`Nikikumbuka hilo
tukio, wakati mwingine najikuta nikicheka mwenyewe….’akasema mwanadada huku
akicheka, akiendelea kuhadithia kisa hiki, …
‘Maana kwa jinsi gani
nilivyotoka kwenye huo msitu, nashindwa hata kuelezea,hii ni kuona jinsi gani
mwanadamu anavyoogopa kifo ambacho anahisi ni cha mateso…’akatulia.
‘Nashangaa sana pale
mtu anapotaka kujiua, lakini mtu kama huyu mwambie, kuna nyoka au simba, aje
amtafue ili afe, hatakubali…..’
‘Basi siku hiyo
imebakia kama historia kichwani mwangu…
Kisa chetu kinaendelea hapo…
Siku hiyo nilikimbia
sijawahi kukimbia hivyo katika maisha yangu, ulikuwa unakimbia na ukigeuka
nyuma unawaona wadudu wale wapo juu yako, karibu yako kabisa..wakiwa wanapanua
midomo yao kutaka kukung’ata, siunawafahamu popo walivyo….’akasema mwanadada
akimuhadithia mama kisa hiki.
‘Na cha ajabu japokuwa wadudu wale walikuwa karibu, lakini
hakunigusa, alikuwa ule mlio wao huku akichezeza mabawa yake, na akipanua ule
mdomo wake, unajikuta ukiogopa, na kuongeza mbio… nilikimbia na sijui wenzangu
ilikuwa hivyo hivyo au vipi, lakini tulipokuja kuhadithiana kila mmoja
alijikuta akicheka,…..’akasema.
‘Tuligundua kuwa lengo na nia ya wale ndege, popo, ilikuwa
sio kutuzuru, nia yao ni kututoa msituni, na sio kutuuma, kama tulivyojua
watafanya hivyo, na kama wangelitaka kufanya hivyo wasingeshindwa….’akasema
‘Cha ajabu nilipomaliza eneo la msitu tu na kuingia kwenye
mashamba, maeneo ya wazi, kwenye mipaka ya msitu na mashamba ya watu, wale
ndege walisimama na hawakuvuka ule mpaka, wale wadudu walibakia pembeni mwa huo
mpaka wakiruka huku na huku, kuzunguka miti, kama vile wanafanya doria, mtu
asirudi tena, na kama kweli wanahakikisha hakuna anayerejea, na wengine wakawa
wanatukdolea macho kututisha…’.
‘Kwakweli sikuamini, nilisimama nikainama, na kujaribu
kutafuata hewa, na baada ya dakika kadhaa za kutulia na kuhakikisha nipo
salama, nikageuka kuangalia wenzangu, na niligundua kuwa kila mmoja alikuwa
sehemu yake, akipumua kwa shida, na hakuna aliyekuwa anaamini kuwa katoka humo
msituni salama,
Mara nikakumbuka, jambo, na hapo akili ikarejea kwenye
mwendo wa kawaida, nikageuka huku na kule, nilikuwa nikiwaangalia wale
waliokuwa wamewabeba majeuhi, je na kwao
ilikuwaje, je watakuwa wameweza kuwabeba hawo majeruhi, au wamewatelekeza,
…nikaanza kutembea kuwafuata wenzangu, na bahati nzuri nikakutana na mkuu,
akiwa kashikilia bastola, akiwa kama anawaelekezea wale ndege kama kuwatisha.
‘Mkuu unataka kufanya nini, hilo lililotupa ni dogo…unatafuta
mengine tena….’nikasema na mkuu akaanza kucheka.
‘Hivi wewe unaakili kweli, yaani unacheka, wakati uliona
jinsi gani hawa wadudu walivyokuwa wakitaka kutuuma….’nikasema na huyo mkuu
akaendelea kucheka, na maaskari wengine waliokuwa karibu na wao wakaanza
kucheka.
‘Nyie watu mnacheka u kwa vile hamjui historia ya hawa
wadudu, sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili,…, nasikia ukikiuka msharti,
kama uko huko msituni, ukajifanya unawinda kwa bunduki, hawa wadudu,
wanacharuka hivyo hivyo, na ole wako, uwapige, watakufuata kwa wingi hadi
nyumbani kwako, na watahakikisha wanakudonoa hado unabakia mifupa, hapo tu
wametufukuza kwa vile hawakuwa nia mbaya
na sisi, huenda kwa vile hatukuwadhuru wao, ila tumekiuka miiko ya kupiga
risasi….’akasema mmoja wa maaskari anayefahamu historia ya huo msitu.
‘Ilishawahi kutokea hivi karibuni kwa watu unaowafahamu?’
akauliza mwanadada.
‘Ndio kwa wawindaji na watu waliokuwa wakitafuta madini,
kwani humo kwenye huo msitu kuna sehemu zina madini, ukiweza kuyafuma wewe
unakuwa tajiri, lakini wengi waliobahatisha kuyapata, waliishia kugombana na
kuanza kutupiana risasi, na hapo wakajikuta wakitolewa mbio na hawa wadudu…’akasema.
‘Sasa tutafanyaje maana tunahitajia kurudi, ili kukusanya
ushahidi……’akasema mwanadada.
‘Kurudi kwa leo haiwezekani, huwezi kupita hapo, mpaka hawo
wadudu waondoke, na kuondoka kwao ni mpaka waone sote tumeondoka eneo hili..’akasema
huyo mtu.
‘Oh, wangeniuma nisingesita kutumia silaha….’akasema mkuu,
na kumwangalia mwanadada, huku akiendelea kucheka, na alipomuona mwanadada
akimwangalia kwa hasira , yeye akasema;
‘Duuh, kweli kifo kinaogopewa, sikujua kuwa mwanadada unaweza
kukimbia kiasi hicho, maana nilikuwa nyuma yako, na nilikuona ukikimbia kama
unapaa….’akasema mkuu, lakini alimuona mwanadada akihangaika kuangalia huku na
kule, na hapo akauliza.
‘Unatafuta nini tena mpendwa, umesikia kuwa leo huwezi
kurudi tena humo msituni…, au bado wewe una moyo wa kuingia huko msituni..kama
upo tayari twendeni?’ akasema mkuu akijifanya yeye haogopi.
‘Mimi nawaangalia majeruhi,….je wamewahi kutolewa,au ndio
wametelekezwa huko msituni?’ akauliza mwanadada, na hapo mkuu, akaangua kicheko
tena na kusema;
‘Yaani sasa hivi ndio unalikumbuka hilo,wakati wewe ulikuwa
ukikimbia hata bila kumjali mpenzi wako, watu kama nyie, ndio wale linapotokea
tatizo kama hili, kama alikuwa na mtoto wake mchanga anambwaga hapo chini, au
anamsahau kabisa, na anakuja kukumbuka baadaye …’akasema huyo mkuu huku
akigeuka kuwaangalia wale ndege.
‘Sasa mwanadada, tufanyeje, turudi kuwafuata wenzetu
majeruhi msituni, kama kweli unawajali,
kama kweli unampenda mpenzi wako, ….?’akasema mkuu huku akichekana na mwanadada
akazidi kukasirika, akijua mwenzake anamzihaki na huo ulikuwa sio muda wa
masihara, na mkuu alipoona hivyo, akachukua simu yake na kuanza kuwasiliana na
watu wake , akasema;
‘Mumeshawafikisha hao majeruhi hospitalini?’ akauliza na
kusikiliza kwa makini, halafu akageuka kumwangalia mwanadada huku uso ule wa
kucheka ukiwa umebadilika, na kuwa uso wa kikazi zaidi akasema;
‘Wameshawafikisha majeruhi hospitalini, na mwanasheria keshaingizwa
chumba cha upasuaji,….hali yake sio nzuri….’akatulia huku akimwangalia
mwanadada ambaye kwa muda huo alionekana mwenye huzuni nyingi.
‘Sikiliza mwanadada, kama mtu huyo ni wakupona atapona tu, na
sote ndilo tunaloliomba, lakini ukumbuke kuwa hapa tupo vitani, na vitani
usitegemee kushinda tu,kuna kushindwa, kuna kuua na pia ukubali kuwa kuna kuuwawa
pia, huwezi ukaua tu,na wewe mwenzako dhamira yake ni hiyo hiyo kukuua,..kwa
hali kama hiyo wewe ukiwa msitari wa mbele wa mapambano ukubali yote…’akasema
mkuu, na mwanadada akamwangalia kwa macho yaliyojaa hasira,
Mkuu akageuka kuangalia upande mwingine, na kabla hajasema
kitu mwanadada, akaishika bastola yake vyema mkononi na kusema;
‘Huyo mtu atakuwa kaelekea wapi?’ akauliza mwanadada, na
mkuu, akamgeukia na kusema;
‘Kama bado yupo huko msituni, atakuwa kaliwa na hao ndege,
lakini kwa hali iliyotukuta sisi, hata yeye sizani kama atakuwa kabakia humo
msituni, huenda yupo mahali, anaugulia hilo jereha la risasi na huenda
keshakufa….’akasema mkuu.
‘Nataka nimuone akiwa hai, na ikiwezekana niitumie silaha
hii kwake…’akasema mwanadada kwa hasira.
‘Huwezi, unasema tu kwa hsira, lakini nikujuavyo wewe,
huwezi kufanya kitu kama hicho,…’akasema mkuu, na kugeuka upande ule aliokuwa
kaangalia mwanzoni, akatoa simu yake kutaka kuwasiliana lakini kabla hajafanya
hivyo mara wakasikia sauti za mlio ya bunduki, upande mwingine nje yauka juu,
na uanza kuzunguka zunguka huku wakizidi kutoa sauti za kutisha.
‘Nini tena hicho jamani, mnataka hawa ndege watuvamie tena,….aah’akasema
mwanadada, na mkuu akamwangalia mwanadada na kusema
‘Vijana hawo, huenda wameshamnasa huyo mtu wetu…’akasema
mkuu
Ilikuwa sio mbali sana na pale mkuu na mwanadada,
wakakimbilia huko waliposikia huo mlio wa bunduki, na kwa mbele kidogo wakawaona
wenzao wakihangaika, kama vile wanapambana na mtu, na mkuu na mwanadada wakawasoegelea
wakiwa na tahadhari,silaha zao zikiwa mkononi tayari kwa lolote lile.
Walipofika walimuona yule jamaa akiwa keshazibitiwa, na
mwili wake ulikuwa umelowana damu, japokuwa bado alikuwa akileta ubishi, na
wale maaskari wakahakikisha wamefunga pingu mikononi na miguuni, na kumweka
chini ya ulinzi thabiti,
Mkuu alimwangalia yule mtu, na kutikisa kichwa, akasema;
‘Kama isngelikuwa sheria, nisingekuwakilisha mahakamani,
ningelihakikisha nachukua sheria mikononi mwangu, ….lakini,sheria inanifunga,
najali sana mamlaka niliyopewa..’akasema mkuu, na mwanadada ambaye alikuwa
karibu na huyu mkuu, alikuwa kaishikilia bastola yake, huku mkono ukiwasha,
kwani hasira na chuki vilikuwa vimemzonga sana. Mkuu alihisi hiyo hali akamgusa
mwanadada kwa mkono kumuashiria kuwa tulize hasira zake.
‘Na nawaambia ukweli, mkifanya makosa yakunipeleka jela
nikiwa hai, hamtanipata tena….’akasema huyo jamaa kwa dharau.
‘Huna lolote wewe, uchawi wako umeshafirisika unafikiri
hatukujui,…huna lolote wewe unakwenda kuozea jela…ara ya ngapi ni’akasema mkuu.
‘Mimi nawapa kama tahadhari, kwani mara ya ngapi
nimehukumiwa kufungwa jela, lakini ipo wapi,..kwa sasa ni kweli, sitegemei huo
uchawi, kama mnavyouita nyie, mimi nina ujuzi zaidi ya huo, uliza mimi nilikuwa
nani wakati nipo usalama…..’akasema kwa
dharau
‘Hahaha…ulipokuwa usalama,..mtu kama wewe hustahili kuwa
sehemu kama hiyo, na kama ulibahatika kuingia uliingia kimakosa, ndio maana ukatolea, mtu
kama wewe hustahili kufanaya kazi yoyote ya wito , una roho mbaya kama shetani…’akasema
mkuu.
‘Hahaha, kumbe unajua ehee….Lakini ulizia nilikuwa nani …’akasema
huku akitema damu chini.
‘Kama singelikuwa hili jeraha, watu wako hawa
wasingeliniweza,..ila jeraha limegusa pabaya, …na nimeshaitoa risasi peke
yangu, unaweza hilo,….nyie cha mtoto, nikitaka kufanya lolote hamniwezi,…ulizia
huko nilipokuwa, wenyewe walisalimu amri,…’akasema akimwangalia mkuu kwa dharau
Mkuu alimwangalia kwa makini, na kweli alihisi moyoni kuwa
mtu kama huyu sio wa kawaida kama kaweza kujitoa risasi mwenyewe, basi huyu mtu
ni zaidi ya gaidi, ni shetani, hastahili kuishi, lakini moyoni aliogopa kufanya
lolote, kama kiongozi, …na yule jamaa akaendelea kuongea kwa nyodo na kusema;
‘Hebu angalieni yote niliyoyafanya ni nani angeliweza
kufanya hivyo, …mimi ni jembe, tena jembe ulaya, hakipatikani hivi hivi, na
wajinga hawajui kulitumia, ndio maana najitumia mwenyewe, …mimi nina ujuzi wa
kila kitu,….’akasema huku akitema damu ambazo zilitokana na kipigo, aliumia
mdomono, kulionekana kuvimba.
‘Nawaambia ili mjue, kuwa mimi ninajua kila kitu, hebu
niambieni ni nani angeweze kujenga lile handaki, simumeliona wenyewe, mtasema
kaja fundi mkubwa toka huko majuu, hakuna fundi anayeniweza mimi, ukisikia
mtaalamu, basi ujue mimi ni mtaalamu kweli, nyie mnasema mtaalamu kwa mambo
hayo ya ushirikina, hilo lilikuwa kama chambo tu…’akasema kwa nyodo.
‘Hiki ki kichwa, niliwasoma watu, nikajua udhaifu wao upo
wapi,….watu wanaogopa sana ushirikina, wanaogopa sana nguvu za giza,…ndio maana
hata watu wa dini wanatumia mwanya huo kuwaogopesha watu, …na mjnja kama mimi
nikaona nitumie mwanya huo…’akasema.
‘Nawaambia hili , kwasababu huenda msipate muda wa kuongea
na mimi, msiponiua nitapotea na hamtaniona tena….’akasema.
‘Mimi nilifanya uchunguzi huo baada ya kufanya utafiti wa
kisayansi, kuhusu hisa ua uzaifi wa mwanadamu, …uwoga, niligundua kuwa
mwanadamu ni mwoga sana, hasa kwa yale ya kufikirika,…’akasema huku akikunja
uso kuonyesha anafikiria jambo.
‘Na niligundua kuwa sehemu nyeti ni hiyo, ya dhana za
uchawi, na hpo nikaanza kucheza napo,…kwa vile nina kipaji cha uganga, nina
kipaji cha asili cha unajimu, utabiri, na hayo wanayoita mizimu, nikafahamu
kuwa ninaweza kutumia kipaji hicho na kutajirika…..’akatulia.
‘Ni nani kakumbia kuwa waganga, watu wa namna hiyo
hawatakiwi kuwa matajiri….hizo ni hisia hasi, ni hisia za watu wenye ubinafsi,
na ni hisia za watu wasioenda shule…mimi nimeenda shule, na nikasoma zaidi ya
kwenda shule, nafanya utafiti wangu mwenyewe, ukiingia kule kwenye handaki
utaona chuo change, kuna maabara, ya kila namna, na hivi karibbu nilikuwa
nafanaya utafiti wa kuunda silaha ya maangamizi…’akasema na watu wakawa
wanamuangalia kama mwehu.
‘Shangaeni…lakini msishangae sana ya shetani, hayo ni cha mtoto kwa ibilisi….’akasema
na kucheka kwa dharau.
‘Ndio maana nawaambia kuwa mimi ni jembe, lakini lipo kwa
watu wasiojua kulima,…unajua kwanini nilishindwa kukaa jeshini,…kwasababu hiyo
hiyo, kuwa unaongozwa na watu wasiokwenda shule, wanatumai nguvu nyingi bila
akili, hawashauriki,…wao wanajua kushoto kulia, lakini hawajui kuna chini na
juu, na kati ya kushoto na kulia…hawajui..hawaeelzeki, na baya zaidi kuna
wanaojifanay miungu watu…’akatulia.
‘Afande, afande….ni nani atamuabudua binadamu mwenzake,
binadamu ambaye hajui kabisa, silaha hiyo aliyosihika imetengenezwaje, hajui
kabisa, uwezo wa mwanadamu upoje, katika jambo fulani…mii najua na naweza
kukujua hivi sasa unafikiria nini….’akatulia.
‘Ndio maana siogopi, maana nimeshwafahamu lengo lenu ni
nini..namuogapa sana huyu mwanamke…hiki nacho ni kichwa kingine…’akasema
‘Lakini sio kumuogoa kwa kuogopa mtakapofikiria nyie…naogopa
akili yake…na sijui alinigunduaje, …alinichota kiajabu na kuniweka ulingoni,
mwa mahakama, na hapo, akajumlisha na kutoa, akanigundua…na mtu kunigundua
mimi, sio mchezo…’akatulia.
‘Sasa kwa akili zenu ndogo, hebu jiulizeni lile handaki
lilijengwa na nani kama lilivyo, ile ni mikono yangu …ni nani angeliweza
kufanya haya yote peke yake, ni akili yahali ya juu, na bado kama mtaniachia
huru, kama mtanifunga, mjue nitafanya mabaya zaidi ya hayo, ….moyo wangu
unatamani kuwa mfalme chini ya ardhi….mnaweza hayo…’akasema kwa dharau na
mwanadada, akainua bastola kutaka kumaliza kazi,lakini mkuu akamuwahi na
kumzuia mwanadada, asifanye hilo alilotaka kulifanya.
‘Ole wako…..uombe mwanasheria apone, la sivyo, nitahakikisha
nakupeleka huko huko mkakutane kwenye mikono ya sheria
isiyodanganyika..’akasema mwanadada, na yule jamaa akamwangalia mwanadada kwa
dharau, na kusema;
‘Napenda sana mwanamke kama wewe, mwenye kujiamini, lakini
huyo ndugu yako, eti mkuu, hana lolote, ….ndio maana hata binti yake,
akamkimbia na kuja kwangu, …lakni namuheshimu kwasababu ni baba
mkwe..hahahaha….binti yake kazimia kwangu,…mimi ni mtaalamu wa kila kitu, jembe…’akasema
kwa dharau akimwangalia mkuu kwa macho yanayosinzia sinzia,kuonyesha kuwa nguvu
zilikuwa zikimuishia, huenda ni kutokana na kupoteza damu nyingi,na mkuu
akamwangalia kwa hasira, na alichofanya ni kumpiga teke la tumboni, na huyu
jamaa akainama na kuguna kwa maumivu.
‘Mhh, hapo sasa wewe mwanaume…lakini hujafanya kitu, ni kama
kumpiga paka kwa fimbo…hahahaha…hamtaki niwasimulie mengine, shauri lenu,msije
mkawa mnazua, sikilizeni kutokwa kwangu mwenyewe,hahahaha….’akacheka kwa dharau
‘Mpelekeni kituoni na hakikisheni hapati nafasi yoyote ya
kutoroka, akitoroka na nyie muhakikishe mnacha kazi,….mtawajibika, tunataka
aone kuwa sis hatutanii…kama anatumia vumba sisi tunatumia chuma…na ole wako,
ujifanye mjanja,…nitakutafuta hadi huko ardhini unaposema unataka uwe mfamle,
na tutakuzika huko huko…’akasema mkuu, na yule jamaa akacheka kidogo, na
kumgeukia mwanadada, akamwangalia kwa macho yaliyochoka, halafu akatabasamu kwa
dharau na kusema;
‘Mpenzi, pole sana, mchumba wako, kashetangulia,…lakini
kiukweli sikuwa na lengo la kumuua, yule ni rafiki yangu, kanisaidia mambo mengi
sana, bila ya yeye kujua,…ni bahati mbaya, wakati tunazuiana, risais
ilifyatuka, sikuwa na nia hiyo, ….sio mbaya wangu yule, kwanini nimuue…’akasema
na kujifanya ana huruma.
‘Ila nakuahidi kitu kimoja, sitakutupa, usiwe na wasi wasi
mimi nipo nitachukua nafasi yake…’akasema na mwanadada, aligeuka na kwa haraka
akatupo teke lililompata huyo jamaa tumboni, na yule jamaa aliguna na kukunja
uso kwa machungu, na akahema mara moja na kusema;
‘Mhh,..unapiga teke kama mwanaume, oh,.....'akakohoa kwa muda, halafu akainua kichwa huku mate yakimtoka na damu akasema;
'Lakini, sikilizeni ni..niwaambie
ukweli, ni bora mniue, kwani nikipata nafasi , nitahakikisha kuwa haya yote
mliyonitendea mnayapata vile vile jino kwa jino…nawahakikishia hilo, mtaona….na
wewe uta…shukuru kuwa umenipata mimi ns io huyo jamaa yako mnafiki, leo kwako
kesho kwa mwanamama, ….’akasema na maaskari wakamkokota na kumuingiza kwenye
karandinga
NB. Kumbe hatujafika kwenye hitimisho …haya huyo ndiye
mtaalamu, sema wewe
WAZO LA LEO:
Ubaya sio sifa ya kujisifia, matendo mabaya sio sifa ya kujisifia mbele za watu,
ni kama mtu anajitembeza uchi mbele ya watu akipata kuwa yeye ni mjanja, huo
sio ujanja ni ujinga. Ukiwa na hali kama hiyo ujue umeshatekwa na shetani, na
unahitajika kutubia na kujirudi haraka iwezekanavyo.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment