Baada ya ile DvD ya mwanzo kumalizika, Mwanadada akageuka kumwangalia
huyo mkuu wa kitengo cha upelelezi, na yule mkuu alikuwa bado yupo kwenye
mshangao kwa yale alyoyaona kwenye DvD hiyo na badala ya kuongea yale
aliyoyaona kwenye hiyo Dvd, huyo mkuu akawa anaongea jambo jingine kwa kusema;
‘Jana nilikuwa nakutafuta sana….’akasema huku akiitoa ile DVD kwenye
laptop yake na kuhakikisha kaihifadhi vyema kwenye mfuko wa plastiki.
‘Ulikuwa unanitafutia nini,
kwanini hukunipigia simu,…ndio nakumbuka niliona ujumbe wa kwenye simu yangu,i lakini
sikuwa na uhakika ujumbe huo umetoka
kwanani,…ila kwa sasa ndio nimegundua kuwa kweli ulitoka kwako, kwasababu namba
iliyotumika ni ngeni kwangu, ni kwanini ukatuma huo ujumbe wa maneno kwenye
namba ya simu isiyo ya kwako…. ?’
‘Sikujua kuwa sina salio
kwenye simu yangu , kwani nilisha-andika huo ujumbe kwenye simu yangu, na
nilipotuma nikagundua kuwa salio halitoshi, ndio nikaamua kuutuma huo ujumbe
kwenye simu nyingine, …sikupenda kujiandika mimi ni nani, nikijua kuwa utaelewa
kuwa ni mimi…’akasema huyo mkuu.
‘Kwa hali ilivyo sasa,
inahitajika kuwa muangalifu, …..sikupenda kubahatisha, kwani kama ungelikuwa na
umuhimu na mimi nailijua ungenipigia simu…’akasema mwanadada.
‘Ndio mimi niliyekutumia huo
ujumbe,.. hiyo namba ni ya mke wangu, ambayo huwa haitumii mara kwa mara….nilikuwa
nayo kwa muda ule’akasema huku akichukua ile DvD, nyingine, na akawa anaitoa
kwa makini kwenye kasha lake.
‘Ulikuwa unanitafuta kwa
jambo gani,….maana nakumbuka uliniambia nisiwe nakutana na wewe mara kwa mara,
nina imani ulikuwa na jambo muhimu sana, japokuwa hukusisitizia…usilete ule
utani wako…?’ akauliza mwanadada huku akitabasamu.
‘Hapana huo sio utani, hata
hivyo, baadaye niliona hakuna umuhimu kwa hilo, kwani nilikuwa nimekutana na
jambo jingine muhimu zaidi….’akasema huyo mkuu.
Mwanadada, akawa akawa
anajaribu kuyachuja mambo kwenye akili yake, kama singelikuwa heshima kwa huyo
mkuu, angemwambia atulia kwanza, kwani kuna kitu muhimu anataka kukiwaza,…lakini
kwa heshima ya huyo mkuu, akaendelea kama atakavyo huyo mkuu.
‘Ni kuhusu hukumu ya kesi ya
mwanadada…’akasema huyo mkuu wa askari kanzu na mwanadada ikabidi ayapuuze
mawazo aliyokuwa nayo mwanzoni na kumgeukiwa huyo mkuu, na wakawa wanaangaliana,
na huyo mkuu akageuka pembeni kama vile
hataki huyo mwanadada ajue hisia zake.
‘Kuna nini kuhusu kesi ya
mwanadada,…kwani nijuavyo mimi, bado hukumu haijatolewa…. ?’ akauliza
‘Hukumu ilishapitishwa, …kama
ujuavyo kuwa yule hakimu alishaisikiliza kilichokuwa kimebakia ni kutoa hukumu
mbele ya mahakama, na kwa bahati mbaya, aliondoka kabla hajaitoa mahakamani…’akasema
huyo mkuu.
‘Ndio lakini hiyo hukumu ni
siri, mpaka itolewe mahakamani, sasa ilivujaje?’ akauliza mwanadada.
‘Kama ujuavyo huyu hakimu
alihamishwa kwa haraka sana, kiasi kwamba hakupata muda, wa kukabidhiana na
mwenzake, ….sasa sijui wakati anaondoka, ndipo mambo haya yalifanyika, au ni
yeye mwenyewe alifanya hivyo, hapo nashindwa kuelewa maana namuamini sana yule
hakimu, asingeliweza kufanya hivyo..’akasema huyo mkuu.
‘Sijakuelewa bado….’akasema
mwanadada huku akiendelea kumwangali yule mkuu, ambaye alikuwa kaangalia
pembeni.
‘Lakini hata hivyo,
hakijaharibika kitu, maana huyu hakimu mpya kaona aipitie hiyo kesi upya, na mimi namuunga mkono kwa wazo hilo,
ili kuondoa utata….’akasema.
‘Bado mimi sijakuelewa,…..’akalalamika
mwanadada.
‘Unajua ilibidi hukumu hiyo
ivuje, na hata mimi nisingeliweza kulifahamu hilo, lakini hakimu hiyo alituita
upande wa usalama, na kuongea na sisi, …kwani alifanya hivyo,….. kumbe
alishaisikia hii kesi wakati yupo huko alipokuwa, na yeye alikuwa na kesi kama
hii, inafanana kwa kila kitu, unajua sasa hivi akina mama wameamuka kudai haki
zao, na yeye aliweza kuhukumu vyema huko alipotoka,....’akatulia.
‘Nakusikiliza mkuu….’akasema
wakili mwanadada, kwani hadi hapo alikuwa hajathibitisha ni nini hasa
anachotaka kusema huyo mkuuna hakutaka kumuhoji kama mahakamani .
‘Alipofia hapa na kuliona
hilo jalada la kesi hiyo, akashangaa …hakuamini, ikabidi akutane na wazee wa
mahakama, na wahusika waliosimamia hiyo kesi…’akasema.
‘Wazee walikubali kuwa hiyi
ndio hukumu halali,…ila kuna baadhi wakawa hawakubaliani, na hapo ikatia shaka,…na
akaanza kufanya uchunguzi wa kwake binafsi, hakimu huyo sio mchezo,
hakukubaliana na wazee, waliosema kuwa hukumu hiyo lipitishwa, kutokana na
taratibu za mila na desturi…’akasema
‘Hakimu hakukubali, akaanza
kufuatilia mwenyewe, ….na hapo akaanza kujenga chuki na baadhi ya wazee ya mahakama hiyo,na baadhi ya wahusika wengine kwenye ngazi za serikali kwenye kanda
yetu hii,na hili limeshaanza kujitokeza wazi, kwani analalamika kuwa hapewi
ushirikiano wa karibu, kitu ambacho anahisi kuwa kuna jamboo kubwa limejificha….’akasema
‘Mimi nimemshauri,….na wengi
wameona hivyo, kuwa ili kuondoa fitina kesi hiyo isikilizwe upya…’akasema huyo
mkuu.
‘Mkuu, samhani kidogo, kwani
hukumu ilisemaje?’ akauliza Mwanadada, kwani ile DvD ilitaka kuanza, lakini
akaisimamisha ili ikianza wawe wametuliza mawazo yao na kuona kilichopo. Mkuu huyu
akatulia kwa muda kama anawaza jambo huku akiwa anaangalia ile laptop, kama
vile anasubiri hiyo DvD ianze kucheza, na baadaye akamgeukia mwanadada, na
kusema;
‘Pesa sio mchezo, nasema
hivyo, kwasababu sioni kuwa kuna sababu nyingine ya kuweza kumbadili mtu, na
kuiacha haki na ukweli kama sio pesa,labda kuna mambo yalitokea, lakini ….nilipopitia,
na kuchunguza eneo hili, nimeona kuna mchezo mbaya unachezwa kwenye kanda yetu
hii,…lakini hata hivyo,sio kwa yule hakimu, namfahamu sana, huenda kuna jambo
kubwa zaidi ya hilo….’akasema huyo mkuu.
‘Hata kuhamishwa kwake, sio
kwa kawaida….’akasema mwanada kusisitizia hilo.
‘Ndio hivyo…hata yeye
mwenyewe alishangaa…’akasema huyo mkuu
‘Ina maana alishitukizwa…na
je wakati anaondoka, uliwahi kumuuliza kuhusu hiyo hukumu?’ akauliza.
‘Mhh, hapana nisingeliweza
kumuuliza kitu kama hicho, kwani najua sheria za kimahakama, hiyo ni siri, hadi
hapo itakapotolewa mahakamani,…lakini ndio hivyo, yeye alipata barua usiku, na
kesho yake anahitajika kwenda kwenye kitu kingine, eti kwasababu kuna kesi
kubwa anahitajika akaisimamie…na huko ndio kutakuwa kituo chake cha kazi…’akasema
mkuu huyo.
‘Sasa kama ni hivyo, huoni
kuwa kama ni mchezo mchafu, utakuwa unawahusu wakubwa zaidi yake, labda na yeye
awe anahusika….?’ Akauliza.
‘Nilipoangalia hii DvD, ….naona
tunahitajika kuwa waangalifu sana,…na nakushauri, kukutana kwetu kuendelee kuwa
kwa nadra, na usimwamini mtu yoyote kwa sasa…kuwa makini zaidi ya tulivyokuwa, na
tujitahidi hi kesi ifanyike kwa haraka iwezekanavyo, kabla ushahidi haujapotea
kabisa….’akasema.
‘Lakini hujaniambia hukumu
hiyo ilikuwaje? Akauliza mwanadada, pale mkuu huyo alipoaka kuicheza ili Dvd,
na mkuu huyu akatulia, na kuuondoa mkono wake, kwenye sehemu ya kuianzisha hiyo
DvD.
‘Mwanamama, alishindwa
kwenye hiyo kesi…’akasema huyo mkuu.
‘Eti nini, haiwezekani
kabisa, …’akasema mwanadada, akimtolea macho huyo mkuu.
‘Hukumu aliyoikuta huyo hakimu, ilionyesha
kuwa Mwanamama, alikuwa kashindwa kwenye hiyo kesi, na y a kuwa alitakiwa
kukabidhi mali zote kwa wanafamilia, ….’akasema
‘Haiwezekani, …..haiji
akilini hata kidogo, ina maana huyo hakimu ndivyo alivyohukumu hivyo, sizani
kama yule hakimu ndio yeye aliyehukumu hivyo sizani…hapo kweli kuna jambo…..’akasema mwanadada.
‘Sasa kama huamini, ….nenda
kaumuulize mwenyewe huyo hakimu,…hata hivyo, huyo hakimu kasema ataipitia upya
hiyo kesi, na ili kuondoa utata, anataka isikilizwe upya…na ndivyo hata sisi
tulivyomshauri…’akasema
‘Isikilizwe upya kwasababu
ipi..tuangalie na sheria, maana huwezi kusema kesi inasikilizwa upya, bila ya
sababu za kimsingi…’akasema mwanadada.
‘Sababu ndio hizo…kwanza
hakuna anayejua hukumu ilikuwaje,kwani haijasomwa mahakamani, haya tunayaongea
kama uvumi….ujua hilo,…..’akasema huyu mkuu, akimwangalia mwanadada.
‘Na hata hivyo sababu
zinaweza kutafutwa, hakishindikani kitu, na kwa vile sisi tunaona kuna umuhimu
wa hilo, mimi naona bora iwe hivyo,,…hata mimi nilimshauri afanye hivyo, kwani
kama ingelitolewa hukumu hiyo iliyokuwa imetolewa, sizani kama kungelikuwa na
amani…na akiitoa yeye, unafikiri jamii itasemaje,…yeye ndiye kahukumu hivyo,sio
mwenzake aliyeondoka…’akasema huyo mkuu wa upelelezi.
‘Kumbe ndio maana hawo jamaa
walikuwa wakitamba…..lakini hapo najiuliza je hawa wenzetu walijuaje kuhusu
hukumu hiyo, kuwa wameshinda, huoni kuwa kulikuwa na njama….aah,…’akasema
wakili mwanadada akiwa kavunjika nguvu, na akaianzisha ile DvD ya pili ianze kuonyesha
‘Mimi nitang’ang’ania nione
hiyo hukumu ya mwanzo, na hapo ndipo nitakata rufaa kwenda mahakama ya juu,
najua hapo haki itapatikana vyema, lakini kwanza tumalizane na hi kesi yetu
inayotukabili…huenda ikasafisha kila kitu, na huenda hata kesi hiyo haitakuwa
na msingi wa kuskilizwa upya,…lakini he hukumu halali ipo wapi, maana nahisi
hiyo sio hukumu halali…?’ akawa kama anauliza mwanadada.
‘Mimi sioni haja ya kufanya
hivyo….kuwa asome hukumu hiyo aliyoikuta halafu wewe ukate rufaa, cha muhimu,
tumpe nafasi huyo hakimu mpya asafishe ofisi yake, mimi nina imani kuwa mahakama
na utendaji wa eneo hili utabadilika, na wale wote wanaoiharibu mahakama hiyo
na eneo hili kwa ujumla wataondolewa, mmoja baada ya mwingine….’akasema mkuu.
‘Mhh, ngoja tuona hii DvD
kwanza, maana inaanza kwa mbwembwe, na kama vile inatuonyesha hili
tunalolizungumzia…..samhani lakini mkuu’akasema mwanadada, na wote wakatulia
kuiangalia…
**********
Mwanadada ambaye alichelewa
kufika mahakamani, kama ilivyokuwa siku ya kesi iliyotangulia, alingia
mahakamani na kama kawaida baadhi ya watu waliokuwemo humo, walisimama kutaka
kumuona vyema, na hakimu akagonga rungu lake, kutaka utaratibu uwepo, na
ilionekana kuwa kulikuwa na malumbano ya wakili mtetezi na waendesha mashitaka.
‘Muheshimiwa hakimu, kwanini
kuna ukiritimba kwa hawa waendeshaji wa hii kesi, kwani huyo mwanadada ndiye
nani, mpaka tumsubiri yeye…’sauti hiyo ilikatishwa, pale mwanadada huyo alipoingia,
na ndipo watu wakainuka kumwangalia akiingia na hakimu kugonga rungu lake
kutaka utaraibu uwepo.
‘Samahani nimechelewa, kwani
ilibidi nikutane na mashahidi wapya waliojitokeza, na isingelikuwa busara
kuwasikiliza kwanza, kabla hawajasimama kutoa ushahidi wao, na kwa mtizamo huo,
naona tubadili kidogo, ratiba yetu, ….’akasema mwanadada,akiteta na wenzake.
‘Hakimu kakasirika sana,…’akasema
mwenzake.
‘Usijali, yeye mwenyewe
atakuja kurizika, akisikia ni sababu gani zilizonichelewesha,…hilo niachieni
mimi….’akasema
‘Sawa kwahiyo unataka
tumsimamishe nani kwanza?’ akauliza.
‘Mtamuona, hapa hata
mwenyewe nashindwa nimuanze yupi, maana wote wana umuhimu, ngoje, nione, ….’akasema
na kutuma ujumbe wa simu kwa mtu
anayesimamia mashahidi.
‘Lakini umesema kuna
mashahidi wamejitokeza, kwani w atatusaidia nini kwenye hii kesi, tunaongeza
mashahidi kabla hatujamalizana na hawa tulio nao, huoni kama tunajichanganya….’akasema
mwenzake.
‘Niamini mimi, ….hautujichanganyi
kabisa, wewe utaona, ….watakaochanganyikiwa ni hawo washitakiwa na wakili wao,….niamini
mimi …’akasema na sauti ya hakimu ikasikika na kumkatiza.
‘Haya tuanze, kesi yetu, na
natoa onyo kwa mara ya mwisho, kwa upande wa waendesha mashitaka, hii tabia
isirejee tena, hatuna muda wa kupoteza, kwa
kumsubiri mtu mmoja, …’akasema hakimu kwa ukali, na mwanadada akasimama
na kuinama kuonyesha unyenyekevu, akasema;
‘Ndugu muheshimiwa hakimu,
hali ya barabara zetu inajulikana, nilikutana na foleni, kwani kulitokea ajali
mbele yetu,…’akajitetea.
‘Wenzako walifika vipi hapa
acha vizingizio…haiyo haikubaliki…..?’ akauliza hakimu, lakini kabla mwanadada,
hajijibu, hakimu akasema;
‘Haya tusipoteze muda, tuendelee,
hilo nitalifanyia kazi baadaye, ….’akasema na mwanadada akatabasamu, akijua
kuwa hiyo ya kulifanyia kazi baadaye haitakuwepo tena siku ya leo ikiisha…
‘Ndugu muheshimiwa hakimu,
hatutamsimamisha shahidi wetu wa kesi iliyopita kama tulivyokuwa tumepanga,
kwani licha ya afya yake kuwa sio nzuri, lakini pia kuna mambo muhimu yamejitokea,
na tumeona ni muhimu sana kwenye hii kesi,afike shahid wetu mwingine …’akasema mwanadada
na wakili wa utetezi akatoa piangamizi.
‘Ndugu muheshimiwa hakimu,
kwanini wenzetu wanapenda kuvuruga utaratibu, …wanatufanay sisi tuwe na wakati
mgumu wa kujitetea, kwani tulishajiandaa kwa ajili ya shahidi aliyepita, ambaye
kwa maneno ya wakili muendesha amshitaka,alisema huyu shahidi ana ushaidi,
kwanini anaogopa kuutoa huo ushahidi….’akasema huyo wakili mtetezi.
‘Sisi ndio tunaoendesha hii
kesi, na hilo halitavuruga kabisa utaratibu wa hii kesi, na huyo shahidi
atasimama na ushahidi unaohitajika utawakilishwa, hilo lisikupe shida, ila kuna
ufafanusi wa hilo, …ambao ni muhimu uwekwe wazi …ndio maana tunamuhitaji
shahidi huyu atakaye simama sasa hivi….’akasema wakili mwanadada, na hakimu
akaingilia kati na kusema.
‘Naona tusipoteze muda, na
hakikisheni,kuwa huyo shahidi anaendeleza pale ulipoishia , na awe kweli anafafanua
hicho alichokuwa akiwakilisha huyu shahidi aliyepita, ni kweli nimepokea
taarifa kuwa shahidi aliyepita anaumwa, lakini dakitari kasema anaweza kufika, …ila
hataweza kuongea kwa muda mrefu,…’akasema hakimu.
‘Muheshimiwa hakimu, sisi
hatuna pingamizi na hilo, tunachohitajai ni ushahidi, …hasa kwa huyo shahidi
kujiweka wazi, maana jinsi alivyokuja kwenye kesi iliyopita, ilikuwa kama tunamsikiliza
shahidi aliyefichwa …..tunaomba huyo shahidi awe muwazi, tumone aje akiwa yupo
wazi, ili tuhakikishe kuwa ndio yeye kweli…’akasema huyo wakili mtetezi.
‘Hilo litafanyika,…’akasema
wakili muendesha mashitaka na hakimu akasema;
‘Haya muiteni huyo shahidi wenu
mpya….’akasema hakimu, na wakati wanasubiria huyo shahidi kuingia wakili mtetezi akainama kuongea na mteja wake,
na ilionekana walikuwa wakibishana jambo, lakini wakili huyo akawa anamtuliza
mteja wake.
Mlango wa mashahidi ukafunguliwa,
na mara akaingia shahidi, na watu wote wakashindwa kujituliza na wengine
wakasimama kumwangalia, na hata upande wa watetezi haukuweza kuvumilia,
walijikuta wakisimama, na kuhakiki kile walichokiona….
NB: Je unahisi huyo shahidi
ni nani?
WAZO LA LEO: Tetea haki, ukisimamia kwenye haki, bila kuogopa, kwani haki yenyewe itakulinda.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Haki ndio kila kitu Baba, haya ngoja tumwone huyo aliyeingia.
Post a Comment