Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, August 27, 2012

Mbio sa sakafuni huishia ukingoni-8
Kipindi cha kampeni kilipofika sikuwa na wasiwasi, nilijiamini kupita kiasi maana najua kuongea, lakini kumbe kuongea haikuwa tija, kulikuwa na mengine zaidi ya hayo. Tukafika huko kijijini, na siku ya mwanzo ikabidi nianze kwa kwenda kujitambulisha kwa viongozi mbali mbali wa vijiji na kata, ambao wengine nilikuwa siwajui, baada ya kujitambulisha, nilitayarishiwa mikutano ya mwanzo ya kujitambulsiha vyema kwa wanachi.

Mikutano hiyo ilianzia mbali na kijiji nilipotokea,ili watu wanifaahmu vyema, ilibidi wakati mwingine kutembea kwa miguu, baiskeli na hata pikipiki, ilimradi kuonyesha kuwa nipo karibu na wananchi, ilibidi niasahau kabisa kuvaa suti, na wakati mwingine, ilibidi nivue viatu, na kutembea pekupeku kule kweney matope, kusipopitika, kwa kipindi kama hicho, nilimsalimia kila mtu, hata mtoto mdogo, na kuna mmoja alinitanai kuwa kuan sehemu nilichanganyikiwa na kutoao salamu kwa mtoto kkwa kusema

‘Shikamoo mwanangu…..’ ulikuwa ni utani.

Mambo yalianza kuwa magumu kwenye baadhi ya vijiji, maana nikiwa kwenye jukwaa, nikiwa naanza kutoa mambo yangu, ambayo nilijua kuwa kama ni watu wanaopenda mambo ya siasa wangelivutiwa sana na mpangilio wa hotuba zangu, nilisahau kuwa hawo ni wananchi wa kawaida tu, ambao mambo ya kisiasa na mpangilio wahituba za kitaalamu, kwao ni kama kupotezewa muda, …kuna sehemu pale nilipoanza tu, nikasikia watu wengine wakisema.

‘Vipi huyo amekuja kujaje hapa, mbona watu tuna njaa,…

Nikamuliza mtu wa pale, akaniambia wenzangu wakifika hapo wanapika wali kama sherehe na wengine wanagawa vinywaji, wanagwa khanga, kofia ….nikamwambia mwekahazina wangu ajaribu kununua vinjwaji, lakini haikuwa rahisi,maana watu walikuwa wengi sana, na hata hotuba yangu haikufuatiliwa kama nilivyotarajia, kwani wengi walikuwa hawana haja ya kusikiliza nini ninachongea, zaidi ya kudai vitu….

‘Kwa mtaji huu, tunahitajia kuwa na pesa nyingi sana….’nikasema.

‘Usijali huu ndio mwanzo tu…hata hivyo, kwa hali ilivyo sasa pesa ni muhimu, sijui nyie mumekujakujaje….’akaongea mmoja wa washauri wahuko kwenye vijiji.

Kikao kingine tukajipanag, tukaona tutafute vitu vya kuwafurahisha wananchi,ngoma, miziki, na vivywaji rahisi kama sherehe, watu wakala, na hapo ikawa ahueni, lakini ilikuwa ni gharama na nikijua nimeshawawezea, lakini haikuwa rahisi hivyo, maana kumbe mambo ya kampeni sio kuongea tu, sio vivywaji tu, sio kula tu, sio kugawa khanga tu, na kofia kuna mengine ya ziada.

Kuna kijiji kimoja, wakati naanza kuhutubia tu, niliona kama mchanagumeingia machoni, …nikajaribu kuondoa ule mchanga, lakini haikuwa rahisi, nikaanza kujisikia vibaya, nikaomba maji ya kunywa, na nilipopewa chupa ya maji, nikashituka, maana yale maji  yaligeuka rangi, ilikuwa i damu tupu,…

‘Vipi haya maji gani yana rangi nyekundu,…?’ nikauliza

Yeye akayaangalia na kusema mbona yapo kawaida tu, akanishangaa, akaniambai ni macho yangu tu.Sikujali niyatumbukiza kinywani, ….nikisema hayo ni mazingaumbwe, lakini yalikuwa hayapiti kooni, ilikuwa kama mtu anakunywa maji kwa pupa halafu yamapalia, nikaanza kukohoa mfululuzo, na mara nikaanza kuona marue rue machoni, na mbele yangu niliona majitu marefu yakutosha yakiwa yananijia, nikagwaya, nikitafuta mwanya wa kukimbilia.

‘Vipi wewe mbona husemi kitu..’nikasikia watu wakianza kulalamika ….Mshauri wangu akanisogelea na kuniuliza kama kuna tatizo lolote, …nikiwa sijiwezi, nijikakamua huku nikimuomba mungu znisaidie, nikamwambia yule mshauri wangu,….

‘Hali sio shwari, naona mambo ya ajabu ajabu hapa, nahisi kuna jambo hapa….’nikasema na yulemshauri akaongea na wazee fulani wa hapo, na mzee mmoja,akaja na kusimama pembeni yangu, na alipoangalia kule mbele, akamnongoneza yule mshauri wangu, kuwa hapo kwa leo hatuwezi kufanya lolote, maana tumeingia huo miji wa watu bila kibali.

‘Kibali gani tena, mbona taratibu zote zimefuatwa….’akalalamika mshauri wangu.

‘Sio kibali cha serikali, huku nako kuna vibali vyake,…ndio maanamlipokuja niliwauliza mumepata kibali cha kuingia huku, mkasema ndio,na mimii nilijua labda mumeshapaat hicho kibali….’akasema huyo mzee.

‘Sasa tufanyeje….?’ Akauliza mshauri.

‘Hapa mkuatano haupo tena, mpaka tupate hicho kibali….’akasema huyo mzee.
Mkutano ilibidi uahirishwe, na watu wakatawanyika wakizomea, na nikajua kuwa huko sina langu tena, na hata hivyo, hali yangu ikawa,mbaya nikawa najisikai vibaya sana, hadi nikapelekwa kwa wazee wa kijiji, na huko nikaambiwa ili niweze kufanya lolote kwenye eneo hilo inabidi niwekwe sawa,…

‘Mimi imani yangu hainiruhusu mambo hayo,….’nikalalamika.

‘Sio swala la kuamua hapa, inabidi uwekwe sawa, kama kweli unahitaji kuhutubia maeneo haya, na kama unahitaji uwe salama kimwili wako,…wenzako wakija hoa nilazima wamuone mzee wa kijiji, …’nikaambiwa.

‘Mzee gani huyo?’ nikauliza.

‘Mzee Matulinga….’nikaambiwa.

‘Mzee Matulinga….?!, huyo si ndio babu wa rafiki yangu, ….atanisaidia kwelihuyu mtu?’ nikasema kwa kushangaa maana Mzee huyo ndiye babu wa rafiki yangu, ambaye sasa ni adui yangu mkubwa.

‘Inabidi ufanye hivyo, hata kama ni babu wa rafiki yako, vinginevyo hutawea kufanya lolote…na siazni kama uanweza kurejea kwenu salama…’nikaambiwa, na hali yangu ikawa mbaya sana, na wazee wakatumwa kwa huyo mzee. Baadaye nikaambiwa niende kwa huyo mzee, na kukutana ana kwa ana na huyo mzee, mwili wote ulisisimuka.

Nilikuwa namsikia tu, na kwa jinsi anavyotisha, …waandai huyo alikuwa anapigana na samba peke yake, hadi anamuua,. ..ana visa vingi vya kutisha, na wengine walifikia kusema huwa anakunywa damu za watu….nikajipa moyo na imani yangu haba, nikisema yeye ni binadamu tu kama mimi….alikuwa kava mmbo yake mwilini, kuashiria kuwa yeye ni mganga, au kiongozi wa wazee, wataalamu wa kienyeji,wao wanajua maana ya mavazi hayo….aliponiona ,  alinaingalia kwa jicho la chuki, akaniambia bila kunificha….

‘Wewe ndiye unajifanya mjanja sana, sasa tuone ujanja wako’akaniambia, na sikuwa na jinsi, ilibidi wenzangu wambembeleze  huyo mzee, ili anisamehe, n yeye akatoa sharti la kunisamehe kuwa nisifanye mikutano yoyote hapo kweney hichoo kijiji, kwani ni miliki yake, na anayestahili kufanya vikao hapo ni yule aliyekubaliwa na wao ikiwa na maana ni mpizani wangu amabye anaungwa mkono na yule rafiki yangu.

Basi ikabidi kweli niondoke maeneo hayo bila mikuatano, na kwenda maeneo mengine, na huko nikawa nakutana na matuko mengine, lakini hayakuwa mabaya kama huko nilipotoka. Na mara kwa mara nilikuwa na mke wangu, akinisaidia kuwahamasisha wanawake wenzake. Kwakweli mke wangu alifanya kazi kubwa sana, lakini ilihitaji ghrama nyingi, na ilifikia mahali akaniambia kuwa yeye hataweza tena, kwani pesa tunayotoa haitoshi.

‘Sasa tufanyeje mke wangu?’ nikamuuliza.

‘Tuuze lile gari la daladala na ikibidi tuweke rehani ile nyumba yetu ya kupangisha, kama kweli tunahitaji huo ubunge ..’kauli hiyo ilinivunja nguvu, maana tumetumia pesa nyingi, na tumeuza karibu kila kitu, sasa itakuwaje kama tukiukosa huo ubunge,

‘Mke wangu hilo ni sawa, lakini je itakuwaje, kama tusipofanikiwa, huoni kuwa tutabakia uchi….’nikalalamika.

‘Kama kweli unaupenda huo ubunge, huna jinsi, ….’akanishauri, na ikabidi tufanye hivyo ili kuweza kupata pesa kwani zile pesa za wafadhili hazikutosha.

Na kipindi mambo yanakwenda vibaya mke wangu hakukumbuka hilo, na hapo ndipo nikakumbuka yale yale yaliyotokea kweney kampeni, yalikuwa sawasawa nay ale yale yaliyotokea kipindi mke wangu, kwa wakati huo akiwa binti Mrembo, alipochukuliw na wale jamaa, ambao waliomteka nyara siku ile ya harusi…

********

Nilipotoka nje nilikutana na shangazi mtu, akaniuliza ;

‘Wewe ni nani..’

‘Mimi ni mpambaji wa bibi harusi, kuna vitu aliniangaizia…’nikandanganya kwa haraka huku nikikwepa kabisa kumwangalia, na mara kelelle za watu zikazidi kuonyesha kuwa waowaji wapo karibu, na ndichokilichosaidia, kwani shangazi alishaanza kunsigelea, kwani alinitilia mashaka, lakini watu wakawa wamekuja kwa kasi nahapo nikapata mwanya wa kumtoka huyo shangazi.

‘Wewe kama nakujau, wewe sio…’akaanza kuongea, na mara mtu mmoja akaja ksmhika shangazi mkono,akisema shanagzi aanitwa na akina mama, nikashukuru na haraka nikakimbilia kule walipokuwa wenzangu.

‘Wewe vipi mbona umetoka na hatujapata ishaar yoyote kuwa tuje, na naona mambo yameshaharibika,…’akasema mmoja wa watu wangu.

‘Kuna watu wamefika an kumteka nyara bibi harusi…’nikasema.

‘Watu gani hao?’ nikaulizwa.

‘Mimi sijui, walikuwa na mabausa wawili, wenye vifua kama wainua vyuma,..’nikasema.

‘Sasa tufanyeje?’ akauliza jamaa yangu mmoja.

‘Hata sijui tufanyeje na nahisi kama shangazi mtu kaniona,..’nikasema.

‘Hilo sasa balaa, maana utasingiziwa wewe kama ndiye uliyefanya hayo yote, na kwa mtaji huo tunatakiwa tuondoke hapa haraka…’akanishauri mwenzangu mmoja , na wengine wakakubaliana na hilo wazo,  na kwa harakai tukatafuta usafiri wa kutoka eneo hilo, na wakati tupo njiani simu yangu ikaita, kwa nambaisiyojulikana,nikaipokea kwa wasiwasi.

‘Wewe ndiye rafiki wa binti Mrembo?’ nikaulizwa

‘Kwani wewe ni nani?’nikauliza swali kwa sauti ya ukali.

‘Sikiliza kwa makini, sisi ndio hawo tuliomteka nyara huyu binti, na huyo binti  tunaye hapa, na kama unamhitaji ufike na shilingi milioni tano kamili, vinginevyo hutampata tena,….’ile sauti ikasema..na kwa mbali nikasikia sauti ya huyo binti akilia.

‘Nyie majambazi ….kama mtamzuru huyo binti, nitwatafuta kwa kila hali, na cha moto mtakiona, nyie watu gani hamna huruma,mnachukua huyo binti wa watu hana mbele wala nyuma, halafu mnataka kuniingiza kwenye matatizo,mimi…sikizeni mimi sina pesa kama hiyo….mnafikiri mimi pesa kama hiyo nitaipata wapi?’ nikauliza.

‘Hahahaa…wewe unapenda tu, unafikiri huyu binti thamani yake ni shilingi ngapi, wewe….acha upuuzi huo, …unasikia sisi hautujui wapi utazipatia hizoo pesa, ila kama kweli unamuhitaji huyo binti, fika kituo kikuu cha mabasi, pale pembeni kuna mgahawa wa maziwa, ulizia mama Maziwa, utaonyeswa wapi alipo huyo binti, ..

Cha kufanya wewe kwanza hakikisha hiyo pesa umeweka kwenye bahasha iweke kwenye mfuko wa Rambo, ….ukifika kwenye hicho kibanda, wewe agiza maziwa, na wakati unalipia , mpe huyo mama huo mfuko, wewe mwambai huu ni mzigo wa rafiki zangu, watakuja kuuchukua, akikuulizia ni nani, huyo rafiki yako mwambie ni Baunsa,…inatosha, wewe mpe huyo mama, sisi tutakuwa tunakuona, na ukifanay lolote kinyume na haya maelekezo…..’na kabla hajamaliza mimi nikamkatisha na kusema;.

‘Mimi hizo pesa sina ….’nikasema kwa wasiwasi,kwani ni kweli nisingeliweza kuzipata hizoo pesa kirahisi hivyo, hata kama nikiuza baaadhi ya vitu vyangu, na ni nani atakubali kununua vitu vyangu kwamuda huo mfupi!.

‘Wewe una shilingi ngapi?’ nikaulizwa.

‘Labda nimejitahidi kwa kukopa ninaweza kupaat shilingi laki tano…’nikasema

‘Wewe sasa unatania unajau mwenzako katoa mahari ya shilingi ngapi?’akaniuliza.

‘Mimi sijui hayo ya mwenzangu…kwani alitoa mahari ya shilingi ngapi?’ nikauliza.

‘Yeye alitoa mahari ya milioni tano, achilia mbali zawadi mbalimbali…sasa akihitaji pesa yake irudishweje unafikiri tutapatia wapi pesa ya kumrejeshea…?’ akaniluza.

‘Mimi hayo siyajui, ila kiukweli pesa ninayoweza kuipata ni hiyo, kama haiwezekani basi, …nitaongea na polisi wao watajua nini la kufanya…’nikasema na huyo mtu akakata simu huku akyonza kwa ahsira.
Na mimi ikabidi niongee na wenzangu, kuwaambia nini hawo watu wanachohitajia, na mmojawapo akasema;

‘Wewe kama kweli uanmpenda huyo binti jitahidi hata kama nikuuza baadhi ya vitu vyako, ili upate hiyo pesa, na ikibidi weke rehani pikipiki yako…’akasema na kweli moyoni nilikuwa tayari kufanya lolote, ilimradi nihakikishe nampata huyo binti,…lakini milioni tano..

‘Mimi nashauri tuwaarifu polisi maana watu kama hawa  ukiwaendekeza kwa pesa, wanaweza waakzichukua nab ado wasikukabidhi huyo binti…’akatoa wazo mmoja wetu.

‘Hapana, tukifanya hivyo, tunaweza tukamfanya huyo binti akazuriwa, na ikampa taabu katika msiha yake yote, anaweza akabakwa, akaambukizwa magonjwa……hapana kwa sasa wazo hilo la polisi  tuliweke pembeni…’nikasema.

‘Haya sasa hizo pesa zitapatikana wapi…?’akauliza mmojawapo, na hapo tukakaa kimiya kwa muda, na mmoja wao akasema;

‘Mimi nitajitahidi kutafuta laki tano, lakini reheni ni pikipiki yako….’akaniambia mmoja wa watu wangu na mwingine akasema laki tatu,, na mwingine lakini tatu, na mwingine…. mpaka  ikafikia hiyo milioni tano.
Na mara simu ikapigwa tena,niakulizwa nimefikia wapi maana kuna mtu kasema yupo tayari kuitoa hiyo pesa ili amchukue huyo binti.

‘Kama huna hiyo pesa binti utamkosa, maana kuna mijamaa hapa haijawahi kumpata mwanamke miaks kumi, ndio imetoak jela juzi, na mmojawapo kasema ataitoa hiyo pesa, na binti atamchukua yeye, tunachohitaji sisi ni kuhakikisha huyo binti haolewi na huyo jamaa anayejifanya ni tajiri, ndio maana tukamteka nyara,….’akasema huyo jamaa

‘Nitaitafutahio pesa , lakini hakikisheni huyo binti hapati matatizo yoyote…ole wenu mkimfanyoa lolote baya, nitahakikisha mnajuta kuzaliwa’nikasema.

‘Wewe, toka lini mtu mzima akatishiwa nyau,….Ikifika jioni ya leo , kama hujazipata hizo pesa, basi, tutajua nini lakufanya, …na kama utawaambia polisi, basi sisi tutamfanya huyu binti kitu mbaya, na hata ukimuona tena, hutamtamani,…..’akasema huyu mtu kwa sauti ya kilevilevi… .

‘Nitajuajee kuwa mpo naye, na nitahakikishaje usalama wake,?’ nikauliza na mara nikasikia akiongea na mwenzake.

‘Haya wewe ongea naye, na hatutaki ujanja wowote, hiyo namba kama unavyoiona haipo kwenye mitandao yenu, ni namba maalumu…’akasema kwa kujiamini.

‘Haloooh…’sauti ya kinyonge ikasema , ilikuwa ni sauti yake kiukweli.

‘Vipi upo salama?’ nikauliza.

‘Mimi sijui ni nini kinaendelea, kwanini mnanifanya hivi,…hawa watu wamenichukua kwa nguvu, …jamani mnataka nini kwangu, hamuoni  kuwa hili litamletea balaa bibi yangu, mimi sijui mnataka nini kwangu, kwanini mnatuonea , tumewakosea nini, yule bibi wa watu hana kosa lolote, ….’akaanza kulalamika huyo binti kwenye simu.

‘Mwambie jamaayako atoe pesa sisi tutakuachia, lakini kwa masharti kuwa hutaolewa na huyo jamaa yako tajiri,…’sauti ikasikika ikisema.

‘Kwani ni mimi nimepanaga hivyo, waulizeni wazazi wangu…’akalaalmika huyo binti.

‘Tuwaulize wao kwani wao ndio wanaoolewa, wewe unatushangaza kweli ,ina maana mume umetafutiwa, usitudanganye hapa, wewe unachokimbilia huko ni huo utajiri, humjui kabisa huyo jamaa, alivyo, atakuoa na mwisho wa siku utatemwa, ataolewa mwingine…’sauti ikasema.

‘Mimi mnanichanganya tu, …halloh, …’akasema huyo binti kwenye simu, nafikiri alipona simu bado ipo hewani, na mimi nikasema;

‘Mimi siwajui hawo watu waliokuteka nyara, wamedai nitoe milioni tano ndio wakuachie….fikiria milioni tano, …..’nikasema.

‘Kwahiyo wewe hutawezi kuzipata hizo pesa,…nakuomba sana, tafadhali, nisaidie, kama kweli unamjali bibi yangu, na kuomba uzitafute hizo pesa, maana hawa watu walivyo, wanaweza kunifanya lolote baya, na hata kumwanagmiza bibi yangu,hapa walipo wanavuata bangi, na ikishindikana  …waambie polisi….’na mara simu ikakatwa.

NB; Je nilichukua hatua gani..

WAZO LA LEO:  Ukiamini ushirikina, ukauteka moyo wako, basi ujue ni rahisi kuathirika na mambo hayo,lakini kama utamwamini mungu ukweli wa kumwamini, kuwa ndiye mlinzi wako, sio rahisi kuzurika na mambo hayo.


Ni mimi: emu-three

4 comments :

Ammy k or Mimi ammy said...

safi sana kaka, nilipotea nimerudi upya. naona moto ni uleule. keep it up.

Yasinta Ngonyani said...

Haki ya nane Mungu ndiye muweza na ukimtumaini yeye atakulinda na hutazurika. Pamoja daima.

emu-three said...

Ammy karibu tena, tunataraji umekuja na mengi, usihofu kutuhabarisha, sisi kama kawa.

Ndugu wangu YASINTA, kama kawa, ni kweli,lkn bwana wengi mungu wanamwamini kwa mdomo, moyoni hakuna kitu. Imani sio mchezo!

Ammy K said...

Asante. Bila shaka nikiwa nalo lazima kuhabarishana.