Basi nikapata ajira kirahisi, na kila tukipata nafasi, bosi
wangu huyu akawa akinisimulia maisha yake, huko alipotokea na madhila aliykutana nayo, hadi kufikia hapo alipo, akiwa mumiliki wa kampuni yenye wafanyakazi wa kila idara.
Siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu nikawa sasa ni mwenyeji, na mtu niliyeanza
kuzoeana naye mapema alikuwa yule dada wa mapokezi, alianza kuniachangamkia sana,
kiasi kwamba wengi wakahisi tofauti, hata hivyo kwa yale niliywahi kuyaona siku
ile ya kwanza, sikutaka kuwa naye kwa urafiki wa ndani, kwanza alishaniambia
ana mchumba, na pili wanaume wanapigana kwa ajili yake.
‘Kaka leo nakuomba unitoe chakula cha mchana.....’nilishitushwa
na sauti hiyo, wakati nasubiria ofisi ifunguliwe, nilifahamu kuwa na yeeye
ameshafika, lakini sikutegemea yeye kuniomba hivyo.
‘Mhh!, leo?.... hapana, nina kikao na bosi.....’nikamwambia.
‘Lakini kaka kwanini unakuwa kama unanikwepa, kwani
unaninaje...?’ akaniuliza.
‘Hapana, unafahamu mimi bado mgeni kwenye kampuni hii,
isitoshe mimi sina kawaida ya kuwa karibu sana, na wachumba wa watu....’nikasema
na yeye akacheka, sana, na kunisogelea akawa kama ananinong’oneza.
‘Mimi nataka niwe rafiki wako wa karibu, maana unafaa
sana...usijali ile kauli yangu kuwa nina mchumba, huyo ni geresha, ....’akasema
na mimi nikamwangalia kwa macho yakutahayari. Kwakweli msichana huyu ni mrembo,
nahisi ndio maana wanaume wengi walikuwa wakijigonga kwake, lakini mimi sio mtu
wa kugombea mapenzi, sikutaka kabisa kuwa na urafiki naye, na nilishakanywa na
bosi, kuwa hataki urafiki wowote wa kimapenzi kwenye kampuni yake.
Wafanyakazi wakaanza kuja mmoja mmoja, na mazungumzo yetu
yakakatishwa, lakini kabla hatujaachana naye, akanisogelea na kusema;
‘Kumbuka nataka unitoe chakula cha mchana, tafuta njia za
kumkwepa bosi wako, bosi, bosi...sio bosi wa kila kitu, ..sisi tunamjulia yule,
ana wivu sana...kuna kitu muhimu nataka kukuambia, ...muhimu sana...’akasema na
kuondoka.
*********
Siku hiyo kweli nilikuwa na miadi na bosi wa hiyo kampuni,
na ya baada ya kazi za ofisini za asubuhi, bosi akaniita ofisini kwake, tulikaa
huku tunapata maji, na hapo akaanza kuongea na mimi, ili kuniweka sawa.
Kwakweli kwa kipindi hicho kifupi, mimi nilimuona ni mtu anayejali wafanyakazi,
tofauti na wanavyomuongelea pembeni, sijui labda ilikuwa mimi kwa vile ni mgeni,
lakini sikuona hu ubaya wake.
‘Mgeni vipi, naona sasa umeshakuwa mwenyeji, au sio?’
akaniuliza na mimi nikasema.
‘Ni kweli nimeshaanza kuzoea hali ya hapa, ...sio mgeni
tena...’nikasema.
‘Kwahiyo nisikuite mgeni, nitakuita mhasibu wangu,
inatosha...’akasema huku akinywa maji kidgo.
‘Sawa an mimi nitakuita bosi wangu....’nikasema
‘Tukiwa kazini, nione kama mwenzako, usiniogope kama bosi
wako, nawashangaa sana wafanyakazi
wangu, wakiniona utafikiri wameona simba, huo sio utendaji mnzuri wa kazi,kufanya
kazi kwa kuogopana ni kutokujiamini,...hali kama hiy inakufanya uwe kama
mtumwa, badala ya kuwa mtendaji wa kazi. Mimi huwa najiuliza sana, kwanini
ufanye kazi pale unapomuona bosi katokea wakati
hukuwa na mipango hiyo,...
‘Mimi nijuavyo, kabla ya kazi yoyote unakuwa umeshajipanga,
nitaanza hiki na kile, kwa utaratibu au ratiba fulani kichwani mwako, nifanye
hiki kwanza, halafu kitafuatia hiki, na taratibu hizo hazitakiwi ziseme mpaka
bosi atokee, au sio, sasa iweje, umekaa, bosi katokea, mbio mbio, unashika
makaratasi, unajifanya unawajibika, huko ni kujidanganya, na matokeo yake ni
kuwa ukiondoka watu hawafanyi kazi maana wamezoea kusimamiwa...
‘Mimi nataka ufanye kazi kama kazi yako, kwa kujituma, hata
kama mimi sipo, ufanye kazi, ukijua kuwa kazi hiyo ni wajibu wako, au sio..?,
ndivyo nilivyofanya mimi, nikajijenga hivyo, hadi leo,...na ukiwa na hula ya
kujituma bila kusimamiwa, utafanikiwa sana katika maisha yako, hata ukiwa na
kazi yako mwenyewe hutapata shida...vinginevyo, kufanya kazi kwa kuonyesha kuwa
unafanya, huo ni unafiki wa kujidanganya mwenyewe...’akasema.
‘Mhh, ni kweli...’nikasema
‘Unaona wale waliopigana siku ile ulipofika, niliwapa barua
ya kuwasimamisha kwa muda, kwasababu
walipigana kazini hiyo ni kinyume cha sheria za kazi, lakini pia hawakutaka
kusema ukweli, lakini tetesi zikanifikia kuwa kumbe wawili hao, walikuwa wakigombea msichana, ni
aibu kabisa...'akasema akitikisa kichwa.
'Mimi nawashangaa watu, yaani watu wazima na akili zao wanagambana kwasababu ya mapenzi, mapenzi
hayagombewi bwana,....mapenzi yanakuja yenyewe, ukiona watu wanagombana kwa ajili ya mapenzi, watu hawo wana walakini, ....halafu cha ajabu msichana mwenyewe ana mchumba wake, na huyo jamaa yake ni mkali kama nini, ana hasira , ni watu wa huko Mara, sasa sijui, akisikia kuwa kuna mtu anamsogelea mpenzi wake, itakuwaje,...kuna mtu atakuja kupigwa risasi, na jamaa mwenyewe ni askari, lakini aliyekwenda shule.
Sasa wale jamaa,nimesimamisha kwa muda wakajifikirie
wanataka kazi au wanataka mapenzi, sisemi kuwa wasiwe na wapenzi, lakini hayo
ni nje , baada ya kazi, pili ni makosa kabisa kupigana kazini...’akasema
nikijua kafanya hilo kama onyo kwangu.
‘Na huyo binti nimempa barua kali, kuwa maswala ya mapenzi
mkiwa kazini ni marufuku, haya yanasababisha watu wasifanye kazi...’akatulia
‘Lakini hawo uliwasimamisha kwa muda, umewasaidia vipi,
maana naona kama uhasama wao ni zaii ya mapenzi, mimi nilisikia watu wakisema, uhasama wao umegusia hata imani zao za dini na
siasa...?’ nikamuuliza
‘Nilifahamu kuwa nikiwafanyia hivyo, kutatokea nini, maana
haikupita muda nimepokea simu toka kwa waheshimiwa, mmojawapo baba yake ni muheshimiwa
fulani , kaanza kwa kunilaumu, hata bila kujua chanzo ni nini...’akasema bila
kujibu swali langu, sijui hakunielewa au ana malengo yake mengine, na mimi kama
kawaida yangu nikamuuliza swali.
‘Anakulaumu nini huyo muheshimiwa?’ nikamuuliza.
‘Kwanza kaanza kusema kuwa kampuni yangu ina
ubaguzi,...’akasema
‘Ubaguzi gani.?’nikamuuliza kwa kushangaa
‘Hakusema ubaguzi gani hata nilipomuuliza, yeye aliendelea
kuongea tu.
‘Wewe inaonekana unakiuka taratibu za kazi na ajira,....’akasema
‘Taratibu gani nimekiuka muheshimiwa...’nikamuuliza
‘Unawezaje kuwafukuza kazi watu bila barua za maonyo,
uliwahi kuwapa barua za maonyo,hujawahi, kwahiyo wewe hufuati taratibu za ajira
na kazi,...’akaniambia.
‘Lakini muheshimiwa mimi sijawafukuza, nilichofanya ni
kuwasimamisha kwa muda, kwa amkosa waliyofanya, wakirudi tutakaa nao, ili
wajifunze, kama ni maonyo nimeshawaonya sana, kama wamekuambia sijawahi kufanya
hivyo, wamekudanganya muheshimiwa..’nikamwambia
‘Eeeh, huyo ni muheshimiwa halafu ukamwambia nini....?’
nikamuuliza pale nilipomuona yupo kimia kwa muda.
‘Usipowarejesha hawo wafanyakazi baada ya siku tatu, nitahakikisha
kampuni yako inafungiwa..’akaniambia hivyo.
‘Mhh, sasa hilo balaa, sasa utafanya nini, warudishe kazini?’
nikamuuliza na kumwambia nay eye akaniangalia machoni kwa muda, halafu akasema;
‘Nakumabia haya ili na wewe ujifunze, kuwa kila jambo lina
mitihani yake, usione kuwa mimi ni bosi nina wafanyakazi, ..nina pesa,
ukafikiri utakuwa salama, hutakutana na mitihani kama hiyo, ...watu kama hawo
wapo sana, na sio kwamba hawafahamu taratibu na sheria, wanafahamu, lakini
hulka na siliak zao ni hivyo, kusigishana...’akasema.
‘Eti unaniuliza nitafanya nini, nimeshafanya nilichofanya,
hakuna kurudi nyuma, ...nawasubiri hao wafanyakazi warudi kwa muda
niliowaambia, na wakirudi nataka barua ya maelezo kwanini walifanya hivyo, na
kama hawatatajieleza vyema, nitajua cha kufanya...mimi sigopi, maana nafuata
sheria, hii ni kazi , hii ni ajira kama mtu anataka kufanya kazi basi afanye
kazi kwa taratibu na sheria,vinginevyo, mimi sitasita kuchukua hatua,...’akasema
akonyesha sauti ya ubosi.
‘Mhh, mimi bado nina mashaka, kuhusu huo ubaguzi aliokuambia huyo muheshimiwa, huoni kuwa
labda, ni mambo ya malumbano yao ya kidini na siasa, na huyo muheshimiwa ana
chama chake au sio....?’nikamuuliza.
‘Unafahamu jamii yetu kwa sasa inaharibika, na chanzo
kikubwa ni kutokuwa makini na mambo yetu, tumekuwa bebdera fuata upepo, ...na
hili linanikumbusha ile kauli ya adui ujinga..., mtu anaweza akawa amesoma vizuri tu, akapata
cheti, ...,lakini akili hajaelimika...alisoma akakariri nadharia za wenzake,
lakini hakuziingiza kwenye utendaji akaona kweli zinafanya kazi...hili ni
tatizo.
‘Sasa basi, kama mtu angelisoma akaelimika hayo yote yasingelitokea,
nikuambie ukweli, dini ni sheria za mungu, ni kama sheria hizi za kidunia,
lakini dini inagusa sana moyoni, sasa usipokuwa makini ukajua ni kitu gani
unatakiwa ufanye kwa wakati gani, wewe utaitikia tu amiini....’ akatabasamu.
Nikuambie ukweli, sio kila mtu mwenye dini anaifahamu dini
yake vyema, na sio kila mwanachama wa siasa anaifahamu siasa ya chama chake
vyema, na hili ni kosa, wengi wanaufahamu wa juu kwa juu, sio ule wa mapana
yake, ndio maana kwenye sheria kuna wanasheria, japokuwa tuna ufahamu kidogo wa
sheria, lakini wapo waliobobea kwenye
sheria, wameisomea hiyo nyanja kwa undani zaidi, halikadhalika kwenye dini kuna
wanazuoni wake, wameiosomea dini kwa nafasi yake...sasa sisi kila mtu ni mwanasiasa,
kila mtu ni mtaalamu wa dini, tunajidanganya,...
‘Mimi ninashangaa sana iweje kila mtu anafahamu sheria za
dini, anajinadi na kulumbama hata kitabu cha dini chenyewe hakijui , hakipo
mkononi, unaongea unabishana,..halafu upo ofisini, mnabishana , mnalumbana, na
mwenzako, unapoteza muda wa kazi amba utakuja kulipwa, huoni hapo unamnyinya
mwajiri wako, hil hatulioni.
‘Sikatai watu wasiulizane mambo ya dini, ni kawaida, hata
mimi naweza kukuhoji kutaka kujua,..na kila mtu ana ufahamu wake wa yale mambo ya
kawaida ya dini yako na utendaji wa
ibada na matendo mema, lakini sio kwenye malumbano,sio kwenye hukumu, huko kuna
utaalamu wake, hiyo kazi wanatakiwa waifanye viongozi wa dini..nimewaambia
wafanyakazi wangu, na nakuambia na wewe malumbano ya kidini sehemu ya kazi ni
marufuku...’akasema.
‘Sasa hawa watu wameanza kunitishia, kuwa watanionyesha jeuri yangu..kuwa eti ni
mbaguzi, kuwa eti....hata siwaelewi.’akasema huku akionyesha kutahayari usoni
‘Wamekuambia watakuonyesha Jeuri gani..na ni akina nani hao?’
nikamuuliza
‘Sijui ...nmeona karatasi imeandikiwa, labda wanataka
kunishitaki au kunivizia nyumbani wanipige, lakini mimi siogopi mtu, kwa vile
nafahamu fika nipo kwenye sheria, sijamfanyia mtu ubaya...’akasema
‘Nimekuelewa bosi, pole sana...’nikasema
*********
‘Sasa ngoja nikuelezee kidogo historia yangu;
‘Mimi ni wa pili katika familia ya baba aliyekuwa na wake watatu,
na mama yangu mzazi alikuwa mfanyakazi
wa hospitalini na akiwa kazini akakutana na baba wakapendana wakaoana. Mama akabatika
kupata watoto wanne, wa kwanza akiwa mwanaume, wa pili mimi na wawili chini
yangu, wote wakiume.
Kwahiyo katika tumbo la mama yangu nilikuwa mwanamke peke
yangu.
‘Ulijisikiaje kuwa mwanamke peke yako?’ nikamuuliza
‘Wakati mwingine kiutoto, unaona kama umeonewa vile, kwani
utaona watoto wa kiume wakiwa na michezo yao ya kiume kama mpira wa miguu, na
mimi nataka nicheze, wananikataza, ...kuna kazi nyingine unaambiwa ni zako wewe
mwanamke, wanaume wanakuwa hawazifanyi...
‘Wewe ni mwanamke, huwezi,...’wananiambia, nikitaka kucheza
mpira na wao, lakini mimi naona naweza, kwahiyo wakati mwingine inakuwa ni
ugomvi, lakini kaka zangu walinipenda
‘Maisha ya kuanza
kuishi mbali na mama yangu mzazi, yalianzia pale nilipokuwa na umri wa mwaka na
nusu, kwa jinsi nilivyohadithiwa na mama yangu mkubwa, maana yeye ndiye aliyenilea nikiwa
mdogo hadi miaka minne...’akasema.
‘Nasikia mama wa kambo ni wabaya sana vipi mama yako huyo wa
kambo?’ nikamuuliza.
‘Kwa jinsi mama yangu huyo mkubwa alivyonilea siwezi
kumtofautisha na mama yangu mzazi, na sikuweza kufahamu kuwa mama wa kamb ni
wabaya. Mama yangu huyo, alinipenda sana kama malikia ndani ya nyuma...’akasema.
‘Hukutamani kurudi kwa mama yako, maana ulikuwa mdogo sana?’
nikamuuliza.
‘Kwakweli mwanzoni kabisa ule uhali wa kumkosa mama
ulikuwepo, lakini sio sana kutokana na mama huyo alivyotulea,kwahiyo
nilipapenda sana nyumbani kwa mama mkubwa kuliko hata sehemu yangu
niliyozaliwa, na hii ni kawaida kwa mtoto,hujenga mapenzi na kupazoea pale
alipolelewa zaidi ya pale alipozaliwa....’akasema.
‘Sasa kwanini mlichukuliwa kwenda kuishi na mama yenu
mkubwa?’ nikamuuliza
‘Mimi na ndugu zangu, tulichukuliwa kwenda kuishi na mama
mkubwa kwasababu mama alishikwa na ujauzito, na mimi nilikuwa mdogo sana, umri
wa mwaka mmoja na nusu, kwahiyo nilihitajia mtu wa kunilea, siwezi kukumbuka
vyema maisha ya udogo wangu, zaidi ya kuwa mama mkubwa alikuwa mama mzuri sana,
na hakuwahi kutunyanyasa, hata siku moja, hadi nikafikisha miaka minne.
Nikiwa na umri wa miaka minne, baba akatuchukua na kwenda
kuishi tena na mama yangu mzazi, na kwa vile nilishazoea maisha ya nyumbani kwa
mama mkubwa, ilinipa taabu sana kuyazoea maisha mengine, japokuwa huko ni kwa
mama yangu mzazi,...Maisha yalikuwa magumu sana kipindi hicho, maana kipato cha
mama, na sisi wanne, hakikudhi haja, ilikuwa ni hali ngumu kwa ujumla, lakini
tulizoea maana ni kwetu ni kwetu.
‘Kwani baba alikuwa hatoi pesa ya matumizi....?’ nikamuuliza
‘Alikuwa akitoa, lakini kilikuwa kiasi kidogo, shughuli zake
hazikuwa kubwa sana,...’akasema
‘Baba alikuwa na mke mwingine wa tatu, yeye alikuwa na
afadhali kidogo ya maisha,,,’akasema , na kusubiria kama nitauliza swali, na
alipona sijauliza swali akaendelea kuongea;
Maisha ya uke wenza yana mitihani yake, hasa pale wanawake
wanapokuwa na tabia za ubinafsi, ,mama mwingine, mke wa tatu wa baba, alikuwa
na tabia yake mwenyewe, sikuwa nimemfahamu vyema kabla, mwanzoni nilikuwa
nahisi mama wote wana tabia moja, tabia ya upendo kwa watoto, kama alivyokuwa
mama mkubwa.
Mimi niliombea na mama yetu huyo mwingine awe na tabia kama za mama mkubwa. Na kwa vile pale kwa mama tulikuwa tunaishi maisha
ya shida hali ngumu , baba akasema mimi
na kaka yangu mkubwa twende tukaishi na mama yetu huyo.
Sikufurahia sana kumuacha mama, na wadogo zangu wengine, maana
mama ni mama yako, lakini kutokana na nakama za kimaisha tukaona aheri twende huko tukabadili mazingira, nikiwa na kumbukumbu za mama mkubwa , kuwa hata mama huyo
huenda akawa mnzuri kama mama mkubwa.
‘Unaposema mlikwenda ina maana mama zako hao walikuwa
wakiishi mbali mbali sana, kiasi cha kusafiri?’ nikamuuliza.
‘Ndio, ... mama mkubwa alikuwa akiishi huko mikoani kusini,
mama huyo mdogo alikuwa akiishi hapa kwenye mka huu, lakini mjini, na sisi tulikuwa tukiishi huko
kijijini , mwanzoni tulikuwa pamoja na
baba, lakini baadaye baba akaenda kuishi na mama huyo mdogo mjini, ambapo wana
mgahawa na biashara nyingine.
*********
‘Mama sisi tunakwenda kwa mama wa kambo....’nikamwambia mama
yangu siku tuliyoambiwa kuwa tunakwenda kuishi na mama huyo wa kambo, mke wa baba
yangu. Nilishangaa kumuona mama hana raha usoni, sio kawaida yake, ikabidi
nimuulize mama.
‘Mama mbona huna
raha, ...kwasababu tunaondoka au kuna tatizo jingine?’ nikamuuliza
‘Wanangu nimeongea na baba yenu na yeye akaona iwe hivyo, muende
mkaishi huko mjini, ili muweze kusoma
vyema, kama mnavyoiona hii hali hapa nyumbani, chakula chenyewe ni cha shida,
na mnatakiwa kusoma, ...’akasema mama akionyesha uso wa huzuni.
‘Lakini mama mbona unaonekana kama huna furaha, ?’
nikamuuliza mama.
‘Aaah, wanangu, siwezi kuamini kuwa huko mtaishi kwa
amani,na inanisikitisha kuwa watoto wangu mumekuwa wakutangatanga,leo hapa
kesho kule, na mnapoondaka hapa, mimi nitabakia niwaza sijui huko mtaishije,
sijui mnafanywa nini, ni kawaida kwa mzazi...’akasema mama.
‘Mimi usiwe na wasi wasi na sisi...’akasema kaka
‘Lakini yote maisha, na ninachotakiwa kukifanya ni kumkabidhi
mungu, yeye atawalinda, nyie jitahidini sana kuishi vyema na mama yenu huyo,
muheshimuni na ishini vyema na wenzenu...’akatuambia.
‘Mama usiwe na huzuni, mimi nafahamu mama huyo atakuwa mzuri
tu, mbona mama mkubwa alitulea vizuri sana..’nikasema nikikumbuka maisha yetu
na mama mkubwa ambaye alitulea kama watoto wake wa kuzaa.
‘Wanangu binadamu wote sio sawa....lakini msiwe na wasiwasi,
mungu atawasaidia..’akatuambia
Basi safari ikafika tukaagana na nilimuona mama akitokwa na
machozi, lakini kwa kipindi kile sikujua mama ana maana gani, mimi na kaka
yangu tukaondoka.
Unafahamu tena utoto, furaha yetu ilikuwa kusafiri, na
sehemu yenyewe tunayokwenda ni mjini,bsi
mioyoni mwetu tulikuwa na hamasa tele, ...hata wadogo zangu walikuwa wakililia
na wao waende, lakini baba alisema tunaotakiwa kwenda ni sisi wawili tu. Mimi na kaka yangu .
Tukaingia kwenye basi, tukaondoka, tukiwa hatuna ufahamu ni
maisha gani tunykwenda kukabiliana nayo huko mbele, na mara kwa mara nilikuwa
naiona taswira ya mama yangu akiwa na huzuni, lakini baadaye usingizi
ukanishika, nilijikuta naamusha na kuambiwa tumeshafika...
NB: Karibuni kwenye kisa hiki kipya , natumai tutajifunza
mengi
WAZO LA LEO:
Tusipende kubishana na kuingia kwenye malumbano kwa mambo tusiyokuwa na ufahamu
nayo vyema, kwani kila jambo lina taratibu zake, na misingi yake, na watu wake
wa kuyasemea.Ndio maana kuna wanasheria, madakitari wahasibu, wanasiasa nk, sio
kila mtu ana ufahamu wa kila nyanja. Ukijiafanya unajua sana,
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Keep this going please, great job!
Stop by my web site - their website (rayfordmpvk.blogs.experienceproject.com)
Post a Comment