‘Msomali, unahitajika kuna mgeni wako…’ nikasikia nikiitwa,
nikainuka haraka, nikijua kuwa mwadada wakili kesharudi, lakini cha ajabu
nilikutana na mtu mwingine tofauti,..mtu ambaye sikutegemea kabisa kuwa
nitakutana naye, .
‘Tangu ufarakane na familia kwa ajili ya mwanamke wako,
nimekuwa sipati uzingizi, hata safari ya kuja huku sikuitarajia, na hata sikuwaambia
wazazi wako kuwa nakuja kwako, nimeagana kuwa nafuatilia mambo yangu ya
kibiashara, najua kama ningewaambia kuwa nakuja kwako, wangelipinga kwa nguvu
zao zote,….’akasema .
Niliposikia hivyo moyo wangu uliniuma sana, sikutaka iwe
hivyo, kwani kwa ujumla nawapenda sana wazazi wangu, na sikutajia kuwa itafika
muda, niwe mbali nao, nikaimana chini huku moyoni nikitubu na kuomba kwa mola
anijalia nitoke pale nakiwaone. Nikasema;
‘Na mimi sikutaka kuwasumbua kuhusiana na maswali yangu,
ambayo najua hamsitahili kuhusishwa, haya nimejitakia mwenyewe, naona nipambane
nayo mwenyewe…hadi mwisho wake, sioni kuwa itashindikana, lakini , nataka
nionane na wazazi wangu, …’nikasema.
‘Unalosema linaweza kuwa sawa, lakini ukumbuke kuwa kuna
wazazi wako wanasononeka, na wazazi kwa mtoto haifutiki kama wangali hai, kila
siku inayopita bilakusikia lolote kutoka kwako, ndivyo uanvyozidi
kuwaumiza,..ujue, kila unalopambana nalo wanalihisi mwili, mwao, ukiwa na
matatizo kuna hisia zinawajia wanaju tu sasa mwanetu yupo pabaya….na hili
nimeliona kwa dada yangu, hana raha kabisa…’
Hapo akawa kaniuliza kweli, nilijaribu kumuwaza mama yangu,
najua jinsi gani anavyonipenda,na nilitaka nifike kwake nikiwa na zawadi ya
aina yake, nakumbuka siku moja aliniambi kuwa, zawadi kubwa ninayotaka kutoka
kwako ni mjukuu…sasa mjukuu nitampataje kwa halai kama hii,….nakasema kwa sauti
ya huzuni….
‘Nimkuelewa sana mjomba, ndio maana sitaki kabisa wajue haya
yanayonisibu, mategemeo yangu ni kuwa nikishajiweka sawa nitakuja nikiwa na
hali nzuri ili niwape faraja, lakini kwa sasa nikija nitazidi kuwaumiza, hebu
fikiria wamenisomesha hadi nje, nini nimewapatia zaidi ya haya matatizo….ndio
maana nashindwa kwenda kuonana nao uso kwa uso nikiwa katika halai kama hii…’nikasema
huku nikitamani kulia.
‘Sikiliza mjomba, haya ni maisha ya kawaida, na ukizaliwa
duniani lazima ujue kuna shida na raha, lakini vyovyote iwavyo, hustahili
kuikwepa jamii yako, ….umekosea ..inabidi ukubali hilo, na ukiwakosea wazazi
wako, kinachotakiwa ni kwenda kuwaomba msahamaha, wao hawana tatizo na wewe. Ni
wewe tu ufike usema wazazi wangu samhanini, …ukipata Baraka zao, hutaamini,
kila kitu kitakunyookea…..’akasema mjomba.
‘Ndivyo nilivyopanga, …lakini sio katika hali kama hii,
nikuambie mjomba, ilibakia kidogo tu nije huku,lakini huwezi amini, kila
nikijipanaga, linatokea tatizo kubwa la kunizuia, kama unavyoona sasa, mimi
sina kosa, nimejitolea tu kwa tatizo ambalo nikikusimulia utasema natunga
uwongo, lakini mungu ndiye anajua …..’nikasema na mjomba akatabasamu na kusema;
‘Unajua mimi sio mtoto mdogo, najua mengi, na mengi
nimeyapitia, ila mimi sikuwahi kufungwa jela, wewe umevuka mpaka, najua nini
kinakusumbua, na hapo ulipofikia nasjua kabisa umeshajifunza, cha muhimu ni
kutafuta mke mwema, ukatulai naye, …..’akasema mjomba.
‘Mke mwema,mmh, sasa hivi sipapatiki tena, na itachukau muda
mpaka niamua kuwa sasa mke wangu ni huyu, …..kwasababu nimeshaumwa na nyoka…’nikasema
na mjomba akanikatisha an kuniuliza.
‘Kwani mkeo imekuwaje…?’ akaniuliza.
‘Kwani huna taarifa, mbona keshafariki dunia…..’nikasema na
mjomba akaniangalia usoni kwa mshangao.
‘Lini, …mbona hilo kwangu ni geni, kwanini kijijini hawajui
maana familia yao nilikutana nayo, na sikusikia wakiliongela hilo, maajabu
kabisa na wewe ukakaa kimiya hukutaka hata kutuambia, nyie watoto mbona
mnapotea , sio vyema namna hiyo….’akalalamika mjomba.
‘Mjomba, yeye nasikia aliwaambia marafiki zake kuwa akifa,
hatakai kabisa apelekwe huuko kijijini na hata huyo ambaye aliyempokea
aliaambiwa kabisa, kama akifa hata taarifa zake zisipelekwe huko kijijini,….’nikamwambia
mjomba.
‘Kwani kafa lini?’ akauliza mjomba.
‘Mbona miezi mitatu imeshapita…..’nikasema na mjomba
akaniangalia kwa muda halafu aksema;
‘Sio kweli….’akasema na kuangalia juu.
‘Kwanini unasema sio kweli….?’nikamuuliza.
‘Ingelikuwa ni wiki moja iliyopita ningekubaliana na hilo,
lakini miezi, ….hapana ,lakini ngoja nisiseme mengi, maana dunia hii ina mambo,
hayo uliyoniambia yananishngaza kabisa, ….hapana, haiwezekani, na kwanini iwe
hivyo….’akasema mjomba na mimi sikumuellewa kabisa.
‘Mjomba unataka kusema nini, uliwahi kukutana na huyo
mwanamke karibuni, maana hapo unanichanganya.
‘Sikiliza mjomba, inaonekana wewe umetumbukizwa katika mambo
ya viini macho,maana sizani kuwa ni msukule, au ni jinamizi, …ila kwa vile na mimi
sina uhakika na hilo, ngoja nikirudi kijijini nitakwenda kuoanana na wazazi waa
huyo mkeo, nijue zaidi, lakini nikuambai kitu, msiba ukitokea kwa mtu yoyote wa
aple kijijini, wte tutajua,….hilo la mke, nalisikia toka kwako leo hii…lakini
sina ushahidi zaidi….’akasema mjomba. Na mara akaja askari kumwambia mjomba
kuwa muda umekwsiha.
‘Mjomba, ….umeniweka njia panda, naomba lolote utakalolipata
huko nijulisha mapema, maana hujanielewesha ….ama kwa hili langu litakwisha, ni
jambo dogo tu,….usije ukawaambia wazazi wangu, …’nikasemana na mjomba alionekana
kuchanganyikiwa na taarifa niliyompa,
akaniangali tu kwa macho yaliyojaa
huzuni, akageuka na kuondoka.
Ni siku iliyokuwa ngumu sana kwangu, kuja kwa mjomba
kuliniongezea simanzi, na maongezi yetu yalinifanya nisiwe na amani, sijua
mjomba ana maana gani, ….lakini nikaona hilo alilosema mjomba haliwezekani,
maana mimi mwenyewe nilishuhudia mwili wa Kimwana ukizikwa, ingwaje ni kwa
siri,….
‘Hapo mjomba kachemka, na huenda wazazi wake hawajui kabisa,…..’nikajikuta
nikisema.
Moyoni nikaahidi kuwa nikitoka hapo ni moja kwa moja kwenda
kuwaona wazazi wangu, nilijiona mkosaji na licha ya kujua nimekosa bado
nimekuwa mkaidi….na kuja kwa mjomba kulikuwa kama nuru fulani imeniingia
akilini,….
Nikawaza kuhusu tatizo lililopo mbele yangu na kumkumbuka
wakili mwanadada, kwakweli huyo dada nilishamuweka kama mmoja wa ndugu zangu,
amekuwa karibu sana na mimi na amejaribu kunisoma na kunijua,kwakweli siku
mbili hizi alizoondoka bila kuwa karibu naye nimekuwa kama mkiwa,…
‘Natamani arudi haraka, ili nijue nini kinaendelea huko
,maana bila yeye nashindwa kujua hili tatizo limefika wapi, na lini dhamana
yangu itakubaliwa, na je huyo mgonjwa anaendeleaje, na nitapata wapi nafasi ya
kumuoana…’nikajikuta nikiongea mwenyewe kama punguani.
*******
Mkuu alikuwa kasimama ofisini kwake na mara akaingia wakili mkuu
wa kitengo cha sheria, mkuu alipomuona
akashikwa an mshangao, na haraka akasimama na ule mshangao ukaabdilika na kuwa
furaha, haraka akamwendea ,wakashikana mkono, akamwangalia kwa makini na halafu
akamuuliza hali yake.
‘Kwakweli najisikia nafuu kidogo,…na nimeona ili nipone
kabisa, nahitjika kuchapa kazi, nikikalala tu, nitaumia,…nilichogundua ni kuwa
kila nikipta shinikizo litakalo nipa wasiwasi, ndipo nahisi maumivu, na hili
linaniogopesha kwani kazi zetu hizi hazikosi misuko suko,..nashindwa hata
nifanye nini….lakini kwa sasa nasema mbele kwa mbele...’akasema wakili.
‘Afya ni bota kuliko chochote, kazi ipo, na ukiwepo au
usipokuwepo itafanyika tu, wewe angalai afya yako kwanza, cha muhimu ni kuhakikisha
kumwa umepona kabisa, ili ukija ofisini uwe na afya ya kufanaya kazi….’akasema
mkuu.
‘Ndio najua hilo, lakini …kinga ni bora kuliko tiba,
nimeshajijua wapi niliteleza, na ndio maana najaribu kufukia mashimo, lakini
kila ukifukia, ukigeuka unakuta limefukuliwa…..nimefika ofisini nimekutana na mambo
mengi hayajafanyiwa kazi, na sasa kesi mbili zimekuja, bado hazijawekwa sawa,
haya mimi siyataki, …..halafi nikuulize…kwani huyo mwanadada aliyepigwa risasi anaendeleaje?’ akauliza.
‘Kwakweli bado hajawa na kauli,walimfanyia upasuaji na kutoa
ile risasi, na wanasema kuna athari zilitokea kutokana na hiyo risasi, na mengi
yanategemea majaliwa ya mungu….’aksema
mkuu.
‘Kwahiyo mpaka sasa hatuwezi kuiita kesi ya mauaji,….na huyu
mshukiwa naona bado yupo rumande, na kiutaratibu anatakiwa kupelekwa gerezani,
haiwezekaani akabakia hapo mahabusu kwa muda wote huu, hili mumelifikiriaje?’
akasema wakili.
‘Ndivyo ilivyo, lakini kila ukiangalia ushahidi ulivyo, tunashinndwa
kuamua….ndio vipengele vingi vinamuweka matatani, lakini ukiangaia kwa namna
nyingine ni janga limetokea na kwa vile hakuna mshukiwa mwingine yeye anonekana
kama ndiye mkosaji….’akasema mkuu.
‘Mimi nimesoma kesi nzima, na kila kitu kipo wazi, ….inabidi
uchunguzi wa kina ufanyike na kama yeye anahusika awe ni fundisho maana hili ni
tatizo, na kwa vile mimi nimeliona kwa vitendo, nataka tupambane nalo na
kuhakikisha wote wanahukumiwa….nataka iwe fundisho kwa hawa watu, ndio maana
nimejikongoja leo kukuamabia kuwa sasa nipo tayari kuingia mahakamani
kupambana na hawa watu…’akasema wakili.
‘Sawa, lakini cha muhimu ni afya yako ….’akasema mkuu.
‘Na dada wakili yupo wapi, sijamuona siku mbili hizi maaan
alikuwa mara kwa mara akinitembelea, lakini skuku mbili kawa kimiya, nimepga
simu yake haipatikani, yupo wapi….?’ Akauliza.
‘Hivi sijakuambia, amekwenda Kenya,….’akasema mkuu.
‘Amekwenda Kenya kufanya nini….?’ Akauliza kwa mshangao, na
kabla mkuu hajajibu kitu akasema kwa hasira.
‘Huyu mwanammke vipi….anaacha kesi muhimu anakwenda
kustarehe,haya ndio matatizo ya hawa wanawake, ukiondoka kidogo tu, ukirudi
mambo yanakwenda shanghala baghala…sasa kaondoka sina hata taarifa….hizi ni
taratibu za kazi kweli ’akasema kwa hasira.
‘Ukiondoka ofisini, wapo watu wanaendelea nayo, ….hajaenda
kustarehe kama unavyodai ni moja ya kufutilia maswala ya hii kesi,…ina maana
kila hatua ya kila aianchokifanya natakiwa akuambie, ujue wewe ulikuwa likizo
ya ugonjwa na tuliona sio vyema kukushiriksha kwenye hizi kesi, ili upambane na
afya yako kwanza.’akasema mkuu.
‘Mimi ninachojiuliza, kesi hii inahusianaje na huko Kenya,
kama ni kuhusu yule mama Docta, tulishaona kuwa hana hatia, na hahusiki tena,
na mambo yanayotokea hapa kwa sasa hayamuhusu,..kwasababu unaona hayupo , lakini
mambo kama hayo yanatendeka…vifo hivi ni majanga haya ni ya watu wa humu humu….’akasema
wakili akiangalia saa yake.
‘Alichopanga yeye ni kuwa antaka kuona chimbuko la haya
matatizo, maana kila ukifuatilia unagundua kuwa mambo mengi yameanzia kwa huyo
mama Docta, wahusika wengi walikuwa wafanyakazi wake,….sasa kaona kuwa kuna
haja ya kukutana naye aone kwanini imetokea hivyo…’akasema mkuu.
‘Hainiingii akilini, haiji kabisa,…..labda kama ana mambo
yake mengine, sio mbaya, hata hivyo nilishamuona kuwa anataka kujitoa
serikalini awe wakili wakujitegemea, ndio maana anakusanya marupurupu apate
msingi….au kaenda kutafuta wafadhili,…unafikiri mchezo kuwa na ofisi yako
mwenyewe,…..’akasema huyu wakili.
‘Lakini mimi sikupenda wazo lake la kujitoa serikalini ni
wakili mnzuri sana, hasa inapofikia maswala ya kesi za kifamilia …ana hekima ya
kuzishughulikia, mara nyingi yeye anaangalia kwa undani na matokeo yake tunakuja
kugundua tatizo ambalo usingeligundu akirahisi…’akasema mkuu.
‘Sawa aende huko, mimi nitabakia serikalini na nitapambana
na uhalifu kwa nguvu zangu zote ,mimi ni mwanaume bwana,….na kama ikibidi
nitapambana naye kwenye ulingo wa mahakama …maana akiwa wakili wa kujitegemea
itafika muda tutakutana mahakamani….’akasema huku akijiandaa kuondoka.
‘Sikutarajia kusikia kauli hiyo toka kwako, maana nilitaka
nyie muwe pamoja,badala ya kutofautiana na kujenga ushindani,…kesi hizi
zilizofuatana zinahitaji mshikamano, ukumbuke kuna mauaji bado hatujayatatua ,
sasa limezuka hili jingine, hatujui kama itaishaje, tunaomba huyo mgonjwa apone,
akipona atatusaidia sana, na asipopona tutajikuta kwenye kesi nyingine ya
mauaji,…kesi zinapandana..’akasema mkuu..
`Yote sawa tutayamaliza tu,….nitahakikisha yanakwisha yote
ndani ya ulingo wa mahakama, na wote wanaohusika watapambana na mkono wa
sheria,….wamejitakia wenyewe….na huyu dada wakili akirudi, kama atapitia hapa
kwako naomba umwambie aje ofisini haraka, ….’akasema na kuondoka.
*****
Wakili mwanadada altua uwanja wa ndege wa Dar-es-salaam,
huku akiwa hajui afanyeje ili aeleweke, kwani alishafikia uamuazi wa kuwa
wakili wa kujitegemea, na taratibu za kuanzisha ofisi yake zimeshakamilika,
lakini ofisini hawataki kumruhusu. Akiwa anatafakari hayo na mengi
aliyoyagundua huko alipokwenda, aliona jambo jema ni kuhakikisha hizo kesi
zilizopo mbele yake zimekwisha.
Kichwani alikuwa kabeba mengi ambayo anahisi wengi
hawataamini,na ili waamini inahitajika kuwa na ushahidi wa kutosha , mapaka
muda huo hakuwa na ushahidi wa kimahakama, na ili uweze kuishawishi mahakama
inabidi kutafuta vielelezo, na mashahidi ,ambao bado hajakubaliana nao, ili
waje kuthibitisha hayo,…mwenyewe alijikuta akiwa kwenye mshangao, akasema
kimoyomoyo, siku itafika na ukweli utadhihiri.
Alipofika nyumbani kwake aliwasha simu yake ya mezani ambayo
aliitegesha kwa ajili ya kupokea ujumbe wa sauti, na mara akakutna na
mfulululizo wa ujumbe ukitoka kwa wakili mkuu wa kitengo chao cha sheria, na
kwa ujumla alikuwa akitaka wakutane haraka iwezekanavyo.
‘Kumbe huyu mtu keshapona, …na huu ndio muda wangu wa
kujiandaa kuachana na kitengo chao….’akasema huku akijipumzisha, lakini kila
alipjaribu kutafuta angalau usingizi, akajiukuta akili haitulii, akainuka pale
kitandani na kwenda kuchukua mazoezi kidogo..
Wazo likamjia kuwa kwanza akaonane na mkuu wa kituo cha
polisi, alitaka apate muda aongee naye, , huyi ndiye mtu pekee aliyekuwa
akimwamini kwa muda huo, na alimuhitaji ili aweze kufuatilia baadhi ya mambo,
na wazo hilo lilipomjia akilini, akajiandaa kuondoka . Alisoma baadhi ya ujumbe
kwenye hiyo simu yake, na mara akaona ujumbe usio na jina,…ulisema;
‘Unakumbuka nilikutumia vitu,ili uvifanyie kazi,je umefikia
wapi…?’ akajiuliza ni vitu gani
hivyo,….na mstari wa mwisho ulisema, `naomba ukishavifanyia kazi unirudishie
mwenyewe, na kama umeshindwa naomba unijulishe maana huyu mtu haeleweki….’ Akakumbuka
ni vitu gani, na hapo akasema kimoyo moyo,
‘Sijashindwa bado, natafuta muda muafaka…’
Alipoona hakuna zaidi akatoka hapo nyumbani kwake na
kuelekea kwa mkuu wa kituo chao cha usalama, wao wanamtambua kwa jina la Mkuu,
na alipofika akamkuta akiwa kwenye vikao na vijana wake, akasubiri.
Na mkuu alipomuona
akawaondoa vijana wake na kumwita wakili huyu mwanadada aingie ofisini kwake, na kuanza kumuhoji kwa
kusema;
Wakili mwanadada akiwa kavaa miwani yake, akakaa kwenye kiti,
na mkono akaupeleka kidevuni, kidole kimoja kikawa kimeshika shavuni, na
kuwangalia moja kwa moja usoni Mkuu ambaye alionekana mwenye hraka, Mkuu
akasema,
‘Vipi umesharuditoka huko Kenya, kuna habari gani huko,
maana mwenzako anakusubiri kwa hamu sana, na alitoa maagizo kuwa ukija tu,
kwanza umuone yeye…na swali kubwa ni kwanini uliondoka bila kumpa taarifa, na
kuna kitu gani muhimu kilichokupeleka huko kama sio starehe…..’akasema mkuu.
‘Kwa mpangilio wangu kwanza nataka nikuone wewe, kwasababu
kuna mambo yanahitaji ufuatiliaji wako, naomba tuongee kwanza kuhusu hilo kama
una nafasi,kama huna tupange siku nyingine…’akasema mwanadada.
‘Haya nipe kwanza taarifa zile zilizokupeleka huko....kwa
haraka, kwa ujumla kwasasa hivi sina nafasi ya maongezi marefu, ratiba hainiruhusu
kabisa, je ulifanikiwa…?’akasema mkuu.
‘Kama huna huo muda ni bora tusubiri baadaye,…kwani maongezi
haya hayahitaji uharaka, ila ynahitaji umakini wa kutafakari, ….mmh, ila jambo ambalo nataka kukutonya ni kuwa
nataka kuanza mikakati ya kuachana na kazi hizi za serikalini, nilishakuambia hilo, lakini muda kamili wa kuachana na hiyo ofisi
nilikuwa sijakuambi, nataka wiki hii nimalizane na nyie, ili nipate muda wa kujiandaa
kwa ofisi yangu kama wakili wa kujitegemea….’akasema.
‘Kwanini umeamua kufanya haraka hivi,….?’ Akauliza.
‘Kwasababu nikiwa ndani ya hicho kitengo sitaweza kufanya
kazi yangu vyema, naona kuna siasa nyingi na kulindani kwingi, na ubinafsi
mwingi, hili linanikwaza mimi kutimiza malengo yangu ya kupambana na watu wanaotumia
madaraka yao vibaya, na nia yangu kubwa sio huko, ….sio kisiasa, nikisema
madaraka vibaya usije ukazania nataka kujiunga na mambo y akisiasa, hapana, …..mimi
lengo langu nataka nitimize ndoto yangu ya kuwa wakili wa kujitegemea wa
kuwasaidia akina mama…’akasema wakili mwanadada.
‘Kwani huko Kenya ndipo kwenye wafadhili wako, maana hilo
wazo limefumuka baaada ya kurudi hiyo safari yako, ….?’ Akauliza.
‘Hapana sina wafadhili….naanzisha kwa nguvu zangu mwenyewe, nilichojifunza
huko, ni kuona wenzangu wameweza, na wapombali sana, na nilipoongea nao nikagundua kuwa inawezekana
, na haihitaji mtaji mkubwa, ….
‘Mimi naona utakuwa unakimbia vita, na kama vile mtu
anakimbilia nchi ya jirani, kwa vilencho yake ina vita, na wakati huo yeye ni
askari,….nakushauri kwanza hakikisha umemaliza hizo kesi kabla hujaondoka,ili
uilinde hadhi na heshima yako,….na hilo la kuacha kazi serikalini na kuwa
wakili wa kujitegemea, hakuna anayekukatza, ila ni vyema ukuafuata utaratibu….’akasema
mkuu.
‘Utaratibu upi tena mkuu, mimi nilishamalzia mkataba
wangu wa ajira, na niliombwa nisaidie tu
baadhi ya kazi kwa vile huyo mwenzangu alikuwa anaumwa,na sasa keshapona, au
bado anaumwa….?’ Akauliza mwanadada.
‘Kasema keshapona na ana motomoto wa kuhakikisha hizo kesi
zimekwisha haraka iwezekanavyo, nakwa ujumla amekuwa mbogo,ofisini kwake watu
wanachapakazi sio mchezi, kwakweli ni mtendaji mzuri….’akasema mkuu.
‘Mimi silipingi hilo kuwa huyo jamaa ni mtendaji mzuri,
lakini kuna mambo mimi nay eye hatuivani, na Ili kumaliza haya matatizo
nahitajika niwe huru, na nilishajifunza kuwa nikifanya kazi na huyu mwenzangu,
nakwazika,huwa mara nyingi ana tabia ya kunizarau kama mwanamke,..ana tabia ya mfumo
dume hata kweney kazi, mimi sipendi huo mtindo, kazi ni kazi, na mambo ya
milana desturo kuwa mke hawezi hili, asiwe msemaji mkuu, sijui…..hapana hayo
hayana nafasi kwangu, na ili niweze kumuonyesha kuwa sivyo hivyo anafofikiria
ngoja..….
Mara simu ikalia na mkuu akaipokea na kuiskiliza,….
‘Unajua nilishasahu,natakiwa kwenda kuonana na mwenzako kwa
ajili ya kukamilisha maandalizi ya hii kesi mpya, ndio huyo kanipigia simu,
nakuambia amekuja na moto mkali, ….hata mimi nimefurahia kuwa kazi zinakwenda
mbio mbio,sipendi kuwa na mlolongo wa kesi nyingi katika kituo chetu, kaniambia
kuwa yeye yupo tayari, ….kwahiyo tunaweza tukafuatana, au unahitaji kupumzika
kidogo….?’akasema mkuu.
‘Sawa tunaweza kufuatana, lakini msimamo wangu ndio huo…nafikiri
umenielewa na kesho nahitaji tuwe
pamoja, …..’akasema.
‘Tutaongea huko,….lakini kuna nini kikubwa umegundua huko,
hujaniambia bado..? akauliza mkuu.
‘Nimegundua mengi sana, ambayo kama nitafanikiwa kupata huo
ushahidi ,basi hali itabadikilka kabisa, na kwakweli nihitaji nguvu za ziada,
ndio maana nimesema nikiwa humo ndani ya kitengo chetu sitaweza kufanikiwa,….kinachonikwaza
ni hiz kesi mbili ambazo zipo mhakamani, na nipo uapnde ambapo sitaweza
kupambana vyema …..nataka kama ikiwezekana nijitoe upande huo niwe uapnde wa
kujitetea…’akasema wakili mwanadada.
‘Hapo mimi sijakuelewa, inabidi unipe muda, tuongeee vyema,
maana huko ni kukimbia kupambana na wahalifu na kutaka kukaa upende wao,
hainiingii akilini…’akasema mkuu.
‘Vipi kuhusu hali ya yule mgonjwa….?’ Akauliza wakili
mwanadada.
‘Hali yake bado haijawa njema…na jana alizindukana
akaendeela kumtaja Msomali…
‘Sasa kwanini hamkumkutanisha na huyo Msomali?’ akauliza
wakili dada.
‘Wakili wetu aliweka pingamizi kuwa asiruhusiwe kumuona mpaka
na yeye awepo, na mudahuo alipozindukana huyo wakili alikuwa mahakamani kwenye
kesi nyingine, na tusingelwieza kumtoa, ikabidi tuahirishe hilo zoezi…’akasema
.
‘Kwahiyo huyo mgonjwa sasa keshazindukana….?’ Akauliza
wakili
‘Alizindukana hiyo mara moja, na alikaa kwa muda, na baadaye
akapoteza fahamu tena….’akasema mkuu.
‘Kwa mtizamo huo natamani ikiwezekaan hata leo, niwe wakili
wa kujitegemea, ili niweze kuifanyia kazi hii haraka, …..maana sio mantiki, ya
kumzuia huyo jamaa asionane na huyo mgonjwa, wakili wetu,ni mchapakazi mahiri,
lakini huwa akiang’ang’ania kitu chake huwezi kumbadili mawazo,..mimi naomba
ufanya kilaiwezekanavyo Msomali akutane na huyo mwanadada, na mimi nitajitahidi
niwepo,….’akasema wakili mwanadada.
‘Sawa
tuombe kesho huyo mgonjwa awe nahali nzuri…’akasema mkuu
NB: Kila hatua ni kwenda mbele, sikutarajia hiki kisa kitafikia huku, lakini kisa kama kisa hakikosi mkasa, naombe tuwe pamoja, tu....tusichoke,....
WAZO LALEO: Kuna mtu mwema mmoja aliniambia kuwa kama ingeliwezekana, ilitakiwa kila ukipata chochote, katika riziki yako, ulitakiwa umkabidhi mzazi wako yeye ndiye akugaie matumizi yako. Lengo lake hapa ililikuwa kunionyesha umuhimu wa wazazi.
Tuwakumbukeni wazazi ,tuwajali na tusikae mwezi,miezi bila kuwajulia hali na kila riziki unayopata hata kama kidogo namna gani, ukumbuke kwa ndani yake kuna sehemu ya mzazi wako, tuwajali wazazi wetu kwa kila hali, kwani ni nani kama wazazi wetu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment