Sikuamini kuwa kweli nimetolewa , japokuwa ni kwa
dhamana, na hata nilipotpka nje, bado
nilikuwa na wasiwasi, nikawa nageuka nyuma, nikihisi kuwa nitaambiwa nirudi. Kwa ujumla kipindi masiku niliyokaa hapo mahabusu kilikuwa ni kipindi cha mateso kwangu ambacho sikuwahi kukutana nacho kabla....
Hata hivyo, ni kweli nimepata dhamana, je ndio itakuwa nafasi ya kuweza kupigania ukweli wa hili jambo, ili haki itendeke, kwa vipi, sikuwa na uelewi kwa muda huo, nilihisi kuwa na wasiwasi zaidi, na nikajikuta nikiangalia huku na kule, kama kumtafuta mtu nisiyemfahamua ni nani....
Kwa ujumla aliyefanya hayo
yote hdi dhamana kupatikana ni wakili aliyetafutwa na mdada, akishirikiana na mdada mwenyewe, sikuelewa
ni kwa jinsi gani waliweza kulifanikisha hilo..na kwa muda huo , sikujali sana ni hilo, kuwa ni jinsi gani walifanya,mimi nilikuwa na jambo jingine lililokuwa likinisumbua, kuwa sasa naingie kwenye mtego mwingine, ukweli, ...
'Sasa naumbuka....'nikajisemea kimoyoni..
Tuendelee na kisa chetu......
Wakati nipo na mdada, tunaongea kumbe wakili naye
alishafika, yeye alipita moja kwa moja kwa wahusika, kufuatilia hatua za mwisho
za hiyo dhamana, hakukuwa na kipingamizi kwani wakubwa walishapitisha, kwahiyo,
wale wahusika wa hapo walichofanya ni kuweka kumbukumbu zao sawa kuwa kweli nilikuwepo
hapo na nimeachiwa kwa dhamana.
Nilipomaliza kuongea na mdada, nikarudi mahabusu...nikiwa
sijakuwa na uhakika wa dhamana hiyo japokuwa mdada alinigusia kuwa
imeshapiitishwa. Kwahiyo niliporudi ndani, nikawa nimetulia nikisubiria tu.
Haikuchukua muda nikaitwa na kuambiwa niende sehemu ya
kuchukua vitu vyangu, kwani nimeshakubaliwa dhamana yangu..sikuamini kuwa kumbe
ni kweli,...basi nikafanya hivyo, na baadaye akaja wakili, tukawa tukatoka naye
hadi sehemu ya kusubiria mambo mengine ambayo yalikuwa hayajakamilika, na hapo
tukawa tunaongea na huyo wakili
‘Bahati yako, hukupelekwa huko gerezani, ungepelekwa huko
kazi yake ingekuwa pevu, maana huko bwana, kutoka kwake ni mpaka twende
mahakamani...na jamaa wa kule sio wote ninaofahamiana nao, kazi yetu hii
inakuwa rahisi kama unafahamiana na watu...na watu sio kila mtu...’akasema huyo
wakili huku akitikisa kichwa. Mimi niligeuka kumwangalia, na nilipoona yupo
kimiya nikasema;
‘Mhh, hata hivyo
mpaka sasa sielewi kinachoendelea....’nikasema na kugeuza kichwa kuangalia
mblele halafu nikageuka kuangalia huku huku na kule, nilikuwa kama namtafuta
mtu, au kuonyesha mashaka fulani.
Ni kweli, moyoni nilikuwa sijiamini,...na hata hivyo sikuwa
na uhakika hasa ni kitu gani ninachokiogopa au kuwa na wasiwasi nacho, je ni
kutokuamini kuwa niko angalau huru kwa muda, au kuna jambo jingine linanisumbua
kichwa changu. Nahisi nilikuwa naona aibu, nahisi, kama vile naogopa
kufaminiwa, japokuwa sipo kwenye tendo la kufamaniwa, kiukweli, nilikuwa kwenye
wakati mgumu, na Wakili aliponiona jinsi ninavyohangaika, akaniuliza;
‘Naona kama hujatulia, una wasiwasi gani?’ akauliza
‘Wasiwasi eeh, umeonaeeh!? Mmh, , ..hapana, siunajua tena,
ni lazima ukiwa sehemu kama hizo, unakuwa kama hujiamini vile, hivi wewe
ulishawahi kufungwa, kama hivi...?’nikasema na kuuliza
‘Hahahaha, Unaonaeeh,.....ndio hapo uone umuhimu wetu, kama
sio sisi ungelikuwa wapi, ....hahahaha, mimi bwana kama nikufungwa
ningelishafungwa sana, lakini ujanja, na kutumia hii....ndio maana sijawahi
kufanywa hivyo.....’akacheka kwa sauti ya kitajiri, huku akigusa kichwa chake
kwa kidole, kuashiria kuwa anatumia akili, na huku akinipiga piga mgongoni kwa
kiganga cha mkono wake.
‘Mshukuru sana mdada, amefanya kazi kubwa sana, huyu
mwanamke sio mchezo anajiamini na anaweza, japokuwa mimi ni wakili wake, lakini
bila ya juhudi zake, na kujotolea kwenda kuongea na watu mashuhuri,
tusingelifanikiwa kabisa, ....nimekuwa naye sambamba, nikifuatilia yale mambo
ya kisheria,na kumshauri hili na lile, lakini mwanamke huyu ni jembe ....’akatulia
na kusimama, kama vile kasahau kitu, halafu akanigeukia na kusema;
‘Yule wakili wa kampuni yako aliwahi kuja tena,...?’
akaniuliza
‘Hajawahi,....’nikasema nikijiuliza hata mimi ilikuwaje ,
huenda aliongea na mdada,akamueleza kuwa hahusiki tena.
‘Nikuambie ukweli kama ungelibakia na huyo wakili wako wa
kampuni, ambaye ninayemfahami, ni wale watu, wanaotaka kufuata utaratibu,
.....wewe kwenye nchi zeutu hizi utafuata utaratibu, ...hao wasimamizi wenyewe
wa utaratibu hawafuati utaratibu, wewe ujifanya unafuata utaratibu
utakesha...kuna wakati unatakiwa uchukue maamuzi magumu, japokuwa sio
utaratibu...’akasema
‘Ina maana....?’nikasema
‘Ninachotaka kukuambia ni hivi, kila mara unatakiwa uangalie
alama za nyakati, unafahamu...., ukiona kunastahili hiki fanya hivyo, dalili
zitajionyesha, ..cha muhimu ni kuiiamini, angalia dalili kwanza kama kuna
uwezekano, kama hakuna angalia mbadala wake, hii ni nchi yetu tunajijua
wenyewe, akili ichanganye, tumia bongo, ....’akawa kama anaonyesha kichwa chake
kwa kidole.
‘Sasa kwa hili lako, nimelisoma kwa makini, kiujumla, hakuna
ushahidi wowote wa kuwabana nyie, ndio, bastola ina alama zenu za vidole,
lakini kwa hali hiyo, sio ajabu, ....cha muhimu hapo ni muda wa tendo, muda wa
mdada kupoteza fahamu....hapo inabidi kumshukuru docta....’akatulia
‘Muda ....muda na muda ambao wewe ulitoka nje, ...utakuta
mauaji yale yalifanyika muda ambao wewe haupo na mdada keshapoteza
fahamu,....ndio muda ambao jamaa alipigwa risasi,...hapo muda unawabana,wameshindwa
kuweza kuliunganisha hilo...’akaulia
‘Ama kwa ushahidi mwingine uliopatikana,huna mshiko, hauna
vigezo...na ukilinganisha na matukio yenyewe, unakuta nyie mpo salama, kuna
jingine la msingi, ....’akageuka kuangalia nyuma.
‘Lipi hili?’ nikamuuliza
‘Kuhusu huyo mtu mwingine, aliyekuwa na ndevu,hilo ndilo
polisi wanalitafuta , huyo mtu ni nani, na wao wameshikilia kuwa ndiye muuaji,.swali
kubwa hata mimi najiuliza,huyo mtu ni nani,na kwa hivi sasa ni bora
asipataikane kwanza ...akipatikana tu kuna mawili,yeye akawa muhusika, au akalta
matatizo, hata hivyo huenda kupatikana kwake, kukaimaliza hii kesi, au kuzua
balaa jingine....’akasema
‘Huyu mtu hawezi kuwa ndiye muuaji, kumbuka, wakati mimi
natoka sikuwahi kuona mtu mwingine yoyote, niliwaacha mdada na
marehemu...’nikasema
‘Atakuwa alijificha, na inaonekana anamfahamu sana mdada na
matatizo yake hayo, kwahiyo alikuwa anajua nini anachokifanya, ndio maana
hamkumsogelea, au atakuwa kafanya namna ambayo hisia za mdada zisingliweza
kumnasa, hayo yanawezekana, hata hivyo kwa
jinsi docta anavyosema, hata kama angejificha wapi, mdada akiwa katika hali
hiyo angemuona, kwani anakuwa na hisia kama za mbwa, ananusa na kujua chochote
kilichopo karibu yake, ...’akasema
‘Kwahiyo...unataka kusema nini hapo?’ nikauliza
‘Hapo ni kitendawili,...tega ni tege, na mteguaji sio kazi yetu.hiyo ni kazi ya polisi...tuwaache wao
wafanye kazi yao, ...na hapo inanituapa muda wa kujipanga vyema, .unaonaeh,
ndio maana tunataka tukae pamoja tuone hilo tutafanyaje ikiwa hivi au vile,...kwani
hatima ya yote hayo, kuna kusimama mahakamani...una ona hapo,...’akasema
‘Mimi bado nashindwa kumuelewa huyo mtu mwingine, mbona
anakuwa ni jinamizi, mimi nilikuwepo mle ndani sikumuona, hapana, siamini, mna
uhakika kulikuwepo na mtu mwingine humo ndani....?’ nikauliza
‘Nimeshakuambia hilo halituhusu kwa sasa, hiyo ni kazi
yao,...unafahamu....wakati wanahangaika hivyo,...sisi tunafanya yetu, kwa
ujumla, hapa hakuna kesi kabisa dhidi yenu, kama kweli mliyoniambia ndivyo
ilivyokuwa, basi kesi hapo hakuna, vinginevyo, labda muwe mumenidanganya,...’akasema
na kuonyesha mkono wa ushindi.
‘Mdada yeye anasema nini kuhusu huyu mtu wmingine?’
nikamuliza
‘Mdada, mhhh, achana anye huyo, tatizo ni kwako,...hata
hivyo, ya mdada yaache pembeni kwa sasa, hayakuhusu usijichanganye kabisa na
kuhusu yeye....’akatulia
‘Mdada ana kinga ya kitaalamu, kwa kipindi hicho hakuwa
yeye, kama wanataka wamtafute huyo
aliyekuwa ndani yam dada kipindi hicho, sawa, ....unajua vitu kama hivyo
visikie tu, mashetani kuapagawa , kuchanganyikiwa, mmmh, hata mimi siamini...’akatulia
kama akiwaza jambo.
‘Mimi mwenyewe nilipiga kichwa hapo, nikaongea na docta, docta
wakeeeh,mmmh, kanihakikishia mambo hayo yapo na yanatambulikana kitaalamu, yapo
kwenye kundi la watu wenye matatizo ya ubongo, akili, yeye anaweza kuhakiki hilo kitaalmu, ,.....unaona
hapo, ndio maana yeye mambo yake tulimaliza kirahisi tu, ...kwenye sheria mtu
mwenye matatizo ya akili, hana hatia, anakinga..hahaha, haya mambo ukiyajulia,
unapeta...’akasema.
‘Kwa namna hiyo vyovyote iwavyo, mimi ndiye ninayebakia
hapo, kuwa nastahili kujibu kesi, kwa vile mdada hayupo tena...?’ nikauliza
nikionyesha wasiwasi.
‘Mhh, usiumize kichwa chako kwa hilo, hiyo ni kazi yao,na
kazi yangu kukutetea,...kuna watu wanalipwa kwa kazi hiyo, hatuna haja ya sisi
kumiza kichwa saaana, mimi nitakachofanya ni kucheza na vipengele vya
sheria...wenyewe wanasema mambo mazuri hayatai haraka, au sio, sasa sisi
tunakuwa kama yule ndege mla mizigo, hana pupa, anasubiri udondoke tu,
....unaona hapo..’akasema akionyesha kweli hana wasiwasi.
‘Mhh, ni lazima niwaze, kwa hilo....’nikasema
‘Unasikia sana, ukiwaza jambo ukaumiza kichwa kuwa huenda
itakuwa hivi au vile, ukaumia sana, hata kabla ya muda wake, ikafika huo muda
kweli ikawa ndio upande wa kuumia, huoni kuwa utakuwa umejiumiza mara
mbili....ni bora usibiri, kama nikuumia, utaumia huo muda ukifika, na kama ni
kupata hutakuwa na hasara,...unapata kwa faida tu....unaona hapo, sijui kama
unanielewa....’akasema akiniangalia. Na aliponiona nipo kimiya akasema;
‘Kila kila kwa wakati wake, ..unaonaeeh, wenzako
walijipanga kulifanya hilo, sio kwamba wamekurupuka tu, kwahiyo, hapo unatakiwa
utumie akili, lakini usiumize akili kihivyo, waachie wanastahiki kuumiza
kichwa, wafanay hivyo, sisi tunakuwa kama huyo ndege mla mizigo, ....unaona hapo...hicho
kwa ujuma ni kitendawili...’akasema
‘Lakini vyovyote iwavyo ni lazima haki itendeke, muuaji
apatikane afikishwe kwenye vyombo vya haki..’nikasema
‘Na hiyo sio kazi yako,...nisikie sana hapo, na hiyo sio kazi yangu, mimi kazi yangu ni kukutetea
wewe, nihakikisha wewe,...hushitakiwi, na ukishitakiwa, unashinda kesi,...hakuna
swala la kushindwa kesi hapa...., ‘akatulia akawa kama anawaza.
‘Sizani kama unanielewa, nikuambie ukweli, hawa watu hawana
kesi dhidi yako, wamekushikilia tu, ili waonekana wanafanya kazi,...wanachofanya
kwa sasa ni kuvuta muda, .....kwa hali hiyo mnyonge atakayeingia kwenye anga
zao, ndio huyo anakuwa chambo...wewe wakakuona ni chambo hawakujua kuwa nyuma
yako yupo mdada.....’akatulia kidogo.
‘Sasa kwa vile taratibu zao za kufanya kazi mimi nazifahamu,
...huhitajiki tena hapo kusubiri taratibu ...hapo hakuna cha kufuata utaratibu,
kama alivyotaka kufanya wakili wenu wa kampuni,..nikuambie ukweli, huyo wakili
wenu angekuchukua muda sana kulifuatilia hili, kwani ndio hao watu wa kufuata taratibu, na bongo kwa hilo, ooh, `ngoja,
subiri, silioni zitakuwa nyingi, usipojulia utasaga makalio, uskisubiri,
utamaliza soili za kiatu ukifuatilia, wewe huku unasota jela ...’akagonga gonga
kiatu chini.
‘Mhh, unaonekana wewe unaufahamu sana na mambo haya, hujali
kuvunja sheria?’ nikamuuliza
‘Nani kavunja sheria, ....mimi hata siku moja sivunji
sheria, nafuta muelekeo wa sheria, sheria inaweza ikapindishwa, ....kwa
makusidi maalumu, mimi ninachofanya nikufuatilia jinsi inavyokwenda,..kwa mfano
leo hii walishapanga kukupeleka huko
gerezani, ...sasa ahpa ungefanya nini,..mtu usie na hatia ungelienda kusota
jela, utaumia, na huenda wakakumaliza huko huko....utakaa kimiya, utasubiri,
utaratibu, ...hapo ni akili kichwani mwako...’akasema akiniangalia kwa makini.
‘Kwahiyo una maana....’nikataka kusema na yeye akanikatisha
na kusema;
‘Nikuambie ukweli kama isingelikuwa juhudi zangu na uzoefu wa
mambo haya, usingelipewa hii dhamana, ...ndio maana mdada aliliona hili mapema,
huyu dada ni kichwa, anajua kuyasoma mambo, sio kwamba hakutaka huyo wakili
wenu aifanye hii kazi, ....angaliacha afanye kwa vile na yeye alikuwa na kesi
yake,lakini akaona umuhimu wako, wewe ni mfanyakazi mwenzake, na hayo
yaliyotokea yalitokea wakati nyie mnamjali ....’akasema.
‘Mhhh, ...ni kweli, nisingelienda hap ohayo yote
yasingelitokea, na .....’nikatulia kidogo na baadaye nikasema
‘Haya mimi nawasikiliza nyie maana mambo yamekuwa ni kama
mgeni kwenye nchi ngeni hata hujui uende wapi....’nikasema
Baadaye aliitwa na akawa anaongea na muhusika wa maswala ya
dhamana, na kupewa amsharti, na mimi nikawa nasikia anachoambiwa, na baadaye
akasaini, kitabu cha humo, na wakakabidhiana nyaraka, na walipomaliza hilo
zoezi, yule wakili akanijia na kuniambie tuondoke...
‘Ulisema wewe unakuwa kama mgeni kwenye nchi ngeni au sio?’
akaniuliza
‘Ndio kwa hali ilivyo....’nikasema huku tukitembea kuelekea
nje.
‘Ndio hivyo, sisi tutakuwa wenyeji wako...usijali, cha
muhimu ni kusikiliza na kufuata yale unayoelekezwa hadi hili tatizo liishe,
maana hapo ni mwanzo tu....bado kesi haijafika mahakamani, bado...sijui
yatakayofuata baadaye, maana mwenye kovu usizani kapoa....’akasema na kuanza
kutembea na mimi nikawa namfuatilia nyuma, kwa mwendo wa hatua za kuhesabu.
‘Hata hivyo
muheshimiwa, dhamana ni kitu kingine,...haitanisaidia
sana, ukilinganisha na kesi yenyewe, nikuulize ,.... vipi kuhusu kesi yenyewe, umejipanga
vipi, .....maana ninaweza kutoka kwa dhamana, kesi ikaja nikaonekana nina hatia,
wakati mimi sijafanya hilo kosa...’nikasema
‘Hilo limeshafanyiwa kazi, usijali...ni kazi ndogo tu, kama
nilivyokuambia, polisi wenyewe wamechanganyikiwa, ....ni kitendawili, ...maana
jinsi ilivyotokea na vielelezo walivyo navyo, wanajikuta hawapati muafaka wa
pamoja, wao wenyewe wamajikuta wakigawanyika makundi mawili kila mmoja akiwa na
dhana yake....hapo ndipo wanapokosea....’akasema
‘Sasa itakuwaje...?’ nikauliza
‘Cha muhimu ilikuwa wewe utoke kwenye anga zao, ili tuweze
kuliangalia hili swala kwa pembeni, kwani mambo mengine yanakuwa magumu wewe
mlengwa unapokuwa haupo nasi,... huwezi kujua huko wanakuuliza kitu gani,...polisi
wana mbinu,...na huwezi kusema hili limewashinda inawezekana ni moja ya mbinu
zao, mhalfu wameshampata....lakini wanasubiri wakati muafaka, ndio maana nasema
sisi tusimuize kichwa, ilimradi tunafahamu hatuna kosa....
‘Ndio maana tunataka uwe karibu nasi, ili tujue utaongea
nini, ...wakati ukifika,...mimi nawafahamu sana hawa watu wanaweza hata kutumia nguvu kukulazimisha kuongea..ukiwa
kwenye mikono yao, au kusaini nyaraka wanavyotaka wao,hilo pia linawezekana...kwahiyo
ni muhimu uwe nje, ili tuwe na uwezo wa kukudhibiti,....’akasema
‘Una maana gani kusema hivyo...mnataka kunidhibiti mimi kwa
vipi?’ nikauliza
‘Hapa ndipo mdada alipocheza, kunitafuta mtu kama mimi,
kichwa cha vipengele vya sheria, ...’akasema huku akitembea kwa madaha.
‘Sikiliza ndugu,usiumize kichwa chako kabisa, wewe mwenyewe
utakuja kugundua hilo baadaye, ....kwa hivi sasa ni wewe uwe kwenye anga zetu,
na mambo ya usalama nini na nini..inabidi kuyaangalia..anyway, usijali sana, maana kiukweli, kama ilivyosikika kutoka kwao
wenyewe ni kweli, kuna watu wanaweza kukumaliza kama wakiona unafahamu jambo
litakalowaingiza matatani...hilo linawezekana...’akasema na kusimama na mimi
nikasimama karibu yake.
‘Hivyo basi tunahitajika uwe sehemu ambayo tutahakikisha,
haitokei hivyo, wanadai kuwa, upo kwenye hatari, kuna watu wanataka
kukunyamazisha kwa hali yoyote ile...anyway,
mimi sina uhakika sana na hilo, cha muhimu ufike nyumbani,kwangu kwa hapo
nimeshamaliza kazi yangu...’akasema
‘Mhh, hapo sasa mnanitisha ina maana hakuna utaratibu wowote
mliopanga wa kuhakikisha usalama wangu kama kweli hicho kitisho kipo,.....?’nikauliza
‘Tumalipanga hilo, .... tumeona kwa vile kuna hii kesi na
sisi ndio tumekudhamini, inabidi ukae karibu na sisi, yaani karibu na eneo
ambalo nitaweza, au watu wangu wataweza kukuona na kuhakiki nyendo zako,
unafahamu hii kesi ina ugumu wake, hasa inapifikia kwenye sehemu hii ya
kudhamini mtu,..’akageuka kuniangalia.
‘Kwanza wewe mwenyewe unaweza ukaingiwa na wazo la kijinga,
ukaamua kutoroka,au watu wakaja kukufanyia lolote, huwezi jua,..na mimi ndiye
mdhamini wako, na lolote likitokea mimi nitakuwa matatani, kwahiyo mimi
nikaonelea ukae sehemu maalumu, ambayo
mimi na watu wangu tutaweza kukuona na kuhakiki usalama wako....’’akasema
‘Sehemu gani hiyo maalumu, kwasababu mimi siwezi kuishi
mbali na nyumbani kwangu, kwanza kwa hivi sasa nataka twende nyumbani kwangu...’nikasema
‘Nyumbani kwako??..., wewe una nyumba hapa mjini?’
akaniuliza kama ananishangaa, na mimi nikasema;
‘Sehemu nilipopanga...ni kweli, sina nyumba hapa mjini’nikasema
na yeye akatikisa kichwa na kusema;
‘Ndio kama ni muhimu kufika huko ulipopanga hakuna shida, nitakupeleka
huko uchukue unachokichukua, ...halafu tunakwenda kukuonyesha wapi,
unapostahiki kukaa, hadi hapo mambo yatakapokuwa sawa, ili na mimi nijirizishe...’akasema
‘Kwanini muwe na wasiwasi na mimi, nawahakikishia kuwa mimi
siwezi kutoroka, na sina mtu wa kunihatarishia maisha yangu, ,msiwe na wasiwasi
na mimi...pia mimi ni mfanyakazi, nina kazi yangu,..’nikasema
‘Ni muhimu niwe na uhakika, ...hata hivyo, mengi mtaongea na
mdada, tuone jinsi gani ya kufanya, ila ningekushauri ufanye kama
nilivyokuagiza, sitaweza kuhakiki usalama wako ukiwa mbali na mimi,niamini
ninayokuambia, nina uzoefu na mambo haya...usalama wako kwa sasa, nahisi pia
upo matatani, japokuwa sitilii maanani sana, lakini lisemwalo lipo, ..kama
halipo, hutapungukiwa kitu ukiwa umejihami...’akasema
‘Una maana kusema hivyo...?’nikauliza
‘Mimi kazi yangu ilikuwa ni kuhakikisha nafanikisha
unatolewa kwa hao watu, na hilo nimelifanya, hata hivyo, sheria inahitajia
nihakikishe upo salama, na uwepo kesi ikianza...unaona hapo, ndio maana sitaki
lije litokee jambo, niharibu sivii yangu...na nahisi kuna watu wapo nyuma yako,
kuna watu wanaoenkana kukufuatilia, sina uhakika kuwa ni watu wenye mlengo
mwema, .....’akasema
‘Watu gani hao...?’ nikauliza
‘Utaongea zaidi na mdada, ila ninaloweza kukuambia ni kuwa
uwe makini, na kama ingelikuwa ombi langu...’akasema
‘Ombi gani?’ nikamuuliza
‘Ukakae sehemu niliyokuchagulia mimi, ili niweze kuhakiki
usalama wako....’akasema
‘Mimi hata sijui nifanya nini kwa maelezo yako tu, nahisi
kuna jambo lipo, na huenda hata wewe unalifahamu, na inanifanya nisiwaamini, wewe
na watu wako, nona kama mna ajenda ya siri dhidi yangu...’nikamwambia
‘Anyway, hayo mtaongea na mdada, mtakavyokubaliana mimi sina
shaka...nimekuelezea hilo ili uone hali halisi, hapo ni wewe kutumia akili
yako, kulitafakari hili nililokuambia..., unafahamu dunia hii ione ilivyo, sio
kila king’aacho ni dhahabu, sio kila anayekuchekea ni mtu mwema
kwako....wenzako tunajua ni nini cha kufanya kwa muda wake, wakati mwingine
inabidi, utumie mbinu ya kuuma na kupiliza ilimradi mambo yaende sawa, siku
zinakwenda...’akasema
‘Mimi sikuelewi una maana gani hapo....., ujue wewe ndiye
wakili wangu, na usalama wangu upo kwenye mikono yako, unakumbuka ulivyoambiwa
na huyu mtu aliyekukabidhi kuwa mimi ni mtu wao na usalama wangu kwa sasa upo
mikononi mwako, na ulikubali kuwa utahakikisha nipo salama kwa ajili ya hiyo
kesi, leo unaniambia mambo kama hayo....’nikasema
‘Kwani nimekuambia nini kibaya...nimekutonya tu, ili na wewe
utumie akili yako, kama upo tayari ukakae sehemu niliyokuchagulia mimi, lakini
kama bado unahisi ni bora ukakae kwako haya....ila ninalokuambia ni kuwa uwe
makini....’akasema
‘Kuwa makini kwa vipi,?’ nikauliza
‘Mimi nitajitahidi kadri ya uwezo wangu, nitafanya kila kitu
ambacho kinaweza kutambulikana kuwa niliwajibika juu yako, lakini kuna mengine ni
juu ya uwezo wangu, sheria unalifahamu hilo, sitaweza kuhukumiwa kwa hayo, yanayofahamika....kwahiyo
ikitokea hayo, ambayo ni juu ya uwezo wangu sitaweza kualaumiwa...’akasema
‘Kama yapi?’ nikauliza
‘Nimekushauri ukakae sehemu ninayotaka mimi, ili niweze
kuhakikisha usalama wako, umepinga, na ukiwa kwako, unaweza ukafanya mambo
ambayo, sitaweza kuhakiki, chakula chako, maji yako...na mengineyo, mimi siwezi
kujua unakula nini, unakunywa nini, utakwenda wapi, na linguine muhimu sana,
nakuonya.....usipende kwenda kwenye majumba ya starehe kwa sasa, au kutoka
sehemu zisizojulikana....’akasema
‘Mimi siwezi kufanya hivyo....najua nina kesi kubwa mbele
yangu, mimi sana sana nitakwenda kazini tu...’nikasema
‘Safi kabisa, na mimi nitajitahidi kuhakikisha usalama wako
upo, kuna walinzi watakuwa karibu yako, sio lazima uwajue...’akasema.
Tukawa sasa tumefika kwenye gari lake, na mara nikasikia
honi ya gari, ..tukageuka kuangalia , mdada alikuwa kwenye gari lake,
akaonyeshea ishara ya kutuita, na kwa haraka wakili huyo akaanza kutembea kule
kulipokuwa na gari la mdada, mimi nikabakia nimeduwaa, nikaona mdada
anaonyeshea ishara kuwa na mimi niende.
Tulifika pale lilipokuwa gari la mdada, akasema
‘Muheshimiwa huyu mtu naondoka naye mimi, ...’akasema
‘Mhh, lakini sijamalizana naye...na..ali...’akasema
‘Usijali, ...’akasema mdada huku akiniashiria mimi niingie kwenye gari
lake....na yule wakili akabakia ameduwaa , na mimi sikuwa na la zaidi.....nikamwangalia wakili, na yeye akageuka pembeni...
NB: Kwa leo inatosha eti?..ila mtandao ni ishu!
WAZO LA LEO:
Kusoma kunatusaidia kujua jambo kwa usahihi wake, au kwa uhakika, unaposomea
nyanja fulani, unakuwa na upeo mpana zaidi wa hiyo nyanja, au taaluma
uliyoisomea, lakini sio kwamba utafahamu kila kitu kinachohusiana na hilo
jambo,kama binadamu tunaweza kuwa na walakini,na mwingine akawa anafahamu
zaidi, au kwa njia tofauti, lakini kwa mantiki hiyo hiyo ...kwahiyo basi
tukubali kukosolewa, kuelekezwa, au hata tukiambiwa kuwa hapo tumeteleza tuwe
ni wepesi, kusikiliza kwa masilahi mema
ya lile jambo.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment