Kesi ya
mauaji ya mtoza ushuru ilianza kwa kasi waendesha mashitaka wakiwa wamejipanga vyema, wakiwa na ushahidi na vielelezo vyao, na muendesha mashitaka alitamba kuwa kesi itakiwsha mapema, kwani kila kitu kipo tayari, na hali ilivyojionyesha ni kuwa mlinzi
huyo ndiye muuaji, japokuwa alikana shitaka hilo kuwa yeye hakuua.
Muendesha
mashitaka akawa anamuita shahidi mmoja baada ya mwingine, wakifuatilia tukio
lenyewe lilivyokuwa, na kila shahidi aliyesimamishwa kutoa maelezo yake ilionyesha
wazi kuwa mlinzi wa mdada yupo hatiani. Hata ule usemi wa avumaye bahari papa,
kumbe samaki wengine wapo ukasahaulika. ushuru
Wakati wa
mapumziko nikapata muda wa kukaa na mpelelezi, ambaye mara nyingi alionekana akitoka
na kuingia, kila simu yake ilipoita, kwa vile sikuwa mbali nay eye, niliweza
kusikia mngurumo wa taratibu wa kuashiria kuwa kuna mtu anataka kuongea nay eye,
kwa hali kama ile, sizani kama alipata muda mzuri wa kuifuatilia hiyo kesi, nilipokaa
naye nikamuuliza
‘Kwa jinsi
kesi ianvyokwenda, inaonyesha wazi kuwa kweli huyu mlinzi ndiye aliyemuua mtoza
ushuru,au wewe unasemaje?’ nikamuuliza
‘Mengi
yaliyotokea huko ndani imekuwa ni kazi kubwa sana kuupata ukweli wake,kwani
wote waliokuwa huko ndani hawataki kusema ukweli,ukiwemo wewe mwenyewe, nah ii inanipa
shaka kwua huenda haki isitendeke, ...’akasema
‘Kwa vipi,
wewe mwenyewe umeona maelezo ya mashahidi na jinsi tukio lilivyokuwa, ukweli
wote umeshatajwa, unataka mimi niseme nini tena....’nikalalamika.
‘Una uhakika
na hilo, ...?’ akaniuliza
‘Uhakika kwa
vipi, kwani wewe ulitaka niseme nini tena, ?’ nikamuuliza
‘Una uhakika
kuwa hayo yaliyosemwa na hao mashahidi yana ukweli wote, sikatai kuwa waliyosema
sio kweli..ni kweli maana mengi ya hayo niliyaona mwenyewe kwa amcho yangu,
lakini bado kuna ukweli mkubwa haujasemwa,....’akasema
‘Kama upi?’
nikamuuliza
‘Hebu
niambie huyo mtu aliyekuwa na ndevu ni nani, ...?’ akaniuliza
‘Unarudi
kule kule,...nilishakuambia mimi huyu mtu simjui, huenda huyo mlinzi alitunga
uwongo wake tu...’nikasema
‘Una uhakika
na hilo?’ akaniuliza
‘Sasa kama
wanasema alikuwepo mtu kama huyo kwanini huyo mtu asikamatwe kama muuaji,..?’
nikamuuliza
‘Hajaonekana...ndio
maana nakutaka wewe uniambi ukweli, kwanini huniamini,...nataka kumaliza hii kesi,
kabla hukumu haijatolewa...’akasema
‘Mimi
nilishakuambia, hakuna mtu kama huyo, ..mimi sikumuona, hata huyo mlinzi
mwenyewe sikumuona akiingia, kwahiyo kiukweli, mimi ni kama vile nilikuwa nje,
kipigo cha mdada kilinipoteza akili, na huyo aliyenipiga nyundo kichwani ndiye
akanimaliza kabisa, sikuona ...na akili hakuwa na utulivu wa kuona kilichokuwa
kikiendelea...’nikasema
‘Kama unavyoona
maelezo yote wanayotoa hao polisi, hawajauliza jinsi gani huyo mlinzi
alivyoingia, hiyo imekuwa siri ya mlinzi na watu wake waliomtuma,...kama
ningeliupata ukweli angalau kidogo ningeliweza kuyageuza haya mashitaka, na
kuelezea mahakama kuwa mlinzi hajasema ukweli wote, lakini bado sijapata
ushahidi wa kutosha….’akasema
‘Ina maana
ungeliwaambia polisi kuwa huyo mlinzi alipitia dirishani, lakini wewe mwenyewe
umesema hufanyi kazi na hao polisi, kwanini sasa unavunja miiko ya kazi yako…?’nikamuuliza
‘Mimi
nafanya kazi kwa mtizamo wangu,..na sio kwamba sifanyi kazi na polisi, ila kwa
tuklio hili, imabidi nijitenge, kwa jinsi ilivyokuwa, lakini mwisho wa siku
nikishakamilika,natakiwa kuonana na hao hao waendesha mashitaka....’akasema
‘Kwa mtizamo
wako, umesema huenda haki isitendeke,
kwa vipi una hisi mlinzi sio yeye aliyemuua mtoza ushuru?’ nikamuuliza
‘Tutaona
huko mbele,…siwezi kusema lolote kwa sasa, ila bado kuna sintofahamu kwenye hii
kesi, ...na nakupa nafasi ya mwisho ya kufikiri, uniambie ukweli wote kabla
hukumu haijatolewa, ukumbuke, mlinzi sasa hivi yupo kubaya, atahukumiwa kwa
mauji na huenda sio yeye muuaji, huoni huo ni unyama...’akasema na marasimu
yake ikiita
‘Samahani
kidogo niongee na hii simu,...’akasema na akasogea pembeni na haikupita kidogo,muda
wa mahakama ukawa umeshafika, na mashahidi mbali mbali waliendelea kuitwa,
wakiwemo askari waliofika, ambao waliwahi kunikamata mimi, na muda ukawa
umeisha kesi ikaahirishwa.
‘Jiandae
mhasibu, nitakusimamisha kama shahidi...’ilikuwa sauto ya muendesha mashitaka
akiwa anapita pale nilipokuwa nimesimama nikimsubiri mpelelezi,
‘Mimi
hapana, kwanini....?’ nikauliza
‘Wewe na
mdada zamu yenu imeshafikia, mjiandae , nitaongea na nyie baadaye ili kuyaweka
mambo sawa...’akasema na kunikabidhi barua, na hakutaka kuongea na mimi kwa
kirefu,akaondoka, nilibakia kama mtu aliyepigwa kofi la kushitukiziwa
‘Vipi,
nasikia kesho kutwa kesi ikiendelea wewe na mdada huenda mkasimamishwa kutoa
ushahidi?’ sauti ya mpelelezi ikanishitua toka kwenye lindi la mawazo,
nikageuka kuangaliana naye, na akawa akiniangalia usoni, na mimi nikasema;.
‘Kaniambia hivyo
muendesha mashitaka, na mimi sikupenda kusimamishwa kwasasa, japokuwa nafahamu
kuwa muda wangu utafika na mimi nitoe ushahidi wangu, lakini hata hivyo naona
kama sijajiandaa kwa hilo’nikasema.
‘Kujiandaa
kwa vipi?’ akaniuliza
‘Hata sijui,
najiona kama nipo njia panda, na sijui nitaulizwa nini, na je hayo
nitakayoeleza hayataweza kuwaathiri, watu nisiopenda ...’nikatulia
‘Tatizo lako
unajaribu kukwepa ukweli, kwa hivi sasa huna ujanja ukweli wote unatakiwa
usemwe, ili haki itendeke, nilishakuuliza toka awali, uniambi ukweli, ili na
mimi niwee kukushauri, lakini hujapenda kufanya hivyo, ngoja usimame kiziambani
huenda ukazindukana...’akasema
‘Naona iwe
hivyo, nikisimama kizimbani nitasema yale yanayostahili...nitajitahidi kufanya
hivyo, lakini, sio kuwa hayo ninayofahamu mimi yataweza kubadili mstakabali
mzima wa kesi hii, sizani maana kiukweli mimi sijui lolote, ..’nikasema huku
nikijaribu kuwaza ni ukweli gani anaoutaka huyu mpelelezi.
‘Nikuambie
ukweli, mauaji ya mtoza ushuru, ni sehemu ndogo tu ya tatizo lenyewe, kuna
kundi haramu lililojianzishia himaya na sera za umimi, wao walishajiona ni watawala
wa kudumu, wanaweza kufanya wapendavyo...hili kundi ni lazima ling’oke...’akasema
‘Kundi gani
hilo?’ nikauliza
NB: Nawatakia
wikiendi njema.
WAZO LA LEO:Kuua damu isiyo na hatia ni kosa
kubwa sana, kumsingizia mtu ubaya asioutenda ni dhuluma kubwa sana, tuwe
wakweli na pale tunapotoa shutuma tuwe na uhakika nayo, kwani huwezi kujua ni
kwa jinsi gani unavyoweza kumuathiri mtu mwingine kwa kusingiziwa kosa asilolifanya.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment