Siku babu aliponialezea ukweli kuhusu maisha yangu,
nilijihisi vibaya, nikajikuta najenga hasira moyoni, …sijui kwanini, ….kwanza
hata babu alipomaliza kunismulia, mwanzoni nilihisi ni moja ya zile hadithi
zake anazopenda kunismulia, lakini…..
‘Hiyo sio hadithi, huo ni ukweli kuhusu maisha yako….’akasema
babu.
‘Kwakweli, sikuamini, hadi pale nilipoamua kwenda kwa mama
na kumuomba aniambie ukweli ulivyokuwa, na kama nilivyotazamia,…. mama hakutaka
kuniambia ukweli, kwani baada ya kumuomba afanye hivyo, alijifanya ana kazi
nyingi, akawa anaendelea kufagia wakati alishamaliza kufagia....
‘Mama mimi siwezi kuamini kile alichonisimulia babu,… nataka
ukweli kutoka kwako, je hayo aliyoniambia babu ni kweli, au ananivunga na
hadithi na visa vyake, na kunifanya nihisi kuwa ni ukweli wa maisha yangu…mimi
ni kweli hayo babu aliyonisimuliai?’ nikamuuliza mama.
‘Sijui kakusimulia kitu gani….., lakini vyovyote alivyokusimulia…..,
kama ni kuhusu maisha yangu, hayo hayakuhusu kabisa…na wala usinichanganye….,
wewe bado mtoto mdogo unahitajika kusoma na sio kukimbilia kujua maisha yangu
au ya babu au bibi yako, …au…mare-he-..oh, ‘hapo akatulia, na baadaye akasema
kabla sijasema kitu;
‘Kwanza ni kwanini babu yako akusimulie mambo yasiyokuhusu….?’mama
akanigeukia na kuniangalia huku macho yakiwa yameshatanda ukungu wa machozi.
‘Maisha yako yanayofungamana na babu…kama ni hivyo
yananihusu, maana kwa maelezo ya babu wewe ulikuja kuishi naye, wakati
nazaliwa, na kumbe…..oh, mama naomba unieleze ukweli, ni kweli hayo babu
aliyoniambia…?’ nikasema kwa hasira nikiwa na mimi nimemkazia mama macho, kitu
ambacho hakikuwahi kutokea kabla katika kuishi kwangu na mama.
Kwa ujumla mimi mama yangu nampenda sana, na sikutazamia
kuwa kunaweza kukatokea jambo ambalo lingeliweza nimuone mama vinginevyo…, na
mama alijua hayo, na ilionekana wazi kuwa hata yeye hakupenda kuniumiza kwa
lolote lile kwani alinipenda sana,…na huenda ndio maana alikuwa akinificha
ukweli wote kuhusu maisha yangu.
‘Mwanangu sikiliza, hayo unayohitajia nikuelezee, hayakufai
kwasasa, sio kwamba sitaki kukuelezea, lakini kwanini nikuumize moyo wako
mwanangu, wakati huu unahitajika kutuliza kichwa chako kwa ajili ya masomo yako…elimu
yako ni muhimu kuliko hayo unayotaka kuyafahamu….na hayo hayatakusaidia kitu
zaidi ni kukusononesha moyo wako…’akasema mama.
‘Mama kiukweli , kuanzia leo, kama usiponiambia huo ukweli
wa maisha yangu, ulivyokuwa, hadi mimi nikawa sina baba…sina ndugu, tunaishi
kwa watu baki, ….akili yangu itakuwa haizingatii masomo tena….’nikasema na mama
akaniangalia kwa macho ya kusikitika, lakini nilikuwa nimezamiria hivyo, kuwa
nijue chimbuko la maisha yangu.
‘Mama,…sawa umeniambia baba yangu alifariki au sio, hayo ni
mapenzi ya mungu,…siwezi kupingana na hilo, lakini siku zote hutaki kuniambai
baba yangu alifariki vipi…inaonekana kuna kitu kimejificha kwenye kifo chake….’nikatulia
nikimwangalia mama , ambaye alibakia kuniangalia kwa macho ya huzuni.
‘Haya kuna hayo kanisimulia babu, ambayo..oh, yanasikitisha,
kuhusu bibi, hayo yana ukweli gani,….hebu niambie ni kweli hayo yalitokea…?’
nikamuuliza mama.
‘Kama nilivyokuambia awali, mimi siwezi kuota nikafahamu
hayo uliyoongea na babu yako, na sijui kwanini aliamua kukuambia hayo…ambayo
siwezi kujua ni mambo gani hasa kuhusu mimi,au huyo bibi….hebu niambie babu
yako kakuambia kitu gani?’ akauliza mama.
‘Tuanzie na hapo…kwanza kwanini unasema ‘huyo bibi….’, ni
kweli babu sio babu yangu wa kuwazaa
wazazi wako,…..ni kweli kuwa huyu babu ni babu wa kunilea tu?’ nikamuuliza.
‘Jamani hayo yote yanakuhusu nini, babu ni babu tu, awe
asiwe babu wa kumzaa mama au baba yako, yote ni sawa, yeye ni babu yako, kwanini
unamsema huyo babu kwani kakusimanga …..?’ akauliza mama.
‘Hajanisamanga lolote,..babu wa watu, siku zote ananipenda
sana, na ndio maana hapendi kunificha ukweli wa jambo lolote, na toka jana
amekuwa akinisimulia kisa ambacho nimeshangaa kuwa kumbe ni ukweli wa maisha
yangu, jinsi yalipoanzia kwa mikosi,…kwa ujumla nampenda sana babu yangu, na
sipendi kusikia watu wakisema kuwa huyo sio babu yangu, ila mimi nakushangaa
wewe mama yangu ambaye hutaki kuniambi ukweli…kila jambo unanificha, hata lile
ninalostahili kulifahamu…kwanini mama….?.’nikasema na kuamaliza kwa kuuliza.
‘Ina maana babu yako huyo kakuambia nini kinachokusumbua
hadi ufikie kuniuliza, kama kakusimulia kuhusu maisha yangu, basi inatosha,
mimi sipendi kuyaongea hayo yaliyopita,….na kama kakuambia, kuwa wewe sio
mjukuu wake halisi, mimi sipendi kusema lolote kwa sasa naomba uyaache maisha
yangu kama yalivyo…’akasema na kuinuka.
‘Mama usiponiambia ukweli, mimi sitakula, na wala sitakwenda
shule tena…’nikamwambia.
‘Sasa hapo unanitafuta ubaya, hivi, huyo babu yako
kakusimulia mambo gani…. mbona babu yako amekiuka makubaliano yetu .. ?’ akasema
mama.
‘Makubaliano gani mama ….?’ Nikauliza huku nikiwa na hasira.
‘Mwanangu achana na hayo, nafanya hivyo kwa maslahi yako,
ipo siku nitakusimulia mwanzo hadi mwisho, lakini sio kwa muda kama huu,…nielewe
mwanangu..’akasema mama.
‘Mama, ninachohitajia kujua kwa sasa ni kuwa je ni kweli
hayo babu aliyonisimulia,….maana
ninavyoona wewe una mengi….ambayo huenda hutaki mimi niyajue…sawa, labda
ni kwa ajili ya hayo yaliyotokea yanakukwaza….lakini hata mimi nina haki ya
kufahamu hayo yote,….’nikasema na kukaa chini, nikisubiri mama aongee.
Mama alitulia, na akageuka huku na kule , kama vile
anatafuta upenyo wa kukimbilia, na baadaye alatulia, akajiegemeza kwenye ufagio
aliokuwa kaushika, na kuinamisha kichwa akitumia huo ufagio kama kiegemezo,
alikaa hivyo kwa muda, na baadaye akasogea na kukaa karibu yangu, akanishika
begani akasema;
‘Mwanangu hata sijui nianzie wapi, ….kila siku nikikumuka
yaliyotokea, ninajuta sana, nikiwazia hayo yaliyotokea ….’akatulia, na
kuangalia pembeni.
‘Mwanangu , mimi na mume wangu tuliishi maisha ya shida sana
kabla hatujaweza kujenga nyumba, nyumba ambayo baadaye iligeuka sehemu ya
uwanja wa vita….nyumba niliyoitolea jasho, na kuihangaika, nikishirikiana na
mume wangu,…lakini baaadaye …oh….’hapo akatulia na kuanza kutoa machozi.
Kwakweli kwa ile hali, nikajikuta tena namuonea huruma mama…sikupenda
mama alie, kwani inavyoonyesha maisha yake ni ya huzuni,…na mikasa ya
kusikitisha, na ilionyesha kuwa akisimulia, inakuwa kama kutonesha jipu…nikatamani
nimuambia asiendelee, lakini nikaona haina haja…ni lazima nijue ukweli ulivyo…
‘Baadaye ilikuwaje mama,…ina maana kumbe ile nyumba hukuiuza,
kama mlivyoniambia awali…kumbe ilichukuliwa kwa nguvu, au sio mama, kwanini
tusiende mahakamani kama ni hivyo?’ nikauliza nikiwa na hamaki za kutaka kujua
zaidi.
‘Mahakamani!….oh, sitaki tena hayo mambo…nilihangaika hadi
nikaribie kutolewa roho…hapana, kama wameona ni jasho lao waachie wachukue,
lakini mungu atakuja kunilipizia jasho langu lilopotea bure…’akasema mama.
‘Mama kama ni haki ukienda mahakamani utaipata tu….’nikwambia
mama, na yeye akaendelea kuonga akisema;
‘Mwanangu mimi na mume wangu tulipooana hatukuwa na lolote,
yalikuwa ni maisha ya kubangaiza tu, hakuna mbele wa nyuma, ….na hata kuja
kuishi naye ilikuwa kwa bahati tu, kwani alishanifukuza moyoni mwake, toka siku
ile nilipomtamkia kuwa nina ujauzito wako…lakini ya mungu mengi…..’akatulia na
kuangalia juu. na machozi yakaanza kumtoka, na baadaye akainamisha kichwa chini akiwa kakishikilia....
Alipofika hapo, nikajikuta nakumbuka maelezo ya babu, ambaye
ndiye alinifanya nimsakame mama ili anihakikishie kuwa hayo babu aliyoongea ni
kweli,..nikawa nayakumbuka maongezi yangu na babu huku mama naye kiongea yale
yale aliyonisimulia babu
*******
‘Mama yako alipata shida sana, kwenye uja uzito wako, wazazi
wake walimtimua nyumbani wakidai kuwa kaleta mkosi , na aibu nyumbani, kwahiyo aende
huko huko kwa aliyempa huo uja uzito huo, ….na alipokwenda kwa huyo mwanaume, naye
akamfukuza kwa panga, na kusema hamjui, na wala hataki kusikia lolote kutoka
kwake…’babu yake ndivyo alivyomsimulia mjukuu wake.
‘Mimi siitambui hiyo mimba, na niskuone ukifika hapa kwangu
tena….’akasema huyo mwanaume
‘Kwahiyo babu ndio kusema kuwa mimi sina baba, au ni kweli
kuwa mama alikuwa na baba wengi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua baba
yangu ni nani, kwa maana hiyo mama yangu alikuwa akifanya….oh,….?’ Hapo nikatulia
kusema lolote, nikimwangalia babu.
‘Hapana, mama yako hakuwa muhuni,..ni ujana tu ulimdanganya,
kwani rafiki yake alikuwa huyo huyo, na walianza urafiki wao wakiwa wadogo,
wakazoeana, na kwa vile wazazi hawakujaribu kuwaasa au kuwaelekeza ubaya wa
kuingia mambo ya kikubwa mapema, basi wakajikuta wametenda kosa,
lilomsababishia mama yako kupata shida …..’akasema babu.
‘Baba unaye….kwani katika maisha ya binadamu, hakuna asiye
na baba, hata kama baba huyo ilitokea akafariki mapema, bila kumuona, lakini kiukweli
baba alikuwepo, ….’akasema babu.
‘Ila ilivyotokea ni kuwa mama yako, alipomfikia huyo
mwenzake…alimkana, katu katu akamkana na kujifanya hamjui tena…’akasema babu.
‘Mama yako alipofukuzwa kwao, yeye aliona jambo jema ni
kumuendea huyo mwenzake, na kumueelzea ukweli, japokuwa hakuwahi kumwambia
mapema kuwa katiak hayo wliyokuwa wakifanya mambo yameharibika….’akatulia babu.
‘Mama yako alifanya kosa, hilo, kuwa ilitakiwa kumwambia
mwenzake mapema, kuwa mambo yameharibika, na ili akisakamwa na wazazi wake,
aweze kumtaja huyo mwenzake, lakini hakuwahi kufanya hivyo, huenda alikuwa
akisubiri wakati muafaka….’akatulia babu.
‘Baada ya kufukuzwa kwao, akamwendea mwenzake, na huku akiwa
na matumaini ya kupokewa vyema, kama walivyokuwa wakifanya hivyo siku zote,
lakini mwenzake alipomuoana mama yako akija na kanga kichwani, akahisi kuna
jambo kubwa
‘Wewe vipi, mbona unakuja kwangu saa hizi, siku zote
unanimabia kuwa huwezi kuja kwangu muda kama huu, wazazi waki ni wakali, sas
aumefuata nini muda kama huu, usiniletee matatizo, …’akasema huyo mwanaume,
wakati huo ni vijana’akasema babu.
‘Nimefukuzwa nyumbani…’akasema mama yako.
‘Eti nini, umefukuzwa nyumbani, …ndio unakimbilia kwangu,
kwani hapa ni seehmu ya kuhifadhi wakimbizi, ….hapana nenda kwa ndugu zako, sio
hapa, utaniletea matatizo bure….’akasema huyo rafiki yake.
‘Yaani leo hutaki kunipokea kama siku nyingine, kwa vile tu
nimekuambai kuwa nimefukuzwa, na wala hutaki kujua kwanini nimefukuzwa?’
akauliza mama.
‘Sihitaji kujua, ….kwanza nijue ili iweje, wewe ondoka hapa
kwangu, sitaki matatizo, kwani baba yako alishanichimbia mkwara, …namuogopa
sana….’akasema huyo mwanaume.
‘Mimi nimekuja kwako kwasabbu nina uja uzito wako….’akasema
mama yako bila kusubiri kuulizwa ni kisa gani kilichomfanya afukuzwe na
kukimbilia kwa huyo jamaa.
‘Eti nini, una ujauzito wangu….ooh, ondoka ondoka tena
haraka, nenda huko huko kwa hawo waliokupa huo ujauzito, mimi sikujui, na wala
sijui huo ujauzito……ondoka…sitaki hata kukuona….umenielewa, nasema ondoka
haraka…usinitolee macho hapa kama unataka kukata roho….’akasema huyo mwanaume
bila aibu huku mama akitoa macho ya kushangaa,hakuamini kuwa huyu ndiye yule
aliyekuwa mpenzi wake, ambaye kila wakikutana ilikuwa ni mpenzi, daling, nakupenda….
‘Yaani leo hii unanikataa,kwasabbu ya huu uja uzito…wakati
mwanaume ninayemjua ni wewe peke yako na wewe unatambua hivyo, na karibu watu
wengi wanafahamu hivyo, haiwezekani, mimi siondoki humu ndani…’akasema mama
huku bado akiwa haamini.
‘Ohooh, hivi unitambui mimi eeeh,….unasema…., huondoki humu
ndani kwangu, ngoja nikuonyeshe kazi….’akasema huyo mwanaume na akachepuka
kidogo, na aliporudi alikuwa kashikilia sime, …ikiwa inameremeta, akaja nayo, na kabla
hajasema kitu akampiga mama mgongoni na hiyo sime kwa ubapa, na alimpiga kwa
pigo la nguvu..’akasema babu.
‘Nakumbia usipoondoka hapa ukiwa hai basi, nitakuondoa mwenyewe
ukiwa maiti....’akasema huyo mwanaume, na mama yako alipomwanglia huyo jamaa,
akajua kweli mwenzake kazamiria ….kweli ile sura ilikuwa ya kiuaji, sura ambayo
aliiona mara moja wakati jamaa huyo alipokuwa akipambana na wabakaji waliotaka
kumbaka huyo mama, kipindi cha nyuma.
Siku hiyo mama yako, alikuwa katoka kwa huyo jamaa, na
wakati yupo njiani akirudi kwao, mara akakutana na hawo wabakaji, wavuta bangi,
wakamshika mama yao na kuanza kumburuza vichakani,…..mama yako akawahi kupiga ukulele,
na jamaa , akasikia sauti ya mpenzi wake. Hakusubiri, aakfuatilia hiyo sauti.
Alipofika hapo kichakani, akawakuta jamaa wakiwa wanajiandaa
kufanya mambo ya machafu, huyo jamaa mzuka ukampanda, akabadilika na kuwa
mnyama, aliwarukia hawo watu na kutoa kipigo ambacho kilikuwa ni cha kuua….
Wale jamaa, walitoka hapo, wakiwa wameumizwa vibaya sana, na
ilibidi wajitahidi kukimbia kwa shida, kwani kila hatua, umauti ulikuwa
ukiwaita….wakakimbia, na mama yako, alibakia kuduwaa akimwangalia huyo jamaa
yake…..hakuamini kuwa ndiye yule yule anayemfahamu.
‘Alibadilika sura, ikawa kama sio yake, macho yake aliyatoa
pima, na kubadilika rangi na kuwa mekundu,…alitisha, na hata alipomaliza
kuwaadhibu hawo watu, mama yakoa ansema aliogopa kabida kuandamana na huyo
jamaa yake.
Sura kama hiyo akaiona siku hiyo….akajua kuwa akiendelea
kubakai hapo, atafanywa , kama walivyofanywa hawo jamaa waliotaka kumbaka, ….
ikabidi atokea nje na kukimbia….’akasema babu na kutulia, na kuniacha nikiwaza,
ina maana baba huyo ni yupi, ni huyo marehemu, au kuna baba mwingine.
‘Babu.... baba ni yupi huyo?’ nikamuuliza.
*******
NB: Oh, kisa hiki kimeanzia hapo, ngoja nikusanye nguvu,
tukijalia tena nitakuja na mambo mapya ya kisa hiki.
WAZO LA LEO:
Mnapokuwa marafiki, mke na mume,…(hasa vijana ambao wa shuleni) jaribu sana kuangalia
athari za matendo yenu, kwani kosa dogo tu linaweza kuwaharibia mipnagilio ya
maisha yenu ya baadaye , …..
Kwanza jiulizeni, je wakati umefika wa kufanya hilo
mnalotaka kulifanya, je kweli hayo ndio mapenzi ya ukweli, au ni tamaa za
kimwili tu. Subirini, pangeni na kukubalina kabla ya kujiingiza kwenye
mahusiano ya ndani.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
viebrasqueeva xaikalitag Fawtrarse [url=http://usillumaror.com]iziananatt[/url] PrieriRes http://gussannghor.com Kepthughele
Kisa cha kujifunza mengi sana...Ila nimekuwa najiuliza mara nyingi sana kwanini wanaume wakimpa mimba msichana wanakataa kabisa na kumfukuza?
kisa hiki kinafundisha mengi sana
inatufundisha sn
Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
* upendo
inaelezea * inaelezea kivutio
* kama unataka ex wako nyuma
*acha talaka
* kuvunja obsessions
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa kinga
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
* bahati nasibu
* uchawi wa bahati
Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp:+2349046229159
Post a Comment