‘Mhasibu
wewe na mdada mna mahusiano gani?’ nikaulizwa swali hilo baada ya kutoa maelezo yangu nikisimamiwa
na muendesha mashitaka, nilijitahidi kuelezea yote ninayoyakumbuka siku ile, na
nilipomaliza, akasimama wakili mtetezi na uniuliza maswali mengi na baadaye
akaniuliza hilo swali la mtego;
‘Ni
mfanyakazi mwenzangu...’nikajibu kwani nilishajiandaa nalo na sikutaka kuelezea
zaidi.
‘Ina maana
mkiwa wafanyakazi mnakuwa huru, au wewe ni tabia yako ya kumtembelea mdada,
muda wowote, hata kwenda kulala pamoja ...’akasema wakili na wakili wangu
akaingilia kati kulipinga hilo kuwa hayo ni maswala binafsi na hayana ukweli
‘Kama
likesha humo, alifanya nini, hakulala humo, hawaulala humo , yeye na mdada,
ukumbuke bosi alishaondoka, wakabakia wawili unafikiri kilitokea nini, walikaa
macho,...ni ukweli usipingika kuwa walilala, ...nimekosea nini hapo...’akasema
wakili mtetezi
‘Kauli yako
ya mwanzo umesema nililala naye...’nikajitetea
‘Hukulala
naye?’ akauliza
‘Sikulala
naye, kwasababu alikuwa mgonjwa, na kazi yangu ilikuwa kuhakikisha yupo salama,
na akiamuka niweze kumsaidia...’nikasema
‘Swali ni
kuwa muda wote huo mlikuwa macho hamkulala?’ akauliza
‘Kuna muda
tulilala..’nikasema
‘Sasa
unakataa nini, inaonekana wewe una tabia ya kukataa ukweli..’aasema huyo
wakili, na kabla sijajitetea akauliza;
‘Turudi siku
ya tukio, waati mlipokuwa na mfanyakazi mwenzako, mkakesha usiku kucha,unasema
kuna muda mlilala, au sio, nyie wawili au sio, nakushangaa kweli, maaan kwenye maelezo yako umesema una mchumba wako...’aasema
na watu wakacheka.
‘Hebu
niambie, je siku hiyo unasema alifika marehemu mkaongea naye, akakupa mzigo wa
mdada, na wakati unaelekea ndani , marehemu akatokea kwa nyuma akiwa an
bastola..sawa?' akauliza na mimi kabla sijajibu swali akaendelea kusema;
'Kwahiyo kumbe ni wewe uliyeongea na mlinzi, au baada ya mlinzi
kuongea na mtu mwingine, wewe ndio ukatoka kwenda kukutana na marehemu, maana
kutokana na maelezo ya mlinzi, yeye anasema aliongea na mtu aliyekuwa na ndevu, na alikuwa
mtu tofauti na wewe hebu tuambie humu ndani mlikuwa watu wangapi?’ nikaulizwa.
‘Ni kweli
mimi ndiye niliyeongea na mlinzi, na hakukuwa na mtu mwingine, na mlinzi akaniambia
kuwa kuna mgeni wa mdada nje, na mimi nikaenda kuonana na huyo mgeni, na huyo
mgeni alikuwa ni ndio huyo marehemu,akanipa huo mzigo wa mdada, na wakati
naelekea ndani, ndio marahemu akatokea kwa nyuma akiwa an bastola, haukuwa na
mtu mwingine,....’nikasema
‘Lakini
mlinzi kasema aliongea na mtu aliyekuwa na ndevu, sio wewe, je huyo mtu
mwingine ni nani?’ akaniuliza
‘Mimi
simjui, ...’nikasema na moyoni nilijihisi vibaya, kwani sikuweza kusema ukweli,
na kwa mbali kitaswira nikamuona mdada, akitabasamu huku kashika shavu akinisanifu na kusema; 'masikini mhasibu...'.
‘Hebu sema
ukweli wako, wewe siku hiyo ulikuwa na ndevu?’ akauliza wakili huyo
‘Hapana, sikuwa
na ndevu , na hata nikiwa nazo huwa nazikata, huwa zinaota kidogo sana, lakini
sio kwa kiasi hicho mlichosema nyie....na sina tabia ya kufuga ndevu...’nikasema
‘Ukumbuke
upo chini ya kiapo, tena cha dini yako, je ni kweli kuwa siku hiyo hukuwa na
ndevu, na kwanini mlinzi anasema kuwa yeye aliongea na mtu mwenye ndevu, ina
maana yeye anasema uwongo, je sio wewe unayesema uwongo, wakati umeshaapa, hivi
wewe kweli unamuamini mungu wako?’ akaniuliza
‘Ndio
namuamini mungu wangu,...’nikasema
‘Na unakiri
uweli kuwa haya unayotuambia ni ya kweli yote, kuwa wewe siku hiyo hukuwa na
ndevu?’ akauliza na kabla sijajibu wakili wangu akaingilia kati kuwa wakili
huyo analazimisha nitoe jibu kwa vitisho
‘Ndugu
muheshimiwa hakimu, simuulizi kwa vitisho, hapa tunachohitajia ni ukweli, na
ukweli ulivyo ni kuwa huyu jamaa ndiye aliyekuwa humo ndani, na kwa kauli yake mwenyewe
amesema hakuna mtu mwingine aliyeongea na mllinzi zaidi yake, ina maana ni yeye
aliyeongea na mlinzi, na mlinzi anasema mtu aliyeongea naye alikuwa na
ndevu,..je huyo mtu ni nani, mwenzetu huyu anasema hamjui, ...sasa tutaelewaje,
na huyo mtu mwingine ni nani....’akasema kama anauliza
‘Ina maana
kulikuwa na mtu mwingine, ambaye wao hawakumuona, ...je huyo mtu mwingine
ambaye wao hawakumuona ni nani, ...?’
akauliza swali na kuniangalia machoni
‘Mimi simjui
huyo mtu mwingine....’nikasema nikionyesha udhaifu wa sauti
‘Muheshimiwa
hakimu, hii inaonyesha jinsi gani huyu sivyo mkweli na nahisi anataka kuficha
ukweli, ni kwa amsilahi ya nani,...kwa mtizamo huo tunaweza kumuhukumu mtu
asiye na kosa, ..’akasema wakili mtetezi,
na wakili akaambiwa athibitishe hilo.
‘Mimi
nitalithibitisha hilo kuwa mshitakiwa kakamatwa kimakosa , kuna mtu mwingine
ambaye anastahili kukamatwa kwa kosa hilo, lakini hajapatikana...’akasema na
kunigeukia mimi, akauliza;
‘Mhasibu,
wakati ukiwa humo ndani, wakati marehemu alipokulazimisha uingie naye ndani
mkiwa na huo mzigo, ni kitu gani kiliendelea?’ nikaulizwa
‘Niliingia
na marehemu akiwa nyuma yangu akiwa kanielekezea bastola, na tulipofika
chumbani mdada hakuwepo, hakuwa kalala chumbani kwake, alitoka, na ndiyo
ilikuwa nusura yake kwani marehemu alishajiandaa kumfanya lolote, na mara mdada
akatokea akiwa keshabadilika, akaweza kumdhibiti marehemu, na marehemu akawa
hamuwezi tena mdada, mimi baadaye nikapigwa na kitu kichwani,....’nikasema
‘Unasema
mdada alikuwa keshabadilika, kwa vipi?’ nikaulizwa
‘Alikuwa
kapagawa ,kashikwa na mashetani, huwa hali hiyo humtokea mara kwa mara, na
akiwa hivyo anakuwa na nguvu za ajabu....’nikasema
‘Umesema
mdada aliweza kumdhibi marehemu na bastola ikawa imemtoka mikononi,na unasema
kuna muda ulipigwa na kitu kichwani, je ulipigwa na kitu gani?’ nikaulizwa
‘Nahisi ni
nyundo..’nikasema
‘Unahisi
lakini huna uhakika?’ akauliza huyo wakili
‘Ndio nahisi
maana sikuona hicho kitu..’nikasema na wakili mtetezi akamuangalia wakili
muendesha mashitaka aliyeonyesha kama anataka kuingilia kati, lakini wakili
huyo akabakia kimiya na wakili mtetezi akauliza.
‘Kwanini
wewe ulihisi kuwa ni nyundo, na sio jiwe au kitu kingine?’ akaniuliza
‘Kwasababu
nyundo inafahamika, mtu akikugonga nayo ni tofauti na jiwe, kwa mtu unayefahamu
nyundo utajua kabisa hiyo ni nyundo iliyonigonga..’nikasema
‘Lakini
hukuwa na uhakika kabisa kuwa hicho ulichopigwa nacho ni nyundo, inawezekana
ikawa kitu kingine kinachofanana na nyundo?’ akauliza wakili mtetezi
‘Inawezekana
lakini kiwe na mfano huo ....’nikasema
‘Je ulimuona
huyo aliyekupiga na hiyo nyundo?’ akauliza
‘Sikumuona
kabisa...’nikasema
‘Je wakati
upo hapo, akili yako ilikuwa sawa, kuwa ulikuwa na uwezo wa kuona vyema, na
kuangalia huku na kule?’akauliza
‘Ndio sikuwa
nimepoteza akili, niliweza kuona vyema, siwezi kusema niligeuka sehemu zote,
hapana, kwasababu muda mwingi, na hasa kwa muda huo nilikuwa namuangalia mdada,
na wakati mwingine marehemu, kwani muda huo alikuwa hai...’nikatulia kidogo
‘Nilikuwa
namuangalia mdada, kwani alikuwa sio yeye tena, na nilikuwa natafuta mwanya wa
kukimbia lakini pia, niliogopa marehemu anaweza kuiwahi ile bastola na kumpiga
nayo mdada...’nikasema
‘Kwahiyo
muda wote huo, humo ndani mlikuwa wewe, mdada na marehemu?’ akaulizwa
‘Kwa ufahamu
wangu ndio tulikuwa sisi watatu tu...’nikasema
‘Kwanini
unasema kwa ufahamu wako, na nimekuuliza swali la kupambanua ufahamu wako, kuwa
je ulikuwa na akili timamu, ulikuwa na akili ya kwueza kujua kinacotokea humo
ndani,ukakubali kuwa ulikuwa na akili timamu, au nikuulize tena hilo swali,
kuwa je wakati huo, akili yako ilikuwa sawa,..?’ akauliza
‘Nimesema
kwa ufahamu wangu kwasababu, inavyoonyesha, kulikuwa na mtu mwingine aliyeweza
kuja , kuingia bila mimi kumuona, na ndiye aliyenipiga na nyundo kichwani...’nikasema
‘Huyo mtu alitokea
wapi?’ akauliza kama anajiuliza , lakini akawa kaniangalia mimi
‘Siwezi
kujua...’nikasema
‘Kwahiyo
unahisi tu kuwa huenda kulikuwa na mtu mwingine...inawezekana hakukuwa na mtu
mwingine wakati huo, inawezekana kuwa mdada ndiye aliyekupiga na hicho kitu
kama nyundo?’ akasema huku kaniangalia, na sikujua ni swali au anatoa maelezo
na mimi nilipoona ananiangalia tu, nikasema;
‘Nyundo
ingetoka wapi, hakukuwa na nyundo humo ndani..’nikasema kwa mshangao
‘Una uhakika
gani, ina maana wakati umo humo ndani uliweza kukagua nyumba yote na ukahakikisha
kuwa humo ndani kulikuwa hakuna nyundo..mmmh, kumbe kweli, ...’akasema na watu
wakacheka na mimi niksema
‘Sio kweli,
hizo ni dhana zako tu, mimi nilifika hapo nikiwa mgeni kabisa, na nia na lengo
letu, ilikuwa kumsaidia mdada...’nikasema
‘Kama sio
kweli, hebu niambie wewe umesema ulikuwepo hapo kama mgeni, ulifika tu
kumsaidia mgonjwa...sasa una uhakika gani kuwa sio mdada aliyechukua nyundo,
iliyokuwa mahali anapopajua yeye akakugonga nayo kichwani? Akauliza
‘Nina
uhakika maana muda mwingi nilikuwa namuangalia mdada, kwani kwa muda huo ndiye
aliyekuwa ni tishia kwangu, kwahiyo inawezekana wakati naangalai hivyo, huyo
mtu alikuja kwa nyuma na kunigonga kichwani na nyundo, atakuwa alikuja kwa
nyuma akafanya hivyo..’nikasema
‘Wakati
unapigwa na hicho kitu kama nyundo ulikuwa umeangalia wapi?’ akauliza
‘Tulikuwa
tumeelekea mlango wa kutokea nje,....’nikasema
‘Kwahiyo
aliyekupiga na hiyo nyundo alikuwa katokea nyuma, ...iwe ni chumbani au chumba
chochote, sio kutokea nje....?’ akauliza wakili muendesha mashitaka
‘Ni kweli, kama
angelitokea mlango wa nje, wa kutoka nje ningelimuona,...’nikasema
‘Kwahiyo
wewe unakiri kuwa wakati wote ulipokwua humo ndani hukuwahi kumuona mtu mwingine
zaidi ya mdada na marehemu, ?’ akauliza
‘Ni kweli,
sikumuona mtu mwingine..’nikasema
‘Na mlinzi
alikuwa getini akilinda, na kama angeliingia ungelimuona akiingia pale mlangoni, sawa
au sio sawa?’ akauliza
‘Ndio
nigelimuona akiingia labda awe ameingia kwa kupitia sehemu nyingine...’nikasema
‘Kwani kuna mlango
mwingine wa nyuma wa kuingilia kwenye hiyo nyumba?’ akauliza
‘Hapana
nijuavyo mimi upo mlango mmoja tu wa kuingilia ndani...’nikasema
‘Unamuona
huyo mtuhumiwa hapo mbele, hukuwahi kumuona akiingia humo ndani?’ nikaulizwa
‘Sikuwahi
kumuona wakati huo, ...’nikasema na wakili mtetezi akageuka kumuangalia wakili
muendesha mashitaka kama ana swali, na wakili muendesha mashitaka akasimama na
kuanza kuniuliza maswali.
