Mwanadada wakili alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio, na
moja kwa moja aliingia ndani, na kukuta watu wa huduma ya kwanza wakifanya kazi
yao, hakupewa nafasi kabisa, akaona haina, akasogea pembeni kuwapa nafasi, …na
haikuchukua muda mara ule mwili ukainuliwa kwenye machela tayari kwa kukimbizwa
hospitalini,….
Hakuana na jinsi, alitaka kumuona kuwa ni nani, lakini
haikuwa rahisi hivyo, askari hawakumpa nafasi hiyo, walisema kazi yao ni
kujaribu kuokoa maisha ya huyo mtu hawawezi kumchelewesha hapo zaidi, ikabidi
atulie na akawa anaangaza macho huku na kule mara mara akamuona, jamaa kakaa
pembeni, huku kainamisha kichwa chini,akamsogelea na kumgusa kwenye bega kwa nyuma.
‘Vipi …ooh, ni wewe, umefikaje huku….?’ Akamuuliza kwa
kushangaa alipogundua kuwa ni mtu anayemjua.
‘Oh,…afadhali umefika, hapa nilitaka nikupigie simu, kumbe na wewe umekuja, afadhali maana hawa
polisi hawana dogo, Mimi ndiye niliyewapigia simu polisi,lakini nawajua
wanaweza wakanigeuka , wema wangu uanweza ukaniponza….’akasema.
‘Imekuwaje wewe uwapigie simu, ulifikaje huku, Ina maana
hapa unapajua….hebu niambia kwa ufupi na kwa hara…’akasema wakili mwanadada, na
kabla hajaongea kitu, mkuu na kundi lake wakaingia na walipoona watu wakimalizia
kazi mbali mbali mle ndani, akawaona wapenafasi kwanza,ili awaulize kila mmoja
kwa wakati wake.
‘Imebidi awahishwe hospitaliu haraka,…huenda tukaokoa maisha
yake,….’akasema askari kumwambia mkuu.
Mkuu akamsogeza huyo askari pembeni, karibu na tuliposimama,
huyo askari ndiye aliyefika hapo mapema na kundi lake baada ya kupigiwa simu,
akamuuliza swali la kwanza;
`Hebu niambie,ulifikaje hapa..?’ akauliza swali la utata.
‘Tulipigiwa simu na jamaa mmoja,…..mmh, yule pale,…’akanyosha
kidole kunielekeza mimi.
‘Huyu jamaa kwenye simu alituambia kuwa amefika hapo baada
ya kupigiwa simu na …..huyo aliyefikwa na hayo maafa,….mapaak sasa hatujamjua
ni nani, huyo mwanadada, alisema kuwaanamuhitaji huyo jamaa kwa haraka , hayo
ni kwamaeelzo yake ya haraka, sijamuhoji vyema, nimemuweka pembeni kwanza ili tumalize
hayo ya muhimu…’akasema huku wote wawili wakiniangalia mimi
‘Tutamuhoji baadaye, wewe elezea kuhusu kazi yako,nini
ulikiona uligundua nini…’akasema mkuu.
‘Nilipofika hapa, nilifika na kikosi kamili, maana nashukuru
huyo jamaa alitupa maelezo safi kabisa, kwahiyo tulkuja tukiwa tumejiandaa, niliuagiza
docta na kundi lake wafike hapo haraka, pia tulikuja na wataalamu wa alama za
vidoela na wachukua picha, na wachunguzi wote niliwapata kwa haraka, kwahiyo
tulipofika hapa kila kitu kilifanyika kwa haraka, hakuna kilichokosewa,
tumewaachia sasa madocta wamalizie kazi yao ili watupe taarifa….kwasasa wamesha
mchukua huyo ….eeh ,tuseme majeruhi hadi hospitalini’akasema huyo askari.
‘Kwahiyo unaweza kusema nini kuhusu hili tukio…?’ akauliza
mkuu.
‘Ni tukio la kutaka kuua, kwa kutumia bunduki, …kwasasa
tunaweza kusema ni majambazi, lakini hatuja wan a uhakika nalo,….siwezi kusema
ni mauaji maana hatujapata taarifa ya docta, lakini huyo muathirika kapigwa
risasi,…na ngoja tumsubiri docta atuambie wapi na athari yake, lakini mimi na
wenzangu tuiimkuta akiwa bado hajapoteza fahamu….
‘Naona pale dirishani, kumemeguka, ina maana ile ni sehemu
risasi ilipopitia kutoka kwa nje, ….’mkuu akaangalia pale dirishani na kiyoo
kilikuwa kimevunjika kidogo,….na alipokichunguza vyema akagundua kuwa kile
kiyoo kilikuwa na matundu, na risasi ilipenye kwenye moja ya tundu, ilikosea
kidogo ndio maana kiyoo kimemeguka…na kile kipende kilichomeguka kikaanguka
chini na kusambaratika.
‘Ndio mkuu, pale ndipo risasi ilipopitia, wataalamu
wamepapima, na huyo muuaji alikuwa kwa nje, akalenga shabaha kupitia kwenye moja
ya matundu ya hicho kiyoo, akiwa anmuona huyo mwanadada kwa ndani
tundu…’akasema huyo askari.
‘Kwahiyo huyo muuaji alikuwa kasimama kwa nje, au sio….?’akauliza
mkuu.
‘Hapana kutokana na mtaalamu wetu wa silaha anasema mlengaji
alikuwa mbali kidogo, na ukiangalia kule, kuna jengo ambalo lipo juu kidogo,
ina maana mtu akiwa kule anaona huku kwa ndani, na kwa vile taa hapa zilikuwa
zinawaka, kama unavyoziona, licha ya kuwa ni jioni jioni,….tulizikuta hivi
hivi,….’akasema na kuangali juu, kweli taa zilikuwa zinawaka.
‘Ukiwa kwenye lile jengo unaweza kuona huku, ukitumia silaha
yenye darubini unaweza ukaona vyema tumejaribu hilo kwa haraka….’akasema huyo
askari.
‘Sijawaelewa , ina maana huyo aliyekusidia kuua alikuwa
kwenye lile jengo, akatumia silaha yenye darubini kumlenga huyo
…..mmh,muathirika,je alijuaje kuwa kuna tundu kwenye hili dirisha…na kweli
unaweza kuona ndani ukiwa pale, mbana naona kama haiwezekani,kama ni usiku
sawa,lakini jioni hii?’ akauliza.
‘Tumechunguza hilo, unaweza ukaona,taa hizi nikali sana, na
viyoo vya nyumba hii vinaonyesha vyema,hata ukiwa pale unayaona haya matundu
vyema..na hasa ukitumia silaha yenye darubini….’akasema huyo askari.
‘Hata hivyo ni kazi kweli kupenyesha risasi kwenye haya
matundu, aliwezaje kufaya hivyo?’akauliza mkuu.
‘Yapo matundu mengi, labda alibahatisha tu, na bahati risasi
ikapenya kwenye hilo tundu, licha ya kuwa ilikosea kidogo, ….sizani kuwa ni labda
ni shabaha ya huyo mtu, kuwa alikusudia hiyo risasi ipenye kwenye tundu…kama
itakuwa hivyo basi atakuwa mlenga shabaha mahiri…’akasema huyo askari.
‘Ehe, kwahiyo mumeshajua ni aina gani ya silaha
iliyotumika…au mpaka risasi itokewe…?’ akauliza mkuu.
‘Kwa makisio ya mtaalamu wetu, baada ya kuchunguza jereja
amesema ni risasi ya silaha kubwa,…na ni hizi zinazoweza kulenga toka mbali,….lakini
pale kwenye jengo sio mbali sana..’akasema huyo askari, na kutlia kidogo,
halafu akasema tena;
‘Naona ingekuwa ni bora tukasubiri hiyo risasi ikatolewa kwanza
ndipo tukaweza kutoa maelezo yaliyo sahihi….kwasababu mengine yote yamekamlika
imebania kazi ya madocta…’akasema huyo askari
‘Hiyo ni sahihi kabisa na je mumeshaongea na huyo
aliyewapigia simu…?’akauliza mkuu na yule Askari akageuka na kuangali huku tulikosimama na
dada wakili, na kabla mkuu hajapata jibu alilolitaka akatusogelea pale tulipo
na kuniangalia kwa mshangao, na baadaye akamwangalia dada wakili akatabasamu na
kusema,…
‘Usiseme kuwa wewe ni wakili wake, hatajibu maswali mpaka
umruhusu…’akasema kwa utani huku akitabasamu.
‘Na ndivyo ilivyo, mimi ni wakili wake toka siku nyingi, ila
kwa wewe na kwa leo nakuruhusu umuhoji maswali yote unayotaka..’akasema wakili
mwanadada.
Mkuu aliniangalia kwa makini, halafu akasema;
‘Naona tunakutana mara kwa mara, na kukutana kwetu inakuwa
katika hali isiyo rasmi, vipi unataka kujiunga na polisi nini, maana kila
ninapokwenda na kukuta upo, na kuwepo kwako kunakuwa sio kwa heri, haya hebu nieleze ilikuwaje?’
akauliza mkuu.
‘Mimi nilikuwa nyumbani kwangu ninapokaa, na nikapokea simu
, ….nilipoiangalia hiyo namba ilikuwa ngeni kwangu,….nilizarau kuipokea, lakini
ilipoita mara ya pili nikaipokea na mara
nikasikia sauti ya kike, ilikuwa ikiongea kwa taratibu, labda ili watu
wasisikie au ni kutokana na hali ya kiafya, sikujua ni kwanini, ila sauti
ilikuwa ya kama kunong’ona….’nikasema.
‘Ilisemaje hiyo sauti….?’akauliza.
‘Ilisema, kuwa …niende nyumba na 512, mtaa huu hapa Sinza, ….na nifike
haraka, kwanza sikupaelewa, licha ya kuwa alinieleza , akanifafanulia nifikie
wapi, na ni vyema nichukue boda boda ii nifike haraka, na akasisitiza kuwa ni
muhimu, nikichelewa nitakuja kujuitia katika maisha yangu yote…nikamuuliza
kwanini na yeye ni nani?’nikatulia kidogo.
‘Ehe elezea tu, tunataka kupata maelezo ya haraka haraka, ikawaje…?’
akauliza mkuu.
‘Alisema nitajua nikifika huko,…halafu nikasikia kama sauti
ya kiyoo kikivunjika, au kama hicho, mara na na sauti ya `aaaaah’ na ikawa
kimiya, lakin nilihisi hiyo simu bado ipo hewani’nikasema nikujaribu kukumbuka
ilivyo kuwa…
*******
Siku hiyo nilikuwa nimepigika kweli, watu siku hizi husema
nilikuwa nimefulia, na kila nilipojaribu kutafuta chochote sikuweza kupata,
nikaenda kwa mama mmoja niliyomzoea, akanipa ukoko, na nikamsaidia kusafisha
vyombo, basi tumbo lilipojaa, nikaaona nikajipumzishe chumbani kwangu,kwanza nilioga nikuwa nimenyoa jana , kwahiyo sikujusumbua kuangalia ndevu,kwani huko ninapokwenda kufanya kazi hotelini usiku wanahitaji uwe mtanashaji. Kuna mtu mmoja aliniwahi kunishauri nijiunge na wanamitindo.,....eti ninafaa sikupenda hilo wazo,
Nikaona nijipumzishe tu, kwani unaweza ukatoka kutembea ukakutana na mabalaa, na mimi najaribu kuyakwepa,....sizitkai mbichi hizi,sina pesa, nitafanya nini, nikaamua nipige mbavu,maana nilikuwa na sehemu ya kufanya kazi, ni bora nikusanye nguvu.
Nikiwa ndani ya usingizi,nikaota ndoto kuwa nipo kijijini
kwetu, lakini ndoto hiyo ilinirudisha siku nyingi nyuma, nikiwa natoka shuleni,
nikakutana na msichana mmoja, sikuwa na mjua,msichana huyo akaniambai kuwa mimi
ni mtu mbaya sana,
‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza.
‘Kwasababuu wewe unaharibu watoto wa watu halafu unawaacha
njia panda….akaniambia nimewaharibu hata kwenda shule hawawezi,….na wazazi wao
wamewafukuza…’akasema huyo msichana mgeni kwangu.
‘Mbona mimi sijafanya hivyo, wapo wapi hawo watoto?’nikamuuliza
‘Wale pale….’akanionyesha kwa vidole,na kweli pale niliona
watoto wamelazwa, lakini cha ajabu chini ni watoto, lakini kwenye vichwa vyaoo
ni watu wazima,na mmojawapo niliyemuona ni Kimwana, yeye alikuwa kilia na
machozi yake yalikuwa nii ya damu, na sura nyingine ambayo najaribu kuiwaza ,lakini
siikumbuki vyema,… ilikuwa yenyewe inaniangalia kwa kushangaa,…
Nikamuuliza huyo msicahana mbona ni wana sura za namna hiyo,
kichwani watu wazima lakini kiwili wili cha kitoto,akacheka na kusema, wewe
hujioni, kichwani mnaonekana watu wazima, lakini mtendo yenu ya kimwili ni ya
kitoto, aheri hata ya mtoto, utasema anafanya hayo kwasababu ni mtoto, hebu
jiangalie wewe…’akasema na mimi nilipojiangalia, nikajikuta mwili wangu ni wa
kitoto…
Nilishituka kwa hofu toka usingizini, na sikuweza kulala
tena,nikiwazi hiyo ndoto, mara nyingi nikiota ndoto, huwa ina maana fulani, au
inanieleekza jambo fulani, lakini ndoto hiyo haikuwezakunipa maana halisii ni
nini, nikaamua kuipotezea na nikajinyosha kidogo na kabla sijamaliza kujinyosha
simu ikalia.
Nilipotizama ile namba, nikaiona ni ngeni kabisa machoni
mwangu, nikaidharau na kuinuka kitandani,simu ileiliita mapaka ikakatika,
nikasema hapigi tena, lakini mara akaanzakupiga tena, nikasema moyoni ni bora
kusikiliza huenda ni simu ya pesa, nikaipokea;
‘Fika haraka hapa Sinza, ukifika hapa Kwaremi, ingia
barabara inyofuata hadi nyumba namba SN X500, nipo ,fungua mlango utanikuta..’ikasema
sauto ya kunong’ona. Nikamwambia kuwa huko sipajui na sina nafasi kwa sasa.
‘Ni muhimu sana,..usipokuja utajijutia masiha yako yote,
nahitaji kukuona kwa jambo muhimu sana kwa ajili ya maisha yako ya baadaye….chukua
boda boda, wengi wanapajua hapa mahali…nitamlipa huyo mwenye boda boda…’akasema
kwa sauti hiyo hiyo ya kunong’ona.
‘Kwani wewe ni nani ….na umenijuaje….?’ Nikamuuliza.
‘Usiulize maswali mengi,unapoteza muda,weweukifikahapa
utajua kila kitu na hata kie ambacho ulikuwa hukijui utakijua…njoo haraka…’mara
nikasikia sauto ya kama `’kaaah’ naweza kusema ni sauti ya gilasi au kiyoo
kilichovunjika, nasema hivyo baada ay kuona hivyo viyoo vilivyovunjika hapo,
lakini kwa muda ule sikuweza kutambua ni sauti ya nini.
‘Ila nilichosikia cha wazi ni hiyo sauti ya `aaaah’na
kutulia,nikabaki kusema `halooh, haloooh’ lakini sikusikia sauti nyingine sehemu
ya pili, nikainuka kitandani haraka, na kutoka nje, ukumbuke sina pesa na ni
nani angekubali akuchukue bure, ..bahati nilipotoka nje tu, nikamuona rafiki
yangu mmoja,
‘Vipi broo, huna abairia leo…?’ nikamuuliza.
‘Kuna abiria mmoja kaniita nikamchukue huko Sinza, sasa
najaribu kuliangali pikipiki langu maana huyo ni mtu wapesa…’akasema huyo
rafiki yangu na moyoni nikasema mambo si hayo.
‘Hata mimi nafika huko, lakini sina pesa, kuna jamaa
kaniambia nikifika huko atanipatia chochote, naomba lifti…’nikasema.
‘Wewe kila siku huna pesa….hujui nikikupakiza wewenitakosa
abiria njiani,lakini twende tu, utanilipa tukifika…’akanimbia na mimi nikapanda
kwenye hiyo pikipiki na haraka tukafika Sinza, na nilipomuulizia mitaa ya hapo,
akasema Sinza anaijua sana kwani ndipo alipokulia na hata hiyo nyumba anaifahamu,
ni nyumba nzuri, iliyojengwa kwa haraka sana…
Basi akanifikisha na kuniambia kuwa pesa nitampa huko
nyumbani, name nikashukuru na kueleka kwenye hiyo nyumba. Kwakweli ilikuwa ni
nyumba nzuri, imezungushwa geti la nguvu, nikafika kwenye geti na kukutata
hakuna mlinzi, nikafungua mlango wa geti na kuingia ndani….nje kulikuwa na
bsutani nzuri,nikaitamani ile nyumba.
Nikaharakisha kwenda kugonga mlango wa hiyo nyumba, lakini
kulikuwa kimiya, nikafungua mlango na kuona upo wazi, nikaingia ndani. Macho
yangu yalitua kwenye dirisha moja kwa moja, nikaona pale palivyomegeka, na
kipande cha kiyoo kimedondoka chini na kuvunjika, nikaona ajabu,….sikuwa na
mawazo ya kuangalia skafauni.
