Hakimu aligeuka kumwangalia mshitakiwa, ambaye alikuwa muda
wote kainamia chini, kama ilivyokawaida akaambiwa ajitetee kabla ya
hukumuhaijapitishwa, na tofauti na watu walivyofikiria, kuwa huyo jamaa
hataongea tena, tofauti na watu walivyokuwa wamefikiria kuwa huyo jamaa
kachanganyikiwa, ....jamaa yetu huyo akiwa kizimbani akaanza kuongea, na neno
lake la kwanza lilikuwa hili;
‘Nawaombeni sana msamaha kwa hayo niliyowatendea...’akatulia,
na kuinama, na alikaa hivyo kwa muda,halafu alipoinua kichwa machoni kulikuwa
kumejaa machozi, lakini akaendelea kusema;
‘Najua sitaeleweka, njua sikueleweka, nafahamu kila mmoja
keshaniweka kwenye kundi la watu wabaya, ambao hawastahili hata kuishi,...kwa
hayo yaliyotokea, ...siwalaumu, hata ingelikwua mimi ningelifanya hivyo, yote
hayo ni udhaifi wa kibinadamu, sote hatupo kamili, ....’akatulia.
‘Kama nilivyowaambia awali, lengo langu lilikuwa hivyo, kuwa
ninachofanya ni kulinda mali asili ya nchi yetu, huenda sikueleweka, na
sitaweza kueleweka, lakini kama isemwavyo, hujafa hujaumbika, tusubiri, nikifa,
tusubiri, nikitoweka, na hayo niliyoyatabiri yakitokea, mtanikumbuka....’akainama
tena.
‘Ardhi ndio asili ya kila mwanadamu, tumetoka kwa udongo
tutareja kwa udongo, ndio maana wenzetu walioendelea hawafanyi mchezo na ardhi yao,
huwezi ukafika mgeni ukapewa ardhi, kama tunavyofanya hapoa kwetu...watu
wanakuja wanapewa ardhi kwa mkataba wa mika ambayo binadamu wa sasa hawezi
kufikia....wanapewa ardhi, wanachimba madini watakavyo..haina thamani kwetu,
kama ilivyo na thamani kwao...’akatulia.
‘Tusifanye mchezo na ardhi, toeni vingine, lakini sio ardhi,
kama kuna kiongozi anatoa aradhi kwa wageni, basi huyo sio mzalendo, nadiriki
kusema hivyo, kwasababu hajali kiazai cha nchi hii..hajali watoto wetu, wajukuu
, na vitukuu, watakuja kuishi wapi....’akaangalia juu.
‘Mimi nilikuwa sio kiongozi, lakini kama ningelipata nafasi hiyo, mbiu yangu, ingelikuwa ardhi kwa wazawa, ....ardhi ni mali ya
wazawa, ardhi ni mali ya wananchi, na sio mali ya kugawa ovyo ovyo, kwahiyo
ningelitoa nafasi ya kumiliki ardhi kwa kila raia, na hilo ningeliwekea
kipaumbele, kuwa kila anayemiliki ardhi awe na hati miliki..isiwe ni taabu
kuipata, kama ilivyo sasa.....mnaona wenywe inavyokuwa taabu kupata hati miliki,
maana, wanataka kuwapa wakuja...mimi hilo nisingelikubaliana nalo kamwe...’akatulia.
‘Nimeambiwa nijietete, nashindwa kujua natakiwa kujitetea
kwa lipi...kwasababu niliua, kwasaababu nilihadaa kwasababu nili...ooh, kwanini
hamuangalii lengo langu lilikuwa ni lipi, kwanini hamuangalii, ili lengo hilo
litimie, ningelifanya nini, kama kulikuwa na vikwazo ningelifanya
nini....hamtaki kuliangalai hilo, kwasababu hamnielewi na hata kuja
kunielewa...
‘Mimi naomba msamaha, kwa wale waliopatwa na maafa hayo, kwa
vile, hawakujua lengo langu, ni kweli, kuna tabia mbaya ya kuwaua, wazee,
wakisingiziwa uchawi,..na mimi nilitumia hilo katika kufanikisha amlengo
yangu...najuata sana, na nawaomba wale wote wenye tabia kama hii waiache, maana
wazee ni ...hazina ya taifa, kama tusipowaheshimuna kuwapa haki yao, taifa
halikuwa na baraka...’akageuka huku na kule kama anamtafuta mtu.
‘Kwakweli nilisikitika sana, pale nilipomuona mama mkunga
akitokea hapa mahakamani kuja kutoa usahhidi, kibiandamu, tulishamsahau,
tulijua keshakufa... na alipotokea katika hiyo hali iliniuma sana, nikawa
anjiuliza, hivi kweli mimi nimekuwa mnyama kiasi hichi, ina maana mimi nimekuwa
ibilisi, muuaji, ..nikamuomba mungu anisaidia,..na ndipo nikapaat wazo la kuja
kusema niliyoyasema...’akatulia.
‘Niliendelea kuwasingizia watu wengine,..oh, kaka yangu,
nikamsingizia kuwa ndiye aliyefanya hayo yote, nilifanay hivyo, ili niendelee
kufanya utafiti wangu, lakini yaonekana haikuwa bahati yangu, na naumuomba sana
msamaha kaka yangu kwa kubeba mzigo huo mzito...namshukuru kuwa amekuwa ndugu
wa ukweli, japokuwa hatanielewa, kama ambavyo hamtanielewa nyie...’akageuka
kumtafuta kaka yake, na akamuona akiwa kakaa viti vya pembeni.
‘Nawaomba msamaha mabinti wadogo niliowahi kuwachukua kama
majaribio katika kufanikisha utafiti wa dawa yangu, na ...nashindwa kulielezea
hilo, kwasababu halikuweza kufanikiwa, kwasaabbu sikupata muda, na sikupata
ushirikiano,...ni jambo la kitaalamu, na lisahaulike hivyo, ....ama kwa binti wa
mkuu wa kitengo cha upelelezi, nakiri kuwa nilimpenda, na nilitaka awe mpenzi
wangu, hata ikibidi nimuoe, lakini alionioana mimi ni mzee...akawa anamtaka
kijana mwenzake,namuomba msamaha kijana mwenzako kwa hayo niliyomfanyia, hilo
nakiri ni kosa....’akageuka huku na kule.
‘Nimeambiwa nijitetee, na kama nilivyosema awali, lengo
langu halikuwa baya, kama mnaona lilikuwa baya, najitetea kuwa mnisamehe,
lakini sikuwa na lengo baya kama mnavyofikiria nyie, ...na nitafanya makosa
kama sitawaomba wale wote niliowashirisha kinamna bila wao kujua,....kuna jamaa
wa mtandao wa simu, yeye hakujua lolote, pale nilipomuahadaa kuwa amfanyie yale
aliyofanyiwa mwanamama...wengi wamelisahau hilo.
‘Nawaomba msamaha nyote....’ akasema huku akionekana kama
anatetemeka, halafu akatikisa kichwa kama kuondoa kitu, halafu akainua kichwa
na kumwangalia hakimu, akasema;
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, nakuomba unielewe nia na
madhumuni yangu hayo, kwa masilahi ya vizazi vijavyo, kwa masilahi ya uzalendo
wa taifa hili,....’akatulia huku akionekana kama kuyumba, halafu akajitahidi
kusimama vyema, na kuendelea kusema.
‘Muheshimiwa na wewe, kama hutanielewa, basi, ....ninachoweza
kusema ni kuwa nakutakia kazi njema, na siku moja tutakunana mbele ya hakimu
mkuu, atakuthibitishia nia na lengo langu, ....ni hayo tu muheshimiwa hakimu...’akamaliza
na mara akaangalia mbele na kuanza kutetemeka,...akadondoka chini....
Kwa haraka askari akamwendea, na kumkagua, akainua uso na
kumwangali hakimu,akasema
‘Inaonekana kapoteza fahamu....’
‘Muiteni dakitari..’amari ikatolewa na hakimu akatoa saa moja
la mapumziko.
*********
Mwanadada akiwa na Mwanamama, kwenye chumba cha mapumziko,
wakisubiria muda wa kuingia mahakamani tena baada ya mshitakiwa kudondoka na
kupoteza fahamu, kitu kilichokuja kutambulikana ni kutokana na hali aliyokuwa
nayo ya kukataa kula, ....
Wakina mama hawa walikuwa kimiya, kila mmoja alikuwa
katingwa na mawazo yake, na moja kati ya hayo ni hali ya mwanasheria ambaye
alikuwa hajaweza kuzindukana , na kutokana na maelezo ya dakitari kama leo
hatazindukana, hawatakuwa na jinsi nyingine, itabidi wayaondoe yale mashine
aliyowekewa.
‘Docta, kwanini, hajazindukana, na kwanini muyaondoe hayo
mashine, acheni, …’akawa analalamika mwanamama, na mwanadada,alikuwa kainama
chini huku machozi yakimtoka.
‘Sio kwamba tunapenda kufanya hivyo…ni taratibu, lakini tutaona
itakavyokuwa , tukikutana na jopo la madakitari, huenda tukapata ushauri zaidi,
….nahisi kuna tatizo na huenda tukiyaondoa haya mashine tunaweza kupata
ufumbuzi wa moja kwa moja.....’akasema docta na kuondoka.
Walipotoka hapo hospitalini asubuhi, wakaelekea mahakamani,
kila mmoja akiwa kimya, utafikiri wamesikia taarifa ya msiba.Mwanamama akiomba
kivyake na halikadhalika mwanadada akiomba kivyake, na akilini mwa mwanadada,
alishafikia uamuzi kuwa kama mwanasheria atazindukana na kupona, basi ikiwezakana mwanasheria huyo amuoe mwanamama,
sio yeye...
Alifikia uamuzi huo, pale alipoona jinsi gani mtoto wa mama
huyo anavyompenda mwanasheria, na aliona kama ataolewa yeye , mtoto huyo atamkosa
mtu muhimu sana, na huenda mtoto huyo ataweza kuishi maisha ya kinyonge,
japokuwa angaliweza kumchukuwa yeye wakaishi naye baada ya kufunga ndoa na
mwanasheria huyo, lakini mtoto huyo hataweza kuachana na mama yake.
‘Je nikubali uke wenza....?’ akajiuliza huku akivua miwani
yake, na kuishikilia mkono na kusisogeza mdomo,akiwa anawaza mbali , na akasema
kimoyo moyo,
‘Hapana kwasasa hilo halipo akilini mwangu....inawezekana
kwa baadaye, lakini sio kwasasa, cha muhimu ni hawa watu wawili waoane kwanza,
mimi nitaendelea kusubiri, ili kumalizia masomo yangu ambayo nilishayaanza...mengina
nitaju huko baadaye, huenda, akatokea mwingine nitakaye mpenda kama
mwanasheria....hilo linawezekana’ akawa anawaza ivyo.
Hata hivyo, kila alipopata mwanya wa kumwambia mwanamama,
kunatokea kizuizi,mpaka wakajikuta wapo mahakamani, akaliwekea muda, kuwa
akipata nafasi tu atamuelezea wazo lake hilo.
‘Nitamshauri hata mwanasheria afanye hivyo, japokuwa
nampenda sana, lakini siwezi kuwa mchoyo, na kuiacha hiyo familia ikikosa mtu
wa kuihudumia,kwa ajili ya yule mtoto ngoja iwe hivyo...mimi bado nahitaji muda
sipo tayari kwa ndoa kwa sasa’akasema kimoyo moyo.
Wakati yeye anawaza hayo, mwanamama, alikuwa na mawazo
tofauti, kwani akilini alikuwa akiwazia jinsi gani ndoa ya wapendwa hawo wawili
itakuwa, na alidhamiria kuwa yeye atakuwa mpambe muhimu wa mwanadada, na akawa
akisema moyoni;
‘Natamani siku hiyo ifike, hawa watu wawili ni muhimu sana
kwangu, nataka waoane, waishi maisha ya raha,kwani wanastahili hilo,....nitakuwa
natenda sio haki kuingilia ndoa y watu hawa wawili na nitalipinga wazo hilo la
kirithiwa kwa nguvu zangu zote.....’akawaza hivyo.
Walipokuwa kwenye chumba cha mapumziko, wakisiburia, kuingia
tena kusikiliza kama mshitakiawa ataweza kuendelea au ndio kesi itaahirishwa
tena, walikaa hivyo hivyo bila kuongea ,
na mwanadada akataka kuliongelea wazo lake, lakini kabla hajafungua mdomo, mwanamama
akauliza;
‘Una uhakika huyu mtaalamu hajaigiza huko kudonoka kwake,
kama ilivyo kawaida yake kupoteza muda tu...?’ akauliza
‘Kwakweli sijui, hata mimi simwamini, lakini dakiatari
kathibitisha kuwa alikuwa kapoteza fahamu, na hadi natoka huko ndani bado
alikuwa hajajitambua, na dakitari aakshauri kuwa asisimame kuongea tena, ..hata
hivyo, sizani kitaharibika kitu, kwani hukumu, ilishapitishwa, ....’akasema
mwanadada
‘Ina maana ulishaiona hiyo hukumu?’ akauliza mwanamama.
‘Tusingeliweza kuiona, mpaka isomwe, lakini sisi kama waendesha mashitaka haya,
tulishajua .....na hatukutakiwa kuongea lolote,..tusubiri, maana utetezi wake
una nafasi katika hiyo hukumu...’akasema mwanadada.
‘Je nikuulize swali, ilikuwaje hadi tukasikia kuwa
mshitakiwa katoroka?’ akauliza mwanamama.
‘Hata mimi nilishangaa niliposikia taarifa hiyo, ilivyokuwa
ni kwamba, siku kiongozi wa kijiji alipokwenda kumtembelea ndugu yake, kuna mtu
alimuona kiongozi huyo akitoka pale jela, alipokuwa huyo mshitakiwa, sijui
alikuwa na lengo gani, mtu huyo akaenda kumfahamisha askari wa zamu ambaye
alikuwa nyumba ya jirani akipata chakula cha mchana.
‘Kumbe yule askari, alikuwa na nyumba ndogo hapo jirani, na
alikuwa akitumia na hiyo nyumba ndogo, wakala na kulewa,akajisahau kuwa yupo
akzini, ...sasa alipasikia taarifa hiyo, akakurupuka mbio,na kuanza kutoa amari
kuwa mshitakiwa katoroka na atakuwa kaenda huko kijijini, ...
‘Waliopewa taarifa hiyo, na wao ndio walikuwa ndio wanaingia
zamu,...uzembe mdogo wa kuaminiana,walipokea zamu bila hata ya kukagua kuwa
kila kitu kipo sawa,..ni kweli kila kitu kilikuwa sawa, mshitakiwa alikuwepo,
ila alijificha humo humo ndani, kutokana na kuchanganyikiwa kwao,wakahamaki na
kuanza msako,...
‘Nendeni kijijini huyu jamaa atajifanya yeye ni kiongozi wa
kijiji, kwahiyo mkamateni,hata huyo kiongozi wa kijiji, ili wasije
wakatuchanganya...’akatoa amri huyo askari wa zamu.
`Ndivyo ilivyotokea, na tulipofika hapo kituoni, tulimuona
huyo mshitakiwa akiwa kajikunyata chooni, kama sio yeye...’ alipofika hapo wote
wakacheka.
’Mpendwa mwanamama, nilikuwa na jambo nataka kukuomba,
nataka unielewe naliongea hilo kwa nia njema kabisa, na usinipinge, kwa vile
utafikiria kuwa nimejitoa mhanga, hapana, nimeliwazia hilo na ninaona ndio
sahihi, nakuomba sana safari hii tusipingane,....kama nilivyo wakili wako na
mshauri wako mkuu, naomba ulikubali hilo...’akasema mwanadada.
‘Kuna nini unataka kuniambia, wewe niambie tu, maana kweli
wewe ndiye mshauri wangu mkuu, na kila unalonishauri linakuwa la msingi, na
sizani kwamba utanishauri jambo lisilo na maana, ...mimi nitakukublia tu, ...’akasema
mwanamama na mwanadada akatabasmu na kuanza kuongea...
‘Nilikuwa nakuomba hivi.....’
Na mara sauti ya watu kuitwa mahakamni ikasikika na wote
wakakimbilia ndani, kusikia ni nini kitaendelea...
‘Oh, tutaongea baadaye...’akasema mwanadada huku akikimbilia
ndani
NB: Natumai seehmu ya mwisho wa kisa hiki itahitimisha kila
kitu, je mwaansheria atapona, na akipona atachukua hautau gani, kumuoa
mwanadada au mwanamama.Je mshitakiwa atahukumiwa vipi,
WAZO LA LEO:
Hutakuwa na imani ya kweli ya upendo wa dhati kama hautakuwa radhi kumpa
mwenzako kile unachokipenda kwa nia safi na kwa wema . Mpende jirani yako,
saidianeni kwa shida na raha, kwa kufanya hivyo amani ya kweli itapatikana.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment