasema
‘Usiku
wake, kabla, au jana yake, hakuna
chochote mlichosikia, mlichoona …?’ akaulizwa
‘Tulisikia..hata
mimi niliona, kuna mtu aliuwawa, na kulikuwa na taratibu za kumzika, lakini
wahusika hawakukubali mazishi yafanyike, wakadai mtu wao afanyiwe uchunguzi…kwahiyo
kulikuwa na watu wageni, askari, na taratibu kama hizo,….ila nilisikia mlango
wa hiyo nyumba, ukifunguliwa mara kwa mara kuashiria kuwa huyo jamaa alikuwepo….’akasema
‘Jamaa
yupi?’ akaulizwa
‘Si
huyo mwanga….’akasema
‘Lakini
hukumuona?’ akaulizwa
‘Tunaogopa
hata kumuona siku hizi, maana nasikia ukimwangalia sana, unapotea kimiujiza….’akasema
‘Kuna
watu yamewatokea hayo?’ akauliza
‘Wapo,
ndio kwani siri..na inasadakiwa na kwasababu ya huyo mwanga…anaogopeka kweli
kweli…’akasema
‘Hamna
mtu anayeweza kumjua vyema sura yake..hebu angalieni hizi picha hapa…’wakaonyeshwa
picha mbali mbali, lakini hakuna aliyeweza kuzitambua kuwa zinafanana na huyo
mtu.
‘Huyu
arehemu anayemiliki hoteli ya Paradise, alikufakufaje?’ akaulizwa mtu
anayeifahamu hiyo familia
‘Kwanza
alipotea , akawa anatafutwa sana, baadaye ukaonekana mwili wake, akiwa amekufa,
wakaja kumzika hapo makaburini , mimi mwenyewe nilishuhudia mazishi yake…’akasema
‘Sasa
kwanini mama yake alidai kuwa hajafa?’ akaulizwa
‘Ni
kuchanganyikiwa tu, kwani mtoto wake alikuwa huyo huyo, na alikuwa anampenda
sana, kwahiyo kufa kwake, akawa kachanganyikiwa, na watu wanahisi ni kutokana
na mambo yao ya kishirikina yaliwageuka…’akasema
‘Walikuwa
na mambo hayo?’ akaulizwa
‘Aaah,
sana, unafikiri, hebu angalia utajiri walioupata, wameupata pata vipi, kwanza
ni wanga, halafu mtoto huyo alikuwa jambazi,….simsemi vibaya maiti, lakini mtu
gani haonekani, mchana kalala , usiku tu ndio anatoka, anakwenda wapi……mimi ni
mtu wao wa karibu, lakini nikuambie ukweli, tangu alipofariki baba yao, na huyo
mtoto akapewa umiliki, ikawa ndio mwisho wa kumuona huyo jamaa, ..unamsikia
usiku tu akiongea na watu wake….’akasema
‘Kwahiyo
hata sura yake huijui , sura ya ukubwani….?’akaulizwa
‘Mhh, Sura
nikimuona naweza kuikumbuka, sina uhakika sana..lakini mmh, unajua ni siku
nyingi, ni kipindi hicho alikuwa bado kijana kijana….unafahamu, vijana siku hizi wanabadilika haraka sana, na hata hivyo kiukweli, ukikua na sura
zinabadilika, ..ili huyu jamaa toka ujanani, alipendelea sana kuvaa mawani nasikia hadi usiku..sijui alikuwa akificha nini
sura yake au ni matatizo ya macho,….’akasema
Walihojiwa
watu wengi, lakini hakuna aliyweza kuikumbuka sura ya marehemu au picha yake,
na wote walidai kuwa huyo mumiliki akufa kweli, ila mwili wake hakuna aliewahi
kuuona..
‘Sasa
tufanyeje…?’ akauliza muendesha mashitaka akimgeukia Inspecta Moto
‘Nasubiri
kibali …mimi nina uhakika, hao waheshimiwa wanahusika, na wao watakuwa wanajua mengi, na
hata kuhusika, wakisimama kizimbani , niachie mimi….’kasema Moto.
‘Moto….unanichekesha
kweli, unataka urudie kazi yako ya uwakili, wewe sasa ni askari kazi hiyo
niachie mimi, lakini ujue ni hatari kubwa, kama wataoenekana hawana hatia ujue
na wewe kazi huna…..’akasema mwendesha mashitaka.
‘Najua,….lakini
ni lazima iwe hivyo, ngoja tupate hicho kibali…’akasema na simu ya Moto ikalia,
na alipoangalia, akaona ni ujumbe, unamuhitaji kwenda makao yao makuu…..
NB:
HIYO NI KATIKA HARAKATI ZA KUWEKANA SAWA, SASA TUNAINGIA MAHAKAMANI, NA ITAKUWA MWANZO WA HITIMISHO
TUWE PAMOJA
WAZO ZA LEO: Kila kazi ina utaratibu wake, na ndio maana kuna nyanja mbali mbali za kusomea
hizo kazi, ni ajabu kuona mtu anajifanya yeye anafahamu kila kazi, iwe ni ofisi au mitaani,
na matokea yake kazi nyingine, zinaendeshwa kiholela, na kiutaratibu usio sahihi, na matokeo yake ni
kushuka thamani ya ile kazi,…kwanini tusiwape nafasi wanastahiki, kwanini
tuhodhi madaraka tu kwa ubinafsi wa masilahi na huku tunalalamika kuna upungu
wa ajira wakati mtu mmoja kashikilia ajira ya watu watatu,…utendaji mbovu….tuliangalie
hili kwa masilahi ya wote..
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment