Nilikuwa nimekaa kwenye kona ya kile chumba cha mahabusu, huku nimejikunja kama mkiwa. Kwakweli ilikuwa imeniuma na moyoni nilikuwa nimekasirika sana,...hapo nilikuwa mahabusu tu, kichwani mwangi nilikuwa nimepanga kuwa nitagoma kabisa kupelekwa huko Segerea au Ukonga, sikubali kupelekwa tena huko.
Kwa ujumla sikuamini kuwa
nimefikishwa mahala kama hapa tena, hata baada ya kuwa mwangalifu na maswala ya kuvunja sheria, lakini hujafa hujaumbika, ....nikiwa nimekunjata nikawa namumimba mungu, nisije nikapelekwa huko jela,…iliniuma
sana kuona kuwa dunia hii haina wema,yaani kujitolea kwangu huko,kuwafahamisha
polisi kuhusu hilo tukio ndio ninashikiliwa eti kwa kuisadia polisi.
‘Usijali hizi ni taratibu za kawaida, utatolewa, na
wamekushikilia kwa sababu ya maelezo yako uliyowapa, ilinakuweka mahali ambapo
yoyote angeliweza kukuhisi kuwa uanahusika. Na linapotokea jambo kama hili la
kesi za jinai, kama hii, ukatiliwa mashaka ni lazima wakushikilie kwa ajili ya kuisaidia
polisi.
‘Kwa vipi wanahisi ni mimi na maelezo gani niliyotoa yanayoniweka
kwenye mashaka..?’ nikamuuliza.
‘Ukumbuke kuwa huyo mtu kauliwa kwa silaha na muuaji anajua
kulenga shabaha, wewe alipokuuliza mkuu kuwa unaweza kutumia silaha ulisemaje?’
akamuuliza dada wakili.
‘Nilimuambia ukweli,…nilimwambia ndio najua kutumia
silaha,maana niliwahi kupitia mujibu wa sheria, kule tunafundishwa yote,
nakumbuka tulipopelekwa uchaka, huko tulifundishwa mbinu zote za kivita na
kwenye shabaha nilikuwa mtu wa kwanza, sikukosa hata moja…..niliizoea silaha
utafikiri nilizaliwa nayo….’nikasema kwa majisifu.
‘Sasa hayo maelezo yako yanakuweka pabaya, sio kwamba ni
vibaya kusema ukweli, lakini kwa fikira zao, na tetesi walizo nazo polisi na
hata kwa mtizamo wa mtu yoyote kwa haraka haraka, muuaji alikuwa anajua vyema
kulenga shabaha….na wewe unajua kulenga vyema shabaha. Na je alipokuuliza
swali, kuwa ulipoingia humu ndani ulifanyeje, ulimjibu vipi…?’ akaniuliza dada
wakili.
‘Unajua kuna mambo mengine unajifunza kutokana na uzoefu,
mimi kwa ajili ya kujindaa kuja kufanya kazi kwenye ofisi yako mpya mwakani,nimekuwa
nikihudhuria mafunzo ya sheria na upelelezi, na huko nimejifunza mambo mengi ya
kujihami na kujilinda,….kuna sehemu tumefundishwa kuwa unapofika kwenye tukio
unalolitilia mashaka….’nikatulia kidogo pale nilipomuona dada wakili akionyesha
uso wa furaha.
‘Endela kuongea, mbona unakatisha ameno,…nimetabasamu
kwasababu ya kusikia hivyo, kujiandaa kwa ajili ya ofisi yangu,…., safi
kabisa,nashukuru kusikia hivyo, haya niambie umejifunza nini huko ambacho
umekitumia kwenye hili tukio?’ akaniuliza.
‘Unapofika sehemu yenye mashaka, ni vyema ukachunga kuacha
alama za vidole, sasa mimi nilipofika hapo kweny hiyo nyumba,…niliingiwa na
wasiwasi, hasa pale nilipogonga mlango na kuona kupo kimiya, nilichofanya ni
kuvaa soksi,…unajua nilichofanya ni kuvua soksi zangu za miguuni, na kuzivaa
mkononi, kuogopa kuacha alama za vidole….’nikasema bila wasi wasi.
‘Hapo unafikiri polisi wataamini kuwa ulifanya hivyo kwa
ajili ya kujihami,…. swali kubwa kwao, ni je ulijuaje kuwa kuna tatizo, mpaka
uvae hizo soksi,….lazima hapo watakutilia mashaka. Na je walipokuuliza kuwa
ulipoingia ndani ulifanya nini ulisemaje?’ akaniuliza swali jingine.
‘Niliwaambia kuwa nilipoingia ndani,cha kwanzakuona ni tundu
kwenye kiyoo, na kuvunjika na pale chini kuonekana vipande vya kiyoo, …na
baadaye nikagundua kuwa kuna mtu yupo sakafuni,….kama nilivyowaelezea mwanzoni,
na pia huyu mtu alikuwa akanionyesha kwa kidole kule kwenye kabati la vitabu,….sikuona
kitu,….ila wakati nasubiri polisi waje, nikaanza kupekua huko kwenye kabati
aliponionyeshea, …na hapo nikagundua kibksi, chenye jina langu, labda ndicho
alichokuwa akinionyeshea, na kilikuwa kimeandikwa jina langu,….’nikasema.
‘Hapo pia wamekutiliwa mashaka, maana inaonyesha kulikuwa na
kitu wewe unakitafuta, hasa hilo boksi, ulipomuona yupo kwenye hali mbaya, au
….lengo lako lilikuwa ni hilo boksi, kwahiyo ukamtishia kuwa akuonyeshe hilo
boksi au umulizie….kwa ujumla wao wanahisi kuwa kunajambo, hapo kati kati, kati
yako na huyu mwanadada na hilo boksi, na wanahisi kuwa kwenye hicho kiboksi kuna
kitu muhimu sana kwako,bado wanalichunguza….’akasema wakili mwanadada.
‘Lakini ngoja nikuulize swali, kama ungelikuwa wewe seehmu
yangu ungelifanyaje, maana tuzungumze katika hali halisi, wewe mtu kakuita
uende kwake, na umefika umeikuta hali kama hiyo na zaidi kakuonyeshea hivyo kwa
kidole, utasema hapana ngoja mpaka polsi waje…, hata hivyo niligundua vitu
ambavyo sikutaka polisi wavione…nikavificha….’nikasema na hapo wakili akashituka.
‘Eti nini….ulificha kitu gani, ..na ole wako polisi
wakigundua hilo….’akasema wakili kwa mashaka.
‘Aaah, naogopa hata kusikia kauli hiyo, yaani ningekuambia usiniambie
jambo hilo,lakini kwa ajili ya utafiti wangu,inabidi nilijue, lakini….ooh,…..hapana
kama inawezekana nipe hivyo vitu nikawakabidhi wenyewe…’akasema wakili
mwanadada.
‘Una uhakika kuwa nikikupa utawakabidhi wenyewe, una uhakika
kweli na hilo…na nani utampa ambaye unamwamini…ndio huyo wakili wenu, ambaye
keshaumwa na nyoka,….na huenda bado yupo mikononi mwa hawo watu kwa kashifa
iliyomkuta, …wewe huoni hilo, ….ndio maana anachelea kusimamisa kwenye hizo kesi,
bado wanamtishia kuwa ukisimama tutakuumbua, wewe huoni hilo …?’ nikamwambia
huku nikimwangalia kwa wasiwasi.
‘Unajua yeye anajua sheria, usimuone hivyo, na wakati
mwingine, unaogoap usije ukashindwa kusimamaia haki kwa jambo fulani, inabidi
kidogo ukae pembeni, mfano ni kesi ya mkeo, na wewe ni wakili ,hutaweza
kuisimamia vyema,…hapo inabidi umpe mtu mwingine aisimamie,….na mambo mengine
juu yake ni tuhuma tu,….’akasema na kutulia kama vile anawaza jambo,halafu
akasema;
‘Kiutaratibu yeye ndiye anayestahili kupewa hivyo vitu, ujue
kwa sasa ndiye mkuu wetu wa kitengo cha
sheria, ….’akasema huku akikunja uso.
‘Siwezi kumpa mtu kama yule,hata huyo mkuu wenu….siwezi
siwezi,…., nimekuambia wewe tu kwasababu ni mtu ninayekuamini, vinginevyo
ningelikaa kimiya….’nikasema kwa msisitizo.
`Ujue hivyo vitu ulivyochukua ni sehemu ya vitu vya
ushahidi,…..sheria hapo itakubana sana,….hutakiwi kuficha kitu chochote kwenye
tukio la kesikama hizi , unavuruga ushahidi na utachukuliwa kama mshukiwa
muhimu wa hiyo kesi…..’akasema wakili mwanadada.
‘Nalijua hilo, lakini….unakumbuka siku ile Kimwana
alipouliwa…..wewe hukuchukua vitu fulani kutoka kwake, hukuchukua simu na saa
yake,….mbona hukuikabidhi kama viti muhimu kwenye hiyo kesi…hujakiuka sheria
hapo..?’nikamuliza na yeye akaniangalia kwa uso wa wasiwasi,…..
‘Mimi najua kwanini nilifanay hivyo, kisheria….na
ningejitetea kisheria, je Wewe?,…. hebu achana na hilo….hata hivyo vilitoweka
kiajabu vile vitu, nilichukua nikitaka nimkabidhi mtu ninayemuaminii, sikuwa na
uhakika na wale watu waliofika pale na nilishaanza kuwashuku watu kwenye
kitengo chetu, kuna watu nilishaanza kuwatilia mashaka,…lakini cha ajabu
nilikuta vyote havipo….na hili linaniweka katika hali ngumu, kuwa kuna mtu
ndani ya kitengo chetu, anatumiwa,aua anahusika….’akasema wakili mwanadada.
‘Unajua niliviona kwenye hilo boski …..sasa na hiyo simu,
halafu vimewekwa kwenye kimfuko cha plastiki kimeandikwa juu Kimwana,
….’akasema.
‘Niliandika mimi hivyo….siku nilipovichukua,….’akasema
wakili mwanadada.
‘Oooh,sasa vimefikaje kwa huyu mwanadada, mbona mambo ya
ajabu…?’nikauliza kwa mshangao.
‘Ndio maana nsemakuna mtu ndani ya kitengo chetu cha sheria
anatumiwa, ….na nimejaribu kila njia nimeshindwa kumgundua, maana vitu kama
hivi hutakiwi kukisia tu, unahitajiak uwe na ushahidi uliokamilika,…na mtu kama
huyo amejiandaa vya kutosha….’akasema mwanadada na akaniuliz akuna viti gani
vingine nilivyovichukua, nikasema;
‘Kuna nakala ya ile picha yangu ya utotoni….na picha kama ile
niliyomkuta yule dada aliyeidondosha kule siku ile ,…yule aliyekuwa akinikimbia….na
vyote hivyo nimevificha…, pia nilikuta mkanda wa CD’s…ulikuwa na jina langu,…nahisi
una mambo yangu,…..mmh, ambayo nahisi ni yale waliyokuwa wakinituma akina
Kimwana na mama Docta, nikayafanye kwa manufaa yao,….’nikatulia hapo kidogo
nikiwaza jambo.
‘Nikuambie ukweli sikupenda yale mambo yaje kujulikana
katika familia yangu, maana wao ndio walionilazimisha, kufanya hayo yaliyopo
humo, nikataka kuuharibu pale pale, lakini muda ulikuwa hautoshi,…na cha ajabu
nilikuta baadhi ya barua zangu za ujanani, nilizokuwa nikiandikiana na yule
msichana wa kijijini…’nikatulia nilipoona wakili mwanadada akiniangalia kwa mshangao.
‘Eti nini, barua za ujanani, ulizokuwa ukimwandikia nani, ….oh,
na umeviweka wapi hivyo vitu, kweli nilitakiwa nivione kabala hawajavchukua
hawa watu?’ akaniuliza.
‘Hizo barua ni zile nilizokuwa nikimwandikia yule binti wa
kijijini, yule niliyejuana naye tukiwa watoto,..na kwasasa tafadhali, ….
usitake kujua wapi nimeviweka, sitaki kabisa kumpa mtu hivyo vitu, ….maana kuna
vitu vynagu muhimu sana,….vile nilivyokuwa navyo vimeshapotea, sasa nimevipata hivyo,
itakuwa kumbukumbu yangu,….’nikasema.
‘Navihitaji haraka,….hiyo ni kwa usalama wako, …. inabidi
unielekeze wapi vilipo,….na hakuna vitu vingine?’ akauliza huku akionyesha uso
wa mashaka..
‘Nilivyochukua ni hivyo kwa haraka, unajua lile boksi
lilikuwa na vitu vingi sasa, na jinsi ilivyokuwa sikuweza kuamua kwa haraka,
kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha muda ulikuwa hautoshi,….maana baadaye polisi
waliingia, na mimi nikalirudisha lile boksi pale pale….’nikasema kwa
harakaharaka.
‘Kwa ujumla hivyo vitu vyote unatakiwa uvikabidhi kwa polisi,
na kama wataona vinahitajika kuhifadhiwa kwa minajili ya kulinda hadhi ya
kibindamu, watafanya hivyo, lakini kwa kibali maalum,. Hatujajua hatimaya huyo
mtu, maana hali yake ni tete sana, nilipokwenda kumuona, ….oh,mungu mwenywe
ndiye ajuaye, dada wa watu yupo kwenye hali mbaya sana…’akasema wakili
mwanadada kwa sauto ya huruma.
‘Oh, nilitaka niende nikamuone,lakini hawa jamaa
hawaniruhusu….na mmoja ananidhihaki na kusema kuwa nataka kwenda
kummalizia….’nikasema huku nikiwa nimekunja uso kwa hasira.
‘Unajua
kinachowashangaza ni kuwa,kila anapopata fahamu anakutaja wewe, hili ni
mojawapo ya jambo linalowafanya polisi wakushikilie, ….kwanini, awe anakutaja
wewe, anaweza akawa anakutaja wewe kama kukushitakia kuwa wewe ndiye
uliyemfanyia hivyo, au anakutaja wewe kwa nia njema, labda ana ujumbe anataka
kukufiksihia wewe,hatuji,….’aliposema hivyo akanitia simazi, nikawa nawaza
mengi, na nilishindwa hata cha kuongea, nikabakia kimiya.
‘Na huenda nikasafiri….’akasema.
‘Ukasafiri…!’ nikasema kwa mshangao ,halafu nikaongezea
kusme;
‘Sasa ukisafiri mimi itakuwaje hapa,ina maana mimi nitakaa huku rumande mpaka lini…je huwezi ukawaambia
waniachie kwa dhamana?’nikalalamika.
‘Itakuwa safari ya siku mbili, sizani kuwa nitakaa siku
nyingi…nia na lengo ni mamaDocta, na maeongezi yangu hayahitaji ufuatiliaji wa
jambo jingine,…na kuhusa dhamana yako, utapata tu,…kwa hali ilivyo siwezi
kuwaingilia kwa sasa,i kuna mambo ya kisheria yanayohitajiwa kuwekwa
sawa…lazimakuwa na hatua fulani ya uchunguzi kabla hawajaamua kukuachia kwa
dhamana, hata mimi siwezi kuyaingilia hayo kwa sasa’akasema huyo mwanadada.
‘Kwahiyo unasema unasafiri, unakwenda wapi?’ nikamuuliza
‘Nakwenda,hapo jirani tu, …Kenya…..nia na lengo langu ni
kukutana na huyo anayejiita Docta mama, uzuri ni kuwa nimebahatisha kuongea
naye kwenye simu, …na kwa kweli huwezi amini kuwa ni yule alikuwa hapa, anangea
vyema kabisa na akakubali nimtembelee, maana kwa muda huo nikiwa naongea naye
alikuwa kwenye mikutano yake, akasema kama namuhitaji kwa maongezi ni vyema
nikutane naye….’akasema.
‘Unasema Docta Mama…..?’ nikasema kwa kuhamaki, halafu baadaye
nikatuliza hamaki zangu na kusema taratibu;
‘Mimi huyo mama sitaki hata kumsikia, yaani hapana,hata
sikuelewi, wa nini huyo,….unajua ndiye aliyesababisha yote haya…unamtakia
nini..?’ nikauliza kwa hasira.
‘Kama ndiye aliyesababisha yote haya,basi ni muhimu
nikakutana naye, najua nitapata mengi sana, hasa kuhusu Kimwana, na hawo
wanawake wengine watatu, ambao wamekuwa kama miujiza, maana hawa wengine wawili
wametoweka kiajabu,tumebakiwa na huyu ambaye naye ni mahututi…’akasema wakili
mwanadada.
‘Na kweli hivi wale wakina dada wengine wapo wapi maana wote
wana tabia moja, ya kuwa na manywele mengi,….lakini sura zao tofauti….ila
nimegundu kitu fulani,kuwa tembea yao, inafanana, na hata ukichunguza
viwiliwili vyao havitofautiani sana, labda mavazi yao na..na..usoni, kuna
tofautia nikimaanisha sura zao, hasa usoni naona kuna utofauti,….lakini
macho….unajau kuna kitu nilitaka kukuambia, mbona macho yao kama yanafanana….’nikasema
nikiwaza.
‘Mhh, hilo sikuligundua maana sikuweza kuwaona hawo wengine
kwa karibu sana..zaidi ya huyo mahututi ambaye
nimekuwa nikikutana naye mara kwa mara, hawo wengine, zaidi nimesikia kutoka
kwako…’akasema wakili.
‘Kwahiyo huko Kenya unakwenda kikazi au ndio huo utafiti wako…?’
nikamuuliza.
‘Yote mawili, ….lakini zaidi ni kutokana an utafiti wangu,
kwanini akatoweka, na najua atakuwa anawafahamu sana Kimwana na huyu mwanadada
tuliye naye hospitali, nitawaomba wakuruhusu ukamuone huyo mgonjwa, nilitaka
niwepo ukimuona, lakini kama atazindukana na kuwa katika hali njema nimewaomba
uende ukamuone, ili tujue ni kwanini anakutaja wewe.
‘Oh, isije nikawa ni mtu wake wa mwisho kuniona, naogopa
sana hilo, maana watu wakiwa katika hiyo hali na unasikia wanamuhitaji mtu
fulani aje, …..inakuwa kama vile huyo mtu nayehitajiwa ndiye mtu wa kukamilisha idadi ya watu anaotakiwa
kuwaona kabla hajafa...naomba sana isiwe hivyo maana itanitesa sana katika
maisha yangu,….’nikasema na kujaribu kuikumbuka sura ya huyo mwanadada. Lakini
ilikuwa haiji akilini, naona sura tatu tofauti, nikasema;
‘Kwahiyo huyo Docta mama hukuwahi kumuulizia lolote kuhusu
haya yaliyotokea hapa?’ nikauliza
‘Nilimuulizia akawa kama anashangaa, na kudai kuwa hajui
lolote ninaloongea, na ndio akasema angehitaji kukutana na mimi ,kwani
namuuliza mambo mageni kwake,…..’akasema wakili dada.
‘Lazima atasema hivyo,mjanja sana yule mama, elimu yake,
anaittumia sivyo ndivyo…unatakiwa ujiandae sana, maana unakwenda kukutana na
mjanja,nasikia anajua sana hula tabia za watu, yeye kayasoema hayo
kiundani,….’nikasema.
‘Tutaona, hata mimi nimeyasomea hay ohayo, na zaidi ya hayo
naijua sheria….nilitka kabla ya kuondoak nikaonane na huyo mwanadada huko
hospiatalini,…’akasema huku akiangalia saa yake.
‘Hata mimi natamani nimuone, sijui kwanini natamani sana nimuone,
niongee naye, nijue aliniitia nini, na zaidi ya vile vitu vilivyokuwa kwenye
hilo boksi, kuna taarifa gani kuhusiana navyo,…angala hata kama hajazindukana
natamanini tu, niwe naye karibu, nimjue vyema , niione sura yake vyema….moyo
wangu unamuwaza sana yeye kwa hivi sasa….’nikasema.
‘Kwa kifupi umempendahuyo mwanadada,hata kama humjui…au?.’akasema
wakili na kucheka.
‘Sijui kama ni hivyo….szani kuwa ni kuhusu kupenda,….sijui,
…’nikasema na dada wakili akainuka pale alipokuwa amekaa, huku akiwa kajawa na
tabasamu mdomoni, na huku akitingisha kichwa na kusema;
‘Wanaume bwana. ..katu, hamueleweki.'.
NB. Jamani ndio hivyo tena, wanasema cha mwenzako `mavi'.....samahani kwa kutumia neno hilo, ila ni namna ya kutaka kukufikishia ujumbe.
WAZO LA LEO: Siku zote haziwi sawa, maisha kama ilivyo safari kuna kushuka na kupenda,...kuna mabonde na mito,yote yachukulie kama changamoto za kimaisha.
Kwa wanandoa msikate tamaa pale mnaposigishana , mjue kuwa kama kwenu kunafuka moshi kwa wengine kunawaka moto, kama sio kuteketea kabisa, ...lakini yote ni maisha, ongeeni, jadilianeni na tafuteni tatizo lipo wapi, mtayashinda majaribu...
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Tupo pamoja kwa saana mkuu
Kaka MUNGU aendelee kukutunza,una maneno ya kutia moyo sana
Anony wa may 23 2012 6.06 PM, na mdogo wangu hapo juu, nashukuruni kuwa nami, tuendelee kuwa na moyo huo huo, TUPO PAMOJA
Post a Comment