‘Kwahiyo
tunakwenda wapi?’ nikamuuliza mdada akiwa anaendesha gari kwa mwendo wa kasi,
akageuza uso wake na kuniangalia halafu akaangalia mbele, na kusema;
‘Kwanza ni
kwenda kujipongeza mengine baadaye..’akasema huku akitabasamu, na alivyokuwa
akiendesha, utafikiri yupo kwenye mashindani.
‘Huu mwendo wa
nini, huoni ni hatari....?’ nikamuuliza na yeye akatabsamu, na kusema
‘Unaijua
hatari wewe...tulia mwanaume wee, ajabu kabisa mwanaume kuwa muoga hivyo, huu
sio mwendo mbaya...lazima tuwahi mapema, kuna mapangilio maalumu huko, na huenda
tunasubiriwa...’akasema
‘Na akina
nani tena?’ nikauliza
‘Surprise...’akasema huku akitabasamu
‘Mimi leo
nisingelipenda kukutana na watu, akili yangu haijatulia,...’nikasema
‘Basi kwa
hali kama hiyo, ...unahitajia kitu kama hicho ...cha starehe, ukitoka hapo
unaanza upya, cha muhimu, akili yako iachane na hayo, ...sahau kabisa...’akasema
‘Lakini
....’nikaanza kulalamika, na yeye akageuka mara moja kuniangalia akasema;
‘Usitake
kuniuzi, sikiliza ninachokuambia kwa masilahi yako mwenyewe, unasikia ‘akasema
‘Sijisikii
kabisa kukutana na watu, hapa nilipo nahisi kama nipo uchi...’nikasema
‘Nakushauri
kitu, kama huna la maana la kuongea kwasasa ni bora unyamaze, hadi tufike huko
ndani, mimi nina imani utafurahi tu, utayaondoa hayo yote yaliyopo kichwani
mwakoi...’akasema huku akizidi kukanyaga mafuta, ulikuwa mwendo mkali sana.
Nilikaa
kimiya, sikutaka kuongea tena, nikatuliza kichwa changu na mara akili yangu
ikajikuta inakumbuka mazungumzo haya;
‘Mimi naondoka, nimefikia kwa
shangazi ,nilikuja jana,nikaambiwa upo na mazungumzo na wakili wako,
nikaulizia, kuhusu kesi yako...wakawa hawaniambii cha maana..hata hivyo,nimeshaambiwa
kuwa unashughulikuwa kuhusu dhamana yako,...
‘Sasa, siwezi kwenda kwako,
unapoishi, unafahamu taratiu na mile zetu, kwa vile hatujafunga ndoa ,siwezi
kwenda huko kwako unapoishi, nimefikia huko kwa shangazi yangu,....’
‘Shangazi yako yupi huyo, anaishi
wapi hapa mjini...?’
‘Karibu na hiyo hoteli kubwa ya inayoitwa,...aa,
Kajificheni...’
‘Oh,kumbe mna ndugu yenu hapa mjini,
na anaishi karibu na hiyo hoteli mbona simfahamu, yupoje, mbona hatujawahi
kukutana naye, huyo ndugu yako ananifahamu mimi..?’
‘Anakufahamu sana...’;
Mhh,kumbe ni
shangazi yake , ndiye anayempelekea umbea huko kijijini, na inaonekana ana
nifahamu sana, na huenda ameshaniona mara nyingi nikiwa na mdada, na......oh,
sasa natakiwa kuwa makini,...sasa nitafanyaje na huyu mdada ndio kaniganda,
nikisema niachane naye, anaweza kupandisha na hata kuyatuma hayo mapicha yake
mabaya..sasa...
‘Hili sasa ni
janga, kweli nimumbuka....’nikajikuta nikisema kwa sauti na mdada akaniangalia
kwa makini na kusema
‘Unaongea
peke yako au unaongea na mimi....?’ akaniuliza
‘Naongea
peke yangu....’nikasema
‘Utachanganyikiwa,
wanasema mimi nina matatizo ya kiakili,....kumbe tupo wengi, hahaha, inabidi na
wewe uende ukamuone mtaalamu wa magonjwa ya akili....’akasema
‘Mimi
matatizo yangu, sio kihivyo....’nikasema
‘Huenda pia
ikasaidia kwenye hii kesi....’akasema
‘Kwa
vipi...?’nikauliza nikimwangalia kwa kauli hiyo.
‘Kama kweli
una matatizo hayo ya ya akili, itakuwa kama mimi, walipothibitisha kuwa kweli
mimi nina matatizo hayo, unaona ilivyokuwa, waliogopa hata kunishika,
wakaogopa, ...kuwa nikipandisha huko mahabusu hakutakalika......hahaha, ...watu
waoga jamani, ...mmh japokuwa ni tatizo, lakini namshukuru mungu, kumbe kila
kitu kina umuhimu wake....’akasema .
‘Lakini hilo
ulilo nalo sioni kwanini waliite ni tatizo ...kwani huo ni ugonjwa wa akili,
..’nikasema kama nauliza
‘Wewe una
utaalamu gani wa kulisemea hilo, hayo ni maswala ya wataalamu wa mambo hayo,
madocta bingwa wamelithibitisha hilo,...sio kwamba napendelea hivyo, kwani
kiujumla hiyo hali inanotesa sana ikianianza, na ikiisha ninakuwa mwili wote
unauma.... sipendi kabisa hiyo hali,...lakini sasa utafanyaje, na...inafikia
muda, natamani kumpata wa kumlaumu, ..hata hivyo sitamlaumu nani..’akasema
‘Wanaume...’nikasema
kwa utani
‘Haswa, ni
kweli, ....hata hivyo, ...hata sijui nifanye nini hii hali ipoteee, ndio
nimeshauriwa niolewe, nikishaolewa, hii hali itakwisha kabisa....’akasema
‘Oh,
...kumbe...’nikasema
‘Ndio hivyo,
na natakiwa niolewe na mtu ninayempenda,...na hisia zangu zimeshanionyesha huyo
mtu ni nani, ndio maana hata kutokee nini, siwezi kukuumiza wewe...’akasema
‘Ina maana
....’nikasema na kukatisha
‘Yah, ndio
hivyo, ...lakini hayo tutakuja kuyaongea baadaye, tumalizane na hili lililopo
mbele yetu, hata hivyo, kwasasa , hatutakiwi kuwaza mambo mengine,
nimekuambiaje...?’ akawa kama ananiuliza
‘Ni muda wa
kustarehe...’nikasema
‘Ndio
hivyo....kwa ajili yako,...nimeambiwa nisinywe pombe, lakini nashindwa kujizuia, nikinywa pombe mara
nyingi naishia kwenye matatizo,..na nashukuru siku nilizowahi kwenda na wewe
umegeuka kuwa msaidizi na mlinzi wangu muhimu.....’akatulia na kuniangalia
‘Kwahiyo
leo, leo ni lazima tunywe unaonaje dear...?’ akauliza
‘Hapana,
mimi siwezi kunywa, na nilikuwa nakushauri kitu..., kwanza mimi sijaoga,
sijajiweka sawa, nimetoka jela, na ujuavyo kule, usafi ni wa shida, nahitajia
muda wa kuoga, na kujiweka sawa,...najisikia vibaya sana kwenda sehemu kama hizo
nikiwa hivi...itanipa wakati
mgumu...’nikasema
‘Ile ni
hoteli, ina kila kitu, hebu angalia hapo nyuma ya gar kuna nini?’ akaniuliza na
mimi nikageuka nyuma ya gari kuangalia, niliona mfuko,...
‘Kuna nini?’
nikauliza huku nikiuangalia ule mfuko kwa makini.
‘Surprise....lakini usijali, kila kitu
kipo sawasawa, ukifika hapo hotelini, utapata huduma zote, ni siku ya furaha
leo, maana tumeweza kufanikisha jambo muhimu sana, sio rahisi kama
unavyofikiria wewe,..’akasema
‘Ni
kweli....’nikasema
‘Wewe huwezi
kujua kwa jinsi gani jambo hilo lilivyokuwa gumu,....nimehangaika sana na huyo
wakili, yote hayo ni kwa ajili yako, uone jinsi gani ninavyokupenda, je
nikuulize, tangu upate haya matatizo huyo anayeitwa mchumba wako aliwahi kuja,
au hata kukupigia simu? ‘akaniuliza.
‘Alishawahi....’nikasema
baada ya kusita kidogo
‘Kufanya
nini?’ akauliza na mimi nikatabasamu na kusema;
‘Kufanya
yote,...kupiga simu, kuja kuniona...na kuangalia kama anaweza kusaidia
lolote...’nikasema na akawa kama kashituka na kusema
‘Mhh, kumbe
ni kweli.....’akasema na kutulia kama anawaza jambo fulani, na mimi nikamuuliza
‘Kweli
kuhusu nin?’ nikamuuliza
‘Kuwa huyo
mtu, alionekana hapa mjini....’akasema
‘Oh,
umejuaje, ni nani alikuambia, kwani unamfahamu?’ nikamuuliza
‘Tatizo lako
bado upo dunia nyingine, ..sasa hivi dunia ni kijiji, nilishapata taarifa hiyo,
lakini sikuitilia maanani, kwa vile aliyeniletea taarifa hiyo, alikuwa na mambo
mengi ya kuniwakilishia, ...mmh, inanipa muwasha washa, ....ok, hebu
niembie, huyo mtu bado yupo hapa mjini?’
akaniuliza
‘Sina
uhakika....’nikasema
‘Huna
uhakika, mbona unaongea kama huna raha, ...hukupendezewa na ujio wake?’
akaniuliza
‘Sikutarajia
na sikupenda afahamu hili tukio...’nikasema
‘Ndio maana
nakuona upo dunia nyingine, tukio kama hili linajulikana na watu wengi, iweje
mtu wako wa karibu kama huyo ashindwe kufahamu, ningeliona ajabu kama angekuwa kimya, hata
asije kukuona,.... ikizingatiwa kuwa
huyo ni mtarajiwa wako....’akasema kwa sauti isiyo na furaha.
‘Wasiwasi
wangu ni kuwa kama bado yupo hapa mjini, anaweza kunifuatilia, na hii inaweza
kuleta mchafuko nisioutaka...’nikasema
‘Hilo
unalo...’akasema na kutulia kimiya.
‘Mhh, haya
bhana,...’nikasema
‘Kumbe ndio
maana upo hivyo,..nimekupata,....’akasema na akawa kama hana raha, na mimi
nikawa kimiya, ...akasema;
‘Hata hivyo,
kwani wasiwasi wako ni nini..kuwa huyo mchumba wako atatuona tukiwa wawili?’
akaniuliza
‘Mhh...wewe
huni kuwa hilo ni tatizo?’ nikamuuliza
‘Unaona, hilo ndio tatizo
la kuchukua visicha vya kijijini, mnawaharibu mabinti wa watu, na kuwahadaa, kiakili wanakuwa hawajui hata maisha yanavyokwenda, ...'akasema
'Hayo ni mawazo yako...'nikasema
'Ok, sawa ni mawazo yangu, ....hata hivyo
yeye bado mdogo, atakuwa anaelewa, kuwa mimi ni mfanyakazi mwenzako, na
isitoshe, mimi ndiye msaidizi wako wa hii kesi,kwahiyo kuwa pamoja na mimi sio
tatizo, labda awe na lake jambo, na kama lipo lake jambo, ni bora afahamu
mapema, kuwa yeye na wewe basi....’akasema
‘Eti
nini,....?’ nikauliza nikionyesha mshangao, na yeye akaniangalia akiwa katoa
macho, na kusema;
‘Ina maana
hukunielewa nilivyokuambia mwanzoni , kuwa sitaki kusikia maswala ya ndoa
yako....usitake kunichanganya, umesikia, kama unataka mengine nisikie tena hiyo
kauli,...’akasema na kuwa kimiya, niliogopa kuongea naye, asije akabadilika,...
Tulifika
kwenye hiyo hoteli, na moja kwa kwa moja akalipeleka gari ndani kabisa, kuna
sehemu maalumu ya kuweka magari kwa wanachama, na yeye ni mwanachama, na
alipolisimamisha akatoka na kunifungulia, akasema
‘Here we are...’ akasema akishika mkoba
wake kwa mkono mmoja, na mkono mwingine kashikilia mlango wa gari
lake...akanitupia jicho la haraka na kusema;
‘Leo hii
wewe ni mtu muhimu sana, ni lazima nifanye hivi, usione ajabu,...’akasema
‘Nashukuru
sana....’nikasema
‘Usijali,
ujue kuwa leo ni kufurahi kwa kwenda mbele, sitaki kusikia kingine zaidi ya
furaha,....’akasema na mimi nikawa kimiya tu.
‘Unasikia
nilichokuambia, tafadhali sana, usije ukafanya lolote la kuiharibu hii
siku...nakuaptia ukifanya hivyo, utanibeba, ...’akasema akinyosha nyosha nguo
yake na kujiangalia kwenye kiyoo kilichokuwepo, kwenye mkoba wake.
‘Nitajitahidi
kufanya hivyo....’nikasema
‘Haya, ...natumai
umenielewa mpenzi...’akasema na kunisogelea, tukawa tumesimama sambamba, yeye
akiwa mkono wangu wa kushoto, tulitulia kidogo, mara akapitisha mkono wake
kunishika kiunoni,..nilishituka kwani sikutarajia hich kitendo, akanishikilia
na kuegemeza kichwa chake begani kwangu, halafu akasema;
‘Sikiliza
nikuambie kitu, sasa hivi sahau yote, akili yako iweke kwenye furaha, ...’akasema
na mimi nikajitahidi kutabasamu, na hapo nikawa najitahidi kuuondoa mkono wake,
kwani kwa mahali kama pale sikutaka afanye hivyo, niliangalia huku na kule
nikiwa na wasiwasi, na yeye akawa anajaribu kunishika zaidi, na aliponiona
nahangaika kuuondoa mkono wake, akachekea
na kusema;
‘Hahaha
masikini mhasibu, napenda hiyo eeh, ....kumbe na wanaume nao wapo hivyo,...acha
hiyo mhasibu, usiniaibishe bwana...,’akaniangalia moja kwa moja usoni, halafu
akasema;
‘Nikuambie
kitu, wewe ukiwa na wasiwasi hivyo, na huo uwoga wa kinafiki, unapendeza sana,
nataka uwe hivyo hivyo, hadi hapo utakapoweka pete kwenye kidole
hiki.....’akasema akinionyeshea kidole chake, na muda huo alikuwa ameniachilia,
na mimi nikaweza kupumua kidogo, tukaanza kutembea kuelekea mlango wa ile
hoteli.
NB: Mtihani, mtihani, mitihani, baba yangu anaumwa, ....naomba dua na maombi yenu kwa
wingi, mwenyezimungu amsaidia apone, kwa uwezo wake yeye muumba wa kila kitu.
WAZO LA LEO: Hisia za wanadamu hutofautiana,
hasa katika kupokea taarifa nzito, kuna wengine nafsi zao zinaweza kujenga
ujasiri, wa kuweza kupokea lolote na wana uwezo wa kuhimili hali yoyote ile, wao
wamejaliwa kuwa na mioyo migumu, lakini wapo wengine wenye mioyo
dhaifu,...huenda ni kutokana na nakama za kimaisha, au madhila mbalimbali ya
maisha yao, kwao wao, jambo dogo huwa ni kubwa,..hawana uwezo wa
kuvumilia..hayo ni maumbile...Cha muhimu hapa ni kuwa na hekima ya jinsi gani
ya kutoa taarifa nzito kwa wengine, kwani jambo dogo tu linaweza kuathiri afya
ya mtu.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Fantastic goods from you, man. I've consider your stuff prior
to and you're just too fantastic. I really like what you have acquired right here, really like what you are saying and the way during which
you are saying it. You're making it enjoyable and you still take care of to keep it
sensible. I can't wait to read much more from you. That is really a terrific
site.
Also visit my site: best diet plans sacramento
Post a Comment