‘Krutaaah…’ sauti kali ya kijeshi ikasikia,
na mara sauti nyingine ndani ya kundi ikatoka bila hata kutegemea.
‘Mojaah’…
Watu wakageuka upande ule sauti ilipotokea
wakishangaa, na mara yule jamaa mbaye alisema mara ya kwanza neno `kruta’
akasogea pale sauti ya `moja’ ilipotokea na kuwasimamisha vijana watatu,
akawaambia wamfuate.
Sote tuliokuwa pale ndani tukabakia
tumeshangaa, na hapo nikakumbuka wakati nipo ndani ya mujibu wa sheria, kwenye jeshi la kujenga taifa, ambapo vijana
wengi wakimaliza kidato cha sita hulazimia kupitia mwaka mmoja jeshini. Mwaka
huo uligawanyika sehemu mbili, miezi sita ya mwanzo ni mafunzo ya kijeshi na
ukakamavu , na miezi sita mingine na kazi za kujenga taifa.
Hapo nikakumbuka kuwa unapojiunga jeshini
kwa mara ya kwanza , mnatambulikana kwa jina hilo la kruta, kuwa nyie hamjui
lolote, na kila amri ikitolewa ili uifuatilie vyema unahesabu, …kama ni kitendo
kimoja utasema `mojaaa’ kwa ukakamavu. Na hata ukiitwa unatakiwa kusema neno
hilo, `mojaa’ wakimaanisha wewe hujajua chochote na hiyo lugha ndio lugha yako
ya awali.
Mtaendelea hivyo hivyo kwa muda, kuwa kila
jambo akiamrisha afendi wenu, mnaitikia hivyo, na ukiwa mlegevu, kuitamka hiyo
moja, utaadhibiwa, …lazima utamke kwa ukakamavu na kusimama kwa ukakamavu,
…..na hata wakati wa kutembea unatakiwa uwe unaimba, kwani wewe hujajua, na kutembea kwako ni kwa kunyakua,…Unanyauka huku umeweka mikono mbele ya kifua….
Hizo ni sheria na taratibu za kijehi,
ambazo humjenga mtahiniwa, kuwa na nidhamu, nidhamu ambayo baadaye utaiona matokea yake. Kwani ikifikia hatua za mbele kila askari anajua nafasi yake, na
ni jinsi gani anatakiwa amuheshimu kiongozi wake,…hili halikutokea hivi hivi tu,
bali lilianza pale huyo mtahiniwa alipokaribishwa na kuanza kujengwa kimaadili
ya kijeshi...ukakamavu, utii, na uwajibikaji!
Katika jamii yoyote ukianzia ngazi ya
familia, kuna taratibu mbalimbali zimewekwa ndani ya familia husika au jamii husika, nia na lengo ni kuwa na mfumo
mmoja, mfumo utakaojenga nidhamu na utii, . Sizani kwamba jamii au
taifa, linaweza likawa linaishi ovyo ovyo, tu, hakuna kitu kama hicho, ndio
maana kuna sheria, ndio maana kuna KATIBA.
KATIBA ya nchi ndio taratibu mama, japo
kuwa ndani yake kunataribu nyinginezo, zikiwemo za kidini, ambazo Katiba haiwezi ikaingilia huko, ila inazilindia na kuhakikisha taratibu hizo zinafuatwa na walengwa husika, bila kubughudhiwa. Kila dini ina namna yake ya kuabudu, katiba
haiwezi ikasema lazima tuwe na mfumo mmoja wa kuabudu, hapo itakuwa imeingilia
uhuru wa imani za watu. Lakini katiba lazima iwepo ili kulindia hizo imani, na
uhuru wa kuabudu.
Sasa hivi tupo katika mchakato wa kukusanya
maoni ya katiba yetu, na watu maalumu wanapita sehemu mbali mbali na kuwakusanya
watu ili watoe maoni yao kuhusina na katiba. Na wale wenye nafasi hufika kwenye
hivyo vikao, …ukiangalia idadi ya watu wanaohudhuria ni ndogo sana. Ni ndogo
sana ukilinganisha na uzito wa hicho kitu chenyewe.
Katiba ndio mfumo wa nchi, ndio taratibu
ambazo kila mtu anatakiwa azifuate, hili lilitakiwa lijulikane na kila raia, na
ili lijulikane ilitakiwa kila raia kwanza aijue katiba yake, ajue taratibu zake
za nchi, ili akiwa katika utendaji wake wa kikazi, akiwa anawajiba na mambo
yote ya kijamii, asiende kinyume na katiba yake. Lakini je watu wanalijua hilo?...je
ni raia wangapi wanaijua katiba yao? Je somo la uraia shuleni linaeleweka
vyema? Na raia wa kawaida wanahusishwaje na somo hilo ?
Nakumb uka kipindi cha mwalimu nyerere,
kulikuwa na njia nyingi za kuhamasishana, huwa hata akitoa hotuba zake, vikundi
vya miziki, vikundi vya utaamduni na hata mshuleni, wanakaririri maneno yale ya
hotuba. Ni njia mojawapo ya propaganda, iliyosaidia kila mmoja kuelewa nini
kiongozi wake anataka, na kweli kuanzia mtoto hadi mkubwa akawa anaelewa, na
ukumbuke kulikuwa hakuna runinga.
Kusudio langu hapa ni kutaka kuelezea
umuhimu wa kuelimisha jamii katika kila jambo, ya kuwa jamii kama jamii
inahitaji msukumo, ili ielewe na kufuata taratibu zilizokubalika, na hili
haliweze kufanyika na kutekelezwa kirahisi, kunahitaji juhudi za ziada. Kwa
mfani sasa hivi jamii kubwa imezama kwenye mambo ya mawasiliano ya kutizama,
kama runinga, …simu za mikononi,..hata redio sasa hivi hazina nafasi sana.
Ni vyema viongozi wetu wakatumia vifaa
hivyo kufikisha ujumbe , kwani ingawaje tupo kwenye michakato ya kukusanya
maoni ya katiba, lakini asimilia kubwa ya wananchi hawajui katiba ni nini, na
hata kilichokuwepo kwenye katiba hawakijui japokuwa sehemu kubwa yake
wanaitenda kimatendo,…
Ndio hapo nikakumbuka taratibu za kijeshi
kuwa raia, au watu kwa ujumla wengi wao ili waweze kufuta vyema taratibu za
kijamii, ili waweze kuelewa vyema taratibu za kijamii, wanahitaji msukumo, na
msukumo huo unaweza kuanzia mahali, …kama sasa hivi ndio mchakato wa kukusanya
maoni, kwetu sisi kizazi kipya ndio kama kruta jeshini, tuanze kuelimisha jamii
kwa kila njia ili hata wakiwa wapi, ukisema moja , watasimama ….na hapo utajua
huyo ni Mtanzania.
Kawaida
ili ujue ugumu wa jambo, ni pale unapoanza kulitenda, na jinsi unavyosonga
mbele ndivyo unavyogundua jinsi gani vyema ya kulifanya hilo jambo ili liwe
rahisi zaidi, ili liwe na manufaa zaidi na ili lisilete manung’uniko kwa baadhi
ya watu, ndio maana watu, ndio maana taifa, ndio maana viongozi , ndio maana
raia wakaona kuna umuhimu wa kuipitia hiyo katiba upya, kutoa maoni na huenda
tukapata kitu chenya manufaa kwa raia wote. Sasa ni muhimu hili likapewa
kipaumbele…tusije tukaruka mkojo na kukanyaga…
Hilo ndio wazo letu la ijumaa ya leo:
IJUMAA NJEMA.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Ni kweli katiba wengi hawaijui, wanaisikia tu!
Wananchi wanahitaji elimu kuhusu katiba kwani si wote waliosoma huo uraia, hakuna atakaewapa hyo elimu zaidi ya hao viongozi waliowachagua kusimamia hiyo katiba, vinginevyo watakuwa wakichangia kitu wasichokijua na mwisho wa siku matatizo yakaongeza.
Post a Comment