Baada ya maelezo hayo
mtaalamu akatulia akisubiria maswali kutoka kwa mwanadada, na mwanadada naye akawa
katulia akisubiria kibali kutoka kwa hakimu. Hakimu alikuwa akiandika jambo, na
alipomaliza akamwangalia wakili mtetezi, kama ana jambo lolote, lakini wakili
upande wa utetezi, alikuwa katulia, kama vile hayupo.
Tuendelee na kisa chetu,
‘Wakili mwanadada unaweza kuendelea…’akasema hakimu
Mwanadada alimsogelea mtaalamu na wakawa wanaangaliana,
kabla hajaanza kumuuliza maswali, na yule jamaa alihakikisha haangilii pembeni
akamkazia macho mwanadada, na huku akiwa anabenua mdomo kwa dharau, na
mwanadada aliangaliana na mtu huyo kwa muda, kabla hajageuka kumwangalia hakimu
na kusema;
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, hawa ndio watu wanatumia tamaa
zao binafsi na kutafuta visingizio vya kuhalalisha matakwa yao binafsi, hawa
ndio wanaotumia majukwaa ya kisiasa, kuwarubuni watu, ili watu wafanya maasi,
na baadaye wao waweze kufanya mambo yao, kwa masilahi yao binafsi…’akatulia
mwanadada na kugeuke kidogo kumwangalia mtaalamu, na mataalamu akawa
anatabasamu.
‘Hawa ndio wale anaotumia maeneo ya dini, na kutafuta vipengele
vichache wakachanganya na mambo yao na kuwahadaa waumini wao, ambao huenda sio
wajuvi sana wa dini, na kutapakaza sumu za matakwa yao, wakiwa na malengo yao
ya siri, kwa manufaa yao binafsi….ndio hawa, na ndio hawa hawa wanaotumia
ukabila, mila na desturi, kwa kuzipotosha, huku wakitafuta wafuasi, kwa manufaa
yao binafsi….na mila na desturi zinaonekana ni mbaya kumbe ni kutokana na watu
kama hawa.’akatulia na kumwangalia hakimu.
‘Muheshimiwa hakimu, mimi sioni kwa nini eti mtu utafute
jambo jema kwa kutumia njia ya ubaya siyokubalika kisheria…haiji akilini,kama ni jambo jema,
basi kuna utaratibu wake, ambao ukiufuta utaweza kuliwezesha hilo jambo liwepo ,
sio kwa kuwarubuni watu, na kuleta maasi, sio kwa kupoteza roho za watu wasio
na hatia, eti wanakuwa vikwazo kwako, hilo haliingi akilini, na huo ni ushetani….’akasema
mwanadada.
‘Kama ni kweli, mwenzetu huyo aliona hayo, kuwa aridhi ina
madini, ardhi ina mali asili, ambayo kwa mtizamo wake, itakuja kuchukuliwa na
wageni, alikuwa na njia nyingi halali za kufuata,….kuna taratibu zipo,
kisheria, na angeliweza kufanikiwa hilo bila kutumia `ubaya’…usihalalishe ubaya
wako, eti kwa vile una malengo mzuri baadaye…haiwezekani….fuata sheria, fuata
utaratibu, tuneglikuelewa..kama kweli unayodai ni sahihi’akasema mwanadada.
‘Ya Marekani na nchi za Ulaya tuwaachie wao wenyewe,
tusijfananishe na wao, kwani wao wana uwezo wao, na wanajua ni nini
wanachokifanya na wana sheria zao, na kwani kama kweli tuna malengo mema,
kwanini tusijifananishe na wao kwa mambo mazuri wanayoyafanya, tukawa wazalishajisihaji
wazuri, wasomi wazuri, tukaweza hata kwenda mwezini..’akagauka kumwangalai
mtaalamu.
‘Ndugu Mtaalamu, uliyofanya sio sahihi, na uliyowafanyia
watu sio mambo mema, unahitajika kutubu, kuwaomba msamaha, na msamaha
hautakubalika, kama hutatubu dhmabi zako, utasema ukweli kwa jinsi ulivyo
fanya…ili kweli watu wajue kuwa wewe ulikuwa na malengo mema, lakini ulitumia
taratibu ambazo wewe ulizania ni sahihi kumbe ni makosa…’akasema mwanadada. Na
akawageukiwa watu na kusema;
‘Huweze kuumiza raia wasio na hatia…kwa ajili ya kufanikisha
malengo ya ndoto zako ambazo hazikubaliki, …hilo umekosea sana, na watu kama
nyie mkiachiwa kwenye jamii, mnaweza kuwa ni kero…kero kubwa sana,amani
itatoweka, angalieni wenzetu wanavyoishi kwa shida, wanakuwa wakimbizi,
wanatangatanga, watoto wanapoteza maisha, ...jamani hatujifunzi kutokwa kwa
wenzetu, mnaua wazee kwa kisingizio cha uchawi, kumbe ni watu kama nyie,
mnawapotosha watu...hiyo sio halali...’akatulia, na baadaye akamgeukia huyo
jamaa.
‘Nchi ikiwa haikalili, amanai ikatoweka, uchumi utaporomoka,
....hali zitakuwa duni, na mpaka make sawa, mje mrejeshe uchumi wenu, wengi
watakuwa wamepoteza maisha, ...na huenda msiweze kabisa kuurejesha uchumi wenu
kuwa kama ilivyokuwa awali...wengi watabakia na mafundo moyoni, visasi...hakuna
faida, ...tuache hayo, tutubu, na tuwe na mtizamo chanya..’akasema mwanadada na
kumwangalia mtaalamu, huku akisema;
‘Ili tukuelewe vyema kuwa kweli ulikuwa na malengo mema, kwa
mtizamo wako...’akatulia halafu akageuka kuwaangalia watu , halafu akamgeukia
tena huyo jamaa na kusema;
‘Kama unavyodai wewe kuwa, ulikuwa na nia njema, ....kwa
jinsi ulivyokuwa ukifikiria wewe...kumbe sio sahihi, na sasa umeshafahamu
ukweli,... ninataka ujibu maswali yangu haya kwa uwazi, na kwa kujiamini, kama
kweli hayo uliyokuwa ukiyafanya uliona ni sahihi kwa kipindi hicho…’akasema
mwanadada akawa kamkodolea macho huyo jamaa na yule jamaa akatabasamu huku
akiwa na yeye kamtizama mwanadada, na huku akitikisa kichwa kama kukubali na huku
akiendelea kutabasamu, na kujifanya hana wasiwasi na hayo maswali akasema;
‘Uliza nitakujibu, …utakavyo..hamna shida, kwani sioni tofauti….uliza
nakusikiliza muheshimiwa wakili
mwanadada….’akasema na maneno hayo ya mwisho akayatamka kwa taratibu, kama
ana yakariri.
‘Je wewe ndiye uliyekwenda hospitalini na kumuua Jemedari
kwa sumu?’ akaulizwa na swali hilo lilikuwa kama la kushitukizia kwake, akawa
kama kashituka, halafu akatabasamu na kusema;
‘Mimi nilishasema
mengi niliyoyafanya nilikuwa nafanya kwa nia njema …kuhakikisha kuwa
mali asili, viasili na rasilimali ya nchi vinabakia mikononi mwa wanachi,
lakini watu kama Jemedari walikuwa ni kikwazo,hawajui,… siwezi kuwalaumu…elimu
na uoni wa mbal ulikuwa shida kwao, lakini je hapo ningelifanya nini, kwa mtu
kama huyo,…’akamwangalia mwanadada.
‘Wewe unamfahamu vyema Jemedari, ni wale watu wanaojifanya
wanajua sana sheria na wanataka kuzifuata kama zilivyo,…wewe, hata hawa
unawaita muheshimiwa hakimu, mnajifanya mnafhafuati kila kitu, kama
kilivyo…..wakati mwingine unafumba macho,…sasa nikuambie uuata
sheria….mnajidanganya…lakini siwalaumu….’akatulia kitikisha kichwa.
‘Sasa kwa, mtu kama Jemedari, ilibidi afanyiwe hivyo, kwasababu alijifanya
mfuata sheria, na hakujua kuwa sheria zipo, na hata hawo watungaji wenyewe wa
hizo zinazoitwa sheria hawazifuati kihivyo…nawafahamu sana mambo yenu, lakini
kwa vile mumeshika mpini, sasa hivi siwezi kusema kitu….’akawa anamuonyeshea
hakimu kidole.
Wakili mwanadada akataka kumsimamisha ajibu swali, lakini
kabla hajamwambia kitu , jamaa huyo akaendelea kuongea;
‘Usiwe na wasiwasi, subiri nikujibu, usiogope, mimi ndiye
ninayekujibu,….na nitawajibika mimi, usimuogope muheshimiwa, niliwahi kukutana
waheshimiwa zaidi yake…aah, ok….’akasema na kuonyesha mkono kama kudharau.
‘Nikuambie ukweli, wale waliopewa majukumu hayo ya kusimamia
hizo mnazoziita sheria,….ili eti wajahakikisha sheria zinafuatwa, , ndio hao
hao wa kwanza kuzivunja…japokuwa unasema
nisiyataje hayo mataifa makubwa,…lakini ndio mfano halisi,…ni nini
wanachokifanya,angalieni kwa makini, demokrasia wanayoitaka itumiwe, je kweli
wanaifuata kama inavyotakiwa..kwao wao sawa, lakini kwa wengine…sivyo hivyo,
….wao ni kwa jinsi watakavyo wao iwe, sio wananchi wa nchihusika watakavyo,
kama wao hawataki iwe hivyo…umenielewa…?’ akawa kama anauliza
‘Angaieni mifano hai,
mnaona wenyewe yanayotokea kila kukicha…sio bahati mbaya wenzetu walitumai akili, ….wanajua nyie bado
mumelala,…manachonganishwa mnagombana, na mkigombana kwao ni sawa na mlevi,
akishalewa, siumnasukuma tu…..hamjui kabisa, …lakini hawanidanganyi mimi kwasababu
nimesoma nafahamu hayo…’akasema na kutulia kidogo.
‘Kwahiyo ukisema sheria, …bado zipo na zitaendelea kuvunjwa,
kama watendaji na wasimamizi wenyewe wnaongoza kwa kuzivunja …..viongozi wetu
wenyewe sio waadilifu,..kama ni waadilifu hebu chunguza mishahara yao, na mali
walizo nazo,….wamazipatia wapi, kama sio sio kuvunja sheria…mtaendelea kulala,
wenzenu wananeemeka…’akatulia.
‘Kama kweli watendaji na wasimamizi wa hizo sheria,
wangelikuwa wakizifuata vyema wakawa waadilifu, na kuhakikisha kuwa kila mtu
anawajibika kwa kosa lake kwa haki,mimi nisingelikuwa hapa, mimi ningelikuwa
mtu mwingine, kabisa, muheshimiwa au afande,…lakini nikatendewa ubaya, na
sheria zikapindishwa kwa vile mimi sio mtoto wa mtu fulani……unafahamu sana…kama
hufahamu ndio hivyo….’akatulia na kabla mwanadada hajasema neno yeye akadakia
na kusema kwa haraka;
‘Yaliyonipata huko, ndiyo yaliyonisukuma niwe hivi nilivyo….wamenikomaza
wenyewe, waache niwafundishe, na nijitolee kwa ajili ya nchi yangu na vizazi
vijavyo, najua leo nyie hamtanielewa, alkini vizazi vijavyo vitanishukuru
sana….watanikumbuka, …’akatulia huku akitikisa kichwa.
‘Hujajibu swali langu….naona umegaukwa mwanasiasa, ungeenda
ukajiunga na vyama vya kisiasa, ungeliweza kufanya hayo kwa urahisi zaidi,
lakini sio kwa njia hiyo, sasa nataka ujibu swali langi, je wewe ndiye
uliyemuua Jemedari, kwa sumu?’ akaulizwa
‘Jibu unalo tayari..hiyo ni kazi yako kuthibitisha…., kama
mliweza kuingia ndani ya lile handaki na kuingia kwenye chumba changu cha
maabara, mumeona kila kitu, na jinsi gani nilivyofanya, yote yapo kwenye mikanda
mliyoiona humo ndani sikuficha kitu, …siwezi kujibu hilo swali, kuwa ni mimi au
sio mimi…hiyo ni kazi yako kuwathibitishia watu wako, mimi nimeshajielezea
lengo langu lilikuwa ni nini.’akasema
‘Wewe ndio uliyetengeneza hizo sumu, je ilikuwaje yule uliyemtuma
akawa hana soda yenye sumu kama mlivyopanga…na ukaja kuipeleka wewe…?’ akauliza
na mtaalamu akacheka
‘Kila jambo lilipangwa kitaalamu, sikuwa na haja ya
kuwaingiza watu wengine kwenye mambo yangu, japokuwa nlitaka jamii ione
hivyo,…ile sumu, ilitengenezwa, lakini hakiuwa sumu,niliwaelekeza lakini
nilijua haiwezi kuleta madhara,…na nilijua kuwa kuna watu waliiga, lakini
hawakujua jinsi ya kuichanganya…..’akatulia.
‘Ina maana ni kweli kuwa hiyo sumu iliyopelekwa ilipelekwa
na kiongozi wa kijiji?’ akauliza
‘Hilo utajijibu mwenyewe, maana mimi nilikuwa sehemu zote,
kiongozi wa kijiji, na mtaalamu, siwezi kukutafunia kila kitu….nyie watu
vipi,akili zenu ni butu ehe….’akashika kichwa kuashiria kutokuelewa.
‘Nilichotaka ni mtu aingie kule na ajulikane kuwa yeye ndiye
kamuwekea hiyo sumu, ili na mimi nije baadaye kufanya mambo yangu, na ndivyo
ilivyokuwa,…..yeye alimpa ile soda, lakini haikuwa na nguvu, na mimi nikaingia
nikaweka chupa iliyokuwa na soda yenye sumu,…na siku za mjamaa zilishafika,
akainywa…’akakunja uso kuashiria kuhuzunika.
‘Ilivyokuwa ni kwamba nilipoingia nilimkuta jemedari
kapitiwa na usingizi, mimi nikaiweka ile chupa ya soda pale mezani, nilijua,
kwa ujuvyi wa kiakili za kibinaadamu, jemedari ataamuka a kuinywa hiyo soda, na
ndivyo ilivyokuwa. Jemedari, alizindukana kutoka usingizi, akaona chupa ipo
pale akajua ni soda kaletewa, akaichukua na kunywa,….hakujua kuwa hiyo ndio ilikwa
tiketi ya kifo chake alichokuwa akikitaka,..na ndiyo ilikuwa njia ya kusafisha
vikwazo, katika kutimiza yale niliyokusudia….yenye malengo mema kabisa kwa wenyewe kuelewa…’akatulia.
‘Mtu kama Jemedari angeliendelea kuwepo nisingeliweza
kuulinda ardhi ya wazawa, maana yeye ndiye aliyepewa dhamana ya ulinzi wa
kijiji, jemedari alikuwa kiongozi wa mali ya kijiji , na alijifanya kufuata
sheria, ….hata pale nilipojaribu kumuelezea dhamira ya waheshimiwa wetu wa
kuuza ardhi zetu kwa wakuja, hakunielewa,…..kwanini nisimuondoe kwa sasa, ili
ardhi isje ikachukuliwa na wakuja baadaye….hapo nina kosa gani..’akasema
akitikisa kichwa kwa kutamba.
Mwanadada akamwangalia muheshimiwa hakimu,na kutabasamu,
halafu akamgeukia mtaalamu na kumuuliza swalii jingine;
‘Na wale vijana waliohusika kuchoma moto kwa mama mkunga
kwanini uliwaua?’ akaulizwa
‘Hao vijana walishanigundua …..kuna jambo lilitokea,
wakanigundua kuwa mimi ni mtu wa sura mbili, na nilijua kuwa itafika muda
watatoa siri,…kwa wengi wanafahamu kuwa walikufa kwa vile walichanganyikiwa kwa
kumchomea mama mkunga nyumba……haikuwa hivyo…ilikuwa kwasaabbu nilijua itafka
muda wataongea ukweli kunihusu mimi…nikawaondoa kwa sumu maalumu, ambayo
mumeikuta kwenye maabara yangu….umesikia sana, nawaambia ukweli ili mnitie
kitanzi mapema, sijali, kwani nimetimiza wajibu wangu.’akasema huku akikunja
uso kwa hasira.
‘Lakini kuna mmoja aliokoka, kwanini?’ akauliza mwanadada.
‘Huyu aliyeokoka, aliokoka kwa vile hakunijua mim, na
hakuwepo siku hiyo, na nikatumia mbinu ya kumwambia babu yake, kuwa amkanye
kijana wake, asije akanywa hiyo dawa, na kweli huyo kijana alipofika siku hiyo
akasingizia kuwa amefunga, na nikamwambia atakunya akifika nyumbani jioni…na ukumbuke
muda huo nilikuwa kama kiongozi wa kijiji,hakunitambua,….’akatulia.
‘Unaona sikuwa na lengo baya kwa mtu ambaye hana lengo baya
kwangu..ni wale ambao nilifahamu kuwa watakuwa ni kikwazo, kwangu…..ndio
niliowaondoa, au kutumia njia ya wao kuondolewa, sio lazima nifanye mimi…kwanini
niwaumize wale wasio husika, hapana mimi sio mbaay kihivyo….’akasema.
‘Ukiangalia wengi watanilamu sana kuhusu mama mkunga, ni
kweli inasikitisha sana, mama kama huyo kufanyiwa aliyofanyiwa,lakini kulikuwa
hakuna njia nyingine…..na yeye kama angeendelea kuwepo, ingekuwa vigumu kwangu
kuipata ile sehemu…nasikitika kuwa hilo halikufanikiwa, na ….na ina maana eneo
hilo sasa litakuwa mali ya wakuja…wenyewe mtakuja kuona, ….’aakgeuka
kumwangalia hakimu.
‘Muheshimiwa ahkimu, haya ninayoongea nataka yaandikwe, ili
mje kuwa mashahidi,….watakuwa hawo wanaoitwa wawekezaji, watapewa hilo eneo, na
mali asili yote itakwenda nje…..kazi yangu yote niliyoifanya inakuwa kazi bure…sawa
..lakini mimi nimejaribu kadri ya uwezi wangu….mtaona itakavyokuwa….’akasema.
‘Je hawo mabinti
ulikuwa ukiwachukua kwa kazi gani…?’ akaulizwa.
‘Mabinti?!..’akauliza kwa mshangao, halafu baadaye akawa
kama kaumbuka jambo, na kusema
‘Hahaha, unamaanisha, binti wa mkuu wa kitengo cha
upelelezi, nilimchukua, kwasababu ile ile, kuwa nilisingiziwa kuwa nimembaka
binti wa mkuu wangu, kwanini nisifnaye hilo kiukweli ili nije kuhukumiwa
kiukweli..hata hivyo, mabinti niliowachukua kabla, niliwachukuwa kwa ajili ya
uchunguzi wangu ….kama ningepata muda mngekuja kuona baadaye hilo nilichokuwa
nikikifanyia utafiti…’akasema huku akiangalai chini.
‘Tatizo ni kuwa nyie mnatafuta umaarufu, ndio maana
mumenikatili, lengo langu muhimu sana, ..nakumbuka umesema kuwa kwanini
tusiwaige wazungu, kwa utaalamu wao..hiyo ni hoja nzuri sana, lakini unaitamka
kinadharia, mimi naitenda, ...’akatikisa kichwa kama kukubali.
‘Mimi siifanyi kinadharia, kama nyie ndilo maana nilikuwa na
maabara, nilikuwa nalifanyia kazi hilo…..lakini sikupata muda,….kwahiyo hilo
halikuweza kukamilika kwasababu yenu, lakini sivyo kama mnavyojua nyie, kuwa
labda nilikuwa nimefanay hivyo kwa tamaa zangu, au kwa ubinafsi wangu. Hakuna kitu
kama hicho kwangu, tatizo ni kuwa hamnielewi…mimi sio hivyo mnavyofikiria nyie,
kwa akili zenu ndogo,...’akawa anaonyesha kichwani kwa kidole.
‘Ama kwa, huyu binti wa mkuu, ilibidi afanyiwe hivyo, kwa
kulipiza yale mabaya niliyobambikiwa, yeye mwenyewe alikuwa huko, kabla ya
kuhamishiwa hapo, anayafahamu hayo yaliyotokea huko, lakini hakusiaidia kitu,
kama anakumbuka vyema, atanikumbuka ...anayway, hayo ni mambo ya siri,
hamstahiki kuyafahamu…..ni hivyo tu.’akatulia na mwanadada akamwangalia kwa
jicho lililojaa hasira.
‘Hayo unayoongea ni kwa ajili ya kujitetea, kamwe huwezi
kufanya ubaya eti kwa ajili ya wema,hilo halipo, ubaya huzaa ubaya...labda kama
utafanya ubaya, kwa minajili ya kutetea haki, kwa minajili iliyokubalika
kisheria...lakini hayo yako hayakubaliki
kisheria, ....unachofanya sasa ni yale ya mfa maji unajitetea kwa vile
umegundulikana ubaya wako,…wewe utadirikije kumteke binti mdogo kama huyo, na
kumdhalilisha,hukuona kuwa yule ni sawa na binti yako, hivi kweli kama angelikuwa
ni binti yako kafanyiwa hivyo, ungelifurahia?’akauliza mwanadada kwa hasira.
‘Usijifanya unajali, kwanini hawakunijali mimi, hata mimi
nilikuwa mtoto wa mkulima, tena masikini wa kutupwa...je wazazi wangu hawana
uchungu kama huo, unaounadi wewe,.., hawakujali hilo, kuwa wazazi wangu
walikuwa wakinitegemea mimi angalau na wao wapate kakibanda, ukumbuke waliuza
kila kitu chao ili nisome,…je baada ya hapo ulitaarajia nini,.... msiangalia
kwenu tu, angalieni na kwetu ,walalahoi…..sijitetei kwa kuwa mnanona nimekosa,
mimi sijafanya kosa....tatizo lenu ni kuwa hamnielewi tu....’akasema huku
akiwaangalia watu.
‘Kama ni tamaa za kimwili, kwanini nisingelitumia pesa na
kuwachukua wasichana wanaojiuza, wapo wengi, tena wazuri tu, ni kazi rahisi,….lakini
sikuwa na kusudio hilo…..kwa hawo mabinti wengine, nilikuwa nawafanyia utafiti,
ambao mwisho wa siku ningegundua kitu, dawa, ambayo ingekuja kuwasaidia wao
wenyewe...lakini ooh, watu nyie, mumenikatili...na uchunguzi wangu huo
haukuweza kukamilika, kama mnahitajia kuufahamu
ni utafiti gani, basi nipeni mwaka mmoja, mtaona ni kitu gani nilikuwa
nakitafuta..kwasasa siwezi kuwaambia ni kitu gani….’akasema.
‘Na kuhusu eneo la mwanamama,….’akauliza na kabla hajamaliza
mtaalamu akadakia na kusema;
‘Mwanamama, hakuwa tatizo sana kwangu, tatizo kwangu ilikuwa
ni jemedari, na kwahiyo nilichofanya ni kuwachonganisha tu, ndio dunia ilivyo
sasa, ukiwa na akili, utawachezea watu upendavyo…..nilichofanya ni kupiliza
fitina kidogo tu, kuwa wakina mama
hawastahili kumiliki ardhi, hiyo haikuwa kazi kubwa, wengi wanafahamu hivyo,
siunajua tena mfumo dume….’ Akawa baadhi
ya hayo maneno anaongea kama ananong’ona.
‘Hiyo fitina ikafanya kazi yake, na Jemedari bila kujua,
akanisaidia kukamilisha hilo, japokuwa nilikuja kugundua kuwa wewe ni kikwazo,
ndio maana nikamtafuta mtu akumazlie, na kama ningedhamiria kukumaliza,
ningelifanyahivyo mapema, lakini kwanza nilitaka ujue unapambana na mtu gani….hilo
la kugongwa na gari, ilikuwa kama kukutisha tu,..bahati yako…lakini sikupenda
wewe ufe….nilitaka uje upambane na mimi.....’akasema huku akitabasamu.
Mwanadada aliposikia hayo maneno, akamwangalia huyo mtu, na
baadaye akamgeukia hakimu na kusema;
‘Muheshimiwa hakimu, huyu mtu hayupo sawa…kwa kumsaidia
naomba akachunguzwe akili yake vyema, nahisi kuna tatizo,….’akasema mwanadada
na Mtaalamu akacheka, alicheka kwa muda, halafu akasema;
‘Hivi mimi na nyie ni nani anahitajika kuchunguzwa akili,
….mimi sina matatizo ya akili, ….hilo eleweni , ila naitumia akili yangu
ipasavyo, nyie, hamtaki kuzitumia akili zenu vyema, na kama mngelizitumia akili
zenu vyema, mngelinielewa…nyie ndio mnastahili kuchunguzwa akili zenu...sio
mimi’akasema huku akitiksia kichwa kwa kujiamini.
‘Kwa kauli yako hiyo, naona umesihiwa maswali, tumuachie
muheshimiwa hakimu afanye vitu vyake, nafahamu atafanya nini…..na sitajutia kwa
hayo niliyoyafanya,….kamwe, ….sijutii, kwasababu niliyafanya hayo kwa maslahi
ya nchi na vizazi vijavyo….eleweni hivyo,....nashukuruni sana, …’akasema an
kuinama kidogo halafu akashika mashavu na kuwa kama mkiwa, au mtu anayesubiria jambo na baadaye akaiondoa na kutabasamu....huku akiwa kashika shavu moja, hakuonyesha wasiwasi..
Hakimu alimwangalia kwa muda, na baadaye akawaita mawakili wote
wawili wa utetezi na huyo muendesha amshitaka, akawa anateta nao na baadaye
akasema;
‘Tunaiahirisha hi kesi, na siku ya hukumu itatajwa,
mtafahamishwa….na mshitakiwa ataendelea kuwa rumande, …kwa ulinzi mkali....’akasema
na kuinuka kwa haraka, ilionekana hakimu alikuwa kakerwa sana na kauli ya huyo
jamaa , lakini hakutaka kusema zaidi alimtupia jicho mara moja na kuondoka zake.
Wakili mwanadada akamgeukia mtaalamu ambaye alikuwa
akipitishwa kupelekwa rumande huku akilazimisha kusimama , na huku akigeuka
kumwangalia mwanadada, lakini wale askari wakawa wakamsukuma atembee...
Wakili mwanadada alipoona hivyo akataka kujua ni kwanini jamaa
huyo anavutana na wale askari, je kuna kitu anataka kumwambia, akawageukia wale
askari na kuwaambia wamuacha aongee anachotaka kuongea, na huyo jamaa
alipoachiwa akawa kama anajipuliza kuondoa uchafu, kwa dharau, na kugeuka kumwanglia mwanadada, wakawa sasa
wanatizamana uso kwa uso, na huyo jamaa , kwanza huyo jamaa akatabasamu, tabasamu
lake la dharau, halafu akasema sauti;
‘Hongera binti Kibaraka, msaliti….hongera sana, maana watakuvisha
nishani ya ushujaa, lakini haina maana yoyote kwako wala vizazi vijavyo….hiyo nishani ya kukukoga kwa
ujinga wako….’akawa kama anatema mate chini kwa kashifa.
‘Wewe na hawa wanaojifanya ni askari, nyote ni vibaraka,
wasaliti, wajinga, wasio taka kutumia akili zao vyema, wakaona mbali...wasiojua
ni nini wanachokifanya, wanaigiza kama mbwa anayetumwa na bwana wake,….kamata
huyo..kimbia, kule…hana lolote analopata, zaidi ya kutumikishwa, lakini
akizarauliwa kama mnyama tu,….mmh, nawasikitikia sana….’akawa anatikisha
kichwa.
‘Unasikia sana wewe binti, mimi mbele ya mungu, nitakuaj
kuvishwa nishani iliyotukuka, ….japokuwa machoni mwenu, mnaniona ni mtu mbaya
sana, lakini sivyo hivyo kamwe….kwa yule anayefahamu lengo langu atanishukuru,
na hao nio vizazi vijavyo, sio nyie….nyie mnachojali ni masilahi, a sifa ndogo
tu, hamna lolote…lakini mwisho wa siku wanakuja kufaidi wengine, wenye vichwa
kama changu….wajanja, wataalamu…’akawa anajitahidi kushika kichwa lakini yule
mlinzi akawa kamshikili barabara.
‘Niachie wewe, siwezi kufanya lolote, ninachotaka ni
kumpasha huyu kibaraka mwenzenu,…na nawaambia iliyo wazi, nyie viabara, ole
wenu iwakute hiyo siku, siku ambayo wenye mali hizi, watawashitukia,….ole ,
wenu,…na kama na mimi nipo hai, ole wenu nipata muda nitoke jela, nikiwa hai,..’akakunja
uso kwa hasira.
‘Ole wenu nitoke jela nikiwa na nguvu zangu, wewe na huyo
unayemuita muheshimiwa hakimum na nyote mlioshirikiana, nitahakikisha nawafanyia
jambo ambalo hamtalisahau, kitu mbaya….mtaona…ole wenu….maana mumenikatili kuilinda
mali asili ya vizazi viajavyo…’ akageuka kuwaangalia hawo maaskari, na baadaye
akamgeukiwa mwanadada na kusema;
‘Nyie hamjui tu, mtakuja kujau ikiwa `too late’ muda huo, yamebakia mashimo yasiyo na kitu,..ardhi isiyo ardhi tena, maana ardhi ikiwa na madini,
ikiwa na rutuba thamani yake hupanda, sasa wajanja wameshachukua kila kitu,
thamani yake itakuwa haipo tena , sana sana, itakuwa ni ardhi kwa ajili ya
kukuzikieni tu wasaliti nyie, mtakuwa mizigo isiyo na thamani….’akawa kama anathema
mate.
‘Sawa hamna shida, nifungeni TU…..wema wangu hauna maana
kwenu….lakini hautaoza kamwe, utakuja kukumbukwa kwa wenye akili, kama zangu….’akasema
huku akitoa macho ya hasira na huzuni.
‘Wewe una matatizo, haupo sawa….mpelekeni huko, akasubiri
hukumu yake’akasema mwanadada
‘Hahaha…mtabakia hivyo hivyo….usisahau maneno yangu,…muombe
mungu waninyonge….lakani hata wakininyonga, maneno yangu yapo, lengp langu
jema, liatendelea kukumbukwa, na kifo change kitakuwa cha kishujaa…..hilo
halipingiki…’akasema na huku akisukumwa kuondoka.
NB: Ni hayo kwa leo
WAZO LA LEO:
Tunapokuwa kwenye jamii, tukawa na mawazo, ambayo tunahisi yanaweza kuisadia
jamii, ni vyema tukawahusisha wanajamii, tukayajadili kwa pamoja, kwani huenda
yakawa na manufaa, a huenda kwa mtizamo wako uliona yana manufaa, na wakikutana
watu wengi, yatachambuliwa na kukubaliwa au kukataliwa kwa manufaa ya uma, huo
ndio utaratibu mwema, kwani kwenye wengi hapaharabiki neno.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment