Tulitoka nje ya lile
pango huku tukiwa tumekata tamaa ya kumpata huyu mtu tena,ikizingatia kuwa yeye
analifahamu hilo pango lilivyo, na sisi japokuwa tupo wengi, lakini njia za
kupita zilihitajia mtu mmoja mmoja,…
Bado tukiwa na
matumaini ya kumpata huyo mtu akiwa hai, tuliharakisha kutoka, ili kuungana na
wenzetu waliokuwa wakijibisha risasi na huyo jamaa, na baadaye kukawa kimiya,
ikiashiria kuwa huenda huyo mtu alishatoka nje,
Swali likawa je kama
huyo mtu kawahi kutoka nje, itakuwaje,
kwani hatukukumbuka kumuacha askari zaidi ya mwanasheria, wote tulikimbilia
kuingia ndani..na je hiyo amri ya kutokutumia risasi huko nje, itawezaje
kuepukika, na mtu kama huyo?
Tuendelee na kisa chetu......
Tukajitahidi na sisi kutoka nje kwa haraka haraka, na
tulipofika nje, tuliwaona askari wetu wamesimama huku wameelekeza silaha zao
upande wa pili, kama wanawinda kitu, na mkuu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka
na bastola yake mkononi, akawauliza vijana wake
‘Yupo wapi’ akauliza
‘Mkuu kaingia kwenye hicho kichaka, na cha ajabu haonekani
tena, lakini tuna uhakika yupo hapo, na tunahisi kuwa hayupo peek yake,…’akasema
mmoja wapo, na wote wakaelekea kwenye hicho kichaka na kwa mbele wakaona watu
wawili wakiwa kwenye mapigano na kila mmoja akiwa kamshika mwenzake mkono, ili
kuzuia silaha yake, isielekezwe kwake.
Msaidieni mwanasheria, lakini msitumie silaha, kumbukeni
tulivyoambiwa, ….’akasema mkuu, huku nay eye akielekea kule ambapo mwanasheria
alikuwa akipambana na huyo mtu, na ilikuwa vigumu kuingilia kwani zile silaha
walizoshika zingeliweza kufyatuka na kuleta madhara kwa yule ambaye
angeliwakaribia, kwahiyo ikawa kutafuta jinsi ya kusaidia.
Mwanadada ambaye alikuwa nyuma akiwa na yule binti, alifika
eneo hilo na kuona hiyo hali, na hapo akasema;.
`Mbona mumesimama, hamumsaidi mwenzenu…’akasema mwanadada, akikimbilia
kule kwenye mapigano kati ya mwanasheria na huyo jamaa na alipofika tu,
akasikia mlipuko wa risasi,…..oh, mwanasheria akapanua mdomo, na kudondoka
chini, na yule mtu alipoona hivyo, akainuka kutaka kukimbia, lakini hakuweza
hata kuinua mguu.
Risasi ililengwa bara bara, kutoka kichani, na yule mtu
akatoa macho ya uwoga, na kudondoka chini, na hapo mwanadada na mkuu, wakawa
wameduwaa, ina maana kazi yote imekuwa ni bure, ina maana masharti ya msituni
yamevunjwa, na haijulikani ni kitu gani kitatokea.
Mkuu akamkimbilia yule mtu, na kuhakikisha hana silaha, na
akamshika kuangalia kama yupo hai, na akainua kichwa kumwangalia mwanadada na
kusema;
‘Mhh, haponi, unaona risasi ilipopigwa, kama akipona ni
bahati yake…lakini ni nani kampiga risasi?’ akauliza huku akingalai upande ule
aliofikiria kuwa huenda ndipo mpigaji alipokuwa, na eneo lile lilikuwa na
kichaka, akasema;
‘Hamjamuona mtu eneo hilo?’ akauliza
‘Hakuna mtu, ila kuna dalili kuwa kulikuwa na mtu eneo hilo,
atakuwa amekimbia, wenzetu wawili wanamfuatilia, na gari la wagonjwa
limeshafika, naona wengine wanakuja kuwachukua majeruhi, …’akasema askari
‘Sawa, huyu …’akampiga na buti usoni
‘Bado yupo hai, mbona anaonekana kama kafa…’akasema huyo
askari.
‘Acha afe, nyie hangaikeni na watu wetu, ..’akasema huyo
mkuu, akimgeukia binti yake, na akamsogelea. Bini yake, alikuwa katulia kimiya,
na alipoona baba yake anamsogelea akawa kama anaogopa, na kutoa macho,
‘Pole binti yangu, haya yamekwisha, usiogope tena…’akasema
na huyo binti akawa anatoa macho kuangalia, na mkuu alijua kuwa binti yake
anamuogopa yeye, na akawa anajitahidi kumsogelea huku akitabasamu, na hapo
binti yake akainua mkono na kuonyeshea nyuma ya huyo mkuu.
Mkuu, akashangaa, na akageuza kichwa nyuma, kuangalia ni
nini binti yake anaonyeshea, na mwanzoni hakuwa na mawazo yoyote zaidi ya kuona
kitu cha ajabu ambacho kilimfanya binti yake atoe macho, lakini alipoweka
fikara zake vizuri, akagundua…
‘Oh, huyu mtu ka..ka….ka…’akashidw hata kumalizia na binti
yake akasema;
‘Karuka kama ndege na kupaa hewani…’akasema
‘Haiwezekani….’akasema huyo mkuu
‘Ndio,huwa lile koti alilovaa akilinyosha, linakuwa kama
mabawa ya ndege, na huruka kwa haraka haraka, kama anapaa…’akasema na mkuu,
akamwangalia binti yake kwa mashaka, hakujua kuwa binti ake anamfahamu huyo mtu
kiasi hicho, akasema;
‘Umejuaje hayo….?’ Akauliza na binti yake, akainama kwa
woga, …..
********
Mwanadada akakimbilia pale alipolala mwanasheria na kumuinua
kichwa, na kwanza aliangalia pale jereha lilipo, ilikuwa kwenye mkono wa
kushoto, ni karibu kidogo na eneo la moyo,…akachukua leso yake na kuweka kwenye
lile jeraha ili lisiendelee kuvuja damu, na mmoja wa watu wa usalama
anayefahamu mambo ha huduma ya kwanza akafika na kuanza kumsaidia…
Na alipowekwa vyema, mwanadada, akamsogelea na kumwangalia
huku akihisi mwili mzima ukimuisha nguvu, akakaa karibu na alipolala huyo
mwanasheria, na kunyosha miguu yake, akainua kichwa cha mwanasheria na kukiweka
mapajani mwake, na kujaribu kulia, lakini hakuna cha machozi, wala sauti ya
kulia, akainama na akawa kama kamlalia kichwani mwanasheria huyo, na ghafla mwanasheria
akafunua macho na kumwangalia mwanadada, akasema;
‘Naku-ku-penda sana mwana-na-dada, kumbuka hilo,..na..na
siku zo-te zo-te nili-kuwa naji-ji-tahidi nikuambie kuwa hata iweje, mi-mi sita-kuacha…’akatulia
kama anatafuta pumzi.
‘Tulia mpenzi usijilazimishe kuongea….’akasema mwanadada
akiwa na macho ya huzuni, na akahisi machozi yakija kwa kasi machoni, lakini
hakutaka yatoke ili kumpa moyo mtu wake.
‘Lakini kwanza…. i..i…libidi nitimize wajibu wangu wa
kifamilia…’akasema na kuwa kama anahema kwa kasi, halafu akatulia, na mwanadada
akamwangalia akihisi huenda keshakata roho, lakini mara mwanasheria huyo akafungua
mdomo na kusema;
‘Kwa hali ilivyokuwa, ilibidi nitimize ahadi yangu kwa ndugu
yangu kuwa nitailinda familia yake…’akaongea vyema na mara sauti ikakatika,
halafu akasema kwa haraka haraka
‘Lakini moyoni nilijua kuwa nina ahadi yetu, kuwa
tunahitajiak kufunga ndoa..na..na..ikumbuka sana hiyo ahadi, tuliyowekeana,kuwa
ni lazima tufunge ndoa..ndo-ndoa….sasa sijui kama ita-we-ze-ka-na..’
‘Itawezekana mpenzi, usikate tamaa, nakuomba sana usiniache,
tutimize ahadi yetu ya ndoa, tafadhali usiniache…nakupenda sana mpenzi, ….’akasema
mwanadada huku akishindwa kuyazuia machozi ambayo yaliazna kutoka kama maji.
‘Sijui…sijui..mwanadada..nahisi siku zangu zimefika, …,
iliyobakia sio uwezo wangu tena, …namuachia mungu , kwani namuona kaka yangu
akinisubiria kwenye makazi ya milele,..nakuomba sana, kama nitakufa,ilinde
familia yangu, …'akasema huku akikunja uso kuonyesha maumivu.
'Nina...maana mwanamama na mtoto wake, wapeni haki yao …hilo lilikuwa
ni jukumu langu..sasa, naona nimeshindwa kulitimiza, kaka zangu watanilaumu…la…la..kini,
utaweza kunisaidia…niahidi kuwa utanisaidia hivyo…’akasema na kutoa macho
kumwangalia mwanadada, na mwanadada akajitahidi kutabasamu na kutikisha kichwa
kukubali huku akisema.
‘Usiseme hivyo, hutakufa mpenzi, ….mwanamama na mtoto wake
tutaishi nao…..nakuahidi haki yao haitapotea, mimi na wewe tutahakikisha hilo…..’akasema
huku akitaka kupiga ukelele kuwa wawaambie watu waharakishe kulete gari la
wagonjwa, akaangalia lile jeraha, ambalo kwa muda ule lilikuwa halivuji sana
damu…’halafu akageuka kumwangalia mwanasheria usoni, akamkuta keshafunga macho.
Mwanadada alihisi mwili ukimsisimuka, hasira chuki, ..na
moyo wa kisasi ukaanza kumwingia kwa haraka sana, na hapo akamuweka mwaansheria
chini taratibu , kwanza akambusu shavuni, na pili, akachukua ile bastola
aliyokuwa nayo huyu mwanasheria, akaitayarisha tayari kwa kuitumia, na kugeuka
pale alipolala yule mtu wao akiwa kajaa jaziba, na ….
Macho yalipotua pale alipokuwa kalala yule mtu, yalikuta hayupo, ooh, hayupo…akageuka upande waliposimama mkuu na
mwenzake ambao walikuwa wakihangaika huku na kule kumtafuta huyo mtu na wengine
walikuwa wakihangaika kuwabeba majeruhi, na akahisi huenda wameshambeba huyo
mtu na kuondoka naye, lakini akili haikutaka kulikubali hilo, kwa muda upi wamembeba bila ya yeye kusikia , au kuwaona;.
‘Jamani mtu wetu yupo wapi?’ akauliza.
Na wote wakasimama kumwangalia mwanadada huku wakiwa
hawaamini hilo lililotokea, na mkuu akasema;
‘Katoweka kiajabu…binti yangu anasema kamuona akiruka kama
ndege,kwani koti lake lina mabawa, kwahiyo anakuwa mwepesi…tumejaribu kutafuta
kila kona hakuna dalili ya uwepo wake…..’akasema huyo mkuu, akiwa bado hajaka
tamaa…
‘Lakini alikuwa katika hali mbaya ya kukata roho, ndio maana
hakuna aliyemjali sana, mimi mwenyewe nimeona lile jereha, na hali aliyokuwa
nayo…’akasema mkuu, huku akiangalia huku na kule,na mara akaona michirizi ya
damu ikielekea porini...akaitizama.
Akaanza kuifuatilia na kabla hajafika mbali mara kitu
kama radi, kikasikika,upepo mkali ukaanza kuvuma, hadi miti inataka kung’oka,
msitu mzima ukawa kama umeingiliwa na vitu visivyojulikana, makelele kama ya
popo, na milio isiyo ya kawaida ikatawala, harufu mbaya kama uozo wa mizoga
ukatawala puani, na hapo kila mmoja akawa anahangaikakuziba masikio.
‘Jamani hapa hakuna amani tena, tuondokeni haraka…’akasema
mkuu, na mwanadada akageuka kumwangalia mwanasheria ambaye kwa wakati huo
alikuwa kabebwa kwenye machela, akipelekwa sehemu ambayo gari la waginjwa lipo,
maana huko juu kulikuwa hakupandiki na magari, na mwanadada hapo alishindwa
kujizuia akajikuta analia na kusema kwa suati;
‘Nakupenda
mwanasheria, nakuomba usife..ukiniacha nitabakia na nani….ooh, kwanini….’akawa
anasema lakini sauti yake ilikatishwa milio ya ngurumo na sauti za milio ya
popo, na walipoangalia juu wakaona popo wakija pale walipo kwa kasi, na hapo
hakuna aliyesubiria, kila mmoja akaanza kutimua mbio kivyakeaf,
kuelekea nje ya
huo msitu…..
NB:JE kutatokea nin..ni sehemu ndogo ya tukio la msituni,
tukirudi tunaingia kwenye hitimisho la kisa chetu,
WAZO LA LEO:
Maisha ya binadamu sio ya moja kwa moja, kuwa utapata raha, siku zote, kuwa
ndoto zako zitatimia kama ulivyopanga, kuwa utampata rafiki, au wote watakuwa wema kwako, mitihani ya aina mbali mbali inaweza
kukutokea hadi ukafikia kusema kwanini mimi…ndio ni lazima useme hivyo,
kwasababu uhimili wa kibinadamu una mipaka, lakini tukumbuke kuwa yote ni
mapenzi ya mwenyezimungu, tusikate tamaa, na tujipe moyo, kuwa baada ya dhiki
ni faraja.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Hakika Ndugu Wa Mimi HUNA MPINZANI..MUNGU baba amekupa kipaji!!!
Hongera munooo..
Naunga mkono na wazola Leo.
Pamoja saana.
I loved as much as you will receive carried out
right here. The sketch is tasteful, your authored
material stylish. nonetheless, you command get bought an nervousness over that you wish be delivering
the following. unwell unquestionably come more formerly again since exactly
the same nearly very often inside case you shield this increase.
Stop by my homepage: the tao of badass review
Post a Comment