Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, December 14, 2012

Ugumu wa kazi ni kuitenda



‘Krutaaah…’ sauti kali ya kijeshi ikasikia, na mara sauti nyingine ndani ya kundi ikatoka bila hata kutegemea.

‘Mojaah’…

Watu wakageuka upande ule sauti ilipotokea wakishangaa, na mara yule jamaa mbaye alisema mara ya kwanza neno `kruta’ akasogea pale sauti ya `moja’ ilipotokea na kuwasimamisha vijana watatu, akawaambia wamfuate.

Sote tuliokuwa pale ndani tukabakia tumeshangaa, na hapo nikakumbuka wakati nipo ndani ya mujibu wa sheria, kwenye jeshi la kujenga taifa, ambapo vijana wengi wakimaliza kidato cha sita hulazimia kupitia mwaka mmoja jeshini. Mwaka huo uligawanyika sehemu mbili, miezi sita ya mwanzo ni mafunzo ya kijeshi na ukakamavu , na miezi sita mingine na kazi za kujenga taifa.

Hapo nikakumbuka kuwa unapojiunga jeshini kwa mara ya kwanza , mnatambulikana kwa jina hilo la kruta, kuwa nyie hamjui lolote, na kila amri ikitolewa ili uifuatilie vyema unahesabu, …kama ni kitendo kimoja utasema `mojaaa’ kwa ukakamavu. Na hata ukiitwa unatakiwa kusema neno hilo, `mojaa’ wakimaanisha wewe hujajua chochote na hiyo lugha ndio lugha yako ya awali.

Mtaendelea hivyo hivyo kwa muda, kuwa kila jambo akiamrisha afendi wenu, mnaitikia hivyo, na ukiwa mlegevu, kuitamka hiyo moja, utaadhibiwa, …lazima utamke kwa ukakamavu na kusimama kwa ukakamavu, …..na hata wakati wa kutembea unatakiwa uwe unaimba, kwani wewe hujajua, na kutembea kwako ni kwa kunyakua,…Unanyauka huku umeweka mikono mbele ya kifua….

Hizo ni sheria na taratibu za kijehi, ambazo humjenga mtahiniwa, kuwa na nidhamu, nidhamu ambayo baadaye utaiona matokea yake. Kwani ikifikia hatua za mbele kila askari anajua nafasi yake, na ni jinsi gani anatakiwa amuheshimu kiongozi wake,…hili halikutokea hivi hivi tu, bali lilianza pale huyo mtahiniwa alipokaribishwa na kuanza kujengwa kimaadili ya kijeshi...ukakamavu, utii, na uwajibikaji!

Katika jamii yoyote ukianzia ngazi ya familia, kuna taratibu mbalimbali zimewekwa ndani ya familia husika au jamii husika, nia na lengo ni kuwa na mfumo mmoja, mfumo utakaojenga nidhamu na utii, . Sizani kwamba jamii au taifa, linaweza likawa linaishi ovyo ovyo, tu, hakuna kitu kama hicho, ndio maana kuna sheria, ndio maana kuna KATIBA.

KATIBA ya nchi ndio taratibu mama, japo kuwa ndani yake kunataribu nyinginezo, zikiwemo za kidini, ambazo Katiba haiwezi ikaingilia huko, ila inazilindia na kuhakikisha taratibu hizo zinafuatwa na walengwa husika, bila kubughudhiwa. Kila dini ina namna yake ya kuabudu, katiba haiwezi ikasema lazima tuwe na mfumo mmoja wa kuabudu, hapo itakuwa imeingilia uhuru wa imani za watu. Lakini katiba lazima iwepo ili kulindia hizo imani, na uhuru wa kuabudu.

Sasa hivi tupo katika mchakato wa kukusanya maoni ya katiba yetu, na watu maalumu wanapita sehemu mbali mbali na kuwakusanya watu ili watoe maoni yao kuhusina na katiba. Na wale wenye nafasi hufika kwenye hivyo vikao, …ukiangalia idadi ya watu wanaohudhuria ni ndogo sana. Ni ndogo sana ukilinganisha na uzito wa hicho kitu chenyewe.

Katiba ndio mfumo wa nchi, ndio taratibu ambazo kila mtu anatakiwa azifuate, hili lilitakiwa lijulikane na kila raia, na ili lijulikane ilitakiwa kila raia kwanza aijue katiba yake, ajue taratibu zake za nchi, ili akiwa katika utendaji wake wa kikazi, akiwa anawajiba na mambo yote ya kijamii, asiende kinyume na katiba yake. Lakini je watu wanalijua hilo?...je ni raia wangapi wanaijua katiba yao? Je somo la uraia shuleni linaeleweka vyema? Na raia wa kawaida wanahusishwaje na somo hilo ?

Nakumb uka kipindi cha mwalimu nyerere, kulikuwa na njia nyingi za kuhamasishana, huwa hata akitoa hotuba zake, vikundi vya miziki, vikundi vya utaamduni na hata mshuleni, wanakaririri maneno yale ya hotuba. Ni njia mojawapo ya propaganda, iliyosaidia kila mmoja kuelewa nini kiongozi wake anataka, na kweli kuanzia mtoto hadi mkubwa akawa anaelewa, na ukumbuke kulikuwa hakuna runinga.

Kusudio langu hapa ni kutaka kuelezea umuhimu wa kuelimisha jamii katika kila jambo, ya kuwa jamii kama jamii inahitaji msukumo, ili ielewe na kufuata taratibu zilizokubalika, na hili haliweze kufanyika na kutekelezwa kirahisi, kunahitaji juhudi za ziada. Kwa mfani sasa hivi jamii kubwa imezama kwenye mambo ya mawasiliano ya kutizama, kama runinga, …simu za mikononi,..hata redio sasa hivi hazina nafasi sana.

Ni vyema viongozi wetu wakatumia vifaa hivyo kufikisha ujumbe , kwani ingawaje tupo kwenye michakato ya kukusanya maoni ya katiba, lakini asimilia kubwa ya wananchi hawajui katiba ni nini, na hata kilichokuwepo kwenye katiba hawakijui japokuwa sehemu kubwa yake wanaitenda kimatendo,…

Ndio hapo nikakumbuka taratibu za kijeshi kuwa raia, au watu kwa ujumla wengi wao ili waweze kufuta vyema taratibu za kijamii, ili waweze kuelewa vyema taratibu za kijamii, wanahitaji msukumo, na msukumo huo unaweza kuanzia mahali, …kama sasa hivi ndio mchakato wa kukusanya maoni, kwetu sisi kizazi kipya ndio kama kruta jeshini, tuanze kuelimisha jamii kwa kila njia ili hata wakiwa wapi, ukisema moja , watasimama ….na hapo utajua huyo ni Mtanzania.

 Kawaida ili ujue ugumu wa jambo, ni pale unapoanza kulitenda, na jinsi unavyosonga mbele ndivyo unavyogundua jinsi gani vyema ya kulifanya hilo jambo ili liwe rahisi zaidi, ili liwe na manufaa zaidi na ili lisilete manung’uniko kwa baadhi ya watu, ndio maana watu, ndio maana taifa, ndio maana viongozi , ndio maana raia wakaona kuna umuhimu wa kuipitia hiyo katiba upya, kutoa maoni na huenda tukapata kitu chenya manufaa kwa raia wote. Sasa ni muhimu hili likapewa kipaumbele…tusije tukaruka mkojo na kukanyaga…

Hilo ndio wazo letu la ijumaa ya leo: IJUMAA NJEMA.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Ni kweli katiba wengi hawaijui, wanaisikia tu!

Labi martin said...

Wananchi wanahitaji elimu kuhusu katiba kwani si wote waliosoma huo uraia, hakuna atakaewapa hyo elimu zaidi ya hao viongozi waliowachagua kusimamia hiyo katiba, vinginevyo watakuwa wakichangia kitu wasichokijua na mwisho wa siku matatizo yakaongeza.