Malkia mtarajiwa alikwenda hadi sehemu yake maalumu ambapo
aliweka ua, ua ambalo alipewa na mume weka, ua hilo alikuwa kila siku
analipitia na kuweka maji kadri kama alivyoelekezwa na mume wake, na japo kuwa
hakuamini sana mambo hayo, lakini kwa ajili ya kumpenda mume wake, alikuwa
radhi kumtii kwa lolote lile.
Kila mara na kila dakika, alikuwa akimkumbuka mume wake, na
kumbukumbu hizo zikija kichwani, huwa anatulia na kumuombea mume wake huko
alipo awe na amani, na afanikiwe katika kila jambo jema analilofanya, na
ikifika jioni, kumbu kumbu za siku ile ya mwisho, aliyoagana na mume wake
humjia, na maongezi yao hutekwa kichwa chake:
‘Mke wangu nitaondoka kwa ajili ya kufanya mipango ya kumuokoa
huyu mgeni wetu, kama nilivyomuahidi, na sitaweza kuishi kwa amani kama satafanikiwa kumuokoa, tukikumbuka kuwa
huyu amekuja kwetu kama mgeni wetu. Mimi ndiye niliyemchukua huko, na kumleta
hapa, nikiwa na imani kuwa hapakwetu ataishi kwa amani.
‘Lakini kwa taratibu za hapa,na imani za hapa wao wamegundua
mengine, kuwa huyu mtu hatufai hapa, wao wanasema kwa mtizamo wao, kizazi kama
hiki kikikulia hapa, kitaharibu vizazi vya hapa, na ili hili lisiwepo hawana
budi kumuondoa muhusika na mtoto wake akizaliwa atakulia kwenye mikono ya watu
wa hapa na wataweza kukisafisha hicho kizazi.
‘Ama kwa mama mtu, wanasema haitawezekana maana keshakulia
huko alipotoka, hata kama atajifanya ni mwema kwa sasa, lakini utashi wake kwa
ndani hautaweza kubadilika, na kwa imanai za hapa mtu huyu ana hulka mbaya
inayoweza kuangamiza vizazi vyetu, ….hastaili kuishi hapa…
‘Wanasema wangelimfukuza, lakini kwa imani zao, kwa vile
keshakanyaga aridhi, hii nyayo zake zimeshaambukiza sehemu zote alizopita, na
hizo nyayo zinahitajika kufutwa, kwa kuziharibu, na njia mojawapo ya
kuziaharibu ni kumtupia mwili wake mamba ….’
‘Eti nini…..mbona nyie watu ni wauwaji….mnataka kumuua mtu
asiye na hatia…’akasemaamlikia.
‘Ndio maana nataka kufanya juhudi za kumuokoa, na ili nifanikiwe
hili natakiwa niwe nje kwa muda mrefu, na ikibidi huenda nikasafiri, kwani
nikashamuokoa huyu binti, itabidi nimsafirishe mbali na hapa..’akasema mume
wake.
‘Unafikiri unaweza kumokoa kwa jinsi hali ilivyo, na
ukiangalia huko nje wapo walinzi kila kona, utampitishia wapi, au utamtoaje
humu ndani, na kwa hali aliyo nayo….hawo walinzi na wakungwa wanamsubiri huku nje, muda ukitimia wataingia ,
sasa hebu niambia utawezaje kumuokoaj kwa hali hii?’akauliza malikia mtarajiwa.
‘Hilo lisikutie shaka, kwani kila dhamira njema, huwa ia
mafanikio,…sisi dhamira yetu ni njema kabisa, tupo mbali kabisa na imani
zao….’akasema mume wa malikia mtarajiwa.
‘Ina maana huamini imani zao hizo, mbona….?’ Akauliza kwa
kushangaa.
‘Zipo za kuamini, maana usipoamini hutakuwa pamoja na wao, lakini
zipo ambazo hazina mwisho mwema, zinaonekana wazi kabisa kuwa ni imani
zilizojengwa na watu kwa ajili ya maslahi yao. Na hizi kama tutafanikiwa
kuingia madarakani ni lazima tuzipige vita,…’akasema na kutilia.
‘Ni kweli mume wangu, kama tutaingia madarakani, mimi na
wewe tutashirikiana kuondoa hizo imani potofu,….hilo nakuahidi ,…sasa hili la
huyu mwenzetu, maana kama kweli sisi ni viongozi watarajiwa tunatakiwa
tuonyeshe mfano kwa kuanzaia hapa, …tutamuokoaje ?’ akauliza malikia mtarajiwa.
‘Wewe subiri naye hapa, kwani ukiwa naye karibu, hawataweza
kumchukua haraka, ili sisi tupate muda wa kufanya hay tuliyojiandaa nayo, huko
tumeshjipanga, cha muhimu ni kuhakikisha yupo salama, hadi hapo muda wake
utakapofika,….’akasema mume wake, na wakati anaongea hivyo, alikuwa kashika kimtungi
kidogo, kikiwa na ua lililopandwa ndani yake.
Mke wake alimfikia mume wake kumpokea kama kawaida yake,na
akachukua mshale na upinde na kuviweka mahali pake, lakini kile kimtungi
kidogo, kilibakia mikononi mwa mume wake, hakutaka kukambidhi,na yeye hakutaka
kulazimisha kwani alijua huenda mume waka ana maana yake nyingine na kwahiyo
mara kwa mara akawa anatupia macho hicho kibuyu na lile ua lililopo ndani yake
na kila akinyosha mikono kukichukau, mume wake alikuwa kama anasita kumpa,
ikabidi aulize;
‘Hilo ua zuri sana mume wangu, ni zawadi yangu, mbona hutaki
nikupokee au,kuna mwenzangu mwingine?’ akauliza malikia matarajiwa kwa utani.
‘Hakuna mwingine zaidi yako mpenzi wangu, wewe ndiye malikia
wangu, wewe ndiye ua langu la moyo wangu, ua ambalo nilikuwa nikilisubiri miaka
mingi nyuma, na siku nilipokupata kama mke wangu, niliingiwa na uhai wa
matumaini, uhaii wenye matarajio ya upendo na amani, kwani kutokana na wewe
familia na matunda ya familia zitajaa baraka. Wewe ni tumaini langu, wewe
ndiyeua langu, na mungu akitujalia tukaingia ikulu, basin chi yetu hii itajee
neema. Lakini kwa sasa inabidi univumilie, ili niwajibie, ili nitimize yale
yaliytabiriwa….’akasema mume wake.
‘Nimekuelewa mume wangu, najua upo kwa ajili yangu na kwa
ajili ya taifa hili, na mimi nitashirikiana na wewe hadi siku hiyo ikifika, na
kila unalolifanya ujue nipo nyuma yako, na popote utakapokwenda ujua nipo hapa
nakusubiri…na wewe ndiye faraja yangu, ua langu na mtungu wangu auliolibeba
hilo ua, wewe ndiye kila kitu kwangu….’akasema malkia mtarajiwa akiwa bado
analiangalai lile ua aliloshika mume wake.
Mume wake akamsogelea na kumbusu mkewe kwenye paji la uso,
halafu wakaangalia usoni kwa muda, hadi mke mtu akashikwa na aibu, na kuangalia
pembeni, lakini akagundua kuwa kufanya vile ni kosa, huyo ni mume wake hatakiwi
kumuonea aibu, akainua uso uliojaa tabasamu, na mahaba, akamwangalia tena na
mume wake usoni, na wote wakachekana, na mume akasema;
‘Nakupenda sana mke wangu,….ni kweli hili ua ni zwadi yako, na
ua hili utakuwa nalo, liweke sehemu nzuri, na uwe unalinyweshea kila siku, ili
kuonyesha mapenzi yako kwangu. Nikiwa hai, na hilo ua utaliona lipo hai,litakuwa
likinawiri, ….kama utalikuta limenyauka ujue na mimi ….’alipotaka kusema hilo
neno, mkewe akamziba mdomo kwa kiganja cha mkono.
‘Mume wangu achana na imani hizo, mbona unaniweka roho juu,
kwanini unaniambia hivyo,na kwanini ua hili liwe uhai wako, ua ni ua tu, ni
mapambo ya dunia, na uhai wako ni uahi
wako anayejua kuwepo kwake ni muumba peke yake. Mimi kamani kwa imani hiyo,…hapana,
sitaki ujilinganishe na ua hili….’akasema huku akiliangalia lile ua, ambalo
lilikuwa limechipua vyema.
‘Kama nilivyokuambia kuwa mimi hivi sasa ni kama naingia
vitani, na vitani lolote linaweza kutokea, …mimi nakuahidi kuwa nitajitahidi
kwa ajili ya taifa letu, na huu ni mmoja wa mitihani yangu ili kuwadhihirishia
wanajamii kuwa mimi ndiye yule mafalme wao mtarajiwa, nahitajiak kuyafanya haya
kwa ajili yao, na kwa ajili ya imani zao, ili kufanikisha taifa letu teule,taifa
lilitabiriwa, taifa la amani na upendo…’akasema.
‘Mimi najua kuwa moja ya mitihani hii ni kumuokoa huyu
mwanamke ambaye hana hatia, na huyu ni ishara ya wanawake wengi wanaotaabika
katika miliki yetu, nikimuokoa huyu mwanamke mmoja tu,nitakuwa nimewaokoa
wanawake wengi waliodhulumiwa kama huyu…kwangu mimi kila mmoja wa raia wetu ni
muhimu sana…sitakubali hata raia mmoja kudhulumiwa.’akasema huku akimkabidhi
mke kile kimtungi kidogo kikiwa na ua lilichipua ndani yake.
Mkewe akasita kuupokea ule mtungi,lakini kwasababu ni mume
wake kampa,na inabidi amtii, akaupokea ule mtungi, na kuliangalia lile ua,
….akaliangalia kwa muda mrefu, na jinsii alivyokuwa akiliangalia na akili yake
ikawa ianjenga sura ya mume wake kwenye lile ua, ….akashituka, na kuinua uso kumwangalia
mume wake…alikuwa keshaondoka.
‘Mume wangu,….’akaita na kutoka nje, hakumuona,
alishaondoka, na yeye akakichukia kile kimtungi, na kutafuta sehemu moja nzuri,
akakiweka na kuchukua maji akalinyweseha lile , na kila siku alikuwa
akilinyweshea na kuhakikisha kuwa linakuwa katika hali nzuri, yeye kwa
kukufanya hivyo, allijua kuwa anatimiza amri za mume wake, na alitaka mume wake
akirudi anamuonyesha hilo ua, kuwa amefanya kama alivyomuagiza….
********
Alipotoka kulinyweshea lile ua, akarudi ndani ya sehemu yao
wanapoishi, na kwanza akahisi michakato michakato , kama watu wanakimbia,
akageuka kule alipotoka hakuona mtu, akajua huenda ni miongoni mwa wasaidizi
wake wanafanya kazi zao, lakini alipoingia ndani ya sehemu anapokaa , akahisi
kuna mtu kaingia,…akataka kwenda kumuuliza mlinzi wao, ni nani kaingia ndani
bila taarifa yake, na kabla hajainua mguu, akasikia sauti pembeni yake ikisema;
‘Samahani malikia mtarajiwa, …mimi ni kijana wa milki
hii,ninayetoka kwa mzee mnayemuita hasimu, mimi ndiye niliyekuwa naimetabiriwa,
kuja kukuoa wewe, toka awali, nafahamu ulishawahi kuambiwa hilo, japo kwa
kulipotosha,…lakini kwabahati mbaya mwenzangu huyo akaniwahi, na kukuoa
wewe….leo nimekuja kukutembelea na kwa ajili ya kukupa pole..’ila sauti
ikasema.
Malikia akasafisha macho yake kwa kiganja cha mikono, ili
kuondoa ugiza machoni,na alifunua macho akamuona mwanaume, alimtambau hapo hapo
kuwa ni nani, akasema;
‘Sijakuelewa, na nashukuru,kwani wewe ni mgeni, mtu mkubwa
kaika jamii hii,na kuja kwako ni kwa utukufu katika familia zetu, na taratibu
za mgeni, ni kukirimiwa, karibu kwenye kiti, na ngoja nikuletee maji,upooze koo
lako’akasema malikia mtarajiwa na akaenda kuchukua maji na kumpa huyo mgeni. Na
yule mgeni akayapokea huku akimwangalia malikia usoni, na malikia akageuka na
kwenda kukaa pembeni, akasubiri mgeni wake amalize kunywa maji.
Yule mgeni alipomaliza kuyanywa yale maji, akainuka na
kwenda kusimama pale aliposimama malikia mtarajiwa na akamkabidhi malikia kile
chombo cha maji huku macho yake yakiwa hayabanduki kumwangalai yule malikia
usoni, alikuwa kama kashikwa na jambo la kushangaa, na kusema;
‘Mamammaa…kweli,sikujua…’akasema.
‘Hukujua nini muheshimiwa, kijana wa mzee hasimu, leo
umekuja na jamboo gani, ?’akasema malikia mtarajiwa.
‘Kwanza nashukuru sana malikia mtarajiwa kwa ukaribisho wako
huu, ama kweli nimeamini kuwa wewe ndiye malikia mtarajiwa, ua la nchi,
…tarajio jema la taifa letu, uliyestahili kuwa ua la moyo wangu…’akasema na
huku akiwa bado kamwangalia malikia, hadi malikia akawa hajisikii vyema, lakini
kwa ajili ya mgeni ilibidi atulie tu. Na yule mwanaume akaendelea kusemma;
‘Mlikia mtarajiwa moyo wangu utafurahi sana, ukiingia pale
ikulu, ukiwa na yule aliyetabiriwa na kukubalika kama mfalme, na kama
ulivyoona, hali imedhihiri kuwa mimi nilidhulumiwa , mimi ndiye niliyestahili
yako’akasema huyo kijana ambaye kwa muda huo alikuwa na tenga la zawadi nyingi
pembeni yake.
‘Mimi nashukuru kwa kunitembelea, kwani mgeni ni baraka,
lakini kauli yako hainipi wasaa wa kutulia, nashindwa hata kukukaribisha vyema
mpaka nielewe nini maana ya kauli yako hiyo, je kuna nini kimetoka, na kwanini
utamke maneno kama hayo?’ akauliza malikia mtarajiwa.
‘Hata mimi nimeshangaa,kwani nilitarajia kukukuta ukiwa na
majonzi, lakini nakuona ukiwa katika hali ya kawaida kabisa, hii inaonyesha
wazi kuwa kweli ulikuwa humpendi huyo aliyekulazimsiah kukuoa, …mimi ndiye
mpenzi wako wa kweli…nakuomba uzipokee zawadi hizi kama tunu ya upendo wangu
kwako..’akasema huku akimkabidhi hilo kapu lililosheheni zawadi mbali mbali.
Yule malikia akawa anashangaa, hakushangaa kwa ajili ya zile
zawadi, kwani hiyo sio mara ya kwanza kuletewa zawadi kama hizo, sio kutoka kwa
huyo kijana wa mzee hasimu peke yake, lakini kwa wanachi wengi,kila mmoja
alikuwa akifika kwake kumsalimia huja na zawadi, kwani wao wanaamini kuwa yeye
ni malikia mtarajiwa, na malikia mtarajiwa ana baraka, na ukimletea zawadi,
akifurahia mambo yako yataanyooka.
‘Kwanza naomba unifafanulie hiyo kauli yako vyema, ..ama kwa
pole yako naikubali,maana ni kweli mume wangu kasafiri, na kuondoka kwake ni
kwa ajili ya taifa lake, …najua muda wowote atarejea, …najua mengi yatasemwa,
lakini mimi nina imani kuwa atarejea muda sio mrefu’akasema na yule kijana
akaangua kicheko.
‘Hahahaaa…malikia mtarajiwa, na wewe una imani hiyo…toka
lini mamba akawa na urafiki na mwanadamu, ukishafika mdomoni mwake yeye
anakufahamu kama kitoweo chake…hili litambue kuwa huyo mume wako hatarejea
tena’akasema huyo kijana na kumfanya malikia amwangalie kwa mashaka, na
kukumbuka hali zilizokuwepo hapo eneo lao siku mbili sasa. Watu wamekuwa na
ukimiya, na wamekuwa kama wakimkwepa, na kila alipouliza , kila mmoja alitoa
kauli ya utata, kuwa hakuna tatizo.
‘Kuna nini kinaendelea humu, mbona watu hawapo sawa, kila
mmoja anatembea kichwa chini, na kila ninayemuuliza hataki kunipa jibu la
uhakika?’ akamuuliza mmoja wa wasaidizi wake.
‘Hakuna kitu malikia, ni hali ya kawaida maana waume zetu
wote bado hawajarejea, na kuchelewa kwo kunatupa mashaka, kuwa huenda kuna
lolote baya limetokea, na ndio maana kila mmoja anawasiwasi..’akasema huyo
msadizi wake na kuondoka haraka haraka kuonyesha kuwa alikuw akikwepa kuulizwa
swali jingine.
Huyu malikia alikuwa na tabia moja,kuwa alikuwa hapendi
kuchonoa chokonoa mambo, kama akiowa kwenye maongei, huwa unaongea lile alilokusudia
na likashamtoka kinywani,hapendi tena kudadisi, na kuleta maongezi mengi
ambayo,kwake yeye alijua ni kuukaribisha umbeya na utesi, hakunda kuwa na tabia
ya utesi na umbeya.
Kwahiyo yule msaidizi wake na wengineo, walishamjalia tabia
yake hiyo, kama kuna jambo la kuongea
naye, huwa wakishaongea yale muhimu huondoka kwa haraka,lakini kwa hali
iliyokuwepo hapo, malikia alihisi huyo msaidizi wake anajua mengine ambayo yeye
hayajui, akasema kimoyo moyo, atavuta subira hadi muda muafaka ukifika atayajua
hayo yaliyojificha, huenda haambiwi kwasababu maalumu.
****
Akainua uso na kumwangalia yule kijana, akakumbuka taarifa
zake, kuwa mkewe ambaye ndiye aliyejitolea kumuokoa siku ile, alishatupiwa
kwenye bonde la kifo,na huenda keshaliwa na mijoka, akamuonea huruma, kwani ni
kijana anayeonekana mpole, na asiye na hatia, nahapo akasema;
‘Najua upweke ulio nao, na naomba hilo lisikufanye ukakiuka
tabia yako njema,kama zawadi zako ulizokujanazo zina masharti ,nakuomba uondoke
nazo, …na kamauna jingine jipya naomba unifafanulie, lakini liwe la
heri,..’akasemamalikia.
‘Ina maana wewe hujui nini kilichotokea au mpaka leo
wamekuficha, hii inaonyesha jinsi gani wasivyo kuthamini, hivi sasa ulitakiwa
uvae nguo maalumu, zinazoonyesha kuwa kweli ulikuwa ukipenda mume wako,
nakuodoka kwake,ni huzuni kwako…sasa hivi ulitakiwa utolewe humu kwenye eneo
hili , maana halikustahili, wewe ni malikia,..malikia asiyestahili kukaa kwa
watu wabaya…’akasema yule mwanaume.
‘Sijakuelewa?’ akasema malikia.
‘Kama hawajakuambia ni kuwa mume wako, keshakuwa chakula cha
mamba, na mtu kama yeye kama kweli alikuwa mtu msafi, anayestahili kuwa mfalme,
hakustahili kuliwa na mamba, kama kweli alikuwa mfamle mtarajiwa. Kuliwa kwake
na mamba ina maanisha nini, ina maanisha kuwa alikuwa mtu mbaya, alitumia
ujanja wake kukupata kiujanja na sasa mizimu na mababu wamemuhukumu, mume wako
kauwawa na mamba, hilo amini….’akasema yule kijana.
‘Eti nini…wewe umechanganyikiwa nini…hebu niondokee
hapa…ondoka na zawadi zako sizitaki, naona unaniletea nuksi,….mume wangu
hajaliwa na mamba, mume wangu bado yupo hai…hayo yalikuwa maneno ya watu tu, nilishayasikia,lakini
nina uhakika hayana ukweli wowote….’akasema na kukimbilia pale alipoliweka ua
lake, na alipofika na kuchungulia, akajihisi kitu kama sindano kikichoma kwenye
moyo wake kifuani,akadondoka nakuzimia.
NB Tupo pamoja?
WAZO LA LEO: Pendaneni, wanandoa kwa kuiboresha ndoa yenu kwa upendo ulio wa dhati, ili kila siku iwe ni sawa na ile siku ya fungate yenu.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kisa kinasisimua kweli ama kweli mapenzi yana nguvu kuliko mauti..nasubiri kwa hamu kusoma muendelezo....pamoja daima
Post a Comment