‘Muheshimiwa
hakimu,...najua hii kesi ni ya mauaji, ambayo imekuwa na utata mwingi, na utata
huo sio kuwa ni wa bahati mbaya, yote hiyo ni mipango, ilipangwa iwe hivyo, na
imekuwa hivyo...’akatulia kidogo akisafisha koo.
‘Pia
najua kila mtu anataka kujua ni kwanini, ni kwanini auwawe mtoza ushuru,
japokuwa awali nimeshaelezea kwa muhutasari, basi ..leo hii mimi nitawatajia kila kitu, tulieni,
nipeni nafasi, na naomba pumzi isiniishie mapema, kabla sijamaliza kutaja ni
nani alimuua mtoza ushuru, na ....hata huyu mlinzi wa mdada, ....’akawa
anaongea kwa masikitiko..
‘Endelea mzee, akasema
hakimu
‘Sawa muheshimiwa hakimu,
nashukuru sana, nitajitahidi kadri ya uwezo na pumzi atakazonijali mungu
kuliwakilisha hili kwenu,...’akasema na kutulia vizuri kwenye kile kiti
chake...
‘Katika mikakati ya hilo
kundi, kuna muda wakuu , waheshimiwa, wanajikuta wanapambana na matatizo ya mtu
au kikundi ambazho kinawakwaza katika kufikia malengo yao....’akatulia kidogo
‘Basi wao wana kila mbinu,
wamejipanga kwa lolote lile, wahusika wakuu wanapitisha azimio na kusema huyu
sasa basi, huyu sasa ni kikwazo, tufanye nini, lakini pia kunakulindana,
kuhakikisha mwenzetu hapatwi na
madhara,kwahiyo kila mtu akiwa kwenye majukumu ya kikazi ni lazima kuwe na
namna ya usalama wake, na hili ili liweze kufanikiwa, kuna idara maalumu ya
kazi hii, wapo wataalamu waliobobea kuhakikisha kuwa usalama upo...
‘Wapo watu maalumu, muda
wote wanatuangalia kila tunalolifanya...usione nimevaa hili kofia, na koti hili
rafu, ukafikiri ni koti tu, ukafikiri ni nguo tu, usione watu wamevaa masuti ya
namna fulani ukafikiri ni suti tu...hizo zote ni kinga za silaha za kujlinda,...’akasema
na hakimu akawa anamuangalia kwa makini.
‘Muheshimiwa hakimu ukiwa
umevaa hivi unakuwa na mlinzi nyuma yako, kuna watu wanakuona kila unapokwenda,
wametuzunguka kila mahali, ...wakiona upo hatarini tu wanatokea watu wa
kukusaidia, kuna watu wapo kila kona, sasa jiulize mwenyewe hao watu
wamepatikana wapi, sio kundi la mchezo kama mnavyofikiria nyie..’akasema na
watu wakageuka nyuma kuangalia
‘Msiangalie nyuma, maana
hata mkiangalia nyuma hamtawaona, inawezekana hapo ulipokaa huyo aliyepo
pembeni yake ni hao watu,...’aliposema hivyo watu wakawa wanaangaliana.
‘Huwezi kuwajua, anaweza
akawa hata ni ndugu yako, mtoto wako mwenyewe, yupo kwenye kundi lakini ni siri
kubwa ya kundi, hawezi kukuambia, ...lakini wapo hao watu wanatuangalia, wapo
kwenye chumba maalumu cha siri, na mitambo yao, na chumba hicho sio cha kudumu,
leo wapo hapa kesho wapo sehemu nyingine, kutegemeana na hali ya hewa...’akatulia
akijinyosha kidogo.
‘Ila kwa vile nilishajua
mbinu zao, nilishajua ni kitu gani nifanye, siku walipoanza kunihis vibaya,
nikaharibu taratibu za mawasiliano zilizokuwepo kwenye hizi nguo, ...’akasema
akionyeshea liel koti alilovaa,...
‘Kwahiyo toka siku
nilipoharibu hiyo mitambo iliyounganishwa kwenye hizi nguo,wakawa hawanioni
wakawa hawanipati, maana kwenye nguo hizi kuna nyuzi zimeungwanishwa na nyuzi
hizo ni waya ndogo sana zinaweza kunasa matukio, sauti , na kuwezesha silaha isiweze
kupenya..
'Ndio maana hawakujua wapi nilipokuwepo tokea waanze kunitafuta ili
waniue, waulizeni hao jamaa mliowakamata
,wanafahamu zaidi.....lakini kama nilivyosema wana mbinu nyingi na wana watu
wengi, hata huko mahospitalini wana watu wao....’akasema na wale washitakiwa
wakainamisha vichwa vyao, na hakimu akatupa jicho kuwaangalia, na machoni
alionyesha hasira...
‘Najua nikitoka hapa watahakikisha
sifiki huko ninapotakiwa kwenda, lakini hata hivyo, wameshachelewa...kwani yote
nataka niyaweke hadharani hii leo...’akasema na kuwaangalia wale washitakiwa
ambao muda mwingi walikuwa wameinamisha vichwa vyao chini.
‘Nimetimiza wajibu, na
sitajutia kile nilichokifanya kwani yote nimeyafanya kwa ajili ya taifa langu,
toka awali, na sasa pia, nimeamua kujitolea muhanga kwa ajili ya taifa langu,
nikifa nakufa nikiwa nalitetea taifa langu....’akasema kwa sauti ya ukakamavu.
‘Ndio maana sasa nataka
kuyaweka haya hadharani kabla siku yangu haijafika, maana kanuni ya kundi
ukisaliti kundi adhabu yake ni kifo,..nilitakiwa kufa kwa sumu, lakini mungu amenisaidia
nipata muda angalau kidogo, maana sumu hiyo haikwepeshi, najua inanitafuna
ndani kwa ndani, na sijui ilikuwaje hata sumu hiyo ikashindwa kunimaliza mara
moja, kwani sumu hiyo haikwepeshi, haichukui muda....’akasema
‘Huenda ni kwa sababu ya
maombi yangu kwa mungu, kuwa angalau nipate muda kidogo wa kuja kuyasema haya, maana
nimeyaona kwa macho yangu,na pia nikayafanyia kazi, japokuwa waliweza kuiba
nyaraka zote muhimu...’akatulia kidogo
‘Lakini mimi ni mpigananji,
mzoefu, sishindwi kirahisi, bado nina ushahidi ambao unaweza kuwafikisha wote
wanaohusika mbele ya sheria kazi itabakia kwenu nyie mliopewa dhamana ya
kuhakikisha kuwa sheria inatimiza wajibu wake, sijui, na inawezekana hata huku
kwenye mahakama wapo watu wao.....’akasema mzee na hakimu akatabasamu.
Mzee akaonyesha hali ya
kuchoka, na sauti ikawa inakwaruza, na hakimu akaliona hilo akasema;
‘Mzee naona
umechoka,...tunaweza kuahirisha hili zoezi,ukaja kutoa ushahidi wako muhimu
ukiwa na afya nzuri...’akasema hakimu na mzee akajitutumua na kisema;
‘Sijachoka, bado nahisi nina
puumzi ya kutosha kumalizia sehemu hii muhimu, hili ninalotaka kulifanya hapa haliwezi
kuahirisha…sina muda mwingine wa kuja kuyaongea haya, labda kama hamtaki kuyasikia
yote, sizani kama nikitoka hapa nitaweza kurudi tena, sizani , na huenda hata
nisiweze...’akasema mzee kwa shida na kuanza kukohoa mfululiozo, hakimu
akaongea na mtu wake, nahisi alikuwa akimwambia dakitari aitwe.
Mzee hakujali, akajitutumua
baada ya kutulia kidogo, akajinyosha kidogo, na kuvuta kitu kama kamba, kutoka
kwenye koti lake, na mwisho wa ile kamba kukawa na kidude kidogo (flash disk)
‘Ushahidi wote upo
hapa...’mzee akasema na kukiinua kile kidude juu,, kitufe kile kina uwezo
mkubwa wa kuhifadhia kumbukumbu, ni kidogo sana, lakini kina uwezo wa kuweka
kumbukumbu nyingi sana zikiwemo kumbukumbu za matukio ya picha na sinema..
Alikitoa na akageuka
kumuangalia muendesha mashitaka na kusema;
‘Muheshimiwa hakimu
namkabidhi huyu, mbele yako, naye atakukabidhi kwa himaya yako, sijui wenyewe
mtakavyofanya, mimi nimetimiza wajibu wangu....’akasema
Na muendesha mashitaka
akakipokea kile kidude, na kukiangalia kwa makini , halafu akamsogelea muheshimiwa
hakimu, na hakimu naye akakiangalia kwa makini na kusema
‘Wataalamu wetu
watakifanyia kazi..lakini kwa hali uliyo nayo mzee, naona ni bora upumzike
kwanza,...’akasema hakimu
‘Natamani iwe hivyo
muheshimiwa hakimu lakini ni bora nikamalizia sehemu iliyobakia, kwani sijui
....’akatulia kidogo, halafu akasema;
‘Nataka kuwaambia hili mnielewe,
kuwa nikitoka hapa sitaweza kurudi, ila nawaambieni, hicho kidude kina kila
kitu, kama mnataka haki itendeke vyema, basi fanyieni kazi hayo yaliyomo
humo...najua inaweza kutokea pingamizi kwa wajanja, wakatoa hoja hizi na zile,
lakini yote yanahitajika yawafikie wanancho wajue ukweli...’akassema
‘Humo mna kila ushahidi wa
kundi, lini kundi lilipoanzishwa na wanachama wake wake wa awali, kuna mambo
mengi wameyafanya, mauaji ya namna kwa namna...kuna siri za miradi mbali mbali,wanazoziendesha
wao, kuna kumbukumbu za akunti za beni nje ya nchi, na pia mwishoni utaona inaonyesha
jinsi siku mtoza ushuru alivyouwawa...’mzee sasa akaonekana kukosa nguvu
Yule askari akamsogelea na kumshikilia
vyema, akamkagua mzee, na mzee alionekama kuzidiwa, lakini hakutaka kutulia
kuongea, akawa hawezi hata kukaa vyema, ilibidi askari yule amshikilie vyema
kwenye kiti, hata hivyo sauti yake , iliyokuwa ikiendelea kupungua nguvu
ilisikika ikisema;
‘Nasikia mlinzi wa mdada
kauwawa, wamefanya hivyo kwa vile walijua
anafahamu mengi, ni mtu aliyekuwa akinisaidia kazi zangu za hapa na
pale, walijua huyo mlinzi anafahamu kuwa kulikuwa na hizo nyaraka kwa mdada, na
kwa vile wanauhakia kuwa hizo nyaraka watazipata kwa mdada, waliona waondoe
uzia kwa kumuua huyo mlinzi, nina uhakika aliyefanya hivyo ni wakili wake.
Mdada alipewa kazi maalumu
na mtu wa kundi, mdada hakulijua hilo, yeye alijuwa kuwa huyo mtu ni mmoja wa
watu waaminifu wa taifa, na siku nilipokutana na mdada kumuelezea hilo,
hakuniamini, ila aliposikia kuwa siku ile mimi ndiye niliyemuokoa asiuwawe,
alibakia mdomo wazi....
‘Sasa sijui huyu mdada yupo
wapi, kama kawapelekea hawa watiu hizo nyaraka basi zimeshaharibiwa, ...mdada
anamuamini sana bosi wake, akijua ni mtu mwema, kumbe ni wale wale, na huyo mtu
akawa akimtumia mdada kwa masilahi ya kundi, ....mdada hakulifahamu hilo, kama
wamemkamata, sijui kama atakua hai...’akasema
‘Ndugu zanguni, mliokamatwa,
nawaombeni sana, jitakaseni, tubuni zambi zenu, hayo mnayoyatafuta
hayatawasaidia lolote, angalieni waliokwisha tangulia, wapo wapi, kulikuwepo
matajiri wenye kila aina ya sifa za utajiri, wapo wapi,...’akasema akiwaangalia
wale washitakiwa.
‘Kulikuwa na, maraisi, wanaoweze
kutibiwa kwa kila aina ya dawa, lakini wapo wapi, na wapo watu wa kila namna
wenye uwezo wao, lakini utajiri wao, uwezo wao, sifa zao, hazikuwasaidia kitu,
wamekufa, na wataendelea kufa, hebu jiulize, kuna mmoja aliondoka na utajiri wake,….je
utajiri wao uliwasaidia nini…hakuna kitu,...’akasema
‘Nawaombeni sana, na
kuwakumbusha kuwa utajiri, au mali utakayoenda nayo kaburini ni matendo yako
mema kwa watu, wahurumieni wanyonge,
wahurumieni masikini, ambao wanataabika kutokana na dhuluma zenu, huruma hiyo
ndiyo itakayowasaidia, ndiyo utakayokuja kwenda nayo siku yako ikifika…..’ hapo akatulia kidogo na akawa kama anavuta
pumzi kujipa nguvu.
‘Mimi ndiye niliyemuua mtoza ushuru, kwa vile mtoza ushuru alitaka
kumuua mdada…’alipoyasema haya maneno kwa sauti ya utulivu, kama vile
alitaka kila mtu ayaskie, watu waliguna, na hata hakimu akaonyesha kushituka.
‘Ilikuwa hivi,...nilipofika
pale kwa mdada, nikiwa na koti langu la ulinzi, na nilipanga nifike, nikisema
nina jambo nafuatilia, japokuwa haikuwa safari rasimi,...
Nilipofika pale kwa mdada,
nikiwa kiaskari zaidi, nilikutana na mlinzi naye mara moja akanitambua, nikampa
maagizo, na yeye anajua ni kitu gani akifanye, maana nilishaonega anye
kabla,...
‘Mlinzi akaenda kutekeleza
kile nilichomuagiza, lakini muda ukawa umepita, kila kazi ina muda wake maalumu
ukipita inabidi ufanay jambo jingine kwa haraka, mimi niaona nihakikishe, basi
nikasogea kwenye jengo, kwanza nilichungulia dirishani kwa chombo maalumu,...mara
nikamuona mtu akitoka mbio,
‘Yule mtu wakati anatoka,
alikuwa akiondoa midevu kidevuni kwake, mwanzoni sikumtambua, lakinia lipoondoa
zile ndevu ndio nikamtambua,...hata hivyo sikuwa na muda wa kumfuatilia..
‘Kipindi hicho nilikuwa
nimezima mawasiliono yaliyopo kwenye koti na watu wetu wa usalama, kwahiyo
nilikuwa nafanya yangu binafsi, nina kitu kama tocho unaweza kuangalia kupitia
kwa dirisha la kiyoo lililowekewa, kizuizi cha kuona ndani, nikaweza kuona
kinachoendelea kule ndani.
‘Muda ule nilipochungulia,
ndio muda mdada kaanza kuishiwa nguvu, ile hali inayomtokea iliashaanza
kupotea, na ikifikia hapo anakuwa hana nguvu anadondoka,...ukumbuke ili mlinzi
aweze kufanya hiyo kazi, nilimpa maagizo kuwapoteza fahamu hao waliopo ndani...
‘Alishaniambia kuna silaha
maalumu ataitumia, kuwapoteza fahamu hao watu, na kama malivyosikia alitumia
nyundo, yeye ni mjuzi wa yote hayo, sikuwa na wasiwasi na hilo anajua amgonge
wapi mtu ili apoteze fahamu...
‘Nilipoona mdada
anapepesuka na yupo tayari kudondoka, nikageuka kumuangalia mtoza ushuru, mtoza
ushuru, alikuwa anasimama, akiyumba yumba na nilimuona akiifuata silaha,
iliyokuwa sakafuni...hapo nikaingiwa na mashaka, nakaona ni lazima nifanye
jambo…
Nilielekea pale mlangoni,
sikuwa na mashaka, kwani nilikwua nimevaa kinga, risasi haiwezi
kupenya,...nilichotaka ni kumuwahi huyo jamaa kabla hajafanya analotaka
kulifanya...
‘Siku moja kabla
nilishamtuma mlinzi kuhakikisha kwa mdad hakuna silaha, ..kwahiyo nilikuwa na
bastola ya mdada....’akasema na hakimu akawa kama anashangaa
‘Haya mambo yana mipangilio
, japokuwa hili halikuwa mikononi mwa kundi, lakini mimi na mlinzi na baadhi ya
watu wangu niliowaamini tulishalipangilia vyema..
Nilipofika pale mlangoni,
nikiwa na silaha yangu tayari, mtoza ushuru naye alishasimama , sasa alikuwa
kashika bastola akimlenga mdada..na ile hali niliyoiona kwa mtoza ushuru
ilikuwa ni ya tayari kuua...akawa sasa anamuonyeshea mdada ile bastola kumlenga,
akisema;
‘Bye bye mdada, sasa mwisho
wako umefika….’ Akawa sasa anafyatua kiwambo, mimi ni askari nafahamu mtu
anapofyatua kiwambo kidole kinakuwaje,...kwahiyo sikuwa na shaka nilijua kabisa
huyu mtu anataka kuua,...’akatulia
‘Mimi sikutaka mdada auwawe,..maana sikuwa na
uhakika kama kweli mlinzi kazipata hizo nyaraka, hata hivyo, kwanini mdada
auwawe, na auwawe akiwa hawezi kujitetea,. Akili akiniambia ni lazima nimuokoe
huyu mtu , lakini pia sikutaka mtoza ushuru auwawe, maana huko mbele yeye ndiye
anayeweza kujibu mashitaka yote, anafahamu kila kitu, anafahamu mengi kuliko
mimi...’akatulia
‘Kwa muda huo ilitakiwa maamuzi
ya haraka,…nikaona nizuie hayo mauaji,
nikamuwahi huyu mtoza ushuru...lengo ilikuwa kumpiga sehemu ya mikononi, ili
kumvunja nguvu, lakini haikuwezekana,
nilijitahidi iwe hivyo,lakini haikuwezekana....kiukweli sikuwa na dhamira
mbaya, na kumuua yeye iliniuma sana, nikamuwahi kabla hajamfyatulia mdada
risasi…ilikuwa ni kitendo cha haraka sana….
Nilimuwahi kabla hajamuua
mdada, hapo ilikuwa swala la muda, ama mdada auwawe, au .....kwani nilipompiga
risasi, risasi yake ilitokaikawa imemkosa mdada hatua chache na kupiga ukutani,...nilipoona
hivyo sikuwa na jingine, nikaondoka haraka na wakati huo mlinzi alishatoka,
akanipa bahasha, kumbe mle ndani kulikuwa hakuna kitu ...
‘Vilivyokuwepo mle ndani na
mapicha ya ovyo ovyo mengine ni mapicha yam dada aliyowahi kupiga na mkwe....ni
mapicha mabaya yasiyofaa...hata sitaki hata kuyakumbuka...sitaki hata
kuyaelezea niliyachoma moto.....
‘Kitu ambacho nilichokiona
ni cha ajabu, na sijui kwanini askari hawakuelezea, ni ile risasi iliyopiga
hewani ukutani,...risasi hiyo ilitoka kipindi namuwahi mtoza ushuru,...
ukiangalia kwa makini kwa mdada utaona tundu la risasi eneo la ukutani, hiyo ni
risasi iliyotakiwa kumuua mdada...pili risasi iliyomuua mtoza ushuru haikutoka
kwenye bastola yake, japokuwa waliona mabaki ya risasi ya bastola ya mdada,
lakini hili halikuongolewa...
‘Utaona jinsi mambo
yalivyofichwa,...yaligeuzwa geuzwa, hata ripoti ya awali ya wachunguzi
haikufika kwa muendesha mashitaka, iliyofika ni ripoti nyingine iliyopangwa
kinamna...lakini yote yaliyotokea siku hiyo yapo kwenye hicho kidude,
inaokenaka moja kwa moja jinsi ilivyotokea...
‘Kiukweli mimi sikuwa na
lengo la kufanya hivyo, pia haikuwa lengo la kundi hilo haramu, kumuua mtoza
ushuru,. Kifo cha mtoza ushuru ilikuwa ni pigo kwa kundi, maana mtoza ushuru ni miongoni mwa viongozi wa
kundi, waliokuwa wameandaliwa kushika hatamu, japokuwa kulikuwa na sintofahamu
miongoni mwao,...
‘Naweza kusema mtoza ushuru
alikufa kwa bahati mbaya, akiwa katika harakati za kuzipata hizo nyaraka za
siri zilizoibiwa kwake, nyaraka ambazo mtoza ushuru aliniibia mimi, akiwa na
lengo la kuokoa kundi......
‘Mimi nimetimiza wajibu
wangu...sasa naichia kazi mahakama hii, uamuzi ni wenu, mimi ndiye muuaji wa
mtoza ushuru kwa bahati mbaya katika harakati za kumuokoa mdada, mtaona wenyewe
tukio lilivyotokea,....lakini...ooh,...oh, mmh, ......’akasita, na mzee
alionekana akitoa jicho kama mtu aliyeona kitu cha kutisha.
Mara mzee akatulia
kimiya…ilisikika sauti ya kukoroma….hakimu akaamurisha mzee asaidiwe, na
akasisitiza apelekwe hospitalini na dakitari wake aitwe, wakutane njiani, akiwa
anawahishwa hospitalini, lakini hali ya mzee ikawa mbaya zaidi,….mzee hakufika
hata hospitalini, siku yake ikafika, akaiga dunia,…
Mwisho
NB: Yaliyofuata baadaye...
Siri kubwa ya kundi haramu
ilijulikana kutokana na ushahidi aliutoa mzee, na wahusika wengi walikamatwa
japokuwa wengi walikimbilia nje. Mdada hakuonekana kabisa,...
Baada ya kipindi kupita, mchumba
wangu ambaye hakutaka kabisa kuongea na mimi, na familia yao ikawa haitaki
kabisa mawasiliano na mimi, hasa waliposikia kuhusu hayo mapicha aliyokuwa
kayapiga mdada, baadaye mchumba wangu akaolewa na askari, aliyekuwa mlinzi wa
karibu wa mzee
Nilijitahidi sana kumtafuta
mdada, lakini sikuweza kumpata, hata familia yao haikujua wapi mdada alipo, na
wao walisema wameshazoe hiyo hali, hadi leo ninapowaletea hiki kisa,
haijulikani wapi mdada alipokwenda kama yupo hai, au aliuwawa na kundi.....
Mimi badaye nikamuoa mdogo
wake mdada...
NAWASHUKURUNI SANA KWA KUWA NAMI TOKA MWANZO WA HIKI KISA, MIMI NIMETIMIZA WAJIBU WANGU KUFIKISHA KILE NILICHOONA KINAFAA KUFIKA KWAKO, HUENDA HAKIKUWA SAHIHI KWAKO,SAMAHANI KWA HILO...NA NAKUSHUKURU SANA KWA KUNIVUMILIA,...
NA KWA WALE WALIOONA NIMEFANYA VYEMA, NAWASHUKURU SANA KWA KUIFURAHIA KAZI HII, TUPO PAMOJA. LAKINI SITAKUWA MWEMA WA FADHILA KAMA SITAMSHUKURU MLETAJI WA KISA HIKI , SEHEMU ZA SIMULIZI ZA BOSI, MUNGU AMZIDISHIE KWA WEMA WAKE HUO, NA TUTAZIDI KUWA NAYE HUKO MBELENI, MUNGU AKIPENDA...MWISHO WA KISA HIKI NDIO MWANZO WA KISA KINGINE.
WAZO
LA LEO:Kiongozi wangu bora ni yule anayeweka masilahi ya watu
wake mbele, akijua kuwa kapewa dhamana ya watu, na dhamana ya watu ni deni
kwake. Kiongozi huyu hataweza kulala, kula vyema, au kuishi kifahari huku watu
wake wanateseka kwa njaa, na umasikini uliokithiri. Je kiongozi huyu nitampata
wapi, je kweli yupo...?
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Hatimaye wamekamatwa.. Unafikiri mdada atakuwa wapi?....mmhhh mimi naona yupo hai sehemu ...Ahsante sana kwa kisa na kama ww mwandishi ulivyomshukuru mleta kisa basi nami namshukuru kimekuwa ni kisa cha mafunzo mengi sana. Najua kuna kisa kingine kinakuja:-)
Nakushukuru sana ndugu wangu Yasinta, tupo sote kama kawaida yetu, na swali wapi mdada alipo, hata mm sijui, huenda atakuwa nasi akiwajibika. Mhh kweli kisa kingine kinakuja, ngoja tukiweke sawa . Tupo pamoja
Asante sana kwa kisa kizuri,twasubiri kisa kipya,vipi boss wa mhasibu aliishia wapi?na mumewe je?au boss naye alikuwa member wa kundi?
Kisa kipya hicho kinaanza muda si mrefu, kuhusu bosi wa muhasibu, yeye atakuja na simulizi lake kabambe, tuwe pamoja tu. Yeye hakuwepo kwenye lile kundi haramu.
Post a Comment