Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 2, 2012

Ugumu wa kazi ni kuitenda



 Leo nikiwa ndani ya daladala niilisikia watu wakibishana kuhusu idara mbali mbali maofisni, na kila mmoja akiona idara yake ni bora na inafanya kazi nyingi kuliko nyingine, na hata wengine kufikia kusema kuwa kuna  idara nyingine kwenye maofisi hazina  kazi nyingi,lakini ndizo zinalipa. Na nyingine zina kazi nyingi lakini hazilipi,….na wanashauri kutowasomesha watoto wao kwenye hizi nyanja za hizo idara. Nikajikuta nikitabasamu pale nilipokumbuka hadithi ya babu yangu kuhusu punda na mbwa.

Siku mbwa akikutana na punda, wanaishia kukogana na kila mmoja akitamba kuwa ni mbora zaidi ya mwingine, kutokana na kazi wanazozifanya. Mbwa akidai kuwa yeye ni muhimu sana kwa bwana wao, kwa vile kazi anayoifanya ni ya hatarii ya kupambana na wezi, na pia inafanyika usiku ambapo wengi wamelala.

‘Unaona wakati nyie mumelala, mimi napambana na wezi,…kazi yangu ni ngumu na ya hatari, nyie kazi zenu ni laini, mnafanya mchana tena kwa starehe…..’akasema Mbwa akitikisa mkia wake huku akifunua meno yake akihema kwa kujikoga.

‘Kazi yako ni ya kubweka tu, haitumii nguvu, mimi mchana kutwa nabebeshwa mizigo mizito, mizigo ambayo ukibebeshwa wewe utakufa,..huwezi hata kuinuka, ..hebu niambie wewe unaweza kubeba hata ndoo ya maji, ..?’ akauliza Punda.

‘Kama nisipobweka mimi ,nikiona mwizi, huoni hata wewe utakuwa kwenye hatari,….kwahiyo sio kwamba tu kazi yangu ni ya umuhimu, lakini pia nalinda na maisha yako ,nalinda salama wako, inabidi uniheshimu na nipewe maslahi mengi…’akasema Mbwa.

‘Je na mimi nisipobeba hiyo mizigo, na mingine ina chakula chako, wewe utaishi, kazi nyingine zinaingiza pesa, ili bwana akununulie nyama, huoni kuwa mimi najali afya yako?’ akauliza punda.
Mara bwana akatokea, na kumtimua mbwa kuwa aende kwenye kibanda chake kwani kuna wageni ambao wanaogopa Mbwa, na punda naye akaamrishwa aende akabebe mizigo ya wageni….huyo ni bwana hajali wewe ni nani wakati unahitajika kutimiza wajibu wako!

Haya ndiyo maisha ya bwana na wafanyakazi wake, kwa bwana mwenye kuwaajiri hawo `watumishi’ hajali ubora wa mtu, anachojali ni matokea ya kazi yako, jasho lako, na maslahi yake ambayo anahitaji yamletee faida,uwe upo kwenye hatari, au upo kwenye raha, kwake yeye sio muhimu sana, mwisho wa siku anachohiaji na faida yenye maslahi ya kazi yake.

Kisa hiki kikanirudisha kwenye maisha yetu ya maofisini, na sehemu mbali mbali za kazi, ambapo wafanyakazi wengi, kwa kila mmoja kwenye idara yake anajiona ni bora zaidi na kazi yake ina umhimu sana kuliko y mwngine, na hata kudai maslahi zaidi. Na utamkuta mtu akiwa kwenye kazi yake akiwa katingwa na kazi nyingi, utamkuta akilalamika kuwa yeye ana kazi nyingi zaidi ..., na kuona wengine hawana kazi…na anaweza hata kuamrisha kazi zake zichukuliwe kipa umbele…

Ni kweli kuna wengine kazi zao ni zakuongea  tu, na kuongea kwao, ni moja ya mjukumu yao, kuna wengine kazi zao ni kuendesha mitambo, kuna wengine ni makarani, kuna wabunge, kuna walimu na idara zake, kuna mdakitari na idara zake, kuna watu wa usalama na wao wana maidara mengi tu, na akina mama wa majumbani, kuna wafanyakazi wa majumbani, wafanyabisahara, na wengineo, na kila mmoja ana mjukumu yake na mtindo wake wa kufanya kazi....Huwezi ukakosa kazi ya wengine, na kuona hawajui jinsi ya kufanya, kwa vile unataka ifanyike kwa jinsi unavyojua wewe, kwa jinsi ya idara yako inavyofanya....au kwa kudai kuwa idara yako ina kazi nyingi zadi ya nyingine.....

Hii ni hulka ya kukosa hekima, kwani kama mmoja angelikuwa na kazi nyingi zaidi ya mwingine, kusingelikuwa na umuhimu wa idara hizonyingine. Idara hizo zipo kwa ajili ya kurahisisha kazi na kuweza kufikia lengo linalotakiwa kwa mwenyewe, na zina utaratibu wake, na dhima yake kama idara, na ili lengo litimie, kila mmoja ana majukumu yake, utendaji wake, na taratibu zake za kazi.

Itakuwa sio jambo jema na pia ni kukosa hekima pale mmoja anapona wengine hawana maana, wengine hawana kazi, wengine hawajui kazi zao. Ni kukosa hekima, kwani katika mashule na vyuo kuisngelikuwa na umuhimu wa hizo nyanja, …ndio maana watu wanasoma hadi vyuo vikuu kwa ajili ya nyanja fulani, …yote hayo ni majukumu ,na ukumbuke kuwa ubora wa kazi yako ni pale utakapofanikisha lile analolihitajii mwenye nacho, yule aliyekuajiri.

Ni vyema kama ukiwa kwenye idara yako ukathamini kazi za wengine na kuziona ni muhimu kama ilivyo kazi yako, na ni vyema pia kama wewe ni kiongozi wa idara fulani ukathamini kazi za idara nyingie na usiwe mwepesi kuingilia kazi za idara nyingine na kuzikosoa ukaona labda wanavyotenda sivyo ndivyo,…kuna tofauti ya utendaji wa kazi kati ya idara an idara, wengine wana mtindo huu, na wengine wana mtindo mwingine. Hata uvaaji, …lakini yote ni kwa ajili ya kumtumikia muajiri wako.

Ni vyema tukapendana tunapokuwa makazini kwani katika kupendana huko ndiko kutatuwezesha sote kwa pamoja kulisukuma kasia kwa mdundo mmoja, na hata ugumu wa ile kazi  unapungua, na huenda hata tija yenu ikaleta mafanikio, nasema `huenda’ maana siku hizi makazini kuna usemi usemao, kuwahi sikupata, ….na kutenda au… , kuwajibika sio kupata, bali kujulikana na kuonekana kwa bosi ndio kupata na hili ni makosa wanalolifanya waajiri wengi…..

Tukumbuke kuwa sote tuwaajiriwa, na umuhimu wetu hauna maana kwa mwajiri,i zaidi ya kuweza kutimiza malengo yake,..kwake yeye cha muhimu kutoka kwako ni uzalishaji wako, ni uwajibikaji wako, ni nguvu kazi yako…ili apate mslahi yake yenye faida.

Ni waulize wenzangu,  nyie mkinyosheana vidole, mtanufaika na nini, kuwa muonekane bora kwa bwana, ...kama lengo ni hilo, litakuwa ni la muda mfupi tu, ....tunachokifanya hapo ni kuzalisha mfarakano, ambao utaleta kuyumbishwa kwa mtumbwi, na nini matokeo yake, kama sio kuzama, ukizama wengine wapo, watakuja kuutumikia huo mtumbwi…mtumbwa wa bwana, ambaye ni muajiri wako.

Na hapo nikacheka nikikumbuka hadithi ya Mbwa na Punda, sote ni sawa na Mbwa na punda kwa bwana …..thamani yetu ni ule mkataba wa ajira, ukikatika huna maana tena. Tuwajibike, tupendane, tusaidianeni,ili mwisho wa siku bwana atuone ni waoja na moja ya familia yake.

Ujumbe wa leo,…Ubora, urahisi na ugumu wa kazi ni kuitenda,….

NB. Bado naweka sawa sehemu yetu muhimu ya kisa chetu cha `hujafa hujaumbika….ni sehemu muhimu sana, ambayo itakujuza nini kilichokuwa kimejificha, ni kisa chenye mafundisho maonyo, na mtizamo ndani ya ndoa, na maisha kwa ujumla,…ya leo sio ya kesho, yanatokea mengi , nay a ajabu, kwani hujafa hujaumbika.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Kweli mkuu ujumbe umekaa sawa, wamesikia hata wakila jiwe