Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, May 16, 2012

Hujafa hujaumbika-36Mkuu wa kituo, alikuwa makini kusikilza maelezo kutoka kwa vijana wake aliowatuma kazi sehemu tofautitofauti, na kila mara alikuwa akiuliza maswali ili kuona jinsi kazi ilivyofanyika, na kila alipoona kuna kasoro, aliagiza hiyokasoro iafanyiwekazi na taarifa azipate mara moja, na sehemu nyingine alipanga yeye mwenyewe kufuatilia, na hata pale vijana wake walipomaliza kutoa maelezo na ushahidi wa hapa na pale hakurizika na hizo taarifa, akasema ;

‘Mimi bado naona kuna walakini,hata hivyo tujue kuwa kuna kesi mbele yetu, tukiwa na muuaji,ambaye licha ya ushahidi tulio nao , bado hatujaweza kusema yeye ndiye muuaji, licha ya yeye  mwenyewe kukiri kuwa ndiye aliyemuua Kimwana….’akatulia na kuwaangalia vijana wake.

‘Kwa maelezo yake mwenyewe kakiri kuwa lengo lake lilikuwa sio kumuua huyo Kimwana, anadai kuwa lengo lake lilikuwa kumua huyo wakili, kwasababu ya yeye kumuona ni mfuatiliaji wa ammbi ya watu,…ingawaje tumegundua kuwa atakuwa kautumwa, lakini hilo kakataa katakata. Sasa sisi tunatakiwa kutafuta ushahidi wa kuonyesha kuwa katumwa, na nani,….ndiyo kazi yetu kubwa iliyopombele yetu….’akawaangalia ijana wake.

‘Kwa tetesi tunaweza tukamjua ni nani….’akasema kijana mmojawapo.

‘Hatutaki tetesi,tunahiji ushahidi ulikamilika,….kama tungelipata mwanya wa kumbana huyu jamaa mapema tungeligundua mengi, lakini keshakuwa kwenye mamlaka ya wakili wake, na sasahakubali kujibu swali ahdi wakili wake awepo….’akasema mkuu.

‘Sasa swali langu ni kuwa je vielelezo vyote mnavyo…risasi,mashahidi, maana hii kesi inaweza ikatugeukia, ikizingatiwa kuwa tunapambana na kundi lenye pesa, …na hatujajua kuwa wakili atakuwa ni nani…

‘Mkuu na mimi nilikuwa na pendekezo, kesi hii kama tutamuachia mtu wetu inaweza ikala kwetu, kama unavyokumbuka kuwa alishatishiwa na hawa watu,na mpaka sasa familia yake ipo hatarini,….inaweza ikamuathirri kisaikolojia, na akashindwa kutimiza wajibu wake vyema, mimi naona safari hii tumchukue huyo mwanadada wakili, atusaidie?’ akatia pendekezo mmoja wa askari.

‘Hiyo haiweekani kwa sasa,maana sisi tumekamilika, hatuhitaji wakili mwingine, ndiyo yeye bado yupo serikalini,tunawezakumtumia, lakini kwanini tumng’ang’anie yeye , wakati watu wapo wengi, itakuwa ni aibu kwetu,…hilo haliwezekani…hata hivyo sisi sehemu yetu kuamua ni nani,hilo ni swala ka muendesha mashitaka…’akasema na huku akitabasamu.

‘Nimsema hivyo kwasababu huyu wakili mwanadada anajua mengi kuhusu hili kundi, na alishaanza upelelezi wake mwenyewe, na kama alivyotuambia kuwa anafanya utafiti binafsi, natumai kwa kupitia yeye tunaweza tukalisambaratisha hili kundi,….’akasema kijana mwingine.

‘Wazo lako ni zuri, nitalifikiria, lakini mpaka niongee na muendesha amshitaka, wetu , kama atakubali,kwangu haina shaka, kwani hata hivyo kama ulivyosema, yule jamaa yetu tunayemtegeema amekuwa katika wakati mgumu na hawa watu, ….lakini ndio moja ya majukumu yake, sizani kuwa anaweza kutishika na vitisho vya hawo…watu’akasema mkuu.

Na mara simu ya mezani ikalia, na Mkuu akaisikiliza kwa makini na ilipomaliza, akawageukia vijana wake na kuwaambia;

‘Hawa watu wamemuwekaMbogo kuwa ndiye wakili wao. Na kama mnavyomjua Mbogo, ni wakili asiyeshindikana, nashindwa kuelewa kwanini anakubali kumsimamia mtu kama huyo ambaye keshakiri kuwa ni yeye aliyeua…..na kundi lenyewe ni kundi ambalo kila mtu anajua ni kundi lenye malengo mabaya, ..yote ni kwa ajili ya pesa,hata hivyo, hakijaharibika kitu….’akasema na kutulia.

‘Lakini mkuu hatuna shaka kila kitu tunacho ushahidi wa kutosha, na ….’kabla hajamaliza simu ikaita , na mkuu akaipokea, na kusikiliza kwa muda.

‘Kwahiyo wewe unapendeekeza hivyo, huoni kuwa utakuwa umejivunjia hadhi yako…?’ akauliza.

‘Sawa hata sisi tulikuwa na wazo kama hilo, na nilikuwa mbionikuja kwako kuliongea hili swala na wewe, sasa ilimrdi umekubali mwenyewe , basi tutamshauri mwendesha mashitaka, akikubali itakuwa vyema, nafikiri wewe ungeliongea na yeye uone atasemaje ….sawa kabisa,haina shaka…’akatulia kusikiliza.

‘Bado ana ajira na serikali, na tutatumia mwanya huo, na sizani kama atakataa, kwasababu mwenyewe alishajitumbukizwa huko,…nitaongea nayeye mwenyewe….’akatulia tena kusikiliza.

‘Sawa nitafurahi na mimi nikiwa kwenye hichi kikao, ili nitie shinkizo,…kwani sisi tumeshakusanya ushahidi wa kutosha,….’akasema mkuu.

‘Kesho saa tano, sawa kabisa, nitakuwepo…’akakata simu na kuwaangalia vijana wake, na kusema,

‘Naona tulichokuwa tukiwaza ndio hicho hicho, wakili wetu kakisema, anasema kutokana na hali aliyo nayo, anaogopa isije ikaleta malumbano baadaye ambayo yataihusisha family yake, kama mjuavyo hilo kundi lilivyo, halitajali kuzalilisha yoyote, na kutokana na matukio liyokumbana nayo, ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi,anaona kesi hiyo tumpe huyo mwanadada wakili….’akasema mkuu.

‘Safi kabisa…’wakasema wale vijana wapiganaji.
‘Na kwa vile bado yupo kwenye ajira ya serikali kwa upande mmoja, tutaitumia nafasi hiyo hiyo, kabla hajajitoa kabisa, ….kwani alishasema kuwa anataka kujitoa kabisa serikalini na kuanzisha kampuni yake mwenyewe mwakani….’akasemamkuu.
‘Sisi tutatoa ushirikiano wa kila namna, maana kama yupo wakili Mbogo, basi kesi hiyo itakuwa sio ya mchezo, anastahili kupambana na huyo mwanadada…’akasema mmoja wa vijana wapiganaji.
‘Kwani huyo Mbogo ana sheria zake mwenyewe,…mimi sioni kwanini tumuogope,….’akasema mmoja wa askari ambaye mudamwingi alikuwa kimiya.

‘Sio kumuogopa, ila tunachotaka hapa ni hii kesi imalizike tukiwa tumewaweka ndani wale wote wanaostahili na kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayedhulumiwa haki yake kwa ujanja wa kipesa,…hatutaki kupata picha mbaya kama watu wanavyodai kuwa kuna watu wanahukumiwa bila makosa.

‘Namfahamu sana Mbogo ni mjanja wa kisheria anaweza akawachanganya watu kwenye mahakama na mwisho wa siku tukajikuta tumepoteza kesi, na wakati tunaye muuaji, ambaye keshakiri, ila njua akifika mahakamani atadai kuwa kakubali kwa sababu ya kuogopa au tulitumia nguvu…’akasema mkuu.
  
 Kwamtaji huo nataka mwenyewe kufuatilia kila kitu,ili nihakikishe kuwa tunao ushahis wa kutosha, na hakuna sehemu ambayo tutakuwa tumepsasau, ili tukiwakabadhi hawa watu wa sheria wasija wakatusumbua tena baadaye, kazi yetu tutakuwa tumemaliza, na sisi tujiande vyema wakati wa kujieleza, maana mnajua amswali ya huyo jamaa,isije kesi ikakugeukia wewe….’akasema mkuu.

‘Mkuu mbona unatutisha, …’wakalalamika vijana.

*******
Kilikuwa kikao cha dharura ndani ya chumba cha mwenda mashitaka wa serikali, na walikuwa wakiongea kuhus kesi iliyokuwa mbele yao, na vidhibiti mbambali vikawekwa mbele , huku maswali mbambli ya kiulizwa, na baadaye wakili mwendesha ambaye alitarajiwa kuisimamia hiyokesi, akasema;

‘Huyu mwanadada mbona hajafika,au kaghairi,…?’ akauliza.

‘Shida ya usafiri, hebu jaribu kumoigia simu…’akasema mwendesha mwendesha mashitaka
Simu ilipigwa lakini ikawa inasema anayepigiwa simu anatumia simu yake, waendelee kusubiri,na hata waliposubiri na kupiga tena na tena iakwa haipatikani,….na muda uakwa unakwenda,na wote wakaingiwa na wasiwasi.

‘Mimi hapa naona kuna tatizo, inabidi nitume watu wamfuatilie, maana dunia hii ina mengi….’akasema mkuu wa kituo, na akawapigia vijana wake wafike nyumbani kwa wakili,na baada ya nusu saa simu ikapigwa kuwa wakili hayupo nyumbani kwake,…

‘Atakuwa kaenda wapi, je mlipouliza majirani wanasemaje?’akauliza.

‘Wanasema tangu jana hajaonekana kurudi nyumbani…na tulipofika sehemu yake ambayo anafanyia kazi binafsi na watu wake walisema aliondoka ofisini mapema tu, ….kwahiyo kuna sehemu atakuwa kakwama, au hatujui kama baya lolote kakumbana nalo …’akasemahuyo kijana.

‘Fanyeni uchunguzi haraka mjua nini kimetokea.

********

Mtoto wa Msomali, alifika nyumbani kwa wakili kama walivyopanga, alipofika akakuta mlango umefungwa, akawauliza majirani, wakamwambia hajafika,tena tangu jana….akashituka, akaona hisia zake zilivyomtuma ni kweli kuna tatizo, akaamua kuzifuata hizo hisia zake, zikampeleka hadi Mbezi, akiwa kapanda pikipiki, ambayo aliikodi na kuiendesha mwenyewe, akafika sehemu ile ile ambayo waliwahi kuweka pikipiki yao.
  
Alipofika hapo akamuomba huyo jamaa ambaye washajuana kuwa aiache pikipiki yake pale atairudia baadaye, na akatoka pale hadi eneo la nyumba mpya zinazojengwa na kulitafuta lile jengo, na alipoliona akaangaza huku na kule na alipoona kuwa hakuna shaka akaanza kutembea hadi kwenye lile jengoambalo hisi zake zilimtuma, safari hii hakukuta walinzi,akaangaza huku na kule akaona hakuna mtu,akasukuma mlango na kuingia ndani ya hilo jengo. Alipoingia humo ndani kulikuwakimiya, akajua kuwa hakuna mtu.

Akawa anaingia huku na kule kutafuta chochote kutoakana na hisia zake na mara akasikia sauto ya mtu akija usawa wake, akajificha, kwenye upenyo wa mlango. Alitokea jamaa mmoja, pande la mtu, akiwa hana wasiwasi, akapita na kutoka nje…

Alijitoa pale alipojificha na kumchunguza huyo jamaa, yule jamaa alikuwa nje ya jengo, akiwa  anaangalia huku na kule, nafikiri ni kuhakikisha kuwa hakuna mtu karibu na alipothibitisha hilo, akachukua simu yake na kuanza kupiga namba, akatulia na kusema,;

‘Tayari nimeshamfikisha,…nimfanye nini…?’ akauliza.

‘Hajazindukana,…..nina uhakika huo….na nimemfunga barabara ’akasema na kutembea kuelekea getini, alipofika pale akakaa kwenye kiti kilichokuwa kimewekwa, na kusubiri.

Mimi nikaona nisipoteze muda nikaanza kutafuta wapi huyo mtu alipowekwa, na ni wakili kweli, au hisia zangu zimenituma vibaya. Bahati nzuri nikamkuta mwanamke kafungwa kwenye chumba kimojawapo, sikupoteza muda nikaenda na kumfungua haraka, Alikuwa wakili kweli, alikuwa bado kapoteza fahamu, nikajaribu kimtingisha ili azindukane, lakini haikuwa rahisi hivyo,inaonekana  walimchoma sindani ya madawa.

Niliona wazo nzuri ni kumchukua hadi kwenye chumba kingine ambapo kutakuwa na usalama, huku nikitafuta njia za msaada,maana kupambana na lilepandikizi la mtu ni kujidanganya na sijui kama ana silaha gani,….Nilitafuta chumba kingine nikamuweka huyo wakili na kuhakikisha kuwa nimefunga ule mlango.

Nilitoka hadi nje,na kumchungulia yule jamaa nilimkuta bado kakaa pale akiwa anavuta sigara, ina maana kuna mtu anamsubiri, baadaye nikahisi kama mtu anagonga, kwa ndani,nikarudi hadi kule nilipomuweka yule mwanamke, nikamkuta keshazindukana ingawaje bado hakuwa na nguvu,  na muda huo alikuwa kashikilia kichwa chake.

‘Vipi unajisikiaje , maana hapa upo hatarini…..’nikamwambia.

‘Kichwa kinaniuma sana…..hapa tupo wapi?’ akauliza.

‘Wamekuleta huku mbezi, na kuna jamaa nje analinda, …’nikasema.

‘Sasa sikiliza, una simu yako hapa…’akaniuliza.

‘Ndio,….’nikampa na mara akapiga simu na kuongea na huyo anayempigia, akamuelEzea hali ilivyo, na baadaye akanigeukia na kusema,;

‘Sasa wewe sikiliza , kaa sehemu , hakikisha kuwa hakuna mtu anayekuona, mimi nataka kucheza karata yangu maaluma, hebu nionyeshe wapi walipokuwa wameniweka,….’akasema.

‘Mimi nikampeleka na akasema nimfunge kama ilivyokuwa kafungwa, lakini nisikaze kamba,…’nikafanya hivyo.

‘Sasa wewe kaa sehemu ,na akija mtu, toa ishara, nitajua, …..Kuna watu wa usalama wapo njiani,lakini nataka nione nini walichokusudia juu yangu hawa watu,  na ni akina nani..’akasema na nilitaka kumshauri,lakini nikatulia na kufanya kama alivyotaka.

Ilipita muda kidogo na mara nikasikia mlio wa gari  nje ya geti, na gari hilo likasimama,nje kabisa ya hilo jengo barabarani.  Ukapita muda  na baadaye mlango ukafunguliwa,akaingia jamaa mmoja, akaongea na yule jamaa wa mwanzo, ….

Mara huyu jamaa mpya akaja kuingia ndani ya nyumba, nikatoa ishara kama alivyonielekezwa  na Wakili,….
Yule jamaa alikuja na kusimama mlangoni,hakuingia ndani, akawa anavuta sigara,…na kwa ndani nikasikia kama mtu anatembea, nikasogea na kuangali,….nikamuona mwanamke akiwa kavaa miwani ya jua, na manywele mengi…..sijui aliingiaje mle ndani.

**********

Mkuu alijaribu kila njia kuhakikisha kuwa anafika Mbezi haraka iwezekanavyo, na licha ya foleni, lakini aliweza kufika eneo hilo aliloelekezwa na akaliacha gari lake mbali kabisa na lile jengo, akiwa na vijana wake maalumu, wakalikariba hilo jengo wakitembea kwa mguu. Baadaye  akawaambia vijana wake.

‘Sitaki tujulikane kuwa tumefika hapa, ….kwahiyo fanyeni  kila njia muhakikishe kuwa mumeingia ndani ya lile jengo bila kujuliana, kuna watu humo, kwahiyo msipitie getini, na mengine tutajua huko huko….’akasema na baadaye wakatawanyika kila mmoja na njia yake.

Mkuu alifika sehemu aliyoelekezwa, akapanda ile ngazi na kuteremkia ndani, humo akajisogeza hadi chumba alichoelekezwa, akatulia na kusikiliza, hakusikia kitu, akasogea hadi shemu nyingine na alipotaka kufungua mlango akashitukia akiguswa bega. Akageuka haraka akiwa an bastola mkononi.

‘Huko usiingie mkuu, njoo kwa hapa….’akajikuta akitizamana na jamaa ambaye alikuja baadaye kummkumbuka.

‘Wapo wangapi?’ akauliza.

‘Nje wapo wawili, na ndani yupo mwanadada…..ambaye kaingia kule alipolala wakili, wakili sasa kajifanya bado kazirai, kwahiyo huyo mwanadada anajaribu kama kamzindua, hajafanya kitu…’akasema.

‘Ok, safi,…ngoja nikapaone hapo mahali, nione nini cha kufanya…..’akasema mkuu.
Walipofika hapo ambapo wanaweza kuona ndani wakakuta yule mwanadada kashikilia bastola na anailenga kwa yule wakili,…licha ya kuwa wakili bado alikuwa kajilazakama vile bado kapoteza fahamu, lakini baadaye yule mwanadada mwenye manwele mengi,  akaielekeza chini bastola yake na kusema;

‘Kwanini nyie watu hamunielewi……kwanini mnanifuatilia katika maisha yangu, mimi sipendi…sipendi kabisa kuua watu…lakini  mnanilazimisha nifanye yale nisiyoyataka, nyinyi kweli mnayajua maisha yangu mimi,hamyajui,jinsi gani nilivyoteseka,……’akasema na kuanza kutoa machozi na mara wakili akatingishika na kujifanya ndio kazindukana.

Yule mwanadada mwenye manwelemengi alipo-ona vile akamnyoshea bastola na kusema,‘Haya amuka haraka nataka uniambie kwanini unanifuata fuata…..na utubu dhambi zako tayari kwenda huko kusikojulikana?’akasema huku kaielekeza bastola yake kwa wakili.

‘Mimi nipo wapi hapa…?’akauliza wakili.

‘Upo mahakamani, na hakimu ni mimi,….unasemaje?’ akasema huyo mwanadada.

‘Sikiliza nikuambie kitu,mimi sio nia mbaya na wewea…mimi tangia mwanzo nataka kukusaidia, …nataka kujua kisa ni nini, mpaka ukatumbukia kwenye haya mazila, najua ipo sababu kubwa ambayo imekukwaza, nia na lengo langu ni ili niweze kukusaidia sina nia mbaya na wewe….’akasema wakili.

‘Unisaidie mimi….hahaha….wewe unisadie mimi, wakati unataka kuniweka kitanzi kwa kutumia sheria zenu,bila kujali hisia za watu, nyie mnafikiri hayo yaliyotokea yalikuwa dhamiri yangu..mimi sio mnyama kiasi hicho,mimi sio  mhuni au mtu mbaya kiasi hicho,….ila kuna watu wamesababisha nikawa hivyo..na bado wanazidi kuibuka wengine kunifanya nizidi kuwa hivyo….najua mwisho wake ni nini..lakini lazima kwanza nilipize kisasi…’akasema na kucheka kicheki cha dharau.

‘Kisasai gani hicho…?’akauliza wakili.

‘Kisasi gani hicho,….hata nikikuambia huwezi kuamini,kwasababu hayajawahi kukukuta wewe….na siri ya mtungi aijueye kata,….haina haja ya kukuambia, kwasababu huhitajiki kuishi kwa vile umeshaingilia mambo yangu na umeniharibia mipangilio ..’akasema.

‘Sikiliza ,nimeshakuambia lengo langu ni kukusaidia, mimi ni wakili maalumu wakusaidi akina mama, kwasababu najua machungu ya akina mama, hata mimi nimepitia machungu mengi, najua jinsi gani wakina mama wanavyojisikia,…..lakini ili tusaidieni inabidi wewe uniambie ukweli ni nini tatizo lako, kwanini ufikie kusema unataka kulipiza kisasi..kwanani?’akauliza.

‘Nimekuambia haina haja ya w ewe kujua, kwasababu kile niliyewahi kumwambia, aliniona mimi kama mjinga, wananiona mimi kama sina moyo wa kusahau na kuvumilia yote yaliyonikuta, lakini hawajui kuwa nilijaribu hivyo,lakini kila siku iliyopita, nilijikuta nikiumia, ….nikiteseka, na akili ikawa haifanyi kazi ,badala yake inakuwa ikiwaza jambo lile lile….’akatulia.

‘Mimi licha ya kuwa wakili, nimesomea mambo ya akina mama,….jisni gani ya hulka na matatizo ya kina mama..nia na lengo langu ni kutaka kusaidia wale waliopo kwenye matatizo kwa kupitia sheria…mimi nipo tayari kukusaidia kwa njia hiyo, uansemaje…?’ akasema wakili.

‘Eti unsemaje, utanisaidiaje wakati wewe ni maiti….naapa lazima nikuue….nilishaapa kuwa kila atakeyeingilia mambo yangu nitaammaliza…. Na wewe umeyaingilia kwa kiherehere chako, umeshindikana kwa njie nyingine kwa vile wewe ni mjanja,lakini hutakuwa mjanja mbele ya bastola…’akasema huku akiangalia ile bastola.

‘Ndio kama unataka kuniua utaiua, lakini ingelikuwa vyema ukaniambai nini kilihokusibu,…nina hamu sana kusikia kisa chako,…tafadhali naomaba unisimulie….’akasema wakili.

‘Sina muda huo….najua sasa hivi wanakusubiri wenzako ukasimamie kesi ya yule mnayemuita muuaji, na yoe hayo umesababisha wewe….isingelikuwa wewe hayo yoye ysingelitokea, nilishapanag mambo yangu vyema, …ukaja wewe umetibua, sasa …’akapiga risasi ilimkosa hatua chache pale alipolala wakili.

‘Hivi unajua nini unachokifanya….ukiniua mimi ndio uatakuwa umetatua matatizo yako,…haiatsaidia kitu, nakuomba tafadhali niambie nini kilichokusibu, ili tuweze kusaidiana ,hakua lisilowezekana, wewe unaonekana kabisa huna roho ya kinyama, nahisi ni matatiz yanayowakuta watu na kujikuta wametumbukia katika madhila mabaya,….’akasema wakili.

Mkuu akanibonyeza, na kuniambia nikae hapo hapo nisiondoke maana anataka kuingia humo ndani,…mimi sikuweza kumjali, maana nilishahisi kuna hatarai huyo mwanadada anaweza kufayua hiyo bastola na kumuua wakili.

Wakati huo, Mkuu alishatoka pale, na kuingia taratibu kwenye kile chumba, jinsi walivyosimama, wakili aliweza kumuona mkuu akiingia lakini huyu mwanadada alikuwa kampa mgongo mkuu, na wakati huo huo, na mimi snilishaondoka mle nilipokuwa,na kukaidi amri ya mkuu sikukubali wakili azurike nikiwa naona, nikapita upande wa pili wa hicho chumba, ambapo kuna mlango wa mbele, na wakati huo huo mkuu akapitia mlango wa nyuma, ambao pia huingili kwenue hicho chumba.

Yule mwanadada akashituka nafikiri aliona macho ya wakili yakipepesa kuwa kaona kitu, akajaribu kugeuza kichwa na kuangalia huku na kule, mkuu akajificha kwenye mifuko ya `cement’ iliyokuwemo humo ndani, yule mwanadada hakuamini, akasogea nyuma,  na kuangalia , huku akiwa kaishikili bastola yake madhubuti,halafu akageuka kule alipolala wakili mwanadada, akamkuta keshajifungua,…akashangaakidogo na kusema kwa sauti kali;
.
‘Wewe…’alito hiyo sauti huku akionyoshea bastola kule alipo wakili mwanadada akitaka kumlenga risasi, na mimi nikajitokeza kwe mbele,  akaniona, akashikwa na mshangao,…akanielekezea bastola  mimi,….
Kwanza alichofanya ni kuziangusha nywele zake kwa mbele, sijui alifanya hivyo kwa makusudi gani, au ndio `ukitaka kumuua nyani usimtizame machoni, akanyosha mkono kama vile anataka kufyatua risasi,lakini akasita na kugeuza jicho kumtizama wakili,…

 Akawa kama ananisogelea pale nilipo, na macho yetu yalipokutana, ….lilikuwa jicho moja ndilo lillilokuwa wazi,  maana jicho la pili lilikuwa limefunikwa na nywele, aliniangalia kwa hasira, akataka kuongea jambo, lakini akasita, akageuka kumwangalia wakili mwanadada,…akamgeuzia ile bastola, na halafu akanigeukia kinitizama mimi, maajbu yakatokea….

Aliponiangalia safari hii, alishikwa na butwa, kwanza macho yakamtoka kwa woga, halafu,akapanua mdomo kutaka kupiga yowe, haraka akaitupa ile bastola chini na kugeuka kutaka kukimbia huku akipiga ukulele wa kuwaita jamaa zake kuwa waje ndani haraka, kule alipotaka kukimbilia akajikuta anakutana uso kwa uso na Mkuu, ….

Akasimama,woga ukamuingia, nyuma hakuendeki,mbele yupo mkuu, bastola keshaitupa pembeni, ….na kwa wasi wasi akageuka nyuma kuniangalia akanikuta bado nimesimama vile vile nikiwa nimeshikwa na mshangao…..akaitupia jicho ile bastola, ipo mbali na alipo, hawezi kuifikia kabla hajazurika,….

Kwakweli kama huyu mwanadada angelikuwa na nia ya kuniua angeshaniua, maana badala hata ya kujihami au kusimama sehemu ambayo hata kama huyu mwanadada angetaka kuitumi silaha ningeweza kuikwepa, lakini mimi nilikuwa nimesimama kama gogo, namwangalia huyo mwanadada.

Sijui kuna kitu gani nilikuwa nahisi, sio kwasababu ya ile hali ninayoiskia mara kwa mara kuwa nahisi kuwa watu karibu yangu, hapana, nilikuwa nikihisi jambo kutoka kwa yule mwanadada, na hata nikijiuliza huyu mwanamke ni nani…mbona ananikimbia,….na jicho lile lilikuwa kama limeniingia akilini na kujikuta moyo ukienda mbio,sikujua ni kwanini. Na sura hii ni ngeni , ….hapana sio ngeni,…hapo nikawa nababaika, sikuwa na uhakika …nikageuka nyuma kuangalia, kama kuna kitu chochote sikuona kitu…

‘Mwisho wako umefika…huna haja ya kujihangaisha tena,…upo chini a ulinzi …’akasema mkuu akiwa kashikilia bastola mkononi akiwa kamlenga huyo mwanadada bastola. Yule mwanadada kwanza alimuangalia kwa wasiwasi na baadaye akatabasamu na kucheka, akasema;

‘Na wewe,…Hahahaha….eti nipo chini  ya ulinzi, …badala ya kuwaonyeshea hawo mashetani,unanionyeshea mimi, huwaoni hawo mashetani….waliopo nyuma ya huyo…mnafiki.’akasema huku akionyeshea mkono wake kwangu, na Mkuu hakugeuza kichwa kuniangalia, akizania kuwa hizo ni mbinu za huyo mwanamke anatumia mbinu za kumuhadaa, ili aweze kufanya lolote, akageuza jicho tu na kuendelea kumlenga yule mwanadada.

 Na mara wakingia vijana wengine wawili wakiwa na bastola na kwenda moja kwa moja pale aliposimama yule mwanamama, wakamshika na kumpekua, mmoja akaichukua ilebastola iliyokuwa chini ambayo alikuwa nayo huyo mwanadada.

‘Mmmmh,haya nifungeni pingu, twendeni huko gerezani, ….ila bado nasema kuwa lazima nitalipiza kisasi…hata kama huyo….’akaninyoshea mikono mimi, `Atakuwa na walinzi wa jabu…hakuna atakayemchukua….ambaye na kuwa hai….’akasema na kwa uwoga akajaribu kugeuka kuniangalia, lakini kwa haraka akageuza kichwa kuwamgalia wakili na mkuu, akamgeukiwa wakili na kusema.

‘Na wewe unayejitia kimbelembele nakuona unanyemelea mauti yako, nimeshakugundua, ….ipo siku tutakutana na mimi, safari ijayo, sitaongea na wewe tena….itakuwa vitendo, haya nifungeni hizo pingu tuondoke….’akasema huyo mwanadada.

Wale jamaa nje, walisikia wakiitwa, wakakurupuka mbio, na walipofika mlangoni wakakutana na silaha zikiwa zimeelekezwa kwao, na kuamrishwa kuwa wapo chini ya ulinzi, na bila ubishi wakanyosha mikono juu na kufungwa pingu wote wakaingizwa kwenye karandinga na kupelekwa kituo cha polisi.

Je ndio mwisho wa kisa hiki,…..

*********

Ilipofika hapa nikabakia mdomo wazi, kwani rafiki yangu alisimama, na mimi nikiwa an maswali mengi ya kumuuliza, je huyu mwanadada anataka kulipiza kisasi kwa nani na kwanini…na ni nani huyo mwanadada?

Akaniangalia na kusema,….’siku nyingine nimechoka….’

Jamani tuwepo kwenye mtiririko wa hitimisho la kisa hiki, ili tuone ni nini kilimsibu huyu mwanadada mpaka akaamua kufanya hayo aliyoyapanga kuyafanya,ni kisasi cha nini, na kwanini….je huyu mwanadada ni nani?

Wengi wanaweza kutoa hoja hapa,…mbona hapa ilitakiwe iwe ndio hitimisho la hiki kisa, ….tukumbuke kuwa hilo ni tukio lilitokea na sio tamithilya ya kubuni, na tukumbuke kuwa kisa hiki kinaitwa HUJAFA HUJAUMBUKA, sio KISA CHA KISASI….Kisa cha kisasii kinakuja …..

WAZO LA LEO: Hulka,tabia na hata fikara za watu hutofautiana, na usizani kuwa upendavyo wewe ndivyo apendavyo mwenzako, au kila unachokijua na mwenzako atakijua ….unavyowaza wewe inaweza ikawa tofauti na awazavyo mwenzako,…ili twende sawa, tujaribu kuvumiliana, kuuliza na kukubali kasoro za wenzako ukijua na wewe una kasoro zako,... bila kunyanyapaana. 


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Yaani kweli huu mtiririko lazima uendelee kuishia hapa itakuwa na maswali mengi sana mimi nataka kujua mwanadada ni nani na kwanini. Wazo la leo ni funzo nzuri sana. NAMI NAONGEZEA KAMA MTU UNA DUKUDUKU BASI LA MUHIMU NI KUULIZA USIJIFANYE KUJUA.

samira said...

m3 au yule alokuwa mchumba wake mtoto wa msomali utotoni mhh bora ni subiri muendelezo hata hivyo jamaa amekumbana na matatizo mingi ya dunia lazma atakuwa makini sana na life yake
m3 una kipaji sio siri yaani sichezi mbali na glog hii
hongera

emu-three said...

Ni kweli dada Yasinta, kuna maswali mengi bado hayajajibiwa ndani ya kisa hiki, na kila hatua majibu yatakuja yenyewe...
Mpendwa Samira huenda upo sawa,hata mimi sijui ngoja tuone,maaana kisa bado kinaendelea,tupo pamoja