Mjukuu wangu,
nilizindukana na kujikuta nipo hospitalini, nikiwa nimezungukwa na madakitari,
kila mmoja akiwa na shughuli yake,….kwanza kwa akili ya haraka nilifikiria nipo
ahera, lakini akili ilipotulia nikatambua nipo hospitalini kwenye chumba cha
wagonjwa mahututi………..’nilikumbuka jinsi babu alivyonisimulia, wakati huo
mama alikuwa katoka kidogo.
‘Mjukuu wangu, sijawahi kuumwa, kama nilivyoumwa kipindi
hiki, …na iliniuma sana nilipofikiria kuwa kuumwa huku sio kuumwa kule kwa
kawaida, ilikuwa kuumwa, kusababishiwa na watu wengine, watu waliotoka kuchukua
haki za watu…
Nilifungwa muhogo(POP), na kushonwa jereha la kisu,
…sikuamini kuwa kisu hicho hakikuathiri sehemu ya ndani ya mwili, maana siku ile
nakumbuka nilihisi kisu kikipenya ndani, …lakini madakitari walisema hakuna
athari yoyote ndani ya mwili wangu.
Sikiweza kabisa kusimama, au hata kuhema, kwani kila
nikigeuza mwili, nilihisi maumivi kila sehemy ya mwili,….ilikuwa mateso
yasiyomithilika, na kika mapigo ya moyo yalipokuwa yakipiga, ndio maumivi
yalikuwa yakifuatilia mapigo hayo, hapo nikatamani roho itoke haraka ili
niepukane na maumivu hayo. Na kwakweli ilifikia hatua, sikuweza kuvumilia tena,
nikapoteza fahamu.
Siku nilipozindukana tena, niliambiwa kuwa nilipoteza fahamu
kwa siku mbili, na kilichokuwepo akilini mwangu ni hiyo ndoto, ndoto ambayo
kwangu iliniashiria kuwa huenda siku zangu za kuishi zimeshakwisha, kwani ndani
ya ndoto hiyo nilijikuta nipo na mke wangu….
‘Mume wangu kumbuka ahadi yetu ya ndoa, kuwa tusihi kwa raha
na shida,….sasa mbona umeamua kuniacha kipindi hichio cha shida’ mke wangu
akaniuliza.
‘Lakini mke wangu mbona nipo pamoja na wewe….’nikasema
‘Una uhakika na unachokisema…?’ akaniuliza, na swali hili
lilinifanya niinue uso kumtizama,..na nikajikuta nikipatwa na mshituko mkubwa,
kwani mke wangu alikuwa katikati ya moto , moto ulikuwa umemzingira, na yeye
kasimama kati kati yake, hasogei, …
‘’Oh, kwanini huondoki hapa kwenye moto, huoni kwamba
unaungua…’nikasema huku nikijitutumua kiinuka ili niende kumsaidia, lakini
sikuweza maana viuongo vyote vilikuwa vizito, sikuweza hata kusogeza mkono.
‘Unaona, mbone wewe huwezi kusogea hapo ulipo, na wakati huo
huo unauliza kwanini mimi siwezi kuondoka hapa kwenye huu moto….dhamira ya
kweli haipo, ….’akasema na mimi nikawa najitutumua lakini sikuweza kufanya
lolote…
‘Mke wangu nimeshindwa, jitahidi mwenye kuondoka hapo,
utaungua…’nikasema,
‘Mume wangu najua jinsi gani ya kujiokoa mwenyewe na ambaye
aliyenileta hapa duniani ndiye anayejua jinsi gani nitaweza kujiokoa, ….ila
nakushauri jambo moja, ..waokoe hao ulio nao, kwani wanahitajia msaada wako ,
kama ulikubali kubeba jukumu la mzazi, basi hakikisha unatimiza wajibu
wako…’akasema.
‘Nitawezaje kuwaokoa na hii hali?’ nikauliza.
‘Unaweza nini, na hiyo hali, wewe unajiona una hali mbaya hapo ulipo,...unatania kweli, ....wewe hali yako ni nzuri kabisa, wapo wenye hali mbaya zaidi yako, lakini wanajituma kwa vile hawana w kumtumania, wanachechemea, ......, hali uliyo nayo wewe haikuzuii
kuwasaidia watoto, kesho amuka hapo ulipolala, nenda katafute ushahidi, …..’sauti
ikasema na ikawa kama inapotea, nikainua uso kuangalia, na sikuweza kuona kitu
, ilikuwa giza…
‘Sasa huo ushahidi nitaupata wapi?’ nikawa kama najiuliza, na
mara ikawa kama vile nimeshikwa na usingizi, na ndoto nyingine ndani ya ndoto
ikanijia, ..hapo nilijiona nipo kwenye eneo lililojaa takataka, na nilikuwa
kama natafuta kitu…na kwa mbele yangu nikaona mwanamke amekaa, akiwa kashika mkoba,
mkoba huo ulionekana mchafu..na alikuwa haonekani sura yake.
Nikawa namsogelea, hadi nilipomkaribia, mara akageuka na akawa kama anatka kunikabidhi huo mkoba , mimi nikanyosha mkono kutaka kuupokea, lakini kabla
sijaukamata, nikazindukana kutoka kwenye usingizi,kumbe ilikuwa ni ndoto…..
‘Oh, huyu mtu ni nani, mbona anafanana na mke wangu….kwanini
karibu kila siku ninamuota,..?’ nikajiuliza.
Mara akaingia dakitari, na kuniuliza hali yangu, mimi
nikamwambia najiskia sijambo, japokuwa kwakweli hali yangu bado ilikuwa ya
uzaifu, lakini niliona siwezi kulala hapo tena, maana nijuavyo siku hiyo ndiyo
ya kesi ya mwanangu. Nilijaribu kujiinua lakini sikuweza , mwili wote ulikuwa
kama umekufa ganzi.
‘Nesi naomba uniitie mwanangu mpigie simu mwambie namuhitaji
haraka…’nikasema.
‘Kwani vipo baba….wewe tulia, ndio tumekuchukua vipimo,
..haina haja ya kuwa na shaka..’nesi akasema.
‘Nimekuambia mpigia mwanangu simu, haraka, mwamabia afanye
juu chini tuonane…’nikasema na kweli yule nesi akachukua simu yake na kutoka
nje, sijui waliongea nini, lakini baadaye alikuja na kusema
‘Nimeshawapigia simu, ila amesema, leo ndio siku ya kesi, na
kesi yenyewe imepangiwa asubuhi, sizani kama anaweza kufika hapa haraka kama
ulivyotaka,…atakuja baba yake mzazi…’akasema.
‘Basi tena, ….’nikasema na yule nesi akaniangalia kwa
mashaka, …akaondoka kwenda kumuita dakitari, ilionekana alikuwa na wasiwasi na
hali yangu hiyo.
**********
‘Mjukuu wangu, kila siku nikilala, ilikuwa ni lazima namuota
mke wangu, na kila mara ananilaumu kuwa nimemtelekeza, na anadai kuwa na sasa
nimeamua kuwatelekeza watoto, sitaki kujisumbua kwenda kutafuta ushahidi, na
kila nikiuliza huo ushahidi nitaupata wapi, najikuta napelekwa sehemu hiyo
yenye matakataka, na wakati mwingine napelekwa kimawazo tu, kama vile unawaza
kwa kukumbuka sehemu hiyo.
Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kutoka hapo hospitali,
na docta alishanifahamisha, kuwa siku hiyo nitaruhusiwa, na docta akaniambia
kuwa binti yangu alitoa taarifa kuwa nikiruhusiwa, nisondoke, nimsubiri atakuja
mwenyewe kunichukua.
‘Docta, usiwe na wasiwasi, mimi nitaondoka mwenyewe, kuna
jambo nataka nilifuatilie mwenyewe…akija mwambie tutakutana nyumbani…’nikasema
na kuondoka huku nikichechemea, hadi kituo cha mabasi, nikpanda basin a kuondoka.
Nilipofika eneo la kijiji chetu, badala ya kwenda nyumbani anapoishi huyo binti
yangu, nikaamua kwenda kwenye eneo la jengo langu, ambalo lilikuwa limesimama,
..ujenzi ulikuwa umesimama,….nililiangalia kwa macho ya huzuni, nikasema kimoyo
moyo;
‘Ipo siku tu, nyumba hii itakamilika….’nikasema na kugeuka,
nanilipogeuka kuangalia upande mwingine, nikahisi kitu kikiniingia akilini na
nikawa kama navutwa na hisia fulani, ambazo zilikuwa zikinisukuma kwenda
nisipokujua,…hizia hizo zilikuwa kama vile nipo kwenye ndoto, nikaanza kutembea….nilitembea
kwa dakika chache, na kujikuta nimefika kwenye bonde kubwa, bonde hilo ni sehemu
ambayo,taka taka zinatupwa, na nilishangaa,….kwani sikuwa na wazo hili, hata
nilipokwua nikiota kwua nipo kwenye sehemu ya takataka, sikuwa nimeliwaza
hili..
‘Nikawa nimesimama nikiangalai sehemu hiyo, kwani zile hisia
zilikuwa zimeondoka, an nilikuwa nipo na hisia zangu za kawaida, na hapo nikawa
nawaza zile ndoto za mara kwa mara,…nikijaribu kukumbuka zile ndoto, kama
nitaweza kukumbuka ni wapi sehemu ile niliyokuwa nikiiona kwenye ndoto.
Nikaanza kutembea, nikitafuta sehemu hiyo kama ilivyokuwa
kwenye ile ndoto , lakini sikuweza kuiona, zaidi ya matakataka yaliyolundikwa
huku na kule, ….nikajiuliza je inawezekanaje kukipata kitu kama kile sehemu
kama ile,…kwani ni sehemu pana, na kuna malundo kwa malundo ya takataka, na
akili yangu haikumbuki kabisa wapi nilihitajika niende na mara nikakumbuka ..
‘Ukitaka jambo, kwanza
mkumbuke mola wako, omba, huku ukikumbuka yale mema uliyoyatenda…’hii ni
kauli ya wazazi, ambayo mara kwa mara nikitingwa na matatizo inanijia akilini
Nikatafuta sehemu iliyosafi nikakaa na kujituliza maana
mwili ulikuwa umechoka, kutokana na udhaifu wa kuumwa, ….nikajituliza na kitu
cha kwanza nilichokumbuka ni kumuomba mungu, nikafanya ibada nijuavyo mimi huku
nikikumbuka wema wangu niliowahi kuwafanyia watu, …
Kwakweli.niliomba kwa hisia kweli
hadi machozi yakawa yananitoka, na sikumbuki
nilikaa vile kwa muda gani, lakini nilihisi hali ya hewa ikiwa nzito, kuashiria
kuwa kuna moshi unatokea sehemu fulani, na ulikuwa umeelekezwa pale nilipo kwa
upepo, nikasimama, na jicho langu la kwanza lilitua kwenye kibanda cha maboksi…
‘Hiki kibanda kinaishi mtu…?’nikajiuliza na bila kusubiri
nikaanza kutembea kuelekea kwenye hicho kibanda cha maboksi. Ni kibanda
kilichokuwa imejengwa kwa miti na kuzungushiwa kwa maboksi, na ilivyoonyesha
kulikuwa na mtu, …nikasimama nikimwangalia, kwani alikuwa kajifunika nguo kukuu,
zilizochoka choka, na alivyojifunika usingeliweza kumtambua ni mwanamke au ni
mwanaume…ilionyesha kuwa alikuwa akipika, kwani kulikuwa na sufuria iliyokuwa
juu ya mafiga, ambapo kulikuwa na moto, sikuweza kuona ndani ya ile sufuria
kwani alivyokaa alikuwa kazuia nisiweze kuona ni nini alichokuwa akipika.
Kwa mbali nikaona watoto wakichakura matakataka, na
kukusanya vitu mbali mbali….walikuwa wanafanya hivyo kwa mikono yao, bila
kujali athari …na wakati mwingine waliona mabaki ya chakula, wakawa wanachukua
yale mabaki na kuyahifadhi kwenye vyombo walivyokuwa navyo…
Wale watoto wakaniona, ….kwa haraka wakakimbia na kujificha,
….mimi sikuwajali,…nikamsogelea yule mtu, ambaye alikuwa kainama na aliposikia
mchakato wa nyayo za mtu, akawa kama kashituka, akasimama na hakunigeukiwa moja
kwa moja, ila mkononi tayari alikuwa kashika fimbo, ilikuwa na fimbo ya mti
ambayo ilionekana ni nyeusi, na ilionekana ni maalumu kwa kutembelea, huenda
alikuwa akiitumia kutembelea au ilikuwa ndio silaha yake.
‘Samahani sina nia mbaya na wewe….’nikasema, na sauti yangu
ilimfanya yule mtu adondoshe ile fimbo, na taratibu akageuka kuniangalia.
Alikuwa kajifunika sehemu yote ya kichwa na kuacha sehemu ya macho,
akanitizama,…
‘We…we ni nani na unataka nini?’ akaniuliza kwa kigugumizi
kwa sauti ambayo usingeliweza kuitambua ni ya kike au ni ya kiume,….lakini kwa
mtizamo wa haraka ilikuwa ni sauti ya kike. Alionekana kuwa na wasiwasi….lakini
pia alikuwa kama kashikwa na mshangao, uliomfanya awe anasita sita,….
‘Kuna kitu natafuta….wewe unaishi hapa…mbona ni majalalani,
huoni kuwa ni hatari kiafya….’nikasema na kabla sijamaliza, yule mtu akageuka,
na kuinama akafunua maboksi yaliyokuwa yamejilundika, na hapo akatoa mfuko wa
Rambo ukiashiria kuwa ina kitu kizito ndani yake….na kugeuka akawa kama anataka
kunikabidhi. ….mkono wake ulikuwa kama unatetemeka, na hakuweza kuuonyosha moja
kwa moja, ….
Mara nikasikia sauti, nikageuka, walikuwa wale watoto
wamekuja na kusimama nyuma yangu, kila mmoja akiwa kashika fimbo,…nahisi
ilikuwa kama silaha, na yule mtu akawaangalia na kusema;
‘Msijali huyu sio adui, nendeni mkaendelee na shughuli,
chakula kikiwa tayari nitawaita…..’akasema na hapo nikagundua kuwa ni mwanamke,
japokuwa sauti yake ilikuwa ikitoka kwa shida, sijui ni kwasababu ya hizo nguo
alizojifunika au ana kigugumizi….Na wale watoto wakaondoka huku bado wakiwa
wanageuka geuka kuniangalia kwa mashaka.
‘Hawa watoto ….’nikawa nataka kusema neno na huyo mtu
akanikatiza na kusema;
‘Ni watoto wa mitaani, mimi ni mlezi wao, ninaishi nao hapa,
….’akasema huku akiwa anatoa kitu kwenye mfuko wa Rambo, na kilichotoka hapo,
kilikuwa sio kingine ni ule mkoba niliouona kwenye ndoto….
Babu alipofika hapo
akatabasamu, na uso wake ukawa umejaa nuru, lakini kwa mbali machoni,
kuliashiria huzuni…..akatikisha kichwa kama kukubali jambo fulani, halafu
akasema;
‘Sikuweza kuamini mjukuu wangu,….ulikuwa mkoba ule ule
niliokuwa nikiuona kwenye zile ndoto nilizokuwa nikiota kule hospitalini….ni
miujuiza ya mungu…’babu akarejea maneno hayo.
NB: Unaamini miujuza, kama unaamini au huamini, hivyo ndivyo
ilivyotokea, je huo mkoba una siri gani
WAZO LA LEO:,Kumbuka
ipo siku maalumu, inayotambulikana kama ya siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16
June, sijui kama upo makini na siku hii, huenda kwako ni historia tu ya Mauaji
ya Soweto…kwani unaishi kwenye kisiwa cha amani, huna shida…una kazi nzuri,
gari..nk. Lakini kumbuka kuna hawa watoto wa mitaani, unawakumbuka?
Je wewe kama mzazi, unahisije ukiwaona
watoto wa mitaani, au ndio huko kusema, `hawa watoto wanaomba omba tu, hawaendi
shule…’ hawa kwa mateso wanayoyapata hawana tofauti na wale watoto waliouwawa
kikatili,…..wewe hutumii, silaha, lakini unatumia njia nyingine, isiyoonekana,
ya kutokutimiza wajibu wako kama mzazi.
Kumbuka mateso wanayopata hawa watoto, kwanza kisaikolojia
pale wanapoona wenzao wakiwa kwenye sare za shule, au wakipita na magari
wakiepelekwa mashuleni. Lakini pia kuwa
mateso ya afya zao, kwani wengine wanaishia majalalani kuokota yale mabaki ya
vyakula mliyokula na kusaza. Huyu ni
mtoto wako hata kama hukumzaa wewe, kumbukeni kila mtoto ana mzazi, na mzazi
wake ni mimi na wewe
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Ndugu wa mimi Tupo pamoja kabisa..Natarajia ipo siku tutakutana na kufanya hii kitu pamoja..Tupo pamoja kabisa mbiombio tuu zimenizidi..
Mingi Love..
Ndugu wa mimi, naisubiri hiyo siku kwa hamu, natarajia iwe hivyo....Tupo pamoja daima.
hiyo ndoto hiyo duh!!! nasubiri muendelezo
Post a Comment