Mkuu wa kituo, alikuwa makini kusikilza maelezo kutoka kwa
vijana wake aliowatuma kazi sehemu tofautitofauti, na kila mara alikuwa akiuliza maswali ili kuona jinsi
kazi ilivyofanyika, na kila alipoona kuna kasoro, aliagiza hiyokasoro iafanyiwekazi
na taarifa azipate mara moja, na sehemu nyingine alipanga yeye mwenyewe
kufuatilia, na hata pale vijana wake walipomaliza kutoa maelezo na ushahidi wa
hapa na pale hakurizika na hizo taarifa, akasema ;
‘Mimi bado naona kuna walakini,hata hivyo tujue kuwa kuna
kesi mbele yetu, tukiwa na muuaji,ambaye licha ya ushahidi tulio nao , bado
hatujaweza kusema yeye ndiye muuaji, licha ya yeye mwenyewe kukiri kuwa ndiye aliyemuua Kimwana….’akatulia
na kuwaangalia vijana wake.
‘Kwa maelezo yake mwenyewe kakiri kuwa lengo lake lilikuwa sio
kumuua huyo Kimwana, anadai kuwa lengo lake lilikuwa kumua huyo wakili, kwasababu
ya yeye kumuona ni mfuatiliaji wa ammbi ya watu,…ingawaje tumegundua kuwa
atakuwa kautumwa, lakini hilo kakataa katakata. Sasa sisi tunatakiwa kutafuta
ushahidi wa kuonyesha kuwa katumwa, na nani,….ndiyo kazi yetu kubwa
iliyopombele yetu….’akawaangalia ijana wake.
‘Kwa tetesi tunaweza tukamjua ni nani….’akasema kijana
mmojawapo.
‘Hatutaki tetesi,tunahiji ushahidi ulikamilika,….kama
tungelipata mwanya wa kumbana huyu jamaa mapema tungeligundua mengi, lakini
keshakuwa kwenye mamlaka ya wakili wake, na sasahakubali kujibu swali ahdi
wakili wake awepo….’akasema mkuu.
‘Sasa swali langu ni kuwa je vielelezo vyote mnavyo…risasi,mashahidi,
maana hii kesi inaweza ikatugeukia, ikizingatiwa kuwa tunapambana na kundi
lenye pesa, …na hatujajua kuwa wakili atakuwa ni nani…
‘Mkuu na mimi nilikuwa na pendekezo, kesi hii kama
tutamuachia mtu wetu inaweza ikala kwetu, kama unavyokumbuka kuwa alishatishiwa
na hawa watu,na mpaka sasa familia yake ipo hatarini,….inaweza ikamuathirri
kisaikolojia, na akashindwa kutimiza wajibu wake vyema, mimi naona safari hii
tumchukue huyo mwanadada wakili, atusaidie?’ akatia pendekezo mmoja wa askari.
‘Hiyo haiweekani kwa sasa,maana sisi tumekamilika,
hatuhitaji wakili mwingine, ndiyo yeye bado yupo serikalini,tunawezakumtumia,
lakini kwanini tumng’ang’anie yeye , wakati watu wapo wengi, itakuwa ni aibu
kwetu,…hilo haliwezekani…hata hivyo sisi sehemu yetu kuamua ni nani,hilo ni
swala ka muendesha mashitaka…’akasema na huku akitabasamu.
‘Nimsema hivyo kwasababu huyu wakili mwanadada anajua mengi
kuhusu hili kundi, na alishaanza upelelezi wake mwenyewe, na kama alivyotuambia
kuwa anafanya utafiti binafsi, natumai kwa kupitia yeye tunaweza
tukalisambaratisha hili kundi,….’akasema kijana mwingine.
‘Wazo lako ni zuri, nitalifikiria, lakini mpaka niongee na muendesha
amshitaka, wetu , kama atakubali,kwangu haina shaka, kwani hata hivyo kama
ulivyosema, yule jamaa yetu tunayemtegeema amekuwa katika wakati mgumu na hawa
watu, ….lakini ndio moja ya majukumu yake, sizani kuwa anaweza kutishika na
vitisho vya hawo…watu’akasema mkuu.
Na mara simu ya mezani ikalia, na Mkuu akaisikiliza kwa
makini na ilipomaliza, akawageukia vijana wake na kuwaambia;
‘Hawa watu wamemuwekaMbogo kuwa ndiye wakili wao. Na kama
mnavyomjua Mbogo, ni wakili asiyeshindikana, nashindwa kuelewa kwanini
anakubali kumsimamia mtu kama huyo ambaye keshakiri kuwa ni yeye aliyeua…..na
kundi lenyewe ni kundi ambalo kila mtu anajua ni kundi lenye malengo mabaya,
..yote ni kwa ajili ya pesa,hata hivyo, hakijaharibika kitu….’akasema na
kutulia.
‘Lakini mkuu hatuna shaka kila kitu tunacho ushahidi wa
kutosha, na ….’kabla hajamaliza simu ikaita , na mkuu akaipokea, na kusikiliza
kwa muda.
‘Kwahiyo wewe unapendeekeza hivyo, huoni kuwa utakuwa
umejivunjia hadhi yako…?’ akauliza.
‘Sawa hata sisi tulikuwa na wazo kama hilo, na nilikuwa
mbionikuja kwako kuliongea hili swala na wewe, sasa ilimrdi umekubali mwenyewe
, basi tutamshauri mwendesha mashitaka, akikubali itakuwa vyema, nafikiri wewe
ungeliongea na yeye uone atasemaje ….sawa kabisa,haina shaka…’akatulia
kusikiliza.
‘Bado ana ajira na serikali, na tutatumia mwanya huo, na
sizani kama atakataa, kwasababu mwenyewe alishajitumbukizwa huko,…nitaongea nayeye
mwenyewe….’akatulia tena kusikiliza.
‘Sawa nitafurahi na mimi nikiwa kwenye hichi kikao, ili
nitie shinkizo,…kwani sisi tumeshakusanya ushahidi wa kutosha,….’akasema mkuu.
‘Kesho saa tano, sawa kabisa, nitakuwepo…’akakata simu na
kuwaangalia vijana wake, na kusema,
‘Naona tulichokuwa tukiwaza ndio hicho hicho, wakili wetu
kakisema, anasema kutokana na hali aliyo nayo, anaogopa isije ikaleta malumbano
baadaye ambayo yataihusisha family yake, kama mjuavyo hilo kundi lilivyo,
halitajali kuzalilisha yoyote, na kutokana na matukio liyokumbana nayo, ambayo
bado hayajapatiwa ufumbuzi,anaona kesi hiyo tumpe huyo mwanadada
wakili….’akasema mkuu.
‘Safi kabisa…’wakasema wale vijana wapiganaji.
‘Na kwa vile bado yupo kwenye ajira ya serikali kwa upande
mmoja, tutaitumia nafasi hiyo hiyo, kabla hajajitoa kabisa, ….kwani alishasema
kuwa anataka kujitoa kabisa serikalini na kuanzisha kampuni yake mwenyewe
mwakani….’akasemamkuu.
‘Sisi tutatoa ushirikiano wa kila namna, maana kama yupo
wakili Mbogo, basi kesi hiyo itakuwa sio ya mchezo, anastahili kupambana na
huyo mwanadada…’akasema mmoja wa vijana wapiganaji.
‘Kwani huyo Mbogo ana sheria zake mwenyewe,…mimi sioni
kwanini tumuogope,….’akasema mmoja wa askari ambaye mudamwingi alikuwa kimiya.
‘Sio kumuogopa, ila tunachotaka hapa ni hii kesi imalizike
tukiwa tumewaweka ndani wale wote wanaostahili na kuhakikisha kuwa hakuna mtu
anayedhulumiwa haki yake kwa ujanja wa kipesa,…hatutaki kupata picha mbaya kama
watu wanavyodai kuwa kuna watu wanahukumiwa bila makosa.
‘Namfahamu sana Mbogo ni mjanja wa kisheria anaweza akawachanganya
watu kwenye mahakama na mwisho wa siku tukajikuta tumepoteza kesi, na wakati tunaye
muuaji, ambaye keshakiri, ila njua akifika mahakamani atadai kuwa kakubali kwa
sababu ya kuogopa au tulitumia nguvu…’akasema mkuu.
Kwamtaji huo nataka mwenyewe kufuatilia kila kitu,ili
nihakikishe kuwa tunao ushahis wa kutosha, na hakuna sehemu ambayo tutakuwa
tumepsasau, ili tukiwakabadhi hawa watu wa sheria wasija wakatusumbua tena
baadaye, kazi yetu tutakuwa tumemaliza, na sisi tujiande vyema wakati wa
kujieleza, maana mnajua amswali ya huyo jamaa,isije kesi ikakugeukia
wewe….’akasema mkuu.
‘Mkuu mbona unatutisha, …’wakalalamika vijana.
*******
Kilikuwa kikao cha dharura ndani ya chumba cha mwenda
mashitaka wa serikali, na walikuwa wakiongea kuhus kesi iliyokuwa mbele yao, na
vidhibiti mbambali vikawekwa mbele , huku maswali mbambli ya kiulizwa, na
baadaye wakili mwendesha ambaye alitarajiwa kuisimamia hiyokesi, akasema;
‘Huyu mwanadada mbona hajafika,au kaghairi,…?’ akauliza.
‘Shida ya usafiri, hebu jaribu kumoigia simu…’akasema
mwendesha mwendesha mashitaka
Simu ilipigwa lakini ikawa inasema anayepigiwa simu anatumia
simu yake, waendelee kusubiri,na hata waliposubiri na kupiga tena na tena iakwa
haipatikani,….na muda uakwa unakwenda,na wote wakaingiwa na wasiwasi.
‘Mimi hapa naona kuna tatizo, inabidi nitume watu
wamfuatilie, maana dunia hii ina mengi….’akasema mkuu wa kituo, na akawapigia
vijana wake wafike nyumbani kwa wakili,na baada ya nusu saa simu ikapigwa kuwa
wakili hayupo nyumbani kwake,…
‘Atakuwa kaenda wapi, je mlipouliza majirani
wanasemaje?’akauliza.
‘Wanasema tangu jana hajaonekana kurudi nyumbani…na
tulipofika sehemu yake ambayo anafanyia kazi binafsi na watu wake walisema
aliondoka ofisini mapema tu, ….kwahiyo kuna sehemu atakuwa kakwama, au hatujui
kama baya lolote kakumbana nalo …’akasemahuyo kijana.
‘Fanyeni uchunguzi haraka mjua nini kimetokea.
********
Mtoto wa Msomali, alifika nyumbani kwa wakili kama
walivyopanga, alipofika akakuta mlango umefungwa, akawauliza majirani,
wakamwambia hajafika,tena tangu jana….akashituka, akaona hisia zake zilivyomtuma
ni kweli kuna tatizo, akaamua kuzifuata hizo hisia zake, zikampeleka hadi
Mbezi, akiwa kapanda pikipiki, ambayo aliikodi na kuiendesha mwenyewe, akafika
sehemu ile ile ambayo waliwahi kuweka pikipiki yao.
Alipofika hapo
akamuomba huyo jamaa ambaye washajuana kuwa aiache pikipiki yake pale atairudia
baadaye, na akatoka pale hadi eneo la nyumba mpya zinazojengwa na kulitafuta
lile jengo, na alipoliona akaangaza huku na kule na alipoona kuwa hakuna shaka
akaanza kutembea hadi kwenye lile jengoambalo hisi zake zilimtuma, safari hii
hakukuta walinzi,akaangaza huku na kule akaona hakuna mtu,akasukuma mlango na
kuingia ndani ya hilo jengo. Alipoingia humo ndani kulikuwakimiya, akajua kuwa
hakuna mtu.
Akawa anaingia huku na kule kutafuta chochote kutoakana na
hisia zake na mara akasikia sauto ya mtu akija usawa wake, akajificha, kwenye
upenyo wa mlango. Alitokea jamaa mmoja, pande la mtu, akiwa hana wasiwasi,
akapita na kutoka nje…
Alijitoa pale alipojificha na kumchunguza huyo jamaa, yule
jamaa alikuwa nje ya jengo, akiwa anaangalia
huku na kule, nafikiri ni kuhakikisha kuwa hakuna mtu karibu na alipothibitisha
hilo, akachukua simu yake na kuanza kupiga namba, akatulia na kusema,;
‘Tayari nimeshamfikisha,…nimfanye nini…?’ akauliza.
‘Hajazindukana,…..nina uhakika huo….na nimemfunga barabara
’akasema na kutembea kuelekea getini, alipofika pale akakaa kwenye kiti
kilichokuwa kimewekwa, na kusubiri.
Mimi nikaona nisipoteze muda nikaanza kutafuta wapi huyo mtu
alipowekwa, na ni wakili kweli, au hisia zangu zimenituma vibaya. Bahati nzuri
nikamkuta mwanamke kafungwa kwenye chumba kimojawapo, sikupoteza muda nikaenda
na kumfungua haraka, Alikuwa wakili kweli, alikuwa bado kapoteza fahamu,
nikajaribu kimtingisha ili azindukane, lakini haikuwa rahisi
hivyo,inaonekana walimchoma sindani ya
madawa.
Niliona wazo nzuri ni kumchukua hadi kwenye chumba kingine
ambapo kutakuwa na usalama, huku nikitafuta njia za msaada,maana kupambana na
lilepandikizi la mtu ni kujidanganya na sijui kama ana silaha gani,….Nilitafuta
chumba kingine nikamuweka huyo wakili na kuhakikisha kuwa nimefunga ule mlango.
Nilitoka hadi nje,na kumchungulia yule jamaa nilimkuta bado
kakaa pale akiwa anavuta sigara, ina maana kuna mtu anamsubiri, baadaye
nikahisi kama mtu anagonga, kwa ndani,nikarudi hadi kule nilipomuweka yule
mwanamke, nikamkuta keshazindukana ingawaje bado hakuwa na nguvu, na muda huo alikuwa kashikilia kichwa chake.
‘Vipi unajisikiaje , maana hapa upo hatarini…..’nikamwambia.
‘Kichwa kinaniuma sana…..hapa tupo wapi?’ akauliza.
‘Wamekuleta huku mbezi, na kuna jamaa nje analinda,
…’nikasema.
‘Sasa sikiliza, una simu yako hapa…’akaniuliza.
‘Ndio,….’nikampa na mara akapiga simu na kuongea na huyo
anayempigia, akamuelEzea hali ilivyo, na baadaye akanigeukia na kusema,;
‘Sasa wewe sikiliza , kaa sehemu , hakikisha kuwa hakuna mtu
anayekuona, mimi nataka kucheza karata yangu maaluma, hebu nionyeshe wapi
walipokuwa wameniweka,….’akasema.
‘Mimi nikampeleka na akasema nimfunge kama ilivyokuwa
kafungwa, lakini nisikaze kamba,…’nikafanya hivyo.
‘Sasa wewe kaa sehemu ,na akija mtu, toa ishara, nitajua,
…..Kuna watu wa usalama wapo njiani,lakini nataka nione nini walichokusudia juu
yangu hawa watu, na ni akina nani..’akasema
na nilitaka kumshauri,lakini nikatulia na kufanya kama alivyotaka.
Ilipita muda kidogo na mara nikasikia mlio wa gari nje ya geti, na gari hilo likasimama,nje
kabisa ya hilo jengo barabarani. Ukapita
muda na baadaye mlango
ukafunguliwa,akaingia jamaa mmoja, akaongea na yule jamaa wa mwanzo, ….
Mara huyu jamaa mpya akaja kuingia ndani ya nyumba, nikatoa
ishara kama alivyonielekezwa na Wakili,….
Yule jamaa alikuja na kusimama mlangoni,hakuingia ndani,
akawa anavuta sigara,…na kwa ndani nikasikia kama mtu anatembea, nikasogea na
kuangali,….nikamuona mwanamke akiwa kavaa miwani ya jua, na manywele mengi…..sijui
aliingiaje mle ndani.
**********
Mkuu alijaribu kila njia kuhakikisha kuwa anafika Mbezi
haraka iwezekanavyo, na licha ya foleni, lakini aliweza kufika eneo hilo
aliloelekezwa na akaliacha gari lake mbali kabisa na lile jengo, akiwa na
vijana wake maalumu, wakalikariba hilo jengo wakitembea kwa mguu. Baadaye akawaambia vijana wake.
‘Sitaki tujulikane kuwa tumefika hapa, ….kwahiyo fanyeni kila njia muhakikishe kuwa mumeingia ndani ya
lile jengo bila kujuliana, kuna watu humo, kwahiyo msipitie getini, na mengine
tutajua huko huko….’akasema na baadaye wakatawanyika kila mmoja na njia yake.
Mkuu alifika sehemu aliyoelekezwa, akapanda ile ngazi na
kuteremkia ndani, humo akajisogeza hadi chumba alichoelekezwa, akatulia na
kusikiliza, hakusikia kitu, akasogea hadi shemu nyingine na alipotaka kufungua
mlango akashitukia akiguswa bega. Akageuka haraka akiwa an bastola mkononi.
‘Huko usiingie mkuu, njoo kwa hapa….’akajikuta akitizamana
na jamaa ambaye alikuja baadaye kummkumbuka.
‘Wapo wangapi?’ akauliza.
‘Nje wapo wawili, na ndani yupo mwanadada…..ambaye kaingia
kule alipolala wakili, wakili sasa kajifanya bado kazirai, kwahiyo huyo
mwanadada anajaribu kama kamzindua, hajafanya kitu…’akasema.
‘Ok, safi,…ngoja nikapaone hapo mahali, nione nini cha
kufanya…..’akasema mkuu.
Walipofika hapo ambapo wanaweza kuona ndani wakakuta yule
mwanadada kashikilia bastola na anailenga kwa yule wakili,…licha ya kuwa wakili
bado alikuwa kajilazakama vile bado kapoteza fahamu, lakini baadaye yule
mwanadada mwenye manwele mengi, akaielekeza chini bastola yake na kusema;
‘Kwanini nyie watu hamunielewi……kwanini mnanifuatilia katika
maisha yangu, mimi sipendi…sipendi kabisa kuua watu…lakini mnanilazimisha nifanye yale nisiyoyataka, nyinyi
kweli mnayajua maisha yangu mimi,hamyajui,jinsi gani nilivyoteseka,……’akasema
na kuanza kutoa machozi na mara wakili akatingishika na kujifanya ndio
kazindukana.
Yule mwanadada mwenye manwelemengi alipo-ona vile
akamnyoshea bastola na kusema,‘Haya amuka haraka nataka uniambie kwanini
unanifuata fuata…..na utubu dhambi zako tayari kwenda huko kusikojulikana?’akasema
huku kaielekeza bastola yake kwa wakili.
‘Mimi nipo wapi hapa…?’akauliza wakili.
‘Upo mahakamani, na hakimu ni mimi,….unasemaje?’ akasema
huyo mwanadada.
‘Sikiliza nikuambie kitu,mimi sio nia mbaya na wewea…mimi
tangia mwanzo nataka kukusaidia, …nataka kujua kisa ni nini, mpaka ukatumbukia
kwenye haya mazila, najua ipo sababu kubwa ambayo imekukwaza, nia na lengo
langu ni ili niweze kukusaidia sina nia mbaya na wewe….’akasema wakili.
‘Unisaidie mimi….hahaha….wewe unisadie mimi, wakati unataka
kuniweka kitanzi kwa kutumia sheria zenu,bila kujali hisia za watu, nyie
mnafikiri hayo yaliyotokea yalikuwa dhamiri yangu..mimi sio mnyama kiasi
hicho,mimi sio mhuni au mtu mbaya kiasi
hicho,….ila kuna watu wamesababisha nikawa hivyo..na bado wanazidi kuibuka
wengine kunifanya nizidi kuwa hivyo….najua mwisho wake ni nini..lakini lazima
kwanza nilipize kisasi…’akasema na kucheka kicheki cha dharau.
‘Kisasai gani hicho…?’akauliza wakili.
‘Kisasi gani hicho,….hata nikikuambia huwezi
kuamini,kwasababu hayajawahi kukukuta wewe….na siri ya mtungi aijueye
kata,….haina haja ya kukuambia, kwasababu huhitajiki kuishi kwa vile umeshaingilia
mambo yangu na umeniharibia mipangilio ..’akasema.
‘Sikiliza ,nimeshakuambia lengo langu ni kukusaidia, mimi ni
wakili maalumu wakusaidi akina mama, kwasababu najua machungu ya akina mama,
hata mimi nimepitia machungu mengi, najua jinsi gani wakina mama
wanavyojisikia,…..lakini ili tusaidieni inabidi wewe uniambie ukweli ni nini
tatizo lako, kwanini ufikie kusema unataka kulipiza kisasi..kwanani?’akauliza.
‘Nimekuambia haina haja ya w ewe kujua, kwasababu kile
niliyewahi kumwambia, aliniona mimi kama mjinga, wananiona mimi kama sina moyo
wa kusahau na kuvumilia yote yaliyonikuta, lakini hawajui kuwa nilijaribu
hivyo,lakini kila siku iliyopita, nilijikuta nikiumia, ….nikiteseka, na akili
ikawa haifanyi kazi ,badala yake inakuwa ikiwaza jambo lile lile….’akatulia.
‘Mimi licha ya kuwa wakili, nimesomea mambo ya akina
mama,….jisni gani ya hulka na matatizo ya kina mama..nia na lengo langu ni
kutaka kusaidia wale waliopo kwenye matatizo kwa kupitia sheria…mimi nipo tayari
kukusaidia kwa njia hiyo, uansemaje…?’ akasema wakili.
‘Eti unsemaje, utanisaidiaje wakati wewe ni maiti….naapa
lazima nikuue….nilishaapa kuwa kila atakeyeingilia mambo yangu nitaammaliza…. Na
wewe umeyaingilia kwa kiherehere chako, umeshindikana kwa njie nyingine kwa
vile wewe ni mjanja,lakini hutakuwa mjanja mbele ya bastola…’akasema huku
akiangalia ile bastola.
‘Ndio kama unataka kuniua utaiua, lakini ingelikuwa vyema
ukaniambai nini kilihokusibu,…nina hamu sana kusikia kisa chako,…tafadhali
naomaba unisimulie….’akasema wakili.
‘Sina muda huo….najua sasa hivi wanakusubiri wenzako
ukasimamie kesi ya yule mnayemuita muuaji, na yoe hayo umesababisha
wewe….isingelikuwa wewe hayo yoye ysingelitokea, nilishapanag mambo yangu
vyema, …ukaja wewe umetibua, sasa …’akapiga risasi ilimkosa hatua chache pale
alipolala wakili.
‘Hivi unajua nini unachokifanya….ukiniua mimi ndio uatakuwa
umetatua matatizo yako,…haiatsaidia kitu, nakuomba tafadhali niambie nini
kilichokusibu, ili tuweze kusaidiana ,hakua lisilowezekana, wewe unaonekana
kabisa huna roho ya kinyama, nahisi ni matatiz yanayowakuta watu na kujikuta
wametumbukia katika madhila mabaya,….’akasema wakili.
Mkuu akanibonyeza, na kuniambia nikae hapo hapo nisiondoke
maana anataka kuingia humo ndani,…mimi sikuweza kumjali, maana nilishahisi kuna
hatarai huyo mwanadada anaweza kufayua hiyo bastola na kumuua wakili.
Wakati huo, Mkuu alishatoka pale, na kuingia taratibu kwenye
kile chumba, jinsi walivyosimama, wakili aliweza kumuona mkuu akiingia lakini
huyu mwanadada alikuwa kampa mgongo mkuu, na wakati huo huo, na mimi
snilishaondoka mle nilipokuwa,na kukaidi amri ya mkuu sikukubali wakili azurike
nikiwa naona, nikapita upande wa pili wa hicho chumba, ambapo kuna mlango wa
mbele, na wakati huo huo mkuu akapitia mlango wa nyuma, ambao pia huingili
kwenue hicho chumba.
Yule mwanadada akashituka nafikiri aliona macho ya wakili
yakipepesa kuwa kaona kitu, akajaribu kugeuza kichwa na kuangalia huku na kule,
mkuu akajificha kwenye mifuko ya `cement’ iliyokuwemo humo ndani, yule
mwanadada hakuamini, akasogea nyuma, na
kuangalia , huku akiwa kaishikili bastola yake madhubuti,halafu akageuka kule
alipolala wakili mwanadada, akamkuta keshajifungua,…akashangaakidogo na kusema kwa sauti kali;
.
‘Wewe…’alito hiyo sauti huku akionyoshea bastola kule alipo wakili
mwanadada akitaka kumlenga risasi, na mimi nikajitokeza kwe mbele, akaniona, akashikwa na mshangao,…akanielekezea
bastola mimi,….
Kwanza alichofanya ni kuziangusha nywele zake kwa mbele,
sijui alifanya hivyo kwa makusudi gani, au ndio `ukitaka kumuua nyani
usimtizame machoni, akanyosha mkono kama vile anataka kufyatua risasi,lakini
akasita na kugeuza jicho kumtizama wakili,…
Akawa kama
ananisogelea pale nilipo, na macho yetu yalipokutana, ….lilikuwa jicho moja
ndilo lillilokuwa wazi, maana jicho la
pili lilikuwa limefunikwa na nywele, aliniangalia kwa hasira, akataka kuongea
jambo, lakini akasita, akageuka kumwangalia wakili mwanadada,…akamgeuzia ile
bastola, na halafu akanigeukia kinitizama mimi, maajbu yakatokea….
Aliponiangalia safari hii, alishikwa na butwa, kwanza macho
yakamtoka kwa woga, halafu,akapanua mdomo kutaka kupiga yowe, haraka akaitupa
ile bastola chini na kugeuka kutaka kukimbia huku akipiga ukulele wa kuwaita
jamaa zake kuwa waje ndani haraka, kule alipotaka kukimbilia akajikuta
anakutana uso kwa uso na Mkuu, ….
Akasimama,woga ukamuingia, nyuma hakuendeki,mbele yupo mkuu,
bastola keshaitupa pembeni, ….na kwa wasi wasi akageuka nyuma kuniangalia
akanikuta bado nimesimama vile vile nikiwa nimeshikwa na mshangao…..akaitupia
jicho ile bastola, ipo mbali na alipo, hawezi kuifikia kabla hajazurika,….
Kwakweli kama huyu mwanadada angelikuwa na nia ya kuniua
angeshaniua, maana badala hata ya kujihami au kusimama sehemu ambayo hata kama
huyu mwanadada angetaka kuitumi silaha ningeweza kuikwepa, lakini mimi nilikuwa
nimesimama kama gogo, namwangalia huyo mwanadada.
Sijui kuna kitu gani nilikuwa nahisi, sio kwasababu ya ile
hali ninayoiskia mara kwa mara kuwa nahisi kuwa watu karibu yangu, hapana,
nilikuwa nikihisi jambo kutoka kwa yule mwanadada, na hata nikijiuliza huyu
mwanamke ni nani…mbona ananikimbia,….na jicho lile lilikuwa kama limeniingia
akilini na kujikuta moyo ukienda mbio,sikujua ni kwanini. Na sura hii ni ngeni
, ….hapana sio ngeni,…hapo nikawa nababaika, sikuwa na uhakika …nikageuka nyuma
kuangalia, kama kuna kitu chochote sikuona kitu…
‘Mwisho wako umefika…huna haja ya kujihangaisha tena,…upo
chini a ulinzi …’akasema mkuu akiwa kashikilia bastola mkononi akiwa kamlenga
huyo mwanadada bastola. Yule mwanadada kwanza alimuangalia kwa wasiwasi na
baadaye akatabasamu na kucheka, akasema;
‘Na wewe,…Hahahaha….eti nipo chini ya ulinzi, …badala ya kuwaonyeshea hawo
mashetani,unanionyeshea mimi, huwaoni hawo mashetani….waliopo nyuma ya huyo…mnafiki.’akasema
huku akionyeshea mkono wake kwangu, na Mkuu hakugeuza kichwa kuniangalia,
akizania kuwa hizo ni mbinu za huyo mwanamke anatumia mbinu za kumuhadaa, ili
aweze kufanya lolote, akageuza jicho tu na kuendelea kumlenga yule mwanadada.
Na mara wakingia
vijana wengine wawili wakiwa na bastola na kwenda moja kwa moja pale
aliposimama yule mwanamama, wakamshika na kumpekua, mmoja akaichukua ilebastola
iliyokuwa chini ambayo alikuwa nayo huyo mwanadada.
‘Mmmmh,haya nifungeni pingu, twendeni huko gerezani, ….ila
bado nasema kuwa lazima nitalipiza kisasi…hata kama huyo….’akaninyoshea mikono
mimi, `Atakuwa na walinzi wa jabu…hakuna atakayemchukua….ambaye na kuwa hai….’akasema
na kwa uwoga akajaribu kugeuka kuniangalia, lakini kwa haraka akageuza kichwa
kuwamgalia wakili na mkuu, akamgeukiwa wakili na kusema.
‘Na wewe unayejitia kimbelembele nakuona unanyemelea mauti
yako, nimeshakugundua, ….ipo siku tutakutana na mimi, safari ijayo, sitaongea
na wewe tena….itakuwa vitendo, haya nifungeni hizo pingu tuondoke….’akasema
huyo mwanadada.
Wale jamaa nje, walisikia wakiitwa, wakakurupuka mbio, na
walipofika mlangoni wakakutana na silaha zikiwa zimeelekezwa kwao, na
kuamrishwa kuwa wapo chini ya ulinzi, na bila ubishi wakanyosha mikono juu na
kufungwa pingu wote wakaingizwa kwenye karandinga na kupelekwa kituo cha
polisi.
Je ndio mwisho wa kisa hiki,…..
*********
Ilipofika hapa nikabakia mdomo wazi, kwani rafiki yangu
alisimama, na mimi nikiwa an maswali mengi ya kumuuliza, je huyu mwanadada
anataka kulipiza kisasi kwa nani na kwanini…na ni nani huyo mwanadada?
Akaniangalia na kusema,….’siku nyingine nimechoka….’
Jamani tuwepo kwenye mtiririko wa hitimisho la kisa hiki,
ili tuone ni nini kilimsibu huyu mwanadada mpaka akaamua kufanya hayo aliyoyapanga
kuyafanya,ni kisasi cha nini, na kwanini….je huyu mwanadada ni nani?
Wengi wanaweza kutoa hoja hapa,…mbona hapa ilitakiwe iwe ndio hitimisho la hiki kisa, ….tukumbuke kuwa hilo ni tukio lilitokea na sio
tamithilya ya kubuni, na tukumbuke kuwa kisa hiki kinaitwa HUJAFA HUJAUMBUKA,
sio KISA CHA KISASI….Kisa cha kisasii kinakuja …..
WAZO LA LEO:
Hulka,tabia na hata fikara za watu hutofautiana, na usizani kuwa upendavyo wewe
ndivyo apendavyo mwenzako, au kila unachokijua na mwenzako atakijua
….unavyowaza wewe inaweza ikawa tofauti na awazavyo mwenzako,…ili twende sawa,
tujaribu kuvumiliana, kuuliza na kukubali kasoro za wenzako ukijua na wewe una kasoro zako,... bila kunyanyapaana.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Yaani kweli huu mtiririko lazima uendelee kuishia hapa itakuwa na maswali mengi sana mimi nataka kujua mwanadada ni nani na kwanini. Wazo la leo ni funzo nzuri sana. NAMI NAONGEZEA KAMA MTU UNA DUKUDUKU BASI LA MUHIMU NI KUULIZA USIJIFANYE KUJUA.
m3 au yule alokuwa mchumba wake mtoto wa msomali utotoni mhh bora ni subiri muendelezo hata hivyo jamaa amekumbana na matatizo mingi ya dunia lazma atakuwa makini sana na life yake
m3 una kipaji sio siri yaani sichezi mbali na glog hii
hongera
Ni kweli dada Yasinta, kuna maswali mengi bado hayajajibiwa ndani ya kisa hiki, na kila hatua majibu yatakuja yenyewe...
Mpendwa Samira huenda upo sawa,hata mimi sijui ngoja tuone,maaana kisa bado kinaendelea,tupo pamoja
Post a Comment