http://www.swahiliabroad.blogspot.com/
Tumetumwa tukaambiwa tuje, toane tuongezeke, na tukiongezeka, ina maana tunakuwa na familia, na fmilia ya huyu na yule zikiungana tunapata jamii. Jamii ili ziweze kuishi vyema ni lazima kuwa na ujirani mwema. Nashukuru kwenye hii tasinia ya mitandao ya kijamii, tuna wanajamii wengi, majirani, na leo tuna bahati ya kupata jirani mpya, mwenzetu mpendwa, kwa jina anaitwa Justin Kasyome, na ukitaka kumjua zaidi tembelea blog yake anayojulikana kama;
http://www.swahiliabroad.blogspot.com/
Tunaomba mumpokee kwa mikono miwili, kwani pamoja na mengine mengi anakuja pia kwa kuitangaza nchi yetu, ...kwenye utamaduni wetu, kwenye lugha yetu ya Taifa, kama blog yake inavyojielezea, wewe kama jirani mwema, husika kumtambulisha mwenztu huyu kwa wanajamii sote kwenye blog yako
Kwangu mimi na Diary yangu tunasema tupo pamoja.
Ni mimi: emu-three
3 comments :
Karibu sana jirani mpya
asante dada Edna ila nawe naomba unitambulish ekwako kama hautajali!
Twamkaribisha kwa mikono yopte miwili...KARIBU SANA.
Post a Comment