‘Umesikia kuwa kesi inayokuja mimi na wewe ndio tutasamishwa kizimbani kutoa ushahidi?’ nikamuuliza mdada kwenye simu, na mdada kwanza alitulia bila kusema kitu halafu akasema;
‘Yah, of course nimesikia,...’akajibu na kutulia kidogo halafu kabla sijatamka neno jingine akasema;
‘After all, kwasasa haitawezekana, hata hivyo, wewe una wasiwasi gani?’ akasema akionyesha mapozi kama vile haongei kwenye simu,na ilionyesha wazi kama anatafuna kitu, labda alikuwa akipata chakula.
‘Mimi wasiwasi wangu ni kuhusu ukweli ambao tunaendelea kuuficha, nimejitahidi sana kukwepa kuongea huo ukweli wote, lakini nahisi kwasasa sina ujanja ni lazima niwaambie kila kitu, na isitoshe moyoni naumia sana,…’nikasema
‘Ukweli gani tunaoendelea kuuficha, au ukweli gani wewe unaoendelea kuuficha, mimi sijakuambia usiseme ukweli,hebu niambie niliwahi kukuambia hivyo kabla, na kwanini uumie, sikuelewi kabisa..?’akasema madada na kuniuliza na kunifanya niingiwe na mashaka.
‘Ina maana mdada huioni hii hali, haki haitendeki, na ...halafu wewe upo tayari nielezee kila kitu,…?’ nikauliza nikianza kuingiwa na wasiwsi kuwa huenda mdada anataka kuniruka, na kunifanya mimi nionekane muongo.
‘Mimi sijakulewa ukisema ueleze kila kitu,kwani wewe wamekuuliza nini?’ akaniuliza akiendelea kujitafuna.
‘Wanataka nieleze kweli kuhusu yote yaliyotokea siku ile mtoza ushuru alipouwawa, na yote kuhusu mahusiani yangu mimi na wewe….’nikasema
‘Kwani hujawaambia huo ukweli,kuhusu yaliyotokea siku ile, ama kuhusu mahusiano yangu mimi na wewe sizani kwamba yanahusiana na hayo mauaji, na ni nani aweza kukuuliza swali kama hilo, hayo ni mambo binafsi, huyo atakayekuuliza hayo, mwambia aje aongee na mimi mwenyewe, unasikia, kwanza ni nani huyo..?’ akauliza
‘Mdada naona kama unanichanganya,unakumbuka mengi yaliyotokea mle, ambayo nahisi kama nitawaambia yote, ni lazima mimi na wewe tutakuwa hatarini’nikasema
‘Kwanini mimi na wewe tuwe hatarani,…?’ akauliza
‘Kwanza wewe uliniambia nibadili sura,wakati mtoza ushuru anafika,ili asinifahamu,hilo sijalisema, na pia wanataa kujua kuhusu huo mzigo aliokuja kuuchkua huyo mtoza ushuru, na tatu, kwa kiasi kikubwa wanamtaka huyo jamaa aliyekuwa na ndevu, wanasema huyo ndiye aliyemuaa mtoza ushuru,….’nikasema
‘Kwani huyo mtu mwenye ndevu ni nani, na je ni kweli kuwa huyo mtu ndiye aliyemuua mtoza ushuru?’ akaniuliza
‘Unamfahamu huyo mtu ni nani, usitake kusema humfahamu, na ni sawa, sio kweli kuwa ndiye aliyemuua huyo mtoza ushuru, lakini kwa mtizamo wa polisi wanadai hivyo, ndio maana mpaka sasa mimi sijasema huo ukweli..’nikasema
‘Kwa mfano kama ungesema hivyo, kuwa wewe ndiye huyo mtu aliyekuwa na ndevu, je mimi nitakuwa kwenye matatizo gani?’ akauliza
‘Ina maana sasa unaniruka, wewe si ndiye uliyenipa hizo ndevu na ukanivalisha mwenyewe, mdada ina maana sasa hivi wewe upo tayari mimi nishikwe kwa mauaji ambayo sijayafanya, wakati yote hayo yametokawa kwasababu yako wewe, nisingelifanya hayo yote kama isingelikuwa ni wewe ....’nikasema kwa hasira
‘Una uhakika na hilo?’ akauliza huku akiendelea kujitafuna
‘Uhakika...uhakika gani?? ‘nikauliza
‘Wewe mwanaume hebu kwanza jiamini, usiwe mtu wa kuyumbishwa, unavyoongea utafikiri sio mwanaume, usitake nikuzalilishe, unaanza kuniharibia apetite yangu, hata hiki chakula sikitaki tena…’nikasema kitu kikitoa sauti, nahisi ni kiti kilikuwa kikirudishwa nyuma.
‘Sikiliza wewe mwanaume, kama hujafanya kosa huna haja ya kuogopa,kama wanamtafuta huyo mtu aliyekuwa na ndevu, waachie wamtafute hiyo sio kazi yako,…kama ni wewe basi waache wakukamate, tutajua mbele kwa mbele, lakini..eeh, huyo muuaji sio ndio keshakamatwa au ?’akasema na kuuliza mwishoni
‘Kwahiyo niendelee kudanganya, au niseme kila kitu, ....maana kiukweli mimi ndiye huyo mtu mwenye ndevu, na huyo ndiye waliyekwua wakimtafuta kwa muda mrefu, .....na kilichosaidia ni kuwa wamegundua kuwa huyo mlinzi ndiye mshukiwa wa hayo mauaji, sijui itakavyokuwa huko baadaye...unanishauri nini kwa hilo, nikisimamishwa kizambani niseme nini?’ nikauliza
‘Kwani wewe una ndevu,?’akauliza
‘Ninazo,lakini mara zote huwa nazikata’nikasema
‘Kama ni hivyo, huna haja ya kuongopa, cha muhimu ni wewe kusema ukweli, na hilo swala la kuwa wewe ustasimamishwa kizambani, kwasasa halipo, na kama itatokea hivyo, basi wewe hauna haja ya kusema uwongo, wewe sema ukweli ulivyo,mimi ndivyo ninavyokushauri, kama umeongopa hilo ni tatizo lako,unanisikia wewe mwanaume..’akasema
‘Na je wakiniuliza kuhusu mahusiano yangu mimi na wewe niseme nini,..?’ nikauliza
‘Kuhusu mahusiano yangu mimi na wewe kuhusu nini, jibus lipo wazi, waulize na wao mahusiano yao na wachumba au wake zao...tumia akili kidogo, je hapo huna jibu la kusema au nikufundishe kila kitu, hivi wewe shule ulifuata nini, unafikiri shule ni kukariri tu mpe na mtoe,...amuka mwanaume.. masikini mhasibu....’ akanisema na akawa kama anacheka.
‘Unawafahamu mawakili walivyo, mimi nina uhakika watafikia hadi kuniuliza kuhusu mambo yako unayoyafanya, uliyonifanyia mimi na mtoza ushuru?’ nikasema
‘Mambo gani hayo niliyokufanyia au kumfanyia huyo marehemu hebu kuwa muwazi zaidi...?’ akauliza
‘Kuhusu hayo mapicha mabaya uliyochukua kwangu, na ukayatumia kunitishia na kuwatishia watu wengine uliowahi kuchukua mapicha kama hayo kwa ajili ya kupata pesa..’nikasema
‘Una uhakika na hilo unaloliongea na je unayo ushahidi na hizo shutuma zako wewe mwanaume...?’ akauliza kwa sauti nzito kuashiria kakasirika.
‘Ushahidi eeh, sasa unahitajia huo ushahidi, unataka niwaonyeshe na huo ushahidi, au sio….ndio ninao nitawaonyesha simu yangu, inayo hayo mapicha uliyowahi kunitumia…’nikasema
‘Ok, waonyeshe....na nimuhimu kabla hujasema hayo uwe na uhakika,....’akasema
‘Uhakika wa nini wakati umenitumia hayo mapicha na yapo kwenye simu yangu, sijapata muda ya kuangalia vyema, nita...’akasema
‘Hebu tafuta kwenye simu yako uangalie vyema kama kuna mapicha mabaya niliyowahi kukutumia, usipende kuropoka ropoka mambo ambayo hayapo kabisa, hebu angalia haraka usinipotezee muda…’akasema,
Nikakumbuka kweli kuwa siku mbili zilizopita nilijaribu kutafuta ujumbe wa maneno na picha alizokuwa akinitumia mdada kwenye simu yangu, lakini sikuweza kuupata,ni kama kuna mtu alichukua simu yangu akafuta ujumbe wote uliotoka kwa mdada, japokuwa alikuwa akitumia namba isiyo na jina.
‘Mdada usinifanye mimi mjinga, unajua kabisa weweuliwahi kunifanyia hivyo, na ukakiri mbele yangu kuwa hiyo ndiyo kazi yako, ambayo pia ulimfanyia mtoza ushuru na watu wengi kwa nia ya kupata pesa, sasa unanikana kwa vile unaona maji yamefika shingoni…’nikasema na yeye akacheka kidogo.
‘Masikini mhasibu, hivi wewe una uhakika na hicho unachokisema, hebu ongea mambo yenye maana,...hivi nikuulize umenipigia simu kuniambia mambo ya maana au ni huu upuuzi wako, kwanini unapenda kupotezea watu muda wao...nilikuwa nakula, hata hamu ya kula tena haipo...upuuzi mtupu...’akasema kwa hasira
‘Ina maana mdada hayo hayana maana ....?’ nikamuuliza
‘Mhasibu nakuonya tena, sitaki unipigie simu ,kwa upuuzi kama huo,sitaki itokee tena,mimi nina mambo mengi ya kufikiri, hapa nilipo nawaza jinsi gani ya kulimaliza hili, na maisha yako ya baadaye, hilo wewe halikujii akilini, au unafikiri nitaishi na mume asiye-eleweka, wewe mwanaume hebu funguka akili yako, na jitahidi kuwa makini kwa kauli zako,….unasikia, kuna jingine?’ akaniuliza
‘Ni kuhusu mchumba wangu alinipigia simu..’nikasema
‘Mchumba wako! Mhh nani huyo, ni yupi huyo?’ akaniuliza na ilionyesha ni kama mshituko kwake
‘Kwani mimi nina wachumba wangapi?’ nikauliza kwa mkato
‘Nakushangaa mhasibu maana nijuavyo mimi ,....mimi ndiye mchumba wako, au kuna wanawake wengine wamenizidi,....je mimi nilikupigia simu nikakuambia nini?’ akauliza kama vile anafanya mzaha, lakini alikuwa akiongea bila wasiwasi.
‘Mdada haya ninayokuambia ni umuhimu sana, sio maswala ya utani, naomba unielewe ….’nikasema
‘Ongea hayo mambo muhimu niyasikie, kama hayo ndio unayaita mambo muhimu, unaniabisha mpenzi wangu, be serious..dear, haya hebu niambie, kuna nini kimetokea,…’akasema
‘Binti,alinipigia simu kunionya kuwa familia yao imepanga kuniua mimi na wewe, kwani sisi ndio maadui wa familia yao…’nikasema na yeye akacheka sana halafu akasema;
‘Masikini mhasibu, ina maana hapo ulipo miguu inacheza cheza kwa uwoga, pole sana, lakini wewe ni mwanaume au sio, hustahili kuogopa, kwani nikuulize wewe naogopa kufa?’ akaniuliza huku akiendelea kucheka
‘Mimi namekuambia jinsi nilivyoambiwa na binti sasa kama wewe unanona ni mzaha shauri lako...’nikasema
‘Huyo binti unayemuongelea hapo ndio huyo aliyekuwa mchumba wako wa zamani, au sio?’ akauliza
‘Ndio huyo mchumba wangu...’nikasema
‘Hebu rudia tena....’akasema mdada kwa sauti ya kukereheka
NB: Naona hapa tutakesha tukutane tolea lijalo
WAZO LA LEO: Unapojaliwa kuwa na mali, au maisha mema, au sifa yoyote ile, usipende kuwadharau wale wasiojaliwa na hali hiyo, utajiri wako , mali yako na cheo chako, ni vyako, havitakuwa na maana kama wale wanaokuzunguka watakuwa wanakuchukia na kukuombea mabaya. Utajiri ulio bora ni wema wako kwa wenzako.
Ni mimi: emu-three
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment