Moyoni nikawa kama nawashwa washwa, nataka kujikuna , hasira na
msongo wa mawazo vikanijaa sikuweza kuvumilia, nikasema kimoyomoyo,kwanini
niteseke wakati muhusika yupo, na muhusika si mwingine ni mume wangu,
....nikaamua kwenda kukabiliana naye.
‘....Ila kumbuka usimuulize maswali mengi ya kumuumiza
kichwa...’sauti ya docta ikawa ananireja kichwani, lakini hapo hapo sauti
nyingine ikawa inasema;
‘Huenda hayo yanayomtokea mume wako yanahusiana na hilo, ....’
‘Yanahusiana na nini,....?’
‘Ina maana mume wangu kanisaliti, ina maana ata hiyo ajali
imetokana na huo uzembe, na hiyo dhambi, ambayo tuliahidiana isije ikatendeka
kwenye ndoa yetu...haiwezekani, ..sio mume wangu huyo ninayemjua, hapo ni
lazima kuna kitu...’nikajiulizana kugeuka kumwangalia docta ambaye alikuwa
kashikilia simu akiongea na watu wake, na ilionyesha kuwa hana habari na mimi
kwa muda huo nay eye ndiye agenisaidia kujibu baadhi ya hayo maswali, nikasema
kimoyo moyo;
‘Kwanini niume kichwa wakati muhusika mkuu yupo....’nikageuka tena
kumwangalia huyo rafiki wa mume wangu ambaye aligeuka kidogo kuniangalia
akaonyesha ishara ya dakika tano...ina maana nimsubiri, ....kwa dakika tano,
haiwezekani...
‘Hilo siwezi kuvumilia tena ni lazima nikamuulize muhisika
mwenyewe...’nikasema na kumbe docta alinisikia, akageuka kuniangalia kwa
mashaka, na mimi moyoni nikaendelea kuwaza kuhusu uamuaiz wangu huo, na kusema
kimoyo moyo;
‘Hata kama ni kuvunja miiko ya docta...kwani wao ni nani,
....kwani nikimuuliza ndio itakuwaje, atashindwa kujibu, ataathirika, kwa nini
aathirike wakati ni dhambi zake mwenyewe..’nikawaza na kujikuta nikiongea tena
kwa sauti;
‘Sitaweza kuvumilia hili ni lazima nikamuulize..’ nikasema kwa
sauti kubwa, na hapo rafiki wa mume wangu akanigeukia, na kunitizama kwa macho
ya mshangao, na mimi sikumjali nikaharakisha kwenda huko kwa mgonjwa, na yeye
akawa ananifuatilia kwa nyuma huku akiendelea kuongea na simu, laini nilikuwa
nimemuacha umbali kidogo, ...
Nilipofikakwenye mlango wa kuingia kwenye chumba hicho alicholazwa mgonjwa,
niligeuka nyuma, kumwangalia huyo rafiki wa mume wangu, ambaye nilimuona akija
nyuma yangu kwa haraka, alionekana kama anaharakisha kunikimbilia ili kunizuia
nisiingie, ...na nilipogauke kumwangalia akawa ananonyoshea kwa ishara ya
mikono kuwa nisubiri kwanza, na wakati huo hataki kuachia simu, ikiwa karibu na
mdomo,inaonyesha alikuwa akiongea jambo muhimu na huyo anayeonega naye, na
hakutaka kulikatiza...
Mimi...sikumsubiria nikafungua mlango na kuingia ndani kukabiliana
na mume wangu...
Endelea na kisa chetu......
**********
Ni mimi: emu-three
3 comments :
Endeleaaa ndugu wa mm story nzuri Sana.
Endeleaaa ndugu wa mm story nzuri Sana.
Endelea ndugu story nzuri sn.
Post a Comment