Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, May 23, 2012

Hujafa hujaumbika-39



 Nilikuwa nimekaa kwenye kona ya kile chumba cha mahabusu, huku nimejikunja kama mkiwa. Kwakweli ilikuwa imeniuma na moyoni nilikuwa nimekasirika sana,...hapo nilikuwa mahabusu tu, kichwani mwangi nilikuwa nimepanga kuwa nitagoma kabisa kupelekwa huko Segerea au Ukonga, sikubali kupelekwa tena huko.

 Kwa ujumla sikuamini kuwa nimefikishwa mahala kama hapa tena, hata baada ya kuwa mwangalifu na maswala ya kuvunja sheria, lakini hujafa hujaumbika, ....nikiwa nimekunjata nikawa namumimba mungu, nisije nikapelekwa huko jela,…iliniuma sana kuona kuwa dunia hii haina wema,yaani kujitolea kwangu huko,kuwafahamisha polisi kuhusu hilo tukio ndio ninashikiliwa eti kwa kuisadia polisi.

‘Usijali hizi ni taratibu za kawaida, utatolewa, na wamekushikilia kwa sababu ya maelezo yako uliyowapa, ilinakuweka mahali ambapo yoyote angeliweza kukuhisi kuwa uanahusika. Na linapotokea jambo kama hili la kesi za jinai, kama hii, ukatiliwa mashaka ni lazima wakushikilie kwa ajili ya kuisaidia polisi.

‘Kwa vipi wanahisi ni mimi na maelezo gani niliyotoa yanayoniweka kwenye mashaka..?’ nikamuuliza.

‘Ukumbuke kuwa huyo mtu kauliwa kwa silaha na muuaji anajua kulenga shabaha, wewe alipokuuliza mkuu kuwa unaweza kutumia silaha ulisemaje?’ akamuuliza dada wakili.

‘Nilimuambia ukweli,…nilimwambia ndio najua kutumia silaha,maana niliwahi kupitia mujibu wa sheria, kule tunafundishwa yote, nakumbuka tulipopelekwa uchaka, huko tulifundishwa mbinu zote za kivita na kwenye shabaha nilikuwa mtu wa kwanza, sikukosa hata moja…..niliizoea silaha utafikiri nilizaliwa nayo….’nikasema kwa majisifu.

‘Sasa hayo maelezo yako yanakuweka pabaya, sio kwamba ni vibaya kusema ukweli, lakini kwa fikira zao, na tetesi walizo nazo polisi na hata kwa mtizamo wa mtu yoyote kwa haraka haraka, muuaji alikuwa anajua vyema kulenga shabaha….na wewe unajua kulenga vyema shabaha. Na je alipokuuliza swali, kuwa ulipoingia humu ndani ulifanyeje, ulimjibu vipi…?’ akaniuliza dada wakili.

‘Unajua kuna mambo mengine unajifunza kutokana na uzoefu, mimi kwa ajili ya kujindaa kuja kufanya kazi kwenye ofisi yako mpya mwakani,nimekuwa nikihudhuria mafunzo ya sheria na upelelezi, na huko nimejifunza mambo mengi ya kujihami na kujilinda,….kuna sehemu tumefundishwa kuwa unapofika kwenye tukio unalolitilia mashaka….’nikatulia kidogo pale nilipomuona dada wakili akionyesha uso wa furaha.

‘Endela kuongea, mbona unakatisha ameno,…nimetabasamu kwasababu ya kusikia hivyo, kujiandaa kwa ajili ya ofisi yangu,…., safi kabisa,nashukuru kusikia hivyo, haya niambie umejifunza nini huko ambacho umekitumia kwenye hili tukio?’ akaniuliza.

‘Unapofika sehemu yenye mashaka, ni vyema ukachunga kuacha alama za vidole, sasa mimi nilipofika hapo kweny hiyo nyumba,…niliingiwa na wasiwasi, hasa pale nilipogonga mlango na kuona kupo kimiya, nilichofanya ni kuvaa soksi,…unajua nilichofanya ni kuvua soksi zangu za miguuni, na kuzivaa mkononi, kuogopa kuacha alama za vidole….’nikasema bila wasi wasi.

‘Hapo unafikiri polisi wataamini kuwa ulifanya hivyo kwa ajili ya kujihami,…. swali kubwa kwao, ni je ulijuaje kuwa kuna tatizo, mpaka uvae hizo soksi,….lazima hapo watakutilia mashaka. Na je walipokuuliza kuwa ulipoingia ndani ulifanya nini ulisemaje?’ akaniuliza swali jingine.

‘Niliwaambia kuwa nilipoingia ndani,cha kwanzakuona ni tundu kwenye kiyoo, na kuvunjika na pale chini kuonekana vipande vya kiyoo, …na baadaye nikagundua kuwa kuna mtu yupo sakafuni,….kama nilivyowaelezea mwanzoni, na pia huyu mtu alikuwa akanionyesha kwa kidole kule kwenye kabati la vitabu,….sikuona kitu,….ila wakati nasubiri polisi waje, nikaanza kupekua huko kwenye kabati aliponionyeshea, …na hapo nikagundua kibksi, chenye jina langu, labda ndicho alichokuwa akinionyeshea, na kilikuwa kimeandikwa  jina langu,….’nikasema.

‘Hapo pia wamekutiliwa mashaka, maana inaonyesha kulikuwa na kitu wewe unakitafuta, hasa hilo boksi, ulipomuona yupo kwenye hali mbaya, au ….lengo lako lilikuwa ni hilo boksi, kwahiyo ukamtishia kuwa akuonyeshe hilo boksi au umulizie….kwa ujumla wao wanahisi kuwa kunajambo, hapo kati kati, kati yako na huyu mwanadada na hilo boksi, na wanahisi kuwa kwenye hicho kiboksi kuna kitu muhimu sana kwako,bado wanalichunguza….’akasema wakili mwanadada.

‘Lakini ngoja nikuulize swali, kama ungelikuwa wewe seehmu yangu ungelifanyaje, maana tuzungumze katika hali halisi, wewe mtu kakuita uende kwake, na umefika umeikuta hali kama hiyo na zaidi kakuonyeshea hivyo kwa kidole, utasema hapana ngoja mpaka polsi waje…, hata hivyo niligundua vitu ambavyo sikutaka polisi wavione…nikavificha….’nikasema na hapo wakili akashituka.

‘Eti nini….ulificha kitu gani, ..na ole wako polisi wakigundua hilo….’akasema wakili kwa mashaka.

‘Aaah, naogopa hata kusikia kauli hiyo, yaani ningekuambia usiniambie jambo hilo,lakini kwa ajili ya utafiti wangu,inabidi nilijue, lakini….ooh,…..hapana kama inawezekana nipe hivyo vitu nikawakabidhi wenyewe…’akasema wakili mwanadada.

‘Una uhakika kuwa nikikupa utawakabidhi wenyewe, una uhakika kweli na hilo…na nani utampa ambaye unamwamini…ndio huyo wakili wenu, ambaye keshaumwa na nyoka,….na huenda bado yupo mikononi mwa hawo watu kwa kashifa iliyomkuta, …wewe huoni hilo, ….ndio maana anachelea kusimamisa kwenye hizo kesi, bado wanamtishia kuwa ukisimama tutakuumbua, wewe huoni hilo …?’ nikamwambia huku nikimwangalia kwa wasiwasi.

‘Unajua yeye anajua sheria, usimuone hivyo, na wakati mwingine, unaogoap usije ukashindwa kusimamaia haki kwa jambo fulani, inabidi kidogo ukae pembeni, mfano ni kesi ya mkeo, na wewe ni wakili ,hutaweza kuisimamia vyema,…hapo inabidi umpe mtu mwingine aisimamie,….na mambo mengine juu yake ni tuhuma tu,….’akasema na kutulia kama vile anawaza jambo,halafu akasema;

‘Kiutaratibu yeye ndiye anayestahili kupewa hivyo vitu, ujue kwa sasa ndiye  mkuu wetu wa kitengo cha sheria, ….’akasema huku akikunja uso.

‘Siwezi kumpa mtu kama yule,hata huyo mkuu wenu….siwezi siwezi,…., nimekuambia wewe tu kwasababu ni mtu ninayekuamini, vinginevyo ningelikaa kimiya….’nikasema kwa msisitizo.

`Ujue hivyo vitu ulivyochukua ni sehemu ya vitu vya ushahidi,…..sheria hapo itakubana sana,….hutakiwi kuficha kitu chochote kwenye tukio la kesikama hizi , unavuruga ushahidi na utachukuliwa kama mshukiwa muhimu wa hiyo kesi…..’akasema wakili mwanadada.

‘Nalijua hilo, lakini….unakumbuka siku ile Kimwana alipouliwa…..wewe hukuchukua vitu fulani kutoka kwake, hukuchukua simu na saa yake,….mbona hukuikabidhi kama viti muhimu kwenye hiyo kesi…hujakiuka sheria hapo..?’nikamuliza na yeye akaniangalia kwa uso wa wasiwasi,…..

‘Mimi najua kwanini nilifanay hivyo, kisheria….na ningejitetea kisheria, je Wewe?,…. hebu achana na hilo….hata hivyo vilitoweka kiajabu vile vitu, nilichukua nikitaka nimkabidhi mtu ninayemuaminii, sikuwa na uhakika na wale watu waliofika pale na nilishaanza kuwashuku watu kwenye kitengo chetu, kuna watu nilishaanza kuwatilia mashaka,…lakini cha ajabu nilikuta vyote havipo….na hili linaniweka katika hali ngumu, kuwa kuna mtu ndani ya kitengo chetu, anatumiwa,aua anahusika….’akasema wakili mwanadada.

‘Unajua niliviona kwenye hilo boski …..sasa na hiyo simu, halafu vimewekwa kwenye kimfuko cha plastiki kimeandikwa juu Kimwana, ….’akasema.

‘Niliandika mimi hivyo….siku nilipovichukua,….’akasema wakili mwanadada.

‘Oooh,sasa vimefikaje kwa huyu mwanadada, mbona mambo ya ajabu…?’nikauliza kwa mshangao.

‘Ndio maana nsemakuna mtu ndani ya kitengo chetu cha sheria anatumiwa, ….na nimejaribu kila njia nimeshindwa kumgundua, maana vitu kama hivi hutakiwi kukisia tu, unahitajiak uwe na ushahidi uliokamilika,…na mtu kama huyo amejiandaa vya kutosha….’akasema mwanadada na akaniuliz akuna viti gani vingine nilivyovichukua, nikasema;

‘Kuna nakala ya ile picha yangu ya utotoni….na picha kama ile niliyomkuta yule dada aliyeidondosha kule siku ile ,…yule aliyekuwa akinikimbia….na vyote hivyo nimevificha…, pia nilikuta mkanda wa CD’s…ulikuwa na jina langu,…nahisi una mambo yangu,…..mmh, ambayo nahisi ni yale waliyokuwa wakinituma akina Kimwana na mama Docta, nikayafanye kwa manufaa yao,….’nikatulia hapo kidogo nikiwaza jambo.

‘Nikuambie ukweli sikupenda yale mambo yaje kujulikana katika familia yangu, maana wao ndio walionilazimisha, kufanya hayo yaliyopo humo, nikataka kuuharibu pale pale, lakini muda ulikuwa hautoshi,…na cha ajabu nilikuta baadhi ya barua zangu za ujanani, nilizokuwa nikiandikiana na yule msichana wa kijijini…’nikatulia nilipoona wakili mwanadada akiniangalia kwa mshangao.

‘Eti nini, barua za ujanani, ulizokuwa ukimwandikia nani, ….oh, na umeviweka wapi hivyo vitu, kweli nilitakiwa nivione kabala hawajavchukua hawa watu?’ akaniuliza.

‘Hizo barua ni zile nilizokuwa nikimwandikia yule binti wa kijijini, yule niliyejuana naye tukiwa watoto,..na kwasasa tafadhali, …. usitake kujua wapi nimeviweka, sitaki kabisa kumpa mtu hivyo vitu, ….maana kuna vitu vynagu muhimu sana,….vile nilivyokuwa navyo vimeshapotea, sasa nimevipata hivyo, itakuwa kumbukumbu yangu,….’nikasema.

‘Navihitaji haraka,….hiyo ni kwa usalama wako, …. inabidi unielekeze wapi vilipo,….na hakuna vitu vingine?’ akauliza huku akionyesha uso wa mashaka..

‘Nilivyochukua ni hivyo kwa haraka, unajua lile boksi lilikuwa na vitu vingi sasa, na jinsi ilivyokuwa sikuweza kuamua kwa haraka, kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha muda ulikuwa hautoshi,….maana baadaye polisi waliingia, na mimi nikalirudisha lile boksi pale pale….’nikasema kwa harakaharaka.

‘Kwa ujumla hivyo vitu vyote unatakiwa uvikabidhi kwa polisi, na kama wataona vinahitajika kuhifadhiwa kwa minajili ya kulinda hadhi ya kibindamu, watafanya hivyo, lakini kwa kibali maalum,. Hatujajua hatimaya huyo mtu, maana hali yake ni tete sana, nilipokwenda kumuona, ….oh,mungu mwenywe ndiye ajuaye, dada wa watu yupo kwenye hali mbaya sana…’akasema wakili mwanadada kwa sauto ya huruma.

‘Oh, nilitaka niende nikamuone,lakini hawa jamaa hawaniruhusu….na mmoja ananidhihaki na kusema kuwa nataka kwenda kummalizia….’nikasema huku nikiwa nimekunja uso kwa hasira.

 ‘Unajua kinachowashangaza ni kuwa,kila anapopata fahamu anakutaja wewe, hili ni mojawapo ya jambo linalowafanya polisi wakushikilie, ….kwanini, awe anakutaja wewe, anaweza akawa anakutaja wewe kama kukushitakia kuwa wewe ndiye uliyemfanyia hivyo, au anakutaja wewe kwa nia njema, labda ana ujumbe anataka kukufiksihia wewe,hatuji,….’aliposema hivyo akanitia simazi, nikawa nawaza mengi, na nilishindwa hata cha kuongea, nikabakia kimiya.

‘Na huenda nikasafiri….’akasema.

‘Ukasafiri…!’ nikasema kwa mshangao ,halafu nikaongezea kusme;

‘Sasa ukisafiri mimi itakuwaje hapa,ina maana mimi nitakaa  huku rumande mpaka lini…je huwezi ukawaambia waniachie kwa dhamana?’nikalalamika.

‘Itakuwa safari ya siku mbili, sizani kuwa nitakaa siku nyingi…nia na lengo ni mamaDocta, na maeongezi yangu hayahitaji ufuatiliaji wa jambo jingine,…na kuhusa dhamana yako, utapata tu,…kwa hali ilivyo siwezi kuwaingilia kwa sasa,i kuna mambo ya kisheria yanayohitajiwa kuwekwa sawa…lazimakuwa na hatua fulani ya uchunguzi kabla hawajaamua kukuachia kwa dhamana, hata mimi siwezi kuyaingilia hayo kwa sasa’akasema huyo mwanadada.

‘Kwahiyo unasema unasafiri, unakwenda wapi?’ nikamuuliza

‘Nakwenda,hapo jirani tu, …Kenya…..nia na lengo langu ni kukutana na huyo anayejiita Docta mama, uzuri ni kuwa nimebahatisha kuongea naye kwenye simu, …na kwa kweli huwezi amini kuwa ni yule alikuwa hapa, anangea vyema kabisa na akakubali nimtembelee, maana kwa muda huo nikiwa naongea naye alikuwa kwenye mikutano yake, akasema kama namuhitaji kwa maongezi ni vyema nikutane naye….’akasema.

‘Unasema Docta Mama…..?’ nikasema kwa kuhamaki, halafu baadaye nikatuliza hamaki zangu na kusema taratibu;

‘Mimi huyo mama sitaki hata kumsikia, yaani hapana,hata sikuelewi, wa nini huyo,….unajua ndiye aliyesababisha yote haya…unamtakia nini..?’ nikauliza kwa hasira.

‘Kama ndiye aliyesababisha yote haya,basi ni muhimu nikakutana naye, najua nitapata mengi sana, hasa kuhusu Kimwana, na hawo wanawake wengine watatu, ambao wamekuwa kama miujiza, maana hawa wengine wawili wametoweka kiajabu,tumebakiwa na huyu ambaye naye ni mahututi…’akasema wakili mwanadada.

‘Na kweli hivi wale wakina dada wengine wapo wapi maana wote wana tabia moja, ya kuwa na manywele mengi,….lakini sura zao tofauti….ila nimegundu kitu fulani,kuwa tembea yao, inafanana, na hata ukichunguza viwiliwili vyao havitofautiani sana, labda mavazi yao na..na..usoni, kuna tofautia nikimaanisha sura zao, hasa usoni naona kuna utofauti,….lakini macho….unajau kuna kitu nilitaka kukuambia, mbona macho yao kama yanafanana….’nikasema nikiwaza.

‘Mhh, hilo sikuligundua maana sikuweza kuwaona hawo wengine kwa karibu sana..zaidi ya huyo  mahututi ambaye nimekuwa nikikutana naye mara kwa mara, hawo wengine, zaidi nimesikia kutoka kwako…’akasema wakili.

‘Kwahiyo huko Kenya unakwenda  kikazi au ndio huo utafiti wako…?’ nikamuuliza.

‘Yote mawili, ….lakini zaidi ni kutokana an utafiti wangu, kwanini akatoweka, na najua atakuwa anawafahamu sana Kimwana na huyu mwanadada tuliye naye hospitali, nitawaomba wakuruhusu ukamuone huyo mgonjwa, nilitaka niwepo ukimuona, lakini kama atazindukana na kuwa katika hali njema nimewaomba uende ukamuone, ili tujue ni kwanini anakutaja wewe.

‘Oh, isije nikawa ni mtu wake wa mwisho kuniona, naogopa sana hilo, maana watu wakiwa katika hiyo hali na unasikia wanamuhitaji mtu fulani aje, …..inakuwa kama vile huyo mtu nayehitajiwa ndiye  mtu wa kukamilisha idadi ya watu anaotakiwa kuwaona kabla hajafa...naomba sana isiwe hivyo maana itanitesa sana katika maisha yangu,….’nikasema na kujaribu kuikumbuka sura ya huyo mwanadada. Lakini ilikuwa haiji akilini, naona sura tatu tofauti, nikasema;

‘Kwahiyo huyo Docta mama hukuwahi kumuulizia lolote kuhusu haya yaliyotokea hapa?’ nikauliza

‘Nilimuulizia akawa kama anashangaa, na kudai kuwa hajui lolote ninaloongea, na ndio akasema angehitaji kukutana na mimi ,kwani namuuliza mambo mageni kwake,…..’akasema wakili dada.

‘Lazima atasema hivyo,mjanja sana yule mama, elimu yake, anaittumia sivyo ndivyo…unatakiwa ujiandae sana, maana unakwenda kukutana na mjanja,nasikia anajua sana hula tabia za watu, yeye kayasoema hayo kiundani,….’nikasema.

‘Tutaona, hata mimi nimeyasomea hay ohayo, na zaidi ya hayo naijua sheria….nilitka kabla ya kuondoak nikaonane na huyo mwanadada huko hospiatalini,…’akasema huku akiangalia saa yake.

‘Hata mimi natamani nimuone, sijui kwanini natamani sana nimuone, niongee naye, nijue aliniitia nini, na zaidi ya vile vitu vilivyokuwa kwenye hilo boksi, kuna taarifa gani kuhusiana navyo,…angala hata kama hajazindukana natamanini tu, niwe naye karibu, nimjue vyema , niione sura yake vyema….moyo wangu unamuwaza sana yeye kwa hivi sasa….’nikasema.

‘Kwa kifupi umempendahuyo mwanadada,hata kama humjui…au?.’akasema wakili na kucheka.

‘Sijui kama ni hivyo….szani kuwa ni kuhusu kupenda,….sijui, …’nikasema na dada wakili akainuka pale alipokuwa amekaa, huku akiwa kajawa na tabasamu mdomoni, na huku akitingisha kichwa na kusema;

‘Wanaume bwana. ..katu, hamueleweki.'.

NB. Jamani ndio hivyo tena, wanasema cha mwenzako `mavi'.....samahani kwa kutumia neno hilo, ila ni namna ya kutaka kukufikishia ujumbe.

 WAZO LA LEO: Siku zote haziwi sawa, maisha kama ilivyo safari kuna kushuka na kupenda,...kuna mabonde na mito,yote yachukulie kama changamoto za kimaisha. 
 Kwa wanandoa msikate tamaa pale mnaposigishana , mjue kuwa kama kwenu kunafuka moshi kwa wengine kunawaka moto, kama sio kuteketea kabisa, ...lakini yote ni maisha, ongeeni, jadilianeni na tafuteni tatizo lipo wapi, mtayashinda majaribu...


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Tupo pamoja kwa saana mkuu

Anonymous said...

Kaka MUNGU aendelee kukutunza,una maneno ya kutia moyo sana

emuthree said...

Anony wa may 23 2012 6.06 PM, na mdogo wangu hapo juu, nashukuruni kuwa nami, tuendelee kuwa na moyo huo huo, TUPO PAMOJA