Miezi tisa ya machungu ,mateso,maumivu, ilipita kama mchezo,
nikiwa ndani yam situ na mikononi mwa watu ajabu, kuna lipindi nilitamani
nitafute kitu nijiue, lakini huyu mtu wa ajabu alikuwa anahakakikisha hakuna
kitu karibu yangu, kwani alihakikisha kamba aliyonifunga nayo,ilinipa nafasi ya
kufukia sehemu ya kujisaidia na upende wa pili, waliweka maji. Maji ambayo
yalinisaida kutuliza kiu, maana mle ndani ya handaki kulikuwa na jito sana.
Kwasababu walinichukua nikiwa nimepoteza fahamu, kwa muda
huo sikuweza kujua wapi nilipo, nilihisi ni ndani ya handani kwasababu
ukiangalia juu unaona ukuta wa shimo. Siku niliyozindukana nilijikuta
nimefungwa mwili mzima na majani, yanayotoa harufu mbalimbali. Kutokana na
harufi zile nilishindwa hata kuhema, kwano zilikuwa kali sana na mdomoni
nilihisi uchungu sana, ina maana nilikuwa nimenyweshwa dawa chungu, nikawa
napiga chafya mfululizo.
Baadaye huyu mtu wa ajabu ambaye nafikiri ndiye aliyenichukua kutoka kule nilipokuwepo,na kunileta hapo, alikuja na kusimama mbele yangu.
Mtu huyu alikuwa na mchomekundu, nywele laini ndefu,
inaonekana hajawahi kuzinyoa, na akikuangalia macho yake yanatisha. Alikuwa an
ngozi iliyoshupaa kama ya mzee, lakini kwa jinsi alivyokuwa akionekana hakuwa
mzee, labda ni kutokana na wanavyoishi na vyakula wanavyokula.
Alikuwa na mkewe, wakawa wanaongea lugha yao ambayo sikuweza
kuielewa, lakini yule mwanamke, alionekana tofauti kidogo kisura na huyo
mwanaume, yeye alionekana kama sio miongoni mwao, mwili wake na nywele zake
zilionekana tofauti. Hata hivyo yeye alikuwa kiongea lugha yao, huenda wanawake
wapo tifauti na wanaume, niliwaza hivyo mwanzoni, lakini nilikuja kugundua kuwa
yeye asili yake sio miongoni mwa hawo watu.
Yule mwananke akanisogelea
na kunishika, akaniuliza najisikiaje, hapo nikajua kuwa kumbe yeye anajua lugha yangu. Nikajaribu kufunua mdomo,lakini mdomo ulikuw
ani mzito kuongea, nikajitikisa na yeye akanielewa, akasogea pale nilipolala na
kunigeuza geuza, akaninyosha viungo, halafu yule mwanaume akamshika begani, wakaongea lugha yao , wakaondoka na kuniacha
peke yangu.
Maumivu ya tumbo yalikuwa makali sana, na nikawa najisikia vibaya
vibaya , na kuna muda nilijiona kama nataka kupoteza fahamu. Na hali hii
ilikuwa ndio hali ya kila siku siku, hawa watu walihakikisha sitoki hapo
waliponifunga, kazi yao ni kuniletea vyakula, ambavyo mwanzoni vilinipa shida
sana,lakini ikafikia hatua nikaanza kuvizoea, nikawa nakula kuliko kawaida,na
mwili ukaanza kunenepa, tofauti na nilivyokuwa mwanzoni.
‘Hali ya humu ndani mimi sitaiweza, nasikia kama kupoteza
fahamu, na sijisiki vyema’nikamwambia yule mwananke.
‘Hiyo ni kawaida kwasababu ya ujazuito wako, baadaye
itakwisha, kuna dawa tunakupa hizo zitakusaidia’akasema huyo mwanamke, ambaye
alionekana kujua dawa nyingi, maana kila nilipolaalmika hali fulani aliondoka
na kurudi na dawa ya majani, na kuniambia nitafune au ninuse, na utakuaj ile
hali hupungua au kuisha.
‘Kwanini msiniruhusu kutoka nje, maana humu ndani hakuna
hewa?’ nikauliza.
Yule mama akaniangalia kwa macho ya huruma, na hakunijibu
haraka, alitoak kidogo, na baadaye akarudi, akiwa na maji ya moto, na dawa
ambazo aliniambia zitanisaidia kupunguz aile hali ninayoiskia. Aliniangalai kwa
muda, baadaye akasema;
‘Hawa watu ni waajabu sana, mume wangu ndiye aligundua pale
ulipokuwa ukiishi, alikugundua siku nyingi, lakini aliogopa kukuchukua, akijua
jinsi hali ya hapo kwao ilivyo,…’akasema.
‘Hali ya hapa kwao,kwani wewe sio kwenu?’ nikamuuliza.
‘Mimi ni wakuaj huenda kama wewe, lakini hilo kwangu sio la
muhimu sana, la muhimu ni kuwa, mume wangu alikuchukua baada ya wawidaji wao
kukugundua, na wakati wanapanag mipango ya kukukamata yeye akaja kukuwahi, ili
kukuokoa ,na hatukutaka watu wengine wakuone kuwa kakuchukua yeye, lakini wamekuja
kugundua kuwa wewe upo hapa.
`Kiutaratibu watu ambao sio kabila lao,hawatakiwi
kuchanganyikana,mpaka wazee wahakikishe kuwa unakubali na kufuata mila zao,kuna
taratibu zao, na kwanza pia ni lazima upitie kwa wakongwe wa koo, ambao ni
wazee sana, wao wanajua siri nyingi za koo, na ni kama , wachawi kwani wanaweza
kusema mambo yako, hata yale ya siri, sijui wanajuaje.
`Sasa wazee wamegundu akuwa upo hapa, na wazee wanadai kuwa
wewe sio mtu mwema, wanadai ukikaa hapa unaweza kuleta mkosi, kwahiyo
wanahitaji uuliwe, haraak iwezekaanvyo, lakini, wamegundua kuwa wewe ni mja
mzito, sasa hicho ni kikwazo.Na kuuliwa kwako unahitajika upelekwe ukaliwe na
mamba wao wa mizmu.
Niliposikia hivyo, kuwa natakiwa nikawe chakula cha mamba mwili mzima ulizizima,hasa nikifikiria yale
meno ya mamba, na natakiwa nikaatafunwe nayo, nikahema kwa wasiwasi.
‘Wanachosubiri ni wewe ujifungue,maana hawaweze kumuhukumu
huyo kiumbe uliye naye tumboni mwako, hilo haliruhusiwi,kwani wanasema huyo
kiumbe hana hatia, mwenye hatia ni wewe, ndio maana ukafukuzwa huko ulipotoka,
sasa wanasubiri tu ujifungue,na ukijifungua kama ni mtoto mwanaume atapelekwa
kulelewa na kundi la wapiganaji wa kijiji, na kama ni mwanamke, atapelekwa kuwa
mhudumu wa wazee na wakuu wa koo za hadi hapo atakapopaat mtu wa kumuuoa’
Sikutaka hata kusikiliza hayo maelezo, nilianza kusikia
kichefu chefu na moyo ukawa unanienda mbio, na yule mama akagundua na kunipa
dawa, ambayo kila nikiitumia inaleta unafuu fulani, lakini kkwa muda ule
haikusaidia kitu, nikawa nakijaza tu, ili nisikie nini cha zaidi.
‘Wanadai wewe ni kama uchafu uliotupwa, yaani huko ulikotoka
umefukuzwa, na wao hawaweze kuwa jalala la kupokea uchafu’akasema huyo mama.
‘Waligunduaje hayo kuhusu mimi?’ nikamuuliza huyo mama.
‘Nimekuambia vigagula wao, wanajua mambo yasiyojulikana,
wanakujua utafikiri walikuzaa wao, wamelezea maisha yako yote, toka ulipozaliwa
hadi ukaenda kusoma, na ulianza shule nyingine ukiwa mja mzito,..
‘Mume wangu hana jinsi kwasababu yeye ni mtarajiwa wa kiti
kimojawapo cha wakuu wa koo, na ili afanikiwe hatakiwi kwenda kinyuma na
matakwa ya koo zao. Alitaka akusaidia kwa kukutorosha , ili uondoke zako,
lakini kwa sasa anashindwa,kwani wanadai hutakiwi kuachiwa, mizimu yao
inakuhaitaji, inahitaji damu yao, ili iweze kutulia, na kufanikisha mambo yao….sasa’akakatiza
maana aliingia mume wake.
Mume wake akamshika bega ,inaonekana ni ishaar zao, huwa mara
kwa mara akitaka kumwambia kitu mpaka amshike bega. Wakaonega kidogo, na
baadaye wakatoka nje.
Na toka siku hiyo wakawa kila mara wakija wanakuwa pamoja, na huyo
mume hakutaka kumucaha nyuma mke wake, wakawa wanatoka pamoja, kwahiyo sikuweza
kuongea tena na huyo mama, kwa kipindi kirefu, hadi siku moja, huyo
mwanamke akaja akiwa peke yake, na alionekana mwenye huzuni sana, akanipa
chakula , na kunichunguza tumbo langu, inaonekana anajua mambo ya
uzazi,akasema.
‘Unakaribia kujifungua, na mtoto yupo salama tumboni, lakini
yeye ndiye tiketi ya kifo chako, akitoka tu, wewe hutakiwi umaliza hata saa
moja, unahitajika ukatupwe kwenye hawo mamba wa matambiko. Na damu yako
haitakiwi ibakia kwenye aidhi hii, kwahiyo siku ya kujifungua unatakiwa
upelekwe karibi kabisa na huo mto wa mamba.
‘Kuna mwanamke mmoja, atakuja kukuchukua, …ina maana hapa
unatakia uondolewe, huyo mwanamke ndiye mkuu wa mambo yao kwa akina mama, na
ndiye ambaye anatakiwa kuhakikisha kuwa damu yako haibakii kwenye ardhi yao.
Mimi nimemshauri mume wangu atafute mbinu za kukuokoa,
lakini anasema kwake ni vigumu, maana hawo vigagula wanajua kila kitu, kwani
wameshagundua kuwa tuna mipango ya kukusaidia ndio maana huko nje wameshaweka
walinzi watiifu wa hawo vigagula, wananusa kama mbwa.. Kwahiyo wapo wanatakiw
akuhakikisha kuwa kutoka hapa ni moja kwa moja kwenye huo mto wa mamba.
‘Kwani wewe ni nani na umekujaje kuishi na hawa watu,?’
nikamuuliza, maana nilishajua mimi ni mtu wa kufa tu, na ni bora nijue huyu
mwenzangu alikujae hapo. Nilipomuuliz ahilo swali, alitulia kwa muda bial
kusema kitu, baadaye akasema;
‘Kisa changu ni kirefu sana, na sikujua kuwa ningeliweza
kuishi na hawa watu hadi leo, na kwa vile kuja kwangu kwao, wanadai ilikuwa ni
baraka ya familia zo, hawakunizuru. Na nashukuru kuwa mume wangu sio mtu mbaya
na pia kwa vile nimeshazoea mila na desturi zao,najionea kawaida tu, lakini
mwanzoni nilipata taabu sana. Niliingia mikononi mwa hawa watu siku ambayo
sitaweza kuisahau maishani.
*******
Mimi nilikuwa naishi na mama
wa kambo,mama yangu aliachwa na sababu kubwa ni kuwa baba alimpata huyo
mwanamke mwingine, na alitaka amuoe,lakini mama yangu hakukubali, basi mama
yangu akaambiwa aamue mawili, kuwa akubali kuwa mke mwenza au kuachika. Mama
kwa vile alikuw akimjua huyo mke mwenza na alijua kuwa hawatawezekana, yeye
akaamua kuachika.Na kipindi hicho mama alikuwa mjamzito.
Ujauzito huo ulikuwa wa kwangu mimi. Taratibu za kuachika
zilifanyika, licha ya mama kubembelezwa na familia yao, lakini yeye alikataa
kata kata,lakini tatizo lilikuja kuwa mama alikuwa mja mzito, na kiutaratibu
aisngeliruhusiwa kuondoaka hapo kwenye familia ya mume wake mpaka
mamaajifungue, na mtoto anyonyweshe miaka miwli, ndipo mama aatandoke hapo
kwenye miliki ya huyo mume ikabidi mama abakie hapo hadi alipojifungua na
kunizaa mimi.
Alinilea hapo zaidi ya miaka mitatu, na wakati huo baba huyo
keshamuoa huyo mama mwingine, na kipindi mama anaondoka huyo mama alikuwa mja
mzito wa mtoto mwingine. Kutokana na masimango, mateso na vipigo, na hali ya
pale, mama hakuwa na jinsi , ilibidi aondoke, ingawaje, hakupenda, ikiziangatia
kuwa mimi bado nilikuwa mtoto mdogo. Kipindi mama anaondoka nilikuwa na miaka
mitatu hivi.
‘Kama unataka kukaa hapa utakuwa ndiye mfanyakazi wa mke
mwenzako, huoni sasa ni mja mzito, na wewe tumeshaachana, ‘akaambiwa na mume
wake kipindi hicho huyo mke wake ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.
‘Mimi nabakia hapa kwasababau ya mtoto wangu, kama
unaniruhusu niondoke na mtoto wangu hata leo naweza kuondoka naye akiwa mkubwa
nitamleta kwako’akasema mama.
‘Mtoto huyo sio wa kwako, makubaliano yaliyotambulikana ni
kuwa wewe ukishajifungua mtoto unakaa naye hadi miaka miwili, zaidi ya hapo ni
uamuzi wako tu, ila mtoto sio wa kwako tena, ukumbuke kuwa mimi sishindwi
kumlea huyo mtoto,kwasababu ni damu yangu, na ikizingatia kuwa nina mke huyu
mwingine, yeye anaweza kumlea, kwahiyo kama unataka kuondoka, njia ipo wazi,
lakini mtoto wangu hatoki hapa nyumbani’akasema baba.
Basi mama akavumilia kwa muda huo uliokubalika , akiwa ndiye
mfanyakazi wa hapo nyumbani, kuhakikisha anahudumia nyumba, anamsaidia mke
mwenzake, na kwenda shamba, na huku akinilea mimi, maana ingawaje huyo baba
alidai kuwa mimi ni mtoto wake, lakini hakuwa akinijali kimatunzo, zaidi
alikuwa akimjali sana huyo mke wake.
Mama akawa anafanywa kama mtumwa,na huyo mke mwenzake akawa
anamnyanyasa hata wakati mwingine kumchapa viboko.Ilikuwa kama watumwa
waanvyofanyiwa,hana usemi,hana kujieteta, ikafika hatua mwili mzimzulijaa mizchirizi
ya fimbo. Alivumilia kwasababu yangu, alitaka akiondoka niwe katika umri ambao
sitapata taabu, na kweli alivumilia mateso
hayp hado nilipofikiamika mitatu.
Siku hiyo alipoonadoka, sitaisahau,maana hapo nyumbani
kulikuwa hakuna chakula , kwani kilikuwa kipindi cha njaa, watu wanaishi maisha
ya shida sana, na huyo mke mwenzake alishakuwa na watoto wawili tayari na mama
ndiye mlezi, mama ndiye yaya, na ndiye jembe la hapi nyumbani.
Chakula kikipatikana kipaumbele ni familia hiyo,mimi na mama
tunasubiri kama kuna mabaki,kamahakuna tunalala na njaa,sasa mama yeye alikuwa
akihakikisha ananifichia chakula, siku hiyo wakagundua, baba na huyo mama
wakatufuma tukila, walituavamia na kukimwagia kille chakula uchafu, na
kutulazimiash kula na abada ya hapo wakamvua mama nguo na kuanza kumchapao
fimbo, kama mwizi.
Mimi sikukubali, nikaingilia kati na kulala juu ya mgongo wa
mama,ili fimbo hizo zisimchape mama, na bahati mbaya yule mama akanichapa mimi
kichwani, nikapoteza fahamu, nakumbuka kabala fahamu hazijapotea kabisa,
nilianza na maumivi ya kichwa, na giza likawa linanijia machoni taratibu.
Mama aliponiona katika ile hali hakukubali, alimvamia yule
mwanamke, wakaanza kupigana naye, na mama kwa hasira akambamiza yule mama chini,
na kipindi hicho alikuwa mja mzito, baba ambaye alikuwa pembeni na alikuwa
kachanganyikiwa kuona mimi nalalamika kichwa halafu nimetulia kimiya, akajua
huenda nimesha kufa, hakuwa anaona yale mapigano ya akina mama.
Alinifuta pale nilipolala, na akaninikuta ndio nageuza
macho, akajua sasa wameshaua, akainuka haraka, na kipindi hichoo mke wake,
keshabwaga chini, analalamika maumivu ya tumbo. Alipoona hivyo, akamgeukia
mama, na kuanza kumsindilia mangumi,,mimi hapo tena sikuweza kuona, maana giza
lilishatanda machoni,,…nikapoteza fahamu.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Duuh M3 huyo picha inatisha, kisa kipo powa, leo naona hata wazo la siku hakuna!
Woω, that's what I was looking for, what a data! present here at this webpage, thanks admin of this web page.
Also visit my webpage :: small loans
Thank you for sharing. Not to many people in your position are so gracious. Your article was very poignant and understandable. It helped me to understand very clearly. Thank you for your help.
Post a Comment