Nilipogeuka tu nilikutana na mdomo wa bastola ukinitizama, ...bastola ni
ndogo na mdomo wake ni mdogo tu, lakini kwa muda huo niliona kama natizama
bomba..au mtutu wa bunduki,
Macho yakanitoka pima kwa woga, na nilitaka kupanua mdomo nipige
ukelele, lakini sura ya yule jamaa ambaye kwa muda huo alikuwa akinitizama kwa
uso uliojaa makunyazi, ya hasira chuki, macho yakiwa yamemuiva alipanua mdomo
wake na kusema;
‘Nataka twende nikaonane na huyo malaya wako,,....’akasema
‘Ma-la-ya, wa-wa-ngu ni nani?’ nikauliza na mara yule jamaa akainua ila
bastola kama anataka kunilenga akasema;
‘Tusitaniane....uninielewa namtaja nani, kwanza mbona wewe mtu mwenyewe
ni kiozo, unaogopa kama vile hukuzoea hii kazi, wakati wewe ni jambazi,
tapeli...mablackmailer..?’ akaniuliza.
‘Mi...mi nakuapia, sijawahi mimi io jambazi,.....na tafadhali ondoa hiyo
batola mbele yangu, inaweza kunifyatukia....’nikasema huku nikiwa nimeshapiga
magoti.
‘Inuka haraka twende huko ndani nimekuambia nakataka kuonana na huyo
malaya wako, ...siamini kuwa huu mzigo alionipa umekamilika namfahamu sana huyo
mwanamke, na kama asiponipa kila kitu, kinachonihusu mimi , naona ni bora
nikafungwe kwa maujaji,...’akawa anaichezesha ile bastola nikamuona anatupia
jicho kule getini, nahisi alikuwa na wasiwasi na huyo mlinzi asije akamuona.
‘Tusipoteze muda hapa, unafahamu nimehachoka na nyie, nimepoteza pesa
nyingi kwa kuwapa nyie, kwa kazi gani mlionifanyia, ...sina raha na familia
yangu ...siamini haijawahi kutokea hivi kabla, yaani huyu mwanamke
ananizalilisha hivi, ...anataka nimpe shilingiu ngapi ndio anipe uhuru wangu
ungelijua ni kiasi gani alivyoniumiza usingelidirriki kuwa naye...’akasema
‘Hata mimi sitaki....sipendi, lakini ...’nikasita.
‘Hata wewe hutaki nini..., wewe hujawahi kutumia pesa yangu kutoka kwa
huyo mdada, anakulipa kwa kazi hii chafu, .....mimi sijui kama hupendi, hiyo lakini
yako itakutokea puani, njaa zako zitakutokea puani, inuka twende...’akasema
huku akiinua ile bastola kama anataka kuifyatua.
‘Sikiliza...tafadhali, mdada ni mgonjwa, ukiingia hivi ...utamtibua, ana
matatizo ya akili, utampandisha hasira zake na ...na...atakuua..’nikasema
nikijaribu karata nyingine, kwani nilijua kabisa kama ataingia hivi, mdada
atabadilika, na sijui kama kutakuwa na usalama hapo....
‘Hahaha..unasema ataniua, hahaha, unafahamu mimi sasa siogopi kufa, ni
heri kufa kuliko kuzalilika hivi, nimeshaamua kuwa leo iwe mwisho wa haya yote,
nipo tayari kwa lolote lile...’akasema na mara simu yake ikaingia ujumbe,
lakini hakutaka kuiangalai akasema;
‘Haya, inuka haraka twende ndani...’akanigonga kichwani na ule mtutu wa
bastola na akilini nilijua ndio risasi imeshafyatuka na kugonga kichwa kwangu
nikadondoka chini, jamaa akaniangalia huku katoa macho ya hasira, na mimi kwa
haraka nikawa nimepitisha mkono wangu na kushika simu yangu, nikabonyeza kwa
hisia, nikijua hapo nabonyeza namba mbili, namba mbili ni kwa bosi, ...ndivyo
nilivyoegesha nikajua sasa ipo hewani.
‘Unafanya nini, hebu ....’akanishika, na kutoa mkono wangu mfukoni,
akanikagua na kuiona ile simu, akaitoa na kubamiza chini..
‘Unataka kufanya nini.....’akanigonga na kitako cha ile bastola kichwani
hadi nikahisi kichwa kinataka kupasuka,...
‘Nitakuua,..sina utani leo...’akasema na kuangalia getini, mlinzi sijui
alikuwa wapi, maana kama angelikuwa makini angeliona hayo yanayotokea.
Jamaa akanishika shati kwa nyuma na kunisukuma nitembee mbele...
‘Haya twende huko ndani..’akasema.
Kwa haraka sasa nikiwa na wasiwasi kuwa jamaa anaweza kweli kuniua, nikasimama
nikishika kichwa, kama kuna damu zinatoka, nikaona hakuna kitu, huku
natetemeka, nikaanza kueleka ndani...
‘Usifikiri natania, ...leo ndio mwisho wa haya yote, kama huyo malaya anaumwa
wazimu mimi ni wazimu zaidi yake, haya twende,...haraka....’akasema na mimi
nikaanza kutembea kuelekea ndani huku bastola ikinigusa kichwani kwa nyuma.
******
Nyumbani kwa muheshimiwa, ikiwa ni asubuhi na mapema, mke wa mpokea
ushuru wa magari, alikuwa kasimama huku akawa anangalia dirishani, akiongea na
simu na ilionekana anaongelea jambo kubwa sana kwani alikuwa akiongea kwa
jaziba na hata kiti alikiona ni cha moto, mara ake mara asimame, akasema;
‘Mna uhakika na hilo kuwa mume wangu kaonekana asubuhi na mapema
akiingia kwenye nyumba , unasema anaishi mdada, msichana, mrembo,..mungu wangu,
mna uhakika ni mwanamke gani huyo?’ akauliza.
‘Ohooo, ni kile kisichana,nakifahamu, ...mmh, nimeshamuelewa, nitaonana
naye uso kwa uso, leo hii-hii, tena sasa hivi naeleekea huko...ataniambia
ukweli ulivyo, ana nini huyu mume, kakosa nini kwangu, hapana
haiwezekani,...sizani, nahisi kuna kitu,...’akawa anaongea huku kasimama
dirishani mkono mmoja umeshika kichwa.
‘Ninachotaka hakikisheni mnakuwa hapo kuhakikisha akitoka mnamuona, na
hakuna uwezekano wa mtu kuingia ndani,...vyovyote lakini hakikisheni hafahamu
mtu mwingine yoyote, maana sitaki kashifa nyingine’ akasema.
‘ Ni mara ngapi kafika hapo, .....unasema ni zaidi ya mara mbili, ana
kazi gani na huyo mwanamke...gari, ...kwanini mazungumzo hayo yafanyikie
kwake...kwanini isiwe ofisini, huyo mwanamke ana mume, hana...ana mchumba,
hawara....nataka kujua yote hayo..leo hii
ndio,..’akasema
‘Ok, nitakwenda huko huko, maana jinsi mume wangu alivyoondoka leo inaonekana
kuna jambo kubwa anafuatilia, na hizo pesa nyingi hivyo anazipeleka wapi,...alkuambia
ukamchukulie jana, na una uhakika anazo mkononi,....’akatulia kidogo.
‘Una uhakika gani, bahasha,..anyway,yeye
ana pesa zake nyingi za kuchezea, hilo sina uhakika nalo, ila cha kujua kafuata
nini kwa huyo mwanamke, kaondoka asubuhi sana, hata kabla
sijaamuka....alipotoka hapa kwangu hakupitia sehemu nyingine, mna uhakika,
ok,...?’ akawa anauliza na kuandika jambo kwenye kumbukumbu zake.
‘ Nahisi kuna jambo, ok, waambieni hao vijana wahakikishe wanapata
ushahidi wa kutosha, sitaki uzushi, na kama hakuna kitu kama hicho, manafahamu
ni kitu nitakachokifanya, mimi namwamimi sana mume wangu....ok, naelekea huko
huko....’akasema na akatulia kusikiliza
‘Hapana hili swala haliwahusu polisi, kwanini polisi, ....kama tutawahusisha
polisi itakuwa ni kashifa, hatuna uhakika kafuata jambo gani,na ni kitu gani
kimefanyika...kutembea na bastola sio mara ya kwanza, hilo sio ajabu kwangu,
huwa anajihamu kutokana na kazi yake...’akasema
‘Polisi wa nini....achana na mawazo hayo,...’akasema kwa hasira.
‘Basi nitayafahamu huko huko nikifika,....mimi mwenyewe ni polisi ,
najiamini...’akasema na kuanza kujiandaa kuondoka kuelekea huko alipoambiwa
mume wake yupo
********
Wakati hayo yanaendelea nyumbani kwa muheshimiwa, baba mkwe, alikuwa
mjini, alifika kwa shughuli zake, na alipomaliza akawa na hamu ya kwenda kwa
mkwewe, lakini hakupata nafasi hiyo, hadi asubuhi ambapo alitakiwa kurudi
nyumbani kwake, akiwa usingizini
asubuhi, akapigiwa simu;
‘Mhh, ni kitu gani asubuhi hii, ...unasema, hajaonekana nyumbani kwake,
toka jana, yupo wapi, ...kwa mdada, oooh,...una maana yule msichana anayeitwa
mdada, ...kweli anaumwa...., kama anaumwa ndio yeye akalale huko,..haiwezekani,
...’ akawa anajindaa huku kashika simu.
‘Yawezekana kwa vile ni mfanyakazi mwenzao, sawa,...lakini...ok, leo
siwezi kuonana naye, maana naondoka asubuhi hii, ila.....nitapitia kwa huyo
mdada kama anaumwa, sitakaa sana....sasa hivi naondoka...’akasema
Akachukua viatu vyake na kuanza
kuvaa...na mara simu ikalia tena, alipoangalia akaona ni mke
wake...akasalimiana naye, halafu akasema;
‘Mimi ni mwanajeshi bwana, muda wote nimejiandaa, sasa hivi navaa viatu,
kuoga, usitie shaka,...chai nitakunywa huko mbele kwa mbele, muda hautoshi,
....natakiwa kufika huko kabla ya saa nne, kukutana na wale watu...’akasema
‘Kuonana na huyo mkwe wenu...sijapata muda, kabisa...na hata hivyo, mimi
kwa nafasi yangu sio mtu wa kuonana naye,....hajakuwa mkwe, japokuwa kafanya
hayo aliyoyafanya, kuna watu wanamfuatilia, hilo ondoa shaka, kama ni kweli
nitajua ...hawezi , akifanya hivyo nitahakikisha anaozea jela,..’akasema
‘Sawa baadaye...’akasema na kukata simu, na kabla hajachukua mkoba wake,
simu yake ikaita tena, akaipokea, ....
‘Nani , mtoza ushuru wa magari, na yeye kaingia hapo, asubuhi hii, kuna
nini, kazi za asubuhi hivi,...kuna jambo gani hapo, au huyo msichana kazidiwa,
au ni mpenzi wake wa siri, ....unasema ni kawaida yake,...mmmh
haiwezekani...’akatikisa kichwa kama kutokukubaliana.
‘Mke wake si yule muheshimiwa, ok, ok, ...sina haja na mambo yao,
..hayanihusu,...kwanini, ina maana kuna mgongano, una uhakika, ok, nimeanza
kukupata kuwa mtoza ushuru, anamtaka mdada, na mkwe wangu pia inawezekana na
yeye anamtaka au anatumiwa kwa jambo fulani,...’akatulia kusikiliza.
‘Hilo haliwezekani, tafuteni ushahidi sio majungu,..sitaki udaku, mimi
ni mtu wa heshima zangu,...haiwezekani, lakini mimi umuhimu wangu ni huyo mkwe
wangu anafanya nini hapo, kwanini alale usiku kucha hapo,...yah, ndio hivyo nataka
kujua hilo hayo mengine hayanihusu, sitaki kuingilia kazi za watu...’akasema.
‘Ok, nitapitia hapo nihakikishe mwenyewe...mdada nilimpa kazi hiyo, ya
kuangalia nyendo za huyo mkwe wangu, sizani kama anaweza kufanya hivyo, una
uhakika...mbona hamkuniambia kwenye taarifa zenu, ushahidi, sasa mnao...?’
akauliza
‘Unasema mara nyingi wapo naye, huyo mkwe wngu na mdada, labda mdada anafanya hivyo katika kumchunguza
huyo mkwe wangu, namuaminia sana huyo msichana, ...una uhakika, analewa
kupindukia, toka lini akawa mlevi..haiwezekani, ...kama ni hivyo..ooh, ni
lazima nionane naye. ....’akatulia akisikiliza
‘Akifanya hivyo,nitamfunga, hawezi kuniharibia binti yangu afanye uchafu
huo...unasema...ok, ok, naelekea huko huko....’akasema na kukata simu kwa
hasira
‘Haiwezekani...tutaona huko huko...’akasema akijiandaa kuondoka.....
*******
Katika kituo kidogo cha polisi, mpelelezi maarufu anayefuatilia maswala
ya biashara ya madawa ya kulevya na makosa ya jinai, alifika ofisini kwake
asubuhi sana, na alifika hapo baada ya kuwasiliana na vijana wake wanaofuatilia
kazi maalumu, akachukua faili la kesi hiyo, inayofanyiwa uchunguzi, na akawa
analipitia, mara simu ikaita;
‘Ndio niambie,....asubuhi hii?, ...yupo kwa mdada!, ok, vijana wapo hapo
tayari au sio?, ok, sitaki ajue.....je kijana wetu anaweza kuingia
ndani,...hapana asifanye hivyo..., vitu vingine ni kinyume na kazi yetu, ila
kama ni dharura, fanya uonavyo, ...ok, ok, kama mnahisi hivyo, kuwa inawezekana
kukawa na biashara hiyo,...ajanye iwezekanavyo, ila awe muangalifu....ok....’akatulia
akisikiliza
‘Unasema hii ni mara ya pili, ...ni pesa nyingi eeh,...kwani lile gari
lilitokaje...kwahiyo hakuna uhakika wa moja kwa moja, je kumbukumbu za kazini
zinonyesha vipi..kila kitu kipo sahihi, kwahiyo hizo ni dhana za kuzua, huenda
hata kama kuna ukweli, lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja, ndio hivyo?,...unasema
kuna mengine kama yapi, ...shinikizo!!?...ok, ?’ akauliza kwa mshangao
‘Nimekuelewa....hayo yanaanza kuja huku kwetu, na yanaweza kuleta athari
kubwa,..inabidi hilo tulifanyie kazi, nitalifikisha kwa wahusika...’akasema
‘Hilo ....linawezekana, kuwa analazimishwa kutoa hizo pesa, kuziba kashifa,
lakini kashifa kama ipi,..usaliti wa ndoa,...ok, ok,... unauhakika na hilo,
...udaku,...gazeti lipi hilo,achana nao hao, fanyeni yanayotuhusu,hayo mengine,
nitawaambia wahusika... basi,yah, kama kweli hilo lipo, tunahitajika kupata
ushahidi,...’akatulia halafu akasema
‘Hayo ya usaliti wa ndoa, kuwa yametumiwa kama chambo, mmmh, hayo ni
maswala binafsi , hayana kigezo, ninaweza kusema kwa sisi hayatuhusu,yatatumika
kama kweli yanaambatana na kesi yetu, unakwenda huko, ok, tutakutana, kwani
hata mimi mwenyewe naelekea huko nitaonana nao, ....ok, and over...’akakata simu.
NB: Kazi imeanza, fichua fichua,...kashfa, udaku na rushwa. Je hilo litawezekana, kuna nini kipo nyuma ya haya yote, tukutane
sehemu ijayo...
WAZO LA LEO: Mara nyingi aliyezoea
kudhulumu, kutenda ubaya kwa watu ni jambo la kawaida, anaona ni ujanja, ni
bahati yake...nk, ila yeye hapendi kufanyiwa hivyo,kudhulumiwa kwake inauma
sana, atalia sana, kuwa anaonewa, vyovyote iwavyo tukumbuke kuwa ubaya hauna
mwisho mwema, tenda utendavyo, lakini dhuluma itakurudia wewe mwenyewe, ipo
siku itafika na wewe utapata jaza yake.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment