Mama aliendelea
kusimulia kisa hiki, akielezea pale walipokwenda hospipitali kumuona
mwanasheria wakiwa wameongozana na mwanadada, na wakiwa njiani , wote wlikuwa
kimiya, kila mmoja akiwa katingwa na mawazo yake, na kila mmoja akimuomba mola
wake, mwanasheria huyo apone, au wamkuta akiwa hai…..
Swali ni je,
mwanasheria huyu alikuwa akitaka kuwaambia nini wanawake hawa wawili, ukumbuke
kuwa mmoja ni aliyekuwa mchumba wake, na wa pili ni mke wa marehemu kaka yake
na yeye alitakwia kumrithi huyo mama kutokana na mila na desturi zao….
Sasa endelea na sehemu
hii uone ni nini kilitokea,
*******
Mwanasheria alifunua macho taratibu, na kuangalia mbele, na
pale macho yake yakakutana na mwanadada. Mwanadada alikuwa hakuziweka nywele
zake vyema, ahapo akatulia na kumwangalia kwa muda, akapitisha ulimi mdomono
kama anataka kuongea kitu, lakini hakuongea, na kama kakumbuka jambo, akageza
mboni za mcahp na kumwangalia mwanamama, hapo napo akatulia kwa muda,… halafu
akafumba macho., na michirizi miwili ya machozi ikaonekana kitoka machoni.
Ilipita muda kukiwa kimiya, na wakina mama hawa wawili,
waliona huenda mgonjwa hawezi kuamuka tena kwa wakati huo, na wakawa wanangaliana
kila mmoja akisita kuongea kila alichokuwa nacho moyoni, na ikafika muda mwanadada
akitaka kuongea, na alipoanza kupanua mdomo akitaka kuongea, akasitishwa na
sauti kutoka kwa huyo mgonjwa, ikisema;
‘Nashukuru mumefika, na sikutegemea kuwa leo ninaweza
kuamuka na kufungua huu mdomo,na nashangaa leo najiona nina nguvu, na … lakini
nafahamu huenda imetokea hivi ili niweze kuongea na nyie, maombi na dua yangu
huenda imetimizwa, kwani wanasema kila mmoja anapokaribia kufa, mola humpa
muda, ili aweze kujitetea kwa mara ya mwisho….’akatulia akawa kama anakohoa
kidogo.
‘Nahisi hivyo, kuwa mola kanipa muda huu, ili niweze hata
kutubu dhambi zangu, …ahaa…dhambi, kila mmoja ana dhambi zake nyingi tu,
….lakini la muhimu kwangu mimi juu yenu na ili niweze kutoa maagizo muhimu,
ambayo nafikiri ni muhimu kwangu kufanya hivyo, …ninachoshukuru ni kuwa nyie
mumefika kutii maagizo yangu….kwani naogopa hata kukutana na ndugu yangu tena,
kwani kila mara ananitokea na kunilaumu…..’akatulia na mwanadada akasogea
karibu, lakini mwanamama alisimama pale pale alipokuwa amesimama, mbali na kile
kitanda alicholala huyo mgonjwa.
Yule mgonjwa alifunua macho yale pale alipohisi mtu yupo
karibu naye, na akaayfunua kumwangalia huyo aliyekuja kukaa karibu yake, na
macho yake yakakutana nay a mwanadada ambaye alikuwa kakaa karibu naye, huku
akimwangalia kwa macho ya huzuni, yule mgonjwa akafumba macho yake huku
akisema;
‘Nakuomba na wewe mwanamama usogea karibu maana sauti yangu inaweza
ikawa ya shida kusikika, na nataka nyote msikie kile kitu nitakachowaambia….’akasema
na hapo mwanamama akasogea na kuja kusimama karibu, hakukaa karibu na kile kitanda
kama alivyofanya mwanadada, yeye alisimama pembeni huku akiwa kaweka mikono
yake kifuani, kama anaomba ….au kuogopa….
‘Naomba mnisikilize kwa makini, huenda …..sijui, lakini
dalili zote zipo, wanasema ukiwa katika hali kama hii, ya kukaribia kukataa
roho, huwa unajiona, na dalili mojawapo ni kujiona unakuwa karibu na
waliotangulia,…utajiona unawaota,
marehemu…., basi ujue safari imeshafika,…na mimi sioni kwanini isiwe hivyo,
maana nateseka kwa maumivu….na kila mara najiona nipo na ndugu zangu
waliotangulia….na hawaishi kunilamu…’akatulia.
‘Pindi tu, nilikuwa na marehemu, mume wako mwanamama, na
amekuwa akinilaumu kuwa nimeshindwa kutimiza ahadi zangu, nilzomuahidi kuwa
nitawatunza wewe na mtoto, kuwa sitawatelekeza na ya kuwa nitazilinda mali
zenu……lakini anasema sikufanya hivyo, na nimekuwa nikishirikiana na watu
wanaotaka kumdhulumu mke wake na mtoto wake…..nikashangaa sana…’akatulia.
‘Je ni kweli nimeyafanya hayo….sikusita kumwambia kuwa mbona
namejitahidi kutetea mali yake kama alivyoagiza, na ….cha ajabu aliniambia kuwa
mimi ni mnafiki, muoga, na uanasheria wangu hauna maana katika familia, na
sistahili kuwa kiongozi wa familia….’akatulia.
‘Ndugu yangu huyo aliongea mengi, na kudiriki kusema kuwa
nimeshindwa hata kutimiza lile agizo kuwa nimchukue shemeji awe mke wangu,….na
huku wakati alipokuwa duniani, nilikuwa najifanya nampenda, sasa kaondoka,
ninampa mgongo….shemeji nakiri kuwa kweli nilishawahi hata kumwambia kaka yangu
huyo kuwa nakupenda, lakini nilisema yale kama ….na nisingeliweza kuwa na
mawazo hayo kuwa kifa nikuchukue…..lakini ikatokea hivyo’akatulia.
‘Sasa nifanyeje…?’ akawa kama anauliza na kumwangalia
mwanadada.
‘Kaka yangu aliniambia sina la kufanya maana nimechelewa…..nimeshindwa
kutimiza ahad hadi maafa yametokea, kwahiyo sifai tena…..’akatulia.
‘Nikamwambia kama nimechelewa ni nani atakayeweza kuwalinda,
familia yake, na mtoto na ni nani atakayeweza kuzirejesha mali za mkewe na
mtoto?’ akakohoa kidogo
‘Aliniambia keshapatikana mtu wa namna hiyo, na kila kitu
kitarajea kwa mkewe na mtoto, haki ya mtu haipotei bure, lakini sio kwa kupitia
kwangu, mimi nimeshindwa huo mtihani, iliyobakai nirejee huko walipo nikasubiri
hukumu…na ndio maana nataka kutubu dhambi hizo za kushindwa kutimiza aahdi ay
ndugu yangu huyo….’akasema
‘Nikasema naomba muda mwingine ili niweze kuyafanya hayo,
yeye akasema hana mamlaka na hilo, kwani hata yeye aliwahi kuomba hivyo, lakini
hakuweza kupewa huo muda, mwenye mamlaka hayo ni yule yule aliyetupa roho, na
ndiye anayefahamu ni lini mja wake atareja
kwake, yeye hajui na wala hana uwezo wa kunitetea….’akatulia.
‘Basi ndugu yangu huyo akaniambia `karibu kwenye makazi ya
kudumu….lakini hakikisha umeongea na mke wangu na huyo ambaye ni mtetezi wa
haki, na kuwathibitshia kuwa hayo wanayotenda ni halali , na mafanikio yapo
mbele yao…hiyo ndio kauli ya marehemu kaka, na alisema nihakikishe nimewaambia
hivyo…’akatulia.
‘Lakini akasisitiza, kuwa kama nitapata muda, wa kurejea
basi nitimize hayo muhimu ambayo aliniagiza, lakini sio kwa kutetea mali kwani
yupo tayari mtetezi, …na nisimuangushe kwa hayo mengine, lakini yeye hana
uhakika kuwa mimi nitapata muda huo tena…’akatulia halafu akamwangalia mwanadada,
‘Kwasababu hiyo mimi inabidi nikushukuru sana mwanadada kwa
juhudi zako, nashukuru kuwa wewe umeweza kufanya yale ambayo mimi nilishindwa,
kwasababu ya kugubikwa na wimbi nzito la kifamilia,…sikujua kuwa nilikuwa
kwenye mtego, kumbe wenzangu walikuwa wakinitumia kwa maslahi yao binafsi..’akatulia.
‘Sikujua kuwa hata mtalaamu ambaye nilimwamini sana, na
nikawa ninamshauri na kumuelezea kila kitu, nikijua yeye ni ndugu na rafiki wa
kweli, ….lakini kumbe alikuwa ni adui namba moja wa familia yetu…’akatulia.
‘Niligundua hayo, hata kabla hatujafunga safari ya kwenda
huko msituni kwani katika moja ya mipango yake ya hivi karibuni, ilikuwa ni kuniua
mimi baada ya kugundua kuwa nimeshamfahamu …..kwani kuwepo kwangu kungemfanya
ashindwe kukamilisha mipango yake, ya kumiliki ardhi yote, ….na hayo
alishafanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwani ana hati zote za kumuliki eneo lote la
kwetu na la kwao….’akatulia
‘Je alipaatje hizo hati, ….nilishindwa kujua, ….nilishindwa
hata kumfahamu kuwa ni ndumila kuwili,…huwezi amini alivyokuwa akijibadilisha,
kumbe yote tuliyoona kuwa alikuwa akifanya kiongozi wa kijiji, kumbe ni yeye
aliyekuwa akifanya, kwa vile wanafanana na
mzee wetu huyo…na aliyafanya hayo kwa ujanja wa hali ya juu, lakini kila mkosaji hawezi kufuta nyayo zake zote,
…..’akatulia.
‘Nilikuja kumgundua pale mzee wetu huyu yupo mahabusu, …na
kukatokea matendo ambayo yalionyesha kuwa ni mzee wetu huyo ndiye aliyekuwa
akiyatend, nikawa najiulizaa iweje, ina maana kweli mzee wetu huyo ana nguvu za
giza kiasi hicho, aweza kutoka jela, na kwenda kuyafanya hayo na kureeja bila
ya walinzi kufahamu…sikuamini…nikataka kuhakikisha hilo’akatulia kidogo.
‘Siku moja, nikafuatilia, na jamaa yetu huyo alipofanya hayo
aliyotaka kuyafanya….ushaihid muhimu ni pikipiki, japokuwa alikuwa akibadili
mara kwa mara kwa kukodi pikipiki tofauti. Na siku moja nikaingiwa na wasiwasi
na pikipiki, iliyokuwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi huyo mtalaamu, nikataka
kujua huyo mtu ni nani…..pindi kidogo akatoka mtu, akiwa kashikilia mawani
makubwa, alipotoka alichelewa kuyavaa,...
Hutaamini , na sijui kwanini nilifanya hivyo, nilichukua simu yangu ambayo kwa muda huo ilikuwa mkononi na kumpiga picha, kwa haraka…. akachukua
pikipiki na kuondoka, na mimi nikamfuatilia kwa nyuma kwa pikipiki, nikamuona
akielekea msituni….nilijaribu kumfuatilia lakini sikuweza kwenda zaidi..siku
hiyo sikuweza kufahamu ni mtu gani huyo…’akatulia.
‘Ile picha nilipoiangalia vyema, nilimuona ni mzee wa kijiji, nikawa na wasiwasi na hapo hapo nikapiga simu kituo alichowekwa mzee wa kijiji, kuhakikisha kuwa kiongozi huyo yupo
huko jela, na maaskari wakaniambia yupo huko jela, nikawaomba niongee naye na wakawa wakanipa nikaongea naye….
‘Nimekuja kugundua haya, baada ya safari hiyo tuliyokwenda
sote huko msituni kuwa kumbe ni huyu jamaa alikuwa akituchezea,… na ukurudi
nyuma na kuanza kuunganisha haya matukio yalivyokuwa unaweza kugundua kuwa
kumbe ndio yeye…..’akatulia kidogo.
‘Yeye ndiye aliyesimamia kuchomwa moto kwa nyumba ya mama
mkunga, akiwa katika umbile la kiongozi wa kijiji, maana kweli siku hiyo
kiongozi wa kijiji alikuwa hayupo, na hayo mimi nilifanya uchunguzi na kugundua
kuwa kweli hakuwepo…ndio maana nikawa nyumba yake kumtetea…’akatulia.
‘Lakini ukimtetea yeye, ina maana unamweka ndugu yangu
marehemu,….nd dnio maana nikawa mnzito kumtetea huyu mzee, maana jinsi ilivyo
kaka yangu kama wanavyomuita jemedari angelikuwa kwenye hatia,…na ndivyo
ilivyojulikana, ….na hapo nikawa na kigugumiz, na kujiuliza kama sio huyo
kiongozi wa kijiji ni nani mwingine, …kwa haraka haraka kila mmoja alifahamu
kuwa ni kaka yangu, na hata mimi mwenyewe nilifahamu hivyo….’akatulia.
‘Huyu jamaa yetu alikuwa mjanja sana, kwani alijionyesha kaika
jamii, kuwa yeye haruhusiwi kuvua yale mangua yake ya kiganga, kuwa ni mwiko
kuyavua hata mahakamani mlimuona akiingia nayo, na yale manyoya na …jinsi
alivyo kuwa usingeliweza kuijua sura yake halisi…’akatulia.
‘Mimi nilipoanza kumuhisi vibaya, nilijikuta nikimchunguza
kwa karibu, kwanza baada ya kumsikia kuwa katoweka, nikawa namtafuta yupo
wapi…haikuwa kazi rahisi kumgundua wapi alipokwenda, kwani hali yake ya awali
ay kuvaa mavazi yale ilikuwa ndio chumba chake cha siri, na akijitoa kwenye
hali hiyo, huwezi kumgundua tena, na hapo huwa nasi na kuweza kugundu ni nini kinachoendelea…’akatulia.
‘Siku alipotoka mahakamani kutoa ushahidi mimi
nilimfuatilia, akijua kuwa hakuna anayemfahamu, alipotoka hapo, alikwenda moja
kwa moja kwenye jengo bovu, ambapo, alibadili yale mavazi yake, na kuwa mtu wa kawaida,
…alipoondoka mimi niliingia na kuyaona yale mavazi yake, yaklwa yamefichwa,…na
hapo nikagundua kuwa huyu mtu anajigeuza kwa njia hiyo,…kumbe, …..
‘Lakini wakati anatoka pale alikuwa kavaa mawani makubwa,
usingeliweza kumgundua kuwa ni yeye, ….na kwa vile nilikuwa nimepoteza muda,
kuingia pale alipoficha mavazi yake, sikuweza kumfuatilia tena huko
alipoelekea…lakini nikakumbuka tukio la nyuma la huyo mtu niliyemuona nyumbani
kwa mtaalamu, na nikagundua kuwa ni yule yule….japokuwa sikuwa na uhakika kisura,
maana nilimuona kwa mbali…’akatulia
‘Ila niligundua kitu,mwili wake, na viatu alivyokuwa
kavaa…ambavyo, tulipofika huko msituni, ndivyo alivyokuwa kavivaa siku
hiyo….alikuwa mjanja, kiasi kwamba, hakufanya makosa lakini kosa hio
akalifanya, …’akatulia.
‘Pamoja na yote ndugu huyu ni mpenda wanawake sana, hasa
wasichana vigoli….na mmoja wa wasichana aliokuwa akiwataka ni msichana wa mkuu
wa kituo cha upelelezi, na hapo niliweza kupata fununu…niliwahi kuongea na huyo
binti, kipindi cha nyuma, na japokuwa alikataa kunielezea, lakini kwa kupitia
kwa rafiki yake wa kiume, niligundua kwua msichana huyo alikuwa na mwanaume
anamzuzua…kwani rafiki yake huyo wa kiume, alikuwa kamuhisi na alikuwa
kilalamika…
‘Jamaa yetu huyu, alitumia kipaji alichopewa vibaya, kwani
kweli alikuwa na uwezo wa dawa, kweli alikuwa na uwezo wa kutengeneza mazingara
ya kumfanya mtu awe na mfadhaiko ambao ndio hayo tunayoyaita mashetani, na kila
binti aliyemtaka, alimbambikia mambo hayo, na huyo binti anajipeleka mwenyewe
kwa huyo jamaa bila kufahamu ni kitu gani anakifanya….’akatulia.
‘Kwahiyo huyo binti atakwenda hadi anapotaka huyo jamaa na
kujikuta kafanyiwa uzalilishaji, na ila hali ikimuisha,anakuwa hajitambui
ilikuwaje…na ni nani kamfanyia hivyo, na hukimbilia kusema kafanyiwa hivyo ni
jinni mahaba….’akatulia.
‘Niliposikia kuwa huyo binti ana mashetani na huwa
yakimpanda anaweza kupotea, mimi nikaingiwa na hamasa ya kutaka kujua huwa
anapotea kwenda wapi….na wakati nafanya hayo, sikuwa na mawazo ya kuwa jamaa
yetu huyo ndye anafanya hilo,na sikuwa nimelifanya hili kutokana na kesi yetu, …..hapana nilifanya hivyo kwa vile nilitaka
kugundua haya mambo yapoje,…ilikuwa kama sehemu ya kupoteza muda na kugundua
mambo yanayotokea hapa kijijini kwa njia yangu ya kipelelezi…..
‘Huyu binti keshapotea mara kadhaa, na mojawapo nilimgundua
akieleekea huko msituni…nilimfuatilia siku hiyo, na sijui nilikuja kupatwa na
kitu gani, kwani nilipofika eneo la msituni, nikajikuta nimedondoka na kupoteza
fahamu, nilipozindukana ilikuwa imepita nusu saa, na sikuona haja ya kuendelea
kufuatilia nilirudi nyumbani, nikijua kuwa nimeshindwa kuweza kumfuataili huyo
binti.
‘Sasa ..ukiunganisha haya yote, ….kupotea kwa huyo
binti,….kumuona huyo jamaa akijibadili, na kueleka msituni, nikaanza
kuunganisha haya matukio, …..lakini bado sikuwa nafahamu kuwa huyu jamaa ndiye
mtaalamu, …’akatulia.
‘Niligundua hilo siku ile alipokuja kutoa ushahidi..na
nikayapiga yale mavazi yake picha, …na nikawa na hamu ya kuongea na wewe
kukuelezea hicho nilichogundua, lakini wewe ukawa hutaki….na ilipotokea nafasi
hiyo ya kwenda huko msituni, nikaona sasa nakwenda kuhitimisha uchunguzi
wangu…’akatulia.
‘Kwahiyo kutokana na uchunguzi wangu, wote walioshikwa nyuma
hawana makosa, kama wana makosa ni yale yakutumiwa kiujanja na huyo jamaa, bila
ya wao kujua, ….nawaambia hili ili mkienda mahakamani muwe makini na huyu
mtu…pamoja na ujanja wake, pia anafahamu sheria, …muwe makini kwa hilo, lakini
pia muwe makini na watu ambao ni muhimu, anaweza kuwaua wote ili kupoteza
ushahidi…hasa kiongozi wa kijiji, mlindeni sana….’akatulia na akawa anahema kwa
shida.
Mwanadada akageuka kuangalia kile chombo cha kuonyesha
mapigo ya moyo, na akaona kama kinaanza kuonyesha ishara mbaya, akamwambia
mwanamama ;
‘Nenda kamuita docta haraka….’akasema lakini mwanasheria
akasema;
‘Wamesema kuwa wameshaidhibiti ile hali mbaya,, na
iliyobakia nikuuguza majereha….nashukuru kusikia hivyo, na najua kama dakitari
kazi yao ndio hiyo kumpa matumaini mgonjwa hata kama wanafahamu kuwa hatapona…
msihangaika, …kumuita docta.’akatulia.
‘Lakini hayo yote ni mapenzi ya mungu, ninachotaka kusema
hapa, ni kuwa kwanza pendaneni, kama ndugu,…kama nitaondoka, basi majukumu ya
kumtunza,….mtoto, majukumu ya kifamilia, nakuachia wewe, mwanadada, nafahamu
kuwa wewe hujawa familia yangu kwani hatujafunga ndoa, lakini wewe unaweza
kumsaidia zaidi kuliko ndugu yoyote,kwenye familia yangu, na familia yangu,
wote waliobakia ni wakorofi ….’akatulia
‘Kwanini nasema hivyo, ni kutokana na yaliyotokea, siwaamini
tena ndugu zangu,….sikujua kuwa kuna mambo kama hayo ndani ya familia yangu,kwangu
familia ilikuwa kila kitu,…hata hivyo siwezi kuwalaumu kwa hali iliyopo , maana
ndivyo maisha ya kijijini yalivyo, …na ndivyo alivyoweza kuwahadaa watu wengi
hapa kijijini huyu jamaa yetu ….ambaye wengi walimuamini sana.
‘Huyu jamaa alichukua muda kuwasoma watu, na akajua udhaifu
wao, na ndipo akatumia mbinu alizo nazo, kwanza kwa kuwajengea imani kuwa yeye
ni mtaalamu aliyetumwa kukilinda hicho kijiji, na hilo aliweza kulihalilisha
kirahisi kutokana na kipaji alichokuwa nacho, kuwatibia watu na kuwabashiria
mambo mengi, na aliweza kufahamu mengi yaliyokuwa yakitokea ndani ya
familia,….kumbe alikuwa kasambaza waya na vyombo vya kuansia sauti sehemu
nyingi, tu, kama mlivyoona ile antenna kule porini….’akatulia
‘Kila mtu alikuwa akishangaaa iweje mnaongea ndani, kesho
yake, jamaa huyu anakuja kukuambia ulichokuwa ukiongea wewe na mkeo….watu
wakafahamu huyu sio mtu wa kawaida, kweli ni mtalaamu….’akatulia kidogo
‘Ninafahamu kabisa sasa hana ujanja, na ili asiweze lolote,
hakikisheni yule jamaa tuliyekwenda naye msituni yupo….ili kama kuna hadaa za
kimazingara, muweze kumshinda,…..yule jamaa anamfahamu vyema huyu ndugu
yetu,….hilo ni kazi kwenu….’akatulia kwa muda kiasi kwamba wakimama hawa wawili
wakaingiwa na shaka, na mara huyo mgonjwa akasema;
‘Sasa basi kwanza kabisa, nimekuita mwanadada, ili
uhakikishe unafuatilia hati zote za nyumba, hati zote za duka, hati zote za
shamba, ambalo ni mali ya mwanadada, uhakikishe zinaandikwa kwa jina
lake….nimeshaongea na wakili wetu, ambaye ndiye alisaidiana na mimi kuweka
hivyo vitu vyote kwa jina langu, ila hilo shamba sikuwa na ufahamu nalo..lakini
kwa vile kila kitu kitawekwa wazi huko mahakamani, ni jukumu lako mwanadada
kuhakikisha vyote hivyo vinakuwa mikononi mwa mmiliki halali…
‘Nakuambia hivyo maana kila nikipitiwa na usingizi ndugu
yangu huyo hunijia huku akinilaumu kuwa kwanini sifanyi hivyo, kwanini
sikuambii ufuatilai hayo, ya hati miliki,…na naona ni kweli unahitajika
kuyafanya hayo kwa haraka iwezekanavyo, kwani yupo ndugu yangu mkorofi,
haelewei sheria, na ni mtu anayependa shari, sasa mtasumbuana naye sana kama
nitakufa…kabla mambo hayo hayajawekwa sawa….’akatulia
‘Kama nitapona...oh, mungu wangu sijui, ...ila kama nitapona, kitu ambacho sitegemei, basi tutasaidiana
kwa hilo….na dhamira yangu ya kweli ni kama nilivyokuambia mwanadada,kuwa kitu
cha kwanza ni kufunga ndoa mimi na wewe, na kuhusu mwanamama, wewe ndiye
utakayekuwa na maamuzi na hilo…wewe utaamua, kama …..kama ...oh, kama...’akawa anashindwa kumalizia, na kugeuza kichwa kumwangalia
mwanamama ambaye alikuwa mlangoni, akitaka kwenda kumuita docta.
Kukawa na ukimiya na mwanadada ambaye alikuwa kazama kwenye
mawazo, akageuka kumwangalia mawanasheria huyu, akamuona kafumba macho, na
hatikisiki, na alipoangalia kule kwenye mashine ya kuonyesha mapigo ya
moyo,akaona ile misitari ikianza kunyooka,…
‘Muite docta haraka….’akasema mwanadada na mwanamama akatoka
mbio akiita;
`Doctaaa…..
Mwanadada, akabakia akiwa kashika kichwa kama mtu
aliyechanganyikiwa, akiwa keshakata tamaa, ……
NB: Je ndio mwisho wa haya yote, tuwe pamoja kwenye
hitimisho la kisa hiki.
WAZO LA LEO: Haki
inapotolewa kwa ubaguzi, inapoteza thamani yake ya kuitwa haki, kwani haki ni
haki kwa kila mtu anayestahili kuipata. Kila mwenye dhamana na hili awe makini
katika kuigawa au kuisimamia haki, asijali, jinsia, dini au kabila,….ukianza
kuangalia hayo katika kuitoa haki, hiyo itakuwa sio haki tena, na huo utakuwa
mwanzo wa kuleta mfarakano na manung’uniko katika jamii, na lolote baya
likitokea, ujue wewe ndio chanzo, na hukumu ya mungu hutaweza kuikwepa.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment