Kesi ya Jangiri kama muuaji ilikuwa ya aina yake, maana kama
ilivyotarajiwa huyu jamaa alikataa makosa yote ni kudai kuwa alitamka kuwa
ndiye aliyemuua Kimwana kwasababu ya mateso na shinikizo la polisi, alifikia
hadi kuonyesha alama za vidondoa eti vilivyotokana na mateso hayo, sijui aliteswa
saa ngapi,…
Mara kwa mara wakili mwanadada alifika kwenye hiyo kesi na
wakati mwingine alimuachia msaidizi wake,huku akiwa katika uchunguzi wake binafsi,
alikuwa na mambo mengi ya kufuatilia, kiasi kwamba aliona muda haumtoshi, na
leo akiwa ndani ya hii kesi, akapokea simu toka kwa mmoja wa wafanyakazi wake
‘Nipo mahakamani unasemaje?’ akauliza.
‘Kuna mtu kaleta barua hapa, na anasema hiyo barua ni ya
muhimu sana, anataka wewe mwenyewe uipokee…ndani yake kuna mkanda wa CD’s,umeandikwa `confidential…’ na huyo
mletaji anasema anahitaji jibu la harakakutoka kwako…’akasema.
‘Usiufungue huo mzigo, au huo mkanda ,inawezekana ikawa ni bomu,
…nakuja…’akamsogelea msaidizi wake kwenye hiyo kesi na kkumnong’oneza jambo, rafiki yake akakunja
uso, hakupenda abakie peke yake, lakini aliona hilo jambo alilokuja nalo rafiki
yake ni la muhimu ….akakubali aondoke, nakesi ikaendelea,
Alipofika ofisini kwake,akaichukua ile barua na kuiangali kwa
makini, akaichukua ile CD’s , na kuiweka kwenye mashine ya kuikagua na kugundua
kuwa haina hatari, akaichukua na kuingia ndani ya chumba chake cha siri, na
kuiangalia…halafu akamwambia huyo aliyeileta kuwa anaifanyia kazi,...
*****
Mkuu mimi nataka nionane na huyo mshitakiwa, faragha, bila
ya kuwepo wakili wake, ….’akasema wakili mwanadada.
‘Kwanini, siunajau sheri zilivyo….’akasema mkuu.
‘Najua lakini wakati mwingine inabidi ufanye hivyo, ili
kuweza kufanikisha sheria inayotaka kukiukwa…’akasema.
‘Kwani kuna nini umegundua…?’ akauliza mkuu.
‘Hayo ni maswala ya kimahakama, na mbinu za kisheria, kuna
kitu nataka kuhakiki…nikifanikiwa nitakuja kukuambia, wewe jitahidi nionane na
huyo mtu kwa faragha…’akasema na kuondoka.
Ilikuwa usiku na wakili mwanadada akaweza kukutansihwa na
Jangiri, akamwangali kwa makini kabla hajamuuliza swali, nia ni kutaka kumjua
hulka yake, kila mtu na hulka yake, ukiijulia unaweza ukamsoma na hata
kumgundua kuwa anasema ukweli au uwongo,…
‘Mimi naamini kuwa kweli wewe sio uliyemuua Kimwana…’akasema
na kumfanya Jangiri ashikwe na mshangao,akasema;
‘Wewe dada mjanja sana, ndani ya mahakama umekuwa
ukinishinikiza mimi kuwa ndiye muuaji naua wanawake wasio na hatia…sasa unakuja
na mbinu yako hii….hunipati ng’ooo, sawa mimi sio muujaji nimeshasema huko
mahakamani sasa unataka nini kwangu…’akasema.
‘Ndio maana nataka ushirikiano wako, kama wewe sio muujai ni
nanii aliyemuua Kimwana…nilikipaya fununu kutoka kwako, tutaweza kumshika huyo
muuaji, nikuulize swali, wewe na kimwana mlijuana toka lini, ..’akauliza.
‘Hayakuhusu hayo , kama uantaak nijibu lolote, kwanza
namuhitaji wakili wangu,….’akasema na kumwangali huyo wakili kwa mashaka.
