Wakili mwanadada akiwa
kwenye ofisi yake aliyokuwa ameifungua kwa muda kwa ajili ya kufuatilia kesi
hizo, ni ofisi hiyo ilikuwa pembeni mwa duka la mwanadada, alichagua kukaa
sehemu hiyo, ili kukutana na watu mbali mbali aliotaka kuwahoji, lakini baada
ya tukio la kutaka kuuliwa kwa kugongwa na gari, ilibidi asiitumie tena sehemu hiyo
kwa muda, lakini siku ya leo akafika hapo kwani aliahidiana kukutana na mtu
aliyempigia simu kuwa anahitaji kuja kukutana naye.
Akiwa kakaa kwenye meza
yake, akiwaza, na huku kaweka mikono yote miwili kwenye kidevu tayari kwa
lolote litakalo tokea, alihisi joto, akavua koti alilokuwa kalivaa, na kubakia na kivazi kilichoacha sehemu ya mebega wazi, ...akalitundika koti lake ukutani, ....akataka kuchukua silaha yake iliyokuwa kwenye hilo koti, lakini akaona haina haja, akarudi na kukaa kwenye meza, huku akiwa kaweka mikono yake miwili kidevuni kama kwanza.
Badala ya joto, akaanza kuhisi ,mwili ukimsisimuka, na nywele kumsimama,
akahisi kuna jambo, akahisi kuna mtu karibu yake,, na hapo akajilaumu, kwanini
hakuchukua silaha yake akakaa nayo karibu, maana kama ni mtu yupo karibu, hataweza kuinuka, na kuichukua hiyo silaha kabla hajazurika, ...lakini hata hivyo , huyo mtu angelipitaje, wakati nje kuna askari wanalinda, na polisi wenyewe walimuahidi kuwa kutakuwa na ulinzi wa kutosha.
Inawezekana ni huyo mtu keshafika ..kama ni yeye walinzi wangemwambai kuwa kuna mtu anahitaji kuongea na yeye, asingeliweza kuingia bila kuonekana,....akageuka kuangalia huku na kule, hakuona dalili ya mtu, lakini hisia zake bado zilikuwa zikimtuma kuwa kuna mtu yupo karibu,....
'Isiwe taabu,..'akasema na kuinuka kwa haraka, akaliendea koti lake aliona ni bora aichukue hiyo silaha yake akae nayo karibu, maana huenda huyo mtu hana mema, na hali anayoiskia inamuashiria hatari...na wakati anainuka kwenda kuichua hiyo silaha, mawazo yake yakamrudisha nyuma na kukumbuka jinsi alivyoongea na
huyo mtu ambaye aliahidi kuwa atakuja;
‘Unahitaji kukutana na mimi
kwa tatizo gani na kwanini iwe usiku, huoni….’ akauliza
‘Siwezi kukuambia kwenye
simu , ila nina uhakika litakusadia kwenye kesi yako hiyo, na sitaki nionekane
na mtu..’akasema
‘Kesi ipi unayoizungumzia…?’
akauliza mwanadada.
‘Mwanadada, Mwanadada….kwani
wewe una kesi ngapi,….?’ Akauliza huyo mtu.
‘Kwanini usiniambie kwenye
simu….?’ Akauliza mwanadada, na huyo mtu akasema;
‘Mimi najua yote yanayoendelea
kwenye hiyo kesi yenu, na mimi ninajua mengi yaliyofanywa na hawo watu, kwani
walinitumia sana, lakini nimeona kuwa hawanifai, walikuwa wakinitumia tu, nawadai
pesa nyingi sana, na sizani kama wataweza kunilipa, …nimezungushana nao sana,
na imefika sehemu wanaanza kunitishia maisha,…’akatulia kidogo.
‘Kwahiyo kwa vile mnaanza
kutapatapa, sasa mnazungukana, au ….?’ Akasema na huyo mtu akaendelea kuongea bila
kujali anavyoongea mwanadada.
‘Mimi sikubali kudhulumiwa,,
…maana nimefanya mengi ambayo hata sikutaka kuyafanya, lakini kwa shinikizo
lao, kuwa nispofanya, wataniumbua, na familia yangu itakuwa hatarini, na kwa
vile nilikuwa kijiweni muda mrafu sina kazi, ikabidi nikubali,…sikuwa na
jinsi….lakini hata hivyo,nisingeliogopa kuwa maisha yangu yapo hatarini, lakini
familia yangu….’akasema.
‘Kama unahisi hivyo ,
nakushauri ufike kituo cha polisi…uwaambia yote hayo, …’akasema.
‘Kabla sijaenda huko ngoja
nikuambie hilo nililotaka kukuambia ,na kukupa …maana hata huko polisi sikuamini sana, naweza
nikauwawa huko huko, na hili ninalotaka kukuambia likapotea, na huenda wakawahi
kuniua, ….mimi nawaambia ukweli, hamuwajui watu mnapambana nao, na hamuwajui ni
watu gani,..hata hivyo, sitaki nife na kinyongo moyoni…’akasema
‘Sawa wewe fika kwenye ofisi
yangu, utanikuta hapo, ila nakukanya kama una ajenda yoyote ya siri, utajijutia
mwenyewe…’akasema mwanadada.
‘Usiwe na wasiwasi
mwanadada,..hilo nakuhakikishia sina ajenda wala sina kibaya nilichokusudia juu
yako, na wewe hawawezi kukuzuru kwa hivi sasa,…yaliyowahi kutokea yametokea na
yananitesa sana…siwezi kuvumilia tena, na familia yangu ni muhimu sana…’akasema
‘Sawa nitakusubiri hapo….’akasema
na kabla hajakata simu, akasikia huyo mtu akisema;
‘Utanikuta …usiwe na
shaka…’akasema huyo mtu na kukata simu
*********
‘Una uhakika sio hawo watu
wabaya wanaotaka kukuua?’ akaulizwa na Mzee wa kijiji
‘Nina uhakika sio hawo watu,
na kama ni wao, nimeshawekewa walinzi, ambao watakuwa wakinilinda, msiwe na
wasiwasi na hilo…’akasema.
‘Lakini mimi nitakuwa karibu
yako,….sio lazima unione,.’akasema na mwanadada akacheka, na kusema;
‘Yaani baba, bado tu una
wasiwasi na mimi….haya fanya uanavyoweza, lakini nakuomba usije ukaharibu, au
ukajitumbukiza kwenye hatari,maana huyo mtu kasema kama kutakuwepo na mtu
mwingine hataweza kusema hayo aliyokusudia kuniambia…’akasema
‘Usiwe na shaka, yeye
hataniona na hata wewe mwenyewe hutaniona….’akasema baba huyo kwa kujiamini..
Mwanadada alipohisi mwili
ukimsisismuka, akainuka na kusimama, akajifanya kama anapanga makabrasha
yake huku
akijaribu kutafuta njio ya kujihami, …au ni walinzi wanapita pita huko nje,
au..na ghafla akasikia kama sauti ya kitu,….akageuka na mara akajikuta
anaangalia na mwanaume , akiwa kavaa suti na briefcase mkononi na miwani ya
meusi, machoni, na usiku kama ule, aliona ni kitu cha ajabu.
‘Wewe ni nani na umeingia
saa ngapi humu ndani..mbona sijaambiwa na polisi?’ akauliza mwanadada.
‘Usijali, hapa niliingi baada
yaw ewe tu kunikubalia tukutane hapa, jinsi nilivyoingia hata polisi wako
hawajui, na hata wakati unaingia humu ndani nilikuwepo hapo
nimejificha….’akaonyesha pembeni ya kabati, na mwanadada akajikuta akishangaa,
maana kweli alipoingia hakuwazia kabisa kuwa kutakuwa na mtu ndani, kwahiyo
hakujali kukagua humo ndani, ….lakini aliwezaje kupita getini, …’akawa
anajiuliza.
‘Haya niambie ni nini
ulichotaka kuniambia…maana kwa hli kama hiyo umeshaniweka kwenye wasiwasi,
umewezaje kuingia hata bila walinzi kukuona?’ akauliza mwanadada.
Yule mtu akafungua briefcase
yake na kutoa bahasha, na kumimina kilichokuwemo humo ndani, …kulitoka DVD
mbili, na chupa moja ya maji ya kunywa na ndani yake kulikuwa na kitu kama
soda, na hiyo chupa ilikuwa imefungwa vyema kwenye bahasha inayoonyesha ndani.
‘Usinione hivi mwanadada,
mimi niliwahi kufanya kazi za usalama wa taifa nikafukuzwa…mimi ni
komandoo….’akasema na kutabasamu.
‘Hata walipofikia hatua ya
kunifukuza, walijuliza mara mbili tatu, maaan walijua kuwa wanafukuza jembe, walijua
kuwa mimi sio mtu wa kawaida,na wakawa wananifuatlia kila mara, niliishi maisha
kama jela, lkini baadaye wakachoka,na hapo ndipo hawa watu wakanitafuta…
nilijuana na huyu mzee siku nyingi..na amekuwa akinitumia kwenye kazi zake za
ujasusi….’akasema
‘Unazungumizia mzee yupi?’
akauliza.
‘Tusipotezeane muda, siwezi
kukutafunia kila kitu, …’akasema huku akiangalia huku na kule, …kama vile
anahisi kitu, halafu akasogea karibu na kabati akaweka kiti na kusimama, na kwa
juu, akanyosha mkono, na kuchukua kikasha kidogo cha kuwekea pini za ofisi
akakigeuza nyuma na akatoa kitufe kidogo.
‘Kumbe bado kipo, nilikiweka
mimi hiki kitufe, nia ni kujua kila kitu unachokifanya..’akasema.
‘Bado sijakuelewa, …umavitoa
hivi vitu hapa na kuvimwaga juu ya meza yangu, na sijui ni vitu gani,
hujaniambia wewe ni nani na huyo mzee, aliyemzungumzia ni nani, niambie wewe ni
nani ili tuweze kuelewana?’ akauliza mwanadada kwa suti ya ukali.
‘Mimi ni mtu wa karibu wa
mshitakiwa mkuu wa hiyo kesi yako, na ninaweza kusema kila jambo ambalo linahusu
usalama, ufuatiliaji, na…na, na….aaah’ pazia la dirisha lilitikisika kuonyesha
kuwa kulikuwa na mtu kalifungua kwa haraka, na mlio mdogo, ukasikika na harufu
ya risasi ikatapakaa ofisini, na mwanadada akawa kama anainama kukwepa, halafu
akainua uso kumwangalia mwenzake ambaye alishadondoka chini….
Akatoka pale alipokuwa
amekaa, na taaratibu aksogelea pale dirishani na kufunua pazia kwa taratibu, na
lilipofunguka usawa wakuona kitu akagundua,…..sehemu iliyokatwa kwa
ustadi,…halafu akasikia mtu akiguna, akageuka, na akagundua kuwa ni huyo jamaa
yake, alikuwa kalala chini,akilalamika
maumivu … atakuwa kapigw risasi, anainama kumchunguza, ni kweli alikuwa kapigwa
upande wa kushoto, kwa nyuma, na kitendo hicho kilichofanyika kwa haraka, na
huyo mtu alijua ni nini anakifanya, huenda alishajiandaa, na huenda muda wote
alikuwepo hapo….
Mwanadada hakuriski,akarudi
pale kwenye dirisha na kuchunguza kwa makini akalifungua lile pazia, na lile
dirisha lilikuwa limezungushiwa nondo na kuwekwa nyavu , alichofanya huyo mtu,
ni kukata nyavu sehemu ndogo na kuachia nafasi ndogo yakuweza kupenyeza mkono…sijui
hilo lilifanyika muda gani.Mwanadada akajaribu kuanglia nje, lakini hakuona
mtu, na walinzi walikuwa kwa mbele ya nyumba, huku nyuma, kulikuwa kimiya.
Mwanadada akawazakuwa awaite
walinzi, lakini akaona kuwa ni muhimu afanye kazi moja ya haraka, kwani walinzi
wakifika hapo atakosa kila kitu, kwanza alimkagua huyo jamaa, ambaye kwa muda
huo alikuwa katulia kimiya pale sakafuni huku kalala kicha kuelekea chini huku
kaegeme mikono yake, na sehemu ya nyuma ambapo risasi ilipenya, kulikuwa
kunavuja damu …na hapo mwanadada, akaona fanye jambo kumsaidia huyo mtu, kwa
wakti huo alikuwa keshavaa soksi za mikononi,…akatoa kitambaa chake na kukiweka
kwenye lile tundu la risasi na kujaribu kulzina lile shimo la risasi.
‘Aaah, naona
wameniwahi….’akawa anasema kwa maumivu.
‘Ni akina nani hawo?’akauliza
mwanadada.
‘Huyu anaweza akawa mmoja wa
….wa….wa, ..aaah’ akashindwa kumalizia, mwanadada akamsogelea na kujaribu
kumweka vyema, na alihisi huenda keshafariki, na alipopima mapigo ya moyo kwa
vidole viwili, aliona bado yupo hai, alikuwa kapoteza fahamu tu, na damu zikiwa
zikitoka kwenye jeraha hilo la risasi, na mwanadada alitakiwa kufanya haraka
kumuita dakitari, ili kama ikiwezekana aweze kumuokoa huyo mtu…akachukua simu
na kumpigia dakitari mmoja anayemfahamu, alipomaliza akampigia mkuu wa usalama,
aliyepangiwa kulinda eneo hilo.
Akarudi pale mezani na
kuvitumbukiza vile vitu alivyopewa na huyo jamaa kwenye mfuko wa plastiki na
kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa, akachukua ile briefcase ya yule mtu, na nakuifungua
ndani kulikuwa na bastola, ….na vifaa vya kurekodia sauti…akavitoa na
kuvitumbukiza kwenye mfuko huo wa plastiki, alihakikisha kuwa havigusi kwa mkono
wake , kwani alikuwa kavaa sokosi za mikononi.
Akatoka nje na kumuita mmoja
wa walinzi, na huyo mlinzi alipofika, huyo mlinzi akauliza.
‘Kuna tatizo lolote bosi….?’
Akauliza huyo mlinzi
‘Huyu jamaa kapigwa
risasi,…na nina uhakika kazi hiyo imefanywa na mmoja wa walinzi wenu, kwani
haiwezekani, mtu apite hapo bila nyie kujua,, sasa hakikisheni walinzi wote
wanashikiliwa na kukaguliwa silaha zao, ….’akamwambia huyo mlinzi, ambaye
alikuwa kama kashituliwa na umeme.
‘Haiwezekani, kapitia wapi,
nyuma kote huko kuna ukuta,…na na, hebu ngoja kwanza, …’akasema na kukimbili
huko nyuma na baadaye akidogo akarudi akiwa anahema kuonyesha kuwa alikuwa
anakimbia, na wasiwasi ulikuwa umemjaa, akifahamu kuwa hapo atalaumiwa yeye
kama mzembe, na huenda akingia matatani na wakati huo yule docta aliyepigiwa
simu na mwanadada,a likuwa ameshafika.
‘Hapo ndani kuna jamaa
kapigwa risasi, nijuavyo, hawa watu wa
usalama watachelewa kufika, mfanyie huduma ya kwanza, hakikisha huachi alama
zako za vodole…..’akasema na huyo dakitari ambaye ilionekana kuwa kazi kama
hizo keshazifanya sana, akaingia ndani, na haikuchukua muda akatoka.
‘Kila kitu kipo safi, …ila anahitajika
kuwahishwa hospitali haraka iwezekanavyo, kwani…..bado yupo hai…’akasema huyo dakitari
‘Naweza kuongea naye kidogo,
maana wakija hawa waheshimiwa sitaweza kuongea naye tena,…..?’ akauliza
mwanadada.
‘Unaweza…mmh, ngoja nione
cha kufanya…’akasema na wakaingia ndani na mwanadada, na huyo dokitari
akafanya mambo yake na huyu jamaa akawa kama anakoroma.
‘Halloh, unanisikia,mimi ni
mwanadada, hebu niambie ni nani aliyekupiga risasi…?’ akauliza mwanadada,
lakini yule jamaa alikuwa kama anakoroma tu, na dakitari akasema;
‘Anaweza akaongea,hapo
inahitajia muda, mmh …lakini hujaniambia, maana hii sasa ni kesi ya kutaka kuua
au mauaji,..kwahiyo unaniambia nini, nisubiri polisi wafike au niondoke?’ akauliza.
‘Subiri polisi wafike….’na
kabla hajamaliza wakasikia yule mtu akiwa anaweweseka, na hapo mwanadada
akamsogela na kumsikiliza
‘Nenda haraka kao-ongee na yule dereva a-a-ali-yetaka
ku-ku-ku-kuua,…ana mengi za-idi, mmh, ooh, lakini usimwa-mini mtu yo-yote, hasa
polisi…aaaaah, …’akatulia, na mwanadada akasikia mlango ukigongwa na mkuu wa
polisi,akiwa na watu wake walifika.
‘Oh,…yaani umeshamuita
dakitari,..kwanini umefanya hivyo huoni utatuharibia taratibu zetu……..’ akaseama
huyo mkuu wa kituo.
‘Tangu niwaite nyie,…
mumetumia muda gani, huyu mtu yupo kwenye hali mbaya, anatakiwa kuwahishwa
kwenye matibabu, ni lazima nifanye jambo ili kumuokoa..’akasema mwanadada.
‘Natumai hamjaharibu
ushahidi, na wewe dakitari, usiondoke maana umeshajitumbukiza kwenye kesi hii,
utawajibika….’akasema huyo mkuu wa polisi, kuonyesha kukerwa na kitendo
kilichofanyika.
‘Mimi nashauri huyo mtu
awahishwe hospitali, hali aliyo nayo anahitajia upasuaji wa haraka, ili tunaweza
kumuokoa…’akasema huyo dakitari
‘Hiyo sio kazi yako
kwasasa….’akasema huyoo mkuu wa kituo cha polisi, huku akiwaonyeshea vijana
wake waanze kazi.
‘Mimi kama dakitari
nimekuambia hilo, ili liwe kwenye kumbukumbu zenu, ili nikitoa ushahidi wangu
itambulike nilisema hivyo, na wakili yupo hapa atathibitisha hivyo…’akasema
huyo dakitari.
‘Hivi wewe unajiona unajau sana
kazi kuliko sisi, unafikiri mimi hii kazi nimeanza leo,….tusifundishane kazi..hayo
yafanye ukiwa kwenye anga zako, hii hapa ni anga yangu, tusiingliane,
eeh,…kwani hata hukuhitajika kuwepo hapa kwani sisi wenyewe tumekamilika, nina
dakitari wangu atafanya kila kitu, kama ni mtu wa kufa atakufa tu….’akasema
huyo mkuu wa kituo cha polisi.
‘Kama mtamuwahisha hospitali
mnaweza mukamuokoa, na anaweza kupona, lakini, mnavyozidi kupoteza muda hapa,
mnamuweka katika hali mbaya sana, hilo nawashauri mimi kama dakitari…’akasema
tena.
‘Hatuwezi kumchukua haraka
hivyo, ….kuna mambo yanatakiwa yafanyike kwanza, au kuna mambo mumefanya, hapa,
mnataka yasionekane naanza kuwatilia mashaka …’mara simu yake ikaita na
alipoangalia na kuona jina la mpigaji, akatoka nje kwa haraka.
Mwanadada alipoona huyo mkuu katoka kwa haraka, aligeuka kuwaangalia waliopo humo ndani, na aligundua kuwa kila mmoja alikuwa akihangaika na shughuli yake, na yeye kwanza akajifanya kama anataka kupiga simu na taratibu akatoka nje.
Baadaye yule
mkuu wa kituo cha polisi akarudi, na alipoingia akawa anawaangalia watu wake
wakiendelea na kazi, na akawa anawahoji mmoja mmoja, kuwa ni nini wamegundua, na sasa wanaendelea na jambo gani,baadaye akamsogelea yule dakitari, na kuanza kumhoji;
‘Nitahitajia maelezo
yako…’akaanza kusema
‘Hamna shida mkuu…’akasema
huyo dakitari na mara mkuu huyo akageuak huku na kule akitafuta jambo, na
akasema;
‘Huyu wakili mwanadada yupo
wapi?’ akauliza kwa mshangao.
‘Anapiga simu….’akasema huyo
dakitari.
‘Ni nani kamruhusu kufanya
hivyo, mbona mnafanya mambo kienyeji enyeji…’akasema kwa hasira na mara
Mwanadada akingia huku akiwa bado kashikilia simu kuonyesha kuwa alikuwa
kiongea na mtu, na hapo alikuwa akikata hiyo simu.
‘Wewe ni nani kakuruhusu
kutoka nje…na kupiga simu…’akasema kwa hasira akimwangalia huyo mwanadada.
‘Sikumbuki kuniambia kuwa
siruhusiwi kupiga simu, au kupokea simu…’akasema mwanadada.
‘Ina maana wewe hujui kuwa
hayo hayaruhusiwi kwa mshukiwa wa mauaji, huoni wewe upo kwenye kundi la
mshukiwa wa muaji…’akasema huyo mkuu.
‘Oh, nimeshakuwa mshukiwa
tayari, basi nifungeni pingu…’akasema mwanadada akinyosha mikono yake, na yule
mkuu akamwangalia kwa macho yaliyojaa hasira, na kusema;
‘Wewe binti, unajua, …ipo
siku …’akashindwa kumalizia kwani simu yake iliita na yeye akaipokea bila
kuangalia mpigaji na aliposikia sauti, akageuka kumwangalia mwanadada na
kusema;
‘Baadaye….’akakata simu.
Mwanadada akamwangalia huku
akitabasamu, tabasamu la dharau, huku akiangalia pembeni na kusema;
‘Naona wewe unarushusiwa
kuonga na simu, lakini mimi kama mshukiwa siruhusiwi, kwanini uanogopa kuipokea
hiyo simu?’ akauliza mwanadada na huyo mkuu wa kituoa akakunja uso kwa hasira
akasema;
‘Ni nani kaumabia kuwa
naogopa kuipokea, kwanini niogope, huoni hapa tupo kazini, na nikikalia kupkea
simu, hatutaweza kufanya kazi….’akasema huku akiangalia saa yake.
‘Sawa mkuu, ujue tupo
pamoja, mimi haps sifanyi kazi ya uwakili binafasi, nimeombwa na serikali
kusaidi hii kesi, na nahisi kuna watu wa serikali wanahusika..watu weye
dhamana…’akasema mwanadada.
‘Kwanini unasema hivyo,
unajua nini wewe….wewe kazi yako ni huko mahakamani, hii hapa ni kazi yetu,
kama kuna watu wanahusika, tutawagundua tu,…usitie shaka, mimi ninajua ni kitu
ninachokifanya….’akasema.
‘Sawa mkuu, ..halafu sikujua
kuwa wewe na kiongozi wa kijiji, mna mahusiano…’akasema mwanadada, na yule
mkuu, alishituka, kiasi kwamba kile aliyemuona alihisi hivyo.
‘Eti nini….wewe unaota
nini….kwanza hebu tokeni nje tifanye kazi yetu, tutawaita tukimaliza..’akasema.
‘Cha muhimu kwa vile
mumeshachukua picha muwahisheni huyo mtu, labda kama hamtaki aishi…’akasema
yule dakitari na huyo mkuu akamwamgalia kwa hasira na kusema;
‘Hiyo sio azi yako, tokeni
nje haraka…’akasema
‘Mimi kama dakitari,
niliyemuona huyo mgonjwa , nahitajika kukaa hapa ili nihakikishe, …maana loloye
linaweza kutokea, nikasingiziwa mimi…’akasema huyo dakitari na huyo mkuu, akiwa
kama kachanganyikiwa akasema;
‘Haya kaeni,….’akasema na
yeye akatoka nje, na baadaye akaingia na wakati huo yule mtu aliyepigwa risasi
alikuwa akiwekwa kwenye machela huku akiwa katundikiwa dripi ya kumsaidia na
huduma nyingine zinastahiki
‘Muwahisheni hospitali
,maana naona hawa tu wanataka kuniharibia kazi, ….’aaksema huyo mkuu, huku
akiwageukiwa mwanadada na dikatari..
‘Haya niambieni ilikuwaje…
*************
Mwanadada akiwa yupo kituo
cha polisi, kwani ilibidi afike hapo kutoa maelezo kama alivyoamriwa na mkuu wa
kituo cha polisi, na aliruhusiwa kuondoka, kwa kujidhamini yeye mwenyewe, na
kabla hajaondoka akapitia kitengo cha upelelezi, na huko akakutana na mkuu wa
kitengo hicho .
‘Naona niongee na wewe
haraka, huu mzigi hapa, naomba uuhifadhi, na kama ikibisi tutafute sehemu ,
kuna mambo hapa yakifika kwa hapa jamaa, hatutayaona tena..’akasema wakili
mwanadada., na mkuu huyo akaangalia vile vitu, na alikuwa kama anaogopa
kuvigusa.
‘Huoni hilo ulilolifanya ni
hatari…umevuruga taratibu za kipolisi…’akasema.
‘Hilo nalifahamu sana,
lakini kama nisingelifanya hivi, mengi yanayohitajika kweney hii kesi
yangelipotea, kama nilivyowahi kukuambia, mimi siamini kituo chenu
hiki…’akasema wakili mwanadada.
‘Nafahamu hilo,
lakini….’akasema na kuvaa soksi za mikononi, na akaanza kuvitoa vile vifaa, na
alipoiona ile bastola, akashituka,…akawa anaishika kwa uangalifu sana, huku
akiwa kakunja uso, na alipoikagusa, akaichukua na kuiweka kwenye platiki, ikiwa
peke yake.
Akatoa chupa, iliyokuwa na
itu kama soda au juisi,, akaiangalia kwa makini, na halafu akageuka kumwangalia
Mwanadada, akasema
‘Hii sio soda, na kama ni
soda, itakuwa imechanganywa na kitu kingine….’akasema
‘Hata mimi nahisi hivyo,
na ni moja ya vitu alivyotaka nivichukue
huyo mtu kabla hajapigwa risasi, nahisi kuna jambo linalohusiana na hiyo soda
isiyotambulikana…’akasema na huyo mkuu akaiweka kwenye mplastiki na kuandika
kitu juu yake
‘Inabidi ifanyiwe uchunguzi
wa haraka…’akasema na kuendelea kuchunguza vitu vingine, na zile DVD, akawa
kaziacha mezani, halafu akasema;
‘Naona hapa kwasasa hakuna
usalama, ….lakini moyo nahisi tutakuwa tumefanya kosa, kama hatutamshirikisha
mkuu wa kituo…’akasema.
‘Kama nilivyokuambia, na
kama hisia zangu zilivyokuwa toka awali, huyo mkuu, usimwamini tena, …nakuhakikishia
hilo, maana nimemsikia mwenyewe akiongea na simu…’akasema mwanadada na mara
mlango wa mkuu huoo huyo ukagongwa, na ulipofunguliwa mkuu wa kitua akaingia na
alipomuona huyo mwanadada, akashituka.
‘Ina maana bado wewe upo?’
akauliza.
‘Mkuu, mbona huniamini,
nimeshakuambia kuwa mimi nipo pamoja na nyie, kama mkinitenga, nitaweza kufanya
kazi yangu, au umesahau kuwa mimi ni wakili uapnde wa serikali kwenye hii kesi,
…’akasema mwanadada.
‘Ni sawa, lakini inapokuja
katika mambo ya usalama, hata kama ni askari wetu, kakutwa kwenye tukio kaam
hilo lililotokea kwako, hatuwezi kumwamini tena, mpaka ithibitishwe
vinginenvyo,….’akasema.
‘Kwahiyo hata huo uwakili
niuache, mana hamuniamini…’akasema
‘Sijasema hivyo…’akasema
huyo mkuu, na akawa anaziangalia zile DVD, juu ya meza ya mkuu wa kitengo cha
upelelezi, hakusema kitu, akageuka kutaka kuondoka.
‘Mkuu, nilijua kuwa umekuja
kuniona,…’akasema mkuu wa kitengo hicho, lakini huyoo mkuu akawa keshatoka nje.
‘Nahisi anafahamu jambo
kuhusiana na hizi DVD,..naona tufanya jambo la haraka, kabla
hazijapotea,…’akasema huyo mkuu, na akachukua laptop yake na kuanza kuzinakili
kwenye laptop yake na kuhakikisha
zimenakiliwa vyema, halafu akazichukua na kuziweka kwenye mfuko wa palatic, kwanza
akatafuta DVD, nyingine tupu, akaziandika kama kama vile zilivyoandikwa hizo
DVD, nakuziacha pale juu ya meza, halafu yeye na mwanadada wakaondoka, wakiwa
wamechukua mzigo wao
********
‘Hebu niambie ilikuwaje?’
akauliza mkuu huyo walipofika nyumbani mwa mkuu huyo, na wakawa wanaanza kuangalia
ni kitu gani kipo kwenye ile DVD,
‘Ninachoshukuru mungu, ni
kuwa nipo salama, nahisi aliyefanya hivyo, hakuwa na lengo la kunimaliza mimi,
….alikuwa na lengo la kummaliza huyu mtu..na hili linanipa wazo kuwa adui yetu
huenda tunaye…’akasema.
‘Una maana gani?’ akauliza
huyo mkuu
‘Wewe huoni, kiongozi wa
kijiji, yupo ndani, ..asingeliweza kuongea na hawa watu na kutoa amri hili
lifanyike…..na ni nani alijua kuwa nitakutana na huyu mtu,…niliyemwambia ni
mkuu wa kituo na wewe…’akasema na kutulia kidogo, halafu akakumbuka,
‘Kuna kifaa kilipandikizwa kwenye
ile ofisi niliyokuwa nikiitumia, na aliyekiweka na huyo huyo jmaa aliyepigwa
risasi, sasa sijui ,,….huenda kuna vifaa vingine zaidi, kwahiyo hawa watu wananifuatilia
kwa karibu sana, na sio watu wa kawaida kama tunavyofikiria,….’akasema
mwanadada.
‘Sawa nimkuelewa mwanadada,
hilo niachie mimi,…mimi mwenyewe sipaamini tena hapa, na nafanya kazi katika
mazingira magumu sana…nilipoongea na bosi wangu, aliniambia ataniongezea nguvu,
kwahiyo wale vijana, waliokuja na mkuu wa kituo, ni hawo waliotokea Dar, nina
imani nao, watagundua kila kitu, mimi najifanya sihusiki moja kwa moja..’akasema
huyo mkuu wa kitengo cha upelelezi cha kituo hicho.
‘Umefanya la maana sana…kuviwahi hivi vitu, na
pale ilibidi nikuambie hivyo, maana nahisi hata pale ofisini kuna vinagalizi
vya nyendo zangu….’akasema huyo mkuu wa kitengo cha upelelezi
‘Kwanini?’ akauliza
mwanadada.
‘Kuna mambo yanaendelea hapa
na hata mimi yananitia wasiwasi, na kuna pendekezo kuwa nihamishwe kituo hiki,
lakini nimeweza kuongea na bosi wangu huko juu, na kumwelezea hali halisi,..na
kwa kuniamini ndio akanitumia hao vijana, na mimi nawaamini maana nilishawahi
kufanya nao kazi nikiwa huko Dar, na nina uhakika watagundua mengi, lakini
…huyo mkuu wa hapa, mmh, siwezi kusema neno, mpaka hapo uchunguzi
utakapokamilika…’akasema.
‘Hata mimi nimeshamtilia
mashaka,…maana haya matukio yanayotokea kukiwa na walinzi, ..haiwezekani,
nahisi kuna jambo, angalai yule mtu aliyetaka kunigonga, eti imegundulikana
kuwa hana hatia,a likuwa ni mlevi tu, mimi sikukubaliana na hilo, nab ado
nalifanyia kazi….’akasema mwanadada.
‘Nitakuja kukuambia jambo
kuhusiana na hilo, lakini sio leo…’akasema huyo mkuu
‘Unajua kuwa nimegundua
jambo jingine, wakati nasikiliza simu, ya huyo mkuu, akiwa anaongea na mtu
mwingine,…’akasema mwanadada.
‘Umegundua nini?’ akauliza
huyo mkuu
‘Huyo mkuu wako, inasemekana
wanaudugu na Kiongozi wa kijiji….mshitakiwa
mkuu’akasema wakili mwanadada.
‘Unasema kweli…!!!, mamamama,
mbona huyu mkuu, nijuavyo mimi, kwao ni mikoani,..na hata kumbukumbu zake
zinaonyesha hivyo…’akasema huyo mkuu wa kitengo cha upelelezi.
‘Nimesikia kwa masikio yangu
mwenyewe,….’akasema mwanadada
‘Kwani wewe uliskia ninii,
cha kukuhakishia kuwa wana udugu, na huo udugu ni wa namna gani?’ akauliza huyo mkuu
‘Kiongozi wa kijiji ni baba
yake huyo bosi wako,…’akasema mwanadada.
‘Haiwezekani…labda awe ni
baba kutoka kwa nyumba ndogo…’akasema huyo mkuu wa upepelezi.
‘Mhh,…labda, …’akaguna
mwanadada na hapo ile DVD, ikaanza kuonyesha mambo, na kuwafanya watulie kuiangalia,
hawauamini ….
Nb: Mambo yanazidi mambo…ni
nini kimegundilikana tena, je kesi hii itakuwaje, …angalia dhamana
zinavyochezewa sababu ya umimi, udugu,
ukabila….
WAZO LA LEO: Usije ukajidanganya kuwa wewe kwa vile ni muheshimiwa,
au mkuu, uliye na dhamana, unaweza kufanya lolote ukiegemea wadhifa wako, ukawa
unatenda madhambi ya kudhulumu, kuficha maovu ya ndugu zako, au ya jamaa zako,
au kabila lako,..na wengine wanafikia hdi kuua, eti kuondoa ushahidi…kamwe
usidhanie kuwa jambo hilo litaisha kiujanja ujanja tu.
Dhambi kama hiyo itakuandama
milele, kwani siku zote uliowatendea hizo dhambi, ukawadhulumu, nafsi zao
watakuwa wakimlilia mola wao,…na kila mja ana haki yake, na mola ni kwa wote,
kwanini wasisikilizwe..ndugu yangu, jiepushe na dhambi kama hizo, maana kuua nafsi moja bila ya
haki ni sawa nakuuwa nafsi za watu wote.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Mmh emu 3 upo juu Sana batsman hata isiishe km nachek movie vile,
mmmmhhh nasubiri kwa hamu kuona kulikuwa na nini kwenye DVD....ila jamani tuaache ukabila, umimi na undugu tuwe kitu kimoja
Post a Comment