‘Mwanangu nakuusia tena
na tena katika maisha yako kumbuka kutenda wema, jitahidi kugombea kutendea
wema, na ikiwezekana kila kwenye nafasi ya kutenda wema jibidishe uwe wa
kwanza, jipendekekeze kwa hilo na wala usione aibu, hata kama wenzako
watakucheka, na kukuona huna maana, wema huo ni akiba yako, ....’mama akaendelea
kunisimulia kisa hiki huku machozi yakimtoka,
Sikujua kwanini alikuwa akitokwa
na machozi kwa muda huo, nikamsogelea na tukawa tumekumbatiana kimama na mtoto
kwa sekunde chache, na baadaye akanianchi na kuniangalia machoni, na kusema;
‘Mwanangu naikumbuka
sana siku ile ya hukumu, siku ambayo pamoja na kusomwa kwa hukumu ambayo ndiyo
iliyoweza kubadili hisia za watu wengi katika kijiji chetu, lakini pie ndio
siku niliyoweza kutimiza dhamira yangu iliyokuwa moyoni,....nikaweza kujitoa
mhanga, japokuwa ilikuwa ni akzi kubwa sana moyoni....’akatulia.
Siku ile ilikuwa
muhimu katika mustakabali na msimamo wa wanakijiji, na ilikuja kuleta melekeo
mwema, kwa jamii yetu, kwani hukumu ile iliweza kugeuza mtizamo wa waliowengi
kuwa kumbe yawezekana, kumbe, mambo mengine, ni ujanja ujanja wa watu wachache,
kumbe mambo mengine yanatendeka, na swala tu la uamuzi, kumbe kuna watu wajanja
wanatumia udhaifi wa watu wengine kujinufaisha wao wenyewe, na haki za
waliowengi zikachukuliwa kwasababu ya ujinga wetu..
‘Nasema kwasababu ya
ujinga wetu, maana kama tungelisoma na kuyafahamu hayo yote, tusingelinyanyaswa
kihivyo,na watu kama mtalaamu wasingellikuwepo kwenye jamii yetu. Mtaalamu
alishawaona watu wengi bado wamelala, mlalo ambao hautarajiwi kuwa wataamuka
tena...mlalo ambao bado jamii nyingi za Kiafrika tunao, tunahtajiaka kuamuka na
kupangusa macho ili tuweze kuona mbele....’akatulia kidogo.
‘Ni vibaya sana kama
jamii itapuuzia elimu, na ni vabaya zaidi kama jamii itaona kuwa elimu sio muhimu,
elimu ni gharama, lakini vitu kama harusi, sherehe, ni muhimu....basi ujinga utatutawala.
Na matokeo yake ni nini ni kuwa kila mmoja, anakuwa mjanja katika ujinga,...’mama
hapo akatabasamu japouwa kulikuwa na muonekano wa huzuni.
‘Jamii isiyo elimika, kila
mmoja anajiona anafahamu zaidi,ufahamu mdogo tu, ufahamu ambao unaweza ukawasaidia
kwa muda mfupi,lakini kwa mtizamo wa mbali zaidi, ni janga ...hii yote ni
kwasababu hakuna anayefahamu kuwa bado wote wapo ujinganga, na adui yao mkubwa
ni ukosefu wa elimu, adui ujinga, ufahamu huo haupo, kwasababu hakuna aliye na
mtizamo uliojengeka kutokana na elimu, hapo unafikiria nini, kama sio jamii ya
watu walio na hula za hadaa , ujanja-ujanja, utapeli na ulaghai, ndiyo itakuwa
maisha ya kila siku ....
Mwanangu soma sana, na
jitahidi kusoma kwa nia ya kuelimiaka, na kukifahamu kile unachokisoma, ili
uweze kutambua ubaya na uzuri wa kila jambo, na ili pale utakapoamua kutenda
jambo uwe unaufahamu wake, maana elimu pia inaweza ikatendewa sivyo ndivyo..hii
ni kutokana na ujinga ambao ulisha kithiri kwenye hulka za watu, kutoka na hulka
hiyo walishaona kuwa ili upate ni lazima uwe mjanja.
Sasa kwa vile wameona
kumbe elimu ndiyo njia ya kuonekana unafahamu, wao, wanatatafuta njia za
kinamna za kuonekana wana elimu, ndio hapo unaona mitihani inaibiwa, watu
wanagushi vyeti, waonekane wamesoma, watu wanatumia hata lugha tu iwe ndio kigezo
cha elimu badala ya utaalamu wenyewe,...., na hapo ndipo huo msemo wa bora
kupata kuliko kufika unapotumika..
Ni bora mwanangu
ukafika, hata kama hukupata, lakini unafahamu ni njia gani uliyopitia hadi
ukafika, kwani wakati wa kurejea,utakuwa husumbukie tena. Ni bora ukafika,
ukajua umuhimu wa kufika kwako hata kama hukupata kuliko kupata na hujui jinsi
gani hivyo ulivyopata vimepatikana vipi, kwani huenda vyote ni vya dhuluma,
huenda hivyo vitu ni mali ya watu,huenda pia ni sumu ....
Mwanangu elimu iwe ni
ufahamu, sio elimu iwe jina tu kwako, ...elimu ikujenge kitaaluma, ujue ni nini
unachokifanya, ikujaze ujuzi, na sio iwe ni vazi tu, la kujionyesha,.....kuna
watu wanatumia hilo vazi na matokeo yake, wanakula vizivyo halali, ni
waheshimiwa, na wakuu, ni mabwana wakubwa, wanamiliki makampuni, ..lakini
ukichunguza yote hayo wameyapata isivyo halilali, wamapata kutoka kwenye mali
za wanyinge, wasiojiweza, mayatima, kwa
roho zao mbaya, wanamiliki hizo mali...hiyo sio elimu, huo ni ujinga, huo ni
utapeli na hiyo ni dhuluma..’mama akaendelea kuniusia.
‘Mwaanngu mara nyingi
usia wenye manufaa, unaonekana ni kero na kupoteza muda, ndio maana hata kama
utashinda kutwa nzima ukijaribu kuwaelemisha watu busara hizi, wengi wataishia
kusinzia, au kutokukusikiliza kabisa, na kama ni maandishi wengine watasema ni
maelezo marefu, hawana muda kuyasoma...’mama akasema pale aliponiona kama
napiga miayo.
‘Lakini mwanangu cha
ajabu, ukijaribu kuongea umbea, ujinga, mapenzi, nk na yale yasiyofaa kwa jamii, watu watacheka,
na kufurahia,..ndio jamii isiyotahmini elimu, na hata kama walikuwa wakinzia,
wataamuka, na hata kama ulikuwa huna marafiki, utakuwa nao wengi, na kuonekana mjanja, msanii unayejua kuwafurahisha watu...,kwanini...kwasababu
akili zetu bado zipo kwenye usingizi wa kuota ndoto za alinacha....hulaka hii
mwanangu iondoe, soma na fahamu ni kitu gani unachokisoma....
‘Mwanangu, siku ile
hukumu ikiwa inaendelea , tulipata taarifa kuwa mwanasheria kazindukana, na
alikuwa akituhitajia, na kwahiyo mawazo yetu yote yalikuwa yamejikita kwa huyo
mgonjwa, hata kilichokuwa kikiongewa humo ndani kilitupita pembeni ya masikio
yetu, na hata hukumu ilipomalizika kusomwa, tukawa wa kwanza kutoka nje na
kuingia kwenye gari la mwanamama kukimbilia huko hospitalini.
Nikurejesho kwenye
kisa chetu uone jinsi gani siku hiyo ilivyotuteka akili mimi na mwanadada,
kwani hata baada ya hukumu hiyo, sikuwa nimezingatia yale yaliyosomwa, na
sikuwa na umuhimu sana, nayo kwani ilishafahamika ni kitu gani kitafuta. Na hata
baada ya kutoka kwa hakimu ambaye alikuja kutuita tena, kutuelezea ni nini
kifanyike, sikuwa nimetulia kiakili, na hapo mwanadada akaniambia...
‘Usiwe na shaka,
hukumu yote ninayo hapo, nitakuelezea,na yote yatatekelezwa, usiwe na shaha....’akasema
mwanadada aliponiona nikiwa sina raha, ...hebu nikisumilie kidogo ilivyokuwa
siku hiyo...’akasema mama.
Tuendelee na kisa chetu.
**********
‘Mwanangu ni vigumu sana, kukataa jambo, ukiwa unalifahamu
kuwa jambo hilo litakuja kukusaidia katika maisha yako ya baadaye, ni wachache
sana wanaweza kufaya hivyo, wengi watapigania hata kama wanaona hawana haki na
hilo, ni jamii zetu zilizokosa uadilifu, na uadlifu ukiwa adimu,
kinachotutawala ni dhuluma tu.....’akasema
‘Tukiwa kwenye kusomewa hukumu, ndipo tulipopata taarifa
kuhusu mwanasheria, na mimi wakili mwanadada,tukawa na hamasa ya kuonana naye, lakini kutokana na mazingira
yaliyokuwepo mle ndani hatukuweza kutoka, ikabidi tusubiri hadi hukumu
imalizike kusomwa...
Nashindwa kuelewa ni kwanini ilitokea hivyo, kwani usiku
kucha nilikuwa na mawazo na mtu huyo,anayejulikana kama mwanasheria, badala ya kuwazia kesi yetu, ambayo mwanadada
alishaniashiria kuwa tumeshinda, na kilichobakia ni mambo ya kiutaratibu wa kisheriaambayo
sio kazi kubwa kwake, sasa ikawa naliona hilo sio tatizo tena, akili yote
ikahamia kwa mwanasheria, nilijikuta nikimuwazia mwanasheria, kwa muda huo wa
usiku wangu....
Hata tulipofika kwenye kesi, mawazo yangu yote yalikuwa kwa
mtu huyo, sijawahi kumuwazia hivyo kabla, sijui kwanini mawazo kama hayo
yaliuteka ubongo wangu, sijui ni kwa vile, muda wa kuwa naye karibu huenda
ukawa umekwisha, sijui ni kwasababu ya .....sikuweza kujiaminisha kwa hilo, kwa
vile sikutaka iwe hivyo, hata kama moyo wangu ulishaguswa na yeye.....kuwa
huenda nimempenda, na mara nyingi mtu akiwa katika hiyo hali, mkamuona kama
anafariki,au akishafariki, upendo huzidi...
‘Tulipokuwa ndani ya mahakama, badala ya kusikiliza kesi,
ambayo ndiyo jambo muhimu lililotuleta hapo, nikawa namuwaza huyo mtu,
mwanasheria....je hali yake kwasasa inaendeleaje, je atapona, na kama atapona,
nitafanyaje ili nisije nikamuuza moyo
wake, kwani kwa kauli yake ya mwisho ni kuwa anataka atuoe sote wawili, na mimi
hilo naiona lina ugumu, je kama akifa..hapana hatakufa..atapona kwahiyo
nifikirie kama akipona, itakuwaje...na wakati nipo ndani ya dimbi la mawazli
ndipo kikaletwa kikaratasi na mtu mmoja, ..
Kwa muda ule nilijua huenda kikaratasi kile kimetoka kwa
mwanadada, kwani yeye alikuwa mbele kwenye meza ya waendesha mashitaka, na huenda
kulikuwa na ujumbe anataka kunifikishia, maana mimi na mwanadada tulishakuwa
wanandugu wa ukweli...nikakifunua kile kikaratasi, nikaona maandidhi ya juu
yaliyochapishwa, yakionyesha kuwa kimetoka hospitalini, moyo ukalipuka paaah...
‘Oh, kinatoka hospitalini, kinasema mwanasheria kazindukana,
na anatuhitajia mimi na mwanadada kwa haraka...’nilipomaliza kukisoma nikainua
kichwa kumwangalia mwanadada, nikakuta naye kashikilia kikatarasi, na akawa
anageuza kichwa kuniangalia na kuniashiria kuwa nisubiri...
Oh, kwanini tusubiri, huenda huyu mtu yupo katika hali
mbaya,na anaona kuna jambo muhimu la kutuambia...’nikawa najiongelesha
mwenyewe, nikataka nimwambie mwanadada, kwa vile yeye hawezi kutoka mle ndani
kutokana na majukumu aliyo nayo, basi imi nitoke kimiya kimiya, niende
nikaongee na huyo mgonjwa. Nikaandika ujumbe kumuelezea hivyo mwanadada, na ule
ujumbe akapelekewa mwanadada
Mwanadada, akanigeukia na kuniashiria kuwe nisubiri...basi
ikawa sina njia nyingine, nikasubiria, huku hukumu ikiendelea kusomwa, lakini
akili yangu haikuwemo kabisa humo ndani, nikawa namuwazia mwanasheria
‘Nahisi yupo katika hali mbaya sana, nahisi anataak kuacha
usia wa mwisho..au kapona, na anatuhitajia kwa jambo muhimu sana..lakini
kwanini kwa haraka, hapo nikamgeukia mwanadada ambaye alikuwa kwenye meza ya
waendasha mashitaka, na y eye alionekana mwingi wa mawazo, na hapo akili yangu
ikatoka kabisa hapo mahakamani na kuanza kumuwaza huyu mwanasheria,
‘Oh kwanini namuwaza hivyo, namuwaza kama shemeji yangu,
au?...hapana namuwaza kama mtu muhimu katika maisha yangu, kwa vipi, ...mh, kwa
mtizamo wa mwanadada, anatakiwa kuwa mume wangu,..oh, haiwezekani, ...mmh,
lakini kwanini isiwezekane, kama inawezekana akatkuwa, mume wa aina yake, mume
wa kunirithi,mmh, hapana lakini, lakini ....kwa ajili ya mtoto inabidi nikubali
au...?’hapo wazo hilo likaanza kunijaa akilini.
‘Hapana , siwezi kufanya hivyo...ndiyo kwa ajili ya mtoto
sina jinsi....’
Sijui kwanini ilitokea hivyo, hasa baada ya mwanadada
kunitania kuhusu mimi kuolewa na huyo mtu, na sio kuolewa kurithiwa, Nikawa
namuwaza sana huyo mtu, kila kukicha, kila nikiwa na wasaa, akili yangu ikawa
haiachi kumuwaza, ina maana nimeshampenda, hapana, hilo ni kosa .....ina maana
ule utani ndio umeniathiri kiasi hicho, ...kwa ujumla kwanza nilifahamu kuwa
mwanadada ananitania kuhusu mimi kuolewa na mwanasheria, kwa ajili hasa ya
mtoto, na nilipooa anasisitizia nikajua kuwa kweli kazamiria...
‘Kabla ya hapo kiukweli sikupendelea wazo hilo, na halikuwa
kichwani mwangu kama jambo la kuniumiza kichwa, lakini baada ya mwanadada kulitamka
hilo wazo na kunisisitizia, kila mara nilipokuwa nikimuwazia huyu mwanasheria,
kuhusu hali yake nikawa pia nawazia hilo wazo la mwanadada, na hapo nikawa na
maswali mengi yenye je ndani yake;
‘Je kama ingeliwezekana kuolewa na huyu mtu,maisha yetu
yatakuwaje, na je kama atasisitizia anioe kwa hali kama hii nikakubali jamii
itanielewaje, je nitakuwa nafanya jambo la kiungwana,je nafanya hilo kwa sababu
ya upendo au kwa msukumo, je kweli nampenda huyu mtu ...lakini kila nilipowazia
kiundani, nikajikuta nashindwa kupata jibu la uhakika, nikaona kuliko kuishi kwenye maisha hayo ya uwalakini,
maisha yaliyojaa dhana , basi nikoana kuwa ni bora nisiolewe naye.....lakini....likaja
tatizo la mtoto.
‘Kiukweli kilichonisukuma sana , kuliwaza hilo,ni mtoto
wangu, ambaye alikuwa haishi kumtaja baba yake huyo mdogo, kwake yeye
alishamuona ndio baba yake mzazi, ...ndiye anayemfahamu kama baba yake kwani
baba yake alifariki akiwa mchanga hamjui na hajui kabisa kama kulikuwa na baba
yake mzazi mwingine, kwahiyo akiamuka usingizini, ananiuliza baba yake huyo yupo
wapi, akiwa na maana baba yake huyo mdogo....maana wakati mwingine alikuwa
akifika hapo na kushinda hadi usiku, akiwa kahakikisha mtoto kalala ndio
anaondoka...
‘Kwa umri wake, sikuweza kumelezea chochote kuwa huyo sio baba yake, na tangu
awali alishazoeshwa kuambiwa kuwa huyo ndiye baba yake mzazi, na nafikiri
ilifanywa hivyo makusidi, ili niweze kurithiwa na shemeji yangu huyo...kwenye
familia hiyo, walikuwa hawampendi sana mwanadada, kwa kipindi hicho cha nyuma,
lakini jinsi keso ilivyokuwa ikienda, ndivyo, alivyozidi kukubalika kuwa kumbe
ni mtu muhimu sana.
‘Kwakweli si kupendelea hilo wazo,....sasa mwanadada
kalidakia na kunisisitizia nalo, na nahisi kwasababu ya mtoto, na najua
kiundani anampenda mchumba wake, na kuachana naye itakuwa pigo kwake, lakini
huenda baada ya yote hayo, kaamua kuachana naye, kutokana na mila na desturi,
kutokana na haya yaliyotokea , na huenda kutokana na mtoto,yeye kaona ni bora iwe hivyo...na huenda ni bora iwe hivyo, kwasababu ya
mtoto...
Mhh, naona iwe hivyo, hasa kwa ajili ya mtoto, hata mimi
kwasasa naona ni bora iwe hivyo ....naona ...nikubali tu....’nikahitimisha hayo
mawazo
Ilibidi nifikie uamuzi huo mgumu, kwasabbu ya mtoto, nikaona
nikubali tu kwa shingo upande, ilimradi mwanadada karidhia, basi sina budi,
nikaamua kuwa nikikutana na mwaansheria, nitakubali hilo ombi kwa ajili ya
mtoto,...nilipofikia uamuzi huo ndio hiyo hukumu ikawa imeshatolewa, na
mwanadada akanishika begani na kuniambia,
‘Twende hospitalini....
***********
Mwanadada naye kwa upande wake hakuweza kulala, alijikuta
akiwaza mambo mengo akijua kuwa kazi iliyokuwa imemleta hapo kijijini
imekwisha, na wakati wa kuondoka umefika, lakini bado alijiona ana jukumu moja
kichwani, jukumu ambalo, lilitegemea ushirikiano wa watu wawili, mwanamama kwa
uapnde mmoja, lakini pia mwanasheria kwa upande wa pili...
Ama kwa mwanasheria haikuwa taabu sana, kwani alishatoa
mtizamo wake, kwahiyo shida ikawa jinsi gani ya kumshawishi mwanamama, ...hapo
akajiona mawazo ya kesi akayaweka pembeni, kwani alishafahamu hukumu ipoje,
mawazo yake yote yakajielekeze jinsi gani angeliweza kumsaidia mwanamama, na
mwanae,ikizingatia kuwa mwanamama ana mtoto, na huyo mtoto anahitajia matunzo,
na...
Mwanadada alikuwa
tayari kukubali kujitoa mhanga, na kumuachia mwanasheria amuoe mwanamama,
lakini kwa jinsi alivyoona msimamo wa mwanamama, haitawezekana, kwa jinsi hiyo,
hana budi, iliyobakia ni kuendelea na mapenzi yake ni mpendwa wake, mtu aliyempenda
kwa moyo wake wote. Lakini je kwa haya yalitokea, bado mwanasheria ana mapenzi
ya dhati juu yake, je anampenda yeye zaidi kuliko mwanamama, hapo akaingiwa na
kitu kama wivu, kama ilivyo hulka ya kibinadamu.
‘Lakini mwanamama keshajitoa hapa,...’akasema kimoyo moyo,
...inabidi nisiwe mchoyo, inabidi nimshawishi huyu mtu mpaka akubali kuolewa na
mwanasheria,...hili ndilo nalioa ni jambo jema,sasa kama akikataa kabisa
itakwuaje...?’ akajiuliza tena....’Lakini je mwanasheria atachukuliaje uamuzi
wake huo, anaweza akaona simpendi...?’ akawa bado anajiuliza
‘Oh mwanasheria, najua utanielewa tu, hata hivyo tangu
mwanzo ulishaamua kunitema, ukanitekeleza, kwanini sasa isiwezekane, japokuwa kiukweli
nakupenda sana mwanasheria, lakini kwa ajli ya haya, kwa ajili ..hasa ya mtoto,
ninaamua umuoe mwanamama....’akasema kimoyomoyo, akatulia kuukaribisha uamuazi
huo moyoni, na kuendelea kusikiliza hukumu iliyokuwa ikisomwa na muheshimiwa
hakimu, lakini hata hivyo, akili yake, haikuweza kutulia na kuisikiliza, kwake
yeye ilikuwa kama marejeo kwani alishaiona....
‘Nafikiri uamuzi ni huo, lakini inavyoonekana mwanamama,
hatakubali, sasa nifanyeje...?’ akajiuliza tena, wazo hilo lilipomjia
akilini....
‘Oh, kama mwanamama kakataa, na inaonyesha wazi kuwa uamuzi
wake ni huo, sasa nifanyeje, ...oh, kama kakataa basi itabidi nilirudishe penzi
langu kwako mwanasheria na sasa litakuja kwako likiwa na sura mpya, sura yenye
mageuzi ya kweli, kwani mila na desturi ambazo zilikuwa hazikubaliki, zitakuwa
zimeondoka.....mmh, haya yote nimeyafanya, kwa vile ninakupenda mwanasheria, na
nafahamu hata kama ningekuacha umuoe mwanamama, bado ningelikuwa na wakati
mgumu wa kukusahau, sasa, mwanamama kakukataa, nifanyeje...oh, cha muhimu
kwanza upone...’akajikuta anatabasamu.
‘Mimi na wewe mpenzi inabidi tufunge ndoa kabla sijafunga
safari ya kwenda Ulaya kusoma...hii itakuwa ndoa ya baraka, ndoa ambayo imekuwa
ikipangwa na kupanguliwa, lakini sasa itakuwa ya kweli,....hakuna kizuizi tena’akasema
huku akitabasamu.
‘Lakini yule mtoto itakuwaje....hapana, nitakuwa nimefanya
unyama wa hali ya juu,....lazima nitafute njia za kumfanya yule mtoto asiteseke
kisaikolojia, ...kwa vipi, njia niliyoiona ni ya busara ilikuwa ndiyo hiyo kwa
mwanamama, kuolewa na wewe mwanasheria, lakini nijuavyo mimi mwanamama hawezi
kukubali, keshakataa kakataa..basi inabidi nimuombe, nimchukue mtoto,hata hilo
hawezi kukubali, tufanyeje sasa, hapo sijui , hapo sina la kufanya,
maana,....haitawezekana kwa mara moja kukubali uke wenza,...mmh, hilo nalo kwa
sasa naliona ni gumu, labda kwa baadaye, sijui time will tell....
‘Kwanza cha muhimu, ni kukubali ndoa, mimi na mwanasheria tufunge
ndoa ya haraka, najua hilo halina kikwazo, kwa vile mwanamama keshakataa, basi
inabidi hilo nilipitishe, na ndoa hii tutaifunga hapa hapa kijijini, kabla
sijajiandaa kwa safari yangu ya kwenda kusoma,..., nitamkubalia mwaansheria awe
ni mume wangu, kwa masharti kuwa tufunge ndoa kwanza, kabla sijaondoka, na
kipindi hiki nikisubiria muda wa kwenda huko Ulaya, tuwe kwenye
fungate,....mmh, naisubiria hiyo fungate kwa hamu...’hapo akatabasamu tena,
huku akiwaangalia watu waliokuwa wakisikiliza hiyo hukumu.
‘Oh, mungu mjalie mwanasheria apone, ..ili tuwe mke na
mume....’ na mara akagutuka pale alipopewa kikaratasi na mtu mmoja, akakifungua
haraka, na kukisoma;
‘Mimi ni docta,
mwanasheria kazindukana, anakuhitaji wewe na mwanamama, ...haraka...’ujumbe
ukasema
‘Kazindukana, anatuhitaji kwa haraka, kwanini kwa
haraka....’akasema na hapo akageuka upande ule waliokuwa wamekaa mwanamama, na
kumuona naye akiwa anasoma kikaratasi kama kile alichopewa, yeye, na mara
mwanamama akageuza kichwa na wakawa wanatizamana, mwanadada aakatabasamu, na
kumuashiria mwanamama asubiri....
Na akiwa keshatuliza mawazo yake, mara akapokea kikaratasi
kingine, kikiwa kinatoka kwa mwanamama kuwa mwanamama kaona ni busara yeye atoke
kimiya kimiya aelekee huko hospitalini na kwa vile mwanadada ni muhimu sana
kuwepo hapo kwenye kesi hadi mwisho, aendelee kuwepo na kesi ikimalizaka,
mwanadada atakuja huko hospitalini, na ataweza kumuelezea ni kitu gani
kinaendelea. Mwanadada alipomaliza kusoma huo ujumbe, akageuza kichwa na kumuashiria
mwanamama aendelee kusubiria kwani wote ni watu muhimu kwenye hiyo kesi.
Baada ya hukumu kuisha kusomwa, mwanadada,akasimama kwa
haraka akaenda kumwahi mwanamama, na alimkuta mwanamama akiwa kazama kwenye
dimbwi la mawazo, akamshika begani na kumwambia
‘Twende hospitalini....’wakaondoka lakini walipofika mlangoni, wakakutana na na
mtu katumwa kuwa yeye wakili mwanadada na mwanamama wanahitajika kwa hakimu, ni
muhimu sana....
NB: Je kuna nini kitatokea,
WAZO LA HEKIMA: Pamoja
na mipango yetu, pamoja na uhitaji wetu, lakini mwenye mamlaka na yoye hayo ni
mwenyezimungu, wakati mwingine ni bora kukubali yote japokuwa sivyo
tulivyotarajia, na ni vyema tukapana mipango yetu, huku kichwani tukisema
‘akipenda mwenyezimungu’ maana hatuna uhakika wa mia kwa mia kwa yajayo.
*******************************************************
na hii hapa:
****************************************************************************************************************************
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Ni kisa cha kuelimisha/akilisha, sisimua na kuleta raha usomapo yaani kisiishe...Katika maisha yangu nilidhani hizi mila za kurithishwa zimeisha kumbe bado.....Hata mimi sijui kama ningekubali hilo ..ila sasa kinachotakiwa hapo ni kumwambia tu mtoto nadhani haitakuwa mbaya ..ila naona tungeje na tuone itakuwaje....
is decent increasingly favourite, in set out because of complete priced rubble?
This bind has helped a special computing machine to attain destined you
birth your ain hobbies, and strength not kind.
rack up your jewelry pieces, and have a few drops of ketone founded effulgence remover into the Lululemon Outlet Burnaby Free Shipping Lululemon Pants procession depends
on where you can legal document lawsuit opposite players in your cart, which instrumentation inferior second judgment what
you're expiry to be fitted out without compromising your way.
prefer a neutral material and tool. rest a few written record inquisitory for commercial document codes.
It's a snew one. You
Post a Comment