‘Mke wangu inaonekana
wahasimu wameshakusanya kikosi chao cha maaskari na inaaminika kuwa wapo kwenye
ngome yao muhimu, hatujui wana maana gani, na kwa hilo inabidi tujiandae kwa
lolote na hata ikibidi kuingia vitani kwa maslahi ya wanajamii….’akasema
mfalme.
‘Vitani……?’ ‘akauliza
malikia mtarajiwa akiomba hilo lipitie mbali, na akabakia ameduwaa akimwangalia
mume wake, je ni nini kitatokea hebu tuendelee kidogo na sehemu hii……
‘Mke wangu hali invyoonyesha ni kuwa wenzetu wamezamiria
vita kiukweli, labda tutii matakwa yao, ambayo kuyatii kwetu ni kama kujitia
kitanzi wenyewe,….’akasema mfalme mtarajiwa.
‘Kwani wao wanataka nini hasa, wanataka hayo madaraka, au
kuna kingine cha zaidi?’ akauliza malikia .
‘Wanataka madaraka, wanataka waendelee kutawala kama
walivyokuwa wakitawala na kijana wao awe ndiye mfalme wa jamii yetu, wakidao
ndiye mfalme aliyetabiriwa’akasema mfalme.
‘Eti nini, kwa sifa gani alizokuwa nazo hadi wadaii hivyo,
mbona hata wananchi watawacheka, maana huyo kijana hana hizo sifa kabisa, mimi
mwenyewe nimekuwa nikilumbana naye kipindi ambacho haupo, akidai kuwa anioe kwa
vile wewe umeshaliwa na mamba, …..hapana huyo hafai, ….na hilo la vita sizani
kama wanaweza kufanya hivyo’akasema malikia.
‘Wewe kama mama lazima useme hivyo, kwa vile unawatetea
watoto wako au sio?’ akasema mfalme kimzaha.
‘Sio kwamba na watetea, ….ila naona wao wanatumia mbinu za
kushinikiza, kwasababu wenyewe kwenye imani zenu mlisema akitokea mfalme
mtarajiwa hakutakuwa na vita tena, sasa kwanini wajiandae kwa vita?’ akauliza
malikia.
‘Wao wanataka vita kwa vile wanadai kuwa mimi sio mfalme
mtarajiwa, sina hizo sifa, na sifa hizo nimezishinikiza kwa vile nimekuoa wewe’akasema
na kumwangalia mke wake.
‘Mimi mume wangu sipendi kabisa vita,….kama inabidi
nitajitolea kwenda kuongea na wao, ili niwashawishi kusitokee vita’akasema
malikia na mfalme akamwangalia kwa mshangao.
‘Wewe huwajui hawa watu, ….hata kama wewe ni malikia mtu
waneyekuheshimu sana, hawataweza kukusikiliza kama matakwa yao hayajatimizwa,
tunamfahamu sana huyo mzee,…ila mimi nilikuwa na mawazo mengine’akatulia
mfalme.
‘Mawazo gani mume wangu, maana mimi naheshimu sana mawazo
yako, huwa kila ukitoa mawazo yanakuwa yenye tija, hata wanachi wengi
wanakusifia kwa hilo, na wana hamasa kubwa ya kuona mabadiliko, wenyewe
wanasema hata kabla hujatawazwa, wameshaanza kuiona neema, wana uhuru, wana
amani,…na maendelea yameshaanza kujitokeza’akasema malikia.
‘Mimi na wewe ni wazazi, japokuwa hatujabahatika kupata
watoto, lakini tuna ile hisia ya kuwa na familia, hebu chukulia mimi naenda
vitani nauwawa, utajisikiaje,….haya chukulia wale ambao ni hali duni kabisa,
walikuwa wakimetegemea baab yao kwa kila kitu, na kaenda vitani kauwawa,….sizani
kama inaleta picha nzuri…
‘Mume wangu unataka kusema nini….’akauliza malikia.
‘Ninachotaka kusema
ni kuwa vita sio nzuri, na ni vyema tukajitahidi kuikwepa kwa nguvu zote,…maana
kila mmoja ni mzazi , na kama ikija vita uzazi huo hautakuwa na maana tena,
kwani tutatarajia kupotea kwa watu wengi, wanawake wengi wtabakia wajane,
watoto watabakia mayatima,….na vita kama vita haina macho, …sio tu wanaume ndio
watauwawa, hata wanawake,watoto na wazee…
‘Sasa mimi nataka kulikwepa hilo, kwa kuchukua maamuzi
magumu, ….’akatulia.Mkewe naye akatulia kuskia hayao maamuzi magumu.
‘Yote hayo tatizo ni mimi, ….huenda angelichaguliwa
mwingine, kama mfalme mtarajiwa kusingelikuwa na haya yote….sasa kumbe tatizo
ni mimi,….mimi ni na thamani gani mbele ya watu , mbele ya roho za watu
zitakazo teketea, ….yaani watu mamia wafe kwa ajili ya roho yangu mimi, mtu
mmoja, hapana, hapo ndio naona lazima nichukuea maamuzi magumu’akatulia, na
malikia akakodoa macho akiogopa kusikia hilo analohisi ndilo mume wake anataka
kulisema.
‘Nimeonga na babu, kanipinga kwa nguvu zote….na kuniambia
mimi nitakuwa msaliti….lakini uwezo wa mwisho ni wangu mimi, …lolote likitokea
nitakayeumia sana ni mimi …najua wewe tupo pamoja, lakini mwisho wa siku kila
mtu ataninyoshea kidole mimi,…ndio maana nasema nahitaji kuchukua maamuzi
magumu, ….’akatulia.
‘Maamuzi gani mume wangu?’ akauliza malikia.
‘Wao unahisi wanataka tu hayo madaraka…hapana ni pamoja na
roho yangu, hasa mimi na babu, kila kukicha wanatunga mbinu, na hata kama
utawapa hayo madaraka, hawatatulia wakituoni sisi tunapumua…ndio tabia ya hawa
watu, watu kama hawa hawatosheki hata kama ungeliwapa dunia hii yote, mpaka
wasikuone hapa duniani….’akatulia.
‘Kwahiyo unataka kusema nini mume wangu…..?’ akauliza
malikia.
‘Kwanza nahitaji maoni yako, …Je tufanyeje ili kuepushja
hivi vita, je upo tayari kwa mawazo yangu,na maamuzi yangu magumu, hata ikibidi
…..ndoa…’kabla hajamaliza mlango ukagongwa, na malikia akabakia ameduwaa. Mume
akasimama na kwenda kumuona aliyegonga, na akaingia babu, akiwa na wasaidizi
wake.
Wote walipoingia wakapiga magoti mbele yake, na kumuacha kijana wao akiwa ameshangaa, na akaanza kuwainua mmoja mmoja, lakini walikuwa wametulia huku wameinamisha vichwa vyao chini.
********
Mfalme mtarajiwa akaitisha kikao cha usalama, na viongozi wa
kivita na pia aliwahusisha viongozi wa
usalama wa raia na wote wakafika kumsikia mfalme mtarajiwa anataka kusema nini.
Baada ya kuongea na vikosi hivyo, akawaambia alichokusudia na wao wakamwambia
kama sio yeye, wao hawatamkubali
mwingine yoyote.
Baadaye akaitisha mkutano mkuu, ambao mwanzoni alipanga uwe
wa wajumbe wawakilishi tu, na wakuu mbali mbali wa koo, ili asikie maoni yao.
Kikao hiki badala ya kuja wawakilishi pekee, wakafika watu wengi, kwani kila
alieyesikia kuwa kiongozi wao ambaye walikuwa wamemsubiria miaka mingi anataka
kukaa pembeni ili kuepusha vita, aliona afike asikie kwa masikio yake mwenyewe.
Na hapo mfalme mtarajiwa akajua kuwa sasa haongei na
wawakilishi tu, anaongea na sehemu kubwa ya wananchi wanaomtegemea kwa lolote
lile, hakutaka kuwaficha alianza moja kwa moja kwa kuwapa taarifa kuwa wahasimu
wameingia msituni, na inavyoonekana wamejiandaa kwa vita,…
‘Najua mtauliza kwanini, ikiwa bado mfalme hajatawadhwa, na
kwanini wafanye hivyo, wakati tunatarajia ujumbe muhimu toka huko makaoni…ujumbe
huo utakuja, lakini unakuja kwa ajili ya kusikiliza tuhuma zilizopelekwa kwao,
ndio maana hata shughuli za kutawadhwa kwa mfamle mtarajiwa zimesitishwa kwa
muda…’akasema mfalme mtarajiwa.
‘Tungelikuwa wakorofi, shughuli hizo zingelifanyika kwani
yale muhimu yaliyokuwa yakitarajiwa na wanachi yalishatimia,….lakini hatuna
haraka na hilo, kwani uongozi bora ni ule unaojali matakwa na masahi ya raia
wote, ikiwemo wao….’akasema mfalme mtarajiwa.
‘Wenzetu, wamejifanya kuwa mimi sio huyo mfalme mtarajiwa,
hata baada ya dalili zote zilizotabiriwa kuonekana…hii ni kwa vile wao walitaka
kijana wao mdio awe mfalme. Wao wanadai kuwa ukoo wetu una kasoro nyingi, na
kwahiyo haiwezekani mfalme akatoke kwenye ukoo wetu.
‘Na kwa vile ukoo wetu na wao umekuwa ni mahasimu wa
kihistoria, hawakubali kabisa tukae kiti
kimoja, na hasa tukiwa sisi ndio watawala, huenda wangekubali hivyo kama wao
ndio watawala na katikamaisha yangu yote toka utotoni sijaona wakikubaliana na
jambo lolote lilitoka kwenye ukoo wetu.
‘Kwa vile hapa hatupo kisiasa zaidi, tupo kijeshi zaidi, nisingependa
kuwapotezea muda wenu, lakini inabidi niwaweke wazi, ili wakati mkiziaga
familia zetu huku majumbani kwenu, kuwa tunakwenda vitani mjue jinsi gani ya
kuwaelezea, vita sio lele mama, vita inaleta majozni , inaleta umasikini ni
kitu kisichopendeza kwa ujumla, kwahiyo faraja kwa familia zinahitajika
…’akatulia kidogo.
‘Sisi hatupendi na wala hatutaki kulazimisha vita, lakini
wenzetu wanaamua kuanzisha vita….na kama wanataka kufanya hivyo, hatutakaa hivi
tu, wafanye wanalotaka,….tunahitajika kujihami, tunahitajika kuwalinda raia
zetu, mifugo yetu na uhuru wetu, …..’akatulia na kuwaangalia wenzake.
‘Mimi kama ingelikuwa uwezo wangu, ningeliachia hii nafasi
kwanza ili kuepusha hiyo vita, kwani uongozi ni kitu gani, na matakwa ya uma kwa
masilahi ya uma, sio kwa matakwa ya watu binafsi …ndio maana nimewaita, kuwa
ili tuepusha hii vita kwanini mimi nisijitoe kwanza, kwanini kuwepo kwangu kwa
mfalme mtarajiwa iwe ni tatizo, au ni kwasababu ya ukoo wetu. Kama ni hivyo,
basi mimi nipo tayari kukaa pembeni,….hili nimelileta kwenu kama wawakilishi wa
wananchi, ili nyie mlifikirie kwa makini.
‘Labda niwaambie ukweli kuwa mimi sikuwa na wazo kama hilo
kuwa mimi nitakuwa mfalme, sikuwa najua kuwa mimi ndiye mtarajiwa, ….japo kuwa
babu alikuwa akiniambia kuwa kaota, au kaona dalili hizo kwangu….kuwa mimi huenda
nikawa ndiye huyo mtarajiwa…alikuwa akiniambia hivyo kama utani tu,,,'
akasema
akigeuka kule walipokaa wazee.
‘Nakumbuka hata siku ile nilipowasili hapa kama alivyotabiri
huyo mtabiri, hakumini, na alinimbia kabisa, kuwa yeye alijua huyo mtu atakuwa
mtu tofauti kabisa, hakuwa akiamini kuwa huenda nikawa mimi, japokuwa aliombea
iwe hivyo, kwani alishaniona kuwa nina sifa zote za huyo mfalme mtarajiwa,
lakini hata wenzetu, babu mhasimu anadai kuwa kijana wake ana sifa hizo
hizo…’aliposema hivyo watu wakacheka kwa dhihaka.
‘Siri za mfalme mtarajiwa na dalili zake za mwisho
zilitakiwa zitokee siku hiyo iliyotabiriwa, sio lazima niwe mimi hata kama
ninazo hizo sifa, na hata nilipojitokeza siku ile sikuwa najua kuwa ilitakiwa
iwe hivyo….hayo babu hakuwahi kuniambia….na kama mnavyoona ilivyokuwa kwangu mimi
nilishapakwa matope, na hakuna aliyeniwekea akilini tena kuwa nitakuwa ndiye mimi
mfalme mtarajiwa, ila wenzetu walijua sifa za huyo mtarajiwa na alitakiwa
atokee vipi, ndio maana wakamuandaa kijana wao….’akatulia kidogo.
‘Lakini kila lililopangwa kuwa litatokea ….litatokea tu, na
huyo mtabiri aliposema hivyo, hakutaja ukoo gani, hakugusia hali ya huyo
mtarajiwa, alitoa dalili tu….sasa kwanini wao washinikize kuwa kijana wao ndiye
mtarajiwa. Hilo linajionyesha jinsi wenzetu walivyo, na kwa mtaji huo, kama
watashika madaraka, ubinafsi utawekwa mbele,
‘Kama wao wataendelea kutawaa nina imani kuwa jamii yetu
itaendelea kudumaa, na ubaguzi utaendelea kuwepo, hilo hatutaki liendelee
kuwepo. Lakini sio hadi tufikie kwenye vita na kama tatizo ni mimi , basi
kwanini ning’ang’anie hayo madakaraka….’akasema huku akiangalia mbele ya
wananchi ambao walizidi kumiminika kwa wingi.
‘Baada ya mimi kujitokeza wenzangu wakakimbia na kujificha,
na huko wakakusanya kikosi chao ,wakidai kuwa mimi sio mtarajiwa, mimi na ukoo
wetu tumelazimisha iwe hivyo kwa vile eti kwanza nimetumia mbinu za kumuoa
malikia, …
‘Sasa ukiangalia madai yao yanafanana na jinsi walivyokuwa
wakimtengeneza kijana wao, ili aonekane ndiye mtarajiwa, kama ilivyo kwa mwizi
mara nyingi humshuku mwenzake kwa jinsi anavyofanya yeye, na huhisi kuwa
mwenzake ndivyo anavyofanya…’akageuka kuangalia kushoto halafu kulia,, halafua
akaendelea kusema.
‘Hawa wenzetu hawakuishia hapo, wamepeleka malalamiko huko
makaoni kutushitakia, wamesahahu kuwa walipokuwa madarakani walikuwa wakipinga kabisa
makaoni kuingilia mambo yetu, na kila mara walikuwa wakisisitiza kuwa sisi
tunahitajika kuwa huru na hatuhitajiki kuwategemea watu wa makaoni,-walitaka
kila jambo tuliendeshe wenyewe, sasa imegeuka
wanataka makaoniI watusimamie mambo yetu, hata makaoni walipopata hiyo
taarifa walishangaa…
‘Katika m oja ya amdai yao ni kuwa, kwa vile wanaamini kuwa
mimi sio mtarajiwa wanataka niondolewe, na kuwe na uchaguzi wa huru na haki,
…tusimamishwe kwenye kampeni mimi na kijana wao, ili aangaliwe ni nani anayefaa
kuwa kiongozi…wakidai kuwa wana ushahidi na tumua nyingi dhidi yangu kuwa mimi
sio msafi na nilistahili kuliwa na mamba’ akasema na watu wakaguna.
‘Wao wakatoa na angalizo kuwa kama tukikataa, inabidi
niondolewe kwa nguvu, na kwa hivyo ndio
maana wameliweka jeshi lao kwa tahadhari kuwa kama sitakubalina na matakwa yao
basi hawana budi, ya kuitisha vita,…ili awekwe mfalme anayestahili…je wao pekee
yao ndio wanaomjua zaidi huyo mfalme mtarajiwe awe vipi, sasa wao wamgeuka kuwa
ndio wenye mamlaka na uamuzi kuwa ni nani awe kiongozi.
‘Kwa hivi sasa wana kikosi kikubwa, …hatukutarajia hilo,
kumbe waikuwa na mamluki waliotarajiwa kuwa ikitokea hivyo waitwe, ….na
ukichanganya na propaganda zao, wameweza hata kuwaita askari wao wa zamani,
wakiahidiwa kupata nafasi kwenye utawala na mali na kutokana na propaganda zao
potofu ….
‘Kama mnavyojua wenzetu hawa walikuwa wakimiliki njia njia
za kushawishi wananchi, na kidogo kidogo walishaanza kuwahadaa baadhii ya raia,
ndio maana wameweza kukusanya askari kidogo kidogo, na sasa wamekuwa na kikosi
kikubwa,japo kuwa kuna wenzao waliamua kujiunga na sisi, na tumewakaribisha, na
kutokana na wao ndio tukagundua wapi walipojificha…’akasema mfalme.
‘Hatukuamini sana maelezo ya hao askari waliojiunga na
vikosi vyetu, kiusalama na kiuataribu , ikiabidi tufanye uchunguzi, uchunguzi
wa kina,…tukagundua kuwa ni kweli, kuwa wao wameshaliandaa jesho lao na wanachosubiri
kwao ni kutafuta chanzo cha kuanza vita, na habari zilizopatikana huenda
wakatuma wajumbe kuleta madai yao, na kama tusipoyatekeleza basi wao huenda
wakatumia hilo kama sababu ya kuanza vita.
‘Wenzetu hawa wameweka maslahi mbele, hawajali ni nini athari
za vita hivyo kwa sasa…sisi kama rulivyowaambia hatutaki vita, na tutajitahidi
kutafuta kila njia kuepusha hivyo vita, …na kama tatizo ni mimi ,basi nitaachia
haya madaraka ambayo hayajaidhinishwa na uamuzi uwe mikononi mwa raia wenyewe,
….ila hatutaki wananchi walazimishwe, hatutaki kuje kutokea utawala wa
kibaguzi, hilo ndilo tunalochelea.
‘Nilipolipeleka hili swala kwa wazee, kuwa ili tuepushe
vita, mimi nipo tayari kujiuzulu, ili raia wamchague yule wanayemuona anawafaa,
wazee wamepinga hilo kwa nguvu zote, kwani wao walikuwepo kipindi hicho alikuja
huyo mtabiri, na wanasema kama atatokea kiongozi mwingine badala, ya huyo
aliyetabiriwa, lhakutakuwa na amani tena….kwasababu wenzetu wameshajipanga
kumuweka mtu wao…’akatulia.
‘Wazee wemesema uamuzi wangu huo haukubaliki, ni kama na
wasaliti wananchi, wanachi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakimsubiri mtawala
wao, sasa amepatikana, na kwa tamaa ya wachache anapingwa, je sisi
tuliokabidhiwa dhamana ya usalama tuna maamuzi gani?’ akatulia na kuangalia huku
na kule.
‘Nimefikiria sana, na kutokana na mawazo ya wazee, nikaona
ni vyema tukutane, pamoja na kujiandaa kwa vita kwani yote yanawezekana,
….nijuavyo wenzetu hawatatosheka na uamuzi wowote ambao utakuwa kwa maslahi ya
wananchi, …..kwa mfano tukiamua upitishwe uchaguzi wa wananchi wote, na kama
watashindwa, unafikiri nini kitafuta baada ya hapo…lazima watapinga, sasa
tufanyeje?’ akawaangalia wanachi.
‘Ili muwe na maamuzi ya hekima kwanza angalieni familia
zenu, angalieni uchumi wetu, angalieni hali zetu, kuwa tukiingia vitani, athari
kubwa itakuwa kwa familia zetu, uchumi utaharibika, …halizetu zitazidi kuwa
duni…hayo ni baadhi tu ya athari za kivita. Hatuhitaji kuingia vitani, sio
kwamba mimi naogopa, hapana, ila naogopa athari zake, …ndio maana naona nijiwekewe
pembeni niwe kama raia wa kawaida,…’akatulia.
Hapo wajumbe waliokuwepo, wakaanza kunong’ona, ilianza
kidogokidogo, na baadaye ikawa kama vurugu, kila mmoja akitaka kuongea na kutoa
lile lililopo moyoni, na mmojawapo akasema;
‘Hilo hatukubali kamwe….ina maana gani ya kusubiria miaka
hiyo yote, kusubiria mfalme mtarajiwa, na sasa amepatikana, leo hii tukuachie
eti kwa vile wanataka kijana wao awe ndiye mfalme kwa sifa zipi ambazo anazo ….,
hapana, hilo hatukubali, kama ni vitani tutaingia vitani’akasema mmojawapo na
wengi wakashangilia.
‘Hayo ni maamuzi yenu, hamjaangalia maamuzi ya raia wote,….ambao
ndio watateseka, ambao ndio waathirika wa pale wanapa-pambana mafahali wawili…tuwaonee
huruma hawa raia, wametetseka vya kutosha, na kuwahurumia huko ndiko kunakonifanya
mimi niondoke kwenye haya madaraka, ili kusiwepo na vita…’akasema.
‘Ni heri ya kuteseka, baada ya vita kuliko kuwa na utawala
uliopia, kwasababu tulikuwa kama watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe…..ubaguzi,
unyanyasaji na hali duni, zilituandama, tumevumilia hadi msimu uliotabiriwa,
…tunakuomba usituache, kwa kufanya hivyo utakuwa umetusaliti’akasema mama mmoja
ambaye alionekana kuchoka sana na hapo watu wakasimama na kushnagilia kwa wingi
sana na hali hiyo iliendelea kwa muda mrefu.
Baadaye walipotulia mzee mwanasheria akasimama na kuelezea
sheria zilivyo inapotokea hali kama hiyo, na akasema kama mfalme ataamua
kutafuta rizaa ya wanachi, inabidi wajumbe wapige kura kwanza, ili ionekane
kuwa kweli wanamuhitaji au la…lakini kabla ya hapo kunahitajika maoni ya
wajumbe, kuwa kwanini bado wanamuhitaji huyo kiongozi.
Basi yalifuata maoni na mawazo mbali mbali, na hatima ya
yoye ilikubalika kuwa kama ikibidi ni heri waingie vitani ili kuinusuru hiyo
hali, ili kuwalinda raia na mategemeo yao, ..na wajumbe wote waliamua kupitia
raia mmoja mmoja, ili kupata rai zao, …..japokuwa kulikuwa hakuna muda wa hilo
lakini walisema watajitahidi hilo lifanyike ili kuzima propaganda potofu.
‘Basi kama mumeamau hilo, mimi siwezi kuwasaliti, nipo
pamoja na nyie, lakini msimamo wangu wa kuepusha vita upo pale, pale,
nitajitahidi kuzungumza na wao, na kama kuna uwezekano huo, wa kukwepesha vita,
nitaupa kipaumbele,…hata kama kuna njia nyingine inayofaa kukwepa vita, itabidi
tuifuate…. lakini sio kwa kuwaachia wao madaraka,
Hapo watu wakashangilia kwa muda mrefu, wakisema yeye ndiye
mfalme mtarajiwa, hawahitaji mfalme mwingine zaidi yake.
‘Cha muhimu ni wao wakubali kushirikiana kwenye madaraka,…nafasi
hiyo tutawapa, kuna nafasi zo zipo wazi kwa ajili yao, ili tuwe pamoja, hilo naona ndilo la muhimu,
….’akasema mfalme mtarajiwa.
‘Kwahiyo basi, japokuwa tulishajindaa kwa hilo, lakini ni
vyema kuanzia leo tukawa tayari kwa lolote lile, na imebidi tuweke vikosi vyetu
kwenye mipaka, na kuzunguka eneo ambalo ndipo ngome yao ilipo, ili wasiweze
kutoka na kuvamia kwa haraka….
‘Hasa wakiona kuwa propaganda zo hazikufua dafu, basi
wanaweza kuanza kutumia nguvu, ili kupaka matope, kuwa usalama hauwezi kulinda
raia zake’akasema mfamle mtarajiwa
‘Kama mnavyojua ngome yao, hata kama tutawazunguka. Bado
wana sehemu nyingi za kupenya na kuingia huko uraiani ndio maana kwanza
niliwaita wakuu wa ulinzi wa raia …..ili
kuhakikisha kuwa raia hawazuriki kwa lolote lile au vikosi vyao kuingia uraiani
na kujificha…hilo najua tulishaliweka tayari, hapa ninakumbushia tu’akasema
mfalme.
Baada ya kikao hicho,
wataalamu mbali mbali wa kivita wakakutana, na wataalamu wa usalama wa raia
wakajadiliana jinsi gani ya kuwalinda raia na mali yao, wakati mipango ya
kujadiliana ikiendelea na wajumbe kusambaa sehemu mbali mbali kuelimisha
wananchi.
Hayo yakiendelea kumbe mdudu mtu alishapenya na sumu kali,
sumu yenye nia ya kuwaondoa wale wote watakaopinga maamuzi yao, ….kila kona na
kila ukoo kukawekwa ndumilakuwili, …
Je hayo yaliwezekana, je nguvu ya uma na propaganda potofu
ni nani zaidi..
WAZO LA LEO:Kiongozi bora ni yule anayejali maslahi ya wananchi wake kwanza kabla ya kujali maslahi yake binafsi
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Pretty section of content. I just stumbled upon your web site and in accession capital to assert that I acquire
in fact enjoyed account your blog posts. Any way I will be subscribing to your augment
and even I achievement you access consistently quickly.
Look at my blog harga emas perhiasan
I know this site offers quality based content and extra information, is there any other website which presents such
stuff in quality?
Also visit my homepage : harga emas dunia
Wow that was unusual. I just wrote an incredibly long comment but after
I clicked submit my comment didn't appear. Grrrr... well I'm not writing all that over again.
Anyhow, just wanted to say wonderful blog!
My website > harga emas batangan
Asking questions are truly good thing if you are not understanding anything totally, except this
post provides fastidious understanding yet.
Feel free to visit my web site :: harga emas dunia
Post a Comment