Mara nikasikia sauti ya mtu akiguna kuonyesha maumivu,…haraka
nikageuza kichwa kuangalia kule sauti ilipotokea, ooh, nikashikwa na mshituko,
damu, zilikuwa zinavuja toka kwa huyo mtu aliyelala sakafuni, zilikuwa zikitoka
eneo la bega,…karibu na kifua…mawazo yangu yalikuwa labda kapigwa kisu,lakini kulikuwa
hakuna kisu,…nikamsogelea alikuwa mwanadada akiwa na nguo za kulalia, niakogopa
hata kumgusa, nikujua sasa hilo ni balaa
‘Msoma…..mso….mali…naku….naku……’akawa anataka kusema kitu,
lakini sauti ilikuwa hatoki vyema na wala hakuweza kumalizia hilo neno,
alilotka kusema, sikujua anataka kusema
nini, na mara akaonyosha kidole nakunionyeshea kwenye kabati,…nikaangali
sikuona kitu zaidi ya kabati la vitabu….nikamgeukia na kutaka kumuinua.
Lakini nikaona nitakuwa mjinga mtu kaumia badala ya kutoa
msaada naanza mengine,nikapiga simu polisi na kuwapa maelekezo, na bahati
nzuri,walisema kuwa wapo karibu na wanapajua hapo ninapowaelekeza, nikawapa
hali halisi ilivyo.
Haikuchukua muda wakafika,…ndivyo ilivyokuwa mkuu,...'nikamaliza kujieleza.
Nb, leo najisikia hali sio shwari,....tuonane sehemu ijayo mungu akipenda.
WAZO LA LEO: Unaweza ukajikuta ukiandamwa na matatizo lukuki,hata kuwaza yasiyokuwepo, ooh, labda mkono wa mtu, ooh,kwanini mimi....cha muhimu ni kuvumilia na kujikabdihi kwa mungu, maana yote yameumbwa kwa ajili yetu wanadamu, yawe mazuri au mabaya. Jua kuwa mvumilivu hula mbivu.
Ni mimi:
emu-three
8 comments :
pole kwa kutojickia vema... huyu aweza kuwa yule demu wa ahadi yz uttn!
NDUGU YANGU WEZAKO WANAKUIBIA KAZI YAKO, UNAUMIA WEWE WENZAKO WANAFAIDI, JARIBU KUTAFUTA NJIA YA KUMILIKISHA KAZI ZAKO, NI USHAURI TU
m3 vipi unaumwa umesema leo hali sio nzuri au sijaelewa pole sana
daa yaani jamaa kila anapokanyaga ni balaa tu
muendelezo ni mzuri ,binadamu tunakutana na mengi kwenye maisha .la muhimu mtu kutokata tamaa hakuna lisilowezekana
Pam na Samira, ni kweli afya ina migogoro, nashukuru kuwa leo ni Ijumaa, na kesho nipo nyumbani nitakuwa napumzisha mwili....siunajua tena kupigika, unatoka nyumbani usiku unarudi usiku.
Ama kwa mwenzangu uliyenishauri kuwa kazi zinaibiwa,...kwakweli hapo sina uwezo wa kuzia kwa sasa, kama kuna watu wa namna hiyo...mungu atawalipia...
Iliyobakia ni kumuomba mungu atusaidie, ipo siku tutajaliwa an kuweza kuwa na hiyo hati milki na kuchapa vitabu.
Na yule aliyeuliza kwanini siweki tangazo, ...natamani sana iwe ivyo, lakini sio rahisi kwa hapa kwetu bongo,....lakini yote tutaendelea kujaribu, ipo siku,...tuombeane heri.
Tuko pamoja mpaka mwisho, hata kimya kimya....
Shukuru nashukuru kuwa nasi na kuachana na kupita kimiya kimiya.
Unajua unapoandika jambo wenzako ndio wahakiki na washauri wakuu wakiwa kimia hutaweza kujua ujumbe umefika je ni safi
Ndugu wa Mimi,Pole sana kwa yoote, Mungu yu pamoja daima, ipo siku itabaki Story.
Asante kwa Wazo la leo pia.
Pamoja sana sana Ndugu wa mimi.
Ndugu wa mimi Amin dua yako ipokelewe tupo pamoja
Nimesikitika leo yametokea mambo juu ya uwezo wangu, kuna tatizo la umeme kwenye sehemu ninapojishikiza.
Post a Comment