Aliendelea kuongea nesi....
*****
‘Niliogopa, ….yaani nilihisi mwili mzima ukiniisha nguvu ,
kwanza akili haikuamini kwa haraka kuwa ni yeye, pili nilikuwa nikijiuliza kwanini
afanye jambo kama hilo, maana mimi nilijua kama ni mbaya wake ambaye angeliamua
kumfanyia hivyo, angelikuwa baba yake, aliyembaka, …..
Akili ya haraaka ilikuwa jinsi gani ya kumsaidia huyu dada,
nilichofanya nikwenda pale ilipokuwa ile silaha, na kuiweka kwenye mfuko wake,
na mawazoni mwangu, ilikuwa niichukue, nikatafute sehemu ya kuificha, kama sio
kuipoteza kabisa…ikibidi nikaitumbukize baharini.
Kuna kitu kimoja nimejifunza , silaha iliyofanyia mauaji
inakuwa kama imenasa damu ya mtu, na ile damu inailinda ile silaha, maana mimi
nilijua ni kazi rahisi, tu,nitaichukua ile silaha, na njia nitakuwa na muda wa
kuiifua alama za vidole,maana huyu mwanadada, hakuwa amevaa chochote mikononi,
tofauti na wale akina dada wawili, wao walijua nini wanakifanya.
‘Na wewe ulikuwa umevaa chochote mikononi, maana hatukuona
alama zako za vidole?’ akauliza wakili mwanadada.
‘Hilo sio swala la kuniuliza mtu kama mimi,
professional..mimi ni askari, najua nini ninachokifanya, ….nisingeliweza kwenda
sehemu kama hizo nikiwa na mikono mitupu, najua nini kitatokea abadaye,sifanyi
makosa kama hayo…’akasema.
‘Je huenda huyo mwanadada alikuja kuikamata hiyo silaha
baadaye kwa mipango yako, ili ionekane kuwa ndiye kaishika…’akasema wakili
mwanadada.
‘Hayo ni mawazo duni,..kama hujafuatilia vyema, nenda
kafuatilie tena, kama unahitaji zaidi nenda kaanzie kwa huyo aliyemuazima hiyo
pikipiki ,nenda hadi kule alipoiweka, kuna watu walimuona,…na hata wakati
anatoka kuna watu wawili waliweka gari lao, walikuwa wamesimama nje ya gari
lao, wakishangaa nini kimetoeka kule kwa Kimwana, waligeuka kumwangali huyo
mwanadada wakati anatoka pale na kupanda pikipiki…
‘Kwanini wao hawakuiarifu polisi kuwa wameona mtu kama
huyo?’ akauliza.
‘Hilo swali ungeliwauliza wao, na najua nini unachofikiria,
kuwa labda niliwaweka mimi, ili waje kuwa mashahidi wa kuonyesha kuwa walimuona
huyo binti…nakuambia ukweli hivyo ndivyo ilivyokuwa,…amini , usiamini, ..na
hata hivyo, mimi sijali,nipo tayari kwa lolote lile ilimradi niweze kusaidia …’akasema .
‘Haya endelea na maelezo yako, maana hujamaliza,…..’akasema
wakili mwanadada.
‘Hata nikiendelea anona kama huniamini, lakini sio mbaya,
amini usiamini, nitakuambia tu ilivyokuwa, …’akasema na kutulia kwanza kwa
muda, kama vile anawaza jambo.
‘Kwenye hiyo barua yeye alikuandikia nini…maana
unavyonibishia nahisi huenda kakuandikia tofauti na maelezo yangu,…?’
akaniuliza.
‘Haya aliyoniandikia yananihusu mimi,na siwezi kukuambia kwa
sasa, ninachotaka ni kuhakikisha kuwa maeelzo yako yapo sawa na alichoandika
yeye, …..au umeshaanza kujishitukia?’ akauliza wakili mwanadada.
‘Kwanini nijishitukiea wakati ninayokuelezea ndivyo
ilivyokuwa,….sina wasiwasi na hilo, kwasababu nimejiandaa kwa vyovyote vile,
mimi nilishakuw atayari kubeba yote, na hata wakati nakunywa sumu, nilitaka niondoke,
nikiwa najulikana kuwa mimi ndiye niliyemuua Kimwana, ….lakini naona
haikufanikiwa, hata hivyo, kama tutakuabliana nipo tayari kukubali kuwa mimi
ndiye niliyehusika, laini kawaida yangu, huwa sikubali moja kwa moja, hiyo ni
kazi ya usalama kuthibitisha…
‘Makubaliano gani hayo unayotaka tuyafanye mimi na wewe?’
akauiza wakili mwanadada.
‘Uiharibu hiyo barua, na usiseme lolote…..mambo yaishe kimiya kimiya, mimi
nitakwenda kukitumikia kifungo, kama ni cha maisha hewala, kama ni kunyongwa,
hewala,…nipo tayari…’akasema.
‘Kwanini uwe tayari kubeba makosa ya mtu mwingine, ilihali
wewe mwenyewe unajua kuwa hilo ni kosa, sio kwamba wewe unajiona kabisa ni
mkosaji mkuu, kwa kumrubuni binti wa watu, asiye na hatia, kiujanja,ili mwisho
wa siku afanye lileulilotaka kulifanya wewe,…au hujui kuwa tumehsligundua
hilo,..ama usingelikuwa wewe huenda huyo unayemuona anakosa asingelifanya hilo
kosa….kama kweli alifanya yeye….’akasema wakili mwanadada.
‘Hebu nikuulize swali moja, kwanini wewe unaniona kuwa mimi
ni mkosaji,..tangu mwanzo nakuona huniamini na hunipendi, kwa kauli zako na
maswali yako, nimekukosea nini mpendwa…mimi ninajaribu kukuambia ukweli wewe
unaniona na kudanganya..kwanini lakini..?’ akauliza.
‘Ina maana huoni kosa lako toka mwanzo,wewe unaona makosa ya
wenzako, ya wengine huyaoni, hebu nikuulize, kama nisingeliinama siku ile, mimi
sasa hivi ningelikuwa nani….?’ Akauliza wakili mwanadada.
‘Ungelikuwa maiti….hiyo ni vita, huwezi kunilaumu kwa hilo,
pale sote tulikuwa kazini, tifauti yetu ni kuwa mimi nilikuwa upande wa maadui,
na wewe upande wa serikali….lakini lengo letu lilikuwa ni moja kuwa tupo
vitani, huwezi kunilaumu kwa hilo, cha muhimu ni sheri ikufuata mkondo
wake,….’akasema kwa kujiamini.
‘Na kweli itafuta mkondo wake,…hilo nauhakikishia…na huo
mkono wako, uliofunga plaster ulifanya nini…?’akasema wakili mwanadada na
kuuliza swali kwa kiujanja.
‘Hili sio siri, niliumwa na nyoka…..’akasema.
‘Uliumiwawapi na yoka..?’akaulizwa.
‘Niliumwa siku ile wakati naificha hiyo silaha, kwenye
kabati pale kwa nyumbani kwa wakili mkuu…’akasema
‘Siku ile wakati unaificha huyu binti alikuwa wapi?’
akaulizwa.
‘Mimi sijui maana nilifika pale na kukuta hakuna mtu…na
wakati nahangaika kutafuta sehemu ili nikafute hizo alamaza vidole, nikasikia
mtu akija ,nami kwa haraka nikaificha hiyo silaha kwenye hilo kabati, kumbe
kulikuwa na nyoka…akaniuma…’akasema.
‘Wewe unajifanya mjanja sana, uumwena yoka, na uwe na
ujasiri wakufanya hicho ulichokifanya…ile silaha kama ilivyo, na jinsi
ilivyokuwa humo ndani,ingeliweza kuufungua ule mlango,…haingelichukua muda,
ilesilaha ingelidondoka,….’akasema wakili mwanadada.
‘Una maana gani kusema hivyo?’akauliza nesi kwa kushangaa.
‘Nina maana kuwa huyo nyoka pale ulimweka wewe, …na slikuwa
sio nyoka wakweli, ni nyoka bandia, ni plastic, ambayo kama kweli huijui
utasema kuwa ni nyoka, ….uliitupa kwenye jalala, siku ile ulipoona haina kai
tena,…lakini tulikuja kuipata, na ukumbuke wakati unaituoa ulikuwa umeshavua
soksi za mikono, na hapi tukazipata alama zako zamikono….utabisha nini hapo…’akasema
wakili mwanadada,
‘Sasa unataka kusema nini hapo kuwa mimi ndio ….?’ Akauliza
nesi nakukatisha kile alichotaka kusema.
‘Ile silaha uliiweka vile ,pale kimakusudi, ule mlango ulifunguka kwa sababu ya uzito wa ile
silaha, ikatokeza nje, yote hiyo uliipanga mapema, ili huyo binti aione, aishike na aache alama
za vidole kwenye hiyo silaha…..na kweli huyo binti alipoiona wakati anafanya
usafi, aliogopa sana, akijua lolote atakaloongea kwa baba au mama yake
hataeleweka, akairudishia pale kwenye kabati na kuiweka vizuri,ili kama ni baba
yake kaiweka, aje aikute mwenyewe, hakutaka kusema lolote kuhusu kuiona hiyo
silaha hapo....’akasema wakili mwanadada.
‘Hivi wewe unafikiri haya yote ninayokuambia nimeyatunga
kichwani mwangu,…hiyo barua ilisema nini, maana ndiyo msema kweli?’ akauliza
nesi.
‘Hiyo barua uliindika wewe…..na ulichofanya ni kubadili
barua aliyoiandikia huyo binti ya kweli, ambayo uliichana, lakini hukuichana
ipasavyo, tumeiunganisha vipande vyake…na kuona nini alichokuwa kakiandika huyo
binti, ….wewe ulijua ni nini ataandika kwani ulishaongea naye, ukaongezea hayo
yakeo mengine uliyabuni wewe,….’akasema wakili mwanadada, na nesi akacheka kwa
dharau.
‘Na huo mwandiko wake je….maana uwongo wako hauna
maana…’akasema.
‘Wewe unajua kugushi saini za watu, sembuse ushindwe kubuni
mwandiko wa mtu…kwenye kundi unajulikana kwa kuigiza matendo, hadi
kuandika….uliigiza mwandiko wa huyo binti, na ipo siku ulimwanikia kitu
akashangaa na kujiuliza umejuaje kuandika mwandiko wake,..au unajfanya
hukumbuki hilo…’akasema wakili mwanadada.
‘Hivi nani atakuamini hilo, mimi nimelazwa hapa, ni nani
aliipeleka hiyo barua huko nyumbani kwa wakili mkuu….?’ Akauliza kwa mshangao.
‘Ni docta, …aliyeipeleka ni docta, bosi wako, yeye kwa
kutokuwa makini, alishindwa kuvaa kinga za mikononi, alama zake zimeonekana juu
ya bahasha…na vipande vile alivyochana zipo alama zake…’akasema wakili
mwanadada.
‘Wewe ulistahili kuwa mwandishi mzuri wa riwaya, hivi unajua
nini unachokisema…hapo unatunga kitabu cha riwaya ya uwongo…nani ataamini huo
uwongo wako….’akasema nesi huku akikunja uso kama anawaza jambo. Wakili mwanadada akaendelea kuongea na
kusema;
‘Na yote kuhusu kuwa umeambukizwa ukimwi na, wakili mkuu, ni ujanja wa kiini macho ili
jamii ikuonee huruma. Huna ukimwi, wala wakili mkuu hana ukimwi, yote hayo yameshagundulikana….kwani
wakili mkuu keshapimwa na kugundulika kuwa hana huo ukimwi, na tulipogundua
hilo, tulikwenda kuangalia kumbukumbu za afya ya Kimwana, tukagundua karatasi
mliloligushi wewe na dakitari wako, kuwa Kimwana ana ukimwi, lakini sio
kweli,hakuwa nao…..’akasema wakili mwanadada.
‘Eti nini…?’akasema kwa kushangaa.
‘Cheti ulichosema ulikikuta kwa Kimwana, ulikigushi wewe,
….kwa kumtumia huyo huyo docta wako, ambaye imegundulikana kuwa mlikuwa kundi
moja…yote hayo yameshagundulikana….’akasema wakili mwanadada.
‘Eeeh, tatizolako hunijui, hayo yanaweza yakakugeukia, na
ninaweza kufungu amshitaka juu yako kwa kunipakazia uwongo, …hunijui mimi wewe,
lakini ya nini, mimi sijali amini uaminivyo, ilimradi najua sio kweli kwanini
nijali…’akasema huku akikunja uso kwa hasira.
‘Siku ile ulipofika na silaha kule hospitalini, ulitoka naye
kwenye gari , ukiwa umejificha nyuma na silaha yako, walinzi hawakuwa na sababu
ya kulikagua hilo gari lake….na ndio maana hawakukuona ukitoka,….ulisahau
kuondoka na kofia lako la manyoyanyoya, na hili lilikua kuonekana na nesi
msaidizi wako,nikuuliza hilo kofia lilifikaje huko kwenye nguo zako?.’akasema
wakili mwanadada.
‘Hivi wewe unajifanya kuwa hunielewi, au ni mbinu zako za
kunipakazia..hata hivyo mimi nimeshasema sijali, nipo tayari kuhukumiwa kwa
hayo, lakini nafanya hayo kwa ajili ya kumlinda huyo binti…hilo kofia silijui
mimi…na kofia kama hizo zipo nyingi,hukumbuki nilikuambai kuwa mimi nilikuwa na
makofia mengi kwa ajili ya kujificha nikifanya mambo yangu…’akasema.
‘Kama hayo ya kufanya uhalifu na kuwasingizia watu wasio na
hatia….’akasema wakili mwanadada.
‘Huyo binti kama anglikuwepo angelisema yote angelikiri
mbele yako kuwa yeye ndiye aliyeua, na mimi nimjitolea kumlinda,….kwa hali yoyote…’akasema
huyo nesi.
‘Kumlinda au kumtumia kama kinga yako….wewe ulimuhadaa, ili
aondoke hapa jijini,ili uwongo wako ufanye kazi, ….lakini hujui kuwa njia ya
muongo ni fupi…na za mwizi ni arubaini, ujanja wako wote umefikia ukingoni…..’akasema
wakili mwanadada.
‘Kama unakana maelezo yangu kwanini huendi kumuuliza yule
kijana muendesha pikipiki….kuwa kweli alimuazima huyo binti pikipiki, sasa
jiulize huyo binti alikwenda wapi, na alikwenda kufaya nini….’akasema.
‘Ni kweli kuwa huyo binti alikwenda kuazima pikipiki kwa
huyo kijana, na huyo binti alifanya hivyo, baada yaw ewe kumpigia simu ukiigiza
kuwa wewe ni mke wa wakili mkuu, unamuita huyo binti aje huko Mbezi,….’akasema
wakili mwanadada, na nesi akainama kidogo kufichs hisia zake, halafu
akamwangalia wakili mwanadada akiwa na uso wake ule wa ujasiri, huku
akitabasamu kwa dharau.
‘Unatunga hadithi, sio, endelea kutunga hadithi
yako….’akasema.
‘Huyo binti akijua kuwa kapigiwa simu na mama yake,
alikwenda kwa huyo mchumba wake akaazima pikipiki, na kweli alifika huko….wewe
ukavua ile kofia uliyokuwa nayo mwanzoni, ukavaa kofia hiyo ya manyoyanyoya,
ambayo ulisema alikuwa kaivaa huyo binti,ukafanya hayo uliyayasema kuwa
aliyafanya huyo binti, ulipomaliza….kwa haraka ukashuka chini kwenye lile jengo,
ukampiga simu kwa huyo binti kuwa arudi tu nyumbani….’akasema wakili mwanadada.
`Huo ni uwongo nambari moja, wewe unalako jambo…haya
tuyahakikishe hayo mahakamani kama unataka kushindana na mimi,lakini sina muda
huo…mimi nimeshasema nipo tayari kwa lolote lile…kwa ajili ya huyo
binti…kumlinda…’akasema na kutulia huku akiangalia chini.
‘Tatizo lako, unafikiri sote tumefumba macho na msikio, kuwa
akili zetu haizifanyi kazi,…hii kazi sikuianza leo, na ninajua nini
ninachokifanya, yote ninayokuambia yana ushahidi…na mwisho wako umefikia
ukingoni, nilikupa muda wa kujikosha, ukajifanya wewe mjanja, sasa nimeona
nikufunulie ukweli anagaliu kidogo tu, ili ujue kuwa najua kila kitu…..na mengi
yatafuta…’akasema wakili mwanadada.
‘Hiyo ndiyo kauli naitaka kuisikia,mimii sitaki mtu wa kunionea huruma mimi, ili iweje,…mimi
nilishajiandaa kwa hili, najua mwisho wa yote haya ni nini,nilijua kabisa kuwa
nitakuja kukamatwa, na huenda nikanyongwa,
lakini lengo na mdhumuni yangu ..ni
hayo niliyokuelezea, kumlinda huyo binti,..najua wengi watazungumza mengi, …., lakini
ni kwa vile hawanijui dhamira yangu ya
kweli,..mimi sio mnyama kama unavyodhania wewe…mimi nina huruma zaidi yako
wewe…’akasema kwa macho yaliyojaa ukali.
‘Huruma gani hiyo ya kuua watu,kuwachonganisha watu ndani ya
ndoa zao,, kuwa-blackamail…Hiyo ndiyo
unayoiita huruma, na ikizingatia kuwa wewe uliwahi kuwa mtu wa usalama,
unatumia ujuzi ulioupata kutokana na jasho la wanyonge, kodi yao ilikusomesha,
na sasa unakuja kuwatende sivyo ndivyo..’akasema wakili mwanadada.
Yule nesi akacheka kwa dharau…na kuangalia chini, na baadaye
akasema;
‘Hivi huruma yangu na ya kwako unaweza
ukailinganisha,…’akasema wakili mwanadada.
‘Kama wewe una huruma kweli, fanya hilo nililokuambia,
hakikisha kuwa unaiharibu hiyo barua, na hakikisha kuwa haijulikani kabisa kuwa
huyo ….’kabla hajamaliza mlango ukagongwa, na mara akaingia dakitari, akiwa na
mkuu….
‘Natumai mumeongea vya kutosha….’akasema docta.
‘Na yote tuliyoyataka tumeyapata, ….’akasema mkuu.
‘Yote yapi…’akauliza wakili mwanadada akionyesha mshangao,
na nesi akamwangalia wakili mwanadada kwa jicho la hasira, akizania huenda yeye
ndiye aliyepanga hayo yote, akasema neno moja.
‘Ina maana….’kabla hajasema zaidi mkuu akasema;
‘Mimi sio mjinga, sisi tulichofanya ni kuwasiliana na
wenzetu, ambao wanamjua vyema huyu binti, tuliambiwa yote, na kwanini
walimsimamisha kazi huko,kwenye idara ya usalama. Haya mambo hakuyaanzia
hapa,huko ndio ilikuwa kazi yake kubwa. Alipoona kuwa hana nafasi tena ya
kufanya machafu yake huko, ikiwemo kublackmail, …..akaona akimbilie huku kwa
visingizio vya kusalitiwa kwenye penzi.
‘Wakili mkuu hakujua kuwa alikuwa kitumiwa kama ngao,..ndio
huenda kulikuwa na kupnedana ndani yake, lakini mwenzetu alikuwa akitumia huo
mwanya kwa kutimiza malengo yake. Yote hayo tuliyajua, na tulikuwa tukisubiri
wakati muafaka. Na wakati muafaka umefikia, …..’akasema mkuu.
Wakili mwanadada akasogea nyuma na kumuachia mkuu apite
mbele yake, karibu na kitanda alicholala nesi,na nesi alikuwa akijaribu kuficha
uwoga wake, akaangalia kwa yale macho yake ya dharau…
‘Mimi na idara ynagu tulishajua kuna kitu kinaendelea,
tulishajua kuwa wewe wakili mwanadada unajua mengi, lakini hukutaka kuyaweka
wazi mapema kwa mtindo wako wa huruma,…tulikupa muda , ili tuone, jinsi gani
utakvyowahurumia hawa watu, lakini tumeona hiyo njia yako haiwezi kusaidia,
tukaona bila kukuwahi unaweza hata ukaficha ukweli mwingie kwa kuwaonea hawa
watu huruma, …’akasema na kusogelea pale kitandani, akafunua godoro nakutoa
kifaa kidogo, halafu aksema;
‘Hapa kitandani tumeweka chombo cha kunasia sauti,na ukiangalai
pale juu kuna kifaa kingine kinachukua picha, na matukio humu ndani, hii ni kuhakikisha
kuwa kila kitu tulichokihitaji kwa ajili ya kuhitimisha uchunguzi wetu kinapatikana,
yote mliyokuwa mkiongea tumeyasikia,na kwa vile tunajua kuwa huyu jasusi wa
kimataifa, tulichukua tahadhari zote, asije akapotea. ….’akasema mkuu.
‘Ni nani aliyekuambia kuwa sikutaka kuyaweka haya wazi, ni
mambo gani unayosema nayataka kuyaficha mkuu, mbona unaniingilia wakati
nilikuwa nataka kupata kila kitu kwa uwazi….?’ Akasema wakili mwanadada,
akionyesha kutokufurahishwa kwa tukio hilo la mkuu.
‘Hisia zangu zimenituma hivyo….nilishafuatilia yote, huyo
kijana mchumba wa huyo binti nilishaongea naye, nimekwenda hadi huko juu,
Mbezi,nimeongea na wote waliokuwepo hapo,….najua kila kitu..lakini nilikuwa
nasubiri nijue nini mwisho wa yote haya, najua mbinu zako, na huruma yako,
najua nini kitakachofuatia baada ya hapo na tuna mjua huyu nesi, na tumekuwa
tukimfuatilia kwa karibu sana, na kwanini alifukuzwa kwenye kazi yake ya
usalama….’akasema mkuu.
‘Sijakuelewa mkuu, maana naona sasa unaanza kunigeuka,
nilijua unanifahamu taratibu zangu zakuyamaliza haya, ili mwisho wa siku kila
mtu ajutie kosa lake, akiri mwenyewe..mimi sivyo kama unavyonizania,kuwa labda nataak
kuwaficha hawa wahalifu kinamna ….na kwanini useme kuwa unajua mbinu zangu, na
huruma zangu, …?’ akauliza wakili mwanadada akiwa katahayari.
‘Samahani sana ,kwa kuwa nimekuingilia katika taratibu zako
za kikazi,…,lakini mimi kama mtu wa usalama ninapohakikisha kuwa mkosaji
kapatikana na ushahidi upo wa kutosha, natakiwa nilipeleke hili swala
mahakamani,wao watajua nini cha kufanya, hatuwezi tukayapeleka unavyotaka wewe,
hatuwezi kuwabembeleza hawa wahalifu tena maana tumegundua mengi mabaya ambayo
yangelifuatia, ….haiwezekanitukasubiri zaidi..huyu mtu sivyo kama unavyomzania,
ni jasusi kweli….’akasema mkuu.
‘Kwahiyo sasa unataka kusemaje, maana umenivurugia utaratibu
wangu….?’ Akauliza wakili mwanadada.
‘Muhalifu wetu ndio huyu hapa, na tunashukuru kuwa shahidi
muhimu ambaye alitakiwa kupotea na hata ikibidi auliwe, akifika huko kijijini,
sasa tunaye ….….’akasema mkuu na kumbonyeza mwenzake ambaye alikwenda akafungua
mlango, ….
Mara akaingia yule
binti wa kufikia wa wakili mwanadada, wakili mwanadada hakuonyesha kushangaa sana,
ingawaje moyoni, alijiuliza ni kwa vipi walimuwahi huyu binti, kwani yeye
alikuwa na uhakika kuwa keshaondoka kwenda huko kijijini, …kumbe ilikuwa mbinu
ya nesi, ili huyo binti akifika huko kijijini, amaliziwe huko huko…..Yule binti
akaingia, na kusimama mlangoni, akasita na kuonyesha uso wa uwoga, akatizama
kule kitandani…
Nesi ambaye alikuwa kashikwa na butwa, na hasa lipomuona
yule binti, akatoa macho kwa woga akasema `Ssshiti…hawa watu wamefanya nini….’
na mara , akabadilika sura kwa hasira, akataka kusimama pale kitandani, lakini
akasita, akamwangalia yule binti huku akiwa kakunja uso,…Yule binti akamsogelea
pale kitandani, na kusimama karibu na kitanda, akamwangalia kwa uso wa mashaka,
akamgeukia wakili mwanadada , halafu akamwangalia tena yule nesi, akasema;
‘Kweli mimi siamini,….ina maana hata wewe dada yangu
niliyekuamini, unanifanyia hivyo, ina maana hukuwa unanionea huruma, kumbe
ulikuwa na lako jambo, ulikuwa ukinifundisha kutumia bunduki, ili mwisho wa
siku, nionakane nimeua kwa bunduki,…yaani jamani kumbe upo hivyo, umeamua
kunisingizia mauaji, hata mimi…’akawa anatoa machozi akimwangalia nesi.
‘Sikuwa na nia mbaya na wewe kabisa, ipo siku
utanielewa….lakini kwa leo wafuate hawo watu wako unaowaoana wa maana,….mimi
nilikuwa na kusaidia tu….’akasema huku akimkwepa kumwagalia yule msichana
machoni.
‘Siwezi kukuamini tena, kunisaidia mimi kwa kunisingizia
kuua,….unanisingizia mimi kuua..hapana wewe siomtu mwema,…, hata kama nilikuwa
namchukia vipi yule dada nisingelikimbilia kumuua, kwanini nimuue binadamu
mwenzangu….jamani toka lini mimi nikaweza kuua mtu, ….’akawageukia wakili
mwanadada na mkuu, na wao wakawa wanamuangalia tu.
‘Wewe…hukumbuki uliniambia kuwa ukipata silaha utamuua huyo
dada, lao hii unanikana ..’akasema nesi.
‘Nilisema tu kwa hasira, lakini sikufanya hivyo, na
nisingeliweza kufanya hivyo..mimi kule nilipigiwa simu na mama kuwa niende huko
alipo, na mara nikapigiwa simu tena nirudi…sikujua nini kinaendelea, kumbe ..ni
wewe uliyafanya yote hayo…siamini….’akasema huku akilia.
‘Usiwasikilize hawo hawana lolote, …’akasema nesi huku
akionyesha wazi kuwa keshashindwa, akajaribu kujifunika uso na lile shuka,
lakini hakuweza, akawa kama kamwagiwa maji. Yule binti akamwangalia halafu
akasema;
‘Hivi hii dunia nimeikosea
nini, ina maana kuzaliwa masikini ndio kosa, …nawashukuru sana, nyie
mlionifanyia hivi….sina cha kuwafanya, kwanza nitawafanya nini mimi kiumbe
zaifu, na huenda hata nitakaloongea halitasikilizwa, ila mungu wangu ni
shahidi, …mimi hata siku moja sijawazia kumuua mtu….kama nilitamka neno kama
hilo ilikuwa ni hasira tu, kwa vilenilijua hata mimi nimeambukizwa huo ukimwi
kutokana nay eye……’akageuka na kumwangalia wakili mwanadada,ambaye alikuwa
akimwangalia kwa uso wa huzuni.
‘Eti dada mpendwa, kuna siku niliwahi kukuambia kuwa nataka
kumuua huyo dada marehemu…?’ akauliza huku machozi yakitoka, na wakili
mwanadada akawa kimiya .
‘Najua wewe peke yako ndiye utakayeniamini maneno yangu, wewe
peke yako ndio ndugu yangu wa kweli, mungu atakuzidishia …..hawa maaskari
wananikamata eti ….’akageuka kumwangalia mkuu, na akataka kusemakitu, lakini
akawa kama anaogopa, akageuka na kumwangalia nesi ambaye alikuwa katulia
kionyesha hasira za wazi wasi usoni.
Mkuu akasema, ‘Usiwe na shaka binti, ukweli umshadhihiri, na
kwa taarifa ni kuwa wahalifu wote wa hilo kundu, akiwemo, Sokoti, na wengi
ambao walipandikizwa, kila mahali, mahospitalini na maofisni wote wameshakamatwa,
na wote wanatakiwa wakasimame mahakamani, na sheria ndiyo itawahukumu, kama
kuna msahamaha, hilo litajulikana mbele ya sheria, na sio kwa njia hii….’akasema
mkuu akimwangalia wakili mwanadada.
‘Sawa kwani mimi nimekataa, …ilimradi kila kitu kipo wazi,
na wahusika wenyewe tuliwapa muda wa kujitetea lakini wamejitia wanajua zaidi ,
mimi nimenyosha mikono, ila huyu binti wa watu anahitaji ushauri nasaha, ili
asijisikie vibaya, …ni vyema hili likafanyoka mapema, kwani alishahamanika na
kuzania kuwa kweli kaambukizwa,…’akasema wakili mwanadada.
‘Ndio, niliskia kwa masikio yangu, sizani kama mama anaweza kudanganya….na,
hata huyu dada alinishauri niende kijijini …kuna hisia zilinijia kuwa huko
nitapona,…na yeye kanishauri kuwa kweli nitaponyeshwa kwa dawa za asili…eti
kweli jamani ina maana mimi ndio basi tena usichana wangu umekwisha sitaolewa,
tena, maana mchumba wangu akisikia kuwa…..’akatulia na wakili mwanadada
akamshika mkono na kumwambia.
‘Usiwe na shaka mpendwa, wewe hujaumbukizwa ugonjwa, na ili
uwe na uhakika twende ukapime, leo hii lazima ukapime, ili uondokane na hizo
zana potofu, huyu dada yako alidanganya watu, hata huyo Kimwana mwenyewe hakuwa
na huo ugonjwa,..usijali yote utayasikia mahakamani…’akasema wakili mwanadada,
na huyo binti akabakia kushangaa.
‘Ina maana kweli..sina ukimwi, ina maana kweli hata baba
hana ukimwi,…ooh, …asante mungu,…’akanyosha mikono juu na kushukuru.
‘Sasa natumai umeshamuelewa dada yako alivyo, yeye alitumia
udhaifu wa watu ili kufanikisha malengo yake, lakini sasa uwongo wake
umegundulika,….kwahiyo wakili mwanadada
kuanzia sasa, ngoja sheria ichukua mkonod wake,….’akasema mkuu.
‘Kama hivyo ndivyo utakavyo, mimi sina zaidi, njia yangu
ilikuwa na nia njema, ili kuwafanya watu wajijue, na wakiri makosa
yao,…’akasema wakili mwanadada.
‘Hiyi njia yako hapana, haifai kwa watu kama hawa
walikubuhu, hawa ni wahalifu sugu, watatumia kila upenyo kufuta madhambi yao,
bora kuwawahi ili wakatumikie vifungo vyao, kabla hawajaiharibu jamii yetu, je
ulijua huyu mtu, nesi, na pia alikuwa mtu wa usalama, wewe ungelijua kuwa mtu
kama huyu angelidiriki kumpandikizia binti
mnyonge kama huyu madhambi ya uuaji, na kuwapandikizia watu wangine magonjwa
yasiyokuwepo, na wangi wao kuathirika kisaikolojia na hata kupoteza maisha kwa
mshituko…..inasikitisha, sana….’akasema mkuu.
Nesi akawaangalia kwa makini, halafu akamwangalia yule binti
akainuka pale kitandani, na nywele zale zilikuwa zimetawanyika kichwani,
akashika kichwa kuanza kuongea kwa uchungu, akasema;
‘Samahani sana binti, wewe hukujua lengo langu,
nisingekutosa, ni katika mbinu za ushindani tu, na ujue kabisa…hayo yote
hutokea unapokuwa kwenye uwanja wa vita, inabidi utumie kila njia ili ufanikiwe
malengo yako, najua hakuna atakaye nielewa kwa sasa, …ninachoweza kukuomba kwa
sasa ni msahama na hasa kwa ambao hawatanielewa, na wataona nimewakosea,….'akasema kwa uchungu, na kabla mtu mwingine hajasema lolote akaongezea kwa kusema.
'Ila
yote haya niliyawafanya kwa ni njema ya kupambana na watu wasiotosheka, na nisingeliweza kufanya bure, kwani natangaza, dini, ...haiwezekani hawa watu wachume, sisi tuumie, wanaju ni matatizo gani niliyopata waliponifukuza kazi,....hiyo hela waliyoichuma kwa dhuluma, na sisi tumeichukua kwa mtindo huo, .na hata hivyo ni kweli nilimpenda wakili mkuu, na yeye ilibidi atumike, Ili kumkomoa, kwa tamaa yake ya kiwmili..na kwa kunisaliti,...najua hamtanielewa hata nikiwaambia nini, lakini ukweli ndio huo…’akasema na pale pale akashika kichwa na kuanza kulia….na
kwa mara ya kwanza huyu mwanadada lionekana akiwa analia kwa hisia. Ile dharau
na ujasiri ukatoweka….!
Mkuu akamwangalia kwa macho ya ukali, halafu akageuka na
kumwangalia wakili mwanadada,akasema;
‘Hata hivyo,nashukuru sana kwa kazi yako nzuri, bila wewe
tusingeliweza kugundua mengi,…..na sasa upo huru kuwatetea watu wako
mahakamani…natumai watakuwa wanakuhitaji sana..ila huyu mtu wetu hastahili
kubakia hapa inabidi tuondoke naye akalazwe hospitali zetu zenye ulinzi wa
kutosha,….’akasema mkuu, na mara wakaingia ma-askari wengine, ambao walimwamrisha
nesi atoke pale kitandani, na wakamshia mikono huku na huku na kutoka naye nje.
Wakili mwanadada akamshika yule binti mkono na kumwambia;
‘Tunakwenda kwangu , wewe utaishi na mimi ,toka sasa wewe ni
mdogo wangu.
‘Ahsante wewe kweli ni ndugu wa kweli…sitakusahau katika
maisha yangu.
NB: Hapa sio mwisho, kuna sehemu ya mwisho ambayo itatoa
ufafanuzi hasa kwanini KImwana aliuwawa, tuungane na wakili mwanadada kwenye
sehemu hiyo muhimu, tukijaliwa tena. Na pia tutajua nini hatima ya Msoma na
Tausi, na ndoa ya wakili mwanadada. Na kama kuna sehemu yoyote nimejichanganya
naomba wale mliofuatilia hiki kisa mnifahamishe ,maana ni kisa kirefu naweza
nikachangaya.
WAZO LA LEO: Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime, maana ogomvi
wa familia sio wa kukingia kifua, na kulalia upande mmoja, unachotakiwa ni
kuwapatanisha, kwani ukijifanya kulalia upande mmoja,wakija kupatana utaonekana
wewe ndiye chanzo.
Ni mimi:
emu-three
12 comments :
I see! naona kama naangalia bonge la movie. hongera sana, kwakweli sikutegemea ingekuwa hivi. unaonaje ukiuza hizi stori zitengenezewe movie? na wazo la kutoa vitabu limeishia wapi ndugu?
bomba sana mwanawane...nakumbuka ndani ya kisa hiki Msomali alipigiwa simu kwenda Sinza kwenye nyumba moja hivi lakini akakuta mdada kajeruhiwa na kupelekwa hospitali.
sijaona (labda macho yangu yana kengeza) mahali ktk simulizi ameelezewa yeye ni nani, anahusikaje, na alomtungua! Na kama alikufa ama la!
M3,
Nakumbuka wakati fulani ndani ya kisa hiki Msomali alipigiwa simu kwenda kwenye nyumba moja huko Sinza akakutana na kisa cha mdada mmoja kupigwa risasi na kukimbizwa hospitali.
Sijaona (labda nina kengeza) mahali kuhusu huyo mdada ni nani, anahusikaje na sakata hilo, kama alipona, na nani muhusika wa kumtungua na kwa nini!
Ni kweli,labda nije kuelezea baadaye ilikuwaje , lakini zote hizo
zilikuwa mbinu za kiujanja za kundi, ...walikuwepo watu walioweza
kuigiza mtu, matendo, na kuonekana kama muhusika fulani...tutaielezea
hiyo kwenye sehemu ijayo!
Ama kuhusu kitabu/vitabu na movie hilo ni moja ya malengo yangu. Lakini mambo bado magumu, maana mtegemea cha ndugu,au cha mtu ni mavi.
Jembe linalonisaidia ni la ofisi, muda hautoshi, ukiwa ofisini, na cafe nako ni gharama,...lakini bado tuna nia hiyo!
Mimi sijajua kwanini hutumii majina,na kutumia mdada, mke wa,huoni hiyo inachanganya zaidi?
MSINIONE NIPO KIMIYA, JEMBE LINAKOROFISHA, NA KAMA WEHENGA WALIVYOSEMA CHA MTU NI NINI? NA NGUO YA KUAZIMA HASITIRI NINI...
Tuombe mungu, atujalie, maana haya yapo juu ya uwezo wangu, hata hivyo Tupo pamoja!
Kazi nzuri ndugu wangu..nawe usiona nipo kimya nipo nawe...
Nilipotea kwa muda majukumu M3 yamenizidi ila nashukuru nimepata muda kdg ya kuendelea na riwaya yetu mpka mwisho..Tuko pamoja M3, Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako.
Mkuu Wambura, ndugu wangu Yasinta na mpendwa Precious na wengineo ambao hawakutaja majina yao na wale wa kimiya kimiya, nawashukuruni sana kuwa nami.
Kwa ujumla nyote Mumenipa faraja, maana ukiandika huwezi jua nini wenzako wanafikiria mpaka akitoa maoni.
Pole na majukumu Precious, karibu sana tuungane pamoja, na halikadhalika Yasinta ulisema ulikwenda `kalikizo kidogo' karibu tena!
hongera m3 kwa hadithi zako tamu, name nilitaka kuulizia ile part ambayo msomali alienda akakuta mwanadada amelala chini kwenye dimbwi la damu, ila naona ushaitolea ufafanuzi hapo juu.. Big up brother..
однокласник mail ru группа
одноклассники ry
сообщение на одноклассниках
одноклассники online игры ipad2
удалить одноклассниках
Post a Comment