‘Sikiliza nikuambia, …mimi napenda sana kuwa mkweli , na mtu
mkweli kwangu ni rafiki mwema, na nikikuahidi kuwa nitakusadia, ujue kweli
nitafanya hivyo…nataka nikusaidie, lakini pia nataka haki ikitendeke, ili
tumjue aliyemuua Kimwana,….kwa uchunguzi wangu, ile risasi ilitoka kwenya
bastola yako sio hiyo iliyomuua Kimwana….lakini kuna ujanja umetumika na huo
ukweli umefutika,lakini kwa kupata maeezo kutoka kwako naweza
kuufichua…’akasema wakili.
‘Una uhakika na hilo…..?’ akauliza Jangiri.
‘Nina uhakika ndio maana nikatafuta njia za kuongea na wewe,
ili nipate maelezoo yatakayoniwezesha kulinda hoja ayangu….ukishirikiana na
mimi, kesi ya mauaji juu yako itafutika,…siwezi kukuahidi makosa mengine,
lakini hilo la mauaji ninaweza kukuahdi,ikiwa utaniambai ukweli….’akasema
wakili.
‘Ukweli upi unaotaka kutoka kwangu…?’ akauliza.
‘Kwanza niambia jinsi gani ulivyomjua Kimwana….kama kweli
ulivyodai kuwa ulikuwa ukipenda na isingelikwua rahis kwako kumuua…?’ akauliza,
na yule jamaa alikaaa kwa muda kifikiria,akasema baadaye.
‘Ina maana kesi ya mauaji ianweza ikafutwa, na huenda kama
nikufungwa sitafungwa kwa kesi ya mauaji na kweli sio mimi niliyemuua
Kimwana…ni nani basi kafanya hivyo…inawezekanakabisa,nakumbuka
vyema….’akatulia.
‘Hebu kumbuka vyema,….lakini kwanza niambia ulivyomjua
Kimwana…?’akasema wakili.
‘Kimwana ni bosi wangu, lakini kabla ya kuwa bosi wangu,
….alikuwa rafiki yangu..’akatulia na kuwa kama anakumbuka jambo,…na baadaye ndio
akaanza kuhadthia maisha yake na Kimwana…
*******
`Kimwana alikuwa rafiki yangu toka zamani sana, naweza
kukiri mimi ndiye mwanaume wa kwanza kumjua, …na huenda naweza kukiri kuwa mimi
ndiye niliyemuharibu. Nasema hivyo kwasababu, nyingi tu, achilia mbali
kumuingiza mjini.
`Kipindi narudi nyumbani nikiwa na pesa za kumwanga kutoka
na madili yetu ya hapa na pale, nilikutana na huyo msichana akiwa antokea
shule, nikampla lifti , kipindi hicho nilikuwa na gari, maana pesa ilikuwa
hainichezi mbali, nikamtamani huyu binti, licha ya kuwa alionekana mdogo,lakini
alishakuwa msichana aliyevunja ungo.
`Nikaanza kumtongoza, na unavyojua wasichana wa kijijini,
wanajifanay hawapendi kumbe wanapenda, na kumba huyo binti alishakuwa na hisi
hizo zakimapenzi, labda kutokana na makundi rika au aliwahi kusimuliwa au kufundwa,
kwahiyo hata nilipokuwa nikiongea naye, alionekana kujihami kikubwa….’akasema
Jangiri.
‘Hata hivyo kumbe sifa zangu zilikuwa mdomoni mwa kila
msichana, siku ya pili yake nilipomtamkia kuwa nampenda na nipo tayari kumpa
chochote anchotaka ,akaniambai kwua na yeye ananipenda, ila yeye anachotaka ni
mimi nimchkuea tukaishii naye mjini,kwani masiha ya kijijini hayataki…nikaona
mambo sio ndiyo hayo.
Tukasuka mpango,nikamtorosha huyo binti na kuja naye
mjini,…kipindi hicho niliwahi hata kuwekwa ndani kwa ajili yake, maana wazazii
wake walikuja kugundua kuwa mimi ndiye nilimyemtorosha wakanitumia maaskari,
nikakamatwa na kuwekwa ndani.
Nilikaa siku tatu, na aliyewezesha mimi kutoka na huyo huyo
binti,aliwaendea polisi na kuwaambia kuwa mimi ni mchumba wake, na
hakunitosroha yeey, ila yeey ndiye alitoroka an kuja kwangu, kwahiyo kam ni
kumshika wamshike yeye,…
Wazazi walikuja juu kweli, lakini Kimwana alikuwa kazimia
kwangu, akawa hawajali wazazi wake, na kuwaambia kuwa hataniacha mimi kamwe
kwasababu keshanipenda na huko kijijini harudi. Basiwazazi wangefanya nini,
ikabidi wakubali shingo upande.
Nikawa naishi na huyu binti, lakini taarifa zangu zilifika
hukoo kijijini kuwa mimii nafanya shughuli za kijamabzi, kwahiyo binti yao
atapotea, na wakaja kunifuata kuwa wanamtaka binti yao kwasababu mimi ni
jamabzi, nikawahamaki,nilihamaki kweli na Kimwana naye akinisadia na hata
akawafukuza wazazi wake na kuwambai kuwa wasimfuate fuate kuhusu maisha
yake….na ikawa mwishoo wa wazazi wake kumfuatilia.
Maisha yana kkupnda na kushuka, ikafikia mahli sina pesa, na
dili hazipatikani, nikaona sas nitaumbuka na Kimwana ni mtu wa amtumizi,
alikuwa mrembo, kama ulivyomuona na kila mwanaume alikuwa akimtaka, kwahiyo
ilibidi niwe natumia ikiukweli,…sasa nikawa sina kazi ya maana nikawa sina pesa
na kimwana akaniambai moja kwa moja kuwa yeye alinipednea kwasabbu yapesa, sina
pesa, kwahiyo …
‘Ina maana alikuwa hakupendi ,alikuwa akipedna pesa zako
tu….?’ Wakili akimuuliza.
‘Ndivyo ilivyokuwa,na kiukweli Kimwana hana habari na
mapenzi haya ya kupenda eti, nakupenda kimoyoni, yeye anapenda matumizi,
labda niseme mpenzi wake ni pesa, kama
huna pesa huna matumizii huna nfasi kwa huyo binti…’akaseam jangiri.
Basi nikaona nitamkosa, lakini nikabuni mbinu,, nikaoan kwa
ajili ya urembo wake. Lazima nimtumie,nikamawambi nipo tayari kumuachie
ajirushe na wanauem wengine,ilimradi tuapete pesa, lakini tufanye mbinu za
kuishi, nikamsuka mapaka akakubali, tukaanza kazi ya kurubuni wanaume wa watu
wenye pesa,…’
‘Kwa vipi….?’akauliza wakili.
‘Yeye kwasaabbu ya urembo wake, wapo matajiri waliokuwa
wakimtaka, na hawo matajiri walikuwa na ndoa zao,tulichokuwa tukifanya ni yeye
kukubali kwenda nao nyumba za wageni, na mimi nakuja baadaye nikiwa na cheti
cha ndoa kuonyesha kuwa huyo ni mke wangu, na tunamshikilia huyo tajiri kuwa
asipotupa kiasi fulani cha pesa tuankwenda kutoa taarifa polis na
kwamkewake,….wengi walikuwa wakitoa pesanyingi tu, wengine walikuwa wakigoma…
Siku moja nikakutana na mama mmoja ,alikuwa akiendesha gari
lakifahari, nikavutiwa nalo, mwanzoni nilitaka nifanye mpango na washikaji
tuliibe, lakini siku ya pili yake nikakutana na huyo mwanamke akaniita na
kuniambai kutokana na mwili wangu anaona nitafaa kuwa mlinzi wake, lakini
kwanza anatka anaifundishe jinsi gani ya kuwa mlinzi….nikakubali na kwelii
nikapitia chuo cha mafunzo ya ulizni ,kutumi asilaha,nilikuwa najua kutumia
silaha kabla,lakini hapo nilifundishwa kutumiasilaha ya aian yoyote, silaha
jisni ilivyo, na uliznii wa hali ya juu.
‘Basi nikatulia an huyu tajiri mwanamke, na kumwambia Kimwana
kuwa sasa nimepta kazi, atulie nyumbani, haat hivyo pesa niliyokuwa nikipta
ilikuwa haitoshi, ikawa tunafananya dili zetu hizo hizo na siku moja huyu
tajiri yangu akaniuliza Kimana ni nani wangu,..
‘Yule ni mpenzi wangu, kani vipi?’nikasema.
‘Nahitaji kufungua chuo cha warembo, na yeye namuona ni
mrembo kweli, unaweza kumshawishi ajae kwenye hicho chuo,….’akaniamabii na mimi
nikamwambai ahkuna shida, nikamwambia Kimana licha ya kwa mwanzoni aliktaa,
lakini baadaye akakubali na ikawa mwanzo wa yeye kujuana na mama Docta.
Akiwa na mama Docta akapanda chati,nakuanza kunsiahau
mimi,lakini sikujali, maana kazi ninayo, na kama ni wanawake nikiataka
Napata,lakini kiukweli Kimwana nilipenda sana, na hata nikaja kumtamkia kuwa
nataka nimuoe, alicheka sana sikuu hiyo….
‘Lakini mbona nasikia alikuwa lkiolewa na wanuem wengi, au
ndio hiyo kazi aliyokuwa kapewa na huyu mama Docta.?’ Akauliza wakili.
‘Kimwana sio mke wa kuweka ndani, mtu amabye angeliweza
kuishi naye na kuelewana naye, ni mimi peke yake, maaan namjua toka utotoni,
najua nini anachokitaka, na tabia zetu zinaendena wengina wote waliomuoan
zilikuwa ndoa za kibiashara tu…hilo
ninauhakika nalo…ila alipokuja kuolewa na huyo mwanaume,…nani huyu Msomali,
pale niliona mabadiliko, inaonekana alimpenda kiukweli…lakini hata hivyo hata
kama alimpenda kiukweli, badi alikuwa na kasoro, hakuna na pesa, na
kiwamanamapenzi kwake ni pesa…’akasema.
‘Sasa ilikuwaje Kimwana akawa ndio bosi wako?’ akauliza.
‘Kutokana na utendaji wa kikazi, mimi nilikuwa mkali wa
ulinzi na kutumia silaha, tulikuja kugudnu akwua Kiwamana ana maadui wengi
sana, basi tukakubaliana kuwa kila anapokwenda niwe nayemimi,na kwa viletulikua
tukijua kabla haikuw ashida kwangu,….
‘Haya sasa niambia ilikuwaje siku ile y atukio.
‘Siku ile ya tukio. …nilipata taarifa kuwa wewe unatakiwa
uondoek duniani…kwa pesa nyingi tu’ akasema.
‘Ni nani alikupa hiyo taarifa au ni nani aliataka mimi
niondoke dunianai?’ akauliza wakili.
‘Haina haja ya kumtaja mpaka hapo unaweza kujua ni nani,
licha ya kuwa sikutaka kukuambia yote hayo,lakini kwa vile umenihakikishai kuwa
mimi sio muuaji wa Kimwana nitakuambia kila kitu….
********
Baada ya kumaliza mazoezi ya kulenga shabaha, Wakili
mwanadada alimwangalia mkuu kwa muda bila kusema kitu, hata mkuu akajikuta
akijiuliza kwanini huyu mwanadada kila mara ananiangali sana , na ameligundua
hilo mara nyingi, hakutaka kumuuliza, akasubiri, akijua kuwa subira huvuta heri
, huenda kuna kitu anatka kuniambia;
‘Mkuu unajua sana kulenga shabaha,…’akasema wakili
mwanadada.
‘Unanitania, katika walenga shabaha, mimi nipo mbali sana, ….huoni hata wewe leo umenishinda kwa
mbali sana, kwa ujumla mimi siwezi kujisfu kuwa nina shabaha, katika kundi letu
sisi mwenye shabaha sana ni wakili wetu mkuu kwenye kitengo chetu cha sheria,
kila tukifika hapa hakosi hata mara moja,
ana kipaji sana cha shabaha….
‘Mimi sijawahi kuja naye, nikamuona anavyplenga shabaha,natamani nimuone,ili nijue siri ya
uwezo wake huo…nasikia hali yake ni tete, huu ugonjwa wa shinikizo la damu,
unawasumbua watu wengi sana siku hizii…’akasema wakili huku akijaribu kuwaza
jambo.
‘Kwakweli yule ni mkali wa shabaha,…na ni mtu mwenye afya
sana, nashindwa kuelewa hili shinikizo limemshindaje,…lakini ndio hivyo, mwili
wa binadamu ni mwili tu, unawezwa ukalazwa kitandani kwa kuchomwa na sindani
kwenye kidole,…unajua kama isingelikuwa haya matatizo yaliyomkumba, tungekuwa
naye hapa, lakini natumai atayashinda yote,… …’akasema mkuu.
‘Kwani ana matatizo mengine, nilisikia ana matatizo ya
kifamilia, …ilikuwaje….?’ Akauliza wakili mwanadada.
‘Ina maana wewe hujui hayo au unaniuliza kiubembe, hujui
kuwa alikuwa na tuhuma nzito, iliyosukwa na hawa wahuni,…, na picha mbaya
zikatolewa , …akaja kudaiwa pesa nyingi tu na hawo wahuni, alihangaika na baadaye akaamua kulitoa hili
jambo kwetu kisiri, tukasuka mpango ili kuwakamata hawo watu,lakini hatukufanikiwa,…hata
hivyo lilikwisha, ila hapo ndipo afya yake ilipooanza kutetereka…’akasema mkuu.
‘Ina maana ndio maana hakutaka kushiriki kwenye hii kesi?’
akauliza wakili.
‘Haiwezi ikawa ndio sababu ya moja moja,….kwasababu
tulishayamaliza mataizo yake , waliomfanyia hivyo ni vibaka wa kawaida tu,…Siku
walipomletea hizo picha,alipatwa na mshituko mkubwa, na tangu siku hiyo anasema
kuwa amekuwa akipata maumivu makali upande wa kushoto,…na limekuwa ni tatizo
ambalo linamfanya ashindwe kutimiza wajibu wake, anahitaji mataibabu ya hali ya
juu…’akasema mkuu.
‘Unajua hili tatizo halina asili kwa jamii zetu, na mtu
anaweza akafumaniwa isiwe na tatizo, lakini jinsi uchumi unavyokuwa, na watu
kuingia katika maswala ya kisheria katika kurithi mali, …na vitu kama hivyo,
tatizo hilo linakuwa moja ya janga, maana unakuta labda utajiri upo kwenye
familia ya mke, na mume kwao ndio hohe hahe, …..’akasema mwanadada na kutulia
kwanza.
‘Kuna kesi moja iligubikwa na mambo hayo,…katika makubaliano
ya ndoa ,mume aliambiwa kama atakutwa na tatizo,lakashifa hasa hiyo ya kuvunja
sheria za ndoa, ya kufumaniana,au madawa ay kulevya, ….basi ndoa itakuwa
imevunjika…sasa mke akampata mshikaji mwingine ,akaona njie pekee ya kuachana
na mumewe, na kumtumbukiza kwenye kashfa, na alichofanya nii kumtegea mwanamke….’akatulia
kwanza.
Akasuka huo mpango ukiwashirikisha
mke wa mtu na mshikaji wake, wakamtegea huyo mume wa huyo mke, …wakamtafuta
msichana, hawa wanawake wanaojua hizo kazi, wanachohitaji wao ni pesa tu,…na
wanaume mlivyo wazaifu, akategeka na tendo likafanyika na picha zikachukuliwa,….hutaamini
hilo lakini lilitokea….
‘Sasa hapo tamaa ikatawala, huyo mshikaji alichokuwa akimpendeahuyo
mke ni pesa, mengine yanakuja tu, kwasababu ya pesa, na tamaa ya huyo mshikaji
ikamtuma afanye jambo jingine, kwasababu ule mpango wa kumkamatisha huyo mume
wa huyo mke, huyo mshikaji, alikuwa akiujua kiundani na ushahidii uliotakiwa ni
picha ya tukio, yeye akaona kuwa kumbe anaweza kuzitumia hizo picha kuchuma
pesa kirahisi,….’Yule wakili mwanadada akatulia na kumwangalia mkuu wake kama
kweli anamsikiliza na kumuelwa akaendelea kusimulia hiyo kesi kwa kusema.
‘Baada ya lile tukio ushahidi ambayo ni picha akawa kabakia
nazo huyo mshikaji, na wakapanga nini kitakachofuata…kwahiyo sasa ilibakia vitendo,…mke
aanzishe chokochoko kuwa mume wake anatembea nje ya ndoa keshavunja mkataba,….kuna
kitu kilitakiwa huyo mshikaji akifanye kwanza, lakini jamaa akawa hatimizi hiyo
ahadi ili yule mke anze kashikashi, ingwaje kwa ndani ya familia, alishaanza
kwa kumshutumu huyo mume kuwa anatembea nje ya ndoa,na mume akawa mkali na kukataa
kata kata, na kudai ushahidi,….
‘Nia ya huyo mke ilikuwa ni hivyo,kuwa aachane na huyo mume
ili aje baadaye aolewe na mshikaji wake, sababu ni kuwa mume wake ni mvivu
katika maswala ya ndoa,…alimpenda kwa muonekano wa nje, kumbe mambo mengina
hayatimiziki kihivyo, na siku alipokutana na huyo mshikaji kisiri akagundua
kuwa kumbe kuna mambo ambyo hayapati kwa mumewe, yapo kwa waume wengine, kwa
tamaa hizo akaona kuwa huyo mshikaji ndiye
anayefaa kuwa mume wake…’akatulia huyo mwanadada na kutizama chini.
‘Haya mambo yapo jamani, yanatesa jamii, usione watu
wanatoka nakusema mume wangu ,au mke wangu, kuna watu hawana raha inapofikia
katika hayo maswala, lakini yanapelekwa kimiya kimiya, watu wanaumia kimiya
kimiya, kwa kuogopa kashifa, kwa kuogopa, kuwa atatoa siri ya ndoa,…ndoa
zinalege lega, na wengine wanaachana kwa kisngizio kumbe chanzo ndio hicho kisichoelezeka.
Sasa kumbe hata huyu mshikaji, hakuwa na upendo wa dhati na
huyo mke wa mtu, ni kwasababu ya kutaka pesa na mali,..wapo wanaume wa namna
hiyo wengi tu, kama walivyo wanawake wengi tu,..’akasema huyo mwanadada na mkuu
akatikisa kichwa kukubali, akawa huku akiwa anasikiliza hicho kisa cha hiyo
kesi anayoielezea wakili mwanadada.
‘Basi huyo mshikaji akawa anachukua nakala moja ya picha na kumpelekea
yule mume wa mtu kwa siri, na kumwambia kuwa asipomlipa pesa nyingi atalifikisha hio
swala kwa mkewe….hebu fikiri hapo jamaa alipoziona picha picha alikuwaje,
alichanganyikiwa, …. akahaha, na kweli akampa hizo pesa, kwani pesa alikuwa
nazo, kwa kupitia kwenye miradi ya familai ya mke, lakini muonja asali haonji
mara moja, huyo mshikaji akafanya ndio sehemu ya kupatia kipato, ikawa ni
kamchezo….’yule wakili mwanadada akacheka na kusema.
‘Unajua nimegundua jambo, ibilisi akishaingia akilini,
anakuchezea kama mtoto mdogo, huyu mke,akawa anazitaka zile picha, lakini huyo
mshikaji anamzungusha, na bila hizo picha ndoa haiwezi kuvunjika na yeye keshampenda
huyo mshijaki, na mume kambana hapati mwanya wakwenda kuyapata yale ambayo
hayapati toka kwa mume wake…akaona anawekewa kiwingu, akaamua kumtegea sumu
mumewe….’akatabasamu tena huyo wakili na mkuu akasisimuka na hicho kisa,
akasikiliza.
‘Sasa siku hiyo kaweka kinywaji chenye sumu, akitarajia kuwa
mume wake akija atakinywa, yeye akwa akwa aktoka kwenda kazini, ….mume ana
kawaida ya kurudi mchana kupata chochote, nay eye ndiye mwenye ufunguo wa
nyumba, akasahau kuwa alishawahi kumpamshikaji wake ufunguo, ili wakija asipate
shida ya kuingia ndani.
Sasa huyo mshikaji anajua kuwa huyo mume muda kama huo
anakuwa nyumbani, na alihitaji pesa, akachukua nakala nyingine na kwenda huko
kwa huyo mume wa mtu, alipofika kwa kujiamini,akafungua mlango na kuingia ndani….
Alipoingia ndani akakuta
mezani kuna maandalizi,….yeye hakujali
sana, akacukua kinywaji na kujimiminia, akajisaidia na chakula, hana wasi wasi,
huku akisubiri, akaweka gilasi mojayakinywaji akanywa, akawa anakunywa
taratibu, huku akisubiri, lakini jamaa siku hiyo akakutwa an foleni y magari
akawa kachelewa kufika….mshikaji , akaongeza gilasi ya pili,….tumbo likaanza
kuuma.
‘Mume anakuja anakuta mtu yupo chini mapofu yanamtoka mdomoni…hajiwezi
kabisa, haraka akaita polisi na jamaa akakimbizwa hospitalini,…akafia njiani, na yule mume akashikwa kuwa yeye ndiye kampa
sumu huyo jamaa….sasa angali kesi kama hiyoilivyo,…inaumiza kichwa sana,
unataiwa uwe makini, ukichukulia juu juu, utasema kweli, huyo mume ndiye kampa
sumu huyo jamaa kwasababu ya hiyo tabia ya kumdai pesa kwa kutumia picha chafu…..’akatulia
na kumwangaliwa mkuu .
‘Hapo ndipo uchunguzi ,akili na hekima inatakiwa kutumiwa,
ukichukuliwa juu, juu ,….utafunga watu wasio na hatia,….ndio maana naogopa sana
hizi kesi zinazofungamana na jamii na,…mahusiano,…usipokuwa makini utaumiza watu
wengi wasio na hatia badala ya kuponya….’akasema wakili mwanadada.
‘Nikuulize hicho kisa kina maana gani kuhusiana na hii kesi
yetu….?’akauliza mkuu.
‘Nilikuwa nataka kukuonyesha jinsi gani haya mambo ya kutishiwa
kuwa usiponilipa pesa nitatoa siri yako jinsi sasa yanavyokuwa sumu kwa watu,
ni kama uuaji wa namna fulani,inabidi jambo hili lifanyiwe kazi ya haraka na
jamii ielimishwe,…’akasema huyo wakili mwanadada na alipoona mkuu katulia
akamuuliza swali,
‘Na je tuhuma kwa huyu mama docta kuwa ana michezo kama hiyo
imefikia wapi,?’ akauliza wakili.
‘Tatizo kubwa mambo kama haya hayana ushahidi, wale wanaotishiwa
hawataki kuyaleta hayo mashitaka kwenye usalama, wakiogopa kuwa siri zao
zitajulikana, na matokeo yake tunawapa nguvu sana hawa watu, nafikiri ndio
silaha yao kubwa, kuwa wanafanya namna ambayo mtu waliyemlenga hataweza kutoa
hiyo taarifa polisi
‘Huyu mama docta kaondoka muda sasa…..nafikiri karudi kwao
Kenya….’akasema mkuu
Wakili akatulia kwa muda bila kusema neno, huku mara kwa
mara akimwangalia mkuu huyo, alijua kabisa hisia zake zinaweza zikapingwa na
mkuu, lakini kila mara alipowaza hilo jambo aliona inawezekana, kinachotakiwa
ni kuhakikisha anakusanaya ushahidi, na ikiwezekana amshirikishe huyo mkuu kwa
kila hatua, akageuka na kumwambia mkuu;
‘Samahani sana mkuu, usione kwanini nimetulia kimiya hivi
bila kusema kitu, nilikuwa nikijaribu kujiuliza mwenyewe , na kutafakari kile
ninachotaka kukuambia, najua unaweza usiniamini, lakini nahisi inaweza ikawa
ndivyo hivyo, licha ya kuwa sijaweza kupata uhakika wa moja kwa moja…..’akasema
wakili mwanadada na kutulia kwa muda.
‘Wewe ongea na kusikiliza…’akasema mkuu.
‘Mimi nina uhakika kuwa Jangiri siyo yeye aliyemuua
Kimwana,…’akasema wakili.
‘Unasema nini,…mbona ushahidi upo, na yeye mwenyewe alikiri
mbele yangu kuwa yeye alikuwa na nia ya
kukua wewe, lakini bahati mbaya risasi ikampiga Kimwana,amekuja kukana baada ya
kumpata huyo wakili wao,….kama umjuavyo yule wakili anajua kucheza na sheria….’akasema
mkuu.
‘Risasi iliyomuua Kimwana haikutoka katika bastola aliyokuwa
nayo Jangiri,taarifa hii imebadilishwa kinamna, na ukweli kufichwa, kitu
ambacho kinaonyesha kuwa kuna mtu ndani ya wanausalama anahusika na hiki kifo,
au kafanya hivyo kwa shinikizo fulani, lakini hilo la kufanya kwa shinikizo
halina nguvu, ….naoana kafanya hivyo makusudi ili kuhakikisha kuwa ukweli
haujulikani,…’akasema wakili mwanadada.
‘Haiwezekani…’akasema mkuu na kumwangali wakili mwanadada.
‘Nakuomba leo twende kule Mbezi nikakuonyeshe ushahidi ambao
huenda ukakufungua macho, lakini usiseme lolote kwanza kwa mtu yoyote, hili ni kati
yangu mimi na wewe tu…kwasababu ikijulina nina uhakika kutakuwa janga kubwa…’akasema
wakili mwanadada, na kumfanya Mkuu kumwangali huyu mwanadada kwamacho ya
wasiwasi.
‘Usishangae mkuu, mambo hayo yapo, na usione kuwa labda u
kiongozi, unafuatilia kitu, kuna mengine yanatokea nje ya uwezo wako, leo
unayemuamini na yeye akajitahidi kuaminika kesho anaweza akahini huo uaminifu,
huenda kajitihadi kikomo cha uwezo wake, akasema basi ngoje iwe hivi, akijua
haitajulikana…hujafa hujaumbika, na ukistaajabu ya Musa ….’akasema huyo
mwanadada na kabala hajamalizia huo usemi simu ikapigwa…..
NB: Sehemu hii nimeiandika kwa shida sana, sijui kama ipo sawa, tuzidi kuwepo kwenye sehemu ijayo..
WAZO LA LEO: Katika maisha haya usichukulie kila jambo kuwa ni sawa au si sawa, cha muhimu ni kuwa na uhakika nacho,maana ukiwa na pupa na hamasa ya kila jambo unalolisikia utaumia bila faida yoyote; Pupa huua, na mwenye pupa hadiriki kula tamu.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Hongera mkuu,...nimeona hapo juu unatangaza watu waweke matangazo, ina maana hujapata hata moja, haiwezekani,mbona wenzako wana matangazo kibao,ya makampuni ya simu,na blog zao hazina mambo muhimu saaana.
Nikuambie kitu, huwezi kupata mpaka uwaendee.kwakweli inaniumiza sana, kuona muandishi mzuri kama wewe huna tangazo hata moja, likakusaidia.
Kufumaniwa sio mchezo kila kitu kinasinyaa.
Hongera mwaveja
Post a Comment