Tukumbuke kuwa malikia
mtarajiwa kaamua kwenda kumtembelea Maua ili kumfahamisha nini kinachoendelea
kuhusiana na mtoto wao. Ili kufika huko inabidi kukatisha msitu ambao una kila
aina ya hatari kuanzia ya wanyama na sasa kuna hatari ya adui wa kivita,..Mzee
Hasimu na kundi laki.
Tukumbuke pia kuwa
kipindi hicho ilifahamika kuwa mtoto huyo bado yupo na kundi la mzee Hasimu,
wakimshikilia kama chambo ili kuwezesha madai yao. Na pamoja na kumtumia huyo
mtoto kama chambo, lakini pia walishapeleka malalamiko yao huko wanakokuita
makaoni.
Pamoja na hayo, kundi
hilo lilishajiweka kwenye hali ya kivita, wakitafuta sababu yoyote, …na hata
kama kuua kwa kusingizia ….propoganda potofu, za kuwadanganay raia, na kila
mbinu za kisiasa. Na kulionyesha kuwa wao ni zaidi, kundi hilo liliwasili sehemu
hiyo yenye ulinzi mkali inayojulikana kama sehemu takatifu bila kutegemewa,
japokuwa kulikuwa na ulinzi mkali, lakini kundi hilo kwa utalaamu wao liliweza
kupenya na kufika hapo ofisi kuu, kitu kilichomshitua sana mfalme,
Je ni nini kitaendelea
baada ya hapo, je malikia atafika safari yake salama, ?hebu tuione sehemu
kidogo, kabla hatujaendelea na mchakato wa mgangano wa kisiasa katika kugombea
madaraka, tuwe pamoja …..
******
Malikia mtarajiwa alisonga mbele akiongozwa na kikosi
maalumu, wakikatisha msitu, na kujaribu kukwepa kabisa sehemu ambazo zinakisiwa
kuwa ndio ngome ya mzee hasimu, na kila hatua waliyopita ilimfanya malikia aanze
kuingiwa na wasiwasi na hata kujijutuia kwa mauamuzi hayo ya kwenda kumuona
Maua, aliona ni heri kumbe angekubaliana na mume wake kuwa wasubiri kwanza hadi
kutulie, lakini yeye alishinikiza kuwa lazima akaonane na Maua ili kumwelezea
hali halisi.
Alijipa moyo kuwa raia wote wa jamii hiyo ya msituni wana
imani ya kumuheshimu malkia na hata kuamini kuwa hata wanyama hawawezi kumdhuru
malikia, kwani kabarikiwa, na analindwa kimiujiza, na hilo lilipma moyo kuwa hakuna
anayeweza kumfanyia lolote baya, kwani kwa imani yao kumdhuru malikia ni sawa
na kumdhuru mama yako mzazi, ….
Imani za hawa watu, zinamtukuza sana Malikia kama na
wanafikia kusema kuwa mkono wa malikia una baraka, ndio maana kila mmoja anahijika
kushikwa kichwani na malikia huyo, na huweze kukutana nay eye ukuiachia hiyo
bahati, ni lazima ujitahidi akushike kichwa na kukubariki ….
Kwa imani zao hizo, kama ingeliwezekana kila siku
walihitajika kupata baraka hizo kwa kushikwa kichwani na mkono wa malikia,
lakini kwa ajili ya majukumu na wingi wa watu isingeliwezekani kufanyika hivyo
kwa kila siku. Na wengi hujitahidi angalau wafike kwa malikia mara moja kwa
wiki, hapo utaona jinsi gani malikia alivyokuwa na kazi kubwa.
Wao wanaamini kuwa mtu akiumwa, akiwa na shida yoyote, wa
kumlilia ni mama wa wanafamilia, yaani malikia nay a kuwa yeye ndiye mwenye
baraka za kuondoa ugonjwa, au matatizi yoyote yale ambayo yameshindikana ndani
ya familia husika, kwahiyo malikia anakuwa kama dakitari mkuu wa magonjwa yote…
Malikia mkuu ndiye mtendaji wa mambo ya kijamii, kwa mfano
raia akijifungua yeye anahitajika kumbariki mtoto, na kumpa jina linalomfaa,
yeye anaheshima kuwa ndiye mkuu wa wakunga wote , malikia anatakiwa kubariki
ndoa za watu zikifungwa, hata kama ni kwa mbali, lazima apewe taarifa na yeye
hubariki hapo hapo alipo, na akitoa idhini ndoa zinafungwa.
Licha ya kuwa safari hiyo ilikuwa ni kificho, lakini wakuu
wa ulinzi wa sehemu ambazo alitakiwa kupita walishapewa taarifa, kwahiyo kila
alipokatisha vikosi vya ulinzi, alisimama kidogo na kutoa mkono wa baraka kwa
wawakilishi hawo ambao walikuwa ni wakuu wa vikosi ambao waliaminika sana. Na,
askari wengine walikuwa hawajui ujio wa malikia, lakini kama kuna waliokuwepo
hapo karibu, ilibidi wajitahidi angalau na wao washikwe kichwa kupata baraka.
Msafara huo ulitakiwa uonekane kama vile malikia alikuwa na
ziara za kubariki vikosi vya ulinzi,haikutakiwa kabisa ijulikane kuwa malikia
alikuwa na safari ya kwenda kumuona Maua, kwani Maua anajulikana kama mtu
asiyehitajika katika jamii, na alishahukumiwa kuliwa na mamba, japokuwa hukumu
hiyo ilitiliwa mashaka na wengi, lakini ilikuwa haijabatilishwa.
Kwa ajili ya ujio wa malikia kwenye vikosi vya ulinzi, ulinzi uliongezwa, na kwa askari wa kawaida
waliambiwa kuwa ulinzi huo unaimarishwa kama moja ya juhudi za kuhakikisha kuwa
wahasimu hawapati mwanya wa kuingia uraiani na kuleta fujo, hawakuambiwa kuwa
kuna msafara wa malikia.
Msafara huo wa malikia uliongozwa na watu wanaojua siri za
huo msitu na njia zote salama, …..lakini hata hivyo, shaka haikuwatoka, kwani
wenzao na wao walikuwa wakijua mengi ya njia za siri, na kwa asilimia kubwa
waliokuwa wakijua siri za njia za msituni, walikuwa watu wa mzee hasimu kwa
vile wao ndio waliokuwa na jeshi kubwa lililokuwa likilinda huo msitu….
Pamoja na kuwepo na ulinzi mkali, vikosi hivi vitiifu vya
serikali iliyopo madarakani, hawakujua kuwa hasimu na kikosi chake maalumu
walishapita kwenye njia za siri na huenda kwa muda huo vikosi hivyo walishafika
kwenye makao, au sehemu inayotambulikana kama sehemu takatifu.
Malikia na watu wake wakaendelea na safari yao huku malikia
akimkumbuka mumewe ambaye alijitahidi sana kumzuia asiondoke, ….lakini
haikiwezekana, kwani alishazamiria safari hiyo iwepo;
‘Mke wangu, naona safari hii tuiharishe, maana kama
unavyoona tupo vitani, na haitawezekana mimi kama mkuu na jemedari wa nchi
niondoke, …’akasema mfalme.
‘Hiyo safari ni muhimu, hiyo ni moja ya sehemu ya
vita,…tusipofanikiwa kwa sasa, tunaweza tukaeleweka vibaya, hatujui mpaka sasa
mtoto yupo wapi, mimi kama mwanamke najaribu kujiweka kwenye nafasi ya Maua, na
kuhisi jinsi gani ningelijisikia kama ningelikuwa mimi ni Maua,…ni muhimu
nifike nionane nay eye ‘akasema malikia.
Mfalme mtarajiwa akatulia
akiwaza, akijua kuwa hili la safari kwa sasa haiwezekani kwake yeye kutokana na
majukumu ya kijamii, yeye anatakiwa awepo hapo wakato wote, na zaidi ya hayo
kesho yake anatakiwa kukutana na ujumbe uliotumwa kutoka makaoni, na hajui
hatarai ya hiyo safari, hata kama ni kuondoka na kurudi siku hiyo hiyo.
Kiutawala angeliweza akatoa amri, akaenda na kufika huko,
lakini sio hekima, na hataeleweka vyema, akageuka na kumwangalia mkewe, mkewe
akamuelewa na kusema;
‘Mke wangu tuna majukumu mengi na hasa wewe ambaye kwa hivi
sasa jicho la wengi linakutegemea wewe, hutakiwi kuondoka hapa hata kwa saa
moja, je huoni kama ukiondoka na akaletwa raia anahitaji huduma yako, utakuja
kusema nini…?’ akauliza mfalme.
‘Moja ya huduma yangu ni kusaidia raia wote, na mmoja wa
raia hao ni huyo mtoto aliyepotea, na kwa vile ninatakiwa kufutilia taarifa
zake, inabidi nionane na mama yake, ili na yeye asisononeke, ajue kuwa mtoto
wake yupo kwenye mikono yetu, japokuwa tunajau yupo kwa wahasimu’akasema
malikia.
Walitulia kwa muda kila mmoja akiwaza lake, na ndipo malikia
akaireejsha ile hoja ya mtoto akasema;
‘Nimekuulizia kuhusu huyo mtoto aliyepotea, inaonekana kama
huna wasiwasi sana kuhusu huyo mtoto, kwa mawazo yangu, mimi nitaenda ….wewe kwa
vile kwa hali ilivyo huwezi kuondoka hapa, mimi acha niende, najua raia wote
hapa wananiheshimu, hata hao wahasimu, hawataweza kunifanya lolote?’ akasema
malikia
‘Hilo kwasasa halitawezekana mke wangu, hakuna ambaye
atakuewa, kutoka kuondoka katika hali kama hii, usalama ni mdogo, na wenzetu
kama wataona hiyo ndio nafasi ya kufanikiwa mambo yao hawatasita kukufanya
lolote,….’akasema mfalme
‘Hilo niachie mimi…hakuna atakayeweza kunudhuru mimi….na nikifika
huko nitajua jinsi gani ya kuongea na huyo mama wa mtoto, ….mimi nawafahamu
sana wanawake wenzangu, na sisi wanawake tunajuana,…hilo niachie mimi, wewe
kubali kuwa twende tukamuona, ili ajue kuwa bado tunamjali’akasema malikia.
‘Sawa kama una uhakika na hilo, ….lakini…nachelea sana
kufanya lolote kabla sijaonana na hawa wahasimu, najua watakuwa wamemshikilia
huyo mtoto, na huenda wana matakwa yao kuhusu huyo mtoto, wanaweza kumtumia
kama chambo….’akatulia akiwaza.
‘Vyovyote iwavyo,..ngoja mimi niende nikamuona huyo mama wa
huyo mtoto, na ningelipendelea safari hiyo iwe ni ya siri, mimi nitaondoka na
wasaidizi wangu wawili na walinzi wawili waaminifu,…unasemaje kwa hilo?’
akasema malikia na kuuliza.
Mfalme alitulia akiwaza usalama wa mkewe, kweli alijua kuwa
kwa imani zao malikia sio rahisi kudhuriwa, lakini wahasimu wanapoona ndio njia
pekee ya kutimiza malengo yao, hawatasita kufanya lolote, na hata kama ni
kumuua wanaweza kufanya hivyo, wakitumia maaskari mamluki ambao hawajui imani
hizo.
Mzee hasimu alipoona kapungukiwa na askari, alituma ujumbe
kutafuta maaskari mamluki ambao wengi wanaishi kwa njia hizo, wanaajiriwa
katika mapigano, baadaye wanalipwa mali nyingi walizokubalina nazo na kurejea
huko walipotoka. Na hili ndilo waliloliogopa sana mfalme mtarajiwa, kwani
askari mamluki haangali ni nani wa kumua, anaua hata watoto, akina mama na hata
wazee, kitu ambacho katika imani zao, hakikubaliki.
Na pia mfalme alikuwa na wasiwasi, kuwa huenda mkewe
akatekwa kama alivyotekwa mtoto, ili kuweza kushinikiza matakwa yao. Hata hivyo
aliona kuwa kweli kuna umuhimu wa mtu kufika huko kwa huyo mama kumuonyesha
kuwa wapo pamoja na yeye, na kwa vile yeye ni mtawala, hatakuwa na ugumu wa
kufika yeye, au kutuma ukumbe,….hapo akayasifu mawazo ya mkewe, japokuwa ni
hatari tupu.
Na ndio maana safari hiyo ya kisiri iliandaliwa, na malikia
akaondoka na watu wake, wakikatisha msitu wenye hatari za kila aina,na wakati
wanakatisha huo msitu, na vikosi vikiwa vimewekwa kwenye tahadhari, kikosi
maalumu cha hasimu kikapenya, na waliweza kupenya, bila hata kugundulika, na
kufika huko ofisi kuu
Taarifa za ugeni huo zilipofika kwa mfalme, ikabidi amuite mkuu
wa ulinzi kumuuliza imewezekanaje hawo watu kupenya hadi kuingia hapo bila
kujulikana, na mkuu wa ulinzi hakuweza kutoa majibu, ikabidi uchunguzi mkali
ufanyike, kwani ilionekana huenda kuna askari walioshiriki kwenye kufanikisha
hilo, hasa askari waliojiunga kutoka kwa hasimu.
‘Hawa wenzetu wanaujua huo msitu kuliko hata sisi, kwahiyo
uweze wao wa kupenya hadi kufika huku ni mkubwa sana, cha muhimu ni kuwa
tumeliona hili, kwahiyo tunahitajika kuongeza nguvu zaidi, na hata ikibidi
tunahitajika kuchukua askari wa akiba’akasema mshauri wa mfalme.
Mfalme aliinama na mawazo yalikuwa mengi,akimuwaza mkewe
ambaye alikuwa ndani ya huo msitu kwa sasa, na pale aliona ni vyema atume watu
wafuatilie usalama wa mkewe, lakini hilo akaliona halitafaa, na akaona kama
atahidi hatari yoyote, kwa vile yupo na wahasimu wake, atahakikisha sheria
zilizokuwepo zinatumika.
‘Mjukuu wangu, utawala wako unahitajika kutumia akili,
unahitajika kutumia hekima, lakini pia kuna wakati
unahitajika kutumia nguvu, ….na
sio nguvu tu, wakati mwingine utahitajika kufanya yale ambayo katika hali ya
kawaida usingelifikiria kufanya hivyo, kwa ajili ya raia wako…’akakumbuka
maneno ya babu yake.
‘Kweli …kama kuna lolote litamsibu mke wangu, hawa watu
sitawasamehe,…’akasema.
********
Mfamle mtarajiwa alibakia akimuwaza mkewe wake, na hapo
akagundua kuwa mke kweli ni sehemu ya mwili wake, masaa machache baada ya
kuondoka mkewe, alihisi mapungufu kwenye mwili wake, akili ikiwa inamuwaza
mkewe….alijitahidi kiume, lakini bado moyo wa wasiwasi ulimuandama, hasa katika
swala zima la usalama wa mkewe.
Japokuwa baada ya
kukubali kuwa mkewe aondoke kwenda kuonana na Maua alihakikisha kuwa njia
atakayopitia kuna watu muhimu wa kikosi chao cha wanajeshi wanainda, lakini kwa
maadui, kama watajua kuna msafara kama huo, wanaweza kutumia mbinu nyingine
yoyote ili wamteke na kufanya lolote wanalotaka,
‘Hilo naomba limuepuke mke wangu….sitasamehe kama lolote
litatokea kwa mke wangu…’akasema kimoyo moyo.
Katika mawazo yake kuna muda alijijutia kwanini kakubali
mkewe aondoke peke yake, aliona ingelifa waongozane kila mara, lakini pamoja na hayo, alijua kuwa wakati
mwingine inabidi iwe hivyo, hawawezi wakaongozana kila safari, hata kama ni ya
hatari, inabidi wajitolee kwa maslahi ya
wananchi wao. Akakumbuka jinsi alivyomwambia mkewe pale alipokuwa akimuga;
‘Mke wangu nakubali kwa shingo upande kuwa uondoke ukamuona
Maua, lakini nafahamu fika, kuwa huu msitu, una hatari nyingi, za kila aina na
ukumbuke wenzetu wameshatega mitego yao kila kona…ukikosea tu ukaingia kwenye
anga zao, hawatakusamehe’akasema mfalme mtarajiwa.
‘Usiwe na wasiwasi mume wangu, umesahau kuwa mimi ni malikia
mama wa wananchi wote ikiwemo wao wenyewe, kama kweli wana imani na imani zenu,
hakuna lolote linaweza kutokea juu yangu…usiwe na wasiwasi mume wangu, mimi
maisha yangu nimeshayakabidhi kwa ajili ya kuwatumikia raia wetu, ikiwemo wao
wenyewe…’akasema malikia.
‘Nashukuru sana mke wangu, kwani kweli wewe ni malikia
alyetabiriwa ambaye haogopi lolote kwa ajili ya raia zake, nakutakia safari
njema, na ukimuoa Maua mwambie tupo pamoja na yeye, na tutafanya kila
iwezekanavyo kuhakikisha kuwa anampata mtoto wake na tutamfikisha mikononi
mwake salama usalamini’. Akasema mfamle mtarajiwa na akambusu mkewe kwenye paji
la uso, na baadaye mkewe akaweka mkono wake juu ya kichwa cha mumewe kama ada
yao.
Mfamle mtarajiwa akajaribu kuyafuta hayo mawazo na kutoka nje
kuelekea kwenye ofisi yake, na kabla hajaingia kwenye hiyo ofisi , mara akamjia
mlinzi wake wa karibu, alipofika alitoa ishara ya salamu, akainama na kusubiri
kupewa kibali cha kuongea, na alipopewa akasema kuwa kuna ugeni umefika.
‘Ugeni kutoka makaoni….mbona wamewahi hivi…,?’ akauliza
mfalme mtarajiwa, kwani ndio ugeni aliokuwa akiutarajia, ugeni huo ulitakiwa
uje kwa ajili ya kusimikwa mfalme huyo, lakini shughuli hiyo ilibidi iahirishwe
kwanza, baada ya wahasimu kupeleka pingamizi makaoni. Lakini wakaahidi kutuma
ujumbe kwa ajili ya kuliangalia hilo tatizo lililofikia hadi kuwekewa pingamizi.
‘Hapana huo ni ugeni wa mzee hasimu na kijana wake na wazee
wenzake’ akasema huyo mlinzi.
‘Ugeni wa Mzee hasimu….ooh, wamejileta wenyewe, safi kabisa…lakini
wamefikaje hapa , bia kuonekana na askari wetu? ’ akasema mfalme mtarajiwa alijaribu
kukificha mshituko alioupata moyoni . Aliwaza kama wao wameweza kufika hadi
hapo bila kuonekana, je askari wao watashindwaje kuingia uraiani na kuanzisha
vita.
Hapo akageuka kushoto kwake , ambapo ndipo wageni wanaposubiria
na kule aliona kundi la watu, na miongoni
mwake akiwemo Mzee hasimu na kijana wake, walikuwa wote wamekunja uso kwa
hasira.
Kundi lile lilikuwa limezingirwa na askari wa usalama, na
walinyang’anywa silaha zao zote, na kuwekwa chini ya ulinzi, kitendo hiki
walikiona kama kuzalilishwa,….hawakuwahi kufanyiwa hivyo kabla kwa vile muda
mwingi wao walikuwa ndio watawala.
Mfalme mtarajiwa akamgeukia mlinzi wake wa karibu na
kumwambia;
‘Sawa hakikisha wanakirimiwa na mwambie mwenzako akawaite
wasaididizi wangu na mzee wangu na washauri wangu haraka iwezekanavyo’akasema na
kuingia ofisini kwake, akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani, je hawa watu
wamekuja kwa jambo gani. Je wamekuja kwa ajili ya huyo mtoto, na kama ni kuhusu
huyo mtoto watakuwa na masharti gani, na je wana ajenda gani ya siri na huyo
mtoto, je huo msafara hakuwahi kukutana na msafara wa mke wake….?
Wakati anawaza hilo akakumbuka ushauri wa wasaidizi wake,
kuwa kundi hilo hasimu, halitatulia kamwe kumletea chochoko , hata kama
watawapa kila kitu, lakini kama watawanyika madakara, haa amdaraka makubwa, ya
kuiongoza jamii yao, hawatatulia ….
‘Sasa dawa yao ni nini?’ akauliza
‘Dawa yao ni kutumia sheria hiyohiyo waliyoitumia kuwauniza
wenzao, ambayo japo kuwa ilikuwa na lengo jema, lakini wao waliitumie kwa
masilahi yao, hasa kwa ajili ya kuwazima wapinzani wao, bila kujua kuwa sheria
hiyo ipo siku itawabana wao wenyewe, kwani dawa ya moto ni moto…’akaambiwa,
hakupenda kabisa huo ushauri, lakini kila hatua anayopita, anajikuta
akilazimika kuitumia.
‘Labda, kuepuka haya kwa ajli ya wananchi…hawa watu inabidi na
wao waionje sheria yao, ili na wao wajue machungu yake….’akasema na kutulia. Na
mara wakaanza kuingia wasaidizie wake, na wazee mbali mbali, kila moja akiwa
akionyesha hasira zake kwa wahasimu ambao walionekana wakiwa wanasubiri nje,
kuleta hoja zao
WAZO LA LEO: Hekima kwa kiongozi ni jambo muhimu sana, pamoja na elimu uliyo nayo , pamoja na uwezo wa kuongea kama huna hekima hutaweza kuwawa na maamuzi sahihi ya kuwarizisha watu wako
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Wapendwa, leo nilijiandaa kuweka kitu kipya lkn kama walivyosema wahenga cha mtu ni nini....basi nikashindwa, tuombe mungu kesho, mweneyzi akijalia, tutaendelea na kisa chetu
Post a Comment