Kipindi cha kampeni kilipofika sikuwa na wasiwasi, nilijiamini
kupita kiasi maana najua kuongea, lakini kumbe kuongea haikuwa tija, kulikuwa
na mengine zaidi ya hayo. Tukafika huko kijijini, na siku ya mwanzo ikabidi
nianze kwa kwenda kujitambulisha kwa viongozi mbali mbali wa vijiji na kata, ambao
wengine nilikuwa siwajui, baada ya kujitambulisha, nilitayarishiwa mikutano ya mwanzo
ya kujitambulsiha vyema kwa wanachi.
Mikutano hiyo ilianzia mbali na kijiji nilipotokea,ili watu
wanifaahmu vyema, ilibidi wakati mwingine kutembea kwa miguu, baiskeli na hata
pikipiki, ilimradi kuonyesha kuwa nipo karibu na wananchi, ilibidi niasahau
kabisa kuvaa suti, na wakati mwingine, ilibidi nivue viatu, na kutembea
pekupeku kule kweney matope, kusipopitika, kwa kipindi kama hicho, nilimsalimia
kila mtu, hata mtoto mdogo, na kuna mmoja alinitanai kuwa kuan sehemu
nilichanganyikiwa na kutoao salamu kwa mtoto kkwa kusema
‘Shikamoo mwanangu…..’ ulikuwa ni utani.
Mambo yalianza kuwa magumu kwenye baadhi ya vijiji, maana
nikiwa kwenye jukwaa, nikiwa naanza kutoa mambo yangu, ambayo nilijua kuwa kama
ni watu wanaopenda mambo ya siasa wangelivutiwa sana na mpangilio wa hotuba
zangu, nilisahau kuwa hawo ni wananchi wa kawaida tu, ambao mambo ya kisiasa na
mpangilio wahituba za kitaalamu, kwao ni kama kupotezewa muda, …kuna sehemu
pale nilipoanza tu, nikasikia watu wengine wakisema.
‘Vipi huyo amekuja kujaje hapa, mbona watu tuna njaa,…
Nikamuliza mtu wa pale, akaniambia wenzangu wakifika hapo
wanapika wali kama sherehe na wengine wanagawa vinywaji, wanagwa khanga, kofia ….nikamwambia
mwekahazina wangu ajaribu kununua vinjwaji, lakini haikuwa rahisi,maana watu
walikuwa wengi sana, na hata hotuba yangu haikufuatiliwa kama nilivyotarajia,
kwani wengi walikuwa hawana haja ya kusikiliza nini ninachongea, zaidi ya kudai
vitu….
‘Kwa mtaji huu, tunahitajia kuwa na pesa nyingi
sana….’nikasema.
‘Usijali huu ndio mwanzo tu…hata hivyo, kwa hali ilivyo sasa
pesa ni muhimu, sijui nyie mumekujakujaje….’akaongea mmoja wa washauri wahuko
kwenye vijiji.
Kikao kingine tukajipanag, tukaona tutafute vitu vya
kuwafurahisha wananchi,ngoma, miziki, na vivywaji rahisi kama sherehe, watu
wakala, na hapo ikawa ahueni, lakini ilikuwa ni gharama na nikijua
nimeshawawezea, lakini haikuwa rahisi hivyo, maana kumbe mambo ya kampeni sio
kuongea tu, sio vivywaji tu, sio kula tu, sio kugawa khanga tu, na kofia kuna
mengine ya ziada.
Kuna kijiji kimoja, wakati naanza kuhutubia tu, niliona kama
mchanagumeingia machoni, …nikajaribu kuondoa ule mchanga, lakini haikuwa
rahisi, nikaanza kujisikia vibaya, nikaomba maji ya kunywa, na nilipopewa chupa
ya maji, nikashituka, maana yale maji yaligeuka rangi, ilikuwa i damu tupu,…
‘Vipi haya maji gani yana rangi nyekundu,…?’ nikauliza
Yeye akayaangalia na kusema mbona yapo kawaida tu,
akanishangaa, akaniambai ni macho yangu tu.Sikujali niyatumbukiza kinywani,
….nikisema hayo ni mazingaumbwe, lakini yalikuwa hayapiti kooni, ilikuwa kama
mtu anakunywa maji kwa pupa halafu yamapalia, nikaanza kukohoa mfululuzo, na
mara nikaanza kuona marue rue machoni, na mbele yangu niliona majitu marefu yakutosha
yakiwa yananijia, nikagwaya, nikitafuta mwanya wa kukimbilia.
‘Vipi wewe mbona husemi kitu..’nikasikia watu wakianza
kulalamika ….Mshauri wangu akanisogelea na kuniuliza kama kuna tatizo lolote, …nikiwa
sijiwezi, nijikakamua huku nikimuomba mungu znisaidie, nikamwambia yule mshauri
wangu,….
‘Hali sio shwari, naona mambo ya ajabu ajabu hapa, nahisi
kuna jambo hapa….’nikasema na yulemshauri akaongea na wazee fulani wa hapo, na
mzee mmoja,akaja na kusimama pembeni yangu, na alipoangalia kule mbele,
akamnongoneza yule mshauri wangu, kuwa hapo kwa leo hatuwezi kufanya lolote,
maana tumeingia huo miji wa watu bila kibali.
‘Kibali gani tena, mbona taratibu zote zimefuatwa….’akalalamika
mshauri wangu.
‘Sio kibali cha serikali, huku nako kuna vibali vyake,…ndio
maanamlipokuja niliwauliza mumepata kibali cha kuingia huku, mkasema ndio,na
mimii nilijua labda mumeshapaat hicho kibali….’akasema huyo mzee.
‘Sasa tufanyeje….?’ Akauliza mshauri.
‘Hapa mkuatano haupo tena, mpaka tupate hicho kibali….’akasema
huyo mzee.
Mkutano ilibidi uahirishwe, na watu wakatawanyika wakizomea,
na nikajua kuwa huko sina langu tena, na hata hivyo, hali yangu ikawa,mbaya
nikawa najisikai vibaya sana, hadi nikapelekwa kwa wazee wa kijiji, na huko
nikaambiwa ili niweze kufanya lolote kwenye eneo hilo inabidi niwekwe sawa,…
‘Mimi imani yangu hainiruhusu mambo hayo,….’nikalalamika.
‘Sio swala la kuamua hapa, inabidi uwekwe sawa, kama kweli
unahitaji kuhutubia maeneo haya, na kama unahitaji uwe salama kimwili wako,…wenzako
wakija hoa nilazima wamuone mzee wa kijiji, …’nikaambiwa.
‘Mzee gani huyo?’ nikauliza.
‘Mzee Matulinga….’nikaambiwa.
‘Mzee Matulinga….?!, huyo si ndio babu wa rafiki yangu,
….atanisaidia kwelihuyu mtu?’ nikasema kwa kushangaa maana Mzee huyo ndiye babu
wa rafiki yangu, ambaye sasa ni adui yangu mkubwa.
‘Inabidi ufanye hivyo, hata kama ni babu wa rafiki yako,
vinginevyo hutawea kufanya lolote…na siazni kama uanweza kurejea kwenu salama…’nikaambiwa,
na hali yangu ikawa mbaya sana, na wazee wakatumwa kwa huyo mzee. Baadaye
nikaambiwa niende kwa huyo mzee, na kukutana ana kwa ana na huyo mzee, mwili
wote ulisisimuka.
Nilikuwa namsikia tu, na kwa jinsi anavyotisha, …waandai
huyo alikuwa anapigana na samba peke yake, hadi anamuua,. ..ana visa vingi vya
kutisha, na wengine walifikia kusema huwa anakunywa damu za watu….nikajipa moyo
na imani yangu haba, nikisema yeye ni binadamu tu kama mimi….alikuwa kava mmbo
yake mwilini, kuashiria kuwa yeye ni mganga, au kiongozi wa wazee, wataalamu wa
kienyeji,wao wanajua maana ya mavazi hayo….aliponiona , alinaingalia kwa jicho la chuki, akaniambia
bila kunificha….
‘Wewe ndiye unajifanya mjanja sana, sasa tuone ujanja
wako’akaniambia, na sikuwa na jinsi, ilibidi wenzangu wambembeleze huyo mzee, ili anisamehe, n yeye akatoa sharti
la kunisamehe kuwa nisifanye mikutano yoyote hapo kweney hichoo kijiji, kwani
ni miliki yake, na anayestahili kufanya vikao hapo ni yule aliyekubaliwa na wao
ikiwa na maana ni mpizani wangu amabye anaungwa mkono na yule rafiki yangu.
Basi ikabidi kweli niondoke maeneo hayo bila mikuatano, na
kwenda maeneo mengine, na huko nikawa nakutana na matuko mengine, lakini
hayakuwa mabaya kama huko nilipotoka. Na mara kwa mara nilikuwa na mke wangu,
akinisaidia kuwahamasisha wanawake wenzake. Kwakweli mke wangu alifanya kazi kubwa
sana, lakini ilihitaji ghrama nyingi, na ilifikia mahali akaniambia kuwa yeye
hataweza tena, kwani pesa tunayotoa haitoshi.
‘Sasa tufanyeje mke wangu?’ nikamuuliza.
‘Tuuze lile gari la daladala na ikibidi tuweke rehani ile
nyumba yetu ya kupangisha, kama kweli tunahitaji huo ubunge ..’kauli hiyo
ilinivunja nguvu, maana tumetumia pesa nyingi, na tumeuza karibu kila kitu,
sasa itakuwaje kama tukiukosa huo ubunge,
‘Mke wangu hilo ni sawa, lakini je itakuwaje, kama
tusipofanikiwa, huoni kuwa tutabakia uchi….’nikalalamika.
‘Kama kweli unaupenda huo ubunge, huna jinsi, ….’akanishauri,
na ikabidi tufanye hivyo ili kuweza kupata pesa kwani zile pesa za wafadhili
hazikutosha.
Na kipindi mambo yanakwenda vibaya mke wangu hakukumbuka
hilo, na hapo ndipo nikakumbuka yale yale yaliyotokea kweney kampeni, yalikuwa
sawasawa nay ale yale yaliyotokea kipindi mke wangu, kwa wakati huo akiwa binti
Mrembo, alipochukuliw na wale jamaa, ambao waliomteka nyara siku ile ya harusi…
********
Nilipotoka nje nilikutana na shangazi mtu, akaniuliza ;
‘Wewe ni nani..’
‘Mimi ni mpambaji wa bibi harusi, kuna vitu
aliniangaizia…’nikandanganya kwa haraka huku nikikwepa kabisa kumwangalia, na
mara kelelle za watu zikazidi kuonyesha kuwa waowaji wapo karibu, na ndichokilichosaidia,
kwani shangazi alishaanza kunsigelea, kwani alinitilia mashaka, lakini watu
wakawa wamekuja kwa kasi nahapo nikapata mwanya wa kumtoka huyo shangazi.
‘Wewe kama nakujau, wewe sio…’akaanza kuongea, na mara mtu
mmoja akaja ksmhika shangazi mkono,akisema shanagzi aanitwa na akina mama,
nikashukuru na haraka nikakimbilia kule walipokuwa wenzangu.
‘Wewe vipi mbona umetoka na hatujapata ishaar yoyote kuwa
tuje, na naona mambo yameshaharibika,…’akasema mmoja wa watu wangu.
‘Kuna watu wamefika an kumteka nyara bibi harusi…’nikasema.
‘Watu gani hao?’ nikaulizwa.
‘Mimi sijui, walikuwa na mabausa wawili, wenye vifua kama
wainua vyuma,..’nikasema.
‘Sasa tufanyeje?’ akauliza jamaa yangu mmoja.
‘Hata sijui tufanyeje na nahisi kama shangazi mtu kaniona,..’nikasema.
‘Hilo sasa balaa, maana utasingiziwa wewe kama ndiye
uliyefanya hayo yote, na kwa mtaji huo tunatakiwa tuondoke hapa
haraka…’akanishauri mwenzangu mmoja , na wengine wakakubaliana na hilo
wazo, na kwa harakai tukatafuta usafiri
wa kutoka eneo hilo, na wakati tupo njiani simu yangu ikaita, kwa
nambaisiyojulikana,nikaipokea kwa wasiwasi.
‘Wewe ndiye rafiki wa binti Mrembo?’ nikaulizwa
‘Kwani wewe ni nani?’nikauliza swali kwa sauti ya ukali.
‘Sikiliza kwa makini, sisi ndio hawo tuliomteka nyara huyu
binti, na huyo binti tunaye hapa, na
kama unamhitaji ufike na shilingi milioni tano kamili, vinginevyo hutampata
tena,….’ile sauti ikasema..na kwa mbali nikasikia sauti ya huyo binti akilia.
‘Nyie majambazi ….kama mtamzuru huyo binti, nitwatafuta kwa
kila hali, na cha moto mtakiona, nyie watu gani hamna huruma,mnachukua huyo
binti wa watu hana mbele wala nyuma, halafu mnataka kuniingiza kwenye matatizo,mimi…sikizeni
mimi sina pesa kama hiyo….mnafikiri mimi pesa kama hiyo nitaipata wapi?’
nikauliza.
‘Hahahaa…wewe unapenda tu, unafikiri huyu binti thamani yake
ni shilingi ngapi, wewe….acha upuuzi huo, …unasikia sisi hautujui wapi
utazipatia hizoo pesa, ila kama kweli unamuhitaji huyo binti, fika kituo kikuu
cha mabasi, pale pembeni kuna mgahawa wa maziwa, ulizia mama Maziwa, utaonyeswa
wapi alipo huyo binti, ..
Cha kufanya wewe kwanza hakikisha hiyo pesa umeweka kwenye
bahasha iweke kwenye mfuko wa Rambo, ….ukifika kwenye hicho kibanda, wewe agiza
maziwa, na wakati unalipia , mpe huyo mama huo mfuko, wewe mwambai huu ni mzigo
wa rafiki zangu, watakuja kuuchukua, akikuulizia ni nani, huyo rafiki yako
mwambie ni Baunsa,…inatosha, wewe mpe huyo mama, sisi tutakuwa tunakuona, na
ukifanay lolote kinyume na haya maelekezo…..’na kabla hajamaliza mimi
nikamkatisha na kusema;.
‘Mimi hizo pesa sina ….’nikasema kwa wasiwasi,kwani ni kweli
nisingeliweza kuzipata hizoo pesa kirahisi hivyo, hata kama nikiuza baaadhi ya
vitu vyangu, na ni nani atakubali kununua vitu vyangu kwamuda huo mfupi!.
‘Wewe una shilingi ngapi?’ nikaulizwa.
‘Labda nimejitahidi kwa kukopa ninaweza kupaat shilingi
laki tano…’nikasema
‘Wewe sasa unatania unajau mwenzako katoa mahari ya shilingi
ngapi?’akaniuliza.
‘Mimi sijui hayo ya mwenzangu…kwani alitoa mahari ya
shilingi ngapi?’ nikauliza.
‘Yeye alitoa mahari ya milioni tano, achilia mbali zawadi
mbalimbali…sasa akihitaji pesa yake irudishweje unafikiri tutapatia wapi pesa ya
kumrejeshea…?’ akaniluza.
‘Mimi hayo siyajui, ila kiukweli pesa ninayoweza kuipata ni
hiyo, kama haiwezekani basi, …nitaongea na polisi wao watajua nini la kufanya…’nikasema
na huyo mtu akakata simu huku akyonza kwa ahsira.
Na mimi ikabidi niongee na wenzangu, kuwaambia nini hawo
watu wanachohitajia, na mmojawapo akasema;
‘Wewe kama kweli uanmpenda huyo binti jitahidi hata kama
nikuuza baadhi ya vitu vyako, ili upate hiyo pesa, na ikibidi weke rehani
pikipiki yako…’akasema na kweli moyoni nilikuwa tayari kufanya lolote, ilimradi
nihakikishe nampata huyo binti,…lakini milioni tano..
‘Mimi nashauri tuwaarifu polisi maana watu kama hawa ukiwaendekeza kwa pesa, wanaweza waakzichukua nab
ado wasikukabidhi huyo binti…’akatoa wazo mmoja wetu.
‘Hapana, tukifanya hivyo, tunaweza tukamfanya huyo binti
akazuriwa, na ikampa taabu katika msiha yake yote, anaweza akabakwa,
akaambukizwa magonjwa……hapana kwa sasa wazo hilo la polisi tuliweke pembeni…’nikasema.
‘Haya sasa hizo pesa zitapatikana wapi…?’akauliza mmojawapo,
na hapo tukakaa kimiya kwa muda, na mmoja wao akasema;
‘Mimi nitajitahidi kutafuta laki tano, lakini reheni ni
pikipiki yako….’akaniambia mmoja wa watu wangu na mwingine akasema laki tatu,,
na mwingine lakini tatu, na mwingine…. mpaka ikafikia hiyo milioni tano.
Na mara simu ikapigwa tena,niakulizwa nimefikia wapi maana
kuna mtu kasema yupo tayari kuitoa hiyo pesa ili amchukue huyo binti.
‘Kama huna hiyo pesa binti utamkosa, maana kuna mijamaa hapa
haijawahi kumpata mwanamke miaks kumi, ndio imetoak jela juzi, na mmojawapo
kasema ataitoa hiyo pesa, na binti atamchukua yeye, tunachohitaji sisi ni kuhakikisha
huyo binti haolewi na huyo jamaa anayejifanya ni tajiri, ndio maana tukamteka
nyara,….’akasema huyo jamaa
‘Nitaitafutahio pesa , lakini hakikisheni huyo binti hapati
matatizo yoyote…ole wenu mkimfanyoa lolote baya, nitahakikisha mnajuta kuzaliwa’nikasema.
‘Wewe, toka lini mtu mzima akatishiwa nyau,….Ikifika jioni
ya leo , kama hujazipata hizo pesa, basi, tutajua nini lakufanya, …na kama
utawaambia polisi, basi sisi tutamfanya huyu binti kitu mbaya, na hata ukimuona
tena, hutamtamani,…..’akasema huyu mtu kwa sauti ya kilevilevi… .
‘Nitajuajee kuwa mpo naye, na nitahakikishaje usalama wake,?’
nikauliza na mara nikasikia akiongea na mwenzake.
‘Haya wewe ongea naye, na hatutaki ujanja wowote, hiyo namba
kama unavyoiona haipo kwenye mitandao yenu, ni namba maalumu…’akasema kwa
kujiamini.
‘Haloooh…’sauti ya kinyonge ikasema , ilikuwa ni sauti yake
kiukweli.
‘Vipi upo salama?’ nikauliza.
‘Mimi sijui ni nini kinaendelea, kwanini mnanifanya hivi,…hawa
watu wamenichukua kwa nguvu, …jamani mnataka nini kwangu, hamuoni kuwa hili litamletea balaa bibi yangu, mimi
sijui mnataka nini kwangu, kwanini mnatuonea , tumewakosea nini, yule bibi wa
watu hana kosa lolote, ….’akaanza kulalamika huyo binti kwenye simu.
‘Mwambie jamaayako atoe pesa sisi tutakuachia, lakini kwa
masharti kuwa hutaolewa na huyo jamaa yako tajiri,…’sauti ikasikika ikisema.
‘Kwani ni mimi nimepanaga hivyo, waulizeni wazazi wangu…’akalaalmika
huyo binti.
‘Tuwaulize wao kwani wao ndio wanaoolewa, wewe unatushangaza
kweli ,ina maana mume umetafutiwa, usitudanganye hapa, wewe unachokimbilia huko
ni huo utajiri, humjui kabisa huyo jamaa, alivyo, atakuoa na mwisho wa siku
utatemwa, ataolewa mwingine…’sauti ikasema.
‘Mimi mnanichanganya tu, …halloh, …’akasema huyo binti
kwenye simu, nafikiri alipona simu bado ipo hewani, na mimi nikasema;
‘Mimi siwajui hawo watu waliokuteka nyara, wamedai nitoe
milioni tano ndio wakuachie….fikiria milioni tano, …..’nikasema.
‘Kwahiyo wewe hutawezi kuzipata hizo pesa,…nakuomba sana,
tafadhali, nisaidie, kama kweli unamjali bibi yangu, na kuomba uzitafute hizo
pesa, maana hawa watu walivyo, wanaweza kunifanya lolote baya, na hata
kumwanagmiza bibi yangu,hapa walipo wanavuata bangi, na ikishindikana …waambie polisi….’na mara simu ikakatwa.
NB; Je nilichukua hatua gani..
WAZO LA LEO: Ukiamini ushirikina, ukauteka moyo wako, basi
ujue ni rahisi kuathirika na mambo hayo,lakini kama utamwamini mungu ukweli wa
kumwamini, kuwa ndiye mlinzi wako, sio rahisi kuzurika na mambo hayo.
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
safi sana kaka, nilipotea nimerudi upya. naona moto ni uleule. keep it up.
Haki ya nane Mungu ndiye muweza na ukimtumaini yeye atakulinda na hutazurika. Pamoja daima.
Ammy karibu tena, tunataraji umekuja na mengi, usihofu kutuhabarisha, sisi kama kawa.
Ndugu wangu YASINTA, kama kawa, ni kweli,lkn bwana wengi mungu wanamwamini kwa mdomo, moyoni hakuna kitu. Imani sio mchezo!
Asante. Bila shaka nikiwa nalo lazima kuhabarishana.
Post a Comment