Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Saturday, June 1, 2013

WEMA HAUOZI-15(na marekebisho kidogo)


Arubaini ikaisha, na hapo nikaruhusiwa kutoka nje,na nikaruhusiwa kubadili hata nguo kwani siku zile arubaini nilikuwa na nguo maalumu, kaniki nyeusi, na nilikuwa siruhusiwi kujiweka msafi au kujiremba, …

Siku kama hiyo ya kumaliza arubaini kunakuwa na shughuli maalumu za kumaliza msiba, wanafamilia , majirani na ndugu hufika hapo nyumbani kulipokuwa na msiba, kwani inakuwa ni siku ya kumuombea marehemu na waliotangulia kabla yake, na hapo pia kuna mambo mengi ya kimila na taratibu za kimila yanakamilishwa ikiwa ni pamoja na kuangalia hatima ya mjane, watoto na mali zilizoachwa na marehemu.

Kuna maswala ya mirathi yanazungumzwa na mtu maalumu wa kusimamia anachagulia, na mjane anajulikana anakwenda kwanani, kwani kutokana na mila za kabila letu mwanamke akishafiwa na mumewe anarithiwa, ….yaana anachukuliwa na ndugu wa mume wako, na hili sikukubaliana nalo na hapo ndipo kukaanza utata, ubishi na manung’uniko, yaliyokuja kuleta mfarakano baadaye, na hata kutokuelewana kati yangu na familia ya marehemu mume wangu…’mama akawa anaendelea kuongea.

Baada ya shughuli za mchana kutwa baadaye ikafikia kipindi cha kikao cha wanafamilia, ambapo hapo kunakuwa na hitimisho la shighuli nzima, ya kuomboleza, na kila mtu anaendelea na maisha yake, lakini tupo sisi , yaani mke wa marehemu, mtoto na mali, hili bado lilikuwa halijazungumziwa na kikao kama hiki ndicho kilihitajiak kulizungumzia.

Katika kikao hiki, alikuwepo, baba yangu mzazi, na mama yangu mzazi, kama wasikilizaji tu, wao waliomba wawepo, japokuwa sio muhimu kwao kuwepo, na hawakukataliwa ila waliambiwa kuwa wao ni wasikilzaji tu, hawakutakiwa kuongea kitu, kiutaribu za mila na desturi za familia hii, kwani mimi sipo mikononi mwao, bado nilikuwa mikononi mwa familia iliyonioa, na nia na lengo lao ni mimi kuendelea kuwepo ndani ya hiyo familia.

Kiutaratibu kama yupo mzee mkubwa wa familia, kwenye hii familia ndiye anafungua kikao, lakini kwenye hii familia walishakuwa na mwenyekiti wao ambaye alishachaguliwa muda mrefu,na mwenyekiti huyo akamkaribisha huyo mzee, ili aongee, na kufungua kikao na kuleta baraka zake, na yule mzee akaanza kuongea;

Mzee huyo alianza mambo yao ya kimila, akaomba kimila na akaongea maswala mengi ya kimila na baadaye akafikia kwenye sehemu muhimu inayonigusa mimi na mtoto na mali, …huyo mzee akaendelea kuongea;

‘Huo ndio utaratibu wetu wa kimila, na hili linafanyika ili wewe usiondoke na kwenda kuolewa na watu wengine, wakati mlishaishi na mume wako na kuwa miongoni mwa familia japokuwa ulikuwa mbali nayo kimatendo, lakini hili lina umuhimu wake,….’akasema huyo mzee wa familia, huyu alikuwa mdogo wa baba wa  marehemu mume wangu.

‘Mkwe wangu…., maana wewe ni mkwe wangu ambaye kama ingelikuwa uwezo wangu, nisingelipenda kabisa uondoke kwenye familia yetu, na hili tutalipigania kwa nguvu zetu zote, ….sijui kama wenzangu uwanalifahamu hilo, lakini mimi kama baba yako, baba mkwe, nakufahamu vyema, wewe ni jembe la familia,…, sitaki uchukuliwe na mtu mwingine nje ya familia hii, ……’akasema huku akitabasamu.

‘Baba endelea akini tunaomba ufanya haraka, kwani kuna watu wa mbali wanataka kuondoka bado kuna utaratibu nyingine zinahitajika kufanyika, bado mambo yapo mengi na yanastahili kumalizwa leo…’akasema mwenyekiti.

‘Yatamalizika tu msiwe na shaka, …mimi baba yenu nipo.’akasema huyo mzee.

‘Sasa ni hivi, kwa utaratibu wetu, mume anapofariki , mke huchukuliwa na ndugu za marehemu, kaka mkubwa au mdogo , anamposa huyo mjane, sio kumposa tuelewane hapo, maana ukisema kumposa ina maana kunahitajika kutoa mahari tena, hapana hayo ni mambo ndani ya familia,…yana taratibu zake, ambazo zitakuja kufuatwa baadaye, muda ukifikia..hapa hatusemi kumposa, ni kumuhamisha toka mamlaka ya ndugu huyu kwenda kwa huyu kwasabbau hizo za msiba, ingawaje waswahili wanatumia neno kurithiwa…mimi silipendi hilo neno maana linaleta maana isiyo stahili….’akasema huyo mzee.

‘Mjane,….nina maana mke wa marehemi ni mtu wetu, ni mwanafamilia, na ndugu yake au kaka yake asipokuwepo, wapo ndugu zake wengine, wanahitajika kumuhudumia ipasavyo hata kipindi kischokuwa na msiba….yale mambo muhimu yote yanayostahiki kumpa huyo mwanamke anatakiwa kupewa, kama kuna dharura kama hiyo, ispokuwa ile hali ya uke na uume…hapo nasema kihekima mnielewe wenzangu…’akakohoa kuashiria jambo.

‘Sasa mume amekufa, ina maana hatutamuona tena, hapo sasa yule mke wa familia, mnielewe vyema kauli yangu, nikisema mke wa familia, naifafanua zaidi, kwani huyu ni mwanafamilia, kwa vipi, maana kwenye familia kuna kaka au dada, au baba au mama, au hata shangazi, kila mmoja anawasifu wake na pia kuwa wake ni…huyu ni mke,….ndio maana natumia mke wa familia, sio dada wa familia nk…hayo ni mambo yenu ya kiswahili, mtanielewa tu….’akakohoa tena.

‘Kwa vile huyu ni mwanafamilia, na mume wake keshafariki, utasemaje hapo, abaki hivi hivi hapana haiwezekani, lazima maisha yaendelee, na asijisikie kama vile mwanzoni…kwa mfano wakati mumewe yupo kulikuwa na huduma muhimu alikuwa anapewa na mumewe, sasa hayupo atapewa na nani, maana kuna huduma ambazo wakati mumewe alipokuwepo, alikuwa akizipata, …na hakuna mwingine aliruhusiwa kumpa ila yeye peke yake,….sasa hayupo, na hatakuwepo ina maana yeye ni basi tena, hilo haliwezekani, ni lazima kuwe na taratibu za kumuwezesha kuzipata kama kawaida, ….mnanielewa hapo vijana?’ akauliza na watu wakacheka.

‘Msicheke,…hili ndilo linafanya familia nyingine zinasambaratika, maana mke kafiwa, na hamtaki kufuata utaratibu, yule mke anakwenda kuolewa na familia nyingine, na ilivyo ya ajabu kwa vile watoto wetu hatuwathamini, kila mtu na wake, mtu hajali mtoto wa mwenzake na wakwake ni wakwake tu …basi huyo mama anaondoka na watoto wake,…hebu fikirieni hapo kwa makini, ….’akashika kichwa kidole

‘Nachukulia mfano kuwa, kama kulikuwa na mwanaume mmoja, na mwanaume huyu akafariki kwenye hiyo familia ya baba na mama waliobahatika kuwa mtoto wa kiume mmoja…na bahati mbaya akafariki, mke kaachwa mjane na mtoto au watoto, na hakuna wa kumrithi, hata kama alikuwepo…' mzee akatulia kidogo na kukohoa, halafu akaendelea kuongea,

'Kwa mfano inawezekana kukawepo na wanaume wengine ndani ya hiyofamilia, lakini kwa mambo yetu ya kisasa, hawataki kumrithi, mama huyo anaondoka na watoto wake….maana usasa kila mtu na watoto wake, ni nani atakubali kubeba majukumu ya watoto wa wenzake, ilihali wakwake mwenyewe anaona kuwa wanamshinda…, hebu angalieni hapo kwa makini, kweli hapo kutakuwa na kizazi endelevu tena…familia hiyo inakufa, kunabakia mahema…mke na mtoto au watoto hawo wanakwenda kuingia kwenye familia nyingie….’akasema huyo mzee.

‘Ni mambo kwa mtizamo wenu mnayoyaona ni ya kizamani yamepitwa na wakati au sio…?’ akatulia kidogo halafu akasema;

‘Na ukizingatia hili gonjwa baya la ukimwi,…ni nani atahatarisha maisha yake kuoa mjane…hapo ndio basi tena, mambo ya kurithiana wake, au wajane kama wanavyoita waswahili yamepitwa na wakati.
Lakini kwanini sisi wazee tunawashauri hilo kuwa kurithiana wajane ni muhimu, nitajaribu kutetea mila zetu hizi ambazo nashukuru kwenye ukoo wetu huu tumekuwa tulifuatilia japokuwa ni kwa shida, lakini tumejitahisi. Kuna sababu nyingi tu,… kuwa huyo tunayemuita mjane, tulishamtambua kuwa ni mwenzetu, ni mwanafamilia….yeye na marehemu walishirikiana kuchuma mali kwa pamoja, leo hii anaondoka, jasho lake litakuwa vipi….’hapo akatulia kidogo.

‘Kimila na kidesturi, mali…oh, naona hapo nimekwenda mbali kabla ya wakati wake….’akatulia kdigo, na baadaye akasema;

‘Kabla sijafikia hapo kwenye mali, natoa mfano halisi ili muweze kunielewa vyema,na mfano huu nitautoa kwa kuwauliza swali, ni kwanini watoto wakizaliwa hawaiti majina yao na mama zao, yaani mtoto bini au binti mama yake, na ukiangalia kiundani zaidi , mtoto huyu anayeujua undani wake zaidi ni mama, kweli si kweli, lakini bado anaitwa mtoto bin, au binti baba yake….’akatulia hapo nakuangali huku na kule.

‘Mama anaweza asiwe mtulivu, akatembea nje, akapata mimba na akaficha na wewe mume unajua ni mtoto wako, bado huyo mtoto anaitwa mtoto bini wewe, au sio,mama hawezi kisiri akasema mtoto bini mimi …ni kwanini, ni kwasababu kwanza wewe mke upo kwenye miliki ya waliokuoa, wewe umetolewa kwenu na kuja kuunganishwa kwenye familia ya mume, wewe sio familia ya huko kwenu tena na kwahiyo chochote kitakachopatikana hapo ni mali ya familia hiyo ya mume wako naona hapo kidogo naanza kueleweka…’akasema huyo mzee na kutulia.

‘Ni nini hekima yake hapo…mnisikilize kwa makini, maana mimi ndiye mzee niliyebakia kwenye hii familia, msiponisikiliza leo, makakubali kuyumbishwa na wakuja, mkajiingiza kwenye mambo yenu ya kisasa, mkaiua familia, na ukoo ukasambaratika msije mkanilaumu mimi au nikaja kulaumiwa mimi kama baba wa familia na ukoo wetu huu…’akatulia na kuangalia huku na kule kuwaangalia waliokuwpo humo ndani.

‘Hili sasa ni tatizo,…mali…mali sasa imekuwa ni tatizo,…watoto sio tatizo, hawagombewi, ulishawahi kusikia mtu kafariki, na wanandugu wanagombea watoto…wapi…..hata siku moja, na kila mmoja anajifanya hawaoni, maana nani atapenda kubeba mzigo wa mwenzake,…mke, baadhi ya familia, wanagombea,…lakini hili sasa linaanza kupitwa na wakati, kilichobakia na sijui kama kitakuja kupitwa na wakati, ni mali,..mali imekuwa ni tatizo….

‘Mambo mengine yanakubalika na yanakwenda shwari, mtoto ni wa baba, ukoo wa baba, hilo halileti utata, lakini ingia kwenye mali….hapo watu macho na msikioa yanazibwa, hapo haki inatafutwa hadi mahakamani, kwa kisingizo cha haki za binadamu..au sijui haki za akina nani, watajijua wenyewe…, watu watagombana hadi kufikishana mahakamani, ni kwanini….mumeshahu mlipotoka, mumesahau kiapo, na makubaliano ya ndoa…..mtoto sio tatizo, mali ni tatizo, jiulizeni hapa kuna nini….

‘Kwanini sisi kama wazee, tunaliangalai kwa mtizamo huo, …hapa kuna hekima yake, kuwa familia hiyo ndiyo wamiliki wa mali, ndio maana wamemleta mke aungane nao kuwezesha familia hiyo kuendelea, na huyo mke huko alipotoka kaiacha familia yao na watu wao, na kuja kuungana na familia ya mume….hilo linaeleweka,….

'Na hivyo hivyo kama kwenye familia aliyoingia mke kama kuna mke atakwenda kwingine kwenye familia za watu wegine, sisi hatutaingia familia hizo. Na lengo la kumleta huyo mke ndani ya familia yetu pamoja na maagizo ya mungu, lakini pia sisi kama wanadamu tunaona kuwa ni sehemu ya kukuza familia hasa pale tunapopata watoto na mali, na hapo kunakuwa na maendeleo katika hiyo familia…sawa?.’akatulia kidogo.

‘Sasa ya mungu mengi, hatuwezi kuyapinga, sasa ndio mume kafariki, ndugu yetu kafarikia, mke ndio kaachwa, mume kaondoka, ..na kisasa, mnasema mali inakuwa nusu kwa nusu, au sio, au mali sasa inakuwa ya mke…mke anachukua hiyo mali kutoka kwenye familia aliyoikuta, anaipeleka kwao,…au kwa mume mwingine ambaye ana familia yake.

Nyie hamuoni kuwa mke huyo badala ya kuisaidia ile familia aliyoikuta amekuja kuibomoa, yale waliyochuma na mumewe, ili kukuza familia,anaondoka nayo… na kwenda kujenga kwenya familia nyingine…na hapo ina maana ukoo unakwisha, ..ukoo utakwishaje…nitalifafanua hili kama ifuatavyo..’akatulia.

‘Ukoo unakwisha kwa vile huyo mama akienda kuolewa kwingine, akizaa watoto watakuwa wa ukoo mwingine, na huenda kwa matashi ya yule mama hata watoto ambao aliondoka nao kwa ukaidi wake au kwa kutelekezwa na familia ya ndugu za marehemu mume wake atawabadilisha ubin, hawataitambua tena familia ya marehemu baba yao…kwahiyo familia hiyo imekufa….’akatulia.

‘Niwaambie ukweli, kuna mambo mengi ya kimila mnayapuuza, lakini wazee wenu walioyaona hayo na kwa hekima zao ndio wakaweka taratibu za kimila….taratibu ambazo siku hadi siku zinapotea, kwa kuiga usasa..haya igeni huo usasa, na mwisho wake, ukoo utakwisha na kusahaulika, mtabakia na usasa na ndio maana mungu anatutunuku magonjwa ya kisasa….na hili limetokea hapa maeneo ya kwetu,kuna koo ambazo zilikuwapo, sasa hivi hazipo tena imebakia historia…na hata kidini tunashauriwa tuuoe, tuzae ili tuijaze dunia, na  ukizaa unaongeza ukoo….’akatulia.

‘Na ilivyo sasa watu kwa uchoyo wao wanataka kuzaa watoto wawili, kajitahidi sana watatu..lakini mtu huyo ana uwezo, ni tajiri, angeliweza hata kuzaa watoto kumi, akawalisha na kuwasomesha, lakini uchoyo wa mali yake…anaona akizaa watoto wengi, watamuacha masikini…wewe, nani kakuambia utaishi milele…mali hiyo ni ya kwako kwa muda tu..unaweza hata usiifaidi, ..kwanini usizaie ukaiona ikitumika ndani ya familia yako….uchoyo tu…hakuna kingine, ni uchoyo..’akasema na watu wakacheka.

‘Mimi huo nauita ni uchoyo…binadamu tuna uchoyo wa nafsi,…kama una uwezo, umejaliwa mali, zaa bwana…zaa uijaze dunia, ….mali hiyo hutakwenda nayo kaburini..utakufa na wenzako watakuja kuifaidi na huenda wakaja kuifaidi wengine kabisa….wewe huoni, mjane anaondoka kwenda kuolewa na mwanaume mwingine, na huenda anakwenda kuolewa na adui yako mkubwa,…ambaye kama ungelikuwa hai, usingelipenda huyu kidume amsogelee, leo mkeo anakwenda kwake na mali yako,….
Sasa kwa uchoyo wako, adui yako anaichukua mali yako anamchukua mke wako, na watoto huenda wakatelekezwa….kuna midume mingine, inasema mimi nimekupenda wewe sio watoto, haisemi wazi kuwa mimi nimekupenda wewe kwasababu una mali..anaficha, anakuoa, anakushawishi, mali inakuwa yake..watoto wako hawatapata chochote, na mke ndio keshapenda, keshapata kidume mpya, basi tena, `chukua kila kitu mume wangu…., yule alikuwa hajui mapenzi.….’ akawa anaongea kwa kubana pua na kuwafanya watu wacheke.

‘Wewe kwa uchoyo wako umekufa na mali yako imekwenda na maji na ukoo umeteketea, maendeleo hakuna tena. Labda ungelizaa watoto wengi, miongoni mwake kungelitokea wenye uwezo zaidi,..na watu wengine wangeliogopa kuisogelea hiyo familia, maana ina jeshi la kutosha…mfano angalieni ukoo wetu, ni 
nani anaweza kutia pua hapa…hakuna, kwasababu tuna familia kubwa…’akasema.

‘Hiyo ndiyo hekima ya kuoa, kuzaa watoto wengi na mume akifa mke asibakie mjane,… asiwe mjane, kwanini awe mjane ilihali kuna ndugu za marehemu ambao watachukua nafasi yake,…..kuna sababu nyingi kama vile ,… mfano kuolewa siku hizi ni shida…eeh, sasa wewe mume kafa, kuliko kubakia mjane ukaadhirika, haraka haraka unapata mwenza, maisha yanaendelea au sio…?’ akauliza na watu wakashangilia.

‘Na baada ya kusema hivyo, mimi kama mzee wa familia, ninatoa rai, kuwa japokuwa hayo yapo, mila na desturi zetu zipo, kuwa mjane arithiwe, bado utashi wa kukubali au kukataa kurithiwa unabakia kwa mjane mwenyewe…msimlazimishe,…na hata hivyo, bado yupo kwenye msiba wa kuondokewa na kipenzi chake, kwahiyo mnahitajika kumpa muda…mpeni muda wa kutosha hayo mengine yatakuja yenyewe…’akamwangalia mjane aliyekuwa kakaa pembeni huku kampakata mtoto wake.

‘Na nyie kaka na ndugu za marehemu, ambao mmmh, mumeanza kumezea mate, muanze kutangaza sera zenu kihekima, ili kusiwepo na neno mjane kwenye familia yetu, pia kusiwepo na neno yatima kwenye familia yetu, maana sisi tupo, baba wapo, mama wapo sasa kwanini kuwepo na mayatima, ondoeni ubinafsi….na baada ya kusema hayo naona niishie hapo na kuwaachia wenyewe muendeleze ratiba yenu…huu ndio wakati wenu vijana…’akasema na kumgeukia mwenyekiti wa kikao ambaye ni kama mkubwa wa marehemu.

Kaka mkubwa akakohoa na kutikisa kichwa halafu akasema;

‘Mnasikia mambo hayo…maana wengine wanasema mimi najitungia mambo yangu mwenyewe, ..mimi sijitungii, nafuta taratibu na mila zetu,…nafanya yale waliyoniachia wazee…’akasema huku akitikisa kichwa, na akamgeukia mzee na kusema;

‘Mzee, mimi nakuhakikishia kuwa sitakubali ukoo wetu upotee, ukoo wetu utaimarika, utaongezeka na maendeleo yataendelea kuwepo, ..na kwa kukuhakikishia hilo, ni kwamba, yule kipingamizi wa uko wetu huu, tumeshamdhibiti…kasambaratika….na sasa kila kitu kipo mikononi mwetu…’akasema na watu wakamshangilia.

‘Mzee, sisi tupo…, na hatutakubali hata siku moja, aje mtu baki na kutuingilia mambo yetu,..sisi tuna familia zetu, tuna ukoo wetu, tuna mila na desturi zetu, kwanini mtu atoke huko kwenye ukoo wake, aje kutuvurugie mambo yetu…huo ni uchokozi wa wazi, hilo halitakubalika, na sasa tumewaonyesha watu kuwa tupo macho kwa hali na mali…na tunafuata sheria na utaratibu…’akasema na watu wakamshangilia.

‘Ama kwa mjane na mtoto…kama alivyosema baba, hapa kwetu hakuna neno mjane, kwahiyo kuanzia leo hilo tukitoka hapa, hatutaki huyu mama kuitwa mjane,…neno hilo kwake linafutika kuanzia leo,…hakuna yatima hapa, mtoto huyu ana baba, tena sio baba mmoja, ana baba zaidi ya mmoja na kila mmoja anapenda kumlea, na kuhakikisha kuwa anakua na kufikia malengo yanayostahili….

‘Baba, na wajumbe wote,…kila kitu kimeshawekwa safi…mtoto atalelewa kama wanavyolelewa watoto wengine, na kwa ajili ya kumfuatilia kwa karibu yupo baba yake keshachukua hayo majukumu, na sisi baba zake wengine tupo,…huyo anakuwa karibu naye tu, lakini sisi tunawajibika kama alivyokuwa akiwajibika marehemu,… hakuna shida kabisa….’akasema huyo kaka mkubwa akiwaangalia mama na mtoto wake.

‘Na kwa kuyaweka hayo mambo safi kisheria, yupo ndugu yetu, ambaye kwa bahati nzuri ni mwanasheria, msomi,….keshafanya kazi yake aliokabidhiwa na familia, kwahiyo kuanzia sasa kila kitu, mama, mtoto na mali zote zipo kwenye mikono ya familia….salama kabisa, na tutahakikisha kuwa havitoki nje ya familia…kamwe, kwa hali yoyote ile’akasema kwa kujigamba.

‘Shemeji kama alivyosema baba, wewe bado upo kwenye majonzi, na majonzi haya ni yetu sote, sisi marehemu alikuwa ni ndugu yetu,..ni mdogo wangu, ..na mtoto wa famiia hii, kwahiyo uchungu kama huo tunao sana, tena sana…kwa kuondokewa na kipenzi chetu hicho…lakini hayo hatuna mamlaka nayo, kuzaliwa na kufa kupo, hatuna mamlaka nako, upende  usipende, yule uliyempenda ataondoka, ….na huwezi kufanya lolote, maana hayo ni mapenzi ya mungu, ….’akatulia.

‘Tukiomboleza zaidi, tukasikitika zaidi, tukalia zaidi, tukajiumiza zaidi , tutakuwa tunakufuru,…maana hapo tutakuwa tunaingilia mamlaka ya muumba, iliyobakia ni kumuombea ndugu yetu huyo alale mahali pema peponi…na maisha mengine yaendelee,…ndivyo dunia ilivyo na ndivyo maisha yalivyo…hatuna jinsi, leo mimi nipo hai, kasha nitaondoka, wanandugu watachukua majukumu….’akatulia

‘Kama ulivyosikia baba , mzee wetu mkongwe wa familia alivyosema, kuwa kwenye familia hii hatupendi na kiujumla haitakiwi, kuwe na neno mjane, kuwe na neno yatima, kwanini hali hii iwepo wakati sisi tupo, …lakini hata hivyo, hatuna haraka nalo kwasasa, litakuja kwa wakati wake, maana kwanza kilichokuwa cha muhimu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kimewekwa kwenye mikono salama, na hilo limeshakamilika, kinachohitajika kwasasa ni uendelezaji wake, …tukiendeleza pale ndugu yetu alipoachia, na hili hatutaliweza bila ushirikiano, ushirikiano wa familia, ukiwemo wewe shemeji yetu…’akasema.

‘Shemeji kuna mengi yamesemwa,…huwezi kuyazuia, kila mtu ana mtizamo wake, hata hivyo hatupo mbalo na hilo, nikiwa na maana kuwa hatutapingana nayo saana, kama yanaendana na maadili ya mila na desturi za ukoo wetu. Sisi sio wabaya kihivyo, kama huyo anayejiita baba yako wa kufikia…alifikia kudai, kuwa eti nia na lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunachukua mali zote za marehemu na kukutelekeza wewe….nani kasema hayo…hayo ni maneno ya mitaani, ya kutaka kutupaka matope’akawa anawageukia wengine.

‘Huu sio msiba wa kwanza hapa kwetu…kuna ndugu zetu wengine walishafariki ndani ya ukoo wetu huu, na mambo yalikwenda shwari, je iweje kwako wewe iwe tofauti..kwani wewe tukutendee ubaya, kwanini wewe uwe utofauti, kwani wewe una tofauti gani na hawo wenzako….?’ Akawa kama anauliza, na akaendelea kuongea kwa harakaharaka;

‘Shemeji nikuambie ukweli na wewe unafahamu hilo.., mimi kwasasa nina wake wawili, mmoja anatokana na kuondoka kwa ndugu yangu,….tukafuata taratibu za kimila, nikamchukua mimi, kwa hiari yake mwenyewe, na wake zangu na mimi mwenyewe tunaishi kwa raha na amani, na watoto wote wana haki sawa, huwezi kuona tofauti,  hakuna shida, hakuna longolongo, kama wanavyosema vijana….sisi kama familia tumekamilika, ..tuna afya barabara, mashababi, ...’akasema huku akijiangalia.

‘Sasa shemeji, kwanza utilize moyo wako, utuone kama ni ndugu zako,…kuondoka kwa mdogo wetu, ndugu yetu, mtoto wetu, sio mwisho wa dunia, tupo, na wataendelea kuwepo, hadi hapo mungu atakaposema sasa dunia imekwisha, na haya, ya kufiwa, yapo, tuyakubali, …lakini ili tuishi kwa amani na upendo, ni lazima kuwe na utaratibu,…utaratibu ndio utakaotuweka pamoja, ….huwezi ukaishi kivyako vyako, ukawa na taratibu zako binafsi, ukadai kuwa ndio usasa…usasa ni utumwa, usasa ni mbinu za kuvunja mila na desturi zetu,…sisi ni waafrika, na waafrika tuna mila na desturi zetu..’akatulia.

‘Ndio maana sisi kama familia , tulipoona ndugu yetu yupo kweye hali mbaya, ilibidi tuingilie kati, maana kuna tiba mbadala…tiba asilia, na angelikubali kuzitumia awali, huenda angelikuwa tofauti, lakini siku zikifika huwezi kuzuia,….lakini hata hivyo kuna tatizo ….kuna tatizo maana siku hizi, uking’ang’ania mahospitalini, mwishowe watakuwekea sumu,….’akasema na watu wakaguna.

‘Msigune, ni kweli… unafikiri, hizi  dawa tunazotumia za hospitalini zina sumu kwa upande mmoja na tiba kwa upande wa pili ni nani anabisha hilo…?’ akawaangalia watu, na watu walikuwa kimiya, akasema;

‘Sasa hivi mgonjwa akiumwa sana, ukazidi kumuongezea madawa yao ambayo yana sumu, unafikiri ni nini tena hiyo, ina maana unamuongezea sumu, unamuua mgonjwa wako kwa sumu…maana ile sehemu ya kutibu haifanyi kazi tena, iliyobakia ni sumu…sumu..sumu..mgonjwa anazidiwa, bado unampa sumu..’akageuka huku na huku.

’Mnanielewa lakini, msija mkaenda huko na kusema nimesema kuwa hospitali wamempa ndugu yetu sumu….tuacheni majungu, ….maana yangu ilikuwa hiyo, kama nilivyoelezea….’akatulia

‘Ndugu yetu kaondoka na mengi…hatuwezi kumlaumu, maana utashi wa binadamu wa kuvumilia unatofautiana, baada ya mjanga na kuwekwa ndani , ..yeye aliona dunia imemtenga, kumbe sio kweli, sisi kama ndugu tulimuita tukamshauri, lakini hakupenda sana kutusikiliza , hatuwezi kumlaumu sana, maana ukizungukuwa na uturi utanukia uturi..sasa hayo tumuachie mungu, na tumuombee kwa mungu amsamehe madhambi yake alale mahala pema peponi,…amini.

‘Shemeji sisi kama wanafamilia, tupo pamoja na wewe, wewe ni mwenzetu, na tunaomba ukubali hilo, usijione kuwa upo peke yako, na kwa kuanzia hilo, tungelipenda undelee kukaa hapa hadi utakapojisikia upo tayari kukaa kwenye nyumba yenu…mliojenga na mumeo…na hata ukipenda mimi nipo tayari unaweza kuwa wa watatu..’akasema na watu wakacheka, na yeye alikuwa hacheki.

‘Ila kuna kitu kimoja tunakuomba utuelewe , maana hili linaweza likapotoshwa, na watu wakakufanya ujiingize kwenye migongano ya kifamilia, kitu ambacho hatukitaki. Kama alivyosema mzee, na kama nilivyokuja kusema, mali zote, kwasasa zipo mikononi mwa familia, hakuna kichoharibika, na tumefauatilia taratibu zote, …za kisheria ikiwemo hati ya nyumba, na duka, kama ujuavyo vyote viliandikwa jina la marehemu.

‘Kwa vile yeye hayupo duniani tena…ni lazima kuwepo mtu mwingine….tuliliwaza hilo kwa marefu na mapana,…. hilo, na tulitaka tumwandike mtoto,…lakini yeye bado mdogo,  lakini ukifuatilia mazungumzo yetu na marehemu ambaye baadaye kwa kuliona hili, kuwa linaweza likaleta utata baadaye, maaan hatujui, huenda akatokea mtu, akakubabaisha, ukaona hututaki tena, ukaamua kuondoka huoni kuwa mali hiyo itapotea, kwahiyo baada ya kuongea na yeye, tukaona kuwa ni vyema, kwa muda, na hilo tunakuhakikishia kuwa ni kwa muda…hadi hapo mtoto atakapokua, hati hizo zije zibadilishwe na kuwekwa jina lake…hii na kwa usalama wa mali za familia na watoto….’akatulia

‘Ndugu yetu, tulijaribu kuongea naye na tukashauriana hilo, akapendekeza kuwa mali zake, ziwekwe kwa jina la mdogo wetu huyu msomi, kwasababu yeye ni mwanasheria, atazilinda, na atajua jinsi gani ya kufuatilia maswala yote yanayostahili, ili mwisho wa siku kusije kuwa na mfarakano au kunyanyasana…sisi kwenye familia hii hatutaki kunyanyasana…hilo nakuhakikishia shemeji, ndio maana mimi nikajitolea kupigania kila kitu alichokiacha marehemu kiwe ndani ya familia na kiwe salama…mtu akitaka ’akasema kaka mtu.

‘Natumai shemeji umenielewa, na kama kuan dukuduku, hapa ndio mahali pake, huenda kuna lolote ungelipenda kukiongea, kushauri, au unaona halikwenda sawa, sisi kama binadamu tunakosea, na mbora ni yule anayekubali kukosa na kujirekebisha, ilimradi wazo hilo lisiwe nje ya taratibu za kifamilia na ukoo wetu kwa ujumla….na shemeji jisikie upo nyumbani, ongea …na kama hutaweza kuongea leo, bado uwanja upo, tunaweza kukutana tena…tukayaongea haya kwa mapana na marefu, na mwisho tutaelewana….’akasema 
kaka mtu na kumgeukia mjane, ambaye kwa utaratibu wa ukoo, hakutakiwa kuitwa mjane tena.

‘Nashukuruni sana, kwa maneno yenu mazuri, na kiukweli , sipingani na hayo maelezo yenu maana yana hekima yake kama alivyosema mzee na wewe mwenyekiti. Mimi ni mama, na mimi ni mzazi, nisipokubali hayo, nitakuwa ni nani, ina maana nitakubali mali za kizazi changu zipotee, ziende nje ya familia, …hapana, mimi kama mzazi siwezi kupingana na mawazo yenu mpo sahihi kabisa, kwahiyo nakubaliana nalo na nitajitahidi kuwa nanyi kama mmoja wa wanafamilia….’nikasema na wote wakashangilia.

‘Ila kwanza niwaambie kama mfiwa, na kama binadamu yoyote huwezi akakubali kuolewa na yoyote kwa muda kama huu, msiba kwangu bado upo moyoni,,..nahitaji muda wa kufikiria, na hasa ukizingatia kuwa hapo unakwenda kuolewa kama mke wa pili au wa tatu…kutokana na mila na desturi zetu, kwani nionavyo hapa wanandugu wote wana wake zao, na wachumba zao kama sikosei…’nikajitahidi kusema na kuwaweka sawa,

‘Kwahiyo naombeni sana, mnipe muda, na mkubali maamuzi yangu yatakayokuja baadaye, lakini kwa kifupi, mimi nisingelikubali kuolewa tena,kwani ….’hapo nikatulia na machozi yakaanza kunitoka, wote walitulia kimiya na baadaye nikaendelea kuongea kwa kusema;.

‘Nisingelipenda ndugu yoyote , sio kwamba siwapendi, au nina kitu nimekiweka rohoni…hapana, lakini ndivyo nilivyojipangia… hata wakati marehemu alipokuwepo duniani nilishamwambia kuwa kama itatokea akatangulia yeye, mimi sitaolewa tena, mimi nitamlea mwanangu na yeye akijaliwa akaoa, nitalea wajukuu zake…’nikasema na wote wakatulia kimiya.

‘Kwahiyo naombeni mnipe muda, na naomba mniache nitulie , na ningelipenda nikakae kwenye nyumba yangu maana hapo ndipo nilipopazoea, …..ina maana tkishamaliza hiki kikao ningeliomba niende nikakae kwangu, …’ nikasema na kuweka mikono kifuani kama kunyenyekea, halafu kwa sauti ya unyenyekevu nikasema;

‘Nawashukuruni sana kwa kunijali, ….na huo ndio udugu wa kweli, na nitazidi kuendelea kuomba misaada yenu ya hali na mali, ….lakini siwezi nikajipweteka, lazima na mimi nifanye kazi, …na ili nifanye kazi ni lazima nianza kwa kusimama, dede….msiwe na shaka na jinsi gani nitakavyoweza kuanza kusimama dede, …’nikatulia na kuwaangalia wazazi wangu ambao muda wote macho yao yalikuwa hayabaduki kwangu.

‘Mimi ni mwanafamilia, hilo sitalipinga hata siku moja, lakini mimi nina tabia yangu ya kujituma, kujiwezesha, na kuhangaika,ndivyo wazee wangU walivyonilea na nimekuja kuona siri ya tabia hiyo, ya kujituma, na kujitolea, kuwa mtu wa mwanzo kujitolea kwa kila jambo, lenye manufaa, hata kama utaumia, lakini kwa vile unafanya kwa nia safi, mungu anakupa uwezo wa ajabu…na hata mimi mwenyewe nataka maisha yangu yawe hivyo, na …namuomba mungu hata mtoto wangu awe hivyo, na hilo nitaliweza nikiwa sehemu yangu, niliyokuwa nikiiishi na mume wangu…’nikasema na hapo watu wakawa wanaangaliana.

‘Ndugu zanguni, kuna jambo nataka niliongee, kwani huenda sikuwahi kuliongea kwenu, au hata kama nililiongea, wengi hawakuniamini,lakini …kuna watu walikuja hata kutaka kunishitaki, nikawaeleza wakafuatilia, wakakubali …sijui walikubali lakini sikuona wakiendelea na mdai yao, hii ni kuonyesha kuwa nipo kwenya haki na ukweli…’hapo nikainua kichwa kumwangalia mwenyekiti, na yeye alikuwa kaangalia mbele, hakuwa akinitizama mimi .

‘Lakini kama mlivyonikubali kama mwanafamilia…natakiwa niwe muwazi mbele yenu. Ndugu mwema anaonyesha upendo wake kwa ndugu zake kwa kuwa mkweli na mwaminifu,….Mimi ni ndugu yenu, na hata kama ni ndugu yenu, bado kuna mambo ya mtu mwenyewe binafsi, ambayo yanastahili kuheshimika kitu kitu chake…hata kama kitatumiwa na wengi, lakini bado kunai le hali ya kusema hiki ni cha ndugu huyu….na ni chetu. Sizani kwa vile ni ndugu, kila kitu kitakuwa cha wote,na kumilikiwa na wote, lazima kuna mmoja ambaye anakuwa na jukumu nacho ….’nikatulia, hapo nikijua kuwa mioyo yao inaanza kwenda mbio.

‘Nikisema hili msinichukuliea kwa ubaya, kuwa napinga umoja wa kidugu, na umoja wa kidugu ni muhimu sana naukubali kwa moyo wote na hata siku moja sitawasaliti ,…mimi sijui kuongea uwongo, wazazi wangu ni mashahidi, labda iwe jambo ambalo sina uwezo nalo, na huenda linahitajia muda wa kulitafakari….mimi kama binadamu naweza kuwa na uzaifu wa namna moja au nyingine….

‘Kwahiyo nasema kuwa kama litatokea la kutokea, kitu ambacho sijakiwaza…na ahadi dhamira yangu ni hiyo kuwa kama nilivyo, kama mwenzangu katangulia basi nahitaji kutulia, kuonyesha upendo kwake, ….siwezi jua ya baadaye maana ya mungu ni mengi, …’ hapo nikaamua kuwachanganya, ili lile nililoanza nalo mwanzoni liwaweke njia panda kwanza.

‘Kama litatokea la tofauti, nitawaambia na kila kitu kitafuata utaratibu wake, ila..kuna jambo limenisikitisha sana ten asana…’nikaanza kuwatia tumbo moto. Na mwenyekiti bado alikuwa katulia, na hakuonyesha dalili ya kushituka, na bado alikuwa kaangalia mbele, akionyesha kuwa yeye ni kiongozi na anstahili kumskiliza kila mtu, hata kama linaloongewa linamkera.

‘Kama mwanafamilia ni vyema mkalijua na kama mlivyosema kama kuna kosa limefanyika ndani ya familia kufanyiwa mwanafamilia, ….na hata nje,….basi kama binadamu tunahitajika kujirudi, na hilo kosa linaweza kurekebishwa,…hilo kwakweli ni kosa mlilolifanya nyie viongozi mliolifuatilia hadi kufikia maamuzi hayo…limenisikitisha sana, na sitatulia….nasema kwa nia njema kwasababu ni haki yangu…, na naomba lije kurekebishwa…kwani kilichofanyika sio sahihi...’nikatulia na wote walikuwa kimiya, labada vikohozi, na chafya ndivyo viliskika.

‘Baba, na shemeji zangu na wanandugu wote, hilo nitakalolizungumza ndilo la ukweli na ndio ukweli wenyewe na ndivyo ilivyokuwa,…’ nikainama chini kuonyesha adabu na kuwapa nafasi ya kupumuoa na nilimuona mwenyekiti akijirekebisha kwenye kiti, kujiweka sawa, akijua kuwa kuna bomu linataka kulipuka, na mimi kwa unyenyekevu nikasema;

‘Nyie kama viongozi wetu wa familia, mumesema wazi, kuwa hamtakubali mtu kudhulumiwa haki yake,..naomba hilo liwe kweli na kwa nia moja, na kwa wote, ili kusionekane kuna ubaguzi, kwani kama itakuwa kinyume chake …mtakuwa wasaliti, …naombeni samahani kwa neno hilo, `wasaliti’ ….nina nia njema kabisa kulitamka hivyo, maana unapoahidi kitu ukaacha kukitimiza kama ulivyoahidi wewe ni msaliti, na lugha sahihi ni kuitwa mnafiki…samahani kwa kauli hiyi. 

'Nasema hili kutoka kwenye moyo wangu na mungu wangu awe ni shahidi, leo hii na kesho kiama, na kama haya nitayayowaambia ni uwongo, mungu anihukumu, na kunizalilisha...nalitamka hili kwenu na mbele ya wazazi wangu walionizaa na kunilea….’nikaanza kwa kujiapiza.

Mwenyekiti akageuka na kuniangalia, na kunikazia macho yake, mimi sikuyajali, na moyoni nikasema nitaongea kila kitu bila kuficha, na sitakubali kudhulumiwa , hata kama kwa kufanya hivyo,nitasababisha kukosana na familia nzima,…nikageuka kumwangalia baba na mama yangu, na hapo nikakumbuka usemi wao;

Mwanangu, ukiwa kwenye ukweli na haki kamwe usiogope, …sema, sema hata kama watakuchukia, lakini baadaye wakigundua ukweli watakupenda…’ Na hapo nikasema kimoyomoyo nitasema ukweli ulivyo na sitaogopa. Na mama akaniangalia huku akiwa kama ananionea huruma, lakini kwa jicho jingine, alikuwa kama ananiambia sema mwanangu kama ni ukweli sema usiogope…..

NB: Je huyu mwanamama alisema huo ukweli na aliongea nini, na alichoongea kitaweza kubadilisha hali ya hewa, angalia msimamo wa hii familia, angalia mtizamo wa huyu mama, na ni nini kitafuta baadaye..naombeni tuwe pamoja na tusaidieni kuufikishs ujumbe huu, labda nimekosea, …basi tusahihishane.

WAZO LA LEO: Mila na desturi zipo, na tumezikuta kwa wazee wetu, zipo nyingi, na nyingi hatuzijui tena kwa vile huenda hazikuwezekana kutekelezeka. Lakini kuna mambo mengi mazuri tumeyapuuzia, na kwa kufanya hivyo tumejikuta tukipata taabu sana,…nachukia kwa mfano wa kutafuta mchumba, kabla mtu hajaoa au kuolewa, wazee wetu walikuwa wakihakikisha kuwa mke au mume wa kuoa au kuolewa anatafutwa kwa kufanyika uchunguzi wa kina kwenye familia anayotoka…ni ni hekima yake, ni kuwa kwa kumpata mume au mke bora ni kwa ajili ya kizai bora, na matokeo yake ni kuwa na familia bora na hili litaweza kujenga taifa lenye amani, hili tumelipuuza, na matokea yake ndio haya..

Pia wazee wetu walikuwa wakiangalia kuwa huyo anayeolewa au kuoa, hana matatizo yoyote ya kiafya au ya kurithi, au tabia za kishirikina, au tabia zozote mbaya…haya yalikuwepo na ukiyachunguza kwa makini utayaona kuwa yalikuwa na faida zake, lakini huenda haya na mengine mengi hayapo tena tumeyapuuza.


 Wazo langu la leo. Zipo mila nzuri, tuzifuate, na kama zipo mila potofu, tuziache, au tuziboreshe ziwe bora zaidi, lakini tusisahau kabisa mila na desturi zetu zenye hekima ndani, na kukimbilia mila na desturi za wenzetu,….kwanini tupuuze mila zetu, ….huo ndio utamaduni wetu na anayeacha utamduni wake ni mtumwa.
Ni mimi: emu-three

9 comments :

Anonymous said...

I seriously love your website.. Pleasant colors & theme. Did you develop this site yourself?
Please reply back as I'm planning to create my own blog and would love to find out where you got this from or just what the theme is named. Many thanks!

Here is my web site - xxx sex

Yasinta Ngonyani said...

Inasikitisha kjwa kweli kuona kuna wengi sana wanaacha mila zetu na kujiingiza katika mila za wengine bila kujua ni nini anachokitafuta...Tupo pamoja

Anonymous said...

Hey there would you mind stating which blog platform you're using? I'm
going to start my own blog in the near future but I'm having a difficult time deciding between BlogEngine/Wordpress/B2evolution and Drupal. The reason I ask is because your layout seems different then most blogs and I'm looking for something unique.
P.S Sorry for being off-topic but I had to ask!



my web site http://www.wildpartygirls.org

Anonymous said...

You can ask every member of the family to pick his or her own chair to
add to the room, so the room consist of a part of each one
of you. Amish handcrafted furniture is still made using their famous dovetail joinery,
and by using mortise and tenon joinery. Cats are not destructive by
nature but they scratch the legs of the table or your sofa to sharpen their claws and to leave
a territorial mark.

Anonymous said...

http://acheterviagrageneriqueenligne1.com/ prix viagra
http://comprarviagragenerico25mg.com/ viagra sin receta
http://acquistareviagragenericoonline.com/ viagra acquisto
http://viagrakaufengenerika25mg.com/ viagra bestellen

Anonymous said...

achat viagra vente viagra france
comprar viagra viagra vademecum
acquistare viagra acquistare viagra
viagra kaufen kaufen viagra

Anonymous said...

buy cialis cheap buy ciais generic cialis generique cialis achat acquistare cialis costo cialis cialis generico cialis generico

Anonymous said...

http://acheter-ciajis-pascher.com/ achat cialis
http://prezzocia1isgenerico.com/ cialis
http://prix-ciajis-generique.com/ prix cialis
http://comprarcia1isgenericobarato.net/ precio cialis
http://comprargenericociajisespana.com/ venta cialis

Anonymous said...

Great post.