‘Mzee mwenzangu, mimi nakupa siku tatu, kama huyo kijana
wako hajaonekana, sisi hatuhitaji zaidi, tunamuhitaji malikia mtarajiwa, kama
sheria zilivyo , kuwa mumewe akifariki, malikia anahitajika kutolewa ahpo
alipokuwa akiishi na kuwekwa wazi kwa ajili ya mume mwingine…’akasema mzee
hasimu.
‘Huyu malikia hastahili kukaa kwenye majozi kwa muda
mrefu,taiaf lake linamuhitaji, anahitajika kukabidhiwa majukumu, ..mimi nawajua
sana nyie, kwanza mumetumia mbinu za kumchukua, na sasa mnaanza kuumbuka, ….’akasema
huyo mzee akiwa anamwangalia mzee mwenzake ambaye alikuwa katulia, na kimiya,
akimsikiliza kwa makini.
‘Hebu jiulize mzee mwenzangu, toka lini, katika historia ya
taifa letu hili, na hata huko tulipotoka hadi tukafik hapa kuanzisha hili
taifa, lini, mfalme mtarajiwa, mtu ambaye tunamtegemea kuwa kiongozi wa taifa
hili, aliwe na mamba…hii ni ishara mbaya kwenu, manhitajika kuliwazia hilo kwa
makini, kuwa kuna kitu mumekosea…..’akasema mzee hasimu, na kutulia kwa muda,
na mzee mwenzake alipoona kuwa huyo mzee hasimu katulia, na hana jingine la
kuongea akasema.
‘Kwanza kabisa niwaambia kuwa mlilolifanya ni kosa kubwa,na
mnajua nini sheria inasema nini kama hilo mlilolisema sio kweli, niwaulize ni nani
kawaambia kijana wetu kaliwa na mamba,…hizo taarifa mumezipata wapi, na kama kungelikuwa
na tukio la msiba, mngelisikia baragumu, mungeliona taratibu za msiba…hamuoni
kuwa mnatuzulia msiba?’ akauliza Babu , huku akionyesha kushangaa, jinsi
taarifa hizo zilivyowafikia hawa watu, na ilikuwa ni siri yao.
‘Hakuna siri hapa duniani, hasa jambo hilo likiwa ni msiba, najua
mlifanya hivyo ili mpate muda wa kujipanga, ili muweze kuweka mambo yenu sawa,
na ikiwezekana mmpate mrithi wake, hilo hatuwalaumu sana, kwasababu kila mmoja
anajua uchungu wa kupoteza kijana muhimu katika familia…lakini sisi tunaomba
taratibu zifuatwe, ili kuliwezesha taifa letu hili lifike kule tunakotarajia’akasema
mzee wa sheria wa upande wa mzee hasimu.
‘Sisi sheria tunazijua sana, na taratibu za msiba zipo wazi,
haiwezekani kutokee msiba katika familia, watu watulie kimiya,…hilo mbona
hamlioni. Na wenzetu hili mlilolifanya linatuweka aktika mshaka na nyie,, kuwa
huenda mna lengo baya kwetu sisi na familia zetu, ….’akasema mzee mmojawapo.
‘Lengo gani baya mzee wetu, sisi tumefanya nini kibaya, kama
wenzenu, tumetimiza wajibu wetu,. Kuwa tumesikia taarifa ya msiba, tukaja kutoa
pole, hizi ni taratibu zetu. Natumai kama tungelikaa kimiya mngelikuja
kutulaumu’akasema mzee wa sheria upande wa mahasimu akijua kuwa hilo
walilolifanya ni linaweza kuwaletea matatizo baadaye.
‘Tumewasikia, na tunachowaambia ni kuwa taarifa hizo sio za
kweli, na kama mna ushahidi kuwa hiz taarifa ni za kweli tunauomba huo
ushahidi, na kama hamna ushahidi, tunaomba mfute kauli zenu, na mwende mrudi na
kipozoe, ..’akasema mwanasheria wa wazee wa babu.
‘Kwanini tufanye hivyo wakaitu tuna uhakika na hilo, …hatuhitaji
kufanya hivyo’aaksema mzee hasimu kwa ujasiri.
‘Sawa kama mnajiamini kw hilo, basi sisi tunawaambia kuwa, kabla
ya hizo siku tatu, kijana wetu ataonekana makaoni akiwa na mke wake, na najua
siku za kukalia kiti chake zimeshafika, hatutataka tena kuzungushana, maana
hapa mumekubali wazi kuwa ndiye mfalme mtarajiwa, na anastahili kukikalia kiti
hicho, kauli yenu na wajumbe wenu wamelithibitisha hilo’akasema babu.
‘Ni mpaka…..maana hizi ni ndoto, hilo najua ni kupoteza muda
tu, kama kweli yupo hai, tunamuhitaji afike na malikia mtarajia makaoni, na siku
hizo tatu zikipita, tutakuja rasmi na anayestahili kuwa mfalme, Na tukija hapa
tutamchukua kwa nguvu, na moja kwa moja tutamtawaza huyo anayestahili kuwa
mfamle maana naona nyie mtatupotezea muda wetu,….hilo tunakuthibitishia, na
mkikaidi, mnajua nini kitawatokea,..hamuoni majanga yanavyowaandama wenzetu…tusipoteze
muda tena’akasema mzee hasimu.
Baadaye wakaondoka huku wakichekea kwa kebehi, na kuwaacha
wazee wa kundi hili wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini, na kila mmoja
akiwaza ni nini cha kufanya, kwani siku tatu, sio nyingi, na siku hizo
zinaanzia muda huo.
‘Sasa mzee wetu tufanye nini, maana kauli yao hiyo ni nzito,
na tumaikubali, hii ina maana kuanzia sasa tupo kwenye mtihani, tunahitajika
tufanye juhudi za makusudi,…’akasema mzee mmojawapo.
‘Hilo wazee wenzangu lisiwatie shaka, kama limeandikwa
halina mjadala, kwanza kabisa naomba mnipe muda wa leo, kesho tutakuwa
tumefikia muafaka, lakini leo nahitaji muda wa kulitafakari hili jambo. Na pili
tunahitajika kumuelezea vyema malikia mtarajiwa, ili asiwe na wasiwasi, na
hili linategemea wananchi wetu,
kutokumshinikiza na tuhuma hizi, …kama ni kweli imetokea hivyo, tutawajibika’akasema
huyo mzee wao.
Mzee yule alipotoka pale hakurudi kwake, moja kwa moja
akaanza safari yake kwenda huko chimbukoni kwao, alijua kuwa huko ataweza kujua
kila kitu , na nini akifanye kwa wakati kama huu, na kama kweli kijana hayupo
hai, itabidi abakie huko kwa muda. Na kabla hajakatiza eneo lao, akakutana na
malikia mtarajia, akionyesha huzuni kubwa usoni,
‘Babu naomba uniambie ukweli, je mume wangu yupo hai, au
hayo wanayosema watu ni uwongo, na kama ni uwongo, kwanini mume wangu hajarudi,
yupo wapi, na kwanini hamuniambii kinachoendelea hapa, na wakati mimi nastahili
kuyajua hayo..’akasema malikia mtarajiwa.
‘Haya nitaongea na wewe, kwasasa hivi naitajika kufanya
jambo, ila nakuahidi kuwa mume wako yupo hai, na hawo wanaozusha hivyo, ni
kawaida yao, …..’
‘Babu…mimi nina mashaka…’akasema na akasita kumwambia kuhusu
lile ua, kwani alikuwa bado na mshaka nalo, kwani ua lile lilikuwa na afya yake
kabisa, hakikupita hata saa moja, liwe limenyauka na kukatikakatika…akatilia
mashaka , akaona arudi tena kuliangalia vyema , lazima kuna kitu kimefanyika.
********
Wakati hayo yakiendelea mzee Hasimu, alifika makoni mwake na
kikundi chake, na walimkuta kijana wao akiwa amesharudi, na wakaanza kumhoji
amefikia wapi kwa kazi waliyompa.
‘Nimefukuzwa na askari wao, …wamenifukuza kama mwizi,
hawajui kuwa mimi ndiye mfalme wao mtarajiwa’akalalamika Yule kijana.
‘Wamekufanyaje, kwani ulitimiza yale tuliyokuagiza uyafanye?’
akaulizwa.
‘Nilifanya vyema kabisa, mimi wakati naongea na huyo malikia
mtarajiwa, wenzangu walikuwa wakifanya yale tuliyokubaliana, na yalileta
matunda, kwani Yule binti, alipofika kuliangalai lile ua lake, alilikuta
limesambaratika, akaanguka na kupoteza fahamu’akasema.
‘Limesambaratika, ..?!..kwani ndivyo tilivyowaagiza,
ilitakiwa mlilegeze kwa moto, ili lionekane limenyauka, na sio kuliharibu,
hamuoni hapo mtakuwa mumetilia shaka, …’Mzee hasimu akasema.
‘Ina maana hilo ua lilikuwa limestawi vyema, mimi nakumbuka
mtaalamu wetu alituambia kuwa kama ua hilo lipo na afya yake huyo kijana
atakuwa bado yupo hai, mbona basi tumekurupuka kwenda huko?’ akalalamika mzee
mmojawapo.
‘Hilo sikuwa nimeliwaza mapema, na sikuwa na imani na hizo
kauli za yule mtaalamu, mimi huwa simwamini sana mambo yake’akasema mzee hasimu
, huku kiwaza hilo alilolifanya kijana wake, na ndani ya moyo wake, akawa
anaingiwa na mashaka na matukio hayo, kama kweli huyo mtaalamu alivyosema ni
sawa, basi, ina maana huyu kijana
atakuwa bado yupo hai,….
‘Hata mimi nalitilia shaka hilo, maana lile ua, kwa taarifa
za Yule mtaalamu, ndio dira ya kuomuonyesha malikia mtarajiwa kuwa mume wake
bado yupo hai au keshafariki, na kama walilikuta hilo ua bado linachanua basi
huyo kijana yupo mahali, na yupo hai’akasema mzee wao mashuhuri.
‘Na kama yupo hai, hapo tutahitajika kuwajibika,…na mjue
tumeshafika kule kwa wazee wenzetu, tukahami, kitu ambacho, hakipo, na
walituasa kwa hilo kuwa turejee na kuja kufuta kauli yetu, tukakana,sasa kama
ni kweli kuwa huyo kijana yupo hai, tunahitajika kuwajibika kwa hilo,…na mnajua
adhabu yake?’ akauliza mzee wa sheria.
‘Adahabu yake ni nini?’ akaulizwa.
‘Mnapomzushia mwenzenu msiba, nyie mnawekwa kundi moja na wachawi,
na adhabu ya mchawi mnaijua, …’akasema huyo mwanasheria akiwaangalia wazee
ambao walibakia mdomo wazi wakiwa hawaamini hiyo kauli, walianza kuingiwa na
wasiwasi.
‘Lakini adhabu zetu zote, zinaamuliwa na wajumbe, kama nusu
ya wajumbe wakikubalina, mzee wetu ambaye ni mkuu wa familia na koo zote,
unahitajika kwanza kujiuzulu, pili kuondoka kwenye eneo takatifu, ili adhabu
kali itolewe juu yako…’akasema mwanasheria wao huku akionyesha wasiwasi, kwa
kauli ile, lakini ndivyo ilivyo, na anastahili kuliweka hilo wazi.
‘Adhabu gani nyingine, na sisi ndio tunaotunga sheria, kama
hicho kipengele kipo, tunahitajika kukiondoa haraka’akasema mzee hasimu na
wajumbe wenzake wakamwangalia kwa kushangaa.
‘Hatuwezi kukiondoa, na ukumbuke kuwa wenzetu pia wana
mwanasheria wao, ambaye kwa pamoja tulikubaliana hilo, kuwa tutazilinda hizo
sheria, kwa mamlaka mliyotupa, na najua haweze kwenda kinyume chake, …ila kinachoweza
kusaidia hapo ni kuwa wajumbe ndio wenye maamuzi ya mwisho wa kuzitekeleza hizo
sheria kwa kura zao’akasema mwanasheria huyo.
‘Wajumbe ni nyie, na sisi tupo wengi zaidi, hapa kwanza ni
sisi sote tuwe na msimamo mmoja, kuwa hiyo adhabu haiwezi kutolewa kwetu, kwani taariza hizo zipo, na kwanini tufikie
kuwaza hilo, kama huyo kijana yupo hai, inabidi tulifanyie kazi hilo’akasema
mzee hasim.
‘Tulifanyie kazi hilo
kazi kwa vipi,kama yupo hai, sheria ipo wazi mzee, mimi naona tumeharakisha
kukimbilia huko, niliwashauri mapema kuhusu hilo, mkasema mna ushahidi kuwa
huyo kijana kaliwa kweli, sasa habari zimekuwa kinyume chake,…tuweni makini kwa
hili, na kuanzia sasa tunahitajika kuwaweka wajumbe sawa, ili wawe pamoja na
kauli yetu iwe nzito’akasema
Mzee hasimu akamwangalia yule mzee mwanasheria, na
kimoyomoyo akasema; `huyu anahitajika kuondolewa kwenye hii kazi, anaweza
kutusaliti kwa msimamo wake huu, hawa watu wenye msimamo mkali, hawastahili
kupewa madaraka kama haya’ halafu akatikisa kichwa na kusema;
‘Hili swala, niachieni kwanza nilitafakari, nahitaji muda wa
leo kulifanyia kazi, baaadaye nitawaita tujue nini cha kufanya, naombeni
tukitoka hapa msimamo wetu uwe ni huo huo, kwasababu hatukukurupuka tu,
tulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa kijana wao hayupo hai, sasa kama hali
imebadilika, sisi kama wahasimu tunahitajika kulifanyia kazi…’akasema kwa sauti
ya ukali.
‘Lakini naomba tuwe makini kuanzia sasa , tufuate utaratubu,
maana uchaguzi unakaribia,, tukienda kinyume,wananchi hawatatuelewa,
tunahitajika tujipange vyema kuonyesha kweli tunahitajika kushika madaraka,
mkumbuke wenzetu huko chimbukoni tulipotoka wanatufuatilia kwa makini sana’akasema
mwanasheria wao.
‘Wewe usiwe na wasiwasi, …huku ni kwetu na hili taifa ni
letu, hawawezi kutuingilia maisha yetu huku, na tukiamua kuwa hivi ndivyo
msimamo wetu, wao hawawezi kuingilia, cha muhimu ni kujipanga na kuwa tayari
kwa lolote lile. Hilo msiwe na shaka nalo,…mimi ni mzee wenu najua nini cha
kufanya’ akasema huku akiinuka kuashiria kuwa kikao kimekwisha.
Mzee huyo alipotoka hapo akaenda kwenye chumba chake maalumu
na kuanza kutafuta njia ya haraka, kwani kweli inaashiria kuwa huenda huyo
kijana wa mhasimu wake yupo hai, na kama yupo hai, inabidi jambo lifanyike,
akatoka pale na kumuita jemedarii wake wa majeshi;
‘Sikiliza tuma kikosi maalumu, cha makomandoo, wamtafute
huyo kijana wa wenzetu, kwani tunahisi huenda bado yupo hai, na tunahitajika
asiwe hai, fanyeni mfanyalo, lakini mwisho wa siku tunahitaji mabaki yake,
yakionyesha kuwa kweli aliliwa na mamba,…’akaagiza huyo mzee,
Jemedari akamwangalia yule mzee, kusubiri amri nyingine, na
alipoona hakuna jingine, akasema;
‘Hilo limefanyika mzee, ..usiwe na shaka, kazi hiyo
itafanyika kama ulivyoagiza’akasema na kuondoka.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Someone necessarily help to make severely articles I'd state. That is the first time I frequented your website page and to this point? I surprised with the analysis you made to make this particular submit incredible. Excellent job!
Feel free to surf my blog ; casinoonlinereview9.co.uk
Post a Comment