‘Umesema
kuwa muda wote wewe ulikuwa unamuangalia mdada, na kwa namna hiyo mdada alikuwa
keshatoka upande wa muelekeo wa chumbani, alikuwa muelekeo wa mlango wa kutokea
nje, akitaka kuwazuia, ...?’ akauliza
‘Ndio...’nikasema
‘Na pia
wakati huo, ulikuwa ukimuangalia marehemu asije akachukua hiyo bastola, kwahiyo
kuna wakati unamuangalia mdada, na kuna wakati unamuangalia marehemu ...?’
akauliza
‘Ndio...’nikasema
‘Kwahiyo
inawezekana wakati unamuangalia marehemu ambaye lengo lake ilikuwa kuichukua
hiyo bastola, huyo mtu aliyekuwa na nyundo, aliweza uingia kwa haraka, bila yaw
ewe kumuona?’ akauliza
‘Inawezekana,
lakini awe ni mtu mwenye uzoefu, na uharaka wa hali ya juu, ...’nikasema
‘Pia huyo
mtu anaweza kutoka chumbani au chumba chochote humo ndani,..’akauliza wakili
muendesha mashitaka na wakili mtetezi akapinga hilo swali kuwa yeye anamulekeza
shahidi kusema aonavyo yeye, na hakimu akakubali hilo pingamizi, na wakili
muendesha mashitaka akasema hana swali jingine na wakili mtetezi akaendelea na
maswali yake;
‘Wewe muda
huo ulikuwa sakafuni, ulikuwa umeangalia wapi?’ akaulizwa
‘Nilikuwa
nimeangalia muelekeo wa mdada, na wakati huo huo namuangalia marehemu...’nikasema
‘Na mdada
kwa muda huo alikuwa wapi?’ nikauliza,
‘Yeye
alikuwa anatemba mwendo ule kama wa kunyata, akitutafuta na alipotuona akawa
anakuja uelekeo wetu, nahisi alijua kuwa tumekimbilia nje, kwahiyo kwa muda ule
akawa kasimama nusu muelekeo wa mlango na nusu muelekeo wa kutokea nje..’nikasema
‘Kwa nyuma
yako kulikuwa na nini?’ nikaulizwa
‘Kwa nyuma yetu
kulikuwa ni muelekeo wa chumba cha mdada, na upande mwingine ni dirisha kubwa
la nje..’nikasema
‘Kwahiyo
huyo aliyekupiga na nyundo, alitokea kwa nyuma yako?’ nikaulizwa wakili
muendesha mashitaka
‘Ndio kwani
angelitokea kwa mbele yangu ningelimuona, na mdada angelimuona..’nikasema na
wakili mtetezi akataka kuniuliza swali lakini akasita na kuangalia saaa, na
hakimu naye akavutika na hali hiyo, akaangalia saa yake na kusema;
‘Muda
umekwisha, kama mna maswali zaidi dhidi ya huyu shahidi mtamuuliza siku ya kesi
ijayo, ...’akasema na mimi nikaweza kupumua, nikatoka na mbele yangu nikakutana
na mpelelezi, ambaye alionekana na furaha usoni, akasema;
‘Bado
unaendelea kuficha ukweli, sijui kwa masilahi ya nani’akasema
‘Nimeficha
ukweli gani?’ nikauliza
‘Akisimama
mtuhumiwa ukweli wote utajulikana na wewe hutaaminika tena, ...hilo ni kosa
kubwa umefanya, wewe unaongea kumlinda mdada, na mdada hana masilahi na wewe,
nikuambie ukweli, mwisho wa siku mdada atakuwa kamaliza kazi yake, na kupata
ajira yake, wewe utakuwa wapi?’ akaniuliza na mimi nikabakia kimiya.
‘Unajua
mdada anafanya hivyo kutokana na shinikizo la watu wake..na wewe anakutumia tu..’akasema kama ananiuliza
‘Akina nani hao watu wake?’
nikauliza nikionyesha mshangao, nikikumbuka kuwa siku hile huenda mdada alipoingia na kukutana na huyu mpelelezi watakuwa waliongea...
NB: Tuishie
hapa kwa leo
WAZO LA LEO: Kosa ni pale unapojua kuwa
unalotenda ni kosa na bado ukarudia hilo kosa, au kuukana ukweli pale unapojua
ni ukweli, lakini kwa sababu zako binafasi au sababu za masilahi, au shinikizo
la watu fulani,wewe ukaukana ukweli. Kumbuka kuwa msema kweli wakati wote ni
mpenzi wa mungu, je msema uwongo ni mpenzi wa nani....
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment