Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 12, 2013

WEMA HAUOZI-20


 Mjukuu wangu, nilizindukana na kujikuta nipo hospitalini, nikiwa nimezungukwa na madakitari, kila mmoja akiwa na shughuli yake,….kwanza kwa akili ya haraka nilifikiria nipo ahera, lakini akili ilipotulia nikatambua nipo hospitalini kwenye chumba cha wagonjwa mahututi………..’nilikumbuka jinsi babu alivyonisimulia, wakati huo mama alikuwa katoka kidogo.

‘Mjukuu wangu, sijawahi kuumwa, kama nilivyoumwa kipindi hiki, …na iliniuma sana nilipofikiria kuwa kuumwa huku sio kuumwa kule kwa kawaida, ilikuwa kuumwa, kusababishiwa na watu wengine, watu waliotoka kuchukua haki za watu…

Nilifungwa muhogo(POP), na kushonwa jereha la kisu, …sikuamini kuwa kisu hicho hakikuathiri sehemu ya ndani ya mwili, maana siku ile nakumbuka nilihisi kisu kikipenya ndani, …lakini madakitari walisema hakuna athari yoyote ndani ya mwili wangu.

Sikiweza kabisa kusimama, au hata kuhema, kwani kila nikigeuza mwili, nilihisi maumivi kila sehemy ya mwili,….ilikuwa mateso yasiyomithilika, na kika mapigo ya moyo yalipokuwa yakipiga, ndio maumivi yalikuwa yakifuatilia mapigo hayo, hapo nikatamani roho itoke haraka ili niepukane na maumivu hayo. Na kwakweli ilifikia hatua, sikuweza kuvumilia tena, nikapoteza fahamu.

Siku nilipozindukana tena, niliambiwa kuwa nilipoteza fahamu kwa siku mbili, na kilichokuwepo akilini mwangu ni hiyo ndoto, ndoto ambayo kwangu iliniashiria kuwa huenda siku zangu za kuishi zimeshakwisha, kwani ndani ya ndoto hiyo nilijikuta nipo na mke wangu….

‘Mume wangu kumbuka ahadi yetu ya ndoa, kuwa tusihi kwa raha na shida,….sasa mbona umeamua kuniacha kipindi hichio cha shida’ mke wangu akaniuliza.

‘Lakini mke wangu mbona nipo pamoja na wewe….’nikasema

‘Una uhakika na unachokisema…?’ akaniuliza, na swali hili lilinifanya niinue uso kumtizama,..na nikajikuta nikipatwa na mshituko mkubwa, kwani mke wangu alikuwa katikati ya moto , moto ulikuwa umemzingira, na yeye kasimama kati kati yake, hasogei, …

‘’Oh, kwanini huondoki hapa kwenye moto, huoni kwamba unaungua…’nikasema huku nikijitutumua kiinuka ili niende kumsaidia, lakini sikuweza maana viuongo vyote vilikuwa vizito, sikuweza hata kusogeza mkono.

‘Unaona, mbone wewe huwezi kusogea hapo ulipo, na wakati huo huo unauliza kwanini mimi siwezi kuondoka hapa kwenye huu moto….dhamira ya kweli haipo, ….’akasema na mimi nikawa najitutumua lakini sikuweza kufanya lolote…

‘Mke wangu nimeshindwa, jitahidi mwenye kuondoka hapo, utaungua…’nikasema,

‘Mume wangu najua jinsi gani ya kujiokoa mwenyewe na ambaye aliyenileta hapa duniani ndiye anayejua jinsi gani nitaweza kujiokoa, ….ila nakushauri jambo moja, ..waokoe hao ulio nao, kwani wanahitajia msaada wako , kama ulikubali kubeba jukumu la mzazi, basi hakikisha unatimiza wajibu wako…’akasema.

‘Nitawezaje kuwaokoa na hii hali?’ nikauliza.

‘Unaweza nini, na hiyo hali, wewe unajiona una hali mbaya hapo ulipo,...unatania kweli, ....wewe hali yako ni nzuri kabisa, wapo wenye hali mbaya zaidi yako, lakini wanajituma kwa vile hawana w kumtumania, wanachechemea, ......, hali uliyo nayo wewe haikuzuii kuwasaidia watoto, kesho amuka hapo ulipolala, nenda katafute ushahidi, …..’sauti ikasema na ikawa kama inapotea, nikainua uso kuangalia, na sikuweza kuona kitu , ilikuwa giza…

‘Sasa huo ushahidi nitaupata wapi?’ nikawa kama najiuliza, na mara ikawa kama vile nimeshikwa na usingizi, na ndoto nyingine ndani ya ndoto ikanijia, ..hapo nilijiona nipo kwenye eneo lililojaa takataka, na nilikuwa kama natafuta kitu…na kwa mbele yangu nikaona mwanamke amekaa, akiwa kashika mkoba, mkoba huo ulionekana mchafu..na alikuwa haonekani sura yake.

Nikawa namsogelea, hadi nilipomkaribia, mara akageuka na akawa kama anatka kunikabidhi huo mkoba , mimi nikanyosha mkono kutaka kuupokea, lakini kabla sijaukamata, nikazindukana kutoka kwenye usingizi,kumbe ilikuwa ni ndoto…..

‘Oh, huyu mtu ni nani, mbona anafanana na mke wangu….kwanini karibu kila siku ninamuota,..?’ nikajiuliza.
Mara akaingia dakitari, na kuniuliza hali yangu, mimi nikamwambia najiskia sijambo, japokuwa kwakweli hali yangu bado ilikuwa ya uzaifu, lakini niliona siwezi kulala hapo tena, maana nijuavyo siku hiyo ndiyo ya kesi ya mwanangu. Nilijaribu kujiinua lakini sikuweza , mwili wote ulikuwa kama umekufa ganzi.

‘Nesi naomba uniitie mwanangu mpigie simu mwambie namuhitaji haraka…’nikasema.

‘Kwani vipo baba….wewe tulia, ndio tumekuchukua vipimo, ..haina haja ya kuwa na shaka..’nesi akasema.

‘Nimekuambia mpigia mwanangu simu, haraka, mwamabia afanye juu chini tuonane…’nikasema na kweli yule nesi akachukua simu yake na kutoka nje, sijui waliongea nini, lakini baadaye alikuja na kusema

‘Nimeshawapigia simu, ila amesema, leo ndio siku ya kesi, na kesi yenyewe imepangiwa asubuhi, sizani kama anaweza kufika hapa haraka kama ulivyotaka,…atakuja baba yake mzazi…’akasema.

‘Basi tena, ….’nikasema na yule nesi akaniangalia kwa mashaka, …akaondoka kwenda kumuita dakitari, ilionekana alikuwa na wasiwasi na hali yangu hiyo.

**********

‘Mjukuu wangu, kila siku nikilala, ilikuwa ni lazima namuota mke wangu, na kila mara ananilaumu kuwa nimemtelekeza, na anadai kuwa na sasa nimeamua kuwatelekeza watoto, sitaki kujisumbua kwenda kutafuta ushahidi, na kila nikiuliza huo ushahidi nitaupata wapi, najikuta napelekwa sehemu hiyo yenye matakataka, na wakati mwingine napelekwa kimawazo tu, kama vile unawaza kwa kukumbuka sehemu hiyo.

Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kutoka hapo hospitali, na docta alishanifahamisha, kuwa siku hiyo nitaruhusiwa, na docta akaniambia kuwa binti yangu alitoa taarifa kuwa nikiruhusiwa, nisondoke, nimsubiri atakuja mwenyewe kunichukua.

‘Docta, usiwe na wasiwasi, mimi nitaondoka mwenyewe, kuna jambo nataka nilifuatilie mwenyewe…akija mwambie tutakutana nyumbani…’nikasema na kuondoka huku nikichechemea, hadi kituo cha mabasi, nikpanda basin a kuondoka. Nilipofika eneo la kijiji chetu, badala ya kwenda nyumbani anapoishi huyo binti yangu, nikaamua kwenda kwenye eneo la jengo langu, ambalo lilikuwa limesimama, ..ujenzi ulikuwa umesimama,….nililiangalia kwa macho ya huzuni, nikasema kimoyo moyo;

‘Ipo siku tu, nyumba hii itakamilika….’nikasema na kugeuka, nanilipogeuka kuangalia upande mwingine, nikahisi kitu kikiniingia akilini na nikawa kama navutwa na hisia fulani, ambazo zilikuwa zikinisukuma kwenda nisipokujua,…hizia hizo zilikuwa kama vile nipo kwenye ndoto, nikaanza kutembea….nilitembea kwa dakika chache, na kujikuta nimefika  kwenye bonde kubwa, bonde hilo ni sehemu ambayo,taka taka zinatupwa, na nilishangaa,….kwani sikuwa na wazo hili, hata nilipokwua nikiota kwua nipo kwenye sehemu ya takataka, sikuwa nimeliwaza hili..

‘Nikawa nimesimama nikiangalai sehemu hiyo, kwani zile hisia zilikuwa zimeondoka, an nilikuwa nipo na hisia zangu za kawaida, na hapo nikawa nawaza zile ndoto za mara kwa mara,…nikijaribu kukumbuka zile ndoto, kama nitaweza kukumbuka ni wapi sehemu ile niliyokuwa nikiiona kwenye ndoto.

Nikaanza kutembea, nikitafuta sehemu hiyo kama ilivyokuwa kwenye ile ndoto , lakini sikuweza kuiona, zaidi ya matakataka yaliyolundikwa huku na kule, ….nikajiuliza je inawezekanaje kukipata kitu kama kile sehemu kama ile,…kwani ni sehemu pana, na kuna malundo kwa malundo ya takataka, na akili yangu haikumbuki kabisa wapi nilihitajika niende na mara nikakumbuka ..

‘Ukitaka jambo, kwanza mkumbuke mola wako, omba, huku ukikumbuka yale mema uliyoyatenda…’hii ni kauli ya wazazi, ambayo mara kwa mara nikitingwa na matatizo inanijia akilini

Nikatafuta sehemu iliyosafi nikakaa na kujituliza maana mwili ulikuwa umechoka, kutokana na udhaifu wa kuumwa, ….nikajituliza na kitu cha kwanza nilichokumbuka ni kumuomba mungu, nikafanya ibada nijuavyo mimi huku nikikumbuka wema wangu niliowahi kuwafanyia watu, …

Kwakweli.niliomba kwa hisia kweli hadi machozi yakawa yananitoka,  na sikumbuki nilikaa vile kwa muda gani, lakini nilihisi hali ya hewa ikiwa nzito, kuashiria kuwa kuna moshi unatokea sehemu fulani, na ulikuwa umeelekezwa pale nilipo kwa upepo, nikasimama, na jicho langu la kwanza lilitua kwenye kibanda cha maboksi…

‘Hiki kibanda kinaishi mtu…?’nikajiuliza na bila kusubiri nikaanza kutembea kuelekea kwenye hicho kibanda cha maboksi. Ni kibanda kilichokuwa imejengwa kwa miti na kuzungushiwa kwa maboksi, na ilivyoonyesha kulikuwa na mtu, …nikasimama nikimwangalia, kwani alikuwa kajifunika nguo kukuu, zilizochoka choka, na alivyojifunika usingeliweza kumtambua ni mwanamke au ni mwanaume…ilionyesha kuwa alikuwa akipika, kwani kulikuwa na sufuria iliyokuwa juu ya mafiga, ambapo kulikuwa na moto, sikuweza kuona ndani ya ile sufuria kwani alivyokaa alikuwa kazuia nisiweze kuona ni nini alichokuwa akipika.

Kwa mbali nikaona watoto wakichakura matakataka, na kukusanya vitu mbali mbali….walikuwa wanafanya hivyo kwa mikono yao, bila kujali athari …na wakati mwingine waliona mabaki ya chakula, wakawa wanachukua yale mabaki na kuyahifadhi kwenye vyombo walivyokuwa navyo…

Wale watoto wakaniona, ….kwa haraka wakakimbia na kujificha, ….mimi sikuwajali,…nikamsogelea yule mtu, ambaye alikuwa kainama na aliposikia mchakato wa nyayo za mtu, akawa kama kashituka, akasimama na hakunigeukiwa moja kwa moja, ila mkononi tayari alikuwa kashika fimbo, ilikuwa na fimbo ya mti ambayo ilionekana ni nyeusi, na ilionekana ni maalumu kwa kutembelea, huenda alikuwa akiitumia kutembelea au ilikuwa ndio silaha yake.

‘Samahani sina nia mbaya na wewe….’nikasema, na sauti yangu ilimfanya yule mtu adondoshe ile fimbo, na taratibu akageuka kuniangalia. Alikuwa kajifunika sehemu yote ya kichwa na kuacha sehemu ya macho, akanitizama,…

‘We…we ni nani na unataka nini?’ akaniuliza kwa kigugumizi kwa sauti ambayo usingeliweza kuitambua ni ya kike au ni ya kiume,….lakini kwa mtizamo wa haraka ilikuwa ni sauti ya kike. Alionekana kuwa na wasiwasi….lakini pia alikuwa kama kashikwa na mshangao, uliomfanya awe anasita sita,….

‘Kuna kitu natafuta….wewe unaishi hapa…mbona ni majalalani, huoni kuwa ni hatari kiafya….’nikasema na kabla sijamaliza, yule mtu akageuka, na kuinama akafunua maboksi yaliyokuwa yamejilundika, na hapo akatoa mfuko wa Rambo ukiashiria kuwa ina kitu kizito ndani yake….na kugeuka akawa kama anataka kunikabidhi. ….mkono wake ulikuwa kama unatetemeka, na hakuweza kuuonyosha moja kwa moja, ….

Mara nikasikia sauti, nikageuka, walikuwa wale watoto wamekuja na kusimama nyuma yangu, kila mmoja akiwa kashika fimbo,…nahisi ilikuwa kama silaha, na yule mtu akawaangalia na kusema;

‘Msijali huyu sio adui, nendeni mkaendelee na shughuli, chakula kikiwa tayari nitawaita…..’akasema na hapo nikagundua kuwa ni mwanamke, japokuwa sauti yake ilikuwa ikitoka kwa shida, sijui ni kwasababu ya hizo nguo alizojifunika au ana kigugumizi….Na wale watoto wakaondoka huku bado wakiwa wanageuka geuka kuniangalia kwa mashaka.

‘Hawa watoto ….’nikawa nataka kusema neno na huyo mtu akanikatiza na kusema;

‘Ni watoto wa mitaani, mimi ni mlezi wao, ninaishi nao hapa, ….’akasema huku akiwa anatoa kitu kwenye mfuko wa Rambo, na kilichotoka hapo, kilikuwa sio kingine ni ule mkoba niliouona kwenye ndoto….

Babu alipofika hapo akatabasamu, na uso wake ukawa umejaa nuru, lakini kwa mbali machoni, kuliashiria huzuni…..akatikisha kichwa kama kukubali jambo fulani, halafu akasema;

‘Sikuweza kuamini mjukuu wangu,….ulikuwa mkoba ule ule niliokuwa nikiuona kwenye zile ndoto nilizokuwa nikiota kule hospitalini….ni miujuiza ya mungu…’babu akarejea maneno hayo.


NB: Unaamini miujuza, kama unaamini au huamini, hivyo ndivyo ilivyotokea, je huo mkoba una siri gani



WAZO LA LEO:,Kumbuka ipo siku maalumu, inayotambulikana kama ya siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16 June, sijui kama upo makini na siku hii, huenda kwako ni historia tu ya Mauaji ya Soweto…kwani unaishi kwenye kisiwa cha amani, huna shida…una kazi nzuri, gari..nk. Lakini kumbuka kuna hawa watoto wa mitaani, unawakumbuka?

 Je siku ya mtoto kwako inakugusaje. Hebu kwanza pitia hapa kwa ndugu wa mimi, upate ujumbe:

http://swahilinawaswahili.blogspot.com/2013/05/kuelekea-siku-ya-mtoto-wa.html

 Je wewe kama mzazi, unahisije ukiwaona watoto wa mitaani, au ndio huko kusema, `hawa watoto wanaomba omba tu, hawaendi shule…’ hawa kwa mateso wanayoyapata hawana tofauti na wale watoto waliouwawa kikatili,…..wewe hutumii, silaha, lakini unatumia njia nyingine, isiyoonekana, ya kutokutimiza wajibu wako kama mzazi.


Kumbuka mateso wanayopata hawa watoto, kwanza kisaikolojia pale wanapoona wenzao wakiwa kwenye sare za shule, au wakipita na magari wakiepelekwa mashuleni.  Lakini pia kuwa mateso ya afya zao, kwani wengine wanaishia majalalani kuokota yale mabaki ya vyakula mliyokula na kusaza. Huyu ni mtoto wako hata kama hukumzaa wewe, kumbukeni kila mtoto ana mzazi, na mzazi wake ni mimi na wewe
Ni mimi: emu-three

3 comments :

Rachel Siwa said...

Ndugu wa mimi Tupo pamoja kabisa..Natarajia ipo siku tutakutana na kufanya hii kitu pamoja..Tupo pamoja kabisa mbiombio tuu zimenizidi..

Mingi Love..

emuthree said...

Ndugu wa mimi, naisubiri hiyo siku kwa hamu, natarajia iwe hivyo....Tupo pamoja daima.

Yasinta Ngonyani said...

hiyo ndoto hiyo duh!!! nasubiri muendelezo