Maua baada yam bio ndefu za masafwa marefu yasiyojulikana
mwisho wake, aliishiwa nguvu, na hakuweza kwenda mbele zaidi maana kwa mbele
yake kulikuwa na majabari, nyika, na miinuko mikali, akasimama, na hata kukaa
chini, na kujilaza kwenye majali laini, akahisi hapo alipolala kuna maji maji.
Kwana kiusalama akatizama huko alikotoka, alichoona ni
misitu na nyika, na karibu yake kuna bwawa kubwa la maji machafu, akalitizama kwa
makini,na hapoa akawaona wale wadudu waitwayo ruba, akasogeza mguu wake mbali na
maji, maana sifa za hawo wadudu wakikuuma huwa wanazama mwilini, na ukitaka
kumtoa na mkono anateleza,kwahiyo labda uwe na ugoro umpake,,au kisu kikali
ukate sehemu ile aliyouma, na kutumia nguvu kumvuta!
Hakuamini kuwa alilipita hilo bwawa bila kujua, na hata bila
kuzama,maana hilo bwawa halipitiki, lina maji na mtope,ukizama humo unapotea
moja kwa moja, hakuna anayejua urefu wa kina chake, na humo ndani utapambana na
hawo ruba na mamba, lakini yeye alipita hapo hadi ng’amboya pili yake bila
kujua , bila kuzama,na bila kuumwa na hawo wadudu, hakuamini!
Alipowafikiria hawo wadudu ikabidi ajikague mwili mzima,
akiwa na wasiwasi wasije kuwa hawo wadudu wamemgandia miguuni mwake kuanza
kuzama ndani, maana wapo kama funza,au minyo mirefu,,lakini hakuona kitu, ila
miguu ilikuwa ikiuma kwa ajili ya kukanya miba,na kuchoka kwa kukimbia
pekupeku,hakumbuki kabisa viatu vilimtoka wapi,kwamuda huo hakujali sana.
Alijituliza na ubavuni akaanza kuskia maumivu makali, kuna
miiba ilimchoma, na sio miiba tu ni miti, kwani wakati anakimbia na kukatiza kunwa wakati mwingine alikuwa akikimbia huku anaangalia nyuma kuona kama anafuatiliwa, na
hapo hujikuta kajibamiza kwenye miti yenye matawi yenye ncha kali, na wakati
mwingine hudondokea miiba hiyo au miti hiyo yeye ncha kali, huenda hapo ndipo
alipoumia ubavuni …
Kuna muda lidondoka, akajikuta kaganda kwenye miti
iliyomchoma na hakuweza hata kujinasua maana ile miti ilimchoma utafikiri
kabanikwa, na wakati anajitahidi kujikwamua kwa utaratibu , mara akasikia
vichakani miti na vijiti vikuvunjika,ikiashiria kuwa kuna kitu kinamnyemelea, akajua huyu ni mnyamamkali, kwa ajili ya ule
uwoga uliompta kwa muda huo, akajinausa kwa haraka kutoka kwenye ile miti na
miba iliyomchoma, na kuanza kukimbia tena.
Wakati anakimbia akasikia nyuma yake kitu kikimfuatilia,
akajua huyu kama sio simba ni chui au fisi, basi akaongeza mbio kukimbia, na
kweli kila mara alipojitahidi kukimbia bado alihisi kuna kitu kikimfuatilia kwa
karibu, lakini kikiwa kimejificha kiasi kwamba hakionekani kwani kulikuwa na
majani marefu, akajua leo anakufa, kamkimbia simba mtu na sasa anapambana na
simba mnyama, alikimbia kuliko maelezo.
Tahamaki ndio yupo ngambo ya hilo bwawa,bwawa ambalo
linatambulikana kama bwawa la mamba, humo kuna mamba,kuna wadudu wabaya, kuna
ruba, na hakuna mtu katika hali ya kawaida anaweza kupita sehemu hiyo.
‘Sasa mimi nilipita juu ya hili bwawa,lenye matope, bila
kuzama?’ akajiuliza na kuangalia sehemu
aliyopita. Na kweli kulionyesha njia aliyopitia na maji yalishaanza kujaa, na
kuyafukia yale majani aliyokuwa kayakanyaga na kulala. Baada ya kuona hivyo, akajiangalia
mwilini na kujiona kweli kajaa matope, nguo hazitamaniki.
‘Sasa nitarudije huko nilipotoka?’ akajiuliza.
Na wakati anawaza hilo mara akasikia kelele, hizo ni kelele
za watu, akajua labda ni baba yake huyo anaendelea kumtafuta, alichofanya ni
kwenda mbele zaidi na huko akafikia kwenye sehemu iliyoshonana, na kutengeneza
kitu kama kiota, hapo akasema itakuwa makao yake ya muda, lakini akaogoa isije
ikawa ni sehemu anapoishi mnyama, au nyoka wakubwa
‘Nitakaa hapa hapa, kwani mimi ni sawa na mfu tu, ngoja tu
nikaliwe na hayo machatu, nitafanyaje kama wazazi hawanitaki tena nina maana
gani kwao ‘akasema ,lakini akili ilipomjia picha ya chatu, akasimama, na mara
kwa mbali akaona kitu cha ajabu.
Kwenye lile bwawa kuna mizizi mirefu ambayo imeshikilia miti
mikubwa, mizizi hiyo ni kama kamba inayoninging’inia kutoka juu hadi kufikia
kwenye lile bwawa. Sasa aliona watu wa ajabu wakiitumia ile mizizi kuninginia
kutoka sehemu moja hadi
nyingine,ilionekana ni kama njia ya usafiri, kuvuka lile bwawa kutoka upande
mmoja hadi ng’amb ya pili. Mtu hutembea na hizo kamba akiwa kama anabemba na
kupokea kamba nyingine baada ya nyingine hadi anafika ng’ambo ya pili, ni kama
wanasarakasi.
Watu wale walikuwa
wamvaa ngozi za wanyama na sehemu kubwa ya mwili wao wapo wazi, na waanwake
walikuwa wameacha sehemu ya mtiti yao wazi,kila mmoja kabeba mishale na upinde,
kuonyesha kuwa ni wawindaji, na wanawake wamebeba vikapu vilivyotengenezwa kwa
ngozi za wanyama. Na Maua alipona hivyo, akili yake ikamkumbusha kuhusu watu wa
ajabu wanaoishi mapangoni.
******
Maua kama walivyo watoto wengine, kila wakikutana na babu za
bibi zao hupenda kudadisi mambo mbalimbali. Siku moja Maua alimuuliza babu yao,
wakati wanapita kwenye msitu huo mkubwa, alitaka kujua kuna nini ndani ya msitu
huo , na kweli kuna watu wanaweza kuingia humo.
Babu yake aliposikia hilo swali, akatafuta mbinu za kuvunga
vunga, ilimradi wapiti mbali na huo msitu,kwani yeye mwenyewe alishasikia toka enzi za utoto wake, kuwa
ukipita kwenye huo msitu na ukaanza kuuongelea mabaya, hutawaweza kufika mwiho
wa safari yako.
Na walipofika mbali na huo msitu , babu yake akamwambia mjukuu
wake kuwa humo ndani ndio kuna watu wa asili, watu ambao wanaishi ndani ya
mapango, na chakula chao kikuu ni nyama, mizizi na matunda ya porini, huwa
wanavyaa ngozi za wanyama.
‘Wapo kama sisi, yaani ni binadamu kama sisi?’ akauliza
Maua.
‘Ndio wapo kama sisi, ni binadamu kama sisi, lakini wao
hawataki mabadiliko, hawataki kuishi kama sisi, maisha yao hayana tofauti na
wanyama wa porini, wao wakituona sisi wanatudharau kuwa tumepotea' akasema
babu.
‘Ina maana kuna muda wanaoenakana, na hata kuongea na sisi
na je lugha yao ipoje, inajulikana?’ akauliza Maua.
‘Utofauti wao ni maisha yao, yasiyotaka mabadiliko, na
kwasababu wamezea kukaa mapangoni, miili yao inakuwa kama ina manyoya , na
wengine wana nywele nyingi, na hawavai nguo kama sisi mara nyingi utawakuta
wamevaa ngozi na magome ya miti.
‘Kwahiyo wanatisha, watakuwa kama wanyama?’ akauliza.
‘Kweli ukiwaoana wanatisha, na watu wengine hudai wanakuala
nyama za watu,’akasema baba na kumfanya Maua aogope.
‘Wanakula nyama za watu..? babu haiwezekani, maana wewe
mwenyewe ulishawahi kunihadithia kuwa watu wanakula nyama za wanadamu ni wanga,
ni wachawi, mtu w akawaida na akili yake timamu hawezi kula nyama za watu..’akasema
Maua.
‘Hizo ni imani za watu, nasikia kuwa kwenye imani zao hawo watu wa ajabu ni kuwa wakila nyama zetu na
kutumia viungo vyetu kwenye mambo yao, wanakuwa na maisha mazuri, na wanafanikiwa
katika mambo yao ya uzazi, imani hizo ni sawa na imani za hawa watu
wanaodanganywa na waganga wa kienyeji kuwa wakipata miili ya albino watapata utajiri, na
wao wenyewe kwa wenyewe wanadanganya hivyo hivyo,kuwa wakipata nyama zetu
watafanikiwa katika mambo yao’akasema babu.
‘Wewe alikusimulia nani?’ akaulizwa.
‘Kuna mwanamke mmoja alitokea huko akapotea na kukutwa
akihangaika, mtu mmoja akamchukua, na waakishi naye, hadi akafikia kumuoa, yeye ndiye aliyakuja kutoa siri za huko. Na
kila siku kuna watu wanapotea kiajbu ajabu,na ukiuliza sana utaambia huyo mtu
alikwenda kuiwinda au kama ni mwanamke utasikia alikwenda kukata kuni, au
warina asali, kwa taarifa za haraka haraka ni kuwa huenda walikamatwa na hawo
watu wa msituni wakafanywa kitoweo,kuliwa na wanyama wakali, au kumezwa na
chatu.
Kisa kama hiki kutoka kwa babu yake, alikisikia kwa wanafunzi wengine
waliohadithia hivyo hivyo , kwahiyoakajua kuwa kweli sio hadithi za babu za
kutunga ,ila kuna ukweli ndani yake,….
Maua na watoto wenzake wakawa hawapiti njia ya huo msitu
toka asimuliwe hiyo habari na babu yake na habari hizi zikawa zimesambaa kila kona,
hata watu wazima wanaogopa kufika huko, labda wawidnaji wa siku moja moja, na
wao kila wakija wanakuja na habari mbaya za kutisha, na wakati mwingine mmoja
wao harudi, hupotelea huko huko kiajabu.
Kwa habari hizo, watu wengi waliamini kuwa huko hakuendeki,
na msitu huo ni msitu wa kifo, sio wa kuendea. Babu yake yeye anasema alikuwa
akifiak siku moja moja kwenda kuchimba dawa zake, na huwa hafiki mbali. Leo hii
yupo ndani ya huo msitu, sio hadithi tena, sio visa vya kusadikika tena, Maua akajionea
mwenyewe, na katiak akili yake hakurarajia kuwa ipo siku ataingia huo msitu, au
ipo siku atakutana na hawo watu. Leo siku
imetimia na myoni akasema ama kweli
lisemwalo lipo.
Maua akaishiwa na nguvu, hakujua sasa afanye nini, kwani
kila mahali kazungukuwa na maadui, hawezi kuvuka hilo bwawa, kwasababu kuna
mamba na ruba, na hata ulivuka hilo bwawa kwa mbele yake ndipo wanapoishi
wanyama kama simba chui na wengineo, kwasababu eneo hilo ni karibu na mbuga za
wanyama. Na huku alipo, akitaka kwenda
mbele zaidi, huko hakuendeki, kwani ni kuna miamab na makorongo, ambayo huishi
chatu, nyoka wakubwa na wenye sumu kali.
Huko kwa taarifa za babu yake, aliwahi kusikia kuwa ukivuka
huo mto kwa mbele hakuendeki, hakuna binadamu aliyewahi kwenda huko , maana ni
maeneo ya chatu, na majoka wakubwa, hata hali ya hewa yake imejaa haufu za
ajabu, harufu yeka tu ni sumu kwa biandamu.
Kukatisha kushoto au kulia, kuna hawo watu wa mapangoni,
ambao hadithi zake zinatisha, ina maana yeye sasa anaweza kuwa kitoweo cha hawo
watu, na hata hivyo, kama atafanikiwa kutoroka maeneo hayo ya hatari, atakwenda wapi, maana
nyumbani napo baba kageuka kuwa simba, simba mkali kuliko simba mnyama….akaona
ni heri , hata kama ana njaa, ni bora tu, ajiudie kwenye kiota chake,
alichofanya ni kutambaa,hadi mbali kidogo naupeo wa wale watu wa ajabu
Na alipokaribia eneo la kiota chake, akasimama na kuanza
kutemba polepole, huku mwili ukitetemeka kwa woga, tumbo likiuma kwa njaa,
mdomo umekauka kwa kiu, na akili imechoka kufikiri, lakini ni lazima ajitahidi
kutafuta chochote ili aweze kuishi, akakumbuka kuwa ndani ya hicho kiota chake
alibakiza matunda kidogo, na aina fulani ya mizizi kama mihogo, ambayo huliwa.
Alipofika kwenye kiota chake akahisi kama harufu ya
nyama,…nyama iliyokuwa ikibanikwa jikoni, akasimama na tumbo likanguruma kwa
njaa, licha uwoga, bado uchu na njaa vilitawala nafasi yake. Hata hivyo
kwasababu ya uwoga, hakuweza kuingia ndani akasimama kwa muda akiwa kaduwaa na
kushindwa kuamua lakufanya.
Akasikia mchakato wa kitu, kama mtu au kitu kinatembea ,
hakuwa na uhakika kuwa sauti hiyo imetoka kwenye kibanda chake cha muda
alichojenga au ni maeneo ya karibu, lakini alikuwa na uhakika kuwa ni sauto ya
kitu kinatembea, akaanza kurudi kinyume nyume, akitaka kukimbia, lakini kabla
hajasogea mbali, akahisi kwa nyuma yake kuna mtu au kitu, kwa jinsi uwoga
ulivyomshika, akaogoap hata kugeuza kichwa,…akasimama. Akahisi mtu au kitu
hicho kinamjia pale aliposimama, akapanua mdomo kupiga ukelele.
Kabla hajafunua mdomo ukelele, akashikwa na kitu begani, ugumu wake kama
chuma, na hata mdomo ulipofunguka, ulishawahiwa na mkono wenye manyoya ukaziba
mdomo wake, vitendo hivyo vilifanyika kwa haraka na kwa jinsi alivyoogopa, na kwa
ajinsi ya njaa, na kwa jinsi ya maumivi ya vidonda mwilini, akajikuta akizama
kwenye giza nene, na kabla hajapoteza fahamu alihisi kama anaiunuliwa hewani,
kama kubebwa..
NB: Kwa wale wanopenda kuigiza picha za mambo ya ajabu, watapenda kisa hiki sehemu hii , hapo ni mwanzo tu
WAZO LA LEO: Tunatofautiana sana katika maisha, kikipato, leo ukilia njaa, na kulalamika shida kuna wengine wanakuona wewe una afadhali, na halikadhalika, kuna ambao hawajui kabisa njaa, au maisha magumu na hata ukimwambia una shida huenda akafikia kukushangaa, na hata kukuona labda wewe ni mzembe. Lakini tujue kuwa yote ni maisha,kupata au kukosa yote ni majaliwa ya muumba, ukipata mshukuru yeye na ukikosa mshukuru yeye pia, kama wasemavyo wahenga, aliyekupa wewe ndiye aliyeninyima mimi.
Ijumaa njema
Ni mimi:
emu-three
19 comments :
wow inasimsimua na kuogopesha kidodo kazi nzuri sana..wazo la leo wengi tusilisahau. Ahsante sana na ijumaa njema sana kwako pia ndugu wangu!!
I wаs reсommеnded this webѕite bу my cousin.
I am not sure ωhеther thіs post is wгitten by him as noboԁу else know such
detailed аbout mу difficulty.
Yοu're incredible! Thanks!
Also visit my site - keyword
Hiyo sura hapo mwanangu. Sasa hivi m3, unatuletea kali ya maporini, kama movie
Wow! In the end I got a weblog from where I know how to really get useful information concerning my
study and knowledge.
Check out my weblog ; http://propertyinturkeyforsale.net
What a data of un-ambiguity and preserveness of valuable know-how regarding unpredicted emotions.
My page - Huoneisto Bodrumista
After looking into a few of the articles on your web page, I seriously appreciate your technique of writing a blog.
I saved it to my bookmark webpage list and will be checking back in the
near future. Take a look at my website too and tell me your opinion.
My page : boligityrkia.net
Please let me know if you're looking for a article author for your site. You have some really good articles and I believe I would be a good asset. If you ever want to take some of the load off, I'd love to write some
articles for your blog in exchange for a link back to
mine. Please blast me an email if interested. Regards!
Review my page :: Ferienwohnung Antalya
Its such as you read my mind! You seem to know so much approximately this, like
you wrote the ebook in it or something. I feel that you can
do with some p.c. to force the message home a little bit, but instead
of that, that is fantastic blog. A fantastic read.
I'll definitely be back.
my website :: how to get rid of acne
It's difficult to find educated people about this topic, but you seem like you know what you're talking about!
Thanks
Feel free to visit my web blog :: How To Get Rid of Hidradenitis Suppurativa
Hey I know this is off topic but I was wondering if you knew of any widgets
I could add to my blog that automatically tweet my newest twitter updates.
I've been looking for a plug-in like this for quite some time and was hoping maybe you would have some experience with something like this. Please let me know if you run into anything. I truly enjoy reading your blog and I look forward to your new updates.
Feel free to visit my site :: acne product
Thank you for the good writeup. It in fact was a amusement
account it. Look advanced to far added agreeable from you!
By the way, how can we communicate?
Also visit my homepage planetecountry.com
I was suggested this blog by my cousin. I'm not sure whether this post is written by him as no one else know such detailed about my difficulty. You're incredible!
Thanks!
Feel free to surf my web site :: stopacneoutbreaks.com
I've been browsing online more than 3 hours today, yet I never found any interesting article like yours. It's pretty
worth enough for me. Personally, if all webmasters and bloggers made good
content as you did, the web will be much more useful than ever before.
Also visit my web page - Acne Treatment
I'm really inspired together with your writing talents as smartly as with the format in your weblog. Is this a paid theme or did you customize it yourself? Anyway stay up the excellent high quality writing, it's rarе to ѕeе а great blog like this one nowadаys.
.
Feel free to viѕit my wеblog: buy ativan
My blog post ativan
Excellent beat ! I wish to apprentice whilst you amend your web
site, how could i subscribe for a weblog web site?
The account helped me a appropriate deal. I had been tiny bit familiar of
this your broadcast offered vibrant clear idea
my blog :: ashlee simpson plastic surgery pictures
Good day! This is my first visit to your blog!
We are a team of volunteers and starting a new initiative in a community in the same niche.
Your blog provided us valuable information to work on. You have done a marvellous job!
Check out my webpage; paid surveys - paidsurveysb.tripod.com,
I enjoy looking through an article that can make men and women think.
Also, many thanks for allowing for me to comment!
my homepage :: quest bars
It's impressive that you are getting ideas from this piece of writing as
well as from our argument made at this place.
Also visit my web site minecraft.net
What's Taking place i'm new to this, I stumbled upon this I've found It positively useful and it has helped me
out loads. I am hoping to contribute & help other users like its
aided me. Good job.
Look into my site: minecraft games
Post a Comment