Kisa kipya kinakuja
Ndugu wapenzi wa diary
yangu, huu ni mwezi ambao mtandao huu wa kijamii uliwekwa hewani, japokuwa
tarehe rasmi haijafika, tumeweza kumaliza kisa kilichokuwa kikiendelea, kisa
cha ‘Baada ya Dhiki Faraja’, kisa hicho kimegusia kuni moja haramu, lililotaka
kuweka mitandao yake kil mahali, ni mbinu za kibinafsi, je hili kundi
lilianzishwaje, swali hili linatufanya turudie kisa kilichowahi kuandikwa kabla
lakini hatukuweza kukimalizia kwasababu za nje ya uwezoo wetu, kisa hicho
kilijulikana kama `dunia yangu..
Hali tunayokwenda nayo sasa, inahitaji kukiweka hicho kisa
tena, kwa namna ya kipekee inayoendana na wakati, wakati ambao una changamoto
nyingi, changamoto za kimaisha, changamoto za kisiasa, changamoto za
kimaadili...tunahitaji kukumbushana na kuelekezana kihekima
‘Dunia yangu’ ni
ndoto walizo nazo wengi, hasa vijana wanapoibukia kuyatafuta maisha, na maisha
yanaanzia utotoni kwenye malezi, na yanakuja kupata maelekezo kwenye elimu,
elimu inakuwa ni dira na nuru ya kutuongoza, lakini changamoto za elimu ni usahihi wa jinsi ya
kuifikisha kwa mlengwa, na jinsi atakavyoipkea na kuifanyia kazi, wakati
mwingine elimu inaweza kuwa chanzo cha chachu ya kufanya yale yasiyofaa..
Kisa chetu kitajaribu kuyamulika hayo kwa mawazo yetu, na
kuona jinsi gani tunaweza kusaidiana kuelemisha jamii kwa mtizamo wa kisa hiki,
mimi kama mwanadamu naweza nisiwe
sahihi, lakini kwa nia moja au nyingine kila mmoja anahitajika kutoa mawazo
yake, huenda yakasaidia na kuleta tija, na wewe uwe mwenza wa kuyafanikisha kwa
kutoa maoni yako, tkumbuke umoja ni nguvu na pia kidole kimoja katu hakivunji
chawa....
Kuna kisa kingine cha simulizi la bosi,...tutaangalia jinsi
gani ya kuweka simulizi hili kwani lina
mafunzo mengi sana, bado tunakusanya hizo simulizi zikiwa tayari, hatutachelewa
kuziwakilisha.
TUPO PAMOJA WAPENDWA
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Pamoja big up,tunasubiri kisa kipya kwa hamu.Unaonaje kama ukiandika kitabu cha kisa kilichopita BAADA YA DHIKI FARAJA,
Twasubiri kwa hamu mno...
Ndio nia yangu kuwa na vitabu vya visa ninavyotunga hapa, lakini yote ni gharama, tuombeane heri tu, ipo siku tutaweza
Nawashukuruni sana kuwa pamoja nami , kunitia moyo, na kuchangia pia, mungu awabariki sana
Post a Comment