Nikawa naandamwa na maumivu ya kichwa, na hata kuwa napoteza
fahamu mara kwa mara, au kuweweseka usiku,nahisi ni kutokana na zile fimbo
alizonipiga nazo mama yangu wa kambo,ingawaje yeye alikataa kuhusu hilo.Na
ikizingatiwa kuwa mama yangu alishaondoka,basi hakuna aliyekuwa akijali sana na
baba likuwa akiondoka asubuhi sana na kurudi usiku na wakati mwingine analala
huko huko.
Akirudi haambiwi ukweli, anaambiwa kuwa nimekuwa kama mtu
aliyekumbwa na mashetani.
Nilikuja kuhadithiwa kuwa mama yangu aliondoka siku baadaye
, baada ya kuhakikisha kuwa nimezindukana, na kwa vile alishapigana na
mwenzake, na mwenzake akalifikisha hilo kwa wazee, kuwa kapigwa na mama hata kumsababishia
ubovu kwenye tumbo wakati yeye ni mja mzito. Ikabidi baba amfukuze mama haraka
nyumbani kwake.
Mimi niliposkia hivyo, nikaanza kulia, nikijua kuwa mama
akiondoka nitakuwa katika maisha magumu, hasa kutoka kwa yule mama, basi nikawa
namlilia mama, na mama akamuomba sana baba niondoke naye, hata kumpigia
mgoti,akisema;
‘Nakuomba sana nipo chini ya miguu yako, nakuomba niondoke
na mwanangu, maana simwamini huyu mke wako. Siwezi kuondoka, kumuachia mke wako,
mwanangu,unaona jinsi gani alivyomfanya ,mkeo hana huruma kwa mtoto
wangu,angalia jinsi alivyompiga, anapiga kama anaua nyoka’akasema mama.
‘Hapa utaondoka wewe mwenyewe, mmaana ukikaa hapa utaniuliwa
mke,huoni ulivyomfanya, karibu apoteze uzazi wake’akasema mbele ya wazee ambao
waliitwa kusuluhisha.
Baada yamaongezi marafu, ikakubaliwa mama aondoke, maana
mimi nilishafkisha umri wa miaka mitatu na nusu, na kwa vile mama alishapewa
talaka hakustahili kubakai hapo tena, na hakuwa na mamlaka na mimi.
‘Mama yaani unataka kuniacha, mimi sikubali kubakia hapa,
nitaondoka na wewe, mama usiniache hapa nitauliwa na huyo mama wa kambo ’nikamwambia
mama yangu.
‘Mwanangu inabidi ubakia na baba yako, ndio utaratibu
ulivyo, unachotakiwa ni kuwa mtoto mwema tu, na mungu atakulinda, na kama
ukionewa mwambie baba yako yeye ndiye mwenye mamlaka na wewe, hata hivyo baba
yako sio mtu mbaya, ubaya upo kwa huyo mke wake, namjua sana’akasema mama.
‘Hapana mama mimi sitaki kubakia peke yangu na hawa watu
wataniua, kila siku unaona yule mama anavyonifanya, hanipendi kabisa ‘nikawa
nalia, lakini haikuasaidia kitu kwani mama asubuhi na mapema nikiwa bado
nimelala ,akaondoka, hakutaka kuniamusha maana alijua kuwa ningelikuwa macho
nisingelikubali kubakia.
‘Wewe chokoraa bado umelala, unafikiri upo hapa kwa ajili ya
kulala, mama yako hayupo keshakuacha, sasa ujue kuwa utazifanya kazi ambazo
mama yako alikwua akizifanya, siwezi kukufulia nguo, au kukuhangaika, amuka
anza kufagia na usafishe vyombo’nikaamusha asubuhi na mapema. Na hayo yalikuwa
maagizo ambayo yalikuja kuwa kazi zangu za kila siku.
Mimi licha ya udogo wangu kiumri, lakini niliweza kufanya
kazi zote, mama yangu tulipokuwa naye alikuwa akinifundisha kidogo kidogo, huwa
aliniasa kuwa niwe mchapakazi, na nijitahidi kujua kila kazi, kwani kuna leo na
kesho. Watu walimshangaa kwanini alikuwa akinifundisha kazi wakati bado nina
umri mdogo. Yeye aliwaambia ni bora anifanyie hivyo, ili nisije nikapata taabu
baadaye.
Kwakweli juhudu za mama zilinisaidia sana,kwani hata mama
huyo aliponiambia nifenye hizo kazi, alijua kuwa nimefundishwa , nilijua kuosha
vyombo, kufagia na kazi nyingi za nyumbani, na watu wengi walinishangaa sana,
maana nilijua kazi nyingi kama mtu mzima, na huyo mama ndio akapatia nafasi ya
kunifanya mimi mfanyakazi wake.
Mimi sikujali maana nilipenda kufanya kazi, kilichoniumiza
ni kule kusimangwa, kwasababu ya umri wangu, hata kama nilijua kuzifaya hizo
kazi, lakini nisingelikuwa na uwezo wa haraka kama mtu mzima, basi ikawa ni
tatizo, mara nyingi anakuwa nyuma yangu na fimbo. Hali hiyo ilinipa shida sana nikawa
nafanya vitu kwa kuogopa, kinyume na alipokuwepo mama yangu.
Kila mara nilikuwa nikimkumbuka mama, na kujiona mkiwa,nikawa
nalia huku nafanya kazi, na wakati mwingine walikuwa hawanipi chakula, napika
mimi, lakini mwisho wa siku nambulia kuonja tu, lakini hilo halikunipa shida
sana, nilipowajulia tabia zao, maana mimi
ndiye mpishi wao, niliweza kula kidogo kidogo, licha ya kuwa mama yangu mzazi alinifundisha
kuwa ukipika usiwe unapenda kulia jikoni..
‘Baba , mbona mama ananifanyisha kazi mimi peke yangu,
wakati wenzangu wapo hawafanyi kazi, mimi naamushwa asubuhi sana na kufanya
kazi zote za nyumbani, wakati mwingina hata shuleni nachelewa au naambiwa
nisiende kabisa’ siku hiyo nikamwambia baba. Baba akamuita mama nakumuuliza
kwanini ananifanyia hivyo, na mama akakataa katakata akisema yeye kazi zote anafanya
yeye, mimi nasingizia tu , kwasababu sitaki kutumwa kazi ndogo ndogo.
Baba hakuwa mjinga akaanza kuchunguza na kweli akagundua
hilo, na alianza kumfokea mama , na kila ikitokea hivyo, baba akiondoka tu nafuatwa
kwa fimbo, na kuandamwa kwa kazi, ikawa nipo kwenye hali ngumu sana. Hali yangu
kiafya ikawa inazorota, na hata mahudhuria ya darsani yalikua mabovu, kwani
hata nikifika shuleni wakati mwingine najikuta nimechoka sana, lakini nilikuwa
na akili ya ajabu, mitihani nilikuwa nafanay vizuri.
Sikupenda kulalamika kwa baab tena. Nikawa najifanyia kazi
zote, ili tu nisikosane na huyo mama, lakini huyo mama hakuwa na jema, bdo
alikuwa akiniandama kwa masimango, na sasa akawa ananisingizia mambo ya uwongo,
kikiharibika kitu au kupotea kitu nasingiziwa mimi. Nilijitetea sana , lakini
walivyokuwa wakifanya ilimfanya baba aamini kuwa eti mimi ni mdokozi.
Siku mbili walinitegea pesa za baba, kwani mara nyingi baba
akirudi kuna sehemu yake maalumu anaweka pesa zake, siku hiyo aliporudi akakuta
pesa zake zimepungua, akaanza kuuliza ni nani kachukua pesa zake, na kwa haraka
mama akasema huenda ni mimi akisema bila aibu;
‘Labda ni huyo binti yako mdokozi’akasema mama akiniangalia kwa jicho lachuki.
‘Huo udokozi kauanza lini, ?’ baba akauliza na mama
akamwambia ndio tabia yangu, nadokoa hata nyama jikoni, naiba pesa nikienda
sokoni na kuzitumia.
‘Mimi sijachukua pesa zako baba, mimi sio mwizi, sijawahi
kuiba hata siku moja ‘nikajitetea,
‘Kama kuna mtu kachukua sizani kama atakuwa kazitumia zote,
labda tufanye msako, chumbani kwao’ akasema mama. Na kwa vile sikuwa na
wasiwasi mimi nikasema ufanyike huko msako, na hakupita muda baba akaja akiwa
na hasira, huku kashikilia mfuko wangu wa shule.
‘Pesa hizi ndani ya mfuko wako umezitoa wapi?’ akauliza kwa
hasira.
‘Baba mimi sijui na sijui zimefikaje hapo kwenye mfuko wangu,
lazima kuna mtu kaziweka humo’nikasema huku nikiwa na wasiwasi. Cha ajabu baba
alinikemea tu siku hiyo na kunionya kama
ikitokea tena hatakuwa na msamaha na mimi. Nilishangaa kwanini hakuchapa siku
hiyo, tofauti na siku nyingine ambazo, nikishitakiwa kwake anachapa kweli
kweli. Nilijua kabisa hakuamini hayoo maneno ya mama, kwani alionyesha kujihami
mapema. Hata hivyo mama alichukua fimbo na kuanza kunichapa akisema
ninamuabisha, na ataonekana yeye hajui kulea.
Baada ya tukio hilo nikawa muangalifu sana kila mara
nachunguza mfuko wangu na sehemu ninayoalala ili wasije wakaniwekea tena mtego
kama huo. Lakini dhamira yao ilifanikiwa siku moja. Siku hiyo nilipewa barua ya
matokea ya mtihani, nilimpa mama, mama akasema niende nikaweke chumbani kwao.
Kumbe mama alikasirika kwa vile mimi kwenye mtihani nimefanya vizuri zaidi ya
watoto wake akaona anikomoe. Mimi bila kujua nikaingia chumbani, na kumbe alishaongea na
baba kuwa mimi huwa naingia chumbani kudokoa pesa, kwahiyo ajifiche mahali
ataniona mimi nikingia chumbani.Mimi nikaingai kama alivyonielekeza mama.
Nilipofika chumbani ikakuta nguo zimedondoka chini,mimi
nikaziokota na kuzikunja vyema na kuziweka kweney kabati,sio mara ya kwanza
kufanya hivyo, nilipomaliza, nikatika na kuingi achumbani kwangu nikiwa na
furaha kuwa baba akirudi akiona matokea yangu ya mtihani atafurahi sana na
ataniruhusu nikamtembelee mama yangu.
Mama yangu alikuwa kaolewa na mume mwingine, na walikuwa
wakiishi kwa amani, na furaha, na huyo mume wake alikuwa tayari niende nikaishi
nao, lakini baba yangu alikataa kabisa, akidai kuwa anazalilishwa kuwa yeye
hajui kutunza watoto.
Basi maranikasiki sauti ya baba akiongea nje, na mimi
nikasubiri, nikijua baba akiingia ndani atakuta amtokea yangu ambayo niliyaweka
sehemu ya wazi, ili ayaone, ikapita muda, na mara nikasiki baba akifoka, na
mara nikaitwa kwa sauti ya hasira.
‘Wewe leo hujawahi kuingia chumbani kwagu,na kama uliingia ulifuata
nini huko na ulifanya nini?’ baba akaniuliza maswali mengi kwa haraka haraka.
‘Nilileta barua ya matokeo yangu ya mtihani, baba hukuyaona
nimefaulu vizuri sana, hiyo barua ipo chumbani kwenu’nikaanza kuongea
nikionyesha uso wa furaha nikijua kuwa baba atanisifia kwa kazi nzuri
niliyofanya, lakini …..kabla sijamaliza nikajikuta nimezabwa kofi la nguvu
shavuni, nikapepesuka huku nikiwa nimeshikwa na mshangao, vipi tena.
‘Leo nimekufuma mwenyewe maana pesa zangu zilikuwa kwenye
nguo,na wewe ndiye uliyeingia na nimekuona kwa macho yangu ukizikunja hizo
nguo, nipe pesa zangu kwanza tena kwa haraka kabla sijakutafuna mzima mzima’akasema
huku akiwa kashikilia fimbo.
‘Baba mimi sijachukua pesa zako, kweli niliingia chumbani
kwenu, nikiwa na nia ya kuweka barua ya kutoka shuleni, humo ndani nikaona nguo
zimedondoka nikaziokota nakuzikunja vyema,lakini sikuchukua pesa zako baba ,
mimi sio mwizo’nikajitetea.
Niliposema kuwa niliingia na kukuta nguo nikazikunja, hapo
baba akaamini kuwa kweli nimezichukua pesazake maana zilikuwa kwenye hizo
nguo,mimi nilikuwa sijui, huenda mama walifanya hivyo makusidi ili ionekane
nimezichukua kwenye hizo nguo!
‘Leo utaniambia ukweli, kwanini tabia hiyo huiachi,mwanzoni
nilikuwa nakutetea lakini sasa naona kuna ukweli ,maana nimekushuhudia mwenywe
ukiingia chumbani kwangu, na ukatoka ..’akasema baba na kwenda ndani ambapo
anaweka fimbo yake maalumu ambayo haivunjiki ukichapwa nayo, na nimjuavyo baba
akianza kukuchapa anaweza akakuumiza vibaya sana,nikaona ni bora nikimbie.
Nikachomoka, na kukimbilia kwenye kichakani kilichopo karibu
na hapo nyumbani, nikajiingiza humo, na muda huo nikamuona baba akitoka akiwa
na panga, nikajua kuwa baba kweli kazamiria kuniua, na aliponiangalia huku na
kule bilakuniona akaingia ndani, nikajua anakwenda chumbani kwetu,ninapolala na
wadogo zangu, watoto wa mke wake na punde akatoka huku kashika pesa mkononi, na
kusema kuwa kaziona kwenye nguo zangu, lakini nusu imetumika.
‘Huyu mtoto leo atanitambua, kumbe kweli ana tabia hiyo
mbaya ya udokozi, kumbe ana tabia mbaya kiasi hiki, yupo kama mama yake,
kiburi, hasikii akiambiwa jambo….sasa hiyo tabia nitaokomesha leo, moja kwa
moja , ni bora nijulikane sina mtoto….‘akasema baba yangu huku kashika panga
mkono mmoja na bakora upande mwingine.
Niliumia sana kusikia hiyo kauli kuwa eti mama yangu alikuwa
na tabia mbaya, kitu ambacho sio kweli. Mama yangu alisifika hapo kijijini kama
mke mwema, mama mwenye tabia njema na hata alipoachika kwa huyo baba wanaume
wenge walimfuata kutaka kumuoa. Na baba aliposikia hivyo aliingiwa na wivu, akawa
anamtangazia ubaya, lakini hakuna aliyemsikiliza, ilijulikana ni kwa sababu ya
huyo mke wake mpya.
Kwa kauli hiyo nikamchukia baba, sikutaka tena kuonana na
yeye na hata ile kauli kuwa kabadilika kwa ajili ya mke wake huyo nikaiondoa
kichwani, nilimuona kuwa ni baba mbaya, asiye na maana kwangu tena.
Pale nilipojificha nilimuona akihangaika huku na kule
akinitafuta na fimbo yake mkononi. Mimi nilikuwa nimetulia kimiya nikiwa
nimeuma kucha kidole kidogo, wanasema ukifanya hivyo, kama umejificha mtu
hakuoni.
Kauli ile ya baba ilinichefua, nikaona niondoke kabisa hapo
nyumbani, sikuweza kuvumilia, nikalia sana huku nikikimbia, kuelekea nisipokujua
nilikuwa nakimbilia tu, nilikimbia, hadi nikafika karibu na huu msitu, sehemu
ambayo watu hutafutia kuni, na wakishakusanya hufika kwenye miti ambayo inatoa
kamba. Na mimi nilifikia mti mmoja wa hizo kamba na kujikuta nachuna kamba na
kuzikusanya hadi nikapata mzigo unaonifaa. Kamba hizi ni imara sana kwani
hutumika pia kujengea.
Wakati nimetulia chini ya ule mti, nilianza kuwaza nini cha
kufanya.
‘Mimi naona sina maana katika hii dunia, maana kila
nilifanyalo hakuna heri, nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kutimiza wajibu
wangu, lakini sifanikiwi, hivi huyu mama anataka nimfanyie nini ili anione mimi
ni sawa na mtoto wake, au nimemkosea nini kikubwa, labda mimi sistahili kuishi
naye, labda nikifa atafurahi. Maana yeye ni mmojawapo ambaye hataki niende
kuishi kwa mama yangu mzazi. Sasa anataka nini kwangu…’nikashika shavu.
‘Kwanini kama hanipendi, hataki nikaishi na mama yangu
mzazi, nimeshagundua huenda raha yake ni mimi nipotee hapa duniani. .labda
nikifa atafurahi.’basi nikawa naongea peke yangu, huku ninalia, huku ninasokota
kamba, mwanzoni nilikuwa najisokotea tu hiyo kamba bila kujua ni ya nini.
Kidogo kidogo nikajikuta nimesokota kamba moja ndefu, nzuri,
na hapo ndipo wazo la kujinyonga likakolea kichwani, nikakumbuka msichana mmoja
aliyejinyonga hivi hivi kwa kamba, sasa hivi watu wameshamsahau;
‘Basi ngoja na mimi
nijue, ili mama huyo asiyenipenda afurahi na moyo wake, na najua baada ya muda
watu watanisahau na hawatajua kuwa nilikuwepo kwenye hii dunia’nikasema huku
nikiitayarisha ile kamba vyema.
Nilipohakikisha imekuwa vyema, nikapanda nayo juu ya mti ,
hadi kwenye tawi kubwa, nikaifunga ile kamba kwenye lile tawi upnde mmoja na
upande mwingine niliokuwa nimetenegneza kitanzi, nikajivika shingoni, nikatulia
huku nikiwaza jinsi mama yangu atakavyolia, lakini sikujali nikijua kuwa atalia
kwa siku kadhaa na baadaye atanisahau na watu wote watakuja kunisahau na mimi
nitakuwa nimeokoka na hayo mateso.
Nikasogea kwenye sehemu ambayo nilijua nikiachia tu ile
kamba inanikaba halafu kitakachofuatia ni kupteza uhai. Nikamuomba mungu
anisaidi nife kwa haraka, na kuomba kuwa
mama yangu asihuzunike sana, anishau kwani nampenda sana ,lakini watu hawo wabaya hawanipendi ndio
maana naona ni bora nikajipumzikie huko ahera,
Nikahesabu moja mbili tatu, nikajiachia, …nakweli kamba
ikashikilia vyema shingoni na kunifanya niwe naelea hewani, pumzi ikaanza kuisha
na shingo ikawa inauma kwa jinsi ile kamba ilivyonikaba, jasho, likaanza kunitoka
pumzi ikawa haitoki, nikajaribu kuitoka ila kamba shingoni,lakini haikuwa kazi
rahisi nikajaribu kupiga kelele ya kuomba msaada, lakini sauti haitoki, mkojo
na hata haja,vikaanza kunitoka,
Nikawa sasa nahangaika kwa kujipiga piga miguu ili kama
ikiwezekana ikatike, lakini ndio ikazidi kunikaba vyema, maumivu ya kichwa,
kukosa pumzi, na hali ngumu ambayo sijawahi kuihisi kabla vikaniandama, niliomba roho itoke
haraka, lakini haikuwa hivyo, na kitu kama mnguruma ukaanza kusikika kichwani, nikajau sasa muda umefika, lakini sikujua ningelipata taabu kiasi hicho, na kabla sijapoteza fahamu
nikahisi nikipaa hewani ,na kichwa kikaginga kitu, sikuweza kujua
nini kilifuata baadaye...
NB: Hivyo hivyo siku zinakwenda.
WAZO LA LEO: Tupende kuwafundisha watoto wetu tabia njema, na kuwazoesha kazi ndogondogo, ili baadaye wasije wakapata taabu, tukue kuwa maisha ni kupanda an kushuka, kuna leo na kesho ambayo hatuijui, tukiwadekeza watoto wetu, wanaweza wakapata taabu badaye, kama walivyosema wahenga,
samaki mkunja angali mbichi
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kazi nzuri M3, natamani ungeliendelea kidogo.
Post a